Kijiji cha Nyasaungu chenye vitongoji vitano (5) kinakamilisha ujenzi wa zahanati yake ambayo inatarajiwa kuanza kutoa Huduma za Afya ifikapo Disemba 2024
Kijiji hiki ni moja ya vijiji vitatu vya Kata ya Ifulifu. Vijiji vingine ni Kabegi na Kiemba ambavyo kila kimoja kina zahanati yake.
Kwa hiyo, ifikapo Disemba 2024, kila kijiji ndani ya Kata ya Ifulifu kitakuwa na zahanati yake! Hatua kubwa sana ya maendeleo kwenye Kata hii!
Vyanzo vya fedha za ujenzi wa Zahanati ya Nyasaungu:
(i) ujenzi ulianza kwa kutumia michango ya fedha kutoka kwa wanakijiji na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo.
Mbunge huyo alipiga Harambee mbili za kupata fedha za kuanza ujenzi wa zahanati hiyo
Wanakijiji wanachangia nguvukazi kwenye ujenzi wa zahanati yao.
(ii) Fedha kutoka Serikali Kuu (Tsh 100m)
Hadi sasa, Serikali Kuu imechangia jumla ya Shilingi Milioni 100 (Tsh 100m).
Ukamilishwaji wa ujenzi:
*Jengo kuu la Zahanati linakamilishwa
*Choo chenye matundu matatu kinajengwa
Mkandarasi amepewa mkataba wa kukamilisha ujenzi wa Zahanati hii (jengo kuu na choo) unaoishia tarehe 30 Novemba 2024.
Huduma muhimu zaendelea kuimarika Kijijini Nyasaungu:
Kujitolea kwa wanakijiji wa Nyasaungu kunaharakisha maendeleo ya kijiji chao:
(i) Shule ya Msingi ipo
(ii) Sekondari inajengwa na imepangwa kufunguliwa mwakani, 2025
(iii) Zahanati inajengwa na imepangwa kufunguliwa Disemba 2024
Serikali inaendelea kuwasambazia maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria, na umeme wa REA.
SHUKRANI:
Wanakijiji wa Nyasaungu na viongozi wao wa ngazi zote wanaishukuru sana Serikali yetu, chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kutoa fedha za kuchangia miradi ya maendeleo ya Kijiji cha Nyasaungu cha Jimbo la Musoma Vijijini
Picha 2 zilizoambatanishwa hapa:
(i) Jengo la Zahanati ya Kijiji cha Nyasaungu likiwa kwenye hatua za ukamilishwaji
(ii) Boma la choo cha Zahanati ya Kijiji cha Nyasaungu likiwa linajengwa
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O Box 6
Musoma
Tarehe:
Jumatatu, 18.11.2024