KIGERA SEKONDARI KUFUNGULIWA JANUARI 2021 – SEKONDARI YA PILI YA KATA

baadhi ya MABOMA ya KIGERA SEKONDARI itakayofunguliwa Januari 2021 – KARIBU UCHANGIE ujenzi huu.

Kata ya Nyakatende yenye Vijiji 4 ina Sekondari 1 ambayo imeelemewa na wingi wa Wanafunzi na baadhi yao wanatembea umbali mrefu (zaidi ya kilomita 5) kwenda masomoni.

Vijiji 2 vya KIGERA na KAKISHERI vimeamua kujenga SEKONDARI yao (KIGERA SEKONDARI) kwani WATOTO wao ndio wanatembea umbali mrefu kwenda NYAKATENDE SEKONDARI.

MICHANGO YA UJENZI ILIYOKWISHATOLEWA

*NGUVUKAZI za Wakazi wa Vijiji vya Kigera na Kakisheri (kusomba maji, mchanga, mawe na kokoto)

*MICHANGO ya FEDHA taslimu ya awali: Shilingi 2,000 kwa kila mkazi (vijiji 2) mwenye umri kati ya miaka 18 na 59.

*WAZALIWA wa Vijiji 2 wanawalipa MAFUNDI na fedha nyingine zinanunua vifaa vya ujenzi.

*SARUJI MIFUKO 150 ya Mbunge wa Jimbo, Profesa Muhongo*

*SARUJI MIFUKO 100 ya Mfuko wa Jimbo*

MAJENGO YANAYOHITAJIKA KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA (2021)

*Maoteo ya Wanafunzi wa Kata ya Nyakatende watakaojiunga na Kidato I ni 190.

*Maoteo ya Wanafunzi watakaojiunga na Kidato I KIGERA SEKONDARI ni 120.

*Maoteo ya Wanafunzi wa Kidato I watakaoenda NYAKATENDE SEKONDARI ni 70.

MICHANGO MINGINE YA MBUNGE WA JIMBO NA DIWANI MTEULE

*Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo atachangia MABATI 108 (bando 9, geji 28)

*Diwani Mteule, Mhe Marere John Kisha atatengeneza MADAWATI 120 ya Wanafunzi wa Kidato I.

*ELIMU KWANZA*

Jimbo la Musoma Vijijini lenye KATA 21, lina:

*Sekondari 20 za Kata/Serikali

*Sekondari 2 za Binafsi

*Sekondari Mpya 5 zinazotarajiwa kufunguliwa Januari 2021 (Bukwaya, Kigera, Nyasaungu, Ifulifu na Seka)

*Sekondari Mpya 5 zitakazoanza kujengwa mwakani (2021) za Kata za: Etaro, Makojo, Mugango, Suguti na Tegeruka.

*HIGH SCHOOLS zitaongezeka kutoka 2 (1 Serikali & 1 Binafsi) hadi 6 ndani ya miaka 5.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini