WANAKIJIJI WAANZA UJENZI WA “DAVID MASSAMBA MEMORIAL SECONDARY SCHOOL”

Wakazi wa Kijiji cha Kurwaki, Kata ya Mugango wameanza ujenzi wa "David Massamba Memorial Secondary School."

Sekondari hii ambayo itakuwa ya pili kwa Kata ya Mugango inajengwa ikiwa imepewa jina la Marehemu Prof David Massamba, mzaliwa wa Kijiji cha Kurwaki, na aliyekuwa bingwa wa mabingwa wa lugha ya Kiswahili.

Kazi kubwa za ustawishaji wa Lugha ya Kiswahili zilizofanywa na Marehemu Prof David Massamba, kwa kushirikiana na Wataalamu wenzake, ni pamoja na:

*Kuandika vitabu vinavyotumika Vyuo Vikuu na Sekondari (Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu)
*Uandishi wa Kamusi ya Kiswahili

Michango ya awali ya ujenzi:
(i) Wanakijiji: Tsh 1,870,000
(ii) Familia Massamba: Tsh 800,000
(iii) Wazaliwa 2 wa Kurwaki: Tsh 750,000
(Dr Rukonge Manoko & Ndg Kawawa Jackson)
(iv) Diwani wa Kata: Tsh 200,000
(v) Wazazi wa Kijiji jirani, Kiriba: Tsh 80,000
(vi) Walimu Makada: Tsh 70,000

Michango ya Mbunge wa Jimbo:
(i) Binafsi: Saruji Mifuko 250
(ii) Mfuko wa Jimbo: Saruji Mifuko 205

Akaunti ya Kijiji ya kutuma michango:
Benki: NMB
Akaunti Na: 30302301539
Jina: Kijiji cha Kurwaki

Tafadhali tunaomba tuendelee kuchangia ujenzi wa Sekondari hii ambayo itakuwa ni kumbukumbu nzuri ya kuenzi kazi nyingi na muhimu sana alizozifanya Marehemu Prof David Massamba kwenye ukuzaji na usitawishaji wa Lugha ya Kiswahili kitaifa na kimataifa.

Picha za hapa zinaonesha:
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo akiwa na wanakijiji wa Kurwaki kwenye eneo la ujenzi wa, "David Massamba Memorial Secondary School." Hiyo ilikuwa Jumatano, 20.3.2024.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatano, 27.3.2024