UJENZI WA SEKONDARI MPYA UNAENDELEA MUSOMA VIJIJINI: KISIWA CHA RUKUBA KIMEANZA UJENZI WA SEKONDARI YAKE

Mwanzo wa ujenzi wa Sekondari ya Kisiwa cha Rukuba - ujenzi wa msingi wa mawe wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja ya walimu.

Jimbo la Musoma Vijijini lina Kata 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374.

Jimbo hili lina jumla ya Sekondari:
*25 za Kata (Serikali)
*2 za Binafsi (Katoliki & SDA)

Sekondari mpya tano (5) zinajengwa kwenye vijiji vitano - Kisiwa cha Rukuba (Kata ya Etaro), Nyasaungu (Kata ya Ifulifu), Kurwaki (Kata ya Mugango), Muhoji (Kata ya Bugwema), na Wanyere (Kata ya Suguti, serikali inagharamia ujenzi).

Sekondari ya Kisiwa cha Rukuba
Wakazi wa Kisiwa cha Rukuba wameamua kujenga sekondari yao ili elimu ya sekondari itolewe hapo Kisiwani badala ya wanafunzi kwenda kupanga vyumba nchi kavu (Kijijini Etaro) kwa ajili ya elimu yao ya sekondari.

Harambee ya kwanza ya ujenzi wa Sekondari ya Kisiwa cha Rukuba ilishafanyika chini ya usimamizi wa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, akishirikiana na Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Musoma Vijijini.

Ujenzi umeanza
*matofali 2,900 tayari yametengenezwa: kila mfuko mmoja (1) wa saruji umetoa matofali 25

*ujenzi wa vyumba viwili na ofisi moja ya walimu umeanza - msingi wa mawe unajengwa (angalia picha za hapa)

Tafadhali sana tunaomba mchango wako:
*Akaunti ya kuweka mchango wako wa fedha ni:
Benki: NMB
Akaunti Namba: 30302300701
Jina la Akaunti:
Serikali ya Kijiji cha Rukuba

Wakazi wa Kisiwa cha Rukuba wamedhamiria kujenga Sekondari kisiwani humo ili kuboresha upatinakaji wa elimu ya sekondari kwa watoto wao - tuwaunge mkono!

Mchango wa Mbunge wa Jimbo
*Prof Sospeter Muhongo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini ameishachangia Saruji Mifuko 100

*Mbunge huyo anatoa tena Saruji Mifuko 50, itakayochukuliwa leo, na ataendelea kuchangia ujenzi huo.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatano, 1.11.2023