KITUO CHA AFYA MAKOJO – WANAVIJIJI WAAMUA KUONGEZA KASI YA UJENZI*

maboma ya OPD na MAABARA ya KITUO cha AFYA cha Kata ya Makojo kinachojengwa Kijijini Makojo.

Kwa Mwaka huu wa Fedha, 2021/2022, Jimbo la Musoma Vijijini linajenga VITUO 2 vya AFYA:
*Makojo: chanzo cha fedha – RUZUKU ya Serikali
*Rukuba (Kisiwa): chanzo cha fedha – TOZO
*VITUO vilivyokwishajengwa na vinavyotoa HUDUMA za AFYA ni:*
*Murangi
*Mugango
*Bugwema
*KITUO KIPYA CHA AFYA CHA MAKOJO*
Kata ya MAKOJO yenye Vijiji 3 (Chimati, Chitare na Makojo) IMEAMUA kuongeza KASI ya ujenzi wa Kituo cha Afya ili kukikamilisha haraka iwezekanavyo.
Kata hii imepewa SHILINGI MILIONI 250 (Tsh 250m) kwa ajili ya ujenzi wa KITUO cha AFYA cha Kata yao. Fedha hizi ni RUZUKA ya SERIKALI yetu.
WANAVIJIJI wanachangia NGUVUKAZI zao kwa kuchimba misingi ya majengo, kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji ya ujenzi.
WANANCHI na VIONGOZI wa Kata ya Makojo wanatoa shukrani nyingi sana kwa SERIKALI yetu inayoongozwa kwa umahiri mkubwa na RAIS wetu, Mhe SAMIA SULUHU HASSAN.
VIONGOZI wa Vitongoji wanahamasisha ushiriki wa Vitongoji vyao kwenye utekelezaji wa Mradi huu.
DIWANI wa Viti Maalum, Mhe Tabu Maregesi Machumu anasimamia ujenzi huu kwa ufanisi na mafanikio makubwa – tunampongeza sana!
MABOMA 2 tayari yanakaribia kuezekwa:
*OPD
*MAABARA
Ujenzi wa miundombinu mingine ya Kituo hiki, k.m. WODI ya Mama & Mtoto, unaendelea kwa kasi na ari mpya.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
10 Feb 2022