BENKI YA CRDB YACHANGIA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA S/M MURUNYIGO

Mkuu wa Wilaya (DC) ya Musoma, Dr Vicent Naano Anney (pichani – mwenye Kaunda Suti ya kijivu) akipokea VIFAA VYA UJENZI kutoka Benki ya CRDB kwa ajili ya S/M Murunyigo ya Kijiji cha Kiemba, Kata ya Ifulifu.

Jumamosi, 4.4.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
AZIMIO LA MKOA WA MARA la kujenga na kuboresha MIUNDOMBINU YA ELIMU kwenye Shule zake za MSINGI na SEKONDARI unaendelea kutekelezwa kwa kasi ya kuridhisha ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma yenye Jimbo la MUSOMA VIJIJINI.
Jana, Ijumaa, 3.4.2020, Mkuu wa Wilaya (DC) ya Musoma, Dr Vicent Naano Anney alipokea VIFAA VYA UJENZI kutoka Benki ya CRDB, Tawi la Musoma.
Ndugu Solomon Marwa, Meneja wa Benki ya CRDB, Tawi la Musoma alikabidhi VIFAA hivyo ambavyo ni: SARUJI MIFUKO 60 na VIFAA vya kutengeneza MILANGO na MADIRISHA. Vifaa vyote vinagharimu Tsh Milioni 2.
WANANCHI wa Kijiji cha Kiemba chenye S/M Murunyigo na VONGOZI wao wanaishukuru sana Benki ya CRDB kwa MCHANGO huo uliopatikana kwa muda muafaka.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dr Vicent Naano Anney, Mkurugenzi Mtendaji (DED) wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Ndugu John Kayombo na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo WANAISHUKURU sana Benki ya CRDB kwa MCHANGO huo na mingine waliyokwishaitoa ndani ya Wilaya yao.

WANAFUNZI 157 WA KIDATO CHA KWANZA  HAWATARUNDIKANA MADARASANI 

Kazi za upauaji na upigaji lipu wa VYUMBA VIPYA vya MADARASA ya KIDATO cha KWANZA (2020) cha BULINGA SEKONDARI ya Kata ya Bulinga.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
BULINGA SEKONDARI ya Kata ya Bulinga ilisajiliwa Mwaka jana (2019) na kabla ya hapo ilikuwa SEKONDARI SHIKIZI ya Nyanja Sekondari ya Kata jirani ya Bwasi.
KATA YA BULINGA yenye Vijiji 3 vya Bujaga, Bulinga na Busungu imekamilisha ujenzi wa VYUMBA 3 VIPYA vya MADARASA kwa ajili ya WANAFUNZI wa KIDATO cha KWANZA (Form I) wa Sekondari yao ya Kata.
MWALIMU MKUU wa Sekondari hiyo, Mwl Nyang’oso Chacha Munyera ameeleza kwamba jumla ya WANAFUNZI waliochaguliwa kujiunga KIDATO cha KWANZA Mwaka huu (Januari 2020) ni 157 na hadi sasa WANAFUNZI 134 ndio WAMEANZA MASOMO Shuleni hapo.
CHUMBA kimoja cha Darasa kilikuwa kinachukua WANAFUNZI 67, na baada ya KUKAMILISHA ujenzi wa VYUMBA 3 VIPYA, sasa kila CHUMBA kimoja cha Darasa kitachukua WANAFUNZI 45 – hakuna mirundikano madarasani!
MTENDAJI KATA hiyo, Ndugu Pima  Mengere amesema upauaji na upigaji lipu VYUMBA VIPYA 2 ulikamilika tarehe 25 Machi 2020 na muda mfupi ujao watakamilisha kazi ya kupiga lipu Chumba cha tatu. Kwa hiyo, WANAFUNZI 134 wa KIDATO cha KWANZA watakaporudi Shuleni (baada ya likizo ya CORONAVIRUS) watakuwa na VYUMBA VIPYA 3 vya Madarasa yao – hakuna mirundikano madarasani.
WANAVIJIJI wamechangia NGUVUKAZI zao na FEDHA taslimu Tsh 10,500 kutoka kila KAYA.
DIWANI wa KATA ya Bulinga, Mhe Mambo Japani (CHADEMA) amesema kwamba kuna MIPANGO imewekwa na WANAVIJIJI ya KUSHIRIKIANA na SERIKALI kupitia HALMASHAURI yao na MBUNGE wao wa Jimbo, KUBORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU kwenye SEKONDARI hiyo na SHULE zote za MSINGI ndani ya Kata yao.
DIWANI huyo amesema ifikapo Januari 2021, MADARASA CHINI YA MITI yatatoweka kabisa. Ameishukuru sana SERIKALI kwa MICHANGO yake kwenye SEKTA YA ELIMU ndani ya Kata yao.
MICHANGO YA MBUNGE WA JIMBO
Mbunge Prof Sospeter Muhongo amechangia:
* MADAWATI, VITABU vingi vya MAKTABA, SARUJI na MABATI kwa Shule zote za Msingi za Kata ya Bulinga.
* BULINGA SEKONDARI: Mbunge huyo amechangia Saruji Mifuko 192 na Vitabu vingi vya Maktaba. MFUKO wa JIMBO umechangia Mabati 108.
WAZALIWA wa KATA ya BULINGA wanaombwa wajitokeze kuchangia MIRADI ya MAENDELEO ya KATA yao ikiwemo ya UBORESHAJI wa Miundombinu ya Elimu kwenye Shule za Msingi na Sekondari.

 ZAHANATI KWA KILA KIJIJI – KATA YA NYEGINA YATEKELEZA ILANI YA CCM

MAFUNDI na VONGOZI wa Kata ya Nyegina wakiwa kwenye eneo la Ujenzi wa ZAHANATI ya KIJIJI cha MKIRIRA, Kata ya NYEGINA.

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
KATA YA NYEGINA ina Vijiji 3 ambavyo ni Kurukerege, Mkirira na Nyegina.
KIJIJI cha NYEGINA kinayo ZAHANATI ambayo inapanuliwa kwa kuongeza WADI ya MAMA na MTOTO. Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo amechangia SARUJI MIFUKO 200 kwenye ujenzi wa WADI hiyo.
KIJIJI CHA KURUKEREGE kilisimamisha kwa muda ujenzi wa ZAHANATI yake baada ya kupata fedha kutoka PIC kujenga VYOO vya S/M Kurukerege. Kazi hiyo imekamilika na sasa wanaendelea na ujenzi wa ZAHANATI ya Kijiji chao. Mbunge wao wa Jimbo atakagua ujenzi huo na kuchangia ipasavyo.
KIJIJI CHA MKIRIRA
kinajenga ZAHANATI yake kwa kushirikisha WAZALIWA wa Kijiji hicho na WADAU wengine wa MAENDELEO.
UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI CHA MKIRIRA
Afisa Mtendaji wa Serikali ya Kijiji cha Mkirira, Ndugu  Sabina  Chacha amesema kuwa WANAKIJIJI wamekusudia kukamilisha ujenzi wa BOMA la ZAHANATI yao ifikapo mwishoni mwa Mwezi huu (April 2020).
WANAVIJIJI wakiongozwa na DIWANI wao, Mhe Majira Mchele, wanachangia NGUVUKAZI na FEDHA taslimu kwenye ujenzi wa ZAHANATI ya Kijiji cha MKIRIRA.
DIWANI huyo ametoa SHUKRANI nyingi kwa WAZALIWA na Kijiji hicho kwa MICHANGO yao iliyofanikisha ujenzi kufikia hatua hiyo. Vilevile, amesema baadhi ya WAZALIWA wa Kijiji hicho wameanzisha UMOJA wao uitwao, “MKIRIRA MAENDELEO” kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa ZAHATI ya Kijiji chao.
DIWANI huyo ameendelea kutoa SHUKRANI zake kwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo kwa kuchangia SARUJI MIFUKO 200 kwenye ujenzi wa ZAHANATI hiyo na kwa MICHANGO yake mingi ndani ya KATA hiyo kwenye SEKTA za Elimu, Afya, Kilimo, Mazingira, Michezo na Utamaduni.
SHUKRANI ZA KIPEKEE zinapelekwa NMB kwa kuchangia MABATI 182. Mhe Amina Makilagi (Mb)  anapewa SHUKRANI nyingi kwa MICHANGO yake.
Aidha, MWENYEKITI wa Serikali ya Kijiji hiki, Ndugu Magogwa Majinge alisema bado kuna UPUNGUFU wa VIFAA VYA UJENZI wa nondo 12 na Saruji Mifuko 40 kukamilisha ujenzi wa BOMA hilo.
UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM (2015-2020) kwenye SEKTA YA AFYA unaendelea vizuri ndani ya JIMBO la Musoma Vijijini kwa USHIRIKA wa SERIKALI na WANANCHI:
* Zahanati Mpya 14
zinajengwa
* Hospitali ya Wilaya moja (1) inajengwa
* Zahanati moja (1) ya Masinono inapanuliwa kuwa Kituo cha Afya
* Zahanati zinazotoa HUDUMA ni 28 (24 za Serikali & 4 za Binafsi)
*Vituo vya Afya vinavyotoa HUDUMA ni viwili (2)
KARIBUNI TUKAMILISHE UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI CHA MKIRIRA NA NYINGINE 13 ZINAZOJENGWA KWENYE VIJIJI VINGINE 13 JIMBONI MWETU

WALEMAVU KWIKUBA GROUP WAPOKEA MKOPO USIOKUWA NA RIBA KUTOKA HALMASHAURI YAO

Baadhi ya Wana-Kikundi cha WALEMAVU KWIKUBA GROUP wakiwa kwenye MRADI wao wa UFUGAJI wa KONDOO na MBUZI, Kijijini Kwikuba, Kata ya Busambara.

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
KIKUNDI cha Watu wenye ULEMAVU kiitwacho, “WALEMAVU KWIKUBA GROUP” kilianzishwa Februari 2019 kikiwa na WANACHAMA 26 ambao kwa sasa wamefika 41.
WALEMAVU KWIKUBA GROUP yenye maskani yake Kijijini Kwikuba, Kata ya Busambara ilianza kwa KUUZA NAFAKA na wamepanua biashara yao na kuanza KUFUGA KONDOO na MBUZI baada ya kupata MKOPO usiokuwa na RIBA wa Tsh 2,400,000 kutoka HALMASHAURI ya Wilaya ya Musoma yenye Jimbo la Musoma Vijijini.
MWENYEKITI wa Kikundi hiki, Ndugu John Ndaro Musulubhi alisema kuwa Kikundi chao KIMESAJILIWA na HALMASHAURI yao na LENGO lao kuu ni KUJITEGEMEA KIUCHUMI kutokana na MAPATO ya BIASHARA zao za NAFAKA na MIFUGO.
MWENYEKITI huyo anaishukuru sana HALMASHAURI ya Wilaya ya Musoma na VIONGOZI wake kwa kutoa MIKOPO isiyokuwa na RIBA kwa WATU wenye ULEMAVU walioko ndani ya Halmashauri hiyo.
MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ametunisha MTAJI wao wa biashara ya NAFAKA kwa kuwanunulia MAGUNIA KUMI (10) ya MAHINDI na amesema watawasaidia kutafuta WADAU wengine wa Maendeleo watakaowatunishia MTAJI wao wa biashara.
Sambamba na MAFANIKIO hayo, WALEMAVU KWIKUBA GROUP  wanataraji kuanzisha  MRADI wa USEREMALA, na wanaomba WADAU wa MAENDELEO na hasa kwa WATU wenye ULEMAVU, wajitokeze kuwasaidia wapate VIFAA VYA USEREMALA.
WALEMAVU KWIKUBA GROUP wanawashauri na kuwashawishi WATU WENYE ULEMAVU po pote walipo kutumia FURSA zinazotolewa na SERIKALI yetu ya kuwafanya WAJITEGEMEE KIUCHUMI.

SHULE YA MSINGI MURANGI B YAKARIBIA KUACHANA NA DARASA NA OFISI CHINI YA MITI

UPAUAJI wa CHUMBA kimoja cha Darasa S/M MURANGI B ya Kijijini Lyasembe, Kata ya Murangi

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
MWALIMU MKUU wa S/M Murangi B, Mwl Kerango Msakambi ameeleza kwamba SHULE hiyo ina jumla ya WANAFUNZI 544, WALIMU 6. Vyumba vya Madarasa vilivyopo ni 7 na UPUNGUFU ni 9. Shule ilifunguliwa Mwaka 2014 na iko Kijijini Lyasembe, Kata ya Murangi.
Chumba cha Darasa lenye WANAFUNZI WENGI kinao 124 (Std III) na chenye wachache ni 59 (Std II).
WANAFUNZI wa Darasa la II hawana Chumba chao cha Darasa, kwa hiyo WANASOMEA chini ya MTI au ikibidi wanapokezana (kusoma kwa zamu) na Darasa la I lenye Wanafunzi 71.
WALIMU hawana OFISI, wanakaa CHINI YA MITI na mvua ikinyeesha wanahamia MADARASANI.
Diwani wa Kata ya Murangi, Mhe Simion Kujerwa amesema kwamba KATA imedhamiria kutatuta TATIZO SUGU la MIRUNDIKANO YA WANAFUNZI Madarasani. WANAVIJIJI na WAZALIWA wa Kata hiyo wameanza kuchangia ujenzi wa MIUNDOMBINU bora kwenye Shule zilizoko ndani ya Kata yao.
KATA ya Murangi, yenye VIJIJI 2 (Lyasembe na Murangi) inazo SHULE ZA MSINGI 4 na SEKONDARI 1.
DIWANI huyo anaishukuru sana SERIKALI kupitia Halmashauri yao na Mbunge wao, Profesa Sospeter Muhongo kwa  MICHANGO ya MIRADI ya MAENDELEO kwenye Kata yao. Ameeleza kwamba MBUNGE wao wa JIMBO amechangia SARUJI, MADAWATI na VITABU vingi kwa SHULE zote nne (4) za MSINGI. MURANGI SECONDARY School imepewa VITABU VINGI vya MAKTABA
UKAMILISHAJI WA DARASA LA S/M MURANGI B
Njia pekee ya kuwatoa WANAFUNZI (Std II) CHINI ya MTI ni KUKAMILISHA Chumba kimoja cha Darasa kinachoezekwa kwa MABATI 54 yaliyonunuliwa na FEDHA za MFUKO wa JIMBO.
MBUNGO wa Jimbo anachangia SARUJI MIFUKO 50 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Chumba hicho. SARUJI hiyo itachukuliwa tarehe 2.4.2020.
Baada ya JENGO hilo kukamilika, Mbunge wa Jimbo atapiga HARAMBEE ya kujenga VYUMBA 2 VIPYA vya Madarasa vyenye OFISI ya WALIMU katikati.
WAZALIWA wa KATA ya MURANGI wanaombwa wajitokeze KUCHANGIA UJENZI huu na MIRADI mingine ya MAENDELEO inayotekelezwa ndani ya Kata yao.
Kwa muda wa takribani MIAKA MINNE na NUSU (4.5 yrs), JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI limeendelea KUJENGA na KUBORESHA MIUNDOMBINU ya ELIMU kwenye SHULE zake zote za MSINGI (114 – 111 za Serikali na 3 za Binafsi) na SEKONDARI (22 – 20 za Serikali na 2 za Binafsi). MADAWATI na VITABU VINGI vya MAKTABA vimegawiwa. Sekondari Mpya 5 zinajengwa zifunguliwe mwakani  (Januari 2021).
WADAU WA MAENDELEO wakiwemo PCI, NMB, CRDB na baadhi ya WAZALIWA wa Vijiji vya Jimbo hili WANAENDELEA KUCHANGIA MIRADI muhimu kwenye SEKTA YA ELIMU ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini – TUNAWASHUKURU SANA!
Picha zilizoko hapa zinaonesha UPAUAJI wa CHUMBA kimoja cha Darasa ya S/M MURANGI B ya Kijijini Lyasembe, Kata ya Murangi.

MATATIZO YA UMBALI MREFU WA KUTEMBEA NA MIRUNDIKANO YA WANAFUNZI MADARASANI YAENDELEA KUTATULIWA

Ujenzi wa Vyumba vipya vya Madarasa unaoendelea kwenye SHULE SHIKIZI BURAGA MWALONI inayojengwa kwenye Kitongoji cha Mwaloni, Kijijini Buraga, Kata ya Bukumi.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
AZIMIO NA. 1 LA UBORESHAJI WA KIWANGO CHA ELIMU NDANI YA MKOA WA MARA
(1) Uboreshaji wa MIUNDOMBINU ya ELIMU ya aina zote katika Shule za Msingi na Sekondari
JIMBO la Musoma Vijijini LINATEKELEZA AZIMIO hilo na mengine matano (5) kwa USHIRIKA wa WANANCHI, VIONGOZI na SERIKALI yao – MATUNDA MAZURI yameanza kuonekana.
SHULE ZA MSINGI JIMBONI
* 111 za Serikali
* 3 za Binafsi
UJENZI unaendelea kwenye SHULE zote za MSINGI ili kuboresha MIUNDOMBINU yao ya ELIMU.
MATUNDA YA AWALI yaliyopatikana tokea UBORESHAJI wa MIUNDOMBINU ya SHULE ZA MSINGI uanze, miaka minne (4) iliyopita ni HALMASHAURI YA WILAYA YA MUSOMA (yenye Jimbo la Musoma Vijijini) kuwa ya KWANZA MKOANI MARA Mwaka jana (2019) kwenye MITIHANI YA DARASA LA NNE (IV).
SHULE SHIKIZI JIMBONI
* 11 zinaendelea kujengwa na baadhi tayari zina WANAFUNZI wa Darasa la AWALI na la kwanza (Std I).
Ujenzi wa SHULE MPYA hizi unazingatia UBORA unaotakiwa kwa MIUNDOMBINU yake.
UJENZI WA SHULE SHIKIZI BURAGA MWALONI
SHULE MPYA hii inajengwa na WAKAZI wa Kitongoji cha Buraga Mwaloni ili KUTATUA TATIZO la WATOTO wao wenye UMRI wa chini ya MIAKA 10 kutembea umbali wa kilometa 5-7 kwenda masomoni kwenye SHULE za MSINGI za vitongoji jirani.
MWALIMU WA KUJITOLEA, Ndugu Dickson Maregesi ndie MSIMAMIZI wa SHULE SHIKIZI Buraga Mwaloni. Amesema SHULE hiyo ilianza rasmi Mwaka 2015 ikiwa na jumla ya WANAFUNZI 117 waliokuwa wanasomea CHINI YA MTI na baada ya kuhitimu hapo WALIENDA kuanza MASOMO ya Darasa la kwanza (Std I) kwenye SHULE ZA MSINGI za Buraga na Chitare ambazo ziko mbali na Kitongoji cha Mwaloni.
Kwa wakati huu, WANAFUNZI 41 wa Darasa la Awali wa SHULE SHIKIZI hiyo wanasomea chini ya MTI.
Ndugu Nyajoge Wanjara, Mwenyekiti wa KAMATI ya ujenzi wa Shule hiyo amesema WANA-KITONGOJI wameanza KUCHANGIA UJENZI wa Shule yao kwa kutoa NGUVUKAZI na Fedha taslimu kiasi cha Tsh 5,000/= kutoka kila KAYA. Kiongozi huyo amesisitiza kwamba  SHULE yao hiyo ujenzi utakamilika na kufunguliwa Januari 2021.
MICHANGO MINGINE
* Saruji Mifuko 50 kutoka MFUKO wa JIMBO
* Saruji Mifuko 100 kutoka kwa Mbunge wao, Prof Sospeter Muhongo
WAZALIWA wa Kata ya Bukumi na hasa wa Kijiji cha Buraga wanaombwa KUTOA MICHAGO ya ujenzi wa Shule hiyo ambayo inahitaji VYUMBA vipya vya Madarasa, Ofisi ya Walimu, Vyoo na Nyumba ya Walimu.
WADAU wengine wa Maendeleo nao wanaombwa KUCHANGIA.

OFISI YA CCM YA WILAYA YA MUSOMA YAANZA KUJENGWA

Uanzaji wa ujenzi wa OFISI YA CCM ya Wilaya ya Musoma Vijijini, yaani UCHIMBAJI wa MSINGI na UFYATUAJI wa MATOFALI.

OFISI YA MUDA ya CCM ya Wilaya ya Musoma Vijijini iko kwenye Kijiji cha Chumwi, Kata ya Nyamrandirira.
Wana-CCM wa Musoma Vijijini (kwenye Vitongoji 374, Vijiji 68, Kata 21) wakiongozwa na KAMATI YA UJENZI wameanza rasmi kujenga OFISI YA CCM ya Wilaya yao.
MWENYEKITI wa KAMATI ya Ujenzi ni Dr Vicent Anney Naano, Mkuu wa Wilaya (DC) ya Musoma na MAKAMU MWENYEKITI ni Mhe Diwani Charles Magoma Nyambita, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma.
Ndugu John Lipesi Kayombo, Mkurugenzi Mtendaji (DED) wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ANASHIRIKI vizuri sana kwenye UTEKELEZAJI wa MRADI huu.
HATUA ZA AWALI ZA UJENZI
Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi amewezesha upatikanaji wa MAWE na MCHANGA wa kuanzia ujenzi. FUNDI ameanza kuchimba MSINGI.
AHADI ZA MICHANGO ILIYOTOLEWA KWENYE HARAMBEE YA UJENZI
KAMATI ya ujenzi INASUBIRI WALIOTOA AHADI za VIFAA VYA UJENZI na FEDHA TASLIMU watimize AHADI zao ili ujenzi uende kwa kasi kubwa.
AHADI YA MBUNGE WA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo alihaidi kutoa MCHANGO wa awali wa MATOFALI 5,000 (elfu tano). Alianza kwa kununua MATOFALI 1,000 kutoka Kanisa Katoliki Nyegina.
KAMATI YA UJENZI imependekeza MATOFALI yatengenezewe karibu na eneo la ujenzi ili kuachana kabisa na GHARAMA za kusafirisha MATOFALI. Kwa hiyo, Mbunge huyo ameanza kununua SARUJI hapo hapo Kijijini (Murangi) ya kutengenezea MATOFALI 5,000.
Vilevile, Mbunge huyo atachangia FEDHA za kumlipa FUNDI ujenzi.
Diwani wa Kata ya Murangi, Mwenyeji wa MRADI huu, Mhe Simion Kujerwa ANAFANYA KAZI NZURI ya kusimamia ujenzi wa OFISI hii  ya CCM Wilaya.

SHULE YA MSINGI MKAPA YA KIJIJINI KASTAM IMEAMUA KUTATUA TATIZO LA MIRUNDIKANO MADARASANI

Kazi inaendelea ya ujenzi wa Vyumba VIPYA vya Madarasa ya S/M MKAPA ya Kijiji cha Kastam, Kata ya Bukima.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
SHULE YA MSINGI MKAPA ilianzishwa Mwaka 2009 na iko Kijijini Kastam, Kata ya Bukima.
Mwalimu Mkuu wake, Mwl
Nyakusanja David Mkangara amesema Shule hiyo ina jumla ya WANAFUNZI 972. Vyumba vya Madarasa VILIVYOPO ni nane (8) na UPUNGUFU ni kumi na nne (14).
Mwalimu Mkuu huyo anasema, “Hawapo Wanafunzi WANAOSOMEA NJE chini ya MITI lakini kuna MIRUNDIKANO MIKUBWA Madarasani ambapo Chumba kimoja cha Darasa chenye WANAFUNZI WENGI kinao 204 (Std III) na chenye WACHACHE kinao 87 (Std VI).”
TATIZO LA MIRUNDIKANO mikubwa Madarasani LINATATULIWA kwa KUJENGA Vyumba Vipya vya Madarasa.
Ndugu Adonias Matijo, Mtendaji wa Serikali ya Kijiji cha Kastam amesema kuwa Kijiji hicho kilipokea Tsh 2,030,000/= ambayo ni RUZUKU (20%) kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Fedha hizo zilitumika KUNUNUA SARUJI na kuanza kufyatua MATOFALI  ya ujenzi wa Vyumba Vipya vya Madarasa.
Mbali ya FEDHA kutoka kwenye HALMASHAURI yao, KILA KAYA ya Kijiji cha Kastam inachangia  NGUVUKAZI na FEDHA Taslimu ya kiasi cha Tsh 6,200/=
VYANZO hivyo vya FEDHA na NGUVUKAZI vimefanya WANAKIJIJI kufanikiwa KUJENGA Vyumba viwili (2) vya Madarasa na Ofisi moja (1) ya Walimu.
KAZI BADO KUBWA, Wanakijiji hao wanaomba WADAU wa Maendeleo na WAZALIWA na Kijiji cha Kastam na Kata ya Bukima kwa ujumla, WAJITOKEZE KUCHANGIA ujenzi wa Vyumba VIPYA vya Madarasa ya S/M MKAPA. HARAMBEE ya Mbunge wa Jimbo itafanyika hivi karibuni.
MICHANGO YA MBUNGE WA JIMBO KWENYE S/M MKAPA
Mbunge wao wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ameishachangia:
* Madawati 160
* Vitabu vingi vya Maktaba
* Saruji Mifuko 60
* Mabati 54
MICHANGO YA MFUKO WA JIMBO KWENYE S/M MKAPA
* Saruji Mifuko 50
* Mabati 54
Diwani wa Kata hiyo (Bukima), Mhe January Simula amesema kwamba KATA YAO  imejipanga kuhakikisha kwamba WANAFUNZI wa SHULE zote za  MSINGI ndani ya Kata yao HAWATASOMEA NJE CHINI YA MITI ifikapo mwakani (Januari 2021).
Diwani huyo anawashukuru Viongozi wa Wilaya na Halmashauri yao, na Mbunge wao wa Jimbo kwa MICHANGO wanayoitoa kwenye MIRADI ya MAENDELEO (Elimu, Afya, Kilimo, Mazingira, Michezo, n.k.) ya Kata yao yenye VIJIJI 3 (Bukima, Butata na Kastam).
JIMBO la Musoma Vijijini LINAJENGA na KUBORESHA MIUNDOMBINU ya ELIMU kwenye SHULE zake zote za MSINGI 114 (111 za Serikali na 3 za Binafsi), SHULE SHIKIZI 11 (kati ya hizi zipo zilizofunguliwa).
Jimbo hili lenye KATA 21 na VIJIJI 68 lina SEKONDARI 22 zenye Wanafunzi (20 za Serikali/Kata na 2 za Binafsi). Sekondari MPYA 5 zinajengwa na zitafunguliwa mwakani (Januari 2021).

KIJIJI CHA ETARO CHAJIWEKA SAWA KUMALIZA TATIZO LA UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MADARASA

Mwalimu Mkuu wa S/M Etaro (Mwl Mangire Stephano Mahombwe) na Mtendaji wa Serikali ya Kijiji cha Etaro (Ndugu Sophia Charles) wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa Vyumba vipya vya Madarasa.

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
WANANCHI wa Kijiji cha ETARO, Kata ya Etaro wanaendelea na utekelezaji wa AZIMIO la MKOA WA MARA LA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU katika Shule yao ya Msingi (S/M Etaro).
UTARATIBU MAALUMU unawekwa wa kuwashirikisha WADAU mbalimbali wa Maendeleo wakiwemo WAZALIWA wa Kijiji  na Kata hiyo ili waweze KUCHANGIA utatuzi wa tatizo SUGU  la UPUNGUFU wa Miundombinu ya Elimu Shuleni hapo.
Akizungumza na Msaidizi wa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Shuleni hapo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Etaro, Mwl Mangire Stephano Mahombwe alisema kuwa S/M Etaro ilianzishwa Mwaka 1995, ina jumla ya WANAFUNZI 1,014. Mahitaji ni Vyumba 26 vya Madarasa, vilivyopo ni 10, upungufu ni Vyumba 16 vya Madarasa.
Mwalimu Mahombwe ameongezea kuwa,  Vyumba vipya Vinne (4) vinavyojengwa vikikamilika, Shule hiyo itakuwa BADO na UPUNGUFU wa Vyumba 12 vya Madarasa.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Etaro, Ndugu Sophia Charles alisema Serikali ya Kijiji cha Etaro inaendelea KUHAMASISHA WANANCHI wa Kijiji hicho na WADAU wa Maendeleo wakiwemo WAZALIWA wa Kijiji na Kata hiyo kuendelea KUCHANGIA UJENZI huo. HARAMBEE ya Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo itapigwa hivi karibuni.
Mtendaji wa Kijiji hicho alitaja VIFAA vya UJENZI vinavyohitajika kwa ujenzi unaondelea kwa wakati huu kuwa ni Mabati 54, Saruji Mifuko 280, Milango na Madirisha.
MICHANGO YA AWALI YA MBUNGE WA JIMBO
Kwenye Shule hiyo Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ALISHACHANGIA:
* Madawati 227
* Vitabu vingi vya Maktaba
* Saruji Mifuko 60
MICHANGO KUTOKA MFUKO WA JIMBO
* Mabati 244 ambayo yameezeka Vyumba 4 vya Madarasa na Ofisi moja (1) ya Walimu
Diwani wa Kata ya Etaro, Mhe Paul Charamba ameishukuru sana SERIKALI kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Musoma kwa usimamizi na ufuatiliaji mzuri wa Miradi ya Maendeleo ndani ya Kata ya Etaro.
Aidha, Diwani huyo amemshukuru sana Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo kwa MICHANGO yake na namna anavyowashirikisha Wananchi Jimboni humo katika kufanikisha utekelezaji wa Miradi yao ya Maendeleo, ikiwemo ya Kata ya Etaro.
KARIBUNI TUCHANGIE MIRADI YA ELIMU KIJIJINI ETARO

UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YA UBORESHAJI WA KIWANGO CHA ELIMU NDANI YA MKOA WA MARA

USOMBAJI WA MBAO za kutengenezea MEZA, VITI na KABATI za OFISI za Walimu zilizonunuliwa na Mbunge Prof Sospeter Muhongo.

WANANCHI wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kushirikiana na SERIKALI yao kutekeleza, kwa MAFANIKIO makubwa,  MAAZIMIO yaliyowekwa kwa ajili ya kuinua kiwango cha ELIMU Mkoani Mara. MAAZIMIO hayo ni:
(1) Uboreshaji wa MIUNDOMBINU ya ELIMU ya aina zote katika Shule za Msingi na Sekondari.
(2) Kudhibiti UTORO wa WANAFUNZI kwa kuweka utaratibu wa KISHERIA wa kuthibiti tatizo hilo.
(3) Utoaji wa huduma ya CHAKULA cha MCHANA Shuleni (Msingi na Sekondari) ni LAZIMA. WAZAZI na JAMII nzima ya Mkoa wa Mara watengenezewe utaratibu wa kuchangia CHAKULA katika SHULE zao.
(4) Kuimarisha MAHUSIANO ya WALIMU na JAMII na NIDHAMU ya WANAFUNZI.
(5) Kudhibiti MIMBA kwa WATOTO wa KIKE na UKATILI wa WANAFUNZI.
(6) Kuimarisha USHIRIKI na USHIRIKISHWAJI wa JAMII katika MAENDELEO ya SHULE.
MSIMAMIZI MKUU wa utekelezaji wa MAAZIMIO hayo ni Mkuu wa Mkoa, Ndugu Adam Malima. akisaidiwa na Wakuu wa Wilaya zote na Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri zote.
JIMBO la Musoma Vijijini LINABORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU kwenye SHULE ZAKE ZOTE ambazo ni:
* SHULE ZA MSINGI 114 (111 za Serikali na 3 za Binafsi), na SHULE SHIKIZI 11 (nyingine bado zinajengwa)
* SEKONDARI 22 (20 za Serikali/Kata na 2 za Binafsi) na 5 MPYA zinazojengwa na zitafunguliwa mwakani (Januari 2021).
SAMANI ZA DAN MAPIGANO MEMORIAL SECONDARY SCHOOL
Sekondari hii ni MPYA iliyofunguliwa Januari 2020. WANANCHI wa Kata ya Bugoji wanaendelea na ujenzi wa Vyumba VIPYA vya Madarasa, Maabara, Ofisi na Nyumba za Walimu.
SAMANI za Sekondari hiyo zinatengenezwa kwa MICHANGO kutoka kwa WANAVIJIJI na MBUNGE wao wa Jimbo.
UJENZI WA SHULE SHIKIZI
Shule SHIKIZI 11 kwenye VIJIJI 11 zinajengwa na kupanuliwa ziwe SHULE ZA MSINGI kamili zinazojitegemea. MALENGO MAKUU ya ujenzi huu ni kutokomeza MIRUNDIKANO Madarasani na UMBALI MREFU wa kutembea kwa Wanafunzi.
TAARIFA ya REDIO iliyoambatanishwa hapa inajitosheleza kwa maelezo.
SHUKRANI kwa VIKUNDI VYA PCI na WATAYARISHAJI wa Sherehe za SIKU YA WANAWAKE DUNIANI kwa kuendelea KUHAMASISHA na KUCHANGIA upatikanaji wa CHAKULA kwenye SHULE za MSINGI na SEKONDARI za Jimbo la Musoma Vijijini.
TATHMINI YA KWANZA ya UTEKELEZAJI wa MAAZIMIO hayo itafanyika tarehe 30 AGOSTI 2020 chini ya Uenyekiti wa Mkuu wa Mkoa wa Mara.

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI: MIKOPO ISIYOKUWA NA RIBA YAENDELEA KUTOLEWA

Halmashauri ya Wilaya ya Musoma IMEFANIKIWA, kwa Mwaka huu wa Fedha (2019/2020) kutoa MIKOPO MARA MBILI.

HALMASHAURI YA WILAYA YA MUSOMA, yenye Jimbo la Musoma Vijijini INAENDELEZA UTARATIBU WAKE wa kushiriki SHEREHE za SIKU YA WANAWAKE DUNIANI kwa kutoa MIKOPO isiyokuwa na RIBA kwa Vikundi vya WANAWAKE, VIJANA na WATU WENYE ULEMAVU.
MWAKA HUU (2020) Sherehe za SIKU YA WANAWAKE DUNIANI zilifanyika juzi Kijijini CHIRORWE, Kata ya SUGUTI.
MGENI RASMI alikuwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini. VIONGOZI wa Wilaya, ukiacha waliokuwa safarini kikazi, waliongozwa na Afisa Utawala wa Wilaya (DAS).
MIKOPO ISIYOKUWA NA RIBA
Halmashauri ya Wilaya ya Musoma IMEFANIKIWA, kwa Mwaka huu wa Fedha (2019/2020) kutoa MIKOPO MARA MBILI.
DISEMBA 2019, HALMASHAURI yetu ILITOA Mikopo ya Jumla ya Tsh MILIONI 116.5 kwenye VIKUNDI 23 vya Jimboni mwetu.
MACHI 2020, kwenye Sherehe za SIKU YA WANAWAKE DUNIANI iliyofanyika juzi Kijijini Chirorwe,  HALMASHAURI yetu ilitoa MIKOPO kama ifuatavyo:
*WANAWAKE, Vikundi 16, jumla ya Tsh MILIONI 98.0
* VIJANA, Vikundi 2, jumla ya Tsh MILIONI 11.0
* WATU WENYE ULEMAVU, Vikundi 3, jumla ya Tsh MILIONI 9.4
PLAU – ZAWADI YA PASAKA KUTOKA KWA MBUNGE WA JIMBO
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo ATATOA ZAWADI YA PLAU (Jembe la kukokotwa na ng’ombe/punda) kwenye SIKUKUU YA PASAKA ya Mwaka huu. VIKUNDI VYA PCI na VIKUNDI vyenye  Mikopo kutoka Halmashauri yetu  VINAVYOJISHUGHULISHA NA KILIMO ni miongoni mwa VIKUNDI vinavyotathminiwa kwa ajili ya kupewa ZAWADI YA PLAU kutoka kwa Mbunge wao.
MAFANIKIO YOTE haya na mengine mengi Jimboni mwetu ni MATUNDA ya UONGOZI mzuri wenye UBUNIFU mzuri wa DC wa Wilaya, Dr Vicent Naano Anney, DED wa Halmashauri, Ndugu John Kayombo na TIMU zao za Wafanyakazi makini.

HALMASHAURI YA WILAYA YA MUSOMA YASHIRIKIANA NA PCI KUSHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 

MGENI RASMI, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof Sospeter Muhongo ALICHANGIA Jumla ya MAGUNIA 11 ya mahindi na MAGUNIA 2.75 ya maharage.

SHEREHE ZA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI, ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, yenye Jimbo la Musoma Vijijini, zilifanyika jana, Ijumaa, tarehe 13 Machi 2020, kwenye Kijiji cha CHIRORWE, Kata ya SUGUTI. MGENI RASMI alikuwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo.
MATUKIO mawili (2)  MUHIMU sana yalifanyika Kijijini Chirorwe: (i) kuchangia CHAKULA  MASHULENI na (ii) HALMASHAURI yetu kugawa MIKOPO ISIYOKUWA NA RIBA kwa VIKUNDI vya WANAWAKE, VIJANA na Watu wenye ULEMAVU.
SHEREHE hizi hufanyika kila Mwaka kwa mzunguko ndani ya Kata za Halmashauri hii na  WARATIBU wake ni HALMASHAURI yenyewe kwa KUSHIRIKIANA na PCI-WE.
PROJECT CONCERN INTERNATIONAL (PCI) ni SHIRIKA la KIMATAIFA lenye MALENGO ya kuboresha AFYA, kukomesha NJAA, kupambana na ugumu wa MAISHA na kuendeleza  WANAWAKE na WASICHANA. PCI ilianzishwa Mwaka 1961 nchini Marekani (USA).
Project Concern International – Women Empowered (PCI-WE) ni MPANGO MAALUM wa PCI unaolenga KUHAMASISHA na KUWEZESHA WANAWAKE kiuchumi na kijamii kupitia UUNDAJI wa VIKUNDI vya KUWEKA na KUKOPA.
PCI-WE NDANI YA JIMBO LETU
* Inahudumia jumla ya Kata 14 ambazo ni: Bugwema, Bukima, Bukumi, Bulinga, Bwasi, Etaro, Ifulifu, Kiriba, Makojo, Mugango, Nyakatende, Nyegina, Rusoli na Suguti.
* Jumla ya VIKUNDI 169 vimeanzishwa ndani ya Kata hizo 14.
WAKUFUNZI WA PCI WAPEWA BAISKELI
* WAKUFUNZI 47 wa wa PCI ndani ya Jimbo letu wamepewa BAISKELI 47 ili kurahisisha USAFIRI wao kwenye maeneo yao ya kazi. MAKABIDHIANO ya BAISKELI hizo yalifanyika wakati wa SHEREHE za SIKU YA WANAWAKE DUNIANI yaliyofanyika jana Kijijini Chirorwe.
VIKUNDI VYA PCI VYAHAMASISHA WASHIRIKI WA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KUCHANGIA CHAKULA MASHULENI
* VIKUNDI vya PCI vya Kijiji cha Chirorwe, kwa kuungwa mkono na VIKUNDI vingine vya PCI, na WASHIRIKI wa Sherehe za SIKU YA WANAWAKE DUNIANI Kijijini Chirorwe, WALIFANIKIWA kuchangia na kukusanya Jumla ya TANI 5.6 za CHAKULA (mahindi na maharage) kwa ajili ya SHULE ZA MSINGI 2 za Kijiji hicho ambazo ni: S/M SOKOINE na S/M CHIRORWE. Chakula hicho kinatosha kutumiwa kwa muda wa Mwaka mmoja.
* Jumla ya TANI 2.7 nyingine za CHAKULA zilikusanywa kwenye hafla hiyo ikiwa ni mwanzo wa UCHANGIAJI wa CHAKULA kwa ajili ya SHULE NYINGINE ndani ya Kata hiyo. Idadi yake (mbali ya hizo za Kijiji cha Chirorwe) ni SEKONDARI 1 na SHULE ZA MSINGI 7.
MGENI RASMI, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof Sospeter Muhongo ALICHANGIA Jumla ya MAGUNIA 11 ya mahindi na MAGUNIA 2.75 ya maharage.
UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YA UBORESHAJI WA KIWANGO CHA ELIMU NDANI YA MKOA WA MARA
MAAZIMIO haya yameishasambazwa sana na anayeyahitaji anaweza kuyapata kutoka OFISI Za ELIMU za Halmashauri, Manispaa na Wilaya za Mkoa wa Mara.
MOJA YA MAAZIMIO hayo ni UTOAJI WA CHAKULA kwa WANAFUNZI wawapo masomoni kwenye SHULE ZOTE za Mkoa wa Mara (Msingi na Sekondari).
*Sherehe za SIKU YA WANAWAKE DUNIANI iliyofanyika Kijijini Chirorwe zimetumika KUTEKELEZA KWA VITENDO AZIMIO HILO (Chakula cha Wanafunzi) ndani ya Jimbo letu.

MAAZIMIO YA KONGAMANO (23.3.2020) LA UBORESHAJI WA KIWANGO CHA ELIMU NDANI YA MKOA WA MARA

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo akiwa kwenye KIKAO na WANANCHI wa Kijiji cha Butata (Kata ya Bukima) wanaojenga Vyumba Vipya 2 vya Madarasa ya S/M Butata iliyoanzishwa Mwaka 1942 na ina UPUNGUFU wa Vyumba 6 vya Madarasa. Mbunge huyo alichangia SARUJI MIFUKO 100.

(1) Uboreshaji wa MIUNDOMBINU ya ELIMU ya aina zote katika Shule za Msingi na Sekondari.
(2) Kuthibiti UTORO wa WANAFUNZI kwa kuweka utaratibu wa KISHERIA wa kuthibiti tatizo hilo.
(3) Utoaji wa huduma ya CHAKULA cha MCHANA Shuleni (Msingi na Sekondari) ni LAZIMA. WAZAZI na JAMII nzima ya Mkoa wa Mara watengenezewe utaratibu wa kuchangia CHAKULA katika SHULE zao.
(4) Kuimarisha MAHUSIANO ya WALIMU na JAMII na NIDHAMU ya WANAFUNZI.
(5) Kuthibiti MIMBA kwa WATOTO wa KIKE na UKATILI wa WANAFUNZI.
(6) Kuimarisha USHIRIKI na USHIRIKISHWAJI wa JAMII katika MAENDELEO ya SHULE.
*WARATIBU na WASIMAMIZI wa UTEKELEZAJI wa MAAZIMIO hayo sita (6) ni Wakuu wa Wilaya (DCs) na Wakurugenzi Watendaji (DEDs) chini ya UONGOZI wa Mkuu wa Mkoa (RC) wa Mara
* Tarehe ya KUTATHMINI maendeleo ya UTEKELEZAJI wa MAAZIMIO hayo ni 30 AGOSTI 2020 (Kongamano la pili)
* HALMASHAURI YA WILAYA YA MUSOMA na Jimbo lake la Musoma Vijijini ILIANZA MUDA mrefu kuboresha MIUNDOMBINU ya ELIMU kwa MALENGO ya kuinua UBORA wa ELIMU kwenye SHULE zake za MSINGI (111 za Serikali & 3 za Binafsi) na SEKONDARI (20 za Serikali & 2 za Binafsi). Shule SHIKIZI 11 zinajengwa kwa kiwango kizuri.
* CHAKULA cha MCHANA Shuleni (Msingi & Sekondari) – shule chache zinatoa CHAKULA kwa Wanafunzi wawapo masomoni. Viongozi wa ngazi mbalimbali wanaendelea kuwashawishi WAZAZI wakubali kuchangia CHAKULA cha WANAFUNZI wawapo masomoni Shuleni.
OMBI
Tafadhali ungana na WANANCHI wa Jimbo la Musoma Vijijini KUTEKELEZA MAAZIMIO ya UBORESHAJI wa kiwango cha ELIMU kwenye SHULE zetu.
MATUMAINI YAPO
Hatimae MWANGA unaanza kuchomoza. Mwaka jana (2019) HALMASHAURI YETU imekuwa ya KWANZA Mkoani mwetu kwenye MITIHANI YA DARASA LA NNE. Tuongeze juhudi kwani ni muhimu kushindana na Halmashauri na WILAYA zote za nchini mwetu. TUTAFANIKIWA!

WATOTO WADOGO WA KIJIJI CHA BURAGA KUEPUKA KUTEMBEA KILOMITA 4-5 KWENDA MASOMONI

Washiriki wa KIKAO cha leo cha WAKAZI wa Kitongoji cha Mwaloni, Kijijini Buraga, na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo.

KIJIJI CHA BURAGA, Kata ya Bukumi kina VITONGOJI 6 ambavyo vinahudumiwa na SHULE MOJA YA MSINGI (S/M Buraga) iliyo kwenye Kitongoji cha Musokwa.
WATOTO wenye umri kati ya miaka 6 na 15 wa KITONGOJI cha MWALONI wanalazamika kutembea umbali wa kilomita 4-5 kwenda MASOMONI kwenye S/M BURAGA.
WAKAZI wa KITONGOJI cha MWALONI wameamua kuanzisha SHULE YA AWALI chini ya MTI ndani ya Kitongoji hicho. Wakati huo huo WAKAZI hao hao WAMEAMUA KUJENGA SHULE SHIKIZI karibu na Darasa hilo la chini ya MTI.
Leo, Jumanne, 10 March 2020, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo amefanya ZIARA KIJIJINI BURAGA kukagua MIRADI YA MAENDELEO ukiwemo MRADI WA UJENZI WA SHULE SHIKIZI YA BURAGA MWALONI.
Ndugu Nyajoge Chirya, Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi ametoa RIPOTI ya ujenzi wa Shule Shikizi hiyo na kusema ifikapo tarehe 15 March 2020, UJENZI uliosimama kwa muda, utaendelea kwa KASI KUBWA zaidi.
MICHANGO YA UJENZI WA SHULE SHIKIZI BURAGA MWALONI
* NGUVUKAZI na FEDHA Taslimu vinachangwa na Wakazi wa Kitongoji cha Mwaloni.
* MDAU wa Maendeleo, rafiki ya Mbunge wa Jimbo (Prof Sospeter Muhongo) alichangia SARUJI MIFUKO 5.
* MFUKO wa Jimbo la Musoma Vijijini umeishachangia SARUJI MIFUKO 50
* Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo atachangia SARUJI MIFUKO 100 kuanzia tarehe 15 March 2020 (ujenzi uliosimama utakapoendelea).
SHULE SHIKIZI HIYO itafunguliwa rasmi Januari 2021. Huo ndio UAMUZI wa Wakazi wa Kitongoji cha Mwaloni, Kijijini Buraga.
OMBI KUTOKA KWA WANANCHI WA KIJIJI CHA BURAGA, KATA YA BUKUMI
* Wananchi wa Kijiji cha Buraga wanaomba WAZALIWA WA KIJIJI hicho na Kata ya Bukumi kwa ujumla WAANZE KUCHANGIA MIRADI ya MAENDELEO ya nyumbani kwao.
JIMBO la Musoma Vijijini lina Jumla ya Vitongoji 374 na Vijiji 68. JIMBO hili lina Jumla ya SHULE za MSINGI 111 za Serikali na 3 za Binafsi. SHULE SHIKIZI 11 zinajengwa na nyingine tayari zimefunguliwa.

WANAVIJIJI WAAMUA SEKONDARI MPYA INAYOJENGWA IWE NA MIUNDOMBINU YA AWALI IFIKAPO TAREHE 1 MEI 2020

KIKAO cha Jumatatu, 9 March 2020 cha WANAVIJIJI na Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa Seka Secondary School.

WANAVIJIJI wa Kata ya Nyamrandirira WAMEAMUA ujenzi wa SEKONDARI MPYA ya KATA yao iwe na MIUNDOMBINU ya kuchukua WANAFUNZI wa Kidato cha Kwanza ifikapo tarehe 1 Mai 2020.
KATA ya NYAMRANDIRIRA ina Vijiji vitano (5) ambavyo ni Chumwi, Kaboni, Kasoma, Mikuyu na Seka. Vijiji vyote 5 vinahudumiwa na Sekondari moja (Kasoma Secondary School) ambayo chimbuko lake ni Kasoma Middle School iliyojengwa Mwaka 1956.
WANAFUNZI 204 wa Kidato cha Kwanza (2020) wa Kasoma Sekondari WAMERUNDIKANA ndani ya Vyumba 2 vya Madarasa. Maoteo ya Mwakani (2021) ni kuwa na WANAFUNZI 318 wa Kidato cha Kwanza kutoka Vijiji vitano (5) hivyo na vitahitajika Vyumba   8 vya Madarasa.
MIRUNDIKANO MADARASANI NA UMBALI MREFU
Mbali ya MIRUNDIKANO madarasani bado lipo tatizo la umbali mrefu wa kutembea kwa baadhi ya WANAFUNZI na WALIMU. Kwa hiyo, SULUHISHO ni KUJENGA Sekondari ya pili ndani ya Kata hiyo.
SEKA SECONDARY SCHOOL
UAMUZI ulifanywa na WANANCHI wa Vijiji 5 vyote kwamba SEKONDARI MPYA ijengwe Kijijini Seka na iitwe Seka Secondary School.
IFIKAPO TAREHE 1 MAI 2020 Sekondari Mpya hiyo inayojengwa Kijijini Seka itakuwa na MIUNDOMBINU ifuatayo: (i) Vyumba vipya 8 vya Madarasa, (ii) Vyoo matundu 10, yaani 4 ya Wasichana, 4 ya Wavulana na 2 ya Walimu. Ujenzi utaendelea wa Maabara, Jengo la Utawala, Nyumba za Walimu, Vyumba vya Madarasa na Vyoo vingine zaidi.
MICHANGO YA UJENZI
* WANAVIJIJI wanachangia NGUVUKAZI na FEDHA TASLIMU
* WADAU wakiwemo Wawekezaji wameombwa waanze kuchangia
* Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ameanza kuchangia SARUJI MIFUKO 250 (kila Kijiji kupewa Mifuko 50).
* WAZALIWA wa Kata ya Nyamrandirira na RAFIKI zao WANAOMBWA waanze kuchangia ujenzi huu.
JIMBO la Musoma Vijijini lina Kata 21 na Vijiji 68. Jimbo hili lina Jumla ya Sekondari 20 za Kata/Serikali na 2 za Binafsi. Sekondari Mpya 5 zinajengwa kwa MALENGO ya kufunguliwa Mwakani (Januari 2021).

WADI YA MAMA NA MTOTO YACHANGIWA SARUJI MIFUKO 200

KIKAO CHA WANAWAKE na MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, kilichofanyika kwenye ZAHANATI ya NYEGINA inayojenga WADI ya MAMA na MTOTO.

ZAHANATI YAKIJIJI CHA NYEGINA inapanuliwa kwa kujenga WADI YA MAMA na MTOTO na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo amechangia SARUJI MIFUKO 200.
UJENZI NA UBORESHAJI WA Miundombinu ya HUDUMA za AFYA Jimboni mwetu UNATEKELEZWA kwa USHIRIKIANO mkubwa na mzuri wa WANANCHI na SERIKALI yao.
HUDUMA ZA AFYA JIMBONI
* JUMLA YA ZAHANATI zinazotoa HUDUMA ni: 24 za Serikali na 4 za Binafsi.
* JUMLA YA VITUO VYA AFYA  vinavyotoa HUDUMA ni: 2 (Murangi na Mugango)
UJENZI NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA AFYA JIMBONI
* HOSPITAL ya Wilaya inajengwa kwenye Kitongoji cha Kwikonero, Kijijini Suguti. SERIKALI imechangia Tsh Bilioni 1.5. WANAVIJIJI na MBUNGE wa Jimbo wanachangia ujenzi huu.
* ZAHANATI MPYA 14 zinajengwa kwenye Vijiji 14. Serikali imechangia ujenzi wa Maboma ya Zahanati za Vijiji vya Chirorwe na Maneke.
* ZAHANATI ya Kijiji cha Masinono inapanuliwa iwe KITUO CHA AFYA. Serikali imechangia Tsh Milioni 400. WANAVIJIJI na MBUNGE wa Jimbo watachangia ujenzi huu.
* ZAHANATI YA BUKIMA inajenga WADI YA MAMA na MTOTO na Mbunge wa Jimbo alichangia SARUJI MIFUKO 100 tarehe 13 JUNE 2018. Ujenzi unaenda kwa kasi ndogo.
MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI (8 March 2020) – TUBORESHE HUDUMA ZA AFYA KWA MAMA NA MTOTO, NA KWA FAMILIA NZIMA.

MBUNGE WA JIMBO AENDELEA KUKAGUA UJENZI NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU KWENYE SEKONDARI ZA KATA

Ukaguzi wa MIUNDOMBINU YA ELIMU ulioufanywa na Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo kwenye Sekondari ya Kata ya Kiriba, KIRIBA SECONDARY SCHOOL.

KIRIBA SEKONDARI ilianza kutoa ELIMU YA SEKONDARI Mwaka 2006. Kwa sasa ina Wanafunzi 672 na Walimu 21. Kuna UPUNGUFU wa Vyumba 2 vya Madarasa.
MATOKEO YA FORM IV YA MASOMO YA SAYANSI (2019)
Mwalimu Mkuu