Busumi Fishing Cooperative Society (Chama cha Ushirika cha Wavuvi wa Kitongoji cha Busumi) kimechukua mkopo nafuu, usiokuwa na riba, kutoka Serikalini kwa ajili ya uvuvi wa vizimba ndani ya Ziwa Victoria.
Ushirika huu wa wanachama 20 umekopa Tsh milioni 117 kwa ajili ya kupata vizimba vinne (4), vifaranga vya samaki, chakula na bima ya ufugaji wao wa samaki.
Wataalamu wa usukaji wa visimba wamekamilisha kazi zao na jana vizimba vilipelekwa ndani ya maji (Ziwa Victoria) eneo la Kijijini Suguti.
Uvuvi wa vizimba, kwa upande wa Jimbo la Musoma Vijijini, umeanza kwa mafanikio mazuri maeneo ya Vijiji vya Kigera (Etuma), Bwai Kwitururu na Suguti. Wavuvi wa maeneo mengine wamehamasika sana na wanajitayarisha kutuma Serikalini maombi ya mikopo ya uvuvi wa vizimba!
Shukrani:
Wavuvi wa Musoma Vijijini wanaishukuru sana Serikali yetu chini cha uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia mikopo mizuri isiyokuwa na riba, na kwa kuboresha uvuvi wao kwa kuufanya wa kisasa wenye mapato makubwa!
Picha zilizoambatanishwa hapa:
Vizimba vya Chama cha Ushirika cha Kitongoji cha Busumi cha Musoma Vijijini vikiwekwa ndani ya Ziwa Victoria vikiwa tayari kwa kuanza kufuga samaki.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Jumanne, 20.8.2024