MWENGE WA UHURU MUSOMA VIJIJINI: HUDUMA ZA AFYA ZAENDELEA KUBORESHWA NA KUIMARISHWA

pichaKiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndugu Abdalla Shaibu Kaim na Timu yake yote wameipongeza sana Serikali na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa michango mikubwa ya kifedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo Musoma Vijijini.

Vilevile, Wananchi na Viongozi wao wa Chama na Serikali wa Musoma Vijijini wamepongezwa sana kwa kazi nzuri wazifanyazo kwenye utekelezaji ya miradi ya maendeleo ya vijijini mwao.

Jimbo la Musoma Vijijini lina jumla ya Kata 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374.

Wanavijiji na Viongozi wao mbalimbali wanaendelea kushirikiana na Serikali kujenga na kuboresha miundombinu ya utoaji wa Huduma za Afya kwenye maeneo yao ya vijijini, kama ifuatavyo:

(I) Hospitali ya hadhi ya Wilaya (1):
*Inaendelea kujengwa kwenye Kitongoji cha Kwikonero, Kijijini Suguti. Huduma ndogo ndogo (OPD) zimeanza kutolewa hapo.

(II) Vituo vya Afya (6):
*Vituo vya Afya vinavyotoa Huduma za Afya ni vitatu (3) - Murangi, Mugango na Bugwema

*Vituo vipya vya Afya vinavyosubiri kupewa wafanyakazi na vifaa tiba ni vitatu (3) - Makojo, Kiriba na Kisiwani Rukuba (inatoa huduma kwa hadhi ya Zahanati)

(III) Zahanati (41):
*Zahanati zinazotoa Huduma za Afya ni ishirini na nne (24) - Bugoji, Bugunda, Bukima, Busungu, Bwai Kwitururu, Chitare, Etaro, Kiemba, Kigera Etuma, Kiriba, Kome, Kurugee, Kwikuba, Masinono, Mayani, Mmahare, Mwiringo, Nyakatende, Nyambono, Nyegina, Rusoli, Seka, Suguti na Wanyere

*Zahanati Binafsi zinatoa Huduma za Afya ni nne (4) - Bwasi (SDA), Mji wa Huruma (Katoliki), Kwibara (KMT) na Rwanga (KMT)

*Zahanati Mpya zinazojengwa ni kumi na tatu (13) - Burungu, Butata, Chanyauru, Chimati, Chirorwe, Kaburabura, Kakisheri, Kurukerege, Kurwaki, Maneke, Mkirira, Nyambono na Nyasaungu

(IV) Magari ya kusafirisha Wagonjwa (Ambulances)
*Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ameleta na kugawa magari matano (5) ya Wagonjwa kama ifuatavyo: Kituo cha Afya cha Murangi (ambulance kubwa ya kisasa), Zahanati za vijiji vya Masinono (sasa Kituo cha Afya cha Bugwema), Kurugee, Nyakatende na Mugango (sasa Kituo cha Afya cha Mugango)

Mwenge wa Uhuru Kijijini Kurwaki
Jana, Jumatatu, 10.7.2023, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndugu Abdalla Shaibu Kaim aliweka Jiwe la Msingi kwenye Zahanati ya Kijiji cha Kurwaki iliyoanza kujengwa na Wananchi wa Kijiji hicho wakishirikiana na Mbunge wa Jimbo, Madiwani na Viongozi wao wengine.

Serikali imeanza kuchangia kwa kutoa Tsh Milioni 50 kwenye ujenzi wa Zahanati hii.

Mwenge wa Uhuru Jimboni mwetu:
*Mkuu wa Wilaya (DC) yetu, Dr Khalifan Haule na Mwenyekiti wa CCM Wilaya yetu, Ndugu Denis Ekwabi, na Timu zao, wanapongezwa sana kwa kusimamia na kuratibu mbio za Mwenge Jimboni mwetu kwa mafanikio makubwa sana - Ahsanteni sana!

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumanne, 11.7.2023