WANAKIJIJI WAPATA MICHANGO YA SERIKALI KWENYE UJENZI NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU

ujenzi wa Vyumba vipya vya Madarasa na Ofisi ya Walimu unaotekelezwa na WANAKIJIJI kwenye Shule yao ya Msingi, S/M KOME B, iliyoko Kijijini Kome, Kata ya Bwasi. 

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
SHULE ya MSINGI KOME B ilifunguliwa Mwaka 2015, Kijijini Kome, Kata ya Bwasi.
KATA ya BWASI ina Vijiji 3 (Bugunda, Bwasi na Kome) na kila Kijiji kina Shule za Msingi mbili (yaani shule moja kila kijiji yenye A&B).
MWALIMU MKUU wa S/M BWASI B,  Mwl Yoel Peter ametoa maelezo ya Shule hiyo kama ifuatavyo:
*Jumla ya Wanafunzi ni 565
*Mahitaji ya Vyumba vya Madarasa ni 10, vilivyopo ni 6
*Mirundikano ya Wanafunzi madarasani ni mikubwa, kwa mfano Darasa la III lenye Wanafunzi 160 wana chumba kimoja cha darasa.
*Wapo Wanafunzi wenye madarasa chini ya MITI.
MICHANGO YA UJENZI NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU KWENYE S/M KOME B
MTENDAJI wa KIJIJI (VEO) cha Kome, Ndugu Fredrick Jeremia amesema WANAKIJIJI WAMEAMUA kuanza ujenzi wa Vyumba vipya vya Madarasa na Ofisi ya Walimu kwenye Shule yao (S/M Kome B).
WANAKIJIJI wanachangia:
*NGUVUKAZI zao kwa kuchimba misingi ya majengo, na kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji ya ujenzi.
*FEDHA taslimu Tsh 2,300/= kutoka kila kaya.
*SERIKALI, kupitia Mradi wake wa PEDP (Primary Education Development Programme) imetoa Tsh MILIONI 12.5 kwa ajili ya kukamilisha Chumba 1 cha Darasa na kununua madawati na meza.
MICHANGO MINGINE ILIYOKWISHA KUTOLEWA SHULENI HAPO
*SERIKALI kupitia Mradi wake wa  EP4R ilitoa Tsh MILIONI 5
*PCI Tanzania imejenga Choo chenye Matundu 10
*MBUNGE wa JIMBO, Profesa Sospeter Muhongo ameishachangia:
 (i) Madawati 62
 (ii) Saruji Mifuko 120
(iii) Vitabu zaidi ya 1,000 vya Maktaba
*MFUKO wa JIMBO ulinunua Mabati 126
UFAULU WA MITIHANI KWENYE S/M KOME B
*Darasa la IV  (2020)
Watahiniwa 36
Waliofaulu  36
*Darasa la VII (2020)
Watahiniwa 33
 Waliofaulu  30
WAZALIWA wa Kijiji cha Kome na Kata ya Bwasi WANAOMBWA wachangie MAENDELEO ya nyumbani kwao – OMBI kutoka kwa ndugu zao.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini