WANAVIJIJI WAMEDHAMIRIA WATOTO WAO WASITEMBEE UMBALI MREFU KWENDA MASOMONI

MIUNDOMBINU inayojengwa  KIGERA SEKONDARI itakayokuwa tayari kupokea WANAFUNZI wa KIDATO cha KWANZA Januari 2021.

Tarehe 18.12.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
KATA ya NYAKATENDE yenye Vijiji 4 (Kakisheri, Kamguruki, Kigera na Nyakatende) inayo SEKONDARI MOJA tu,  NYAKATENDE SEKONDARI ambayo ina MIRUNDIKANO ya WANAFUNZI madarasani. Vilevile, baadhi ya WANAFUNZI wanatembea zaidi ya KILOMITA 10 kwenda masomoni kwenye Sekondari hiyo iliyofunguliwa Mwaka 2006, yenye WANAFUNZI 784 na ina UPUNGUFU wa Vyumba 4 vya Madarasa.
SULUHISHO LA KERO ZA MIRUNDIKANO NA UMBALI MREFU WA KUTEMBEA
VIJIJI 2 vilivyoko mbali na Nyakatende Sekondari VIMEAMUA KUJENGA SEKONDARI yao wenyewe. VIJIJI hivyo ni Kakisheri na Kigera.
MICHANGO YA UJENZI WA SEKONDARI MPYA
MICHANGO ya ujenzi wa Sekondari ya Vijiji hivyo viwili inatolewa na:
*WANAVIJIJI wanachangia NGUVUKAZI zao kwa kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji.
*WANAVIJIJI wanachangia FEDHA taslimu, Shilingi 2,000 kwa kila mwenye umri wa miaka 18 na zaidi.
*WAZALIWA wa Vijiji vya Kakisheri na Kigera WANALIPA GHARAMA za MAFUNDI ujenzi na WANANUNUA  baadhi ya VIFAA vya ujenzi.
*DIWANI wa Kata ya Nyakatende, Mhe Marere John Kisha, ni mmoja wa WAZALIWA wanaochangia ujenzi huu. Vilevile, ameanza kutengeneza MADAWATI 130 ya Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza watakaoanza  MASOMO Januari 2021 kwenye Sekondari hiyo inayoitwa,” KIGERA SECONDARY SCHOOL.”
*MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo AMEISHACHANGIA:
^Saruji Mifuko 150
^Mabati 108
*MFUKO wa JIMBO umeishachangia:
^Saruji  Mifuko 100
MBUNGE wa JIMBO kwa KUSHIRIKIANA na WADAU wengine wa MAENDELEO ataendelea kuchangia ujenzi huu.
MAJENGO YANAYOKAMILISHWA UJENZI
*VYUMBA 2 vya Madarasa vimeishaezekwa na madirisha yamewekwa.
*JENGO la UTAWALA lenye Vyumba (Ofisi 9) limeishaezekwa na madirisha yamewekwa.
*BOMA la CHOO chenye MATUNDU 11 litaezekwa kabla ya tarehe 30.12.2020. Tundu 1 ni kwa Watu wenye ULEMAVU.
*BOMA la MAABARA 2 litaezekwa kabla ya tarehe 30.12.2020
*BOMA la NYUMBA 1 ya MWALIMU litaezekwa kabla ya tarehe 30.12.2020
WANAFUNZI WALIOFAULU
*WANAFUNZI 191 wa Kata ya Nyakatende WAMEFAULU kuendelea na MASOMO ya SEKONDARI.
Kwa hiyo, WANAFUNZI hao 191 watagawanywa kwenye SEKONDARI 2 za Kata, yaani NYAKATENDE SEKONDARI iliyoanza Mwaka 2006, na KIGERA SEKONDARI itakayoanza Januari 2021.
MWENYEKITI wa Serikali ya Kijiji cha Kigera, Ndugu Magafu Katura anatoa MAOMBI ya kuchangiwa SARUJI MIFUKO 300 na RANGI LITA 80 ili kukamilisha Maboma ya Sekondari yao.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini