WANANCHI WA KITONGOJI CHA GOMORA WAAMUA KUONGEZA KASI KWENYE UJENZI WA SHULE SHIKIZI YAO

Kitongoji cha Gomora ni moja ya vitongoji vitatu (3) vya Kijiji cha Musanja, Kata ya Musanja

Vitongoji hivi vitatu (3) vinayo Shule ya Msingi moja iliyojengwa Mwaka 1959 na Kanisa la Mennonite. Shule hiyo (S/M Musanja) kwa sasa ni ya Serikali.

Matatizo makuu yanayowakabili wanafunzi wa S/M Musanja:

*Umbali mrefu wa kutembea kwenda masomoni
*Mirundikano ya wanafunzi kwenye vyumba vya madarasa
*Uchakavu wa miundombinu ya shule iliyofunguliwa Mwaka 1959

Kitongoji cha Gomora chaamua kujenga Shule Shikizi
*Ujenzi wa awali umekamalisha vyumba viwili vya madarasa, ofisi moja ya walimu na choo chenye matundu 6.

Harambee ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, kwa kushirikiana na Kamati ya Siasa ya Wilaya (CCM) iliyopigwa Ijumaa, 29.9.2023 ilikuwa ya mafanikio ya kuridhisha kwa kupata:

*Saruji Mifuko 150, ikiwemo 100 ya Mbunge wa Jimbo na 10 ya Diwani
*Tsh milioni 3 za Halmashauri yetu
*Fedha taslimu Tsh 306,000 zikiwemo Tsh 105,000 za Walimu Makada wa CCM
*Mchanga tripu 3

ELIMU NI KIPAUMBELE CHETU CHA KWANZA KABISA, TAFADHALI NJOO TUCHANGIE UJENZI WA GOMORA SHULE SHIKIZI YA KIJIJI CHA MUSANJA

Wana-Gomora waliahidi kuanza ujenzi leo, na kweli wamefanya hivyo - picha ya hapa inaonesha uchimbaji wa msingi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi ya walimu.

CLIP/VIDEO ya hapa ni kutoka Kitongojini Gomora, tafadhali isikilize.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatatu, 2.10.2023