Na: Wasaidizi wa Mbunge
*Verediana Mgoma
*Hamisa Gamba
*Fedson Masawa
*Vaileth Peter
WANAVIJIJI wa JIMBO la MUSOMA VIJIJINI wamekuwa na mwamuko mkubwa wa KUJITOLEA kuanzisha na KUTEKELEZA MIRADI ya MAENDELEO yao kwenye Sekta za Afya, Elimu, Kilimo, Uvuvi, Ufugaji, Utamaduni na Michezo.
SERIKALI inatoa MICHANGO ya FEDHA kwenye utekelezaji wa baadhi ya Miradi hiyo ya Maendeleo.
JIMBO hili lina KATA 21 zenye VIJIJI 68 na VITONGOJI 374
*VITUO 28 VYA CHANJO YA UVIKO MUSOMA VIJIJINI viko Vijijini:*
1.BUGOJI 2.BUGUNDA
3.BWASI 4.KIEMBA
5.KIRIBA 6.KOME
7.KURUGEE 8.MUGANGO 9.MURANGI
10.MWIRINGO
11.NYAKATENDE
12.NYAMBONO
13.RUKUBA 14.SEKA
15.SUGUTI 16.TEGERUKA
17.WANYERE 18. BWAI
19. RUSOLI 20. BUKIMA
21. BUSUNGU 22. CHITARE
23. ETARO 24.KIGERA ETUMA
25. KWIKUBA 26. MASINONO
27. NYEGINA
28. MUSOMA DC HOSP (Kitongoji cha Kwikonero)
*Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea KUJITOKEZA kupata CHANJO ya UVIKO. Mbunge wao wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo alishachanjwa.
*UTEKELEZAJI WA MIRADI MIPYA KWENYE SEKTA YA AFYA NDANI YA JIMBO LETU*
UJENZI wa:
*Zahanati 15
*Wodi 3 za Mama & Mtoto (Zahanati za Kisiwani Rukuba, Bukima & Nyegina)
*Vituo 2 vya Afya (Bugwema & Makojo: kwa mchango mkubwa Serikali)
*Hospital ya Wilaya inayojengwa na Serikali (haijakamilika: kila Kijiji kinachangia Tsh milioni 2)
*HUDUMA ZA AFYA ZILIZOPO*
*Zahanati 24 za Serikali
*Zahanati 4 za Binafsi
*Vituo vya Afya 2 (Murangi & Mugango)
*Magari 5 ya Wagonjwa (Ambulances 5: zilitolewa na Mbunge wa Jimbo)
*ZAHANATI MPYA 15 ZINAZOJENGWA NA WANAVIJIJI*
1.*BUIRA*: KIJIJI CHA BUIRA, KATA YA BUKUMI
2. *BUSEKERA*: KIJIJI CHA BUSEKERA, KATA YA BUKUMI
3. *BURUNGU*: KIJIJI CHA BUKUMI KATA, BUKUMI
4. *BUTATA* : KIJIJI CHA BUTATA KATA, BUKIMA
5. *BWAI KWITURURU* : KIJIJI CHA BWAI KWITURURU, KATA YA KIRIBA
6. *CHIMATI* : KIJIJI CHA CHIMATI, KATA YA MAKOJO
7. *CHIRORWE* : KIJIJI CHA CHIRORWE, KATA YA SUGUTI
8. *KAKISHERI* : KIJIJI CHA KAKISHERI, KATA YA NYAKATENDE
9. *KURUKEREGE* : KIJIJI CHA KURUKEREGE, KATA YA NYEGINA
10. *KURWAKI* : KIJIJI CHA KURWAKI, KATA YA MUGANGO
11. *MANEKE* : KIJIJI CHA MANEKE, KATA YA BUSAMBARA
12. *MKIRIRA* : KIJIJI CHA MKIRIRA, KATA YA NYEGINA
13. *MMAHARE* : KIJIJI CHA MMAHARE, KATA YA ETARO
14. *NYABAENGERE*: KIJIJI CHA NYABAENGERE, KATA YA MUSANJA
15. *NYASAUNGU* : KIJIJI CHA NYASAUNGU, KATA YA IFULIFU
*Baadhi ya Zahanati hizo zimepokea MICHANGO ya FEDHA kutoka SERIKALI KUU
*Wanavijiji na Viongozi wao (Mbunge wa Jimbo & Madiwani), na baadhi ya Wazaliwa wa Musoma Vijijini) ndio WACHANGIAJI WAKUU wa ujenzi huo.
*Halmashauri yetu (Musoma DC) inashauriwa nayo ianze kuchangia ujenzi wa Zahanati hizo.
*AMBULACE 5 ZA MUSOMA VIJIJINI*
Katika kuboresha Huduma za Afya Jimboni mwao, Mbunge wa Jimbo, Profesa Sospeter Muhongo, alitoa magari matano ya wagonjwa ambayo kwa sasa yamechoka baada ya kutumika kwa muda mrefu, Ambulance hizo zilipelekwa:
*KITUO CHA AFYA MURANGI*: KATA YA MURANGI
*KITUO CHA AFYA MUGANGO* : KATA YA MUGANGO
*ZAHANATI YA KURUGEE*: KIJIJI CHA BUKUMI, KATA YA BUKUMI
*ZAHANATI YA MASINONO*: KIJIJI CHA MASINONO, KATA YA BUGWEMA
*ZAHANATI YA NYAKATENDE* : KIJIJI CHA KABEGI, KATA YA IFULIFU
*OMBI KUTOKA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI*
Wananchi na Viongozi wa Jimbo hili wanaomba MICHANGO ya FEDHA (zikiwemo Fedha za IMF) wakamilishe UJENZI wa MIUNDOMBINU ya AFYA ya Jimboni mwao.
Vilevile, WANAVIJIJI wanaomba MAGARI 2 ya WAGONJWA (2 Ambulances) kwa kuzingatia ukubwa wa Jimbo hili.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini