ELIMU: Jimbo la Musoma Vijijini (Kata 22 zenye Vijiji 68) lina idadi ifuatayo:
*Shule za Msingi za Serikali 111.
*Shule za Msingi za Binafsi 3
*Shule za Msingi mpya zinazojengwa (Shule Shikizi) 13
*Sekondari za Kata 22
*Sekondari za Binafsi 2
*Sekondari mpya zinazojengwa au zilizopangwa kujengwa 10
*High School 1 (iko Kasoma Sekondari) ya masomo ya “arts”
MAABARA ZINAJENGWA KWENYE SEKONDARI ZOTE
Sekondari zote 22 (na mpya zinazojengwa) zinajenga na kuboresha MAABARA 3 kwenye shule zao ambazo ni za Fizikia, Kemia na Biolojia.
Wananchi wa Kata ya Kiriba WAMEAMUA kuchangia ujenzi wa “HIGH SCHOOL” ya masomo ya SAYANSI (PCM & PCB) kwa kuanza ujenzi wa MIUNDOMBINU inayohitajika:
*Maabara 3 za Fizikia, Kemia na Biolojia: tayari zimekamilika na zinatumika.
*Jengo la Utawala limekamilika na linatumika.
*Ujenzi wa Mabweni umeanza, ambao utafuatiwa na ujenzi wa Bwalo la Chakula na Jiko.
Bofya hapa kusikiliza CLIP hii inayoelezea maoni ya Wanavijiji na Viongozi kuhusu Kiriba Sekondari na “High School” wanayoijenga.
Unakaribishwa sana kuchangia ujenzi na uboreshaji wa MIUNDOMBINU ya ELIMU ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini