ZAHANATI INAYOJENGWA KIJIJINI NYASAUNGU KUANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA MWEZI DISEMBA 2024

Kijiji cha Nyasaungu chenye vitongoji vitano (5) kinakamilisha ujenzi wa zahanati yake ambayo inatarajiwa kuanza kutoa Huduma za Afya ifikapo Disemba 2024

Kijiji hiki ni moja ya vijiji vitatu vya Kata ya Ifulifu. Vijiji vingine ni Kabegi na Kiemba ambavyo kila kimoja kina zahanati yake.

Kwa hiyo, ifikapo Disemba 2024, kila kijiji ndani ya Kata ya Ifulifu kitakuwa na zahanati yake! Hatua kubwa sana ya maendeleo kwenye Kata hii!

Vyanzo vya fedha za ujenzi wa Zahanati ya Nyasaungu:

(i) ujenzi ulianza kwa kutumia michango ya fedha kutoka kwa wanakijiji na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo.

Mbunge huyo alipiga Harambee mbili za kupata fedha za kuanza ujenzi wa zahanati hiyo

Wanakijiji wanachangia nguvukazi kwenye ujenzi wa zahanati yao.

(ii) Fedha kutoka Serikali Kuu (Tsh 100m)
Hadi sasa, Serikali Kuu imechangia jumla ya Shilingi Milioni 100 (Tsh 100m).

Ukamilishwaji wa ujenzi:
*Jengo kuu la Zahanati linakamilishwa
*Choo chenye matundu matatu kinajengwa

Mkandarasi amepewa mkataba wa kukamilisha ujenzi wa Zahanati hii (jengo kuu na choo) unaoishia tarehe 30 Novemba 2024.

Huduma muhimu zaendelea kuimarika Kijijini Nyasaungu:

Kujitolea kwa wanakijiji wa Nyasaungu kunaharakisha maendeleo ya kijiji chao:

(i) Shule ya Msingi ipo

(ii) Sekondari inajengwa na imepangwa kufunguliwa mwakani, 2025

(iii) Zahanati inajengwa na imepangwa kufunguliwa Disemba 2024

Serikali inaendelea kuwasambazia maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria, na umeme wa REA.

SHUKRANI:
Wanakijiji wa Nyasaungu na viongozi wao wa ngazi zote wanaishukuru sana Serikali yetu, chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kutoa fedha za kuchangia miradi ya maendeleo ya Kijiji cha Nyasaungu cha Jimbo la Musoma Vijijini

Picha 2 zilizoambatanishwa hapa:
(i) Jengo la Zahanati ya Kijiji cha Nyasaungu likiwa kwenye hatua za ukamilishwaji

(ii) Boma la choo cha Zahanati ya Kijiji cha Nyasaungu likiwa linajengwa

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumatatu, 18.11.2024

MUSOMA VIJIJINI YAENDELEA KUJENGA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI KWENYE SEKONDARI ZAKE ZA KATA

Wanavijiji wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kushirikiana vizuri na Serikali yetu kujenga maabara za masomo ya sayansi kwenye sekondari zao za kata.

Malengo makuu ya ujenzi huo ni:

(i) kuongeza na kuboresha ufundishaji, uelewa na ufaulu mzuri kwenye mitihani ya masomo ya sayansi

(ii) kuongeza idadi ya "high schools" za masomo ya sayansi Jimboni mwetu

Idadi ya Sekondari Jimboni mwetu (Kata 21):

(i) Sekondari za Kata/Serikali: 26
(ii) Sekondari za Binafsi: 2
(iii) Sekondari mpya zinazojengwa: 10

Idadi ya high schools Jimboni mwetu:

(i) Kasoma High School: masomo ya "arts"
(ii) Suguti High School: masomo ya sayansi kuanzia mwakani, 2025
(iii) Mugango High School: masomo ya sayansi kuanzia mwakani, 2025

Sekondari zinazojenga kwa kasi miundombinu ya uanzishwaji wa "high schools" za masomo ya sayansi:

(iv) Mtiro Sekondari (v) Makojo Sekondari
(vi) Kiriba Sekondari (vii) Etaro Sekondari

Ujenzi wa miundombinu ya Elimu ya kuanzishwa kwa Mtiro High School:

Mtiro Sekondari ilifunguliwa Mwaka 2006, na kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 654.

Sekondari hii ni ya Kata ya Bukumi yenye vijiji vinne, ambavyo ni Buira, Bukumi, Buraga na Busekera.

Miundombinu inayojengwa kukidhi viwango vya kuanzishwa "high school" ya masomo ya sayansi ni:

(i) Maabara 3 za masomo ya Physics, Chemistry na Biology

Michango ya thamani ya Shilingi milioni 31 (Tsh 31m) - Wachangiaji: Wanakijiji, Mbunge wa Jimbo, Mfuko wa Jimbo na Halmashauri yetu (Musoma DC)

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, alipiga Harambee mbili (2) za kuanza ujenzi wa maabara hizo.

(ii) Bweni la Wanafunzi
Mchango wa Shilingi milioni 131.4 (Tsh 131.4m) - Mchangiaji: Serikali Kuu

(iii) Vyumba vipya 4 vya Madarasa
Mchango wa Shilingi milioni 100 (Tsh 100m) - Mchangiaji: Serikali Kuu

(iv) Vyoo vipya
Mchango: Shilingi milioni 24.9 (Tsh 24.9m) - Mchangiaji: Serikali Kuu

(v) Maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria: yapo

(vi) Umeme wa REA/TANESCO: upo

Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha:
(i) Maboma ya maabara ya masomo ya sayansi yanayojengwa Mtiro Sekondari

(ii) Vyumba vipya vya Madarasa vinavyojengwa Mtiro Sekondari

SHUKRANI:
Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini na viongozi wao wote wanaishukuru sana Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuchangia ujenzi wa miundombinu ya elimu kwenye sekondari zao za Kata, na kuongeza idadi ya "high schools", hasa za masomo ya sayansi Jimboni mwetu.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumanne, 19 Nov 2024

PROF MUHONGO AMEJIANDIKISHA KUPIGA KURA TAREHE 27.11.2024

Leo, Ijumaa, 11.10.2024, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, amejiandikisha kupiga kura tarehe 27.11.2024.

Vilevile, ametembelea vitongoji kadhaa vya Kata nne, ikiwemo Kata ya kwao ya Kiriba, yenye vijiji 3 na vitongoji 24, na kupata yafuatayo:

(i) Idadi ya wapiga kura waliojiandikisha ndani ya Kata ya Kiriba kwa siku ya leo: 1,856

(ii) Idadi ya wapiga kura waliojiandikisha kwenye Kitongoji cha Miembeni (Kituo cha Afya), Kijiji cha Bwai Kwitururu
Kufikia saa 6 mchana: 22
Kufikia saa 12 jioni: 50
Prof Sospeter Muhongo amejiandikisha hapo

Uhamasishaji:
Wananchi waendelee kuhamasishwa kujitokeza kujiandikisha kupiga kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa tarehe 27.11.2024

Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha:

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, akijiandikisha kupiga kura, na kutembelea vituo kadhaa vya uandikishaji wapiga kura ndani ya kata nne za Musoma Vijijini.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Ijumaa, 11.10.2024

PROF.MUHONGO AMUENZI BABA WA TAIFA HAYATI MWALIMU NYERERE,AWACHANGIA VIJANA KATONI 200 ZA MAJI YA KUNYWA

PROF.MUHONGO AMUENZI BABA WA TAIFA HAYATI MWALIMU NYERERE,AWACHANGIA VIJANA KATONI 200 ZA MAJI YA KUNYWA KWA AJILI YA MATEMBEZI YAO KUANZIA WILAYANI BUTIAMA MKOA WA MARA HADI MKOA WA MWANZA KATIKA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2024 NA KUMBUKUMBU YA MIAKA 25 YA KIFO CHA MWALIMU NYERERE.

Leo tarehe 9.10.2024 Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof Sospeter Muhongo amewatambelea vijana katika ufunguzi wa wiki yao Kitaifa uliofanyika Wilaya ya Butiama Mkoani Mara.

Katika hatua nyingine Prof.Muhongo amepata nafasi ya kuwasalimia vijana hao na kumuelezea kwa kifupi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika historia ya ujenzi wa Taifa la Tanzania na Chama cha Mapinduzi CCM.
Pia amewachangia katoni 200 za maji ya kunywa vijana hao zidi ya 600 ili ziwasaidie njiani katika kumuenzi Baba wa Taifa wakielekea Mkoani Mwanza.

Katika uzinduzi huo Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Bi.Rehema Sombi alikuwa Mgeni Rasmi akiongozana na Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Bi Jokate Mwegelo.

Tunazima zote tunawasha kijani.

MRADI WA MAJI YA BOMBA WA KATA YA TEGERUKA: MKANDARASI KUONGEZA KASI YA KUKAMILISHA MRADI HUU

Kata ya Tegeruka yenye vijiji vitatu vya Kataryo, Mayani na Tegeruka itatumia maji ya bomba kutoka kwenye Bomba Kuu la Mugango-Kiabakari-Butiama lilojengwa kwa gharama ya Tsh bilioni 70.5 (Tsh 70.5b).

Chanzo cha maji ya bomba hili kiko Kijijini Kwibara, Kata ya Mugango, Musoma Vijijini. Mitambo iliyojengwa kwenye chanzo hicho ina uwezo wa kuzalisha maji ya ujazo wa lita milioni 35 kwa siku (Lita 35m/siku)

Mradi wa zaidi ya Tsh bilioni 4 (Tsh 4b) wa kusambaza maji ndani ya Kata ya Tegeruka umepangwa ukamilike ndani ya mwezi miwili ijayo.

Ujenzi wa Tenki la ujazo wa lita 150,000 unakamilishwa Kijijini Mayani kwa ajili ya usambazaji wa maji ndani ya Kata ya Tegeruka - angalia picha iliyoambatanishwa hapa.

Mabomba ya awali ya kusambazia maji ndani ya vijiji vyote vitatu yameishatandazwa.

Bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama:

Maji kutoka kwenye bomba hili yameanza kutumiwa ndani ya Kata ya Mugango yenye vijiji vitatu. Kijiji cha Nyasaungu cha Kata ya Ifulifu nacho kinatumia maji ya bomba hili.

Miundombinu ya usambazaji wa maji ya bomba inajengwa ndani ya Kata za Busambara (vijiji vitatu) na Kiriba (vijiji vitatu) kwa ajili ya kutumia maji kutoka kwenye bomba hilo.

Vijiji vyote 68 vya Jimboni mwetu vina miradi ya maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria. Miradi hii iko kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji.

Visima virefu vya maji vinachimbwa kwa baadhi ya vijiji vya Kata ya Bugwema ambavyo miradi ya maji kutoka Ziwa Victoria itachelewa kuanza kutekelezwa.

Hadi leo hii, vijiji 54 kati ya vijiji 68 vya Jimboni mwetu (77.94% ya vijiji vyote) vinatumia maji ya bomba yanayotolewa Ziwa Victoria - MAFANIKIO MAKUBWA SANA YA SERIKALI YETU!

Picha iliyoambatanishwa hapa inaonesha:
Tenki la maji ya ujazo wa lita 150,000 linalojengwa Kijijini Mayani, Kata ya Tegeruka, Musoma Vijijini

SHUKRANI:
Wananchi na viongozi wote wa Jimbo la Musoma Vijijini tunaendelea kuishukuru sana Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutupatia fedha nyingi za miradi ya maendeleo, ikiwemo ya usambazaji wa maji safi na salama ya bomba, vijijini mwetu.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumamosi, 28.9.2024vvv

MUWASA YAENDELEA KUSAMBAZA MAJI YA BOMBA MUSOMA VIJIJINI

Mitambo iliyofungwa Bukanga, Musoma Mjini, kwa ajili ya kuzalisha maji kutoka Ziwa Victoria ina uwezo wa kuzalisha lita milioni 36 za maji kwa siku - haya ni maji mengi mno ukilinganisha na mahitaji ya maji ya kila siku ya Mji wa Musoma!

Tenki kubwa lenye ujazo wa lita milioni tatu (lita 3m) za maji limejengwa Mlimani Bharima (angalia picha iliyoambatanishwa hapa) kwa ajili ya usambazaji wa maji ya bomba ndani na nje ya Mji wa Musoma.

Serikali imeipa MUWASA jukumu la kusambaza maji ya bomba kutoka Tenki la Bharima kwenda vijiji jirani na Mji wa Musoma, vikiwemo vijiji vya Musoma Vijijini na Butiama.

Maji ya MUWASA kusambazwa Musoma Vijijini:

Kata ambazo zimepangwa kusambaziwa maji ya MUWASA ni nne, ambazo ni Kata ya Etaro (vijiji 3), Nyegina (vijiji 3), Nyakatende (vijiji 4) na Ifulifu (vijiji 3).

MUWASA wameishafanikiwa kusambaza maji ya bomba kwenye baadhi ya vijiji vya Kata ya Etaro (vijiji vya Busamba, Etaro na Mmahare) na Nyegina (kijiji cha Mkirira). Usambazaji unaendelea.

Bomba kuu la Nyegina linatandazwa:

Kazi ya kutandaza bomba kuu la maji kuelekea Nyegina Senta inafanyika wakati huu - angali picha zilizoambatanishwa hapa

Vilevile, tukumbuke kwamba baadhi ya vijiji vya Kata nne zilizotajwa hapo juu, vimeanza kutumia maji ya bomba kutoka vyanzo vilivyojengwa na RUWASA, na BADEA (maji kutoka Mugango).

Miradi ya maji ya bomba Jimboni mwetu:

Vijiji vyetu vyote 68 vina miradi ya maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria.

Vijiji 53 kati ya 68 vimeanza kutumia maji ya bomba (77.94% ya vijiji vyote), na vingine miradi yao iko kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji.

Vilevile, kuna vijiji vinachimbiwa visima virefu vya maji, na kazi hiyo inaendelea vizuri ndani ya Kata ya Bugwema.

Kazi nzuri na kubwa ya usambazaji wa maji ya bomba vijijini mwetu inafanywa na RUWASA, MUWASA, na BADEA (bomba la maji la Mugango-Kiabakari-Butiama).

Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha:
(i) Tenki la maji lenye ujazo wa lita milioni tatu (lita 3m). Limejengwa Mlimani Bharima

(ii) Utandazaji ya bomba kuu la maji kuelekea Nyegina Senta, Kata ya Nyegina, Musoma Vijijini.

SHUKRANI:
Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini na viongozi wao wote tunaendelea kuishukuru Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutupatia fedha nyingi za kutekeleza miradi ya maendeleo vijijini mwetu, ikiwemo miradi ya maji safi na salama ya bomba - Ahsante sana!

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumanne, 24.9.2024

OLDOINYO LENGAI : AN ACTIVE, NON-EXPLOSIVE VOLCANO ON THE GLOBAL GEOPARK NETWORK

The Oldoinyo Lengai volcano is in the Arusha region, about 15 km south of Lake Natron - a home of attractive flamingos!

Oldoinyo Lengai is a very attractive place to visit, both as a tourist and as a scientist. I have been there three times!

The last time of my visit, my leg was injured, and my Maasai friends gave me their traditional medicine (3-day treatment at the camp site). I took it with another causality, my friend from the Vienna Museum of Natural History, Austria.

The climb to the summit:

Due to the hydration problem, the climb begins at around midnight, walking along a single steep path (gradient above 75 degrees). It takes approximately 6 hours to reach the summit!

At the summit, one witnesses an active, very quiet carbonatitic volcanism.

In a simple language, Oldoinyo Lengai is a "white (carbonatite) volcano" that is different from the "black (basalt) volcano" of the Kilimanjaro Mountain. This "white volcano" makes it unique in the world!

Germans working and living in Deutsch-Ostafrika (1885-1918) visited Oldoinyo Lengai

The Maasai friends taught me a lot about the significance of their "God," the Oldoinyo Lengai

I first recommended Oldoinyo Lengai to be on the list of UNESCO's Worlds' Geoparks. I am glad today Oldoinyo Lengai is on that spectacular UNESCO Global Geoparks Network!

It was during my tenure of Chairmanship of UNESCO-IUGS-IGCP Scientific Board that we introduced the concept of geoparks and geosites. The Scientific Board began, in the late 90s, enlisting and providing UNESCO's certificates of recognition to such sites or parks. China leads the world!

Enjoy reading the article, sent to us, on Oldoinyo Lengai by clicking this link..(https://www.livescience.com/planet-earth/volcanos/mountain-of-god-volcano-in-tanzania-is-bulging-study-finds)

Sospeter Muhongo
Sunday, 22.9.2024

MIAKA HAMSINI YA KISIWA CHA RUKUBA: MAENDELEO NA USTAWI WAKE (1974-2024)

Kisiwa cha Rukuba kilitambuliwa na kupewa hadhi ya kijiji Mwaka 1974.

Kisiwa hiki ni moja ya vijiji vinne (4) vya Kata ya Etaro. Vijiji vingine ni: Busamba, Etaro na Mmahare.

Baadhi ya mafanikio yaliyopatikana ndani ya Miaka 50 ya Kisiwa cha Rukuba:

(1) kuwepo kwa Shule ya Msingi yenye vyumba vya madarasa vya kutosha na madawati ya kutosha.

(1a) Shule ina Ofisi mbili (2) za Walimu (Mwalimu Mkuu & Walimu wengine)

(2) kuwepo kwa Maktaba ya Shule ya Msingi

(3) Kila Mwalimu wa Shule ya Msingi kupewa nyumba ya kuishi ya shule

(4) kuwepo Kituo cha Afya kipya (Zahanati imepanuliwa na kuwa Kituo cha Afya). Tsh 500m (ujenzi) na Tsh 100 (vifaa tiba)

(5) Umemejua (solar) kutumiwa na baadhi ya wakazi wa hapo Kisiwani. Kampuni binafsi inauza umemejua.

Miradi mipya inayotekelezwa:
(5) Sekondari inajengwa kwa nguvu za wananchi na viongozi wao

(6) Umemejua unafungwa kwenye Kituo cha Afya. Huu ni Mradi wa REA wa Tsh 345m

(7) RUWASA itafunga miundombinu ya usambazaji wa maji safi na salama baada ya kuwepo umemejua mwingi na wenye uwezo mkubwa

SHUKRANI:
Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Alhamisi, 12.9.2024

WAVUVI WA MUSOMA VIJIJINI WAHAMASIKA KUCHUKUA MIKOPO NAFUU YA SERIKALI YA UVUVI WA VIZIMBA

Busumi Fishing Cooperative Society (Chama cha Ushirika cha Wavuvi wa Kitongoji cha Busumi) kimechukua mkopo nafuu, usiokuwa na riba, kutoka Serikalini kwa ajili ya uvuvi wa vizimba ndani ya Ziwa Victoria.

Ushirika huu wa wanachama 20 umekopa Tsh milioni 117 kwa ajili ya kupata vizimba vinne (4), vifaranga vya samaki, chakula na bima ya ufugaji wao wa samaki.

Wataalamu wa usukaji wa visimba wamekamilisha kazi zao na jana vizimba vilipelekwa ndani ya maji (Ziwa Victoria) eneo la Kijijini Suguti.

Uvuvi wa vizimba, kwa upande wa Jimbo la Musoma Vijijini, umeanza kwa mafanikio mazuri maeneo ya Vijiji vya Kigera (Etuma), Bwai Kwitururu na Suguti. Wavuvi wa maeneo mengine wamehamasika sana na wanajitayarisha kutuma Serikalini maombi ya mikopo ya uvuvi wa vizimba!

Shukrani:
Wavuvi wa Musoma Vijijini wanaishukuru sana Serikali yetu chini cha uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia mikopo mizuri isiyokuwa na riba, na kwa kuboresha uvuvi wao kwa kuufanya wa kisasa wenye mapato makubwa!

Picha zilizoambatanishwa hapa:
Vizimba vya Chama cha Ushirika cha Kitongoji cha Busumi cha Musoma Vijijini vikiwekwa ndani ya Ziwa Victoria vikiwa tayari kwa kuanza kufuga samaki.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumanne, 20.8.2024

WANAKIJIJI WA KATARYO WAAZIMIA KUJENGA SEKONDARI YAO MPYA NA WAWEKA RATIBA YA KAZI ZA UJENZI

Kata ya Tegeruka ina vijiji vitatu na sekondari moja ya Kata iliyojengwa Kijijini Tegeruka.

Wanafunzi wa sekondari kutoka vijiji vya Mayani na Kataryo wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilomita tano kwenda masomoni Kijijini Tegeruka.

Kijiji cha Kataryo kimeamua kujenga sekondari kwa malengo makuu mawili:

(i) kutatua tatizo la umbali wa kwenda masomoni na mirundikano ya wanafunzi madarasani

(ii) kuongeza miundombinu ya elimu ya sekondari kuendana na mabidiliko ya mfumo wa elimu nchini mwetu.

Kikao cha Mbunge wa Jimbo na Wanakijiji (tarehe 13.8.2024):

(i) Kero za wanakijiji ziliwasilishwa na Mbunge wa Jimbo alitoa majibu yenye kukubalika kwa wenye kero.

Tatizo sugu la maji litatuliwa hivi karibuni baada ya Mkandarasi anaejenga mtandao wa usambazaji maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria kulipwa fedha za kukamilisha kazi zake

(ii) Wanakijiji wanaendelea kuwasiliana na Halmashauri yetu (Musoma DC) ili kupewa nyaraka za umiliki wa eneo litakalojengwa sekondari

(ii) Ifikapo tarehe 30.8.2024, Wanakijiji watakuwa wamekalisha masuala ya ardhi, Kamati ya Ujezi itakuwa imeundwa, na michango itakuwa imeanza kuchangwa

(iii) Mbunge wa Jimbo atapiga Harambee ya ujenzi wa sekondari hiyo kabla ya tarehe 30.9.2024. Ujenzi utaanza kabla ya tarehe hii.

KARIBUNI TUCHANGIE UJENZI WA KATARYO SEKONDARI - SEKONDARI YA PILI YA KATA YA TEGERUKA

Viambatanisho vya hapa:
Vipande vifupi vya ngoma ya ki-Sukuma. Jimbo la Musoma Vijijini lina mchanganyiko wa makabila takribani kumi.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumapili, 18.8.2024

HUDUMA ZA AFYA NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Ukubwa wa Jimbo letu:
Kata 21 zenye vijiji 68 na vitongoji 374

Idadi ya hospitali, vituo vya afya na zahanati:

(1) Hospitali ya Halmashauri/Wilaya inayotoa Huduma za Afya (1)
+Imejengwa Kitongoji cha Kwikonero, Kijiji cha Suguti, Kata ya Suguti

(2) Vituo vya Afya vya Kata vinavyotoa Huduma za Afya (3):
(i) Kijijini Murangi, Kata ya Murangi
(ii) Kijijini Nyang'oma, Kata ya Mugango
(iii) Kijijini Bwai Kwitururu, Kata ya Kiriba

(3) Vituo vya Afya vya Kata vinavyosubiri kufunguliwa, vifaa vya matibabu vimeanza kupelekwa (3):
(i) Kijijini Makojo, Kata ya Makojo
(ii) Kijijini Masinono, Kata ya Bugwema
(iii) Kisiwani Rukuba, Kata ya Etaro

(4) Zahanati zinazotoa Huduma za Afya:
(i) 26 za Serikali
(ii) 4 za Binafsi

(5) Zahanati zinazojengwa kwa kutumia michango ya wanavijiji na wadau wao wa maendele ni 17

Baadhi ya zahanati hizi zimeanza kupokea michango ya fedha kutoka Serikalini - tunashukuru sana

Orodha yake inawekwa hapa ili kukaribisha michango kutoka kwa Wadau wetu wa Maendeleo, wakiwemo Wazaliwa wa Musoma Vijijini.

Ujenzi unafanyika ndani ya vijiji 17:
Bulinga, Burungu, Butata, Chanyauru, Chimati, Chirorwe, Kaburabura, Kakisheri, Kataryo, Kwikerege, Kurukerege, Kurwaki, Mabuimerafuru, Maneke, Nyabaengere, Nyambono na Nyasaungu

Picha iliyoambatanishwa hapa inaonesha:
Ujenzi wa boma la zahanati ya Kijiji cha Kataryo, Kata ya Tegeruka

ILANI YA UCHAGUZI YA CCM YA MWAKA 2020-2025 INATEKELEZWA VIZURI SANA NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI - karibuni tuchangie ujenzi wa zahanati mpya vijijini mwetu.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumamosi, 13.7.2024

KISIWA CHA RUKUBA CHADHAMIRIA KUFUNGUA SEKONDARI YAKE MWAKANI (JANUARI 2025)

Kisiwa cha Rukuba cha Jimbo la Musoma Vijijini kimedhamiria kukamilisha miundombinu ya elimu ya awali ya kukiwezesha kuwa na sekondari yake ifikapo Januari 2025.

Kisiwa hiki kinayo Shule ya Msingi moja yenye maktaba na nyumba za walimu za kutosheleza mahitaji yao.

Vilevile, Kisiwa hiki kimechangiwa kwa kiasi kikubwa na Serikali yetu kukamilisha Kituo cha Afya hapo Kisiwani. Sasa kinajenga sekondari yake

Ujenzi wa Rukuba Sekondari:
Ujenzi ulianza kwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo kwenda hapo Kisiwani kuhamasisha na kuanza kuchangia ujenzi kupitia Harambee aliyoipiga hapo Kisiwani.

Michango ya awali ya kuanza ujenzi imetolewa na wafuatao:
(i) Wakazi wa Kisiwa cha Rukuba na Wadau wao wa Maendeleo:
+Fedha taslimu: Tsh 1,708,000
+Saruji Mifuko 72
+Kokoto: Tsh 804,000
+Fedha za Fundi: Tsh 2,300,000
+Fundi wa Matofali: Tsh 500,000
+Nondo
+Nguvukazi: mchanga, maji, kuchimba msingi
(ii) Viongozi wa Wilaya:
+DC Dkt Khalfany Haule: Tsh 500,000
+DED Nitu Palela: Saruji Mifuko 20
(ii) Mbunge wa Jimbo
+Saruji Mifuko 150 (bado 50)
+Saruji Mifuko 205 (Mfuko wa Jimbo)

Ujenzi wa Sekondari mpya Jimboni mwetu:
Jimbo letu lenye Kata 21 zenye jumla ya vijiji 68, lina jumla ya Sekondari 28 (26 za Kata na 2 za Binafsi).

(i) Sekondari mpya zinazojengwa kwa wakati huu vijijini mwetu(4): Nyasaungu, Muhoji, Kisiwani Rukuba na Kurwaki. Muhoji imeanza kupokea fedha kutoka Serikalini (Tsh 75m) - tunajitahidi sekondari hizi zote zifunguliwe mwakani (Januari 2025)

(ii) Ujenzi wa Sekondari mpya kwa kutumia fedha za Serikali Kuu utaanza hivi karibuni (2): Kata ya Nyamrandirira (Kijijini Kasoma) na Kata ya Bukima (Kijijini Butata). Hizi zitafunguliwa Januari 2025.

(iii) Ujenzi wa Maabara:
Ujenzi maabara 3 za masomo ya sayansi kwa kila Sekondari ya Kata unaendelea. Ujenzi huu unafanikishwa kwa michango kutoka Serikalini, na kutoka kwa wanavijiji na viongozi wao.

(iv) Sekondari mpya zitakazoanzwa kujengwa kwa kutumia michango ya wananchi (4):
Wanavijiji wamemuomba Mbunge wao wa Jimbo akapige Harambee za kuanza ujenzi wa sekondari mpya kwenye vijiji vifuatavyo: Mmahare, Kiriba, Kataryo na Chitare. Kazi hii amekubali kuifanya (Julai-Agosti 2024)

Michango kutoka kwa Wazaliwa na Musoma Vijijini na Wadau wetu wa Maendeleo:
Tunaombwa tuanze na tuendelee kuchangia maendeleo na ustawi wa ndugu zetu wa Musoma Vijijini - karibuni tuungane pamoja kivitendo!

Picha kutoka Kisiwani Rukuba:
Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa miundombinu ya awali ya Sekondari ya Kisiwa cha Rukuba kilichopo Kata ya Etaro, Musoma Vijijini

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumapili, 30.6.2024

WANAVIJIJI WANAENDELEA NA UJENZI WA ZAHANATI ZA VIJIJI VYAO

Wanavijiji wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea na ujenzi wa zahanati za vijiji vyao kwa kushirikiana na Madiwani wao, na Mbunge wao wa Jimbo.

Jimbo la Musoma Vijijini lina Kata 21 zenye vijiji 68 na vitongoji 374. Kila kijiji kimedhamiria kujenga zahanati yake.

Utaratibu unaotumika ni huu hapa:
(i) Wanakijiji wanabuni mradi wa ujenzi wa zahanati ya kijiji chao, wanatayarisha eneo la ujenzi, na wanapewa ushauri kutoka kwa Mhandisi wa Halmashauri yetu (Musoma DC)
(ii) Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo anapiga Harambee ya kuanza ujenzi wa zahanati ya kijiji husika
(iii) Mbunge huyo anaendelea kushirikiana na wanakijiji kuchangia ujenzi wa zahanati inayojengwa hadi hapo Serikali itakapoanza kuchangia ukamilishaji wake.
(iv) Serikali hukamilisha ujenzi wa zahanati na kuweka vifaa tiba na wafanyakazi wanaohitajika.

Jimbo letu lina jumla ya Zahanati 29 zinazotoa Huduma za Afya. Kati ya hizo, 25 ni za Serikali na 4 ni za Binafsi.

Jimbo lina Vituo vya Afya sita (6) na Hospitali moja (1) ya Halmashauri/Wilaya.

Zahanati 16 zinaendelea kujengwa:
Vijiji vinavyojenga zahanati mpya ni hivi vifuatavyo: Burungu, Butata, Chanyauru, Chimati, Chirorwe, Kaburabura, Kakisheri, Kataryo, Kurukerege, Kurwaki, Kwikerege, Maneke, Mabuimerafuru, Nyabaengere, Nyambono na Nyasaungu.

Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kataryo:
Kijiji cha Kataryo ni moja ya vijiji vitatu vya Kata ya Tegeruka. Vijiji vingine ni: Mayani na Tegeruka. Kata hii inayo zahanati moja tu inayohudumia vijiji vyote, na imejengwa Kijijini Mayani

Kijiji cha Kataryo kimeamua kujenga zahanati yake kwa kutumia nguvukazi na michango ya fedha za wanakijiji, na baadhi ya wadau wa maendeleo wa kijiji hicho.

Diwani wa Kata hiyo, Mhe Alpha Modikae Mashauri amechangia Saruji Mifuko 50, na amehaidi kuendelea kuchangia ujenzi huo.

Mbunge wa Jimbo ameanza kutoa michango yake, kwa kuanza na Saruji Mifuko 200, nae ataendelea kuchangia ujenzi huo.

Akaunti ya Benki ya Kijiji cha Kataryo:
Benki: NMB
Akaunti Na: 30302300302
Jina la Akaunti: Kijiji cha Kataryo

Wana-Kataryo wanaomba mchango wako uwasaidie kukamilisha ujenzi wa zahanati yao kabla ya Disemba 2024. Tafadhali tuma mchango wako wa fedha kwenye Akaunti ya kijiji chao.

Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha:
Hatua iliyofikiwa kwenye ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kataryo, Kata ya Tegeruka.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumatatu, 3.6.2024

MBUNGE WA JIMBO ANUNUA TRACK SUITS 100 NA JEZI 16 KWA AJILI YA TIMU YA UMITASHUMTA YA MUSOMA VIJIJINI

Timu ya UMITASHUMTA ya wanafunzi wa Shule za Msingi za Musoma Vijijini wako kambini wakifanya mazoezi yakiwa ni kwa ajili ya maandalizi yao ya mashindano ya UMITASHUMTA Mkoa wa Mara.

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo amechangia ushiriki wa wanafunzi wetu kwenye mashindano hayo kwa kununua:
*Track suits 100
*Jezi 16 za wachezaji wa mpira wa miguu

Picha za hapa zinaonesha:
Wanafunzi wakiwa mazoezini kwenye Shule ya Msingi Suguti, Kijijini Suguti, Kata ya Suguti

Michezo na Utamaduni:
Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025 inaelezea umuhimu wa michezo na utamaduni kwa Taifa letu.

Michezo na Utamaduni ni moja ya vipaumbele vikuu vitano (5) vya Jimbo letu, na inatekelezwa vizuri.

Tunawatakiwa wanafunzi wetu ushindi mzuri kwenye mashindano ya UMITASHUMTA

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumapili, 26.5.2024

MAJI YAONGEZEKA ZIWA VICTORIA: BAADHI YA KAYA KISIWANI RUKUBA ZAHIFADHIWA KWENYE KITUO CHA AFYA

Mvua zinaendelea kunyesha, na maji Ziwa Victoria yanaendelea kuongezeka.

Siku ya leo siyo nzuri Kisiwani Rukuba, Kaya ya Etaro kwani kaya tano (5) hazina makazi zimehifadhiwa kwenye Kituo cha Afya cha hapo Kisiwani. Maji yanaendelea kuongezeka, na makazi ya kaya nyingine thelathini na mbili (32) yako hatarini.

Kuongezeka kwa maji ndani ya Ziwa Victoria

Mifano hii miwili itatuonyesha jinsi maji yalivyoongezeka ndani ya Ziwa Victoria kwa upande wa Wilaya ya Musoma:

(i) Kisiwani Rukuba, Kata ya Etaro:
Waathirika wa Kisiwani humo wanasema, "maji yamewafuata" kwa takribani mita 30-40 hadi kwenye makazi yao

(ii) Mji wa Musoma:
Waathirika wanaoishi karibu na ufukwe wa Ziwa Victoria wanasema "maji yamewafuata kwa takribani mita 5" hadi kwenye makazi yao

Picha mbili kutoka Mtaa wa Ziwa (Lakeside street) zimeambatanishwa hapa - picha zenya magugu maji (water hyacinth)

(iii) Ofisi ya Bonde la Ziwa Victoria, Mwanza:
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo amewasiliana na wataalamu wetu walioko kwenye Ofisi hiyo, na kupata jibu lifuatalo:
maji yameongezeka kwa kiasi cha
wastani wa kina cha mita 1.65

USHAURI:
Wananchi wanaoishi karibu na ufukwe wa Ziwa Victoria wanalazimika kufuata ushauri watakaopewa na viongozi mbalimbali, kwa ajili ya kuepuka mafuriko au ongezeko la maji ndani ya Ziwa Victoria.

Vilevile, wananchi wanahimizwa kufuatilia utabiri wa hali ya hewa unaotolewa kila siku na wataalamu wa hali ya hewa wa TMA.

Ziwa Victoria lenye kawaida ya ujazo wa maji wa takribani kilomita za ujazo 2,424 (2,424 cubic kilometres), kwa sasa maji yaongezeka sana! Tuchukue tahadhari kubwa!

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumamosi, 4.5.2024

SHEREHE ZA MUUNGANO: VIONGOZI WA WILAYA WAPANDA MICHE YA MITI NA KUFANYA USAFI KIJIJINI KIGERA

Leo, Watanzania wote tunasherehekea kwa furaha na amani tele ya miaka sitini (60) ya Muungano wetu.

Jimbo la Musoma Vijijini lilikua na ratiba ya siku kadhaa za kupanda miti na kufanya usafi sehemu mbalimbali za vijijini mwetu ikiwa ni sehemu ya Sherehe za Muungano.

Tunamshukuru sana Mkuu wa Wilaya (DC) yetu ya Musoma, Mhe Dkt Khalfany Haule kwa kusimamia na kuongoza vizuri sana matukio yote ya sherehe za Muungano wilayani mwetu.

Shule ya Msingi Ekungu, Kijijini Kigera (Etuma), Kata ya Nyakatende:

Mhe DC wetu aliongoza upandaji wa miche ya miti ya matunda, mbao na kivuli kwenye shule hii.

Vilevile, kila mwafunzi aligawiwa miche mitatu ya kupanda na kutunza kwenye maeneo ya nyumbani kwao.

CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa ni ya matukio mbalimbali yaliyofanyika S/M Ekungu - tafadhali wasikilize wanakijiji wanayoyasema, hasa shukrani zilizotolewa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Ijumaa, 26.4.2024

BULINGA SEKONDARI KUKAMILISHA MAABARA YA FIZIKIA MWEZI AGOSTI 2024

Jimbo la Musoma Vijijini lina mradi kabambe wa ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi (fizikia, kemia na baiolojia) kwenye Sekondari zake zote za Kata. Wananchi na Serikali yetu wanashirikiana vizuri sana kwenye utekelezaji wa mradi huu.

Jimbo hili lina Sekondari za Kata 26 na wanavijiji wanajenga nyingine 10. Sekondari za Binafsi ni mbili (2).

Bulinga Sekondari ni ya Kata ya Bulinga yenye vijiji vitatu (3) ambavyo ni: Bujaga, Bulinga na Busungu. Ilianza kutoa elimu ya masomo ya sekondari Mwaka 2016, na kusajiliwa rasmi Mwaka 2019.

Bulinga Sekondari inazo maabara mbili (2) za masomo ya kemia na bailojia ambazo zinatumika. Maabara moja ya somo la fizikia hakijakamilishwa.

Sekondari hii yenye wanafunzi 610 ilitembelewa na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, kwa lengo la kufuatilia ustawi wake na kupokea orodha ya mapungufu ya shule hii. Hiyo ilikuwa tarehe 12.4.2024

Vilevile, Mbunge huyo aliwakaribisha wananchi kutoka vijiji vitatu vya Kata ya Bulinga kwa lengo la kupokea na kutatua matatizo na kero zao.

Wananchi hao waligawiwa vitabu viwili viwili (Volumes III&IV) vinavyoelezea mafanikio makubwa yanayopatikana kutokana na utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025 ndani ya Jimbo letu.

Ukamilishaji wa Maabara ya Fizikia:
Kikao cha Mbunge wa Jimbo wa Jimbo, wananchi wa Kata ya Bulinga, walimu na baadhi ya wanafunzi wa Bulinga Sekondari kiliazimia yafuatayo:

(i) Maabara ya Fizikia iliyojengwa hadi usawa wa renta ikamilishwe kabla ya tarehe 30.8.2024

(ii) Mabati ya rangi 120 yanayohitajika:
* Kila kijiji kichangie mabati 24, jumla mabati 72
* Mbunge wa Jimbo achangie mabati 24
* Halmashauri yetu ichangie mabati 24

(iii) Mbao na misumari
Wanavijiji na Mbunge wao wamejiwekea utaratibu wa kununua vifaa hivi vya ujenzi.

Michango yote iliyoainishwa hapo juu iwasilishwe kwa Mkuu (Headmaster) wa Bulinga Sekondari ifikapo tarehe 15.8.2024

Michango kutoka kwa Wana-Bulinga na Wadau wengine wa maendeleo:

(i) Wanaopenda kuchangia vifaa vya ujenzi:
Wanaombwa waviwasilishe kwa Mkuu (Headmaster) wa Bulinga Sekondari

(ii) Michango ya fedha ipelekwe kwenye Akaunti ya Shule ambayo ni:
Benki: NMB
Akaunti Na: 30310029434
Jina: Bulinga Secondary School

KARIBUNI TUKAMILISHE UJENZI WA MAABARA YA FIZIKIA YA BULINGA SEKONDARI

Picha za hapa zinaonesha:
Wanafunzi wa Bulinga Sekondari wakiwa kwenye kipindi cha mafunzo kwa vitendo (practicals) ndani ya Maabara yao ya Kemia

Boma la Maabara ya Fizikia linalohitaji ukamilishwaji. Mbunge wa Jimbo alikabidhi Saruji Mifuko 100 ya ukamilishaji wa maabara hiyo.

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini akiongea na wananchi wa Kata ya Bulinga kwenye eneo la Bulinga Sekondari

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumatatu, 15.4.2024

NYANJA SEKONDARI YAAMUA KUANZA UJENZI WA MAABARA TATU ZA MASOMO YA SAYANSI

Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 lina jumla ya Vijiji 68 na Vitongoji 374.

Jimbo hili lina Sekondari 28, kati ya hizo 26 ni za Kata/Serikali na 2 ni za Binafsi (private). Wanavijiji wanajenga sekondari nyingine 10.

Nyanja Sekondari: miundombinu ya elimu:
Sekondari hii ni ya Kata ya Bwasi yenye vijiji vitatu (3) vya Bugunda, Bwasi na Kome. Ilifunguliwa Mwaka 2006, ina wanafunzi 495 na walimu 11.

Sekondari hii haina maabara hata moja, haina jengo la utawala na ina upungufu wa vyumba vinne vya madarasa. Kuna nyumba moja tu ya walimu.

Maabara 3 kujengwa ndani ya miezi 4:
Kikao kilichohudhuriwa na baadhi ya wanavijiji, viongozi wa Chama na Serikali wa Kata ya Bwasi na Mbunge wa Jimbo kiliazimia kwamba ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi (physics, chemistry and biology) uanze mara moja na maboma yawe yamekamilika ifikapo tarehe 15.8.2024.

Mbunge wa Jimbo atarudi shuleni hapo kukagua ujenzi huo.

Upatikanaji wa vifaa vya ujenzi:
Harambee ya Mbunge wa Jimbo iliyopigwa Septemba 2023 iliwezesha kupatikana kwa:
*Saruji Mifuko 41 kutoka kwa wananchi
*Tsh 549,000
*Saruji Mifuko 100 za Mbunge wa Jimbo.

Hata hivyo ujenzi haujaanza kwa sababu mbalimbali ambazo ziko mikononi mwa Serikali ya Kata na vijiji vyake vitatu!

Mchango wa Mfuko wa Jimbo:
Saruji Mifuko 100 imegawiwa kwenye shule hii.

Michango kutoka kwa Wana-Bwasi na Wadau wengine wa Maendeleo:
*Michango ya vifaa vya ujenzi ipelekwe kwa Mkuu wa Shule

*Michango ya fedha ipelekwe moja kwa moja kwenye Akaunti ya Shule ambayo ni:
Benki: NMB
Akaunti Na: 30301200349
Jina: Nyanja Sekondari

WANA-BWASI TUJITOKEZE KUCHANGIA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU YA SEKONDARI YA KATA YETU

Picha za hapa zinaonesha:
Mbunge wa Jimbo akikabidhi saruji ya ujenzi wa maabara tatu (3) za masomo ya sayansi ya Nyanja Sekondari ya Kata ya Bwasi.

Wananchi wakiwa wamegawiwa vitabu viwili viwili (Volumes III&IV) vinavyoelezea mafanikio makubwa yanayopatikana kutokana na utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025 ndani ya Jimbo letu.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

MVUA KUBWA NA UPEPO MKALI VYALETA MAAFA KWA WATU 685 KIJIJINI LYASEMBE

Ijumaa, 5.4.2024 mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali vilileta maafa makubwa Kijijini Lyasembe, Kata ya Murangi.

Jumla ya watu walioathirika ni: 685
Watoto 384
Watu wazima 301

Jumla ya majengo yaliyoharibika:
(i) Nyumba zilizobomoka (17):
17 za wanakijiji
(ii) Nyumba zilizoezuliwa mapaa (61):
59 za wanakijiji
2 vyumba vya madarasa ya S/M Lyasembe

Miti ya shule iliyoharibiwa na upepo mkali (40):
Miti mikubwa iliyong'olewa mizizi: 28
Miti iliyovunjiwa matawi makubwa: 12

MICHANGO KWA WAATHIRIKA
(i) Serikali ya Kijiji inaomba misaada ya aina mbalimbali hususani vifaa vya ujenzi (saruji, mabati, mbao na misumari)

Fedha za michango zipelekwe kwenye Akaunti ya Kijiji ambayo ni:
Benki: NBM
Akaunti Na: 30302300012
Jina: Kijiji cha Lyasembe

(ii) Shule ya Msingi Lyasembe
Shule hii iliyofunguliwa Mwaka 1975, kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 811, na walimu 10.

Shule hii ina jumla ya vyumba vya madarasa 10, kati ya hayo matano (5) ni chakavu. Mawili kati ya hayo chakavu yameezuliwa mapaa! Mahitaji halisi ya shule hii ni vyumba vya madarasa 21, na nyumba za walimu 10 (two in one)

Bodi ya shule imeamua kuhamasisha wanakijiji wajenge madarasa mapya wakianza na jengo lenye vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja.

Fedha za michango zipelekwe kwenye Akaunti ya Shule ambayo ni:
Benki: NMB
Akaunti Na: 3033700134
Jina: Shule ya Msingi Lyasembe

Wazaliwa wa Kata ya Murangi:
Wanavijiji wa Kata ya Murangi (Kata ina vijiji viwili - Lyasembe na Murangi) wanaomba Wana-Murangi wajitokeze kuchangia waathirika wa maafa yaliyoelezwa hapo juu.

Wadau wengine wa maendeleo ya Jimbo la Musoma Vijijini wanaombwa kuchangia waathirika wa maafa yaliyoelezwa hapo juu.

Picha za hapa zinaonesha:
Mkuu wa Wilaya ya Musoma (DC), Dkt Khalfany Haule (na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya), na wananchi waathirika wakiwa kwenye eneo la maafa Kijijini Lyasembe. Hiyo ilikuwa siku ya Jumamosi, 6.4.2024

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo akiwa shuleni Lyasembe kushuhudia uharibifu mkubwa uliobabishwa na mvua kubwa na upepo mkali. Hiyo ilikuwa leo, Jumatatu, 8.4.2024

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumatatu, 8.4.2024

ETARO SEKONDARI INAJENGA MIUNDOMBINU YA ELIMU INAYOHITAJIKA KUANZISHA “HIGH SCHOOL” YA MASOMO YA SAYANSI

Idadi ya shule ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 zenye jumla ya vijiji 68 ni kama ifuatavyo:

*Shule za Msingi 120: 116 (Serikali) na 4 (Binafsi). Shule Shikizi 13 (ujenzi unaendelea)

*Sekondari 28: 26 (Kata/Serikali) na 2 (Binafsi). 10 mpya (zinajengwa na wanavijiji)

Etaro Sekondari:
Ilifunguliwa Mwaka 2006, ina jumla ya wanafunzi 897 kutoka vijiji vinne vya Kata ya Etaro.

Maabara za Kemia & Baiolojia:
Sekondari hii inazo MAABARA MBILI zilizokamilika na zinatumika. Hizo ni maabara za masomo ya Kemia na Baiolojia.

Maabara ya Fizikia:
Maabara ya Fizikia (boma lipo) itakamilishwa ifikapo tarehe 30.4.2024 kwa kutumia vifaa vilivyonunuliwa kwa kutumia Fedha za Mfuko wa Jimbo la Musoma Vijijini. Mbunge wa Jimbo ameikabadhi sekondari hiyo MABATI ya RANGI 120, SARUJI MIFUKO 100 na NONDO 40 kwa ajili ya ukamilishaji wa Maabara hiyo.

Chumba cha Kompyuta:
Kompyuta ishirini na tano (25) zimenunuliwa na rafiki wa Etaro Sekondari ambae ni Northern Illinois University, USA. Chuo hiki kilianzishwa tarehe 22.5.1895

Lengo la kuanzisha "high school" ya sayansi
Kwenye kikao cha hivi karibuni cha Mbunge wa Jimbo na wananchi wa Kata ya Etaro, moja ya maazimio muhimu yaliyofanyika ni uanzishwaji wa "high school" ya masomo ya sayansi, yakiwemo ya "computer science" kwenye sekondari hii.

Imepangwa kwamba Mwezi Julai 2024, Mbunge wa Jimbo ataendesha Harambee ya ujenzi wa mabweni, bwalo la chakula, n.k. ikiwa ni baadhi ya miundombinu muhimu inayohitajika kwa ajili ya uanzishwaji wa "high school"

PONGEZI:
Serikali yetu inapongezwa kwa kutoa michango mbalimbali ya ustawi wa Etaro Sekondari tokea Mwaka 2006

Wananchi wa Kata ya Etaro, hasa wazazi wa wanafunzi wa Etaro Sekondari wanapongezwa sana kwa kukubali kwao kuendelea kuchangia maendeleo ya sekondari yao.

Walimu, chini ya uongozi mzuri wa Mkuu wa Shule, Mwl Jacob Joseph Chagavalye wanapongezwa sana kwa ubunifu wao.

Rafiki zetu wa Marekani, Northern Illinois University nao wanapongezwa sana kwa uwezeshaji wao wa kutupatia na kutufungia mtando wenye Kompyuta 25 hapo shuleni.

Picha zetu zinaonesha:
Wanafunzi wa Etaro Sekondari wakiwa kwenye masomo ya vitendo (practicals) ndani ya Maabara ya Kemia na Chumba cha Kompyuta.

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini akikabidhi vifaa vya ujenzi vya kukamilisha Maabara ya Fizikia ya Etaro Sekondari.

Vilevile, Mbunge huyo aligawa vitabu viwili (Volumes III & IV) vinavyoelezea mafanikio makubwa yanayopatikana Jimboni mwetu kutokana na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025.

TUENDELEE KUCHANGIA UBORESHAJI NA UPANUZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU KWENYE SHULE ZETU ZA MUSOMA VIJIJINI

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Ijumaa, 5.4.2024

WAFUGAJI WA MUSOMA VIJIJINI WAENDELEA KUUNDA VIKUNDI VYA UCHUMI: KATA ZA IFULIFU NA NYAKATENDE ZAOMBA JOSHO LAO LA MWAKA 1956 LIBORESHWE

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo alikaribishwa kutembelea josho na rambo la wafugaji wa Kata za Ifulifu na Nyakatende.

Josho wanalolitumia lilijengwa Mwaka 1956, na kwa sasa linahudumia ng'ombe zaidi ya elfu tano (5) kutoka vijiji saba vya Kata hizo mbili.

Wafugaji wa Kata hizo mbili wameanzisha vikundi kadhaa vya wafugaji, wauzaji maziwa na wakulima wa nyasi za malisho.

Maombi makuu ya wafugaji hao:
(i) Josho la Mwaka 1956 lililojengwa Kijijini Kabegi liboreshwe kwa kuziba nyufa, na liwe la kisasa

(ii) Chanzo cha maji: rambo la Kijijini Kabegi limejaa tope na kingo za kuta zimebomoka hazipo

Mbunge wa Jimbo ameahidi kufikisha maombi hayo Serikalini.

Vilevile, Mbunge huyo aliwagawia wanavijiji vitabu viwili viwili vinavyoelezea mafanikio makubwa yanayopatikana Jimboni mwetu kutokana na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025

Vyanzo vya mapato ya wananchi wa Jimboni mwetu ni:
(i) Kilimo cha pamba, na cha mazao ya chakula (mihogo, mahindi, mpunga, viazi vitamu, alizeti, mbogamboga na matunda)

(ii) Uvuvi wa samaki ndani ya Ziwa Victoria na kwenye baadhi ya mito

(iii) Ufugaji wa ng'ombe, mbuzi, kondoo na kuku

(iv) Uchimbaji wa madini, hususani dhahabu - wachimbaji wadogo wadogo

(v) Biashara za aina mbalimbali

KILIMO, UVUVI na UFUGAJI ni AJIRA KUU za Jimboni mwetu - tuendelee kuboresha mazingira na vitendea kazi vyake.

Picha za hapa zinaonesha:
ziara ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo kijijini Kabegi, Kata ya Ifulifu.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumatano, 3.4.2024

WANANCHI WA KATA YA NYEGINA WAAMUA KUHARAKISHA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA SEKONDARI YAO MPYA

Kata ya Nyegina yenye vijiji vitatu (Kurukerege, Mkirira na Nyegina) inazo sekondari mbili ambazo ni Mkirira na Bukwaya. Sekondari ya Bukwaya ni mpya, ilifunguliwa Julai 2022.

Uharakishaji wa ujenzi wa miundombinu ya Bukwaya Sekondari:
Sekondari hii ina mapungufu mengi na wanavijiji wa Kata ya Nyegina wameamua kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu ya shule yao.

Uamuzi huo ulifanywa kwa kumshirikisha Mbunge wao, Prof Sospeter Muhongo alipotembelea shule hiyo siku ya Alhamisi, 28.3.2024

Tarehe 30.4.2024:
Ifikapo tarehe hii, vyumba viwili vya madarasa ambavyo tayari vimeezekwa vitakuwa vimekamilishwa. Mbunge wa Jimbo amewakabidhi Saruji Mifuko 150 iliyonunuliwa kwa kutumia Fedha za Mfuko wa Jimbo.

Tarehe 30.5. 2024:
Ifikapo tarehe hii, matundu sita (6) ya choo yatakuwa yamekamilika

Mwezi Julai 2024:
Mbunge wa Jimbo atapiga Harambee ya kuanza ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi, ambayo ni fizikia, kemia na bailojia.

Michango ya ujenzi wa Bukwaya Sekondari:
Sekondari hii alianza kujengwa kwa nguvu za wananchi na Mbunge wa Jimbo. Orodha ya michango yote imetunzwa shuleni hapo.

Serikali inashukuliwa sana kwa kuchangia Tsh Milioni 40 (arobaini) zikiwa ni fedha za UVIKO.

Picha za hapa inaonesha:
Mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, na wananchi wa Kata ya Nyegina, wakiwemo walimu na wanafunzi wa Bukwaya Sekondari, na wanafunzi wa Shule ya Msingi Nyegina. Hii ilikuwa siku ya Alhamisi, 28.3.2024

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumatatu, 1.4.2024

WANAKIJIJI WAANZA UJENZI WA “DAVID MASSAMBA MEMORIAL SECONDARY SCHOOL”

Wakazi wa Kijiji cha Kurwaki, Kata ya Mugango wameanza ujenzi wa "David Massamba Memorial Secondary School."

Sekondari hii ambayo itakuwa ya pili kwa Kata ya Mugango inajengwa ikiwa imepewa jina la Marehemu Prof David Massamba, mzaliwa wa Kijiji cha Kurwaki, na aliyekuwa bingwa wa mabingwa wa lugha ya Kiswahili.

Kazi kubwa za ustawishaji wa Lugha ya Kiswahili zilizofanywa na Marehemu Prof David Massamba, kwa kushirikiana na Wataalamu wenzake, ni pamoja na:

*Kuandika vitabu vinavyotumika Vyuo Vikuu na Sekondari (Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu)
*Uandishi wa Kamusi ya Kiswahili

Michango ya awali ya ujenzi:
(i) Wanakijiji: Tsh 1,870,000
(ii) Familia Massamba: Tsh 800,000
(iii) Wazaliwa 2 wa Kurwaki: Tsh 750,000
(Dr Rukonge Manoko & Ndg Kawawa Jackson)
(iv) Diwani wa Kata: Tsh 200,000
(v) Wazazi wa Kijiji jirani, Kiriba: Tsh 80,000
(vi) Walimu Makada: Tsh 70,000

Michango ya Mbunge wa Jimbo:
(i) Binafsi: Saruji Mifuko 250
(ii) Mfuko wa Jimbo: Saruji Mifuko 205

Akaunti ya Kijiji ya kutuma michango:
Benki: NMB
Akaunti Na: 30302301539
Jina: Kijiji cha Kurwaki

Tafadhali tunaomba tuendelee kuchangia ujenzi wa Sekondari hii ambayo itakuwa ni kumbukumbu nzuri ya kuenzi kazi nyingi na muhimu sana alizozifanya Marehemu Prof David Massamba kwenye ukuzaji na usitawishaji wa Lugha ya Kiswahili kitaifa na kimataifa.

Picha za hapa zinaonesha:
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo akiwa na wanakijiji wa Kurwaki kwenye eneo la ujenzi wa, "David Massamba Memorial Secondary School." Hiyo ilikuwa Jumatano, 20.3.2024.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatano, 27.3.2024

KATA ISIYOKUWA NA KITUO CHA AFYA NA ZAHANATI HATA MOJA YAAMUA KUJENGA ZAHANATI MBILI

Kata ya Musanja yenye vijiji vitatu (3) haina Kituo cha Afya na haina Zahanati hata moja kwenye vijiji vyake. Vijiji hivyo ni: Mabuimerafuru, Musanja na Nyabaengere.

Hii ndiyo Kata pekee Jimboni mwetu yenye hali kama hiyo kwa upande wa Huduma za Afya!

Wanavijiji wa Kata hii wanalazimika kutembea umbali mrefu wa zaidi ya kilomita kumi (km 10) kwenda kupata Huduma za Afya kwenye Kata jirani ya Murangi (Kituo cha Afya cha Murangi).

Zahanati ya Kijiji cha Nyabaengere:
Zahanati hii inakaribia kuanza kutoa Huduma za Afya. Maombi ya kufungiwa umeme yamepelekwa TANESCO.

Zahanati ya Kijiji cha Mabuimerafuru:
Mbunge wa Jimbo la MusomaVijijini, Prof Sospeter Muhongo aliendesha Harambee ya ujenzi wa Zahanati ya kijiji hiki siku ya Jumatano, 20.3.2024.

Matokeo ya Harambee hiyo:
1. Fedha zilizopatikana: Tsh 1,350,000
2. Saruji Mifuko 59
3. Kondoo 2
4. Mbunge wa Jimbo: Saruji Mifuko 200 (mia mbili)

Kamati ya ujenzi iliundwa chini ya uongozi wa Ndugu Justine Joshua

Michango kutoka kwa Wadau wa Maendeleo wa Kata ya Musanja:
Uchangiaji ufanyike kwa kutuma fedha za michango moja kwa moja kwenye Akaunti ya Kijiji ambayo ni:

Benki: NMB
Akaunti Na: 30310037402
Jina: Kijiji cha Mabuimerafuru

Picha inaoneshaHarambee ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mabuimerafuru.

Viongozi wa CCM wa Kata na Matawi, na baadhi ya wananchi wa Kata ya Musanja walipewa vitabu viwili viwili vinavyoelezea mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025 ndani ya vijiji vyote 68 vya Jimboni mwetu.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumamosi, 23.3.2024

SIKU YA MISITU DUNIANI (THE INTERNATIONAL DAY OF FORESTS) – MUSOMA VIJIJINI WAISHEREHEKEA KWA KUPANDA MITI MASHULENI

Leo (21.3.2024) ni siku ya Umoja wa Mataifa (UN) ya kukumbushana umuhimu wa misitu ya aina zote.

UN ilipitisha azimio la siku hii (tarehe 21 Machi ya kila mwaka) kwenye Mkutano wake wa tarehe 28.11.2013

Kaulimbiu 2024: Misitu na Ubunifu
(Forests and Innovations)

Jimbo la Musoma Vijijini: Misitu na Ubunifu
Kwa muda wa zaidi ya wiki mbili, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo akishirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt Khalfany Haule, na Meneja wa Misitu (TFS) Wilaya, Ndugu Boniphace Kaberege wamekuwa wakigawa na kupanda mamia ya miche ya miti ya matunda, mbao na kivuli kwenye shule kadhaa za misingi na sekondari za Jimboni mwetu. Kampeni hii ni endelevu!

Sherehe ya Uzinduzi wa Upandaji miti
Jana, TFS Wilaya chini ya uongozi wa Ndugu Boniphace Kaberege ilitoa mafunzo ya umuhimu wa misitu kwa maisha na ustawi wa jamii zetu. Mafunzo hayo yalifanywa kwenye Sekondari ya Suguti.

Wanafunzi na Walimu wote wa Sekondari hiyo, wakiongozwa na Mkuu wao, Mwl Pendo Kaponoke walihudhuria mafunzo hayo.

Wanavijiji wa Kata ya Suguti (Vijiji 4 vya Chirorwe, Kusenyi, Suguti na Wanyere) walihudhuria, wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wa Kata hiyo, Ndugu Alphonce Wambura

"Environmental Ambassadors" - Suguti Sekondari:
Wanufunzi 100 wa Sekondari hii wamekuwa, Mabalozi wa Mazingira chini ya Mwalimu wao wa Mazingira, Mwl Keneth Elias. Hawa wataongoza Kampeni ya upandaji na utunzaji miti ndani ya Kata na Suguti, na kwingineko Jimboni mwetu.

Uzinduzi wa Upandaji na Utunzaji miti kwenye shule zote za Jimboni mwetu
Jana, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini na Meneja wa TFS Wilaya walizindua kampeni endelevu ya upandaji na utunzaji wa miti kwenye shule zote za Jimboni mwetu. Uzinduzi huo ulifanyika Suguti Sekondari.

Picha za hapa zinaonesha:
Matukio mbalimbali yaliyoelezwa hapo juu. Hapo ni Suguti Sekondari, Kijijini Suguti, Kata ya Suguti, Musoma Vijijini.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

The UN International Year of Forests

Tarehe:
Alhamisi, 21.3.2024

KIJIJI CHA KABURABURA KIMEANZA KUJENGA ZAHANATI YAKE – TUWAUNGE MKONO

Wiki jana, uamuzi wa ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kaburabura ulifanywa na wanakijiji wenyewe.

Kamati ya ujenzi iliundwa, na sasa kazi zimeanza kwa kutumia nguvukazi za wanakijiji wenyewe - angalia picha.

Tafadhali tuwaunge mkono kwa kuchangia ujenzi wa Zahanati ya Wana-Kaburabura

Tafadhali tuma mchango wako kwenye Akaunti ya Kijiji chao:

Benki: NMB
Akaunti Na: 30302300684
Jina: Kijiji cha Kaburabura

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumanne, 19.3.2024

MRADI WA UFUNGAJI WA MINARA MIPYA YA MAWASILIANO WAANZA KUTEKELEZWA JIMBONI MWETU

Maombi yetu ya kuomba kuboreshewa mawasiliano ya simu, intaneti, n.k. yaanza kutekelezwa.

Mnara mpya wa VODA umejengwa Kijijini Masinono ndani ya eneo la Bugwema Sekondari. Wanakijiji wanakiri kwamba mawasiliano kupitia mtandao wa VODA kwa sasa ni mazuri sana.

Mbunge wa Jimbo anaendelea kufuatilia maombi yetu ya kuongezewa idadi ya minara ya mawasiliano vijijini mwetu.

Picha ya hapa inaonesha:
Mnara mpya wa VODA uliojengwa ndani ya eneo la Bugwema Sekondari, Kijijini Masinono.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Alhamisi, 14.3.2024

ZIARA YA WAZIRI MKUU MUSOMA VIJIJINI: SERIKALI KUENDELEA KUJENGA KWA KIWANGO CHA LAMI BARABARA LA MUSOMA-MAKOJO-BUSEKERA (km 92)

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa amewaeleza wana-Musoma Vijijini kuhusu uamuzi wa Serikali kuendelea kutoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo vijijini mwao.

Waziri Mkuu aliyasema hayo kwenye mkutano wake wa hadhara uliofanyika Kijijini Bwai Kwitururu, Musoma Vijijini siku ya Alhamisi, tarehe 29.2.2024

Barabara kuendelea kuwekewa lami:
Serikali imesema itaendelea kulijenga barabara letu kuu na muhimu la Musoma-Makojo-Busekera lenye urefu wa kilomita 92 kwa kiwango cha lami. Tuzingatie yafuatayo kutoka Serikalini:

(i) Kilomita 5 zimeishawekewa lami
(ii) Barabara limo kwenye Bajeti ya mwaka huu (2023/2024)
(iii) Kibali kimetolewa barabara litangazwe na Mkandarasi apatikane, na aendelee na ujenzi.

Tafadhali sikiliza kwa makini hadi mwisho CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa, hasa penye kauli ya Serikali kuhusu barabara la Musoma-Makojo-Busekera.

Shukrani:
Wana-Musoma Vijijini tunaendelea kuishukuru Serikali yetu, chini ya uongozi mzuri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha nyingi za kufadhili miradi ya maendeleo vijijini mwetu.

Tunamshukuru sana Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa kwa kututembelea Jimboni mwetu, na kwa kuendelea kufuatilia utekelezaji wa miradi yetu ya maendeleo ambayo ni kielelezo cha mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2020-2025.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatatu, 4.3.2024

JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI: VITABU VINAVYOELEZEA UTEKELEZAJI YA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM (2020-2025) VINASAMBAZWA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea vitabu kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo.

Bungeni:
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, amemkabidhi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa vitabu viwili (2) vinavyoelezea miradi ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025, ndani ya Jimbo letu.

Mbunge huyo anaendelea kuchapisha vitabu vingine hadi mwaka ujao, 2025.

Tovuti ya Jimbo letu:
www.musomavijijini.or.tz

inazo taarifa muhimu za maendeleo ya Jimbo la Musoma Vijijini. Vitabu hivyo navyo viko kwenye Tovuti hiyo.

Pichani:
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea vitabu kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Ijumaa, 16.2.2024

LEO BUNGENI-Jumatano, 7.2.2024

*Prof Sospeter Muhongo ametoa ushauri wa kuboresha elimu yetu iendane na matakwa ya ukuaji wa uchumi wa wakati huu.

*Prof Muhongo ameonyesha umuhimu wa kuwekeza kwenye masomo ya sayansi na teknolojia, na kutolea mfano nchi ya India ambayo mwaka jana (2023) pato lake la Taifa (GDP), lilikuwa la tano (5) Duniani lenye US Dollar Trilioni 3.7, sawa na 3.7% ya GDP ya Dunia.

Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa ambayo ina mchango wote wa Prof Muhongo

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatano, 7.2.2024

UGAWAJI WA VITABU VINAVYOELEZEA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM (2020-2025) UMEANZA

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo ameanza kugawa VITABU VIWILI (Volumes III & IV) vya utekelezaji wa Ilani yetu ya sasa (2020-2025)

Vitabu hivi kama vile viwili (Volumes I & II) vya Ilani ya 2015-2020, vinataja majina ya wachangiaji wa miradi inayotekelezwa Jimboni mwetu.

*Chama Mkoa: wamepewa
*Serikali Mkoa: wamepewa

Ugawaji unaendelea, utafika hadi kwenye Vitongoji. Uchapishaji wa vitabu vipya unaendelea (Volumes IV & V) - Miradi ya maendeleo ya wananchi wa Musoma Vijijini ni mingi!

Wiki ijayo Vitabu 2 (Volumes III & IV) vitawekwa kwenye Tovuti ya Jimbo:
www.musomavijijini.or.tz

Tembelea Tovuti hiyo ya Jimbo letu usome vitabu hivyo na vile vya awali (Volumes I & II, Ilani ya 2015-2020)

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Ijumaa, 19.1.2024

MISIBA KISIWANI RUKUBA: DHORUBA KUBWA YAVUNJA MTUMBWI NA KUSABABISHA VIFO VITATU

Tunasikitika kupoteza ndugu zetu 3 waliokufa maji siku ya Jumapili usiku kuamkia Jumatatu (jana, 15.1.2024). Dhoruba kubwa ilivunja mbao za mtumbwi na maji yakazamisha mtumbwi huo.

