WANAVIJIJI  WANAJENGA VYUMBA 2 VYA MADARASA NA MATUNDU 28 YA VYOO VYA WANAFUNZI

Hatua ya ujenzi iliyofikiwa kwa MABOMA ya Vyumba viwili vya Madarasa, na MASHIMO 28 ya VYOO vya Wanafunzi wa BUGWEMA SEKONDARI ya Kata ya Bugwema.

 

Na: Fedson Masawa

Msaidizi wa Mbunge

WANAVIJIJI wa Kata ya Bungwema yenye Vijiji 4 (Bugwema, Kinyang’erere, Masinono na Muhoji)  wanashirikiana na VIONGOZI wao kujenga Vyumba viwili (2) vya Madarasa, Ofisi moja (1) ya Walimu na Matundu 28 ya VYOO vya Wanafunzi kwenye SEKONDARI yao (Bugwema Secondary School).

Akishuhudia ujenzi unaoendelea shuleni hapo, MSAIDIZI wa MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Ndugu Fedson Masawa, amejiridhisha na maendeleo mazuri kwenye ujenzi huo.

 

MICHANGO YA UJENZI KUTOKA KWA WANAVIJIJI

MTENDAJI KATA (WEO) hiyo, Ndugu Josephat Phinias amesema WANAVIJIJI wamekubaliana kuchanga Tsh 5,000 kutoka kila KAYA kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba vya Madarasa.

Vilevile, kila KAYA inachanga Tsh 15,000/= kwa ajili ya ujenzi wa MATUNDU 28 ya VYOO vya Wanafunzi.

KIONGOZI huyo anaomba WADAU wa MAENDELEO wawachangie MABATI 108 kwa ajili ya kuezeka MABOMA wanayoyajenga.

 

MICHANGO YA

MBUNGE WA JIMBO

Prof Sospeter Muhongo, Mbunge wa Jimbo lenye Bugwema Sekondari ameishaichangia shule hii kama ifuatavyo:

*VITABU vingi vya Maktaba

*POSHO ya Mwalimu 1 wa MASOMO ya SAYANSI kwa kipindi cha MIAKA MIWILI (2).

*SARUJI MIFUKO 70

*Kupeleka WAFADHILI wa ujenzi wa MAABARA

 

MWALIMU MKUU wa Bugwema Sekondari, Mwl Joseph Emmanuel Ndaro ameeleza kwamba SEKONDARI hiyo ilianzishwa MWAKA 2006, ina WANAFUNZI 556. Shule ina Vyumba vinane (8) vya Madarasa, na inapungukiwa vinne (4)

 

MWALIMU MKUU huyo ameeeleza UFAULU wa Shule yao wa Mwaka jana (2020) wa Kidato cha PILI (II) na NNE (IV) kama ifuatavyo:

 

KIDATO CHA II MWAKA 2020

Daraja la I = Wanafunzi 5 (ME 4 na KE 1)

Daraja II = 7 (ME 6, KE 1)

Daraja III = 13 (ME 10, KE 3)

Daraja IV = 51 (ME 24, 27

Daraja 0 = 7 (ME 5, KE 2)

 

KIDATO CHA IV MWAKA 2020

Daraja I = Wanafunzi 3 (ME 3, KE 0)

Daraja II = 4 (ME 4, KE 0)

Daraja III = 8 (ME 7, KE 1)

Daraja IV = 50 (ME 28, KE 12)

Daraja 0 = 24 (ME 7, KE 17)

 

Ofisi ya Mbunge

Jimbo la Musoma Vijijini

www.musomavijijini.or.tz