Kata ya Tegeruka yenye vijiji vitatu vya Kataryo, Mayani na Tegeruka itatumia maji ya bomba kutoka kwenye Bomba Kuu la Mugango-Kiabakari-Butiama lilojengwa kwa gharama ya Tsh bilioni 70.5 (Tsh 70.5b).

Chanzo cha maji ya bomba hili kiko Kijijini Kwibara, Kata ya Mugango, Musoma Vijijini. Mitambo iliyojengwa kwenye chanzo hicho ina uwezo wa kuzalisha maji ya ujazo wa lita milioni 35 kwa siku (Lita 35m/siku)

Mradi wa zaidi ya Tsh bilioni 4 (Tsh 4b) wa kusambaza maji ndani ya Kata ya Tegeruka umepangwa ukamilike ndani ya mwezi miwili ijayo.

Ujenzi wa Tenki la ujazo wa lita 150,000 unakamilishwa Kijijini Mayani kwa ajili ya usambazaji wa maji ndani ya Kata ya Tegeruka - angalia picha iliyoambatanishwa hapa.

Mabomba ya awali ya kusambazia maji ndani ya vijiji vyote vitatu yameishatandazwa.

Bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama:

Maji kutoka kwenye bomba hili yameanza kutumiwa ndani ya Kata ya Mugango yenye vijiji vitatu. Kijiji cha Nyasaungu cha Kata ya Ifulifu nacho kinatumia maji ya bomba hili.

Miundombinu ya usambazaji wa maji ya bomba inajengwa ndani ya Kata za Busambara (vijiji vitatu) na Kiriba (vijiji vitatu) kwa ajili ya kutumia maji kutoka kwenye bomba hilo.

Vijiji vyote 68 vya Jimboni mwetu vina miradi ya maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria. Miradi hii iko kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji.

Visima virefu vya maji vinachimbwa kwa baadhi ya vijiji vya Kata ya Bugwema ambavyo miradi ya maji kutoka Ziwa Victoria itachelewa kuanza kutekelezwa.

Hadi leo hii, vijiji 54 kati ya vijiji 68 vya Jimboni mwetu (77.94% ya vijiji vyote) vinatumia maji ya bomba yanayotolewa Ziwa Victoria - MAFANIKIO MAKUBWA SANA YA SERIKALI YETU!

Picha iliyoambatanishwa hapa inaonesha:
Tenki la maji ya ujazo wa lita 150,000 linalojengwa Kijijini Mayani, Kata ya Tegeruka, Musoma Vijijini

SHUKRANI:
Wananchi na viongozi wote wa Jimbo la Musoma Vijijini tunaendelea kuishukuru sana Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutupatia fedha nyingi za miradi ya maendeleo, ikiwemo ya usambazaji wa maji safi na salama ya bomba, vijijini mwetu.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumamosi, 28.9.2024vvv