SHEREHE ZA MUUNGANO: VIONGOZI WA WILAYA WAPANDA MICHE YA MITI NA KUFANYA USAFI KIJIJINI KIGERA

Leo, Watanzania wote tunasherehekea kwa furaha na amani tele ya miaka sitini (60) ya Muungano wetu.

Jimbo la Musoma Vijijini lilikua na ratiba ya siku kadhaa za kupanda miti na kufanya usafi sehemu mbalimbali za vijijini mwetu ikiwa ni sehemu ya Sherehe za Muungano.

Tunamshukuru sana Mkuu wa Wilaya (DC) yetu ya Musoma, Mhe Dkt Khalfany Haule kwa kusimamia na kuongoza vizuri sana matukio yote ya sherehe za Muungano wilayani mwetu.

Shule ya Msingi Ekungu, Kijijini Kigera (Etuma), Kata ya Nyakatende:

Mhe DC wetu aliongoza upandaji wa miche ya miti ya matunda, mbao na kivuli kwenye shule hii.

Vilevile, kila mwafunzi aligawiwa miche mitatu ya kupanda na kutunza kwenye maeneo ya nyumbani kwao.

CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa ni ya matukio mbalimbali yaliyofanyika S/M Ekungu - tafadhali wasikilize wanakijiji wanayoyasema, hasa shukrani zilizotolewa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Ijumaa, 26.4.2024