JAMII YA WAFUGAJI YAENDELEA KUJENGA SEKONDARI YAKE KIJIJINI MWAO

ziara ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, kijijini Nyasaungu, Kata ya Ifulifu. Mbunge wa Jimbo na Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi, Ndugu Joseph Chome (mwenye T-shirt ya rangi ya njano) wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa Sekondari ya Kijiji cha Nyasaungu.

 

Kijiji cha NYASAUNGU ni kimoja kati ya VIJIJI 3 vya Kata ya IFULIFU iliyo ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini. Ni hii Kata pekee isiyokuwa na Sekondari yake ndani ya Jimbo letu!
JIOGRAPHIA ya Kata hii imewalazimu WANAVIJIJI wa VIJIJI hivi vitatu kujenga SEKONDARI 2 kwa wakati mmoja.
Kijiji cha WAFUGAJI cha NYASAUNGU kimezunguka na MITO na kiko mbali (kati ya kilomita 10 na 15) kutoka vijiji vingine viwili (Kabegi na Kiemba).
N.B. Juzi, Ndugu Chacha alimueleza Mbunge wa Jimbo kwamba amelazimika kumpeleka mwanae akasome Sekondari ya Musoma Mjini baada ya mwanae kushindwa kwenda shuleni kwa siku 3 za mvua zilizonyeesha Kijijini mwao. Njia  hazipitiki!
Kwa hiyo SEKONDARI 2 zinajengwa kwa mpangilio ufuatao:
*Nyasaungu Sekondari:
Inajengwa na Wanakijiji wa Nyasaungu (WAFUGAJI)
*Ifulifu Sekondari:
Inajengwa na Wanavijiji wa Kabegi na Kiemba. Taarifa zaidi za ujenzi wa Sekondari hii utatolewa baadae.
*UJENZI WA NYASAUNGU SEKONDARI*
Juzi, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo alitembelea Kijiji cha Nyasaungu kufuatilia ujenzi wa Sekondari ya Kijiji hicho ulioanza AGOSTI 2019.
Taarifa za ujenzi wa Sekondari hii ya WAFUGAJI wa Kijiji cha Nyasaungu imetolewa mara kadhaa.
WACHANGIAJI WA UJENZI WAKE ni:
*Wanakijiji wenyewe kwa vigezo vya wingi wa MIFUGO yao. Kwa mfano wenye ng’ombe zaidi ya 100 wanachangia Tsh LAKI 2 (200,000).
*Wanakijiji wanachangia NGUVUKAZI
*Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo – fedha zake binafsi
*Mfuko wa Jimbo la Musoma Vijijini – fedha za Serikali.
Halmashauri yetu inaombwa nayo ianze kuchangia ujenzi huu.
MINDOMBINU ILOYOKAMILISHWA:
*Vyumba 3 vya Madarasa
*Choo chenye matundu sita (6)
*Jengo la Utawala: msingi umekamilishwa.
MALENGO MAPYA YA NYASAUNGU SEKONDARI
*Wanakijiji wa Nyasaungu na Mbunge wao wamejiwekea MALENGO MAPYA ambayo ni:
*Jengo la Utawala likamilishwe kabla ya tarehe 30 Machi 2022
*Serikali iombwe kufungua Nyasaungu Sekondari JULAI 2022 iwapo miundombinu ya awali itakuwa imekamilika.
*SERIKALI ikisaidie Kijiji cha WAFUGAJI cha Nyasaungu kama ambavyo inasaidia JAMII ya WAFUGAJI sehemu nyingine za nchi yetu. Mbunge ameishawasilisha ombi hili kwa wahusika TAMISEMI.
TUCHANGIE UJENZI WA NYASAUNGU SEKONDARI – Karibuni sana!
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
22.1.2022