SERIKALI YATOA SHILINGI MILIONI 50 ZA KUUNGA MKONO JITIHADA ZA WANAVIJIJI ZA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA SEKONDARI YAO YA KATA

baadhi ya WANAVIJIJI wa Kata ya Kiriba na MAFUNDI wao wakiwa kwenye ujenzi wa JENGO la UTAWALA la Kiriba Sekondari.

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
23.11.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
JIMBO la Musoma Vijijini lenye Kata 21 na Vijiji 68 lina jumla ya SEKONDARI 20 za KATA, na SEKONDARI MPYA 5 za Kata zinatarajiwa kufunguliwa Januari 2021. Vilevile, Jimbo lina SEKONDARI 2 za BINAFSI za Madhehebu ya Dini.
KATA 5 – Etaro, Makojo, Mugango, Suguti na Tegeruka zimepanga kuanza kujenga SEKONDARI ya PILI ya Kata zao.
KIRIBA SEKONDARI:
VIJIJI 3 vya Kata ya KIRIBA ambavyo ni Bwai Kumusoma (Paris), Bwai Kwitururu (London) na Kiriba VIMEAMUA KUJITOLEA kuboresha MIUNDOMBINU ya Sekondari yao, KIRIBA SEKONDARI.
UBORESHAJI uko kwenye ujenzi wa MAABARA 3, MABWENI 2, JENGO la UTAWALA na NYUMBA za WALIMU.
SHILINGI MILIONI 50 ZA SERIKALI:
SERIKALI yetu inapewa SHUKRANI nyingi kwa kutoa Shilingi MILIONI 50 kuchangia ujenzi wa JENGO la UTAWALA la Sekondari hiyo.
WANAVIJIJI kutoka Vijiji 3 vya Kata hiyo wanachangia NGUVUKAZI kwa kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji. Hayo yamesemwa na Mwalimu Mkuu wa Sekondari hii, Mwl Paul Mtani.
DIWANI MTEULE wa Kata ya Kiriba, Mhe Hamisi Saire ametoa SHUKRANI nyingi kwa SERIKALI na kwa MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo kwa MICHANGO yao MINGI ya kuboresha MIUNDOMBIMU ya ELIMU ndani ya Kata yao.
MBUNGE huyo wa Jimbo la Musoma Vijijini alishachangia KIRIBA SEKONDARI jumla ya Saruji Mifuko 175, Rangi na Vitabu 1,000 vya Maktaba.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini