Kata ya Tegeruka ina vijiji vitatu na sekondari moja ya Kata iliyojengwa Kijijini Tegeruka.
Wanafunzi wa sekondari kutoka vijiji vya Mayani na Kataryo wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilomita tano kwenda masomoni Kijijini Tegeruka.
Kijiji cha Kataryo kimeamua kujenga sekondari kwa malengo makuu mawili:
(i) kutatua tatizo la umbali wa kwenda masomoni na mirundikano ya wanafunzi madarasani
(ii) kuongeza miundombinu ya elimu ya sekondari kuendana na mabidiliko ya mfumo wa elimu nchini mwetu.
Kikao cha Mbunge wa Jimbo na Wanakijiji (tarehe 13.8.2024):
(i) Kero za wanakijiji ziliwasilishwa na Mbunge wa Jimbo alitoa majibu yenye kukubalika kwa wenye kero.
Tatizo sugu la maji litatuliwa hivi karibuni baada ya Mkandarasi anaejenga mtandao wa usambazaji maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria kulipwa fedha za kukamilisha kazi zake
(ii) Wanakijiji wanaendelea kuwasiliana na Halmashauri yetu (Musoma DC) ili kupewa nyaraka za umiliki wa eneo litakalojengwa sekondari
(ii) Ifikapo tarehe 30.8.2024, Wanakijiji watakuwa wamekalisha masuala ya ardhi, Kamati ya Ujezi itakuwa imeundwa, na michango itakuwa imeanza kuchangwa
(iii) Mbunge wa Jimbo atapiga Harambee ya ujenzi wa sekondari hiyo kabla ya tarehe 30.9.2024. Ujenzi utaanza kabla ya tarehe hii.
KARIBUNI TUCHANGIE UJENZI WA KATARYO SEKONDARI - SEKONDARI YA PILI YA KATA YA TEGERUKA
Viambatanisho vya hapa:
Vipande vifupi vya ngoma ya ki-Sukuma. Jimbo la Musoma Vijijini lina mchanganyiko wa makabila takribani kumi.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Jumapili, 18.8.2024