Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo anatekeleza PROGRAMU ya UBORESHAJI wa KILIMO Jimboni humo kwa KUCHANGIA UPATIKANAJI wa PLAU na MBEGU BORA za mazao mbalimbali.
VIKUNDI VYA KILIMO vimeanzishwa ndani ya VIJIJI vyote 68 na tayari vimeanza kugawiwa PLAU huku MBEGU bora za MAZAO ya ALIZETI, MIHOGO, MTAMA na UFUTA zilianza kugawiwa na MBUNGE huyo tokea Mwaka 2016.
VIKUNDI VYA KILIMO VYA KATA YA MURANGI
DIWANI wa Kata ya Murangi, Mhe Kujerwa Simion Kujerwa amesema Kata hiyo ina VIJIJI viwili (Lyasembe na Murangi) na hadi sasa vipo VIKUNDI 15 vya KILIMO ambayo vinajishughulisha na KILIMO cha BUSTANI za mbogamboga, matunda na mazao mengine.
DIWANI huyo ameeleza kwamba VIKUNDI vya KILIMO 2 viitwavyo KILIMO KWANZA (cha Kijiji cha Lyasembe) na IFAD (cha Kijiji cha Murangi) VIMEGAWIWA PLAU za Mbunge wa Jimbo. Aliongeza kwa kusema kwamba KIKUNDI cha WANAWAKE kiitwacho TUPENDANE (cha Kijiji cha Lyasembe) kilipewa MASHINE ya UMWAGILIAJI, mbegu na dawa za mimea.
KIKUNDI cha KILIMO KWANZA cha Kijijini Lyasembe kilianzishwa Mwaka 2018 kikiwa kinatumia MAJEMBE ya MKONO, na sasa kinatumia JEMBE la kukokotwa na NG’OMBE walilogawiwa na MBUNGE wao wa Jimbo – hayo yamesemwa na Ndugu MANYAMA MAKUYU ambae ni Mwenyekiti wa Kikundi hicho chenye WANACHAMA 16 wanaojishughulisha na KILIMO cha MAHINDI na DENGU.
WANACHAMA wa Kikundi hicho wanamshukuru sana MBUNGE wao wa Jimbo kwa kuwaboreshea UFANISI kwenye KILIMO chao.
PROGRAMU ya kuongeza MATUMIZI ya PLAU ndani ya JIMBO la Musoma Vijijini INAENDELEA KUTEKELEZWA kwa mpangilio mzuri unawaohamasishwa na kushirikisha WANAVIJIJI wenyewe. MBUNGE wa Jimbo ameishagawa PLAU 45 na atagawa tena PLAU 40 wakati wa Sikukuku ya Eid al Fitr, tarehe 24 Mei 2020
Zoezi la UGAWAJI wa PLAU (zana bora kuliko jembe la mkono) ndani ya VIJIJI 68 vya Jimbo la Musoma Vijijini ni ENDELEVU na ni sehemu ya MPANGO wa UBORESHAJI wa KILIMO ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.