UFUGAJI WA NYUKI WAANZA KUCHANGAMKIWA MUSOMA VIJIJINI

KIKUNDI cha JIPE MOYO cha Kijijini Buanga, Kata ya Rusoli kikiwa kwenye SHAMBA lao lenye MIZINGA ya NYUKI.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
KIKUNDI cha JIPE MOYO cha Kijiji cha Buanga, Kata ya Rusoli kimeanzisha MRADI wa UFUGAJI NYUKI kwa ajili ya kupanua wigo wa shughuli za ki-uchumi za KIKUNDI hicho.
Kikundi hicho kimepata UTAALAMU wa UFUGAJI wa NYUKI kutoka kwenye MAFUNZO waliyopewa na SHIRIKA la SWISSCONTACT.
MWENYEKITI wa Kikundi cha JIPE MOYO, Ndugu Masamaki Girishom, amesema kwamba Kikundi chao kilianzishwa Mwaka 2018 na kina Wanachama 24. Kikundi hiki linashughulisha na KILIMO, na sasa kimeanza KUFUGA NYUKI.
Shirika la SWISSCONTACT limewapatia VIFAA vya awali vya Mradi huu ambavyo ni MIZINGA 10 na VAZI 1 la kuvunia ASALI.
MRATIBU wa Swiss Contact, Ndugu Nelson Bento amesema kwamba hadi sasa, JIMBONI mwetu, kuna VIKUNDI 7 vya UFUGAJI wa NYUKI, na WANAVIJIJI wengi wanaanza kupenda kufuga nyuki kwa ajili ya kuongeza vyanzo vya  mapato yao.
MRATIBU huyo amesema SOKO la ASALI itakayovunwa Vijijini mwetu lipo.
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo anaendelea kuhimiza WANAVIJIJI waanzishe VIKUNDI vya UCHUMI, vikiwemo vya kilimo cha umwagiliaji, uvuvi na ufugaji wa nyuki.
KARIBUNI TUFUGE NYUKI VIJIJINI MWETU
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini