MDAU WA MAENDELEO ACHANGIA UJENZI WA MAABARA ZA SAYANSI KWENYE SEKONDARI ZA MUSOMA VIJIJINI

Sekondari 3 za Musoma Vijijini zikikabidhiwa Saruji Mifuko 153 kutoka Umoja Security Services yenye Makao Makuu jijini Dar es Salaam.

Leo, Jumatano, 8.3.2023, mmoja wa Wadau wa Maendeleo hapa nchini, NGUVU MOJA SECURITY SERVICES amechangia Tsh 3,520,000 (Tsh 3.52m) kwa ajili ya ujenzi wa MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI (physics, chemistry & biology laboratories) kwenye baadhi ya Sekondari za Musoma Vijijini.

Mwakilishi wao, Afisa wa Polisi Mstaafu, ASP Moyo amekabidhi mchango huo kwenye Duka la kuuza vifaa vya ujenzi la Musoma Mjini. Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo, alikuwepo kushudia tukio hilo.

Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 zenye jumla ya Vijiji 68 na Vitongoji 374 lina jumla ya Sekondari:
*25 za Kata
*2 za binafsi
(madhehebu ya Dini)

Mbunge Jimbo anahamasisha na kuchangia ujenzi wa Mabaara za Masomo ya Sayansi kwenye Sekondari zote 27.

Lengo kuu ni kuwapatia Wanafunzi wa Sekondari zetu fursa nzuri ya kupata elimu ya vitendo, na kuongeza uelewa wao wa masomo ya sayansi.

Vile vile, ujenzi huu wa maabara tatu za masomo ya sayansi kwa kila sekondari ni matayarisho yetu ya kuanzisha HIGH SCHOOLS za MASOMO ya SAYANSI Jimboni mwetu.

Sekondari tatu zilizopokea saruji kwa ujenzi wa maabara zao ni:

Seka Sekondari
*imepokea Saruji Mifuko 51
*haina maabara hata moja
*ilifunguliwa Mwaka 2021
*Mwanafunzi 344
*Walimu 7
*hii ni Sekondari ya pili ya Kata ya Nyamrandirira

Bwai Sekondari
*imepokea Saruji Mifuko 51
*haina maabara hata moja
*ilifunguliwa Mwaka 2023
*Mwanafunzi 139
*Walimu 5
*hii ni Sekondari ya pili ya Kata ya Kiriba

Muhoji Sekondari
*imepokea Saruji Mifuko 51
*Sekondari mpya inajengwa ifunguliwe mwakani (2024)
*hii ni Sekondari ya pili ya Kata ya Bugwema

TUNAKUKARIBISHA UCHANGIE UJENZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU KWENYE SHULE ZA MUSOMA VIJIJINI

Usisahau kutembelea Tovuti ya Jimbo letu ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumanne, 8.3.2023