Mtumbwi ulikuwa na wavuvi 4: mmoja amesalimika (kwao Musoma Mjini) na watatu wamekufa maji (2 kwao Maneke & 1 kwao Nyegina)

Utafutaji wa miili ya marehemu:
*Ajali ilitokea eneo la mbali kutoka Kisiwani Rukuba - mwendo wa takribani masaa matatu kuelekea Kisiwa cha Goziba (Bukoba)

*Mitumbwi 10 inaanza kazi ya kutafuta miili hiyo kesho. Mafuta yanayohitajika ni lita 500 au zaidi.

Michango ya mafuta ya kutafuta waliokufa maji
(i) Wana-Rukuba wamejichangia lita 300
(ii) Mbunge wa Jimbo amechangia lita 200

Maombi ya michango kutoka vyanzo vingine:
Mahitaji ya misiba hii mitatu ni mengi na makubwa. Tafadhali changia misiba hii kwa kutuma fedha kwenye Akaunti ya Kisiwa/Kijiji cha Rukuba.

Benki: NMB
Akaunti Na.: 30302300701
Jina la Akaunti: Serikali ya Kijiji cha Rukuba

Pichani:
Maombolezo yanaendelea pembeni mwa Ziwa Victoria, Kisiwani Rukuba.

Tunamwomba Mwenyezi Mungu awape nguvu na matumaini mema wanafamilia wa marehemu hao watatu. Tuendelee kuwafariji wafiwa!

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumanne, 16.1.2024

HARAMBEE YA MBUNGE YAFANIKISHA UPAUAJI WA MADARASA YA SHULE SHIKIZI KIUNDA YA MUSOMA VIJIJINI

Tarehe 12.1.2024 Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo aliendesha HARAMBEE iliyolenga kukamilisha kazi ya upauaji wa boma la Shule Shikizi Kiunda ya Kijijini Kamguruki, Kata ya Nyakatende.

Boma hilo (picha imeambatanishwa hapa) ni la vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja ya walimu. Boma limejengwa kwa michango ya Wana-Kitongoji cha Kiunda, Diwani wa Kata na Mbunge wa Jimbo.

Ujenzi wa Shule Shikizi Jimboni mwetu
Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 zenye vijiji 68 na vitongoji 374 ina shule za msingi zenye idadi ifuatayo:
*111 shule za Serikali
*4 shule Binafsi
*12 shule shikizi zinazopanuliwa

Harambee ya Shule Shikizi Kiunda
*Gharama zote za upauaji:
Tsh 4,268,000

*Fedha zilizopatikana kwenye Harambee:
Tsh 1,285,000. Wachangiaji:
(i) Wakazi wa Kijiji cha Kamguruki
(ii) Wakazi kutoka Vijiji jirani
(iii) DEO Hamisi Shemahonge
(iv) Viongozi wa Chama Wilaya & Jumuiya zake ambao ni Ndg Jackson Nyakia, Ndg William Magero, Ndg Bwire Mkuku na Ndg Sophia Maregesi

*Mabati yaliyopatikana kwenye Harambee:
(i) Ndg Pascal Maganga: Mabati 24
(ii) Diwani Mhe Kisha Marere: Mabati 36
(iii) Mbunge Prof Muhongo: Mabati 72

Ratiba ya upauaji
*Tarehe 23.2.2024
Mbao za paa (kenji) zianze kuwekwa

*Tarehe 24.2.2024
Mabati yaanze kuwekwa (kuezeka)

Kaimu Mtendaji wa Kijiji (VEO), Ndg Magreth Malima anapewa pongezi nyingi za usimamiaji mzuri wa shughuli za maendeleo ndani ya Kijiji cha Kamguruki

MICHANGO INAKARIBISHWA SANA
Wana-Kitongoji cha Kiunda, na Kata ya Nyakatende kwa ujumla wanaendelea kuomba michango kutoka vyanzo mbalimbali ili kujenga na kupanua Shule Shikizi Kiunda iwe Shule ya Msingi kamili, inayojitegemea.

Tuma mchango wako wa fedha kwenye Akaunti ya Kijiji cha Kamguruki.
Akaunti ya Benki:
Benki: NMB
Akaunti Na: 30302300679
Jina la Akaunti: Kijiji cha Kamguruki

Pichani:
Wakazi wa Kitongoji cha Kiunda na Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Harambee iliyofanyika kwenye eneo la ujenzi wa Shule Shikizi Kiunda ya Kijijini Kamguruki, Kata ya Nyakatende, Musoma Vijijini.

TUENDELEE KUBORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU YA MUSOMA VIJIJINI

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumanne, 16.1.2024

HARAMBEE YA UJENZI WA SHULE SHIKIZI KIUNDA, MUSOMA VIJIJINI

Hatua iliyofikiwa kwenye ujenzi wa miundombinu ya elimu kwenye Shule Shikizi Kiunda ya Kijijini Kamguruki, Musoma Vijijini.

Tarehe:
Ijumaa, 12.1.2024
Saa 8 mchana

Mahali:
Kitongoji cha Kiunda
Kijijini Kamguruki

Akaunti ya Benki:
Benki: NMB
Akaunti Na: 30302300679
Jina la Akaunti: Kijiji cha Kamguruki

Taarifa ya Kiunda:
Shule Shikizi Kiunda inajengwa kwenye Kitongoji cha Kiunda, Kijijini Kamguruki, Kata ya Nyakatende.

Shule hii inatayarisha watoto wa vitongoji 3 kwenye masomo ya awali, baadae watoto hao wanaenda kuanza masomo ya Shule ya Msingi mbali na nyumbani kwao - tatizo la umbali mrefu wa kwenda masomoni.

Ujenzi wa Shule Shikizi Kiunda:
Wote tunakarabishwa kuchangia ujenzi wa shule hii kwa kushiriki HARAMBEE iliyoelezwa hapo juu, au kutuma mchango wako moja kwa moja kwenye Akaunti ya Kijiji cha Kamguruki.

Picha ya hapa inaonesha hatua iliyofikiwa kwenye ujenzi wa miundombinu ya elimu kwenye Shule Shikizi Kiunda ya Kijijini Kamguruki, Musoma Vijijini.

KARIBU TUBORESHE ELIMU VIJIJINI MWETU

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumamosi, 6.1.2024

UHURU NA KAZI – DHAMIRA YA KIJIJI CHA MUHOJI KUFUNGUA SEKONDARI YAKE MWAKANI IKO PALE PALE

Wanakijiji wakilima barabara ya kuingia shuleni (Muhoji Sekondari)

UHURU NA KAZI - DHAMIRA YA KIJIJI CHA MUHOJI KUFUNGUA SEKONDARI YAKE MWAKANI IKO PALE PALE

Wananchi wa Kijiji cha Muhoji, Kata ya Bugwema wameamua kujenga Sekondari yao (Muhoji Sekondari) na dhamira ya kuifungua shule hiyo Januari 2024 iko pale pale.

Ujenzi wa awali unaokamilishwa ni:
*Vyumba 2 vya madarasa
*Ofisi 1 ya walimu
*Vyoo:
matundu 12 ya wasichana
matundu 12 ya wavulana
matundu 2 ya walimu
*Barabara ya kuingia shuleni kutoka barabara kuu (nguvukazi za wanakijiji)

Wachangiaji wakuu wa ujenzi wa Muhoji Sekondari ni:
*Wananchi wa Kijiji cha Muhoji
*Mbunge wa Jimbo
*Mfuko wa Jimbo
*Wazaliwa watatu (3) wa Kijiji cha Muhoji

Halmashauri yetu (Musoma DC) bado haijachangia cho chote!

TARURA imeombwa isaidie ukamilishaji wa ujenzi wa barabara linaloingia Muhoji Sekondari likitokea barabara kuu la Murangi- Masinono-Manyamanyama (Bunda).

Muhoji Sekondari itakuwa ni Sekondari ya pili ya Kata ya Bugwema yenye vijiji vinne (Bugwema, Kinyang'erere, Masinono na Muhoji).

Sekondari moja (Bugwema Sekondari) kwa Kata hii haitoshi, matatizo makuu yakiwa ni umbali mrefu wa kutembea kwa baadhi ya wanafunzi, na mirundikano madarasani!

Ombi kutoka Kijijini Muhoji:
*Wazaliwa au watu wenye chimbuko la Kata ya Bugwema wanaombwa waungane na ndugu zao kukamilisha ujenzi wa Muhoji Sekondari.

*Wadau wengine wa maendeleo wanaombwa sana wachangie ujenzi wa shule hii.

Michango ya fedha ipelekwe:
Benki: NMB
Akaunti Na: 30302301062
Jina la Akaunti: Serikali ya Kijiji cha Muhoji

Picha zilizoambatanishwa hapa:
*Jengo lenye Vyumba 2 vya madarasa na Ofisi 1 ya walimu
*Wanakijiji wakijenga vyoo vya shule (Muhoji Sekondari)
*Wanakijiji wakilima barabara ya kuingia shuleni (Muhoji Sekondari)

UHURU NA KAZI

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe (Uhuru Day)
Jumamosi, 9.12.2023

Jengo lenye Vyumba 2 vya madarasa na Ofisi 1 ya walimu

Wanakijiji wakijenga vyoo vya shule (Muhoji Sekondari)

UJENZI WA MAABARA TATU ZA MASOMO YA SAYANSI KWENYE SEKONDARI YA MTIRO UNAENDELEA VIZURI

Maendeleo ya ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi kwenye Sekondari ya Mtiro ya Kata ya Bukumi, Musoma Vijijini

Rejea taarifa yetu ya Jumatatu, 6.11.2023 kuhusu umuhimu wa kujenga maabara tatu za masomo ya sayansi kwenye Sekondari ya Mtiro ya Kata ya Bukumi.

Ujenzi wa aina hii unafanyika kwenye Sekondari zote za Jimbo la Musoma Vijijini (25 za Kata/Serikali na 2 za Binafsi za Madhehebu ya Katoliki & SDA)

Ujenzi wa maabara tatu za masomo ya Fizikia, Kemia na Baiolojia unaendelea vizuri kwenye Sekondari ya Makojo.

Wanavijiji wa Kata ya Bukumi (Vijiji vya Buira, Bukumi, Buraga na Busekera) wanaendelea kuchangia ujenzi huu.

Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo nae anaendelea kuchangia ujenzi huu. Juzi ameongeza mchango wake kwa kuwapatia Saruji Mifuko 50 (hamsini).

Matofali ya ujenzi huu yanaendelea kufyatuliwa kwenye eneo la ujenzi na kila mfuko mmoja wa saruji unatoa matofali 25 - ubora unaokubalika!

Wanavijiji wanaomba mchango wako, na tafadhali upeleke kwenye Akaunti ya Benki ya Sekondari hiyo ambayo ni:

Jina la Akaunti:
Mtiro Secondary School

Benki (Musoma):
NMB

Akaunti Namba:
30301200299

Tunatanguliza shukrani zetu za dhati!

Picha  hapo juu inaonesha maendeleo ya ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi kwenye Sekondari ya Mtiro ya Kata ya Bukumi, Musoma Vijijini

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatano, 22.11.2023

UJENZI WA SEKONDARI MPYA UNAENDELEA MUSOMA VIJIJINI: KISIWA CHA RUKUBA KIMEANZA UJENZI WA SEKONDARI YAKE

Mwanzo wa ujenzi wa Sekondari ya Kisiwa cha Rukuba - ujenzi wa msingi wa mawe wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja ya walimu.

Jimbo la Musoma Vijijini lina Kata 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374.

Jimbo hili lina jumla ya Sekondari:
*25 za Kata (Serikali)
*2 za Binafsi (Katoliki & SDA)

Sekondari mpya tano (5) zinajengwa kwenye vijiji vitano - Kisiwa cha Rukuba (Kata ya Etaro), Nyasaungu (Kata ya Ifulifu), Kurwaki (Kata ya Mugango), Muhoji (Kata ya Bugwema), na Wanyere (Kata ya Suguti, serikali inagharamia ujenzi).

Sekondari ya Kisiwa cha Rukuba
Wakazi wa Kisiwa cha Rukuba wameamua kujenga sekondari yao ili elimu ya sekondari itolewe hapo Kisiwani badala ya wanafunzi kwenda kupanga vyumba nchi kavu (Kijijini Etaro) kwa ajili ya elimu yao ya sekondari.

Harambee ya kwanza ya ujenzi wa Sekondari ya Kisiwa cha Rukuba ilishafanyika chini ya usimamizi wa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, akishirikiana na Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Musoma Vijijini.

Ujenzi umeanza
*matofali 2,900 tayari yametengenezwa: kila mfuko mmoja (1) wa saruji umetoa matofali 25

*ujenzi wa vyumba viwili na ofisi moja ya walimu umeanza - msingi wa mawe unajengwa (angalia picha za hapa)

Tafadhali sana tunaomba mchango wako:
*Akaunti ya kuweka mchango wako wa fedha ni:
Benki: NMB
Akaunti Namba: 30302300701
Jina la Akaunti:
Serikali ya Kijiji cha Rukuba

Wakazi wa Kisiwa cha Rukuba wamedhamiria kujenga Sekondari kisiwani humo ili kuboresha upatinakaji wa elimu ya sekondari kwa watoto wao - tuwaunge mkono!

Mchango wa Mbunge wa Jimbo
*Prof Sospeter Muhongo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini ameishachangia Saruji Mifuko 100

*Mbunge huyo anatoa tena Saruji Mifuko 50, itakayochukuliwa leo, na ataendelea kuchangia ujenzi huo.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatano, 1.11.2023

SEKONDARI ILIYOFUNGULIWA MWAKA 2006 YAAMUA KUANZA KUJENGA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI

SEKONDARI ILIYOFUNGULIWA MWAKA 2006 YAAMUA KUANZA KUJENGA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI

Nyanja Sekondari ni ya Kata ya Bwasi yenye vijiji vitatu (3) vyenye jumla ya vitongoji ishirini na vitatu (23). Vijiji hivyo ni Bugunda, Bwasi na Bugunda.

Sekondari hii ilifunguliwa Mwaka 2006, na kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 547, na walimu 12 wenye ajira, na 5 wa kujitolea.

Harambee ya ujenzi wa maabara:
Sekondari haina maabara hata moja na mwitikio wa wanafunzi kusoma masomo ya sayansi ni mdogo sana

Kwa mfano, Kidato cha Nne (Form IV) chenye jumla ya wanafunzi 96, ni wanafunzi 13 tu wanaosoma somo la Fizikia.

*Jana, Jumatatu, 9.10.2023, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini na Kamati ya Siasa ya Wilaya (CCM) waliendesha HARAMBEE ya kuanza ujenzi wa maabara za Fizikia, Kemia na Baiolojia za sekondari hiyo.

Mapato ya Harambee:
*Fedha: Tsh 1,105,000
*Saruji Mifuko 141
(ikiwemo Mifuko 100 ya Mbunge wa Jimbo)

Kamati ya Ujenzi:
Kamati ya Ujenzi ya watu wanne (4) imeundwa.

KARIBUNI TUCHANGIE UJENZI WA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI KWENYE SEKONDARI ZA KATA ZA MUSOMA VIJIJINI

Idadi ya Sekondari Jimboni (Kata 21) mwetu:
*25 za Kata
*2 za Binafsi
*5 zinajengwa

Pichani ni Harambee ya jana iliyofanyika Nyanja Sekondari, Kijijini Kome, Kata ya Bwasi

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumanne, 10.10.2023

KILIMO CHA UMWAGILIAJI NDANI YA BONDE LA BUGWEMA

KILIMO CHA UMWAGILIAJI NDANI YA BONDE LA BUGWEMA

Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alidhamiria kujenga miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji kwenye bonde la Bugwema lililoko Musoma Vijijini.

Ujenzi wa miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji ilianza kujengwa Mwaka 1974. Mradi ukasimama.

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, ameiomba Serikali yetu ifufue mradi huo. Serikali imekubali na kwenye Bajeti ya Mwaka huu wa Fedha (2023/2024) - kazi za, "feasibility studies & designing", zimeanza.

Jimbo letu lina mabombe makubwa mawili yenye vigezo vyote vya uanzishwaji wa kilimo kikubwa cha umwagiliaji - hayo ni mabonde ya Bugwema & Suguti.

KILIMO CHA UMWAGILIAJI NDIYO SULUHISHO LA UHAKIKA KWA UPATIKANAJI WA CHAKULA CHA KUTOSHA & CHA BEI NAFUU NCHINI MWETU!

Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO kutoka Kijijini Bugwema - imeambatanishwa hapa.

Tafadhali usiache kutembelea TOVUTI ya Jimbo letu ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Alhamisi, 5.10.2023

WANANCHI WA KITONGOJI CHA GOMORA WAAMUA KUONGEZA KASI KWENYE UJENZI WA SHULE SHIKIZI YAO

WANANCHI WA KITONGOJI CHA GOMORA WAAMUA KUONGEZA KASI KWENYE UJENZI WA SHULE SHIKIZI YAO

Kitongoji cha Gomora ni moja ya vitongoji vitatu (3) vya Kijiji cha Musanja, Kata ya Musanja

Vitongoji hivi vitatu (3) vinayo Shule ya Msingi moja iliyojengwa Mwaka 1959 na Kanisa la Mennonite. Shule hiyo (S/M Musanja) kwa sasa ni ya Serikali.

Matatizo makuu yanayowakabili wanafunzi wa S/M Musanja:

*Umbali mrefu wa kutembea kwenda masomoni
*Mirundikano ya wanafunzi kwenye vyumba vya madarasa
*Uchakavu wa miundombinu ya shule iliyofunguliwa Mwaka 1959

Kitongoji cha Gomora chaamua kujenga Shule Shikizi
*Ujenzi wa awali umekamalisha vyumba viwili vya madarasa, ofisi moja ya walimu na choo chenye matundu 6.

Harambee ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, kwa kushirikiana na Kamati ya Siasa ya Wilaya (CCM) iliyopigwa Ijumaa, 29.9.2023 ilikuwa ya mafanikio ya kuridhisha kwa kupata:

*Saruji Mifuko 150, ikiwemo 100 ya Mbunge wa Jimbo na 10 ya Diwani
*Tsh milioni 3 za Halmashauri yetu
*Fedha taslimu Tsh 306,000 zikiwemo Tsh 105,000 za Walimu Makada wa CCM
*Mchanga tripu 3

ELIMU NI KIPAUMBELE CHETU CHA KWANZA KABISA, TAFADHALI NJOO TUCHANGIE UJENZI WA GOMORA SHULE SHIKIZI YA KIJIJI CHA MUSANJA

Wana-Gomora waliahidi kuanza ujenzi leo, na kweli wamefanya hivyo - picha ya hapa inaonesha uchimbaji wa msingi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi ya walimu.

CLIP/VIDEO ya hapa ni kutoka Kitongojini Gomora, tafadhali isikilize.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatatu, 2.10.2023

HARAMBEE IMEFANIKIWA SANA: KISIWA CHA RUKUBA CHAANZA UJENZI WA SEKONDARI YAKE

HARAMBEE IMEFANIKIWA SANA: KISIWA CHA RUKUBA CHAANZA UJENZI WA SEKONDARI YAKE

Kisiwa cha Rukuba ni moja ya vijiji vinne (4) vya Kata ya Etaro. Wanafunzi wa sekondari kutoka Kisiwani humo wanasoma nchi kavu kwenye sekondari ya Kata yao (Etaro Sekondari).

Wanafunzi hao wanakumbuna na matatizo mengi mno ambayo yanadhoofisha sana maendeleo yao kielimu. Kwa hiyo, wakazi wa Kisiwa cha Rukuba wameamua kujenga sekondari yao Kisiwani humo.

Harambee yenye mafanikio makubwa
Harambee iliyoendeshwa na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini siku ya Jumatano, 27.9.2023 ilishirikisha Viongozi wote wakuu wa Wilaya ya Musoma na Halmashauri yake (Musoma DC).

Wafanyakazi wa kada mbalimbali, wakiwemo Walimu Makada ya CCM walishiriki. Kamati ya Siasa ya Wilaya CCM nayo ilishiriki - ilikuwa ni Harambee ya kipekee kufanyika Kisiwani humo!

Michango iliyopatikana kwenye Harambee hiyo
*Wakazi na Wazaliwa wa Kisiwa cha Rukuba:
Saruji Mifuko 167
*Kamati ya Siasa ya Kata (CCM):
Saruji Mifuko 22
*Kamati ya Siasa ya Wilaya (CCM):
Saruji Mifuko 15
*DED na wenzake: Saruji Mifuko 20
*DC na wenzake: Saruji Mifuko 62
*Mbunge wa Jimbo: Saruji Mifuko 200
*Fedha taslimu: Tsh 248,000
(zikiwemo Tsh 105,000 za Walimu Makada wa CCM)

Karibuni tujenge Sekondari ya Kisiwa cha Rukuba cha Musoma Vijijini.

Furaha & Shauku ya ujenzi wa Sekondari Kisiwani Rukuba
Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO ya kutoka Kisiwani Rukuba iliyoambatanishwa hapa.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumamosi, 30.9.2023

MAJI YA BOMBA KUTOKA ZIWA VICTORIA YAENDELEA KUSAMBAZWA MUSOMA VIJIJINI

ukaguzi wa miradi miwili ya maji ya Musoma Vijijini, na Maabara ya Bulinga Sekondari ya Kata ya Bulinga, Musoma Vijijini.

 

Jimbo la Musoma Vijijini lina Kata 21, Vijiji 68 na Vitongoji 374. Vijiji vyetu vyote vina miradi ya maji ambayo iko kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji.

Miradi ya maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria inatekelezwa kwa kasi kubwa Jimboni mwetu.

Jana, Mbunge wa Jimbo aliambatana na Kamati ya Siasa ya CCM ya Wilaya ya Musoma Vijijini kukagua miradi miwili ya maji ya bomba inayotekelezwa na RUWASA. Utekelezaji wa miradi hiyo ni mzuri - Hongereni RUWASA!

Mradi wa Kata ya Bwasi
*Vijiji vitakavyonufaika na upatikanaji wa maji ya bomba ya mradi huu ni: Bwasi, Bugunda na Kome
*Chanzo cha maji kiko ziwani kwenye Kitongoji cha Bujaga, Kijiji cha Bujaga, Kata ya Bulinga. Vijiji vitatu vya Kata ya Bulinga (Bujaga, Bulinga na Busungu) tayari vinapata maji ya bomba.

Utekelezaji wa mradi huu:
*Ujenzi wa Tenki la ujazo wa lita 150,000 unakamilishwa. Lipo kwenye Kitongoji cha Rugongo, Kijijini Bwasi
*Bomba kuu la kusambaza maji limetandazwa kilomita 18 kati ya 31.5
*Vituo vya kuchotea maji 25 kati ya 35 vimeishajengwa

*Gharama ya Mradi: Tsh 997,714,196 (Tsh 997.7m)
*Mradi ulianza Februari 2023, utakamilishwa kabla ya tarehe 30.10.2023

Mradi wa Chumwi-Mabuimerafuru
Mradi huu unaanzwa kutekelezwa kwenye Vijiji vya Chumwi (Kata ya Nyamrandirira) na Mabuimerafuru (Kata ya Musanja), baadae utapanuliwa na maji yatasambazwa kwenye vijiji vyingine vya Kata hizo mbili.

Utekelezaji wa mradi huu:
*Chanzo cha maji ya mradi huu kiko ziwani kwenye Kitoji cha Nyachumwi, Kijijini Chumwi

*Ujenzi wa Tenki la ujazo wa lita 300,000 unakamilishwa. Liko kijijini Mabuimerafuru

*Bomba kuu la kusambaza maji limetandazwa umbali wa kilomita 13 kati ya 24.24

*Vituo vyote 17 vya kuchotea maji tayari vimejengwa

*Gharama ya Mradi ni Tsh bilioni 1.6
*Mradi huu ulianza kutekelezwa Februari 2023, utakamilika kabla ya tarehe 30.10.2023

Kero na matatizo ya wanavijiji:
Wanavijiji walipata muda wa kutosha wa kuwasilisha kero na matatizo yao. Majibu yalitolewa na Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo. Maswali yaliyohusu Chama yalijibiwa na Mwenyekiti Ndg Denis Ekwabi na Katibu Ndg Valentine Maganga

Kero na matatizo yaliyowasilishwa yalipata majibu ya uhakika na ya ukweli, waulizaji waliridhika!

Vilevile, Maabara za masomo ya sayansi ya Bulinga Sekondari yalitembelewa. Sekondari hii kwa sasa inazo maabara mbili zilizokamilika na zinatumika (Chemistry & Biology). Ujenzi wa Maabara ya Physics unakamilishwa.

SHUKRANI
Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini na Viongozi wao wa ngazi zote wanaishukuru sana Serikali, chini ya uongozi mzuri wa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutupatia fedha za utekelezaji wa miradi yetu ya maendeleo - ahsanteni sana!

Picha za hapa zinaonesha matukio mbalimbali ya ukaguzi wa miradi miwili ya maji ya Musoma Vijijini, na Maabara ya Bulinga Sekondari ya Kata ya Bulinga, Musoma Vijijini.

Musoma Vijijini, TUNAFANIKIWA

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumanne, 8.8.2023

PROF MUHONGO AENDELEA KUJENGA UZIO (UKUTA) KWENYE MAKABURI YA MUSOMA MJINI

Uzio unajengwa kwa kuhakikisha kwamba makaburi yaliyoko nje kidogo ya eneo la mpaka wa makaburi yanaingizwa ndani.

Makaburi yaliyo kwenye eneo la Kanisa la Mennonite la Kitaji, Musoma Mjini yalikuwa hayana uzio (ukuta). Utunzaji wake ni mgumu sana!

Wazo la kujenga uzio kwenye makaburi hayo lilitolewa na Profesa Sospeter Muhongo. Michango ilikaribishwa na kutolewa kwa kusuasua sana, na ikawa ni midogo mno! Michango ilipelekwa kwenye Kanisa lenye makaburi. Ujenzi ukaanza kwa kusuasua sana. Malumbano yakaanza kujitokeza.

Mtoa wazo la ujenzi, Prof Muhongo akaamua yafuatayo:

*Michango isimame, tuepuke malumbano.
*Ujenzi uendelee kwa ufadhili wake, yaani wa Prof Sospeter Muhongo

Maendeleo ya ujenzi:
*Eneo lenye makaburi limesafishwa kwa kukata nyasi na vichaka.

*Mafundi wengine wamewekwa kufanya kazi ya ujenzi.

*Uzio unajengwa kwa kuhakikisha kwamba makaburi yaliyoko nje kidogo ya eneo la mpaka wa makaburi yanaingizwa ndani. Angalia picha.

Nawatakia Jumapili njema

Sospeter Muhongo
Jumapili, 23.7.2023

MWENGE WA UHURU MUSOMA VIJIJINI: HUDUMA ZA AFYA ZAENDELEA KUBORESHWA NA KUIMARISHWA

pichaKiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndugu Abdalla Shaibu Kaim na Timu yake yote wameipongeza sana Serikali na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa michango mikubwa ya kifedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo Musoma Vijijini.

Vilevile, Wananchi na Viongozi wao wa Chama na Serikali wa Musoma Vijijini wamepongezwa sana kwa kazi nzuri wazifanyazo kwenye utekelezaji ya miradi ya maendeleo ya vijijini mwao.

Jimbo la Musoma Vijijini lina jumla ya Kata 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374.

Wanavijiji na Viongozi wao mbalimbali wanaendelea kushirikiana na Serikali kujenga na kuboresha miundombinu ya utoaji wa Huduma za Afya kwenye maeneo yao ya vijijini, kama ifuatavyo:

(I) Hospitali ya hadhi ya Wilaya (1):
*Inaendelea kujengwa kwenye Kitongoji cha Kwikonero, Kijijini Suguti. Huduma ndogo ndogo (OPD) zimeanza kutolewa hapo.

(II) Vituo vya Afya (6):
*Vituo vya Afya vinavyotoa Huduma za Afya ni vitatu (3) - Murangi, Mugango na Bugwema

*Vituo vipya vya Afya vinavyosubiri kupewa wafanyakazi na vifaa tiba ni vitatu (3) - Makojo, Kiriba na Kisiwani Rukuba (inatoa huduma kwa hadhi ya Zahanati)

(III) Zahanati (41):
*Zahanati zinazotoa Huduma za Afya ni ishirini na nne (24) - Bugoji, Bugunda, Bukima, Busungu, Bwai Kwitururu, Chitare, Etaro, Kiemba, Kigera Etuma, Kiriba, Kome, Kurugee, Kwikuba, Masinono, Mayani, Mmahare, Mwiringo, Nyakatende, Nyambono, Nyegina, Rusoli, Seka, Suguti na Wanyere

*Zahanati Binafsi zinatoa Huduma za Afya ni nne (4) - Bwasi (SDA), Mji wa Huruma (Katoliki), Kwibara (KMT) na Rwanga (KMT)

*Zahanati Mpya zinazojengwa ni kumi na tatu (13) - Burungu, Butata, Chanyauru, Chimati, Chirorwe, Kaburabura, Kakisheri, Kurukerege, Kurwaki, Maneke, Mkirira, Nyambono na Nyasaungu

(IV) Magari ya kusafirisha Wagonjwa (Ambulances)
*Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ameleta na kugawa magari matano (5) ya Wagonjwa kama ifuatavyo: Kituo cha Afya cha Murangi (ambulance kubwa ya kisasa), Zahanati za vijiji vya Masinono (sasa Kituo cha Afya cha Bugwema), Kurugee, Nyakatende na Mugango (sasa Kituo cha Afya cha Mugango)

Mwenge wa Uhuru Kijijini Kurwaki
Jana, Jumatatu, 10.7.2023, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndugu Abdalla Shaibu Kaim aliweka Jiwe la Msingi kwenye Zahanati ya Kijiji cha Kurwaki iliyoanza kujengwa na Wananchi wa Kijiji hicho wakishirikiana na Mbunge wa Jimbo, Madiwani na Viongozi wao wengine.

Serikali imeanza kuchangia kwa kutoa Tsh Milioni 50 kwenye ujenzi wa Zahanati hii.

Mwenge wa Uhuru Jimboni mwetu:
*Mkuu wa Wilaya (DC) yetu, Dr Khalifan Haule na Mwenyekiti wa CCM Wilaya yetu, Ndugu Denis Ekwabi, na Timu zao, wanapongezwa sana kwa kusimamia na kuratibu mbio za Mwenge Jimboni mwetu kwa mafanikio makubwa sana - Ahsanteni sana!

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumanne, 11.7.2023

KISIWA CHA RUKUBA KIMEKAMILISHA UJENZI WA KITUO CHA AFYA

Majengo ya Kituo cha Afya cha Kisiwa cha Rukuba, Musoma Vijijini.

Kisiwa cha Rukuba kiko ndani ya Kata ya Etaro yenye vijiji vinne (Busamba, Etaro, Mmahare na Kisiwa cha Rukuba).

Kisiwa hiki cha Musoma Vijijini kina Shule ya Msingi yenye vyumba vya madarasa vya kutosha ikiwepo ziada ya vyumba viwili. Madawati yapo ya kutosha kwa wanafunzi wote. Ofisi mbili (2) za Walimu zipo.

Maktaba ya shule ipo. Kila Mwalimu amepatiwa makazi mazuri. Wana-Rukuba na Mbunge wao wa Jimbo wameanza ujenzi wa Sekondari hapo Kisiwani.

Kukamilika kwa ujenzi wa Kituo cha Afya:
*Wakazi wa Kisiwa cha Rukuba waliamua kupanua Zahanati yao iwe Kituo cha Afya.

*Upanuzi huo ulianza kutekelezwa kwa kutumia michango ya fedha na nguvukazi za wananchi na Mbunge wao, Prof Sospeter Muhongo.

Tsh Milioni 500 kutoka Serikalini:
*Wakazi wa Kisiwa cha Rukuba na Viongozi wao wanaishukuru sana Serikali kwa kuwapatia Tsh Milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya hapo Kisiwani

*Kituo cha Afya kimekalika na kiko tayari kutumika. Majengo manne (4) na miundombinu yake yaliyokamilika ni:
(i) Mama & Mtoto
(ii) Maabara
(iii) Upasuaji
(iv) Ufuaji

Jengo la OPD litatumika lile la Zahanati wakati Jengo jipya likiwa linakamilishwa.

Ombi la Wafanyakazi & Vifaa Tiba:
Wakazi wa Kisiwani Rukuba wanaiomba Serikali (TAMISEMI & Wizara ya Afya) iwapelekee Wafanyakazi na Vifaa Tiba ili Kituo hicho kianze kutoa huduma za Afya Kisiwani hapo - Wakazi wa hapo Kisiwani wanataka wapunguze sana kusafirisha wagonjwa mahututi na mama wajawazito kwenye mitumbwi kwenda Musoma Mjini kwa matibabu!

SHUKRANI
Wananchi wakazi wa Kisiwa cha Rukuba na Viongozi wote wa Musoma Vijijini wanaendelea kutoa shukrani zao za dhati kwa Serikali yetu na kwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwapatia fedha za miradi ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya huduma za afya vijijini mwao.

Tafadhali usiache kutembelea TOVUTI yetu ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumamosi, 8.7.2023

WANAVIJIJI WAENDELEA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUJENGA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI KWENYE SEKONDARI ZAO ZA KATA

Wanafunzi wa Kiriba Sekondari wakiwa wanafanya mazoezi kwenye Maabara yao ya Kemia (Chemistry practical class)

Wanavijiji wa Jimbo la Musoma Vijijini wamedhamiria kujenga MAABARA TATU za masomo ya sayansi kwenye Sekondari zao za Kata. Maabara hizo ni za masomo ya Fizikia, Kemia na Baiolojia.

Jimbo letu lenye Kata 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374 lina jumla ya Sekondari 25 za Kata, na 2 za Binafsi (Katoliki & SDA).

Vyanzo vya MICHANGO ya ujenzi wa Maabara hizo ni:
*Michango ya fedha taslimu kutoka kwa Wanavijiji na Mbunge wao wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo

*Nguvukazi za Wanavijiji - kusomba mawe, kokoto, mchanga, maji na kuchimba misingi ya majengo

*Fedha za Mfuko wa Jimbo

*Fedha kutoka Serikali Kuu, yaani TAMISEMI na Wizara ya Elimu

*Wadau wa Maendeleo zikiwemo Benki za NMB, CRDB, NBC na POSTA

*Baadhi ya Wazaliwa wa Musoma Vijijini

Sekondari zenye Maabara 3 za Masomo ya Sayansi zilizokamilika na zinazotumika ni:
(1) Mugango, Kata ya Mugango, (2) Bugwema, Kata ya Bugwema, (3) Kiriba, Kata ya Kiriba, (4) Nyakatende, Kata ya Nyakatende, na (5) Ifulifu, Kata ya Ifulifu.

(6) Makojo Sekondari ya Kata ya Makojo, itakamilisha maabara ya tatu kabla ya tarehe 30.7.2023

Sekondari nyingine 19 za Kata zinaendelea na ujenzi wa Maabara 3, na lengo ni kukamilisha ujenzi huo mwakani, kabla ya Julai 2024.

Sekondari 4 mpya zinazojengwa (Nyasaungu, Muhoji, Wanyere na Rukuba Kisiwani) lazima majengo ya maabara 3 za masomo ya sayansi yawe sehemu ya ujenzi wa sekondari hizo.

Halmashauri yetu (Musoma DC) inaendelea kushawishiwa na kuombwa nayo ianze kuchangia, kwa kutumia mapato yake ya ndani, ujenzi wa Maabara na Maktaba kwenye shule zetu!

Musoma Vijijini inaomba ipewe "High Schools" za Masomo ya Sayansi:
*Sekondari 6 zilizotajwa hapo juu ziko tayari kuanza kupokea Wanafunzi wa Form V (Kidato cha V) mwakani, Julai 2024

Masomo ya Hisabati na Sayansi kwa ngazi ya awali ya shule za msingi na sekondari ndiyo msingi imara wa taaluma mbalimbali za kiufundi zinazotoa, kwa uharaka, ajira ndani na nje ya nchi.

SHUKRANI
Wanafunzi wa Sekondari za Kata za Musoma Vijijini, Wazazi na Viongozi wao wa ngazi zote, wanaishukuru Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuchangia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya elimu Jimboni mwetu - Ahsante sana.

Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha:
*Wanafunzi wa Kiriba Sekondari wakiwa wanafanya mazoezi kwenye Maabara yao ya Kemia (Chemistry practical class)

*Maabara 2 (Chemistry & Biology laboratories) za Makojo Sekondari zilizokamilishwa ujenzi hivi karibuni. Ujenzi wa Maabara ya tatu (Physics laboratory) ya Sekondari hii utakamilishwa kabla ya tarehe 30.7.2023

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumapili, 2.7.2023

WANAVIJIJI WAPATA MATUMAINI MAKUBWA YA KUANZA KUTUMIA MAJI YA BOMBA

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijinini, Prof Sospeter Muhongo akiongea na WANANCHI wa Vijiji 3 (Tegeruka, Mayani na Kataryo) vya Kata ya Tegeruka. Hiyo ilikuwa siku ya Jumapili, 11.6.2023 wakati Mbunge huyo alipofanya ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa maji ya bomba kwenye vijiji hivyo.

Kata nne (4) zenye jumla ya Vijiji 12, za Jimbo la Musoma Vijijini, zina miradi ya kusambaziwa maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria.

Mradi wa Bomba Kuu la Maji la Mugango-Kiabakari-Butiama
*Gharama za Mradi: Tsh bilioni 70.5
*Uwezo wa uzalishaji: Lita milioni 35 kwa siku
*Mitambo ya kusukuma maji inayotengenezwa China, Hungary na Turkey italetwa nchini hivi karibuni

Ujenzi wa Miundombinu ya usambazaji wa maji ya bomba kutoka Bomba Kuu la Mugango-Kiabakari-Butiama

Kata za Tegeruka na Mugango
*Gharama za Mradi: Tsh bilioni 4.75
*Ujenzi umeanza tokea wiki iliyopita na Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo alienda kukagua ujenzi huo

*Mitaro ya urefu wa takriban km 15 tayari imechimbwa na bomba zitaanza kutandazwa hivi karibuni

*Tenki lenye ujazo wa LITA 135,000 linajengwa Kijijini Kataryo. Hili tenki litapokea maji kutoka kwenye Tenki la Kijijini Kiabakari lenye ujazo wa LITA MILIONI 3

Kata za Busambara na Kiriba
*Tenki la ujazo wa LITA 500,000 limejengwa kwenye Mlima wa Kong'u, Kijijini Kwibara, Kata ya Mugango

*Vijiji 6 vya Kata za Busambara na Kiriba vitapata maji ya bomba kutoka kwenye Tenki hili.

*Miundombinu ya usambazaji wa maji ya bomba kwenye Kata hizi mbili itaanza kujengwa, hivi karibuni, August 2023

SHUKRANI:
Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaishukuru sana Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji ya bomba vijijini mwetu. Kila kijiji kinao mradi wa maji! Ahsante sana!

PICHA
Picha hapo juu  inamuonesha Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijinini, Prof Sospeter Muhongo akiongea na WANANCHI wa Vijiji 3 (Tegeruka, Mayani na Kataryo) vya Kata ya Tegeruka. Hiyo ilikuwa siku ya Jumapili, 11.6.2023 wakati Mbunge huyo alipofanya ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa maji ya bomba kwenye vijiji hivyo.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatano, 14.6.2023

SERIKALI YATOA MCHANGO MKUBWA WA TSH MILIONI 573 KWENYE UJENZI WA WANYERE SEKONDARI

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo akiwa na Wanakijiji kwenye Mkutano uliofanyika jana Kijijini hapo kwenye eneo la ujenzi wa Sekondari mpya, ambayo inajengwa ndani ya Kitongoji cha Mwikoro, Kijijini Wanyere, Kata ya Suguti, Musoma Vijijini.

Jimbo la Musoma Vijijini laendelea kutatua matatizo yanayowakabili wanafunzi wanaosoma kwenye Sekondari za Kata za Jimboni humo.

Matatizo makuu yanayowakabili ni:
*umbali mrefu wa kutembea kwenda masomoni
*mirundikano ya wanafunzi madarasani
*upungufu au ukosefu wa maabara za masomo ya sayansi
*ukosefu wa maktaba
*upungufu mkubwa wa walimu, hasa wa masomo ya Sayansi na Lugha.

Ujenzi wa Sekondari mpya Kijijini Wanyere:
Kijiji cha Wanyere ni moja ya vijiji vinne (Chirorwe, Kusenyi, Suguti na Wanyere) vya Kata ya Suguti yenye Sekondari moja iliyoko Kijijini Suguti

Wanafunzi wa Kijiji cha Wanyere wanalazimika kutembea zaidi ya KILOMITA 30 kwenda na kurudi kutoka masomoni kwenye Sekondari yao ya Kata. Baadhi ya wanafunzi wamepanga vyumba (na wanajipikia) karibu na eneo la shule hiyo.

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo alitembelea Kijiji cha Wanyere kwa malengo makuu mawili:

*kupokea kero za Wanakijiji na kuzitatua
*kuhamasisha ujenzi wa sekondari mpya kijijini hapo.

Michango ya ujenzi wa Wanyere Sekondari:
Mbunge Prof Muhongo aliendesha HARAMBEE ya kuanza ujenzi huo na michango iliyotolewa ni kama ifuatavyo:

Wanakijiji wa Wanyere wameanza kuchangia:
*Nguvukazi za kusomba mchanga, mawe, maji na kuchimba msingi wa jengo moja la Madarasa 2 na Ofisi 1 ya Walimu

*Fedha taslimu takribani Tsh milioni 2.5

Wanakijiji wa Kataryo:
*Saruji Mifuko 30 imetolewa na Kijiji jirani cha Kataryo cha Kata jirani ya Tegeruka. Watoto wa Kijiji hiki jirani wanasoma Kijijini Wanyere.

Mbunge wa Jimbo:
*Saruji Mifuko 100 - Prof Muhongo ameanza kutoa michango yake kwa kuchangia saruji hiyo.

Halmashauri yetu (Musoma DC):
*bado haijatoa mchango wo wote!

Serikali Kuu (TAMISEMI):
Bajeti ya Mwaka 2023/2024, Serikali itatoa Tsh Milioni 573 kupitia Mradi wake wa SEQUIP kwa ajili ya ujenzi wa Sekondari mpya Kijijini Wanyere. Hii itakuwa Sekondari ya pili ya Kata ya Suguti.

Wananchi na Viongozi wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaishukuru Serikali, chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuongeza ubora wa utoaji wa elimu Jimboni mwao.

Usisahau kutembelea TOVUTI ya Jimbo letu ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Alhamisi, 1.6.2023

 

KIJIJI CHA NYASAUNGU CHADHAMIRIA KUFUNGUA SEKONDARI YAKE JANUARI 2024

Kikao cha Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini na Wananchi wa Kijiji cha Nyasaungu, Kata ya Ifulifuli, Musoma Vijijini.

Leo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, ametembelea Kijiji cha Nyasaungu, Kata ya Ifulifu kwa lengo la kutathmini utekelezaji wa miradi yao ya maendeleo.

Miradi inayotekelezwa Kijijini hapo ni ya:
*Ujenzi wa Sekondari
*Ujenzi wa Zahanati
*Uboreshaji wa miundombinu ya elimu kwenye shule yao ya msingi (S/M Nyasaungu)

Kero zilizotolewa na kupata majibu kutoka kwa Mbunge huyo ni kuhusu upungufu mkubwa kwenye upatikanaji wa:
*maji
*umeme
*chakula (ukame)
*walimu wa S/M Nyasaungu

*Ujenzi wa Nyasaungu Sekondari
Kata ya Ifulifu haikuwa na Sekondari yake, na inashukuru Serikali kuchangia kwa kiasi kikubwa sana ujenzi wa Sekondari ya Kata (Ifulifu Sekondari), Kijijini Kabegi.

Kijiji cha Nyasaungu ni moja ya vijiji vitatu vya Kata ya Ifulifu. Kijiji hiki kiko pembezoni na mbali na vijiji vingine vya Kata hii. Vilevile, jiografia yake (mito, vichaka, n.k.) inakifanya kuwa na ugumu wa kufikika, hasa wakati wa mvua - mazingira haya ni hatarishi kwa wanafunzi!

Ujenzi wa Nyasaungu Sekondari umeanza kwa kutumia michango ya:
*Wanakijiji
*Mbunge wa Jimbo
*Mfuko wa Jimbo

Halmashauri inaombwa ianze kuchangia ujenzi wa Sekondari hii ambayo watumiaji wake wengi watakuwa watoto wa wafugaji wa Kijiji cha Nyasaungu.

Nyasaungu Sekondari kufunguliwa Januari 2024
Ujenzi umefikia hatua ya kukamilisha:
*Vyumba 3 vya Madarasa
*Choo cha Matundu 6
*Jengo la Utawala

Michango ya Mbunge wa Jimbo
Mbunge wa Jimbo ataendelea kuchangia ujenzi huu kama alivyofanya hapo awali.

Wanakijiji wameamua kuendelea na ujenzi wa Sekondari yao kuanzia tarehe 10.6.2023. Wakianza ujenzi tarehe hiyo Mbunge huyo atawachangia saruji na mabati.

Kwa sasa, Jimbo letu linajenga Sekondari nne (4) mpya, ambazo ni:
*Nyasaungu Sekondari
(Kata ya Ifulifu, sekondari ya pili ya Kata)
*Muhoji Sekondari
(Kata ya Bugwema, sekondari ya pili ya Kata)
*Wanyere Sekondari
(Kata ya Suguti, sekondari ya pili ya Kata)
*Sekondari ya Kisiwa cha Rukuba
(Kata ya Etaro, sekondari ya pili ya Kata)

Jimbo letu lenye Kata 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374, lina jumla ya Sekondari 27 (25 za Kata, na 2 za binafsi)

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumanne, 30.5.2023

SEKONDARI ZA KATA ZAENDELEA KUJENGA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI

Ujenzi wa Maabara 3 (Physics, Chemistry & Biology) za Mtiro Sekondari ya Kata ya Bukumi, Musoma Vijijini.

Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 lina Sekondari za Kata 25 na za Binafsi 2.

Jimbo hili limeamua kujenga Maabara 3 za Masomo ya Sayansi kwenye kila Sekondari ya Kata. Maabara hizo ni za Physics, Chemistry & Biology.

Sekondari 3 tu kati ya 25 ndizo zina maabara 3, nyingine zinazo mbili au moja.

Sekondari mpya zinazoendelea kujengwa na Wanavijiji lazima ziwe na maabara hizo.

Kwa hiyo, Fedha zote za Mfuko wa Jimbo, zinatumika kwenye ujenzi wa maabara hizo.

MTIRO SEKONDARI
*Sekondari ya Kata ya Bukumi yenye Vijiji 4 (Buira, Bukumi, Buraga & Busekera)
*Ilifunguliwa Mwaka 2006
Haina maabara hata moja

WANAFUNZI WA MTIRO SEKONDARI
*Jumla ya Wanafunzi ni 681
*Jumla ya Walimu wa ajira ya Serikali ni 13, na 4 ni Walimu wa muda (kujitolea) wanaopewa posho kutoka kwa Wazazi wenye watoto shuleni hapo.

Mwitikio wa Masomo ya Sayansi
*Walimu wanaofundisha Masomo ya Sayansi ni wanne (4)
*Walimu wanaofundisha Hisabati (Maths) ni wawili (2)

Jumla ya Wanafunzi wa Form III ni 110
*14 wanasoma Physics
*17 wanasoma Chemistry
*110 wanasoma Biology (kwa kulazimika)

Jumla ya Wanafunzi wa Form IV ni 123
*21 wanasoma Physics
*26 wanasoma Chemistry
*123 wanasoma Biology (kwa kulazimika)

UMUHIMU WA KUWEPO MAABARA KWENYE SEKONDARI
*Takwimu hizo hapo juu zinaonesha mwitikio mdogo sana wa wanafunzi wetu kupenda kusoma Masomo ya Sayansi

*Kuwepo kwa Maabara za Masomo ya Sayansi ni muhimu kwa kufundishia (Walimu) na kwa kujifunza, hasa kwa vitendo (Wanafunzi)

MTIRO SEKONDARI WANAJENGA MAABARA 3 ZA MASOMO YA SAYANSI

Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo, alipiga Harambee ya ujenzi wa Maabara 3 za Masomo ya Sayansi, na matokeo ni MICHANGO ifuatayo:

Wanavijiji wa Vijiji 4
(michango inaendelea kutolewa)
*Nguvukazi ya kuchimba misingi
*Mchanga trip 27
*Kokoto trip 2
*Saruji Mifuko 8
*Fedha taslimu Tsh 1,508,000
*Wazaliwa wa Kata ya Bukumi & Wadau wengine
Tsh 1,500,000

Mbunge wa Jimbo
*Saruji Mifuko 150 (ameanza kwa kutoa 75)

Mfuko wa Jimbo
(Mwenyekiti, Mbunge wa Jimbo)
*Saruji Mifuko 200
*Nondo 49

MAOMBI KUTOKA KWA WANANCHI WA MUSOMA VIJIJINI
Halmashauri yetu (Musoma DC) ianze kuchangia ujenzi wa Maabara za Masomo ya Sayasi kwenye Sekondari zake za Kata, isusibiri kufanya kazi ya kuratibu fedha zinazotolewa na Serikali Kuu!

*Wazaliwa wa Musoma Vijijini waanze au waendelee kuchangia Sekondari za Kata za kwao kwenye ujenzi wa Maabara za Masomo ya Sayansi, na Maktaba.

SAYANSI NI KILA KITU

UCHUMI WA KISASA UNAHITAJI SAYANSI

MAFANIKIO MAKUBWA YA KIUCHUMI YA CHINA, INDIA & BRAZIL YANAENDANA NA UWEKEZAJI MKUBWA KWENYE SAYANSI

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatatu, 24.4.2023

BARABARA KUU PEKEE YA MUSOMA VIJIJINI INAHITAJI KUWEKEWA LAMI: HAIJAPITIKA KIURAHISI KWA ZAIDI SIKU TANO (5)

Eneo la maafa, Kijiji cha Kusenyi, Kitongoji cha Kwikuyu, Musoma Vijijini.

Barabara ya Musoma-Makojo-Busekera (km 92)

*Mvua zinazonyeesha wakati huu zinaleta maafa kwa baadhi ya vijiji vilivyoko pembezoni mwa barabara hii.

*Jana usiku na leo asubuhi, Kijiji cha Kusenyi, Kitongoji cha Kwikuyu kimekumbwa na mafuriko makubwa. Wakazi wa hapo wamepoteza mali zao, kikiwemo chakula walichokuwa wamehifadhi majumbani mwao.

*Mkandarasi aliyejenga km 5 kwenye hili barabara la urefu wa km 92 analalamikiwa kwa kuziba vidaraja vidogo vidogo vilivyokuwa vinapitisha maji kwenda ziwani (Ziwa Victoria)

Umuhimu wa barabara ya Musoma-Makojo-Busekera

*Vijiji 68 vya Musoma Vijijini vinaunganishwa na barabara kuu moja tu, ambayo ni hii ya Musoma-Makojo-Busekera

*Barabara hii inaunganisha Musoma Vijijini na Wilaya nyingine za Mkoa wa Mara, na hatimae inaunganisha Musoma Vijijini na Mikoa ya jirani ya Mwanza, Simiyu, Manyara na Arusha

*Barabara hii inaunganisha Musoma Vijijini na Kiwanja cha Ndege cha Musoma Mjini (& Mwanza), na Bandari ya Meli iliyopo Musoma Mjini

Mazao ya uvuvi (dagaa, sangara na sato) yanasafirishwa kutumia barabara hii.

Mazao ya Kilimo, yaani, mihogo, viazi vitamu, mpunga, mahindi, mtama, matunda, mbogamboga, pamba, alizeti, n.k. yanasafirishwa kutumia barabara hii.

Dhahabu na madini mengine yanasafirishwa kutumia barabara hii.

Wizara ya Ujenzi & Uchukuzi

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo na Viongozi wengine wa Chama (CCM) na Serikali wanaendelea kuiomba Wizara ya Ujenzi & Uchukuzi kuipa kipaumbele barabara hili ijengwe kwa kiwango cha lami.

1980 - 2023
Maombi ya Wana Musoma Vijijini na Viongozi wao ya barabara hii kujengwa kwa kiwango cha lami ni tokea Mwaka 1980!

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe: Jumatatu, 3.4.2023

DHORUBA KUBWA NDANI YA ZIWA VICTORIA YAFANYA UHARIBIFU WA MITUMBWI NA NYAVU – TUNAOMBA MCHANGO WAKO

Sehemu ya uharibifu uliofanyika kwenye Mwalo wa Kijiji cha Busekera, Kata ya Bukumi, Musoma Vijijini

Upepo wenye kasi kubwa na mvua kubwa vilisababisha kuwepo kwa dhoruba kubwa ndani ya Ziwa Victoria juzi tarehe 20.3.2023.

Mialo ya Musoma Vijijini ilikumbwa na dhoruba hiyo na uharibifu mkubwa umefanyika.

Tunaomba tushirikiane kuwachangia wavuvi wetu walioathirika na janga hili.

TATHMINI YA UHARIBIFU

(1) Mitumbwi ya Mwalo wa Kijiji cha Busekera
*Iliyoharibika: 137
*Inayotengenezeka: 108
*Isiyotengenezeka: 29
*Makokoro ya dagaa yaliyoharibika: 29

(2) Mitumbwi ya Mwalo wa Kijiji cha Buira
*Iliyoharibika: 39
*Inayotengenezeka: 29
*Isiyotengenezeka: 10
*Makokoro ya dagaa yaliyoharibiwa: 15

(3) Mitumbwi ya Mwalo wa Kijiji cha Bwai Kumsoma
*Iliyoharibika: 25
*Inayotengenezeka: 21
*Isiyotengenezeka: 4
*Makokoro ya dagaa yaliyoharibika: 15

(4) Mitumbwi ya Mwalo wa Kijiji cha Kasoma
*Iliyoharibika: 10
*Inayotengenezeka:9
*Isiyotengenezeka:1
*Makokoro ya dagaa yaliyoharibika: 3

GHARAMA ZA MATENGENEZO
Mifano ya hapa chini itakupatia picha unayoweza kuitumia kutoa mchango wako.

(1) Gharama za kutengeneza Mtumbwi
*Tsh 1,700,000
*Ubao 1 wa 9"x10"
Tsh 12,000

(2) Gharama za kutengeneza Kokoro la Dagaa
*Tsh 1,400,000

UWASILISHAJI WA MCHANGO WAKO

Tafadhali mpelekee:
DC Wilaya ya Musoma
Simu: 0756 088 624

Michango ya awali:
*Tungalipenda kuanza kuwasilisha michango yetu ya awali kwa wavuvi waathirika siku ya Alhamisi, 30.3.2023

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatano, 22.3.2023

WANAVIJIJI WAAMUA KUJENGA MAABARA TATU NDANI YA MIEZI MITATU

matukio mbalimbali ya: *HARAMBEE ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini ya kuchangia ujenzi wa Maabara za Mtiro Sekondari. Harambee ilifanyika shuleni hapo. *Usombaji wa Saruji na Mchanga wa kuanzia ujenzi

Wanavijiji wa Kata ya Bukumi wameamua kujenga Maabara 3 za Masomo ya Sayansi kwenye Sekondari yao ya Kata, Mtiro Sekondari.

Kata ya Bukumi ina vijiji vinne ambavyo ni Buira, Bukumi, Buraga na Busekera.

TAKWIMU ZA MTIRO SEKONDARI
*ilifunguliwa Mwaka 2006
*idadi ya wanafunzi ni 682
*idadi ya walimu ni 17 (13 wenye ajira ya Serikali na 4 wa kujitolea)
*hakuna Maktaba
*hakuna Maabara hata moja ya Masomo ya Sayansi

*wanafunzi 17 kati ya 110 wa Kidato cha Tatu (Form III), 15.5%, ndio wanasoma Masomo ya Sayansi

*wanafunzi 25 kati ya 123 wa Kidato cha Nne (Form IV), 20.3%, ndio wanasoma Masomo ya Sayansi

*wanafunzi 5 kati ya 682 ndio wamechangia chakula cha mchana

HARAMBEE YA MBUNGE WA JIMBO
Alhamisi, 9.3.2023, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo aliendesha HARAMBEE shuleni hapo kwa lengo la kupata fedha za ujenzi wa Maabara 3 za Masomo ya Sayansi (Fizikia, Kemia & Baiolojia) za Mtiro Sekondari.

MATOKEO YA HARAMBEE
*Michango ya Wanavijiji iliongozwa na Diwani wao, Mhe Munubhi Musa. Wazaliwa wa Kata ya Bukumi nao wameanza kuchangia.

Fedha Taslimu:
Tsh 494,000
Fedha (ahadi)
Tsh 4,493,000
Saruji Mifuko 26
Mchanga Lori 5

*Michango ya Mbunge wa Jimbo, ameanza kwa kutoa:
Saruji Mifuko 150

UJENZI KUANZA JUMATATU, 13.3.2023
*Wanavijiji na Viongozi wao wa Kata ya Bukumi wameamua kuanza kutekeleza mradi huu mara moja.

*Mchanga wa kuanzia kazi tayari umesombwa

*Saruji Mifuko 75 kati ya 150 iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo tayari imefikishwa shuleni.

*Ifikapo Juni 2023, maabara 3 ziwe zimekamilika.

MAWASILIANO YA KUTOA MCHANGO WAKO
*Headmaster
Mtiro Sekondari
0758 487 478

WADAU wa MAENDELEO:
Wanavijiji wa Kata ya Bukumi wanaomba sana Wadau wa Maendeleo wajitokeze kuchangia utekelezaji wa mradi huu ambao ni muhimu sana kwa uboreshaji wa miundombinu ya elimu itolewayo Mtiro Sekondari - tunatanguliza shukrani zetu za dhati kwa wachangiaji wote.

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini anaendelea na kampeni yake ya kuhamasisha na kuchangia ujenzi wa Maabara 3 za Masomo ya Sayansi kwenye Sekondari zote za Jimboni mwao.

Picha za hapa zinaonesha matukio mbalimbali ya:
*HARAMBEE ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini ya kuchangia ujenzi wa Maabara za Mtiro Sekondari. Harambee ilifanyika shuleni hapo.
*Usombaji wa Saruji na Mchanga wa kuanzia ujenzi

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumamosi, 11.3.2023

MDAU WA MAENDELEO ACHANGIA UJENZI WA MAABARA ZA SAYANSI KWENYE SEKONDARI ZA MUSOMA VIJIJINI

Sekondari 3 za Musoma Vijijini zikikabidhiwa Saruji Mifuko 153 kutoka Umoja Security Services yenye Makao Makuu jijini Dar es Salaam.

Leo, Jumatano, 8.3.2023, mmoja wa Wadau wa Maendeleo hapa nchini, NGUVU MOJA SECURITY SERVICES amechangia Tsh 3,520,000 (Tsh 3.52m) kwa ajili ya ujenzi wa MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI (physics, chemistry & biology laboratories) kwenye baadhi ya Sekondari za Musoma Vijijini.

Mwakilishi wao, Afisa wa Polisi Mstaafu, ASP Moyo amekabidhi mchango huo kwenye Duka la kuuza vifaa vya ujenzi la Musoma Mjini. Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo, alikuwepo kushudia tukio hilo.

Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 zenye jumla ya Vijiji 68 na Vitongoji 374 lina jumla ya Sekondari:
*25 za Kata
*2 za binafsi
(madhehebu ya Dini)

Mbunge Jimbo anahamasisha na kuchangia ujenzi wa Mabaara za Masomo ya Sayansi kwenye Sekondari zote 27.

Lengo kuu ni kuwapatia Wanafunzi wa Sekondari zetu fursa nzuri ya kupata elimu ya vitendo, na kuongeza uelewa wao wa masomo ya sayansi.

Vile vile, ujenzi huu wa maabara tatu za masomo ya sayansi kwa kila sekondari ni matayarisho yetu ya kuanzisha HIGH SCHOOLS za MASOMO ya SAYANSI Jimboni mwetu.

Sekondari tatu zilizopokea saruji kwa ujenzi wa maabara zao ni:

Seka Sekondari
*imepokea Saruji Mifuko 51
*haina maabara hata moja
*ilifunguliwa Mwaka 2021
*Mwanafunzi 344
*Walimu 7
*hii ni Sekondari ya pili ya Kata ya Nyamrandirira

Bwai Sekondari
*imepokea Saruji Mifuko 51
*haina maabara hata moja
*ilifunguliwa Mwaka 2023
*Mwanafunzi 139
*Walimu 5
*hii ni Sekondari ya pili ya Kata ya Kiriba

Muhoji Sekondari
*imepokea Saruji Mifuko 51
*Sekondari mpya inajengwa ifunguliwe mwakani (2024)
*hii ni Sekondari ya pili ya Kata ya Bugwema

TUNAKUKARIBISHA UCHANGIE UJENZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU KWENYE SHULE ZA MUSOMA VIJIJINI

Usisahau kutembelea Tovuti ya Jimbo letu ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumanne, 8.3.2023

 

SEHEMU YA PILI YA TAARIFA YA KIKAO CHA MBUNGE WA JIMBO NA WAKUU WA SHULE ZA MUSOMA VIJIJINI

 Walimu Wakuu wa Sekondari za Musoma Vijijini wakiwa na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini kwenye Kikao chao cha tarehe 3.2.2023 kilichofanyika Busambara Sekondari, Kijijini Kwikuba.

Sehemu ya Kwanza ya Taarifa ya Kikao hicho:

Sehemu hii ilitolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo.

*Mahali inapopatikana ni kwenye TOVUTI ya Jimbo letu ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz

SEHEMU YA PILI - UFAULU WA FORM II & IV (2020, 2021& 2022)

*Kwa nini ufaulu siyo mzuri kwenye Sekondari zetu za Musoma Vijijini?

*Nini kifanyike kuongeza UELEWA na UFAULU kwa wanaojifunza (WANAFUNZI)

*Nini kifanyike kuongeza UMAHIRI na UWAJIBIKAJI wa kufundisha kwa WALIMU wetu?

*Majukumu ya WAZAZI ni yapi?

(1) Matokeo yakutoridhisha ya Mwaka jana (2022)
*Kubadilika kwa mfumo wa utungaji wa mitihani unaozingatia umahiri, yaani, "competence based" badala ya ule mfumo uliozoeleka wa kukariri. Matayarisho ya mabadiliko hayo hayakuwepo.

(2) Matokeo ya kutoridhisha ya Miaka 3 mfululizo (2020, 2021 & 2022)

(2a) WANAFUNZI
*Kutembea umbali mrefu kwenda masomoni. Wapo wanaotembea zaidi ya kilomita tano (5) kwenda masomoni

*Wanafunzi kukosa chakula wawapo masomoni (kifungua kinywa & chakula cha mchana)

*Wapo wanafunzi waliopanga vyumba kwenye vijiji vya karibu na Sekondari wanazosoma. Hawa wanafunzi wapangaji wanaishi kwa kujitegemea kama ziishivyo kaya zetu.

*Sekondari nyingi hazina Maabara na Vifaa vyake kwa masomo ya sayansi (chemistry, physics & biology laboratories)

*Sekondari karibu zote hazina Maktaba. Vitabu vya Maktaba vipo vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo

*Uhaba wa vitabu vya kiada ambapo uwiano unapaswa kuwa kitabu kimoja (1) kwa mwanafunzi mmoja (1). Uwiano huo kwa sasa, kwa baadhi ya Sekondari, ni kitabu kimoja (1) kwa wanafunzi watano (5).

*Lugha ya kufundishia ya Kiingereza bado ni tatizo.

Hata lugha yetu ya Taifa (Kiswahili) bado uelewa na ufaulu wake hauridhishi.

(2b) WALIMU
*Upungufu mkubwa wa walimu ambao hauendani na uwiano wa walimu na wanafunzi (ratio: teacher/students). Kwa mfano ipo Sekondari ina wanafunzi 1,012 na walimu 13 tu! Ipo Sekondari mpya yenye wanafunzi 158 na walimu 5!

*Uhaba mkubwa wa walimu wa masomo ya sayansi. Kwa mfano, kuna Sekondari zenye mwalimu mmoja (1) tu wa Hisabati na mmoja (1) tu wa Fizikia kwa madarasa yote (Form I hadi IV)!

*Upungufu na uhaba mkubwa wa walimu unalazimisha Sekondari kufanya yafuatayo:
(i) kuajiri walimu wa kujitolea ambao wanalipwa posho na wazazi, na Mbunge wa Jimbo huwa anachangia kwa baadhi ya Sekondari
(ii) kuweka wanafunzi kati ya 50 na 60, au zaidi ndani ya chumba kimoja cha darasa ili kupunguza mizigo ya vipindi vyingi kwa baadhi ya walimu.

MAPENDEKEZO YA KUONGEZA UBORA WA KUJIFUNZA NA KUFUNDISHA KWENYE SHULE ZETU

(1) WANAFUNZI & WALIMU
*Mapungufu na mahitaji yaliyoelezwa hapo juu, kwa upande wa Wanafunzi & Walimu, yatatuliwe kwa ushirikiano wa Wahusika wote.

(2) WAZAZI
*Wazazi watimize wajibu wao wa malezi mazuri ya watoto wao, na wafuatilie kwa karibu sana mienendo na tabia za watoto wao, k.m. kushinda kwenye runinga (TV), kubeti, kamari na kucheza pool.

*Wazazi watimize wajibu wao wa kuwanunulia watoto wao mahitaji ya shule na elimu kwa ujumla.

*Wazazi wakubali kuchangia chakula cha mchana cha watoto wao wawapo masomoni.

*Wazazi waache kuwapa watoto wao kazi za kiuchumi za familia wawapo masomoni, kwa mfano, kuwatuma kuchunga mifugo, kuvua samaki, kuchimba madini, na kuuza bidhaa sokoni wakati wa vipindi masomoni.

*Sera ya ELIMU BILA MALIPO iendelee kufanunuliwa na Wahusika ili Wazazi wasiache kutimiza wajibu wao wa kuchangia upatikanaji wa elimu nzuri kwa watoto wao.

*Wazazi na Walimu waendelee kuboresha uhusiano kati yao kwa manufaa ya uboreshaji wa elimu itolewayo kwenye shule zao.

