Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo anaendelea kushirikiana na VI Agroforest kugawa bure miche ya miti na matunda kwa wanavijijini na taasisi mbalimbali (k.m. shule, zahanati) Jimboni mwao.
VI Agroforest inafadhiliwa na Serikali ya Sweden na inafanya kazi nzuri ya utunzaji wa mazingira ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini na kwingineko Mkoani Mara.
Miche laki moja (100,000) itakayogawiwa bure wakati wa mvua za vuli (Novemba-Disemba 2022) itakuwa ya miti ya:
*matunda
*mbao/ujenzi
*kuni
*ufugaji wa nyuki
*madawa ya asili
Matayarisho ya miche laki moja (100,000), chini ya Mtaalamu Jacob Malima, yanaendelea vizuri ndani ya Kitalu cha VI Agroforest kilichopo Mjini Musoma.
OMBI KWA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Jimbo la Musoma Vijijini linaiomba Wizara hiyo ifufue Kitalu cha Miti cha Serikali kilichopo Kijijini Suguti.
Usisahau kutembelea TOVUTI ya Jimbo letu ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Jumanne, 25.10.2022