Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
SHULE YA MSINGI BUSEKERA ilifunguliwa Mwaka 1954. Shule hii iko Kijijini Busekera, Kata ya Bukumi.
MWALIMU MKUU wa Shule hii, Mwl Kevin Majogoro amesema kwamba Shule ina jumla ya WANAFUNZI 1,271.
MAHITAJI ya Madarasa ni Vyumba 24, vilivyopo ni 10!
MIRUNDIKANO ya WANAFUNZI madarasana ni mikubwa. Kwa mfano, Darasa la AWALI lina Wanafunzi 234 kwenye chumba kimoja na Darasa la VII lina Wanafunzi 111 ndani ya chumba kimoja!
SERIKALI YATOA MCHANGO WA KUJENGA MADARASA NA VYOO
SERIKALI kupitia MRADI wake wa EP4R imetoa Tsh MILIONI 47.7 kwa ajili ya ujenzi wa VYUMBA 2 vya MADARASA na CHOO chenye MATUNDU 7 ya S/M Busekera.
MICHANGO YA WANAKIJIJI
MTENDAJI wa Kijiji cha Busekera, Ndugu Faustine Majura amesema WANAKIJIJI wameshirikishwa kwa:
*kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji
*kuchimba shimo la choo
*kuchimba msingi wa Vyumba 2 vya madarasa.
SHUKRANI KWA SERIKALI YETU
Wananchi na Viongozi wa Kijiji cha Busekera WANAISHUKURU sana SERIKALI kwa kuwachangia Tsh Milioni 47.7.
MICHANGO YA MBUNGE WA JIMBO
MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo amekuwa akihamasisha na kuchangia uboreshaji wa MAZINGIRA ya KUJIFUNZA na KUFUNDISHIA kwenye SHULE zote za Jimboni mwao.
MICHANGO ya Mbunge huyo kwenye S/M Busekera ni:
*Saruji Mifuko 60
*Mabati 54
*Madawati 94
*Vitabu vingi vya Maktaba
TUCHANGIE KUBORESHA UFAULU WA S/M BUSEKERA
MATOKEO ya DARASA la IV (2020):
*Watahiniwa 123
*Waliofaulu 120
MATOKEO ya DARASA la VII (2020):
*Watahiniwa 69
*Waliofaulu 45
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijni. or. tz