(3) WALIMU
*Walimu waongezewe mafunzo wawapo kazini. Mafunzo yatolewe mara kwa mara ndani ya kipindi kifupi cha miaka 2-3.

*Kuwepo msawazo sawa kwa wingi (fair distribution) wa walimu kwenye Sekondari za vijijini na mijini ndani ya Halmashauri, Wilaya na Mkoa.

*Maslahi ya walimu yaboreshwe kwa kiwango kikubwa, yaani:
(i) Walimu wajengewe nyumba za kuishi hasa wale wanaofundisha vijijini
(ii) Mishahara ya Walimu iboreshwe sana na makato yake yapunguzwe.

Nchi ambazo zinaongoza Dunia kwa ubora wa elimu, mishahara ya walimu wao iko juu kuzidi taaluma nyingi nchini humo!

*Kitengo cha uthibiti ubora kiongezewe uwezo wa kufuatilia shughuli za ufundishaji na ujifunzaji mashuleni

*Kuimarisha lugha za kufundishia na kujifunzia kwa shule za Msingi na Sekondari

*Kutoa motisha kwa wanafunzi na walimu wanaofanya vizuri kwenye mitihani inayotolewa.

*Waliopewa majukumu ya kiuongozi ya kusimamia masuala ya elimu kwenye mashule wawe na uwezo wa kielimu wa kutekeleza majukumu yao.

ELIMU NI UCHUMI
ELIMU NI MAENDELEO

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatatu, 20.2.2023

 

SEKA SEKONDARI – WANAVIJIJI WAAMUA KUJENGA MAABARA TATU ZA MASOMO YA SAYANSI

Seka Sekondari ni sekondari ya pili ya Kata ya Nyamrandirira yenye vijiji vitano.

Sekondari hii iliyojengwa Kijijini Seka, Musoma Vijijini, ilifunguliwa tarehe 5.7.2021.

Sekondari ina jumla ya wanafunzi 344 (Vidato vya I, II & III) na Walimu tisa (9), mmoja akiwa ni wa kujitolea.

Mapungufu makubwa na muhimu ni ukosefu wa:
*Maabara 3 za masomo ya sayansi ya Fizikia, Kemia na Baiolojia.
*Maktaba
*Choo kingine chenye matundu 7
*Jengo la Utawala

HARAMBEE YA MBUNGE WA JIMBO

Leo, Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo, ameendesha HARAMBEE shuleni hapo kwa ajili ujenzi wa MAABARA 3 za masomo ya Sayansi.

MATOKEO YA HARAMBEE YA LEO:

*Wanavijiji wameamua kwamba Maabara hizo zikamilike ifikapo tarehe 30 Juni 2023.

*Wanavijiji watachangia nguvukazi na Tsh 15,000 kila kaya

*Vifaa vya ujenzi vilivyosalia kwenye ujenzi wa kutumia fedha za Serikali, vitumike mara moja, ikiwemo Saruji Mifuko 60.

*Viongozi mbalimbali wa Kata hiyo, wakiongozwa na Diwani wao, Mhe Mwl Nyeoje wamechangia Saruji Mifuko 12 na fedha taslimu Tsh 100,000

Michango ya Mbunge wa Jimbo:
*Saruji Mifuko 150
*Vitabu vya Maktaba box saba (7)
*Mahindi magunia manne (4) ya chakula cha wanafunzi

OMBI MAALUM LA UONGOZI WA SHULE:
Seka Sekondari isaidiwe kupata, computer, printer na photocopying machine - Wanakijiji na Mbunge wao wa Jimbo, watachanga kwa pamoja na kuvinunua ifikapo 30.4.2023

MICHANGO YA AWALI YA UJENZI WA SEKA SEKONDARI
Sekondari hii ilianza kujengwa kwa nguvu za WANAVIJIJI, MBUNGE WA JIMBO, WAZALIWA WA KATA YA NYAMRANDIRIRA na baadae SERIKALI imetoa michango mikubwa.

Michango hiyo ni kama ifuatavyo:

WANAVIJIJI
*Nguvukazi - kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji
*Kijiji cha Seka kilijenga na kuezeka vyumba 3 vya madarasa na kununua samani za ofisi za walimu
*Kijiji cha Kasoma kilijenga na kuezeka vyumba 2 vya madarasa
*Vijiji vya Mikuyu & Kaboni vilijenga na kuezeka maboma 2 ya madarasa
*Kijiji cha Chumwi kilichangia ujenzi wa boma moja la darasa na ujenzi wa choo cha walimu
*Wazazi wanachangia malipo ya posho za walimu wa kujitolea.

SERIKALI imechangia, kwa nyakati tofauti, Tsh MILIONI 25 + 80 + 60. Vifaa vya Maabara na Tsh 891,436,- kila mwezi (uendeshaji) kuanzia Oktoba 2022.

Wanavijiji wa Kata ya Nyamrandirira na Viongozi wao mbalimbali wanatoa shukrani za kipekee kwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa mchango mkubwa, wa ujenzi wa Sekondari yao, unaotolewa wa Serikali anayoingoza - AHSANTE SANA!

MBUNGE WA JIMBO
Michango yake ya awali, kwa nyakati tofauti, ni:
*Saruji Mifuko 200
*Mabati 120

Mfuko wa Jimbo umechangia:
*Saruji Mifuko 330
*Mabati 137
*Nondo 17

WAZALIWA WA KATA YA NYAMRANDIRIRA
Wazaliwa wa Kata hii wamechangia jumla ya Tsh 2,840,000,-

HALMASHAURI yetu hadi sasa mchango wake ni Saruji Mifuko 30 tu!

MGODI WA SEKA
Mchango wa Mgodi huu (MMG) wa dhahabu ni mdogo na hauridhishi!

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Alhamisi, 2.2.2023

 

HARAMBEE ZA MBUNGE WA JIMBO: SARUJI INAENDELEA KUTOLEWA

Viongozi kutoka Muhoji Sekondari wakipokea Saruji Mifuko 50

Jumatano, 25.1.2023, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo alitoa SARUJI MIFUKO 50 kuchangia ujenzi wa Sekondari mpya ya Kijijini Muhoji, Kata ya Bugwema.

Hiyo ni sehemu ya SARUJI MIFUKO 150 aliyoahidi kwenye HARAMBEE ya jana yake ya kuchangia Muhoji Sekondari.

Viongozi kutoka Muhoji Sekondari walikuwepo kupokea Saruji Mifuko 50.

Hii ni Sekondari ya pili ya Kata ya Bugwema

pia Mbunge huyo aliipatia Bwai Sekondari SARUJI MIFUKO 50 na MABATI BUNDLE 2 (mabati 24) Hii ni matokeo ya HARAMBEE ya tarehe 19.1.2023.

Bwai Sekondari ikimaliza hiyo Mifuko 50, itapewa Mifuko mingine 50. Ahadi ya Mbunge huyo ni kuchangia jumla ya Saruji Mifuko 100.

Hii ni Sekondari ya pili ya Kata ya Kiriba

KARIBUNI TUCHANGIE KWA VITENDO UJENZI NA UBORESHAJI WA SHULE ZETU

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatano, 25.1.2023

HARAMBEE YA UJENZI WA SEKONDARI MPYA KIJIJINI MUHOJI

Harambee ya ujenzi wa Muhoji Sekondari ya Kijijini Muhoji, Kata ya Bugwema.

Kijiji cha Muhoji ni moja kati ya vijiji vinne (4) vya Kata ya Bugwema - vingine ni Masinono, Kinyang'erere na Bugwema.

Kata hii ina Sekondari moja iitwayo Bugwema ambayo kwa sasa imeelemewa sana kwa sababu hizi:

*Kidato cha Kwanza (Form I) cha mwaka huu (2023) kina jumla ya WANAFUNZI 362 walioko kwenye Mikondo 7 ya wanafunzi 50 kwa kila mkondo. Iwapo kila mkondo ungalikuwa wa Wanafunzi 40, Form I hii ingalikuwa na Mikondo 9.

*Walimu 10 tu kwa Sekondari yenye jumla ya Wanafunzi 748.

Mbali ya mirundikano hiyo kwenye Bugwema Sekondari, bado wanafunzi wa kutoka Kijiji cha Muhoji wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilomita 24-30 kwenda na kurudu kutoka masomoni.

HARAMBEE YA MBUNGE WA JIMBO

Leo, Jumanne, 24.1.2023, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo ameendesha HARAMBEE ya kuchangia ujenzi wa MUHOJI SEKONDARI.

MICHANGO ILIYOPATIKANA

(i) Wanakijijiji wakiongozwa na Diwani wa Kata, Mhe Clifford Machumu wamechangia:

*Saruji Mifuko 124
*Fedha taslimu, Tsh 305,000

Michango hiyo ya wananchi ni mbali na michango yao mingine ya:
*Nguvukazi - kusomba mawe, mchanga na kokoto.
*Tsh 45,000 kwa kila kaya

(ii) DC wa Wilaya ya Musoma, Mhe Dkt Halfan Haule amechangia:

*Saruji Mifuko 20
*Jana alishiriki kwenye ufyatuaji wa matofali

(iii) Mbunge wa Jimbo amechangia:
*Saruji Mifuko 150
*Ataendelea kuchangia

MALENGO YALIYOWEKWA;

*Ujenzi wa Vyumba 4 vya Madarasa vyenye Ofisi 2 (katikati) za Walimu na Choo chenye Matundu 8 ukamilike kabla ya 30 Julai 2023

*Muhoji Sekondari ifunguliwe Januari 2024

TUNAKUKARIBISHA kuchangia ujenzi wa Muhoji Sekondari. Mchango wako mpelekee:

Mtendaji wa Kijiji (VEO)
Samwel Mourice
0686 557 264
0769 458 012

ELIMU NI UCHUMI
ELIMU NI MAENDELEO

KARIBU TUCHANGIE UJENZI WA SHULE ZETU

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumanne, 24.1.2023

 

MRADI WA BOMBA LA MAJI LA MUGANGO-KIABAKARI-BUTIAMA WAKAGULIWA NA KAMATI YA BUNGE

Mh. Mbunge wa Musoma Vijijini Prof Sospeter Muhongo akitoa mchango wake wakati wa ukaguzi huo

Jumamosi, 14.1.2023, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ilikagua Mradi wa ujenzi wa miundombinu ya Bomba la Maji la Mugango-Kiabakari- Butiama.

Gharama ya Mradi huu ni kubwa:

Tsh bilioni 70.5 kutoka Serikali ya Saudi Arabia (49.12%), BADEA (31.40%) na Serikali ya Tanzania (19.48%)

Tsh bilioni 4.775 za Serikali ya Tanzania kwa ajili kujenga miundombinu ya usambazaji wa maji kwenye Kata za Mugango na Tegeruka

Choteo la maji lilojengwa Kijijini Kwibara, Kata ya Mugango, Musoma Vijijini, lina uwezo wa kuchota LITA MILIONI 35 KWA SIKU

Kamati ya Bunge imerdhishwa na utekelezaji wa Mradi huu ambao utakamilika ifikapo tarehe 30 Juni 2023.

Matokeo ya ukaguzi wa Mradi huu yapo kwenye CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa.

Usisahau kutembelea TOVUTI ya Jimbo letu ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatatu, 16.1.2023

ZAIDI YA BILIONI 4 KUSAMBAZA MAJI KATA ZA TEGERUKA NA MUGANGO

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga ameelekeza ifikapo Februari, 2023 utekelezaji wa mradi wa kufikisha maji kwenye Kata za Mugango na Tegeruka Wilaya ya Musoma Vijijini uwe umeanza ili ifikapo Mwezi Juni, 2023 wananchi wawe wanapata maji.

Ametoa maelekezo kwa nyakati tofauti Januari 5, 2023 mbele ya Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo kwenye mikutano ya hadhara na wananchi wa Kata hizo kwa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maji Mkoani Mara ambazo ni Mamlaka ya Maji Musoma (MUWASA), Mamlaka ya Maji Mugango-Kiabakari-Butiama na RUWASA Mkoa wa Mara.

Amesema utekelezwaji wa mradi ni maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa Mugango-Kiabakari-Butiama tarehe 6 Februari, 2022.

“Mtakumbuka Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Dokta. Samia Suluhu Hassan alifika hapa na kutuwekea jiwe la msingi la mradi wenye thamani ya shilingi bilioni 70.5. Katika mradi huo palikuwa na awamu mbili za utekelezaji lakini maelekezo yake yalikuwa ni kwamba mradi uwe na awamu moja badala ya kuwa na awamu mbili,” amesema Mhandisi Sanga.

Amebainisha kuwa ziara yake wilayani humo imelenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Mugango-Kiabakari-Butiama lakini pia kutoa maelekezo mbalimbali kuhusiana na maendeleo ya mradi sambamba na kuzungumza na wananchi wa Kata za Mugango na Tegaruka ili kuwafahamisha kuhusiana na neema inayokuja ya kufikishiwa huduma ya maji.

“Nimefika hapa kuzungumza na wananchi wa vijiji vyote vya Kata za Mugango na Tegeruka kuwafahamisha kuwa Mheshimiwa Rais Dokta. Samia Suluhu Hassan ametuongezea shilingi bilioni 4.775 kwaajili ya kuhakikisha mnapata huduma ya maji kupitia mradi huu mkubwa wa Mugango-Kiabakari-Butiama,” anabainisha Mhandisi Sanga.

Mhandisi Sanga ameelekeza wataalam watakaosimamia utekelezaji wa mradi kuhakikisha ndani ya mwezi huu wa Januari, 2023 watafute wakandarasi wengine tofauti na huyo anayetekeleza mradi mkubwa ili ikifika mwezi Februari wasaini mikataba na kuanza utekelezaji lengo likiwa ni kwamba pindi mradi mkubwa unavyokamilika mwezi Juni, 2023 nao uwe umekamilika na wananchi wanapata huduma.

Amewaasa wananchi wa kata hizo kuepuka kusikiliza maneno ya mitaani yanayotolewa na wasiopenda maendeleo ya kwamba hawatopata maji. “Kumekuwa na wapotoshaji ambao wanakuelezeni kwamba mnadanganywa, niwahakikishie ndugu zangu Serikali hii ya Chama Cha Mapinduzi inayoongozwa na Mheshimiwa Dokta Samia Suluhu Hassan imejipambanua vyema katika kukabiliana na kero zinazowatatiza wananchi wake,” amebainisha Mhandisi Sanga.

Aidha, alimpongeza Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo kwa ufuatiliaji wake wa mara kwa mara wa miradi ya maji na aliwaomba radhi wananchi wa Kata hizo kwa kuchelewa kuanza utekelezaji kwakuwa walikuwa wakisubiri ujenzi wa mradi mkubwa usogee ambao ndio chanzo cha maji cha mradi husika ili yote ikamilike kwa pamoja.

“Tulichelewa kuanza utekelezaji kwakuwa utatoa maji kwenye mradi mkubwa sasa endapo tungelaza tu mabomba yangelikuwa hayana maji lakini kwa sasa ni wakati muafaka tuanze ili mradi mkubwa unapokamilika hapo Juni na hapa tunakuwa tumekamilisha,” anafafanua Mhandisi Sanga.

Akizungumzia mradi wa Mugango-Kiabakari-Butiama, Mhandisi Sanga amesema maelekezo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Meja Jenerali Suleiman Mzee alipofanya ziara kwenye mradi Desemba, 2022 ndiyo maelekezo ya Wizara ya Maji.

“Mtakumbuka hivi karibuni Mkuu wa Mkoa alitembelea hapa na alitoa maelekeozo kwa wakandarasi na wasimamizi kwamba ifikapo tarehe 30 Juni, 2023 mradi uwe umekamilika na hakuna muda wa nyongeza nasi tunaungana na maelekezo yake na tunasisitiza aliyoyaelekeza yabaki vilevile ifikapo tarehe 30 mradi uwe umekamilika,” amesisitiza Mhandisi Sanga.

Kwa upande wake Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo amesema ameshuhudia jitihada za Serikali kupitia Wizara ya Maji za kumtua mama ndoo ya maji kichwani ambapo amebainisha kuwa vijiji vingi vilivyoko pembezoni mwa Ziwa Victoria tayari vinahuduma ya maji.

Amebainisha kuwa baadhi ya Kata jimboni mwake zikiwemo Kata ya Etaro, Nyegina, Ifulifu, Nyakatende watatumia maji kutoka Musoma mjini na jukumu hilo tayari Wizara ya Maji imelitolea maelekezo kwa MUWSA ya kuhakikisha vinafikishiwa huduma.

“Ninaendelea kuwathibitishia namna ambavyo Serikali yetu ya Chama Cha Mapinduzi inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan inavyopenda jimbo la Musoma Vijijini, mwaka huu tunaouanza Serikali inazidi kuwekeza fedha nyingi ndani ya jimbo letu mbali na mradi wa mugango tumeletewa miradi mingine,” amesema Profesa Muhongo.

Amebainisha kuwa kwa Kata ya Mugango tayari kuna miradi miwili mmoja ikiwa ni huo aliyouzungumzia Mhandisi Sanga na kwamba kabla ya mradi huo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliwapatia fedha kiasi cha shilingi Milioni 600 ambazo walizigawana na Butiama na kwamba zimewezesha maeneo mengi kupata huduma ya maji maeneo ya Kaburabura, Bugoji, Kanderema, Saragana, Nyambono na Mikuyu kufikishiwa huduma ya maji.

Imetolewa na Mwandishi wa Habari
Wizara ya Maji
5.1.2023

SERIKALI YARIDHIA KUFUFUA MRADI MKUBWA WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI NDANI YA BONDE LA BUGWEMA

Timu ya Wataalamu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wakiwa ndani ya Bonde la Bugwema, Musoma Vijijini. Baadhi ya Viongozi wa Musoma Vijijini walishiriki kwenye ziara hiyo.

*Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikusudia kuanzisha kilimo kikubwa cha umwagiliaji ndani ya Bonde la Bugwema. Hii ilikuwa mwanzoni mwa miaka ya 70.

*Bonde la Bugwena ni kubwa mno. Eneo lililokusudiwa kulimwa wakati huo ilikuwa ni ndani ya hekta 10,000. Bonde lenyewe likichukuliwa kwa ujumla wake lina ukubwa wa zaidi ya hekta 20,000.

Miundombinu ya umwagiliaji ilijengwa miaka hiyo, lakini utekelezaji wake ukasimama!

Mazao makuu yanayolimwa ndani ya Bonde hilo ni mahindi, mpunga, alizeti, dengu na pamba.

*Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la kuendeleza Mradi huo wa Bugwema.

Ombi hilo lilitolewa na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo wakati Mhe Rais wetu alipotembelea Musoma Vijijini akizindua Mradi wa ujenzi wa Bomba la Maji la Mugango-Kiabakari-Butiama. Hii ilikuwa tarehe 6 Februari 2022.

Mbunge huyo alirudia kutoa ombi hilo kwenye Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika Dodoma, tarehe 7-8.12.2022

*Jana, Alhamisi, 29.12.2022, Timu ya Wataalamu kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ilitembelea Bonde la Bugwema. Timu hiyo iliongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo, Dr Raymond Mndolwa.

Viongozi kadhaa wa Musoma Vijijini waliambatana na Timu hiyo ya Wataalamu. Baadhi yao ni:

*Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo
*Mwenyekiti wa CCM wa Kata ya Bugwema, Ndugu Ezekiel MacGudo
*Diwani wa Kata ya Bugwema, Mhe Clliford Machumu
*Mtendaji wa Kata ya Bugwema, Ndugu Joseph at Phinias

Taarifa iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ni kwamba matayarisho ya utekelezaji wa Mradi wa Bugwema yanaendelea vizuri kwa ajili ya kuanza kufanya “feasibility studies and designs

Musoma Vijijini wanaendelea kutoa shukrani nyingi sana kwa Rais wetu, Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kuendeleza Mradi wa Kilimo kikubwa cha Umwagiliaji ndani ya Bonde la Bugwema.

Upatikanaji wa chakula kingi cha bei nafuu kunasaidia kushusha mfumuko wa bei kwenye soko la chakula!

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

 

MRADI WA MAJI WA CHITARE-MAKOJO UMEANZA KUKAMILIKA

RUWASA inaendelea kujenga miundombinu yenye ubora na sasa WANAKIJIJI wa CHITARE wameanza kupata maji safi na salama ya bomba.

Vijiji vya Chitare na Makojo vya Kata ya Makojo vimesubiri maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria tokea Mwaka 2013!

Mradi huu ulioanzwa kutekelezwa na Halmashauri yetu (Musoma DC) tokea Mwaka wa Fedha 2013/2014, sasa unarudiwa na unakamilishwa kwa ubora mzuri na RUWASA.

RUWASA inaendelea kujenga miundombinu yenye ubora na sasa WANAKIJIJI wa CHITARE wameanza kupata maji safi na salama ya bomba.

Kwa muda mfupi ujao Wanakijiji wa Makojo nao watapata maji ya bomba hilo.

Tumeomba bomba hilo lijengwe hadi Kijiji cha Chimati ambacho nacho kiko ndani ya Kata ya Makojo. Serikali imepokea ombi letu na kukubali kulitekeleza.

RUWASA inaendelea kufanya kazi zenye ubora mzuri ndani ya Jimbo letu.

FURAHA & SHUKRANI nyingi kutoka Kijiji cha Chitare zimeambatanishwa hapa – Sikiliza Clip/Video kutoka Chitare.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

MVUA ZA VULI – MICHE LAKI MOJA (100,000) YA MITI NA MATUNDA KUSAMBAZWA NA KUPANDWA MUSOMA VIJIJINI

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo akiwa kwenye Kitalu cha VI Agroforest kinachotayarisha miche laki moja (100,000) ya miti na matunda.

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo anaendelea kushirikiana na VI Agroforest kugawa bure miche ya miti na matunda kwa wanavijijini na taasisi mbalimbali (k.m. shule, zahanati) Jimboni mwao.

VI Agroforest inafadhiliwa na Serikali ya Sweden na inafanya kazi nzuri ya utunzaji wa mazingira ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini na kwingineko Mkoani Mara.

Miche laki moja (100,000) itakayogawiwa bure wakati wa mvua za vuli (Novemba-Disemba 2022) itakuwa ya miti ya:
*matunda
*mbao/ujenzi
*kuni
*ufugaji wa nyuki
*madawa ya asili

Matayarisho ya miche laki moja (100,000), chini ya Mtaalamu Jacob Malima, yanaendelea vizuri ndani ya Kitalu cha VI Agroforest kilichopo Mjini Musoma.

OMBI KWA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Jimbo la Musoma Vijijini linaiomba Wizara hiyo ifufue Kitalu cha Miti cha Serikali kilichopo Kijijini Suguti.

Usisahau kutembelea TOVUTI ya Jimbo letu ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumanne, 25.10.2022

VIJANA WALIOENDA KUSOMA INDIA WAMSHUKURU PROF MUHONGO

Vijana 6 waliopata ICCR scholarships za kusoma MSc in Applied Geology nchini India.

Vijana sita (6) walioombewa ICCR scholarships na Prof Sospeter Muhongo kwenda kusoma India wamemshukuru Profesa huyo kwa kuwatafutia scholarships hizo.

Wanafunzi hao sita (6) walisoma MSc Applied Geology kwenye maeneo yafuatayo:

*Coal Geology
*Metamorphic Geology
*Mineralogy
*Mineral Processing

Prof Muhongo amepawa pongezi nyingi za kusoma na kufaulu masomo yao vizuri.

Vijana hao wote sita wanafanya kazi kwenye Taasisi za Serikali yetu.

Shukrani kwa:
Prof S Muhongo
19.9.2022

HATIMAYE MUSOMA VIJIJINI WAANZA KUPATA BARABARA YA LAMI

Mradi wa ujenzi wa barabara ya lami ya Musoma-Makojo-Busekera (km 92) unaanza kuweka matumaini.

KILOMITA 5 KUKAMILIKA OKTOBA 2022

Kampuni ya Gemen Engineering inayojenga kilomita hizo tano (5) imesema itakamilisha na kukabidhi kipande hicho cha kilomita 5 ifikapo tarehe 30.10.2022. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo Injinia Andrew Nyantori.

Leo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo alikagua ujenzi wa barabara hilo ili ajiridhishe na ahadi ya Mkandarasi huyo.

UMUHIMU WA BARABARA HILI KIUCHUMI

Barabara hili ndiyo roho ya ukuaji wa uchumi wa Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21, Vijiji 68 na Vitongoji 374.

Samaki wengi na wa aina mbalimbali wanaovuliwa Ziwa Victoria wanasafirishwa kutoka Musoma Vijijini kwenda kwenye masoko mbalimbali ya ndani na ya nje ya nchi yetu kwa kutumia barabara hili.

Mazao ya chakula ambayo nayo ni ya biashara (k.m. mihogo, mahindi, viazi vitamu, mpunga, na matunda) yanasafirisha kutumia barabara hili.

Musoma Vijijini ni maarufu kwa kilimo cha pamba. Barabara hili ndilo linatumika kusafirisha pamba kutoka vijijini mwetu kwenda sokoni.

Dhahabu na madini mengine yanayochimbwa Musoma Vijijini yanasafirishwa kwa kutumia barabara hili.

UMUHIMU WA BARABARA HILI KWA HUDUMA ZA JAMII

*Hili ndilo barabara kuu na pekee linalounganisha vijiji vyote 68 vya Jimboni mwetu. Kwa hiyo, hili barabara ni muhimu sana kwa usafiri wa wananchi ndani na nje ya Jimbo letu.

*Hili ndilo barabara kuu na pekee ambalo linatumika kwa usambazaji wa vifaa vya elimu, huduma za afya, kilimo, ufugaji, maji, umeme, n.k., ndani ya Jimbo letu.

*Wagonjwa wanaohitaji matibabu kwenye hospital kubwa za Musoma, Mwanza, n.k. wanatumia barabara hili.

OMBI KWA SERIKALI

*Kasi ya ujenzi iongezeke kwa kuongezewa bajeti ya utekelezaji wa ujenzi wa barabara hili.

SHUKRANI KWA SERIKALI

Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO yenye shukrani nyingi kwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatano, 14.9.2022

WAKULIMA MASHUHURI WA ALIZETI WAJENGA KIWANDA KIDOGO CHA KUSINDIKA MBEGU ZA ALIZETI

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo akiwa ndani ya kiwanda kidogo cha kusindika mbegu za alizeti. Kiwanda hicho kitakachofunguliwa mwezi huu kinajengwa Kijijini Masinono, Kata ya Bugwema.

Ijumaa, 9.9.2022, Kikundi cha Changamkeni cha Kijijini Masinono, Kata ya Bugwema kimekamilisha malipo ya kufungiwa umeme kwenye KIWANDA chao cha ALIZETI kinachojengwa Kijijini Masinono. Mbunge wa Jimbo nae amechangia gharama za kufungiwa umeme kwenye kiwanda hicho.

UNUNUZI WA MASHINE YA KUKAMUA MBEGU ZA ALIZETI

*Mwaka 2020, Shirika la SHIMAKIUMU linalojishughulisha na Kilimo na Ufugaji ndani ya Wilaya yetu, lilipatia Kikundi cha Changamkeni mashine ya kukamua mbegu za alizeti.

*Mashine hiyo ina thamani ya Tsh Milioni 35 (Tshs 35m) na uwezo wa kukamua mbegu za alizeti kwa kiasi cha magunia 40 kwa siku.

Shukrani za dhati zinatolewa kwa SHIMAKIUMU kwa ufadhili huo utakaofaidisha Wana Kikundi cha Changamkeni, na wakulima wengine wa alizeti ndani ya Bonde la Bugwema na kwingineko Mkoani Mara.

KILIMO CHA ALIZETI MUSOMA VIJIJINI

Mbunge Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo alianza kampeni ya kushawishi uanzishwaji wa kilimo cha alizeti Jimboni mwao Mwaka 2016, na kwa misimu mitatu mfululizo (ya kilimo) aligawa bure mbegu za alizeti kiasi cha TANI 9.66. Msimu wa Mwaka 2018/2019, Wizara ya Kilimo ilichangia TANI 10.

BUGWEMA YAONGOZA KWENYE KILIMO CHA ALIZETI

Wakulima ndani ya Bonde la Bugwema ndio wanaongoza kwa kilimo cha zao la alizeti ndani ya Mkoa wa Mara.

Kikundi cha Changamkeni kinakusudia kulima Ekari 500 za alizeti ndani ya Bonde la Bugwema.

Mazao mengine yanayolimwa kwa wingi na Wakulima wa ndani ya Bonde la Bugwema ni: mahindi, mpunga, dengu na pamba.

Wakulima wa Bugwema wanasubiri kwa hamu kubwa Mradi kabambe wa umwagiliaji ndani ya Bonde la Bugwema. Mradi huo utaanza kwa ufadhili ya Serikali yetu.

 

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Ijumaa, 9.9.2022

PROF MUHONGO AMSAIDIA MAHITAJI YA SHULE KIJANA WA JIMBONI MWAKE AENDE KUANZA MASOMO YA KIDATO CHA V NYAKATO HIGH SCHOOL

Msaidizi wa Mbunge, Vaileth Peter akiwa na kijana Jastine – wametoka Benki kufanya malipo ya shule, na tayari wamemaliza kununua vifaa vya shule, vikiwemo vitabu vinavyohitajika.

Kijana Jastine Mgaya Bina wa Kijiji cha Kaburabura, Kata ya Bugoji alichelewa kuanza masomo ya Kidato cha Tano (Form V, HGL) kwa kukosa mahitaji ya shule.

Leo, kijana huyo amepata mahitaji yote ikiwemo nauli yake ya kwenda kuanza masomo yake Nyakato High School, Bukoba.

Picha iliyoambatanishwa hapa inamuonyesha Msaidizi wa Mbunge, Vaileth Peter akiwa na kijana Jastine – wametoka Benki kufanya malipo ya shule, na tayari wamemaliza kununua vifaa vya shule, vikiwemo vitabu vinavyohitajika.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatano, 31.8.2023

KAMPENI YA SENSA MUSOMA VIJIJINI – KATA YA MAKOJO WAHAIDI KUHESABIWA KWA KIWANGO CHA ASILI MIA MOJA

Hatua kubwa iliyofikiwa kwenye ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Makojo.

Kata ya Makojo ina Vijiji 3 (Chimati, Chitare na Makojo) imemhaidi Mbunge wao wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo, kwamba wamejitayarisha kuhesabiwa wote, yaani kwa kiwango cha asili mia moja (100%)

Hiyo ahadi ilitolewa siku ya Jumamosi, tarehe 13.8.2022 wakati Mbunge huyo alipokuwa ndani ya Kata hiyo akifanya kampeni ya kushawishi Wanavijiji wa Kata hiyo (na Wageni wao) washiriki kwenye SENSA ya Watu na Makazi ya tarehe 23.8.2022.

Wakati wa majadiliano ya umuhimu wa kila kaya na kila mwananchi kuhesabiwa, Mbunge huyo aliwakumbusha Wana-Kata hiyo VIPAUMBELE vya MAENDELEO ya KATA yao (k.m. Elimu, Afya, Kilimo, Uvuvi) vinavyohitaji ushiriki na uchangiaji mkubwa wa Serikali yetu.

Viongozi wa Kata hiyo waliofuata na Mbunge wa Jimbo kwenye Kampeni hii ni:
*Ndugu Peresi Mujaya
(Mtendaji Kata, WEO)
*Ndugu Lameck Mtaki
(Mtendaji wa Kijiji, VEO)
*Ndugu Daniel Magere
(M/K Serikali ya Kijiji)

Miradi mikubwa ya Kata hii iliyokwishapata au inaendelea kupewa fedha kutoka Serikalini ni ifuatayo:

Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Makojo

Kata imeishapokea Tsh Milioni 500 (Tsh 500m) kutoka Serikalini kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya.

Wanavijiji na Viongozi wao wanaishukuru sana Serikali kwa kuwapatia Mradi huu muhimu sana. Shukrani za kipekee ziende kwa Mhe Rais Samia Suluhu Hassan.

Mradi wa Maji ya Bomba ya Ziwa Victoria

Mradi huu wa thamani ya Tsh bilioni 1.072 (Tsh 1, 072m) ni wa kusambaza maji ya bomba kwenye Vijiji vya Chitare na Makojo.

Mradi ulianza kwenye Mwaka wa Fedha 2013/2014, ulisimamiwa na Halmashauri yetu na umechelewa kukamilika.

RUWASA inajitahidi kurekebisha kasoro zilizopo.

Wananchi wana imani kubwa na Serikali yetu ambayo itahakikisha Mradi huu unakamilika na maji safi na salama yanapatikana ndani ya Kata ya Makojo.

Fedha za UVIKO- 19

*Makojo Sekondari ilipewa Tsh Milioni 60 (Tsh 60m) kujenga vyumba vipya 3 vya madarasa

*Shule Shikizi Mwikoko ilipewa Tsh Milioni 60 (Tsh 60m) kujenga vyumba vipya 3 vya madarasa na Ofisi 1. Shule hii tayari ilishapewa fedha za ujenzi wa vyumba vipya 2 vya madarasa na Ofisi 1 kutoka Mradi wa Serikali wa EQUIP.

Fedha za Mfuko wa Jimbo

*Makojo Sekondari imegawiwa Mabati 158 na Saruji Mifuko 52 kutoka kwenye Fedha za Mfuko wa Jimbo zilizonunua (Mei 2022) vifaa vya ujenzi kwa Sekondari kadhaa za Jimboni mwetu.

Miradi ya TARURA ndani ya Kata ya Makojo

*TARURA imekamilisha na inaendelea kuboresha barabara za eneo hili:

*Barabara ya Makojo- Chitare – Kurugee

*Barabara ya Chitare- Mwikoko Rusoli

Barabara hizi ni muhimu sana kwa uimarikaji wa uchumi wa wavuvi na wakulima wa eneo hili.

BAADHI YA MIRADI MIPYA ILIYOPANGWA KUTEKELEZWA NDANI YA KATA YA MAKOJO

(1) Uvuvi wa Vizimba – wavuvi wako tayari kuanzisha vyama vya ushirika vya uvuvi kwa lengo la kupatiwa mikopo ya uvuvi wa vizimba

(2) Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Chimati unaendelea.

(3) Makojo High School – Wanavijiji wamemuomba Mbunge wao ashirikiane nao kwenye ujenzi wa “High school” hiyo – Mbunge amekubali ombi hilo na kikao cha mradi huo kitafanyika mwishoni mwa Septemba 2022.

UMUHIMU MKUBWA WA KUHESAMBIWA

Wanavijiji wa Kata ya Makojo wanao uelewa mkubwa wa umuhimu wa kuhesabiwa – wanakubali kwamba takwimu sahihi zinahitajika kwa mipango mizuri ya miradi yao ya maendeleo.

Kwa hiyo, Kata ya Makojo, kama zilivyo Kata nyingine 20 za Jimbo la Musoma Vijijini, WATAHESABIWA WOTE, yaani kwa asili mia moja (100%)

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumanne, 16.8.2022

KATA YA BUKUMI INAYOJENGA ZAHANATI 3 NA VYUMBA VIPYA VYA MADARASA YAPEWA SARUJI MIFUKO 200

Jumatano, 3.8.2022 Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini ametoa SARUJI MIFUKO 200 (mia mbili) kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Zahanati 3 na Vyumba vipya 2 vya Madarasa ndani ya Kata ya Bukumi.

Kata ya Bukumi yenye vijiji vinne (Buira, Bukumi, Buraga na Busekera) ina Zahanati moja tu, ambayo iko kwenye Kijiji cha Buraga, Kitongoji cha Kurugee.

Vijiji vingine vitatu vimeamua kujenga Zahanati zake na ujenzi tayari umeanza kwa kasi ya kuridhisha.

MICHANGO ya WANAVIJIJI ni:

*Nguvukazi
*Fedha taslimu, Tsh 10,000 – 15,000

DIWANI wa Kata, Mhe Munubhi Musa amechangia Tsh 100,000 (laki moja) kwa kila Zahanati. Jumla Tsh 300,000 (laki tatu).

MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo amechangia SARUJI MIFUKO 50 kwa kila Zahanati na MIFUKO mingine 50 kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba vipya 2 vya Madarasa ya S/M Busekera.

Kwa hiyo, Mbunge huyo amechanga jumla ya SARUJI MIFUKO 200 yenye thamani ya Tsh 4.5 million.

MICHANGO mingine ya Mbunge huyo kwenye Sekta ya Afya ndani ya Kata hiyo ni kama ifuatavyo:

*Gari la Wagonjwa (Ambulance) kwa Zahanati ya Kurugee, Kijijini Buraga

*Saruji Mifuko 100 (mia moja) kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Bukumi inayojengwa kwenye Kitongoji cha Kukema Burungu.

HUDUMA ZA AFYA NDANI YA JIMBO LETU:

Jimbo letu lina Kata 21 zenye jumla ya Vijiji 68. Huduma za Afya zinatolewa na:

*Hospitali ya Wilaya ambayo bado inaendelea kujengwa

*Vituo vya Afya: 3

*Zahanati za Serikali: 23
*Zahanati Binafsi: 4

UJENZI UNAOENDELEA:

*Vituo vya Afya: 3

*Zahanati za Vijiji zinazojengwa: 17

OMBI KUTOKA KATA YA BUKUMI

Wana-Kata ya Bukumi na rafiki zetu tunaombwa tujitokeze kuchangia miradi hii ya ujenzi iliyoanzishwa na inatekelezwa kwa nguvukazi na michango ya fedha taslimu kutoka wanavijiji wenyewe.

PICHA za hapa zinaonesha:

*Wasaidizi wa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini wakikabidhi SARUJI MIFUKO 200 kwa Viongozi wa Kata ya Bukumi. Hii ilitokea leo, Jumatano, 3.8.2022, Musoma Mjini.

*BOMA la Zahanati ya Busekera

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatano, 3.8.2022

SERIKALI YAENDELEA KUSHIRIKIANA NA WANAVIJIJI KWENYE UJENZI WA VITUO VIPYA VYA AFYA VYA MUSOMA VIJIJINI

Ujenzi unaoendelea wa Kituo kipya cha Afya cha Kata ya Makojo kinachojengwa Kijijini Makojo.

Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 zenye jumla ya Vijiji 68, lina Kata 3 zenye Vituo vya Afya vinavyofanya kazi. Vituo hivyo ni vya:

*Murangi
*Mugango
*Bugwema

Serikali inaendelea kutoa fedha kwenye ujenzi wa Vituo vipya vya Afya, ambavyo ni:

*Kisiwa cha Rukuba
*Makojo
*Kiriba

Kwenye ujenzi huo, Serikali ilitoa Tsh 250m kwa kila Kituo kuanza ujenzi wake.

Serikali imetoa tena Tsh 250m kuendeleza ujenzi wa Vituo hivyo vipya. Fedha hizo za awamu ya pili zitapelekwa kwenye Kata husika siku chache zijazo.

Mchango wa Tsh 500m kwa kila Kituo Kipya kinachojengwa Jimboni mwetu ni mchango mkubwa. Tunaishukuru sana Serikali yetu na kipikee kabisa tunamshukuru sana Rais wetu, Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha fedha za utekelezaji wa miradi hii na mingine zinapatakina – Ahsante sana!

Jumla ya ZAHANATI zinazotoa huduma za Afya Jimboni mwetu ni:

*22 za Serikali
*4 za Binafsi

Jumla ya ZAHANATI mpya zinazojengwa ni:

*15 zinajengwa na WANAVIJIJI na baadhi zimepokea
michango ya fedha kutoka Serikalini.

MICHANGO ya NGUVUKAZI za WANAVIJIJI inaombwa iendelee kutolewa hadi kukamilika kwa ujenzi wa VITUO VIPYA VYA AFYA na ZAHANATI zinazojengwa.

Usisahau kutembelea TOVUTI ya Jimbo letu ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumapili, 12.6.2022

AFRICA’S LOW CARBON ECONOMIES AND THEIR CONTEMPORARY ENERGY MIXES

Former USA President Barack Obama in a discussion with Prof Sospeter Muhongo on energy in Africa, when the former visited Tanzania in 2013

Low-carbon economy also generally known as “green economy” is obligatory for all countries if the objectives of the legally binding international treaty on climate change have to be soundly realised.

The treaty was adopted by 196 Parties at COP 21 in Paris, on 12 December 2015 and entered into force on 4 November 2016.

This international treaty is a global framework safeguarding humanity to avoid climate change hazards and calamities by limiting global warming to well below 2°C and preferably below 1.5°C, mimicking the pre-industrial levels (e.g. 1st Industrial Revolution took place in 1760-1840, and the 2nd one in 1870-1914).

We are today in the 4th Industrial Revolution whose foundation stone is information technology. It fuses together the artificial intelligence (AI), Internet of things (IoT), genetic engineering, 3-D printing and other new technologies.

The main greenhouse gases resulting from human activities include: (i) carbon dioxide (CO2), (ii) nitrous oxide (N2O), (iii) methane (CH₄), and (iv) industrial gases such as sulfur hexafluoride (SF6) and hydrofluorocarbons (HFCs).

CARBON DIOXIDE EMISSIONS

In 2021, global carbon dioxide emissions were projected to reach 36.4 billion metric tons (mt). This would drive the global carbon dioxide concentration to 415 ppm in 2021, compared to 277 ppm in 1750.

There is a very strong positive correlation between a country’s ECONOMIC GROWTH (& PROSPERITY) and GREENHOUSE GASES EMMISSIONS!

The 2021 GDP (nominal) projections of countries show the following:

(i) USA
*US$ trillion 22.94
*CO2 emissions – 15% of the world’s total emissions.

(ii) CHINA
*US$ trillion 16.69
*CO2 emissions – 28% of the world’s total emissions

(iii) JAPAN
*US$ trillion 5.10
*CO2 emissions – 3% of the world’s total emissions

(iv) INDIA
*US$ trillion 2.95
*CO2 emissions – 7% of the world’s total emissions

ENERGY MIX OF USA

2020 Energy consumption by source:

(1) Petroleum 35%
(2) Natural Gas 34%
(3) Renewable Energies 12%
(4) Coal 10%
(5) Nuclear 9%

Renewable Energies (12% of the total):
*Biomass 39%
*Wind 26%
*Hydro 22%
*Solar 11%
*Goethermal 2%

In 2021, USA electricity energy consumption per person per year (per capita) was averaged at 4,437 kWh (kilowatthours)

ENERGY MIX OF CHINA

2019 consumption of energy by source in China was as follows:

(1) Coal 62.2%
(2) Hydro (conventional) 17.3%
(3) Hydro(pumped storage) 0.4%
(4) Wind 5.5%
(5) Nuclear 4.8
(6) Natural Gas 3.2%
(7) Solar 3.1%
(8) Other thermal 2%
(9) Biomass 1.5%

Renewable Energies in China:

In 2020, China added –
*48,000 MW of solar power
*71,000 MW of wind power
*13,000 MW of hydropower

These additions bring about TOTAL INSTALLED RENEWABLE ENERGIES CAPACITY in China to more than 900,000 MW (900 GW).

Out of the 900 GW, solar power accounts for 252 GW while wind power accounts for 281 GW, which was generated by more than 135,000 turbines.

In 2021, CHINA electricity energy consumption per person per year (per capita) was averaged at 3,944 kWh (kilowatthours)

ENERGY CONSUMPTION vs ECONOMIC GROWTH & PROSPERITY

African countries have to LEARN from the TWO LARGEST ECONOMIES of world and adjust their contemporary ENERGY MIXES accordingly

The main economic object is for the Africa’s population to have access to reliable, peridictable and affordable electricity within the realm of the 2015 Paris/UNFCCC Accord (COP 21).

Considing the untapped enormous energy resources of the African continent, a typical ENERGY MIX of an African country would look like this – electricity being generated from:

(A) PRIMARY SOURCES:
1. Natural Gas
2. Coal
3. Hydro

(B) RENEWABLES
1. Solar
2. Wind
3. Tides & Waves
4. Geothermal
5. Biomass
6. Biogas
7. Compressed Natural Gas (CNG)
8. Nuclear
9. Hydrogen
10. Radiant

*Electricity demand in Africa today is 700 terawatt-hours (TWh), with the North African economies and South Africa accounting for over 70% of the total.

*In 2020, STATISTA reported that 9% of all energy generated in Africa came from renewable sources, and that North Africa is the current leader on the continent in terms of renewable energy capacity.

*IRENA (the International Renewable Energy Agency) argue that if the 2015 Paris/UNFCCC Climate Accord has to be globally realized (the 1.5°C limit scenario), then the following has to be done:

(i) Installed Renewable Energies capacity would need to increase to 10,770,000 MW (10,770 GW) by 2030, and 27,800,000 MW (27,800 GW) by 2050

(ii) Solar PV will need to be scaled up to 5,200,000 MW (5,200 GW) by 2030

ENERGY MARSHALL PLAN FOR AFRICA

Since negative consequences of climate change do not respect political and territorial borders, and moreover Africa possesses some of the major carbon sinks, INTERNATIONAL FUNDING for her 54 countries’ contemporary energy mixes is unavoidable.

THE GREEN CLIMATE FUND

*As of 31 July 2020, the Green Climate Fund has raised only US$ 10.3 billion equivalent in pledges from 49 countries/regions/cities. This is a dismal amount for this global climate initiative!

It was established in May 2008 to facilitate greater investments in developing member countries (DMCs) for their prospective “low-carbon and green economies.”

*IRENA estimates that from, now till 2030, Africa requires an annual investment of US$ 70 billion in renewable energy projects for clean energy transformation to take place.

Some energy experts argue that the Power Africa Project of President Obama a five-year Africa-America initiative which was launched by President Barack Obama in Tanzania in July 2013, may be re-introduced with the financial support, in terms of energy grants, from the Green Climate Fund.

The initiative aimed at supporting economic growth and development by increasing access to reliable, affordable, and sustainable energy, especially, electricity, in Africa.

The picture attached herewith shows HE President Barack Obama in deep discussion (on energy in Africa) with Prof Sospeter Muhongo. This was taken in 2013 in Dar es Salaam.

Contribution by:
Sospeter Muhongo
*Chartered Geologist (CGeol)
*European Geologist (EurGeol)

*Honorary Fellow of the Geological Society of London (est. 1807)

*Honorary Fellow of the Geological Society of America (est.1888)

*Honorary Reserach Fellow of the Chinese Academy of Geological Sciences (est. 1956)

Date:
Saturday, 4.6.2022

KAMPENI KABAMBE YA UPANDAJI MICHE YA MITI NA MATUNDA WAANZA MUSOMA VIJIJINI

Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo akigawa MICHE 10,000 kwa Wanafunzi na Wanavijiji wa Jimboni mwetu.

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo ANASHIRIKIANA na VI Agroforestry Project ya AIC (African Inland Church) kupanda miche ya MITI na MATUNDA vijijini mwetu, zikiwemo shule zetu zote na Madhehebu ya Dini zote. Wakulima binafsi nao wanapewa miche ya miti na matunda.

Miche ya miti na matunda inatolewa bure na iwapo inapaswa kununuliwa (k.m. miche ya mivule), Mbunge huyo anainunua na kuigawa bure.

Jana, Jumatano, 18.5.2022, Mbunge huyo aliambatana na Mtaalamu wa Misitu, Ndugu Jacob Malima wa VI Agroforestry Project KUGAWA MICHE 10,000 (miche elfu kumi) kwenye vijiji vya kando kando mwa Ziwa Victoria (Vijiji vya Kurwaki, Kiriba, Bwai Kumsoma), kikiwepo Kisiwa cha Rukuba (miche 4,500)

MVUA ZA VULI ZA MWEZO OKTOBA

Mipango inawekwa na DC (Dr Haule) na DED (Ndugu Palela) wetu kwenye UPANDAJI mkubwa wa MITI na MATUNDA ndani ya vijiji vyetu 68 ikiwemo Milima yetu (k.m. Nyaberango na Mtiro) ambayo kwa sasa ni vipara vitupu.

Malengo yetu ni kupanda MICHE 100,000 (miche laki moja) wakati wa mvua za vuli za Oktoba 2022.

Usisahau kutembelea TOVUTI ya Jimbo letu ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Alhamisi, 19.5.2022

TAIFA LINAHITAJI WANASAYANSI WENGI NA MAHIRI – MUSOMA VIJIJINI KUANZA KUWA NA HIGH SCHOOLS ZA SAYANSI

Musoma Vijijini

Tumepanga tuwe na High Schools angalau 5 za masomo ya sayansi ifikapo 2025.

Jimbo la Musoma Vijijini linayo HIGH SCHOOL moja tu, nayo ni ya masomo ya ARTS (HKL, HGK na HGL). Hii ni Kasoma High School iliyoanza Mwaka 2014, na ni sehemu ya Sekondari ya Kasoma iliyofunguliwa Mwaka 1995.

Jimbo letu lina jumla ya:

*Sekondari 22 za Kata/Serikali
*Sekondari 2 za Binafsi (Madhehebu: Sabato & Katoliki)

Wananchi ndani ya Kata 21 za Jimbo letu wamepanga na wengine wameanza ujenzi wa Sekondari Mpya 10 – moja (Ifulifu Sekondari) ikiwa imepokea kutoka Serikalini Tsh MILIONI 470 za ujenzi wa Sekondari ya Kata hiyo itakayofunguliwa Juni 2022.

UJENZI NA UBORESHAJI WA MAABARA

WANAVIJIJI, kwa kushirikiana na SERIKALI yetu, wameamua kujenga na kuboresha MAABARA zote za Sekondari zetu. MAABARA hizo ni za masomo ya Fizikia, Kemia na Baiolojia.

Mbali ya kuboresha uelewa na ufundishaji wa masomo hayo kwa WANAFUNZI wa KIDATO cha I hadi IV, lengo jingine ni kuanzisha HIGH SCHOOLS za MASOMO ya SAYANSI (k.m., PCM & PCB) Jimboni mwetu.

Tumepanga tuwe na High Schools angalau 5 za masomo ya sayansi ifikapo 2025.

WANAVIJIJi wa Kata ya Kiriba yenye Vijiji 3 wameamua kujenga MIUNDOMBINU ya HIGH SCHOOL ya masomo ya SAYANSI – tafadhali wasikilize kwenye CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa.

SHUKRANI zinatolewa kwa:
*Serikali yetu chini ya uongozi wa Rais wetu, Mhe Samia Suluhu Hassan
*Benki za NBC, NMB, CRDB na TPB
*Baadhi ya Wazaliwa wa Kata ya Kiriba

Usisahau kutembelea TOVUTI ya Jimbo letu:
www.musomavijijini.or.tz

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatano, 20.4.2022

FEDHA ZA TOZO KISIWANI RUKUBA

                      Msingi wa Wodi ya Mama & Mtoto (Fedha za Tozo)

WAKAZI na VIONGOZI wa Kisiwa cha Rukuba, Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kuishukuru SERIKALI na RAIS wetu, Mhe SAMIA SULUHU HASSAN kwa kuwapatia SHILINGI MILIONI 250 za ujenzi wa KITUO cha AFYA cha Kisiwani humo.

FEDHA hizi ni za TOZO ya miamala ys simu.

MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo anafuatilia kwa karibu sana ujenzi unaoendelea Kisiwani humo na kwingineko Jimboni, na hadi kufikia leo (Jumamosi, 5.3.2022) maendeleo ya ujenzi Kisiwani Rukuba ni kama ifuatavyo:

*MAABARA – Msingi wa Jengo lake umekamilishwa leo. Picha 2 zimambatanishwa hapa.

*WODI YA MAMA & MTOTO – Msingi wa Jengo unajengwa na utakamilishwa wiki ijayo. Picha 1 imeambatanishwa hapa.

JENGO LILOJENGWA KWA NGUVU ZA WANARUKUBA & MBUNGE WA JIMBO

Hapo awali, Wakazi wa Kisiwani Rukuba (WanaRukuba) walianza ujenzi wa MIUNDOMBINU mipya ya kuboresha na kupanua Huduma za Afya zitolewazo na Zahanati ya Kisiwa hicho.

JENGO lilofikishwa kwenye renta litakamilishwa na matumizi yake yataelekezwa na Wataalamu wa Afya – Picha imeambatanishwa hapa.

               Boma linalojengwa kwa nguvu za WanaRukuba na Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo

PICHA hapa chini inaonesha Jengo la Zahanati ya Kisiwa cha Rukuba (bati za rangi za bluu na kijani) – hii Zahanati inapanuliwa iwe Kituo cha Afya cha Kisiwa cha Rukuba.

                                         Jengo la Zahanati ya Kisiwa cha Rukuba

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

BARABARA ZINAZOJENGWA NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

A – FEDHA ZA BAJETI YA MAENDELEO (ROAD FUND DEVELOPMENT BUDGET) 2021/2022

(1) Mkirira – Kwangwa Hospital (Gharama: Tsh Milioni 350). Limekamilika kwa 90%

(2) Bukima-Bulinga- Bwasi (Gharama: Tsh Milioni 300). Ujenzi umekamilika

B – FEDHA ZA JIMBO
Masinono – Kinyang’erere (Gharama: Tsh Milioni 500). Likiwemo Daraja la Jitirola na mengine mawili. Hatua za kumpata Mkandarasi zinakamilishwa

C – FEDHA ZA TOZO
(Jumla: Tsh bilioni 2)
Barabara zinazojengwa na utekelezaji umeanza:

(1) Mmahare-Etaro-Nyasaungu
(2) Mugango-Bwai Kwitururu- Kwikuba
(3) Bwai Kwitururu- Bwai Kumsoma
(4) Maneke-Mayani- Kyawazaru
(5) Nyaminya-Kataryo- Kyawazaru
(6) Rwanga-Seka-Mikuyu
(7) Saragana- Nyambono- Chumwi
(8) Kaburabura-Masinono-Bugwema
(9) Bukima-Bulinga- Bwasi
(10) Busekera-Burungu
(11) Chitare-Kurugee-Buraga (Kivukoni)
(12) Kome – Buira
(13) Kigera Etuma-Ekungu
(14) Nyakatende-Kamguruk- Kigera Etuma
(15) Mkirira-Nyegina-Esira
(16) Kurukerege-Nyegina

TAARIFA kutoka:
*Ofisi ya TARURA (W)
*Ofisi ya Mbunge

MRADI WA MAJI WA Tsh BILIONI 70.5 – UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI

Mhe RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, MHE SAMIA SULUHU HASSAN aliweka JIWE la MSINGI kwenye Mradi wa ujenzi wa BOMBA la MAJI la Mugango-Kiabakari-Butiama utakaogarimu Tsh BILIONI 70.5 – haya ni MAJI ya kutoka Ziwa Victoria

Jumapili, tarehe 6.2.2022, Mhe RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, MHE SAMIA SULUHU HASSAN aliweka JIWE la MSINGI kwenye Mradi wa ujenzi wa BOMBA la MAJI la Mugango-Kiabakari-Butiama utakaogarimu Tsh BILIONI 70.5 – haya ni MAJI ya kutoka Ziwa Victoria.

TUKIO hilo lilifanyika ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini, Kijijini KWIBARA, MUGANGO

VIKUNDI vya KWAYA na NGOMA za ASILI vya Jimboni mwetu vilitoa burudani wakati wa sherehe hizo muhimu sana zikizofanyika Jimboni mwetu.

VIDEO zilizowekwa hapa zimerekodi kwa kifupi sehemu ya burudani ya siku hiyo ya tarehe 6.2.2022. Tafadhali sikiliza na angalia baadhi ya NGOMA za ASILI za Jimbo la Musoma Vijijini.

UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM – UTAMADUNI & MICHEZO

*Kila mwaka, siku ya sherehe za NANENANE, Jimbo letu linafanya MASHINDANO ya Kwaya, Ngoma za Asili na Mitumbwi (kupiga makasia).

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
10.2.2022

KITUO CHA AFYA MAKOJO – WANAVIJIJI WAAMUA KUONGEZA KASI YA UJENZI*

maboma ya OPD na MAABARA ya KITUO cha AFYA cha Kata ya Makojo kinachojengwa Kijijini Makojo.

Kwa Mwaka huu wa Fedha, 2021/2022, Jimbo la Musoma Vijijini linajenga VITUO 2 vya AFYA:
*Makojo: chanzo cha fedha – RUZUKU ya Serikali
*Rukuba (Kisiwa): chanzo cha fedha – TOZO
*VITUO vilivyokwishajengwa na vinavyotoa HUDUMA za AFYA ni:*
*Murangi
*Mugango
*Bugwema
*KITUO KIPYA CHA AFYA CHA MAKOJO*
Kata ya MAKOJO yenye Vijiji 3 (Chimati, Chitare na Makojo) IMEAMUA kuongeza KASI ya ujenzi wa Kituo cha Afya ili kukikamilisha haraka iwezekanavyo.
Kata hii imepewa SHILINGI MILIONI 250 (Tsh 250m) kwa ajili ya ujenzi wa KITUO cha AFYA cha Kata yao. Fedha hizi ni RUZUKA ya SERIKALI yetu.
WANAVIJIJI wanachangia NGUVUKAZI zao kwa kuchimba misingi ya majengo, kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji ya ujenzi.
WANANCHI na VIONGOZI wa Kata ya Makojo wanatoa shukrani nyingi sana kwa SERIKALI yetu inayoongozwa kwa umahiri mkubwa na RAIS wetu, Mhe SAMIA SULUHU HASSAN.
VIONGOZI wa Vitongoji wanahamasisha ushiriki wa Vitongoji vyao kwenye utekelezaji wa Mradi huu.
DIWANI wa Viti Maalum, Mhe Tabu Maregesi Machumu anasimamia ujenzi huu kwa ufanisi na mafanikio makubwa – tunampongeza sana!
MABOMA 2 tayari yanakaribia kuezekwa:
*OPD
*MAABARA
Ujenzi wa miundombinu mingine ya Kituo hiki, k.m. WODI ya Mama & Mtoto, unaendelea kwa kasi na ari mpya.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
10 Feb 2022

KISIWA CHA RUKUBA KUSHIRIKI SHEREHE ZA CCM

WAKAZI wa KISIWA cha RUKUBA wakishiriki katika kusomba SARUJI iliyonunuliwa Musoma Mjini na kusafirishwa hadi Kisiwani humo.

Kesho, tarehe 5.2.2022 BOTI KUBWA 2 za kuchukua ABIRIA 80 zitaondoka Kisiwani Rukuba saa 10 alfajiri kuleta WAWAKILISHI wao kwenye sherehe za CCM zitakazofanyika Musoma Mjini.

Kisiwa cha Rukuba ni moja ya vijiji 3 vya Kata ya Etaro ya Jimbo la Musoma Vijijini.

WAKAZI wa Kisiwa cha Rukuba wanaendelea kutoa SHUKRANI nyingi sana kwa RAIS wao, Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia SHILINGI MILIONI 250 kujenga Kituo cha Afya kisiwani humo.

UJENZI umeanza na WAKAZI wa Kisiwani humo wamechangia ifuatavyo:

(i) NGUVUKAZI:
*wanasomba mawe, kokoto na maji ya ujenzi. Vilevile, wanachimba misingi ya majengo yote.

(ii) SERIKALI YA KIJIJI/KISIWA
*Imetumia mapato yake kununua vifaa vya kutumiwa kwenye ujenzi – pump 2 za kuvutia maji kutoka Ziwani na mipira yake, mapipa ya kutunzia maji ya ujenzi.

FEDHA za UVIKO/IMF:
Fedha ziko kwenye Akaunti ya Zahanati yao na tayari zimeanza kutumika kununua:

*Saruji Mifuko 599
*Nondo 210
*Mbao 32 za 1×8
20 za 2×2
*Dawa ya kuua mchwa

TAARIFA hiyo hapo juu imetolewa na Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji/Kisiwa, Ndugu Japhari Ibrahim Kabasa

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
4.2.2022

KATA ISIYOKUWA NA SEKONDARI YAKE YAPOKEA SHILINGI 470 MILIONI KWA AJILI WA UJENZI WA SEKONDARI YA KATA HIYO

Kikao cha Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, na VIONGOZI wa ujenzi wa Ifulifu Sekondari ya Kata ya Ifulifu. Kikao kilifanyika Kijijini Kabegi, ktk eneo la ujenzi wa Sekondari ya Kata.

Kata ya IFULIFU ya Jimbo la Musoma Vijijini ndiyo KATA PEKEE isiyokuwa na Sekondari yake.
Wanafunzi wa Sekondari wa Kata hii wanasoma Sekondari za Kata jirani za Nyakatende na Mugango.
Kata hii ina VIJIJI 3 vya Kabegi, Kiemba na Nyasaungu.
Kijiji cha Nyasaungu kiko mbali na vijiji vingine na wakazi wake wengi ni wafugaji. Taarifa za ujenzi wa Sekondari ya Kijiji hiki cha Wafugaji ilitolewa jana, Ijumaa, 22.1.2022
*UJENZI WA IFULIFU SEKONDARI*
*Vijiji vya Kabegi na Kiemba vilianza ujenzi wa Sekondari yao JUNI 2017
*MICHANGO ya ujenzi wa Sekondari hii inatolewa na:
(i) Wanavijiji – fedha taslimu na nguvukazi
(ii) Mbunge wa Jimbo – fedha zake binafsi
*MAJENGO yaliyokamilishwa kwa nguvu za WANAVIJIJI na MBUNGE wao:
(i) Vyumba viwili vya Madarasa
(ii) Msingi wa Jengo la Utawala umekamilika
(iii) Matofali 1,200 yametengenezwa
*FEDHA ZA UVIKO- 19/IMF ZIMEPOKELEWA*
Kata ya IFULIFU inayojenga Sekondari yake ya Kata tokea JUNI 2017, imepokea kwa shukrani nyingi mno SHILINGI MILIONI 470 kutoka Serikali Kuu.
*Wanavijiji na Viongozi wa Kata ya Ifulifu wanatoa shukrani nyingi sana kwa Mhe Rais wao, Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kuimbuka Kata yao ambayo haina Sekondari yake, na ujenzi waliouanza unasuasua kwa ukosefu wa fedha. Fedha zimepatikana – KAZI IENDELEE!
Juzi, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, alienda Kijijini Kabegi kufuatilia ujenzi wa Ifulifu Sekondari na kujadili na Viongozi wa Kata hiyo kuhusu matumizi bora ya TSH MILIONI 470 walizozipokea kwa ajili ya ujenzi wa Sekondari ya Kata yao.
*USHAURI ULITOLEWA NA MBUNGE WA JIMBO*
*Vijiji 2 vya Kabegi na Kiemba vifanye VIKAO vya WANAVIJIJI kuwaeleza juu ya malengo ya fedha hizo (Tsh 470m) walizozipokea Katani
*Matumizi ya fedha hizo yawekwe wazi sana kwa wanavijiji
*Wanavijiji waendelee kuchangia nguvukazi ili miundombinu muhimu ya elimu ipatikane kutokana na fedha hizo.
*Ujenzi uende kwa kasi kubwa na kwa ubora unaokubalika
*Ifulifu Sekondari ifunguliwe Julai 2022., na Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza na kutoka Vijiji vya Kabegi na Kiemba waendelee na masomo yao kwenye Sekondari yao ya Kata.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

JAMII YA WAFUGAJI YAENDELEA KUJENGA SEKONDARI YAKE KIJIJINI MWAO

ziara ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, kijijini Nyasaungu, Kata ya Ifulifu. Mbunge wa Jimbo na Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi, Ndugu Joseph Chome (mwenye T-shirt ya rangi ya njano) wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa Sekondari ya Kijiji cha Nyasaungu.

 

Kijiji cha NYASAUNGU ni kimoja kati ya VIJIJI 3 vya Kata ya IFULIFU iliyo ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini. Ni hii Kata pekee isiyokuwa na Sekondari yake ndani ya Jimbo letu!
JIOGRAPHIA ya Kata hii imewalazimu WANAVIJIJI wa VIJIJI hivi vitatu kujenga SEKONDARI 2 kwa wakati mmoja.
Kijiji cha WAFUGAJI cha NYASAUNGU kimezunguka na MITO na kiko mbali (kati ya kilomita 10 na 15) kutoka vijiji vingine viwili (Kabegi na Kiemba).
N.B. Juzi, Ndugu Chacha alimueleza Mbunge wa Jimbo kwamba amelazimika kumpeleka mwanae akasome Sekondari ya Musoma Mjini baada ya mwanae kushindwa kwenda shuleni kwa siku 3 za mvua zilizonyeesha Kijijini mwao. Njia  hazipitiki!
Kwa hiyo SEKONDARI 2 zinajengwa kwa mpangilio ufuatao:
*Nyasaungu Sekondari:
Inajengwa na Wanakijiji wa Nyasaungu (WAFUGAJI)
*Ifulifu Sekondari:
Inajengwa na Wanavijiji wa Kabegi na Kiemba. Taarifa zaidi za ujenzi wa Sekondari hii utatolewa baadae.
*UJENZI WA NYASAUNGU SEKONDARI*
Juzi, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo alitembelea Kijiji cha Nyasaungu kufuatilia ujenzi wa Sekondari ya Kijiji hicho ulioanza AGOSTI 2019.
Taarifa za ujenzi wa Sekondari hii ya WAFUGAJI wa Kijiji cha Nyasaungu imetolewa mara kadhaa.
WACHANGIAJI WA UJENZI WAKE ni:
*Wanakijiji wenyewe kwa vigezo vya wingi wa MIFUGO yao. Kwa mfano wenye ng’ombe zaidi ya 100 wanachangia Tsh LAKI 2 (200,000).
*Wanakijiji wanachangia NGUVUKAZI
*Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo – fedha zake binafsi
*Mfuko wa Jimbo la Musoma Vijijini – fedha za Serikali.
Halmashauri yetu inaombwa nayo ianze kuchangia ujenzi huu.
MINDOMBINU ILOYOKAMILISHWA:
*Vyumba 3 vya Madarasa
*Choo chenye matundu sita (6)
*Jengo la Utawala: msingi umekamilishwa.
MALENGO MAPYA YA NYASAUNGU SEKONDARI
*Wanakijiji wa Nyasaungu na Mbunge wao wamejiwekea MALENGO MAPYA ambayo ni:
*Jengo la Utawala likamilishwe kabla ya tarehe 30 Machi 2022
*Serikali iombwe kufungua Nyasaungu Sekondari JULAI 2022 iwapo miundombinu ya awali itakuwa imekamilika.
*SERIKALI ikisaidie Kijiji cha WAFUGAJI cha Nyasaungu kama ambavyo inasaidia JAMII ya WAFUGAJI sehemu nyingine za nchi yetu. Mbunge ameishawasilisha ombi hili kwa wahusika TAMISEMI.
TUCHANGIE UJENZI WA NYASAUNGU SEKONDARI – Karibuni sana!
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
22.1.2022

PROF MUHONGO ATEMBELEA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA

ugeni wa Prof Sospeter Muhongo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, kwenye Tegeruka Sekondari ya Kata ya Tegeruka.

 
 Jumatano, 19.1.2022 Prof Sospeter Muhongo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini alitembelea TEGERUKA SEKONDARI akifuatilia:
 
*Wanafunzi waliokwisha fika shuleni hapo kuanza Masomo ya Kidato cha kwanza (2022)
 
Wanafunzi 54 kati ya 184 tayari wameanza masomo ya Kidato cha Kwanza. Leo ni siku ya tatu toka shule ifunguliwe. Prof Muhongo amepiga PICHA na Wanafunzi hao wa Kidato cha Kwanza – baadhi ya Wazazi na Walimu wako kwenye picha hiyo (kiambatanisho)
 
*Ujenzi wa Miundombinu kwenye Sekondari hiyo:
 
(i) Tegeruka Sekondari ilikuwa ya kwanza, ndani ya Jimbo letu, kukamilisha ujenzi wa VYUMBA VIPYA 3 vya MADARASA kwa kutumia fedha za UVIKO 19/IMF zilizopatikana kwa juhudi za Mhe Rais Samia Sukuhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. SHUKRANI NYINGI SANA kwa Mhe Rais wetu.
 
(ii) Sekondari haina MAABARA na MAKTABA. Mbunge wa Jimbo amekubali kutoa MICHANGO kwa kushirikiana na WANAVIJIJI wa KATA ya TEGERUKA kuanza mara moja ujenzi wa MAABARA 3 za masomo ya SAYANSI (Physics, Chemistry & Biology).
 
TEGERUKA SEKONDARI inahudumia VIJIJI 3, Kataryo, Mayani na Tegeruka. Ina jumla ya WANAFUNZI 509 na WALIMU 12, wakiwemo 5 wa Masomo ya Sayansi.
 
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
19.1.2022

FEDHA ZA UVIKO 19 (IMF): KISIWA CHA RUKUBA CHAKUBALI KUCHANGIA NGUVUKAZI KWENYE UJENZI WA KITUO CHAO CHA AFYA

WAKAZI wa KISIWA cha RUKUBA wakisomba MCHANGA kwa ajili ya ujenzi wa MIUNDOMBINU ya KITUO chao cha AFYA.

KISIWA cha RUKUBA kimepokea SHILINGI MILIONI 250 kwa ajili ya ujenzi wa KITUO cha AFYA Kisiwani humo.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji/Kisiwa hicho, Ndugu Japhari Ibrahim Kibasa, kwa niaba ya WANA-RUKUBA, anatoa SHUKRANI nyingi sana kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan kwa KUKIKUMBUKA KISIWA CHAO ambacho sasa kitakuwa na HUDUMA nzuri za Afya.
“Safari za MITUMBWI za mchana na usiku za kupeleka wagonjwa mahututi na wajawazito Musoma Mjini, sasa hazitakuwepo tena, ” amesema Kiongozi huyo.
Kisiwa cha Rukuba ni moja kati ya Vijiji 68 vya Jimbo la Musoma Vijijini. Kisiwa hiki kiko Kata ya Etaro.
Leo, Ijumaa, tarehe 7.1.2022, WAKAZI wa Kisiwani humo wameanza kusomba mchanga wa ujenzi wa:
*Jengo la Maabara
*Wodi ya Mama&Mtoto
*Kichomea Taka (incinerator)
KISIWA cha RUKUBA kinang’ara sana kimaendeleo. Ndani ya MIAKA 6, Kisiwa cha Rukuba kimekamilisha yafuatayo:
(1) SHULE YA MSINGI:
*Vyumba vya Madarasa vipo vya kutosha na ziada ya chumba kimoja
(2) MAKTABA YA SHULE YA MSINGI:
*Wakazi wa Kisiwani humo walishirikiana na Mbunge wao Prof Sospeter Muhongo kujenga MAKTABA na kuweka VITABU vya kutosha.
(3) NYUMBA ZA WALIMU:
*Mdau wa Maendeleo Kisiwani humo alishirikiana na Wakazi wa Kisiwa hicho kujenga nyumba za Walimu. Kila Mwalimu amepewa nyumba ya shule, na ipo moja ya ziada.
(4) UMEMEJUA (solar):
*Mradi umeanza kutekelezwa wa utumiaji wa “solar”. Zahanati inatumia “solar”
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

MAKTABA NA MAABARA ZAENDELEA KUJENGWA

MAKTABA ya Shule ya Msingi Karubugu, Kijijini Kurwaki IMEKAMILIKA

MAKTABA ya Shule ya Msingi Karubugu, Kijijini Kurwaki IMEKAMILIKA
MICHANGO YA UJENZI WA MAKTABA HIYO
*Wanakijiji wamechangia nguvukazi na fedha taslimu. Daftari linaloonyesha MICHANGO iliyotolewa liko kwenye Serikali ya Kijiji cha Kurwaki.
*WANAFUNZI na WAKAZI wengine wa Vijiji vya Kurwaki na Kiriba, na Viongozi wa Kata zao WANAISHUKURU sana PCI TANZANIA na MBUNGE wao wa Jimbo Prof Muhongo kwa KUTOA MICHANGO MIKUBWA kukamilisha UJENZI wa MAKTABA ya Shule yao ya Msingi.
Wanafunzi wa S/M Karubugu wanatoka Vijiji vya Kurwaki (Kata ya Mugango) na Kiriba (Kata ya Kiriba)
VITABU vya MAKTABA hiyo vimetolewa na PCI TANZANIA na MBUNGE wao Prof Sospeter Muhongo.
Mbunge huyo ataongenezea VITABU kwenye Maktaba hiyo.
MATUMIZI ya MAKTABA ILIYOJENGWA & KUKAMILIKA
*Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari wanakaribishwa
*Walimu wa shule za Msingi na Sekondari wanakaribishwa.
*Wakazi wa Vijiji na Kata za jirani wanakaribishwa.
UJENZI WA MAKTABA NA MAABARA ZA SAYANSI KWENYE SHULE ZA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI UNAENDELEA.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

MAJI YA ZIWA VICTORIA: VIJIJI VINGINE VITATU VYAPATA MAJI YA BOMBA

Vijiji vya Bukumi, Buraga na Busekera vimeanza kutumia Maji SAFI & SALAMA

MWAKA MPYA na CHANZO KIPYA CHA MAJI – Vijiji vya Bukumi, Buraga na Busekera vimeanza kutumia Maji SAFI & SALAMA baada ya Mradi wao wa Maji kukamilika.
RUWASA inaendelea kutekeleza kwa mafanikio makubwa MIRADI ya USAMBAZAJI MAJI vijijini mwetu.
WASIKILIZE (“CLIP” hapa) WANAVIJIJI na VIONGOZI wao wakitoa SHUKRANI zao za dhati kwa SERIKALI yao.
MAJI NI UHAI
MAJI NI UCHUMI
MAJI NI MAENDELEO
Taarifa kutoka:
*Ofisi ya RUWASA
Musoma DC
*Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
1.1.2022

RUWASA YAENDELEA KUSIFIWA MUSOMA VIJIJINI

Wanavijiji wa KASTAMU, BUANGA na BUTATA sasa wanaouhakika wa kupata MAJI SAFI na SALAMA majumbani mwao

Maji safi na salama ya BOMBA kutoka Ziwa Victoria yaanza kutumika ndani ya VIJIJI 3 vya KASTAMU, BUANGA na BUTATA
ANGALIA FURAHA za Wanavijiji ambao sasa wanaouhakika wa kupata MAJI SAFI & SALAMA majumbani mwao.
SHUKRANI nyingi sana zimetolewa. sikiliza “CLIP” iliyoambatanishwa hapa.
Taarifa kutoka:
*Ofisi ya RUWASA
Musoma DC
*Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
27.12.2021

KIJIJI CHA PEMBEZONI CHA WAFUGAJI CHA NYASAUNGU KIMEAMUA KUJENGA SEKONDARI YAKE

Wana-Nyasaungu wanapenda WATOTO wao 70 wa Kidato cha kwanza (2022) waanze masomo kwenye Sekondari yao waliyoanza kuijenga tokea Juni 2019.

Kijiji cha NYASAUNGU ni moja ya Vijiji 3 (Kabega, Kiemba & Nyasaungu) vya Kata ya IFULIFU. Hii ndiyo Kata pekee ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini ambayo haina Sekondari yake – ujenzi wa Sekondari 2 ulishaanza vijijini Kabegi (Ifulifu Sekondari) na Nyasaungu (Nyasaungu Sekondari)
Kijiji cha Nyasaungu kiko pembezoni na umbali kutoka vijiji vingine viwili vya Kata hiyo haupunguwi kilomita 10.  Wakazi wake wengi ni WAFUGAJI.
WANAFUNZI wa Sekondari wa kutoka Kijiji hiki wanaenda kusoma Sekondari za Kata za jirani ambazo ni Mugango na Nyakatende.
UMBALI wa kwenda na kurudi kwenye Sekondari hizo za Kata jirani ni takribani KILOMITA 20.
SERIKALI imetoa Tsh Milioni 470 kujenga Sekondari ya Kata ya IFULIFU ambayo itajengwa kwenye Kijiji cha KABEGI  ambacho kiko takribani KILOMITA 10 kutoka Kijijini NYASAUNGU.
Kwa hiyo, Kijiji cha NYASAUNGU kinaendelea na ujenzi wa Sekondari yake ili kutatua TATIZO la UMBALI (na madhara yake) linalowakabili watoto wao.
UJENZI wa Sekondari ya Kijiji hicho ulianza JUNI 2019 na MICHANGO ya UJENZI inatoka kwa:
*Wanakijiji:
Wanachangia nguvukazi na fedha taslimu (Tsh Milioni 19.7) kwa kuuza mifugo yao. Wasikilize kwenye CLIP iliyowekwa hapa.
*Mbunge wa Jimbo:
ameishachangia Mabati 108, Saruji Mifuko 30 na Nondo 20
*Mfuko wa Jimbo:
umeishachangia Mabati 54 na Saruji Mifuko 80
OMBI KUTOKA KIJIJI CHA NYASAUNGU
*Wana-Nyasaungu wanapenda WATOTO wao 70 wa Kidato cha kwanza (2022) waanze masomo kwenye Sekondari yao waliyoanza kuijenga tokea Juni 2019.
NB: Kijiji cha Nyasaungu –  kimesimamisha ujenzi wa Zahanati ya Kijiji chao ili wakamilishe ujenzi wa Sekondari hiyo.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI LAANZA UJENZI WA “HIGH SCHOOLS” ZA MASOMO YA SAYANSI

Maabara za Kiriba Sekondari

ELIMU: Jimbo la Musoma Vijijini (Kata 22 zenye Vijiji 68) lina idadi ifuatayo:
*Shule za Msingi za Serikali 111.
*Shule za Msingi za Binafsi 3
*Shule za Msingi mpya zinazojengwa (Shule Shikizi) 13
*Sekondari za Kata 22
*Sekondari za Binafsi  2
*Sekondari mpya zinazojengwa au zilizopangwa kujengwa 10
*High School 1 (iko Kasoma Sekondari) ya masomo ya “arts”
MAABARA ZINAJENGWA KWENYE SEKONDARI ZOTE
Sekondari zote 22 (na mpya zinazojengwa) zinajenga na kuboresha MAABARA 3 kwenye shule zao ambazo ni za Fizikia, Kemia na Biolojia.
Wananchi wa Kata ya Kiriba WAMEAMUA kuchangia ujenzi wa “HIGH SCHOOL” ya masomo ya SAYANSI (PCM & PCB)  kwa kuanza ujenzi wa MIUNDOMBINU inayohitajika:
*Maabara 3 za Fizikia, Kemia na Biolojia: tayari zimekamilika na zinatumika.
*Jengo la Utawala limekamilika na linatumika.
*Ujenzi wa Mabweni umeanza, ambao utafuatiwa na ujenzi wa Bwalo la Chakula na Jiko.
Bofya hapa kusikiliza CLIP hii  inayoelezea maoni ya Wanavijiji na Viongozi kuhusu Kiriba Sekondari na “High School” wanayoijenga.
Unakaribishwa sana kuchangia ujenzi na uboreshaji wa MIUNDOMBINU ya ELIMU ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

FEDHA ZA COVID-19 KUPELEKA MAJI KWENYE VIJIJI VINGINE VIWILI VYA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Ujenzi na uwekaji wa baadhi ya MIUNDOMBINU ya Bomba la Maji la Mugango-Kiabakari-Mugango

WANANCHI na VIONGOZI wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kutoa SHUKRANI NYINGI kwa SERIKALI yao inayoongozwa na MHE SAMIA SULUHU HASSAN, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa KUWAPATIA FEDHA ZA COVID-19 kwa ajili ya usambazaji maji ya bomba vijijini mwao.
*Tsh MILIONI 500 zimetolewa kwa ajili ya kusambaza maji ya bomba kwenye Vijiji 3 vya: KANDEREMA, BUGOJI na KABURABURA. Mradi huu wa maji kutoka Ziwa Victoria tayari unatekelezwa, na chanzo cha maji kiko Kijijini Suguti, Kata ya Suguti.
Mradi huu unatekelezwa wa RUWASA, Musoma Vijijini
*Tsh MILIONI 300 zitatumika kusambaza maji kwenye Vijiji 2 vya:  KURWAKI (Kata ya Mugango) na KIRIBA (Kata ya Kiriba). Huu nao ni Mradi wa maji ya Ziwa Victoria na chanzo chake kiko Kijijini Kwibara, Kata ya Mugango
Mradi huu wa Vijiji 2 utakuwa sehemu ya Mradi Mkuu wa Bomba la Maji la Mugango-Kiabakari-Butiama.
TAARIFA ya utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Maji la Mugango-Kiabakari- Butiama, utakaogharimu Tsh BILIONI 70, itatolewa hivi karibuni.
Taarifa kutoka:
*Ofisi ya RUWASA
Musoma DC
*Ofisi ya Mradi wa
Mugango-Kiabakari-Butiama
*Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

FEDHA ZA COVID-19 KUPELEKA MAJI YA BOMBA KWENYE VIJIJI VITATU (3)

Tenki la Maji (Lita 200,000 – lenye ngazi pichani) ya Vijiji vya Saragana, Nyambono na Mikuyu lililojengwa Mlimani Nyaberango, Kijijini Nyambono

JIMBO la Musoma Vijijini limepata Tsh MILIONI 500 za COVID-19 kwa ajili ya kusambaza maji vijijini mwetu.
MATUMIZI YA FEDHA hizo za COVID-19 ni kama ifuatavyo:
*Ujenzi wa TENKI la MAJI la mita za ujazo 200 (lita 200,000) Mlimani Nyaberango, Kijijini Nyambono.
*Usambazaji wa MABOMBA ya Maji kutoka kwenye TENKI hilo kwenda Vijiji vya KANDEREMA, BUGOJI na KABURABURA.
*Mlimani Nyaberango (Kijijini Nyambono) tayari lipo TENKI la MAJI (200 cu.m./lita 200,000) kwa ajili ya MAJI ya Vijiji vya SARAGANA, NYAMBONO na MIKUYU. Tenki hili limejengwa kwa kutumia Fedha za Bajeti za Mwaka 2019/2020
CHANZO CHA MAJI YA BOMBA YA VIJIJI HIVI SITA (6)
*Fedha za Bajeti ya Mwaka 2019/2020 na Mwaka 2020/2021 zimewezesha ujenzi wa MIUNDOMBINU ya kutumia Maji ya Ziwa Victoria kutoka kwenye chanzo kilichopo Kijijini Suguti.
*Maji ya kutoka Kijijini SUGUTI yanapelekwa hadi Kijijini CHIRORWE ambapo mabomba yametandazwa kupeleka maji Kijijini WANYERE na mengine kupeleka maji, kupitia Mlima Nyaberango, kwenda Vijijini SARAGANA, NYAMBONO na MIKIYU.
OMBI KWA WANAVIJIJI
*Wanavijiji wa vijiji vyote 6 wanaombwa kurahisisha upatikanaji wa maeneo ya kutandaza mabomba ya kusafirisha maji yatakayo kuwa kwenye MATENKI 2 Mlimani Nyaberango.
*Wanavijiji wanaombwa kuchangia NGUVUKAZI kuchimba mitaro ya kutandaza mabomba ya maji – tujitolee na tuchangie upatikanaji wa MAJI ya BOMBA Vijijini mwetu.
KUKAMILIKA KWA MRADI HUU
*Imepangwa kwamba, ifikapo tarehe 30 Disemba 2021, MAJI ya BOMBA yaanze kutumika ndani ya VIJIJI 6 vya: MIKUYU, NYAMBONO, SARAGANA, KANDEREMA, BUGOJI na KABURABURA.
SHUKRANI:
*Shukrani za dhati zinatolewa na Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini kwenda kwa SERIKALI YETU, na haswa kwa MHE RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, MHE SAMIA SULUHU HASSAN, kwa kufanikisha upatikanaji wa FEDHA za COVID-19 na nyingine kwa manufaa ya TAIFA LETU.
Taarifa kutoka:
*Ofisi ya RUWASA
Musoma DC
*Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

UIMARISHAJI WA UTAMADUNI NA MICHEZO NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI.

Na: Wasaidizi wa Mbunge
*Hamisa Gamba
*Fedson Masawa
*Verediana Mgoma
*Vaileth Peter
JIMBO la  Musoma Vijijini lenye KATA 21 zenye VIJIJI 68 na VITONGOJI 374 limeamua kufufua na kuimarisha NGOMA za ASILI, KWAYA na MICHEZO ya aina mbalimbali chini ya ufadhili wa Mbunge wao wa Jimbo, Profesa Sospeter Muhongo.
USHAURI unaotolewa ni wa KILA KATA kuunda VIKUNDI au TIMU za kushindanishwa na KATA nyingine.
*MASHINDANO YA NGOMA ZA ASILI & KWAYA*
*Sherehe za kila mwaka za NANENANE zinatumika kumpata MSINDI wa KWANZA hadi wa TATU kwenye mashindano ya Ngoma za Asili na Kwaya. Mbunge wa Jimbo ndiye mfadhili wa mashindano haya.
*MASHINDANO YA KUPIGA KASIA*
*Jimbo lina jumla ya Vikundi/Timu 18 za kupiga kasia
*Mashindano haya hufanyika kila mwisho wa mwaka kwa WAPIGA KASIA kushindana umbali wa kati ya mita 1,000 na 1,500 ndani ya Ziwa Victoria. Mfadhili wa mashindano haya ni Mbunge wetu wa Jimbo.
*MPIRA WA MIGUU JIMBONI MWETU*
*Jimbo lina TIMU 78 za Mpira wa Miguu. Mashindano ya Mchezo wa Mpira wa Miguu yanafanyika kwa nyakati tofauti tofauti Jimboni mwetu.
*Utaratibu unatengenezwa wa kupata TIMU ya MPIRA ya Jimbo letu ambayo itashiriki Mashindano mbalimbali kwenye ngazi za Wilaya na Mkoa. Mbunge wa Jimbo alishagawa jezi na mipira kwa kila Kata, na hivi karibuni ataanza kugawa tena vifaa hivyo.
*Mbunge wa Jimbo alitoa mchango mkubwa kuipandisha TIMU ya BIASHARA kuingia LIGI KUU ya TAIFA.
*Vilevile, Mbunge wa Jimbo letu alikuwa mfadhili mkuu wa TIMU ya WASAGA (Kijiji cha Kasoma) iliyofanikiwa kuingia FAINALI YA LIGI DARAJA LA PILI ya Mkoa wa Mara.
*ORODHA NA IDADI YA VIKUNDI VYA NGOMA ZA ASILI ni kama ifuatavyo:*
*Jimbo lina Vikundi 27 vilivyogawanyika katika Makundi 5 kama ifuatavyo
*1. DOGOLI* : Vikundi 4
*2. GITAA*  :   Kikundi  1
*3. LIRANDI / LITUNGU* : Vikundi 2
*4. MBEGETE* : Vikundi 3
*5. ZEZE* : Vikundi 2
*IDADI YA KWAYA JIMBO MWETU*
*UIMBAJI ni kipaji cha pekee kwa Wana Musoma Vijijini.
*Karibu kila Kijiji kina kwaya moja au zaidi. KWAYA kuu zinazotambulika ni 15.
KARIBU UFURAHIE UTAMADUNI WA MUSOMA VIJIJINI – ILANI YA UCHAGUZI YA CCM INATEKELEZWA KWA VITENDO KWENYE MAENEO YOTE!

WANAVIJIJI WANAJENGA  ZAHANATI MPYA 15 KWA AJILI YA UBORESHAJI WA  HUDUMA ZA AFYA NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

UJENZI unaondelea kwenye baadhi ya ZAHANATI,  VITUO vya AFYA vya Musoma Vijijini.

Na: Wasaidizi wa Mbunge
*Verediana Mgoma
*Hamisa Gamba
*Fedson Masawa
*Vaileth Peter
WANAVIJIJI wa JIMBO la MUSOMA VIJIJINI wamekuwa na mwamuko mkubwa wa KUJITOLEA kuanzisha na KUTEKELEZA MIRADI ya MAENDELEO yao kwenye Sekta za Afya, Elimu, Kilimo, Uvuvi, Ufugaji, Utamaduni na Michezo.
SERIKALI inatoa MICHANGO ya FEDHA kwenye utekelezaji wa baadhi ya Miradi hiyo ya Maendeleo.
JIMBO hili lina KATA 21 zenye VIJIJI 68 na VITONGOJI 374
*VITUO 28 VYA CHANJO YA UVIKO MUSOMA VIJIJINI viko Vijijini:*
1.BUGOJI   2.BUGUNDA
3.BWASI      4.KIEMBA
5.KIRIBA      6.KOME
7.KURUGEE 8.MUGANGO 9.MURANGI
10.MWIRINGO
11.NYAKATENDE
12.NYAMBONO
13.RUKUBA    14.SEKA
15.SUGUTI   16.TEGERUKA
17.WANYERE   18. BWAI
19. RUSOLI    20. BUKIMA
21. BUSUNGU   22. CHITARE
23. ETARO   24.KIGERA ETUMA
25. KWIKUBA    26. MASINONO
27. NYEGINA
28. MUSOMA DC HOSP (Kitongoji cha Kwikonero)
*Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea KUJITOKEZA kupata CHANJO ya UVIKO. Mbunge wao wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo alishachanjwa.
*UTEKELEZAJI WA MIRADI MIPYA KWENYE SEKTA YA AFYA NDANI YA JIMBO LETU*
UJENZI wa:
*Zahanati 15
*Wodi 3 za Mama & Mtoto (Zahanati za Kisiwani Rukuba, Bukima & Nyegina)
*Vituo 2 vya Afya (Bugwema & Makojo: kwa mchango mkubwa Serikali)
*Hospital ya Wilaya inayojengwa na Serikali (haijakamilika: kila Kijiji kinachangia Tsh milioni 2)
*HUDUMA ZA AFYA ZILIZOPO*
*Zahanati 24 za Serikali
*Zahanati 4 za Binafsi
*Vituo vya Afya 2 (Murangi & Mugango)
*Magari 5 ya Wagonjwa (Ambulances 5: zilitolewa na Mbunge wa Jimbo)
*ZAHANATI MPYA 15 ZINAZOJENGWA NA WANAVIJIJI*
1.*BUIRA*:  KIJIJI CHA BUIRA, KATA YA BUKUMI
2. *BUSEKERA*: KIJIJI CHA BUSEKERA, KATA YA BUKUMI
3. *BURUNGU*:  KIJIJI CHA BUKUMI KATA, BUKUMI
4. *BUTATA* :  KIJIJI CHA BUTATA KATA, BUKIMA
5.  *BWAI KWITURURU* : KIJIJI CHA BWAI KWITURURU, KATA YA KIRIBA
6. *CHIMATI* :  KIJIJI CHA CHIMATI, KATA YA MAKOJO
7. *CHIRORWE*  : KIJIJI CHA CHIRORWE, KATA YA SUGUTI
8. *KAKISHERI* :  KIJIJI CHA KAKISHERI, KATA YA NYAKATENDE
9. *KURUKEREGE* :  KIJIJI CHA KURUKEREGE, KATA YA NYEGINA
10. *KURWAKI*  : KIJIJI CHA KURWAKI, KATA YA MUGANGO
11. *MANEKE* :  KIJIJI CHA MANEKE, KATA YA BUSAMBARA
12. *MKIRIRA* :  KIJIJI CHA MKIRIRA, KATA YA NYEGINA
13. *MMAHARE*  : KIJIJI CHA MMAHARE, KATA YA ETARO
14. *NYABAENGERE*: KIJIJI CHA NYABAENGERE, KATA YA MUSANJA
15. *NYASAUNGU* :  KIJIJI CHA NYASAUNGU, KATA YA IFULIFU
*Baadhi ya Zahanati hizo zimepokea MICHANGO ya FEDHA kutoka SERIKALI KUU
*Wanavijiji na Viongozi wao (Mbunge wa Jimbo & Madiwani), na baadhi ya Wazaliwa wa Musoma Vijijini) ndio WACHANGIAJI WAKUU wa ujenzi huo.
*Halmashauri yetu (Musoma DC) inashauriwa nayo ianze kuchangia ujenzi wa Zahanati hizo.
*AMBULACE 5 ZA MUSOMA VIJIJINI*
Katika kuboresha Huduma za Afya Jimboni mwao,  Mbunge wa Jimbo, Profesa Sospeter Muhongo, alitoa magari matano ya wagonjwa ambayo kwa sasa yamechoka baada ya kutumika kwa muda mrefu, Ambulance hizo zilipelekwa:
*KITUO CHA AFYA MURANGI*: KATA YA MURANGI
*KITUO CHA AFYA MUGANGO* : KATA YA MUGANGO
*ZAHANATI YA KURUGEE*: KIJIJI CHA BUKUMI, KATA YA BUKUMI
 *ZAHANATI YA MASINONO*: KIJIJI CHA MASINONO, KATA YA BUGWEMA
*ZAHANATI YA NYAKATENDE* :  KIJIJI CHA KABEGI, KATA YA IFULIFU
*OMBI KUTOKA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI*
Wananchi na Viongozi wa Jimbo hili wanaomba MICHANGO ya FEDHA (zikiwemo Fedha za IMF) wakamilishe UJENZI wa MIUNDOMBINU ya AFYA ya Jimboni mwao.
Vilevile, WANAVIJIJI wanaomba MAGARI 2 ya WAGONJWA (2 Ambulances) kwa kuzingatia ukubwa wa Jimbo hili.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI LAFURAHISHWA KUWEPO KWA FEDHA ZA IMF KWA AJILI YA KUKAMILISHA UJENZI WA SHULE SHIKIZI

Baadhi ya majengo yaliyokamilika katika SHULE Shikizi NYASAENGE, Kijijini Kataryo Kata ya Tegeruka

Na: Wasaidizi wa Mbunge
*Verediana Mgoma
*Fedson Masawa
*Hamisa Gamba
*Vaileth Peter
SHULE SHIKIZI zinazojengwa na baadae kupanuliwa kuwa SHULE za MSINGI kamili zitakazojitegemea ni kumi na mbili (12). SHULE hizo ni:
1. *SHULE SHIKIZI BINYAGO* : KIJIJI CHA KABEGI, KATA YA IFULIFU
2.*SHULE SHIKIZI BUANGA*:  KIJIJI CHA BUANGA, KATA YA RUSOLI
3. *SHULE SHIKIZI BURAGA* : KIJIJI CHA BURAGA, KATA YA BUKUMI
4. *SHULE SHIKIZI EGENGE* : KIJIJI CHA BUSAMBA, KATA YA ETARO
5. *SHULE SHIKIZI GOMORA* :  KIJIJI CHA MUSANJA, KATA YA MUSANJA
6.*SHULE SHIKIZI KAGURU*:   KIJIJI CHA BUGWEMA, KATA YA BUGWEMA
7. *SHULE SHIKIZI KARUSENYI*:  KIJIJI CHA MIKUYU, KATA YA NYAMRANDIRIRA
8. *SHULE SHIKIZI  KIHUNDA*:  KIJIJI CHA KAMGURUKI, KATA YA NYAKATENDE
9.*SHULE SHIKIZI   MWIKOKO*:   KIJIJI CHA CHITARE, KATA YA MAKOJO
10. *SHULE SHIKIZI  NYASAENGE* :   KIJIJI CHA KATARYO, KATA YA TEGERUKA
11.*SHULE SHIKIZI RWANGA*: KIJIJI CHA KASOMA, KATA YA NYAMRANDIRIRA
12.*SHULE SHIKIZI   ZIWA* : KIJIJI CHA MWIRINGO, KATA YA BUSAMBARA
*WACHANGIAJI WA UJENZI WA SHULE SHIKIZI NDANI YA JIMBO LETU*
*SERIKALI KUU*
*Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wanashukiru sana kwa kupokea MICHANGO MINGI kutoka SERIKALI KUU (k.m. TAMISEMI) kwa ajili ya UJENZI na UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU ya ELIMU kwenye shule zetu zote za Jimboni mwetu.
*WANANCHI*
*huchangia NGUVUKAZI za kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji ya ujenzi
*Vilevile, huchangia fedha taslimu kutoka kila kaya
*MADIWANI*
*Madiwani wanashirikiana na Wanavijiji kuchangia Miradi ya ujenzi iliyoko kwenye Kata zao.
*MBUNGE WA JIMBO*
*Prof Sospeter Muhongo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini ni mchangiaji mkubwa wa UJENZI na UBORESHAJi wa Miundombinu ya Elimu kwenye SHULE zote SHIKIZI, MSINGI na SEKONDARI za Jimboni mwetu.
*MFUKO WA JIMBO*
*Iliamuliwa kwamba Fedha za Mfuko wa Jimbo, chini ya Mwenyekiti wake, Mbunge wa Jimbo, zitumike kwenye Miradi ya ujenzi na uboreshaji wa Miundombinu ya Elimu ya shule zetu. Hayupo anayepewa fedha mkononi. Halmashauri hununua Vifaa vya ujenzi na kuvigawa kama ilivyopangwa.
*WAZALIWA WA MUSOMA VIJIJINI*
*Baadhi yao huchangia Miradi ya ujenzi ya Vijijini kwao. Majina yao hutajwa kwenye Ripoti za Ofisi ya Mbunge.
*WADAU WENGINE WA MAENDELEO*
*Jimbo letu linashukuru sana kupata WADAU wa MAENDELEO (k.m. Benki za nchini mwetu, PCI Tanzania, BMZ Ujerumani) ambao wanachangia ujenzi na uboreshaji wa Miundombinu ya Elimu ya shule zetu. Na wao pia majina yao hutajwa kwenye Ripoti za Ofisi ya Mbunge
*HALMASHAURI YETU*
*Ushauri umetolewa kwa Halmashauri yetu  ICHANGIE IPASAVYO, na kwa UWAZI, kwenye Miradi ya Maendeleo ya Wanavijiji wa Jimboni mwetu.
*JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI LIKO TAYARI KUANZA KUTUMIA FEDHA ZA IMF*
*MAKUSUDIO ya matumizi ya FEDHA za IMF yanaoana vizuri sana na MIRADI inayotekelezwa kwa sasa Jimboni mwetu.
TUNAJENGA SHULE SHIKIZI 12, ambazo zimetajwa hapo juu na  tunatoa hapa MIFANO MIWILI kushawishi FEDHA za IMF zichangie Miradi yetu ya ujenzi wa SHULE SHIKIZI za Jimboni mwetu
SHULE SHIKIZI NYASAENGE, KIJIJINI KATARYO, KATA YA TEGERUKA
*Hapo awali, Wanafunzi wa Kitongoji cha Nyasaenge  walilazimika kutembea umbali wa zaidi ya Kilometa 10 kwenda masomoni kwenye Shule za Msingi za KATARYO na KATARYO B.
SHULE SHIKIZI hii imekamilisha Vyumba vipya 2 vya Madarasa na Ofisi 1 ya Walimu. Darasa la Awali lina Wanafunzi 106. Ujenzi unaendelea.
SHULE SHIKIZI GOMORA, KIJIJINI MUSANJA, KATA YA MUSANJA
*Tafadhali angalia PICHA zilizoko hapa zenye Jina la GOMORA.
Wanafunzi wa Kitongoji cha GOMORA wanalazimika kwenda masomoni kwenye Shule za Msingi jirani za Lyasembe (Kata ya Murangi), na  Bwenda (Kata ya Rusoli). Ujenzi wa SHULE SHIKIZI GOMORA unaendelea.
UPATIKANAJI WA FEDHA ZA IMF: PONGEZI NYINGI SANA ZINATOLEWA KWENYE SERIKALI YETU CHINI YA UONGOZI MZURI WA MHE RAIS SAMIA SULUHU HASSAN
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

WANAKIJIJI WA KITONGOJI CHA GOMORA WAJENGA SHULE MPYA KUONDOKANA NA ADHA WANAYOPATA WATOTO WAO YA KWENDA MBALI MASOMONI

Ujenzi unaoendelea wa Vyumba vipya 2 vya Madarasa na Ofisi 1 ya Walimu ya Shule Shikizi ya Kitongoji cha Gomora, Kijijini Musanja Kata ya Musanja

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini kwa sasa linajenga SHULE MPYA ZA MSINGI 12 (Shule Shikizi 12) ili kutatua matatizo sugu mawili ambayo ni:
*Umbali mrefu wanaotembea Wanafunzi kwenda masomoni (umbali wa zaidi ya kilomita 4)
*Mirundikano ya Wanafunzi kwenye vyumba vya madarasa (Wanafunzi zaidi ya 45)
SHULE SHIKIZI 12 zinazojengwa ni: Binyago, Buanga, Buraga, Egenge, Gomora, Kaguru, Karusenyi, Kihunda, Mwikoko, Nyasaenge, Rwanga na Ziwa.
SHULE ZA MSINGI zilizopo ni:
*111 za Serikali
*3 za Binafsi
KITONGOJI CHA GOMORA
Kata ya Musanja ina Vijiji vitatu ambavyo ni Musanja, Nyabaengere na Mabui Merafuru.
WANAKIJIJI wa Kitongoji cha Gomora kilichopo Kijiji cha Musanja wameanza ujenzi wa shule mpya ili kuondokana na adha ya watoto wao kutembea umbali mrefu kwenda masomoni kwenye S/M MUSANJA.
MWALIMU MKUU, Mwl Ngasa Msabi ameeleza kuwa Kijiji cha Musanja kina Shule moja ya Msingi ambayo ni S/M MUSANJA iliyofunguliwa Mwaka 1956, kwa sasa ina:
*Wanafunzi 815
*Walimu 8, Pungufu 10
*Vyumba 7 vya Madarasa, Pungufu 12
WANAFUNZI wa  KITONGOJI cha GOMORA wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya KILOMITA 4 kwenda masomoni kwenye S/M Musanja.
Wengine wanatembea umbali mrefu zaidi kwenda masomoni kwenye Shule za Msingi jirani za Lyasembe (Kata ya Murangi), na Bwenda  (Kata ya Rusoli).
MWENYEKITI wa Kitongoji cha Gomora, Ndugu Sospeter Mjarifu ameeleza kuwa WANAKIJIJI wa Kitongoji hicho wameamua kujenga shule yao kwa kutumia MICHANGO ya WANAKIJIJI, DIWANI wa KATA, MBUNGE wa JIMBO na WADAU wengine wa MAENDELEO.
HADI SASA MICHANGO imetolewa na:
*WANAKIJIJI:
(i) kuchimba msingi wa Vyumba vipya 2 vya Madarasa na Ofisi 1 ya Walimu
(ii) kusomba mawe, mchanga na maji ya ujenzi
(iii) kuchangia fedha taslimu, Tsh 15,000/= kutoka kila Kaya
*DIWANI WA KATA:
Ndugu Ernest Mwira alitayarisha HARAMBEE ambayo yeye na WADAU wa MAENDELEO wamechangia:
(i) Fedha Taslimu Tshs1.3 Milioni
(ii) Mifuko ya Saruji 63 na Nondo 8
*MBUNGE WA JIMBO:
Prof Sospeter Muhongo ameanza kuchangia ujenzi huu kwa kutoa SARUJI MIFUKO 50.
LENGO KUU LA WANAKIJIJI:
“Shule Shikizi Gomora ifunguliwe Januari 2022
OMBI kutoka Kitongoji cha Gomora ni kupata MICHANGO kutoka Halmashauri yetu na kutoka kwa Wadau wengine wa Maendeleo kukamilisha ujenzi wa SHULE SHIKIZI GOMORA.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

SERIKALI YATOA TSH MILIONI 50 KUUNGA MKONO JUHUDI ZA WANAKIJIJI KWENYE UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI CHAO

Hatua zilizofikiwa kwenye ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mkirira, Kata ya Nyegina.

