PROGRAMU YA KUBORESHA KILIMO NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI
* ZANA ZA KILIMO: Programu ya kupunguza UTUMIAJI wa JEMBE la MKONO kwenye kilimo chetu inaendelea vizuri.
ZAWADI MUHIMU ya Eid al Fitr (2020) ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo aliyoitoa kwa WANAVIJIJI wa Jimbo letu ni PLAU 40 (MAJEMBE 40 ya kukokotwa na ng’ombe au punda).
LENGO KUU: kuongeza MATUMIZI ya PLAU badala ya JEMBE la MKONO ndani ya VIJIJI vyetu vyote 68. Hadi sasa (25.5.2020), Mbunge huyo ameishagawa bure jumla ya PLAU 85 kwa VIKUNDI 85 kutoka Vijiji vyote 68.
MGAO mwingine utafanyika wakati wa Sherehe za WAKULIMA, yaani NANENANE 2020.
Tumejiwekea MALENGO ya kuwa na PLAU zaidi ya 20 ndani ya KILA KIJIJI kwa kipindi cha Miaka 2 (2020 & 2021).
* MAZAO MAKUU YA CHAKULA: Mihogo, Mahindi, Mtama, Viazi vitamu, Mpunga, Mbogamboga na Matunda. Malengo yetu ni kuongeza UZALISHAJI kwenye MAZAO hayo ili yatumike kama MAZAO ya CHAKULA na MAZAO ya BIASHARA. Kilimo cha UMWAGILIAJI kinawekewa msisitizo mkubwa na kimeanza kuzaa matunda mazuri.
* MAZAO MAKUU YA BIASHARA: Pamba na Alizeti. Tumeongeza ZAO la ALIZETI na kwa misimu 3 mfulilizo ya Kilimo, takribani TANI 20 za MBEGU za ALIZETI zimegawawiwa bure kwa WAKULIMA ndani ya Kata zote 21. Mbunge Jimbo alichangia takribani TANI 10 na SERIKALI kupitia Wizara ya Kilimo ilichangia TANI 10.
MITAMBO 2 ya Watu Binafsi ya kukamua Mbegu za ALIZETI (viwanda vidogo) imefungwa Jimboni mwetu – Vijijini Saragana na Kusenyi. MITAMBO mingine ya kukamua ALIZETI iko maeneo jirani, k.m. kwenye Miji ya Bunda na Musoma.