Tarehe 12.1.2024 Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo aliendesha HARAMBEE iliyolenga kukamilisha kazi ya upauaji wa boma la Shule Shikizi Kiunda ya Kijijini Kamguruki, Kata ya Nyakatende.
Boma hilo (picha imeambatanishwa hapa) ni la vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja ya walimu. Boma limejengwa kwa michango ya Wana-Kitongoji cha Kiunda, Diwani wa Kata na Mbunge wa Jimbo.
Ujenzi wa Shule Shikizi Jimboni mwetu
Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 zenye vijiji 68 na vitongoji 374 ina shule za msingi zenye idadi ifuatayo:
*111 shule za Serikali
*4 shule Binafsi
*12 shule shikizi zinazopanuliwa
Harambee ya Shule Shikizi Kiunda
*Gharama zote za upauaji:
Tsh 4,268,000
*Fedha zilizopatikana kwenye Harambee:
Tsh 1,285,000. Wachangiaji:
(i) Wakazi wa Kijiji cha Kamguruki
(ii) Wakazi kutoka Vijiji jirani
(iii) DEO Hamisi Shemahonge
(iv) Viongozi wa Chama Wilaya & Jumuiya zake ambao ni Ndg Jackson Nyakia, Ndg William Magero, Ndg Bwire Mkuku na Ndg Sophia Maregesi
*Mabati yaliyopatikana kwenye Harambee:
(i) Ndg Pascal Maganga: Mabati 24
(ii) Diwani Mhe Kisha Marere: Mabati 36
(iii) Mbunge Prof Muhongo: Mabati 72
Ratiba ya upauaji
*Tarehe 23.2.2024
Mbao za paa (kenji) zianze kuwekwa
*Tarehe 24.2.2024
Mabati yaanze kuwekwa (kuezeka)
Kaimu Mtendaji wa Kijiji (VEO), Ndg Magreth Malima anapewa pongezi nyingi za usimamiaji mzuri wa shughuli za maendeleo ndani ya Kijiji cha Kamguruki
MICHANGO INAKARIBISHWA SANA
Wana-Kitongoji cha Kiunda, na Kata ya Nyakatende kwa ujumla wanaendelea kuomba michango kutoka vyanzo mbalimbali ili kujenga na kupanua Shule Shikizi Kiunda iwe Shule ya Msingi kamili, inayojitegemea.
Tuma mchango wako wa fedha kwenye Akaunti ya Kijiji cha Kamguruki.
Akaunti ya Benki:
Benki: NMB
Akaunti Na: 30302300679
Jina la Akaunti: Kijiji cha Kamguruki
Pichani:
Wakazi wa Kitongoji cha Kiunda na Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Harambee iliyofanyika kwenye eneo la ujenzi wa Shule Shikizi Kiunda ya Kijijini Kamguruki, Kata ya Nyakatende, Musoma Vijijini.
TUENDELEE KUBORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU YA MUSOMA VIJIJINI
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Jumanne, 16.1.2024