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 zenye jumla ya Vijiji 68 lina Huduma za Afya zifuatazo:
*Hospitali ya Wilaya ya Serikali, ujenzi unaendelea kwenye Kitongoji cha Kwikonero, Kijijini Suguti.
*Vituo Vya Afya 3 vya Serikali vinatoa Huduma za Afya. Vituo hivi ni:
^ Murangi
^ Mugango
^ Bugwema (Ujenzi wa upanuzi wa Zahanati ya Masinono kuwa Kituo cha Afya unakamilishwa)
*Zahanati ya Makojo imepewa fedha (Tsh 250m) na Serikali kupanuliwa iwe Kituo cha Afya, hivyo kitakuwa Kituo cha Afya cha nne (4) Jimboni mwetu.
*Zahanati 23 za Serikali zinatoa Huduma za Afya
*Zahanati za Binafsi zipo 4, nazo pia zinatoa Huduma za Afya.
*Zahanati Mpya 16 zinajengwa na Wanavijiji. Serikali imeanza kuchangia ujenzi wa baadhi ya Zahanati hizi.
UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI CHA MKIRIRA
Kijiji cha Mkirira kiko Kata ya Nyegina, inayoundwa na Vijiji 3 (Kurukerege, Mkirira na Nyegina). Kijiji hiki kina jumla ya Wakazi 5,696.
Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mkirira ulianza Mwaka 2016. Ujenzi huu unaendeshwa kwa kutumia MICHANGO ya WANAKIJIJI, SERIKALI KUU (TAMISEMI), MBUNGE WA JIMBO, na WADAU WENGINE wa MAENDELEO.
WACHANGIAJI WA UJENZI:
WANAKIJIJI:
*Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mkirira, Ndugu Sabina Chacha amesema kuwa hadi hapo ujenzi ulipofikia nguvu za WANANCHI ni za thamani ya Tsh. Milioni 16. Hii inajumuisha nguvu kazi za kusomba maji, mchanga, mawe, kokoto na michango ya fedha taslimu.
Wanakijiji walikubaliana kuchangia Tsh. 15,850/= kwa kila mkazi wa Kijijini hapo na mwenye umri wa kuanzia miaka 18.
SERIKALI KUU:
*Serikali Kuu (TAMISEMI) imechangia Tsh. Milioni 50. Hii ni kwa ajili ya ukamilishaji (finishing) wa Zahanati hii ya Mkirira. SHUKRANI NYINGI SANA kwa SERIKALI yetu.
MBUNGE WA JIMBO:
*Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo amechangia  SARUJI MIFUKO 200 kwenye ujenzi wa Zahanati hii.
MICHANGO YA WADAU WENGINE  WA MAENDELEO
*Mhe Amina Makilagi
   Saruji Mifuko 180
*Benki ya NMB
   Mabati 180
*Nyanza Road Works Ltd
   (i) Kokoto tripu 6
   (ii) Saruji Mifuko 50
*Mhe Majira Mchele (Diwani wa Kata ya Nyegina) amechangis Tsh 700,000/=
*Kikundi cha WAZALIWA wa Kijiji cha Mkirira wamechangia:
    (i) Kokoto tripu 3
    (ii) Saruji Mifuko 30
    (iii) Nondo 4
MIUNDOMBINU inayojengwa kwenye Zahanati ya Kijiji cha Mkirira ni:
* Opd
* Chumba cha  Daktari
* Maabara
* Wodi la Mama & Mtoto
* Wodi la Wagonjwa wengine
* Chumba cha Wajawazito (leba)
* Chumba cha Uzazi wa Mpango
* Chumba cha dawa
* Chumba cha chanjo
LENGO WALIOJIWEKEA WANAKIJIJI:
*Kwakuwa Wanakijiji wa Kijiji cha Mkirira wamekuwa wakitembea umbali mrefu wa kilomita 8-10 kwenda kupata Huduma za Afya kwenye Zahanati ya Kijiji jirani cha Nyegina, WANAKIJIJI hao wameamua kukamilisha ujenzi wa Zahanati yao ifikapo Novemba 2021. Hayo yameelezwa na Ndugu Paschal Maerere, Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mkirira.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

ELIMU NI KIPAUMBELE MUHIMU SANA CHA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI – VITONGOJI VYAAMUA KUJENGA SHULE SHIKIZI

Ujenzi wa SHULE SHIKIZI ya KITONGOJI cha BURAGA MWALONI, Kijijini Buraga, Kata ya Bukumi.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
TAKWIMU MUHIMU:
Jimbo la Musoma Vijijiji lina:
*Kata 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374
*Shule za Msingi 111 za Serikali
*Shule za Msingi 3 za Binafsi
*Sekondari 21 za Kata/Serikali
*Sekondari 2 za Binafsi
*High School 1 ya Serikali ya Masomo ya “Arts”
MATATIZO YANAYOTATULIWA KWENYE SEKTA YA ELIMU
WANAVIJIJI wakishirikiana na SERIKALI, na WADAU mbalimbali wa MAENDELEO wanaendelea kutatua matatizo yafuatayo:
*Umbali mrefu wa Wanafunzi kutembea waendapo masomoni.
*Mirundikano ya Wanafunzi kwenye Vyumba vya Madarasa
UJENZI NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU
MIRADI inayoendelea Jimboni mwetu:
*Ujenzi wa Maabara 3 za Fizikia, Kemia na Biolojia kwenye Sekondari zote 21 za Kata/Serikali
*Ujenzi wa Vyumba vipya vya Madarasa, Maktaba, Ofisi za Walimu, Vyoo na Nyumba za Walimu kwenye shule zetu.
*Ujenzi wa Sekondari  mpya 12. Hatua mbalimbali zimefikiwa
*Ujenzi wa Shule Shikizi 12, ambazo zitapanuliwa na kuwa Shule za Msingi zinazojitegemea.
KITONGOJI CHA BURAGA MWALONI CHAANZA UJENZI WA SHULE SHIKIZI
KITONGOJI cha Buraga Mwaloni kipo Kijiji cha Buraga, Kata ya Bukumi. Kata hii inavyo Vijiji vingine vitatu (Bukumi, Buira na Busekera)
KIJIJI cha Buraga kina Shule moja ya Msingi (S/M Buraga) ambayo ina:
*Wanafunzi 690
*Walimu 10
*Vyumba 8 vya Madarasa
*Ilifunguliwa Mwaka 1978
Hayo yameelezwa na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo,  Mwl Joseph Paul
WANAFUNZI wa  Kitongoji cha Buraga Mwaloni WANALAZIMIKA kutembea zaidi ya KILOMITA 5 kwenda masomoni kwenye S/M BURAGA. Vichaka vyenye wanyama wakali ni hatari kubwa kwa Wanafunzi!
Wengine wanatembea umbali mrefu kwenda masomoni kwenye S/M CHITARE ya Kijiji cha jirani cha Chitare cha Kata jirani ya Makojo.
MWENYEKITI wa Kitongoji cha Buraga Mwaloni, Ndugu Steven Wanjara ameeleza kuwa KITONGOJI KIMEAMUA kujenga SHULE SHIKIZI yake na MICHANGO ya ujenzi inatolewa kama ifuatavyo:
WANAKITONGOJI:
*Nguvukazi za kuchimba msingi wa Vyumba 2 vya Madarasa na Ofisi 1 ya Walimu
*Nguvukazi  za kusomba mawe, mchanga na maji
*Fedha taslimu, Tsh 19,300/= kutoka kila Kaya
DIWANI WA KATA:
Mhe Munubi Musa ameanza kutoa MICHANGO yake kwa kuchangia Tsh 100,000/= (laki moja)
MBUNGE WA JIMBO:
Prof Sospeter Muhongo ameanza kwa kuchangia:
*Saruji Mifuko 55
*MFUKO wa JIMBO umechangia Saruji Mifuko 50.
OMBI LA MICHANGO linatolewa na Kitongoji cha Buraga Mwaloni kisaidiwe VIFAA vya UJENZI kukamilisha SHULE SHIKIZI yake – Wanafunzi 40 wa Darasa la Awali wanasomea chini ya miti. HALMASHAURI yetu nayo inapaswa kuchangia ujenzi huu.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

MUSOMA VIJIJINI IMEDHAMIRIA KUANZA KUWA NA “HIGH SCHOOLS” ZA MASOMO YA SAYANSI KUANZIA MWAKANI (Julai 2022)

Wanafunzi na Walimu wakiwa kwenye MAABARA wakifanya “experiments” kwenye Maabara ya MUGANGO SEKONDARI.

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
SEKONDARI zote 21 za KATA za Jimbo la Musoma Vijijini zina Miradi ya aina mbalimbali ya ujenzi na uboreshaji wa Miundombinu ya kujifunzia na kufundishia.
MIRADI hiyo ni pamoja na ujenzi na uboreshaji wa MAABARA za masomo ya Sayansi (Physics, Chemistry & Biology).
MIRADI mingine ni ya ujenzi wa Vyumba vipya vya Madarasa, Maktaba, Mabweni, Vyoo na Nyumba za Walimu.
SHULE 2 za Sekondari za Binafsi, zinazomilikiwa na Kanisa Katoliki (RC) na Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA),  nazo zinaboresha Miundombinu yake ya Elimu.
SEKONDARI mpya 12 zinazojengwa au zilizopangwa kujengwa zitakuwa na Miundombinu kama hiyo ya Elimu.
UKAMILISHWAJI WA MAABARA 3 ZA MASOMO YA SAYANSI
Baadhi ya Sekondari zetu tayari zimekamilisha na kutumia Maabara za Fizikia, Kemia na Biolojia.
SEKONDARI hizo ni:
*Kiriba
*Mugango
*Rusoli
*Bugwema (zinakamilika Sept 2021)
Kwa hiyo, MIPANGO ya ujenzi wa “HIGH SCHOOLS” za Masomo ya Sayansi utaanza kwenye SEKONDARI 4 zilizotajwa hapo juu kwa kuanza kujenga:
*Vyumba vipya vya Madarasa ya “High School”
*Bweni la Wanafunzi wa “High School”
*Bwalo la Chakula & Jiko lake
MUHIMU:
Michango ya awali kabisa inatolewa na WANANCHI WENYEWE ambao ni Wanavijiji na Viongozi wao, na Wazaliwa wa Vijiji vyenye MIRADI ya ujenzi – “KUJITOLEA”
UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU YA MUGANGO SEKONDARI
Ofisi ya Mbunge wa Jimbo imeishatoa taarifa za MAABARA 3 ya Sekondari za Kiriba na Rusoli. Leo inatoa taarifa za MAABARA za Mugango Sekondari
MKUU wa Mugango Sekondari, Mwl Chacha Ragita ameeleza yafuatayo:
*Sekondari ilifunguliwa Mwaka 1999
*ina Wanafunzi 800
*Mahitaji  ya Walimu ni 25, waliopo ni 18
*Mahitaji ya Vyumba vya Madarasa ni 20, vilivyopo ni 16
*Mahitaji ya Matundu ya Vyoo ni 34, yaliyopo 24
*Nyumba 18 za Walimu zinahitajika, zilizopo ni 4
MIUNDOMBINU iliyokamilika:
*Maabara za Fizikia, Kemia na Biolojia zote zipo zinatumika
*Maktaba ipo
*Matundu 2 ya Vyoo vya Walimu yapo.
MICHANGO ya Miradi ya ujenzi na uboreshaji wa Miundombinu ya Sekondari hii inatolewa na:
*Serikali Kuu
*Wanavijiji
*Mbunge wa Jimbo
*Wadau wa Maendeleo
*WANAVIJIJI:
na Viongozi wao wa Kata na Vijijini wanachangia fedha taslimu na NGUVUKAZI za kusomba mawe, mchanga, kokoto na maji ya ujenzi.
*SERIKALI KUU:
imetoa michango mingi tokea Mwaka 1999, na hivi karibuni:
(i) TAMISEMI imetoa vifaa vyote vya Maabara zote tatu.
(ii) TAMISEMI imetoa Shilingi Milioni 75 kwa ajili ya ujenzi wa Bweni la wasichana – ujenzi umeanza
*MBUNGE wa JIMBO, Profesa Sospeter Muhongo amechangia:
(i) Saruji Mifuko 130
(ii) Vitabu zaidi ya 2,000 vya Maktaba
*MRADI wa MAJI (BADEA) umeunganisha Bomba la Maji kwenye Sekondari hii.
*SHIRIKA la Water Aid Tanzania limetoa Matenki 2 ya Maji yenye ujazo wa lita 5,000 kwa kila moja.
UFAULU WA MITIHANI YA KIDATO CHA IV (2020)
*Watahiniwa: 83
Div I – 4    Div II – 5
Div III-14  Div IV – 39
Div 0 – 21
MATOKEO YA KIDATO CHA II (2020)
*Watahiniwa: 175
Div I – 8    Div II – 11
Div III-19  Div IV – 121
Div 0-16
OMBI: WADAU wa MAENDELEO tujitokeze kutoa MICHANGO ya ujenzi wa “HIGH SCHOOLS” za Masomo ya Sayansi Jimboni mwetu.

KATA ISIYOKUWA NA SEKONDARI YAKE YAAMUA KUJENGA SEKONDARI MBILI KWA WAKATI MMOJA

Wananchi wa KIJIJI cha NYASAUNGU wakichimba Msingi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Jengo la Utawala la Nyasaungu Sekondari, Kata ya Ifulifu.

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
KATA ya IFULIFU ni moja ya Kata 21 za Jimbo la Musoma Vijijini. Ni hii Kata pekee ambayo haina Shule yake ya Sekondari.
KATA hii inaundwa na Vijiji 3, ambavyo ni Kabegi, Kiemba na Nyasaungu.
Wanafunzi wa Sekondari wanaotoka kwenye Kata hii wanalazamika kutembea umbali mrefu kwenda masomoni kwenye Sekondari za Kata za jirani ambazo ni Kata ya Mugango (Mugango Sekondari) na Kata ya Nyakatende (Nyakatende Sekondari).
WANAVIJIJI wa Kata hii wameamua kujenga Sekondari Mbili (2) kwa utaratibu huu:
*Kijiji cha Nyasaungu, kinajenga Sekondari yake kwa kushirikiana na Mbunge wao wa Jimbo, Profesa Sospeter Muhongo
*Vijiji vya Kabegi na Kiemba, nao wanajenga Sekondari yao kwa kushirikiana na Mbunge wao wa Jimbo, Profesa Sospeter Muhongo
NYASAUNGU SEKONDARI YA KIJIJI CHA NYASAUNGU
MWENYEKIT wa Serikali ya Kijiji cha Nyasaungu, Ndugu Magesa Chacha ameeleza kuwa, Ujenzi wa Sekondari yao ulianza JULAI 2019 na malengo yao ni NYASAUNGU SEKONDARI ifunguliwe mwakani (Januari 2022).
Mbali ya umbali mrefu wa kilomita 24 za watoto wao kutembea kwenda masomoni Mugango Sekondari, WANAFUNZI wa KIKE wanapambana na vishawishi vingi na baadhi kupata mimba na kukatisha masomo yao.
MIUNDOMBINU INAYOJENGWA
*Vyumba 2 vya Madarasa na Ofisi 1 tayari vimeishaezekwa
*Choo chenye Matundu 6, tayari kimeishaezekwa.
*Jengo la Utawala (msingi unachimbwa, na ujenzi utaanza hivi karibuni)
*Maabara 3 zitajengwa
*Maktaba itajengwa
*Nyumba za Walimu zitajengwa
MAKUNDI YANAYOCHANGIA UJENZI WA NYASAUNGU SEKONDARI
*Michango ya Kijiji cha Nyasaungu ni endelevu kulingana na mahitaji ya MIRADI ya MAENDELEO ya Kijiji hicho.
(i) Kaya zenye ng’ombe zaidi ya 100, michango yao ni Tshs 200,000 (Laki mbili)
(ii) Kaya zenye ng’ombe 99-50, michango yao ni Tshs 100,000 (Laki moja)
(iii) Kaya zenye ng’ombe chini ya 50, michango yao ni Tsh. 40,000 (elfu arobaini)
(iv) NGUVUKAZI za Wanakijiji za kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji ya ujenzi.
(v) Michango ya MBUNGE wa JIMBO Profesa Sospeter Muhongo:
*Mabati 108
*Saruji Mifuko 35
*Nondo 20
MFUKO wa JIMBO
*Mabati 54
*Saruji Mifuko 80
WANAKIJIJI na VIONGOZI wao kwa kipekee kabisa, wanatoa shukrani nyingi sana kwa MBUNGE wao wa JIMBO, Mhe Prof Sospeter Muhongo kwa jitihada kubwa anazoziweka kwenye UTEKELEZAJI wa MIRADI ya MAENDELEO ya Kijiji chao – amechangia madawati na vitabu kwenye Shule yao ya Msingi. AMEFUFUA na kuchangia ujenzi wa Zahanati ya Kijiji chao.
OMBI KUTOKA KIJIJI CHA NYASAUNGU
WAZALIWA wa Kijiji cha Nyasaungu, na Kata nzima ya Ifulifu wanaombwa kutoa MICHANGO kwenye ujenzi wa Nyasaungu Sekondari  ambayo itapokea Wanafunzi kutoka Kata yao na Kata za jirani.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA ZA MUSOMA VIJIJINI

kazi inaendelea Kijijini Bugunda kwenye ujenzi wa DARAJA la MTO NYAMWIFA.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
DARAJA la Mto Nyamwifa ni muhimu sana kwenye barabara inayounganisha Vijiji vya Bukima, Bulinga na Bwasi – yaani barabara hii inaunganisha KATA 3 zenye BIASHARA za mazao ya UVUVI na KILIMO.
MTENDAJI wa KATA ya Bwasi, Ndugu Mashaka Kagere  ameeleza kuwa Daraja hilo liliharibika Mwaka 2018 na kupelekea shughuli za kijamii kuzorota sana. Magari ya kusafirisha SAMAKI kutoka Kome Beach yalishindwa kusafirisha bidhaa hiyo. Hata magari ya abiria yalisimama kufanya kazi huko.
MENEJA wa TARURA (W), Injinia Hussein Abbas ameeleza kuwa wamepata SHILINGI MILIONI 300 kutoka MFUKO wa BARABARA (ROAD FUND) kwa ajili ya MRADI wa DARAJA la Mto Nyamwifa na barabara za eneo hilo. FEDHA hizo zitatumika hivi:
*ujenzi wa Daraja
*ulimaji wa barabara ya km 5.0
*ujenzi wa kalavati 3
*uchimbaji wa mitaro na uwekaji wa kifusi sehemu korofi
MKANDARASI M/s Flow Services and Supplies Ltd ndiye anayetekeleza MRADI huu unaopaswa kukamilika kabla ya mvua za vuli kuanza kunyeesha (Oktoba 2021).
WANAVIJIJI wa Kata 3 (Bukima, Bulinga na Bwasi), WAFANYA BIASHARA na VIONGOZI mbalimbali wanaishukuru sana SERIKALI kwa kutoa FEDHA za kutatua TATIZO hili lilowasumbua tokea Mwaka 2018.
MBUNGE wa JIMBO, Profesa Sospeter Muhongo amekuwa akifuatilia kwa ukaribu sana MIRADI  ya BARABARA zote za Musoma Vijijini.
MBUNGE huyo anaishukuru sana SERIKALI kwa kupitisha BAJETI ya SHILINGI BILIONI 2.85 kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa barabara za Musoma Vijijini kwa Mwaka huu wa Fedha (2021/2022).
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

KILIMO CHA UMWAGILIAJI NA UTUMIAJI WA JEMBE LA KUKOKOTWA NA NG’OMBE (PLAU) VYAONGEZA MAVUNO YA KILIMO MUSOMA VIJIJINI

Wanachama wa KIKUNDI cha ANGAZA wakiandaa Shamba lao la Matikiti Kijijini Bukumi.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
SALAMU ZA HERI ZA  NANENANE KWA WAKULIMA WA MUSOMA VIJIJINI
SHEREHE za NANENANE hazikufanyika Mwaka huu kuepuka MADHARA ya KORONA. Tarehe nyingine itapangwa kwa ajili ya Mashindano yetu ya kila Mwaka ya NaneNane – Ngoma za Asili & Kwaya.
Kesho, JUMATATU, tarehe 9.8.2021 kuna uzinduzi wa CHANJO ya COVID-19 kwenye Viwanja vya S/M KWIBARA, karibu na Makao Makuu ya Muda ya Halmashauri yetu.
MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ameishachanjwa (J&J jab) na Wasaidizi wake wote 5 watachanjwa.
CHANJO HII NI SALAMA, SISI SOTE TWENDE TUKACHANJWE
UBORESHAJI WA KILIMO JIMBONI MWETU
JIMBO la Musoma Vijijini linafanya yafuatayo kuboresha KILIMO cha WAKULIMA wake:
*WAKULIMA wanashawishiwa waunde VIKUNDI vya KILIMO ili kurahisisha upatikanaji ya MAHITAJI yao ya Kilimo
*KILIMO cha UMWAGILIAJI kinawekewa mkazo sana, kwani hatuko mbali na Ziwa Viktoria.
*ZAO JIPYA la ALIZETI linastawi vizuri kwenye udongo wetu.
*PLAU, Jembe la kukokotwa na ng’ombe linagawiwa bure kwenye Vikundi vya Kilimo. Hizi ni jitihada za kupunguza utumiaji wa JEMBE la MKONO.
KIKUNDI CHA ANGAZA CHA KIJIJI CHA BURAGA
KIJIJI cha BURAGA ni kimoja kati ya Vijiji 4 vya KATA ya BUKUMI. Vijiji vingine ni Buira, Bukumi na Busekera.
KIKUNDI cha ANGAZA chenye Makazi yake Kijijini Buraga, kilianzishwa Mwaka 2015 na kinafanya shughuli zake za KILIMO kwenye Kijiji cha BUKUMI.
MWENYEKITI wa Kikundi hiki, Ndugu Pius Bwire ameeleza kwamba KIKUNDI chao:
*kina Wanachama 11
*wanajishughulisha na kilimo cha BUSTANI za matikiti, matango, nyanya na maboga aina ya batanati
*baada ya kupata nyenzo bora za kilimo, watapanua mashamba yao ili kupanua KILIMO cha MAZAO ya BIASHARA yakiwemo ya alizeti, mahindi na mihogo.
AFISA KILIMO wa Kata ya Bukumi, Ndugu Alex Mihambo amekuwa akitembelea KIKUNDI hicho na vingine kwa ajili ya kutoa mafunzo, ushauri na maelekezo ya kitaalamu.
AFISA huyo wa Kilimo amesema MAFANIKIO ya KIKUNDI cha ANGAZA yamehamasisha na kutoa mvuto mkubwa kwa WAKULIMA wa KATA hiyo kujiunga kwenye VIKUNDI vya KILIMO na kuanza KILIMO cha BUSTANI chenye kutumia MAJI ya Ziwa Viktoria kwa UMWAGILIAJI.
Wakulima wameanza kuongeza mavuno ya mahindi kutoka magunia 4-5 kwa ekari hadi 8-10 kwa ekari.
MCHANGO WA  MBUNGE WA JIMBO KWENYE UBORESHAJI WA KILIMO VIJIJINI MWAO
MBUNGE wa Jimbo akishirikiana na SERIKALI anafanya/amefanya yafuatayo:
*kugawa bure MBEGU za ALIZETI. Mbunge aligawa bure TANI 9.85 za mbegu za Alizeti, na WIZARA ya KILIMO ilichangia TANI 10 za mbegu hiyo.
*MBUNGE aligawa bure mbegu za mihogo, mtama na ufuta
*MBUNGE anayo Programu yake ya kugawa bure PLAU kwenye Vikundi vya Kilimo vya Vijiji vyote 68 vya Jimbo hili.
MICHANGO YA MBUNGE WA JIMBO KWENYE KATA YA BUKUMI
*kugawa MBEGU za alizeti, mihogo na mtama kwenye Vijiji vyote 4 vya Kata hii
*kugawa PLAU 5 kwenye Vikundi vya  Kilimo vya Kata ya Bukumi ambavyo ni: Amani Group, Mshikamano, Umoja ni Nguvu, Nyabigoma na Majita Group
*kutoa MASHINE ya UMWAGILIAJI kwa Kikundi cha Angaza kutoka kwenye FEDHA za MFUKO wa JIMBO
KARIBUNI TUBORESHE KILIMO VIJIJINI MWETU – Tununulie ndugu zetu PLAU waachane na Jembe la Mkono. VIKUNDI vingi vinaomba MASHINE za UMWAGILIAJI
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

UJENZI NA UBORESHAJI WA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI VYAHAMASISHA WANAFUNZI KUPENDA MASOMO HAYO

Mkuu wa Shule & Diwani wakiwa ndani ya Maabara ya Biolojia

Tarehe 7.8.2021
Jimbo la Musoma Vijijini
Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
*MALENGO YETU:
(i) SEKONDARI zote 21 za Kata/Serikali za Jimbo la Musoma Vijijini ziko kwenye UJENZI & UBORESHAJI wa MAABARA 3 za  Masomo ya FIZIKIA, KEMIA na BIOLOJIA.
Kazi hiyo imepangwa ikamilike kabla ya Disemba 2022.
(ii) SEKONDARI 2 za Binafsi (Kanisa Katoliki & SDA) nazo zimeshawishiwa kufanya hivyo
(iii) SEKONDARI 10 mpya zinazojengwa au zitakazoanza kujengwa hivi karibuni zitakuwa na MAABARA hizo 3 & MAKTABA
(iv) SEKONDARI zilizokamilisha ujenzi na uboreshaji wa MAABARA hizo 3 zianze matayarisho ya kuwa na “HIGH SCHOOLS” za Masomo ya SAYANSI
(v) KAMPENI maalumu zianzishwe za kushawishi na kuvutia WANAFUNZI kupenda kusoma MASOMO ya SAYANSI
*RUSOLI SEKONDARI
Sekondari hii ni ya Kata ya Rusoli. Ilifunguliwa Mwaka 2010 kuhudumia Wanafunzi wa kutoka Vijiji 3 (Buanga, Kwikerege na Rusoli) vya Kata hii.
MKUU wa Sekondari ya Rusoli, Mwl Tausi Juma ameeleza yafuatayo kuhusu Shule hii:
(i) Ina Wanafunzi 444
(ii) Mahitaji ya Walimu ni 15,  waliopo ni 13 na kati ya hao 6 ni wa Masomo ya Sayansi
(iii) Ina MAABARA 3 za Fizikia, Kemia na Biolojia
(iv) Mahitaji ya Vyumba vya Madarasa ni 12, vilivyopo ni 10
UJENZI & UBORESHAJI WA MAABARA ZA RUSOLI SEKONDARI
Ujenzi na uboreshaji wa MAABARA hizi unashirikisha:
*Serikali
*Wanavijiji (NGUVUKAZI)
*Wazaliwa wa Kata ya Rusoli
*Mbunge wa Jimbo
MATUMIZI YA FEDHA ZA SERIKALI
MKUU wa Rusoli Sekondari, Mwl. Tausi Juma ameeleza kuwa Serikali kupitia Mradi wake wa EP4R imetoa:
(i) SHILINGI MILIONI 30 kwa ajili ya:
*ukamilishaji wa Maabara ya FIZIKIA na samani zake
*ujenzi wa TENKI la  kuvunia maji ya mvua ya kutumia kwenye Maabara
*kukamilisha uwekaji wa mfumo wa gesi na umeme kwenye Maabara.
(ii) SHILINGI MILIONI 25 kwa ajili ya ukamilishaji wa Maabara ya KEMIA
(iii) VIFAA vya Maabara vilitolewa na TAMISEMI
*Inakadiriwa kwamba Asilimia 75 (75%) ya Wanafunzi wa Kidato vya I & II wa RUSOLI SEKONDARI  wamehasika na kuvutiwa sana na MASOMO ya SAYANSI ya VITENDO (practicals) kwenye MAABARA zao.
MICHANGO MINGINE ILIYOKWISHATOLEWA RUSOLI SEKONDARI
(i) WAZALIWA wa Kata ya Rusoli kupitia Kikundi chao kiitwacho, “YEBHE CHIKOMESHE” kimetoa MICHANGO MINGI kwenye Sekondari hii ikiwemo ya VIFAA vya MAABARA, COMPUTER, PRINTER & PHOTOCOPY
Kikundi hiki kinaongozwa kwa umahiri mkubwa na Ndugu JEFF MAKONGO.
Vilevile, “Yebhe Chikomeshe” kimejenga NYUMBA (two in one) ya WALIMU wa Sekondari hii.
Kimechimba KISIMA cha MAJI kwa matumzi ya Kijiji cha Rusoli. – AHSANTE SANA SANA “YEBHE CHIKOMESHE” – Kikundi cha Maendeleo yanayoonekana!
(ii) MBUNGE wa JIMBO, Profesa Sospeter Muhongo amechangia:
*Saruji Mifuko 70
*Posho ya Mwalimu wa Kujitolea wa Masomo ya Sayansi
*Vitabu zaidi ya 2,000 vya Maktaba
DIWANI wa Kata ya Rusoli, Mhe Boaz Nyeula na Viongozi wengine wa Kata na Vijiji wanaendelea kutoa SHUKRANI NYINGI SANA kwa MICHANGO & MISAADA wanayopokea kutoka SERIKALINI na kutoka kwa WADAU wengine wa MAENDELEO ya Kata yao, hasa kutoka kwa Mbunge wao wa Jimbo, na Kikundi cha, “Yebhe Chikomeshe.”
UFAULU WA MITIHANI WA RUSOLI SEKONDARI
*MATOKEO YA KIDATO CHA II (2020)
Watahiniwa: 107
Div I= 6     Div II= 9
Div III=26   Div IV =66
*MATOKEO YA KIDATO CHA IV (2020)
Watahiniwa: 64
Div I= 1     Div II= 6
Div III= 7   Div IV= 44
Div 0= 6
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini