KISIWA CHA RUKUBA CHADHAMIRIA KUFUNGUA SEKONDARI YAKE MWAKANI (JANUARI 2025)

Kisiwa cha Rukuba cha Jimbo la Musoma Vijijini kimedhamiria kukamilisha miundombinu ya elimu ya awali ya kukiwezesha kuwa na sekondari yake ifikapo Januari 2025.

Kisiwa hiki kinayo Shule ya Msingi moja yenye maktaba na nyumba za walimu za kutosheleza mahitaji yao.

Vilevile, Kisiwa hiki kimechangiwa kwa kiasi kikubwa na Serikali yetu kukamilisha Kituo cha Afya hapo Kisiwani. Sasa kinajenga sekondari yake

Ujenzi wa Rukuba Sekondari:
Ujenzi ulianza kwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo kwenda hapo Kisiwani kuhamasisha na kuanza kuchangia ujenzi kupitia Harambee aliyoipiga hapo Kisiwani.

Michango ya awali ya kuanza ujenzi imetolewa na wafuatao:
(i) Wakazi wa Kisiwa cha Rukuba na Wadau wao wa Maendeleo:
+Fedha taslimu: Tsh 1,708,000
+Saruji Mifuko 72
+Kokoto: Tsh 804,000
+Fedha za Fundi: Tsh 2,300,000
+Fundi wa Matofali: Tsh 500,000
+Nondo
+Nguvukazi: mchanga, maji, kuchimba msingi
(ii) Viongozi wa Wilaya:
+DC Dkt Khalfany Haule: Tsh 500,000
+DED Nitu Palela: Saruji Mifuko 20
(ii) Mbunge wa Jimbo
+Saruji Mifuko 150 (bado 50)
+Saruji Mifuko 205 (Mfuko wa Jimbo)

Ujenzi wa Sekondari mpya Jimboni mwetu:
Jimbo letu lenye Kata 21 zenye jumla ya vijiji 68, lina jumla ya Sekondari 28 (26 za Kata na 2 za Binafsi).

(i) Sekondari mpya zinazojengwa kwa wakati huu vijijini mwetu(4): Nyasaungu, Muhoji, Kisiwani Rukuba na Kurwaki. Muhoji imeanza kupokea fedha kutoka Serikalini (Tsh 75m) - tunajitahidi sekondari hizi zote zifunguliwe mwakani (Januari 2025)

(ii) Ujenzi wa Sekondari mpya kwa kutumia fedha za Serikali Kuu utaanza hivi karibuni (2): Kata ya Nyamrandirira (Kijijini Kasoma) na Kata ya Bukima (Kijijini Butata). Hizi zitafunguliwa Januari 2025.

(iii) Ujenzi wa Maabara:
Ujenzi maabara 3 za masomo ya sayansi kwa kila Sekondari ya Kata unaendelea. Ujenzi huu unafanikishwa kwa michango kutoka Serikalini, na kutoka kwa wanavijiji na viongozi wao.

(iv) Sekondari mpya zitakazoanzwa kujengwa kwa kutumia michango ya wananchi (4):
Wanavijiji wamemuomba Mbunge wao wa Jimbo akapige Harambee za kuanza ujenzi wa sekondari mpya kwenye vijiji vifuatavyo: Mmahare, Kiriba, Kataryo na Chitare. Kazi hii amekubali kuifanya (Julai-Agosti 2024)

Michango kutoka kwa Wazaliwa na Musoma Vijijini na Wadau wetu wa Maendeleo:
Tunaombwa tuanze na tuendelee kuchangia maendeleo na ustawi wa ndugu zetu wa Musoma Vijijini - karibuni tuungane pamoja kivitendo!

Picha kutoka Kisiwani Rukuba:
Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa miundombinu ya awali ya Sekondari ya Kisiwa cha Rukuba kilichopo Kata ya Etaro, Musoma Vijijini

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumapili, 30.6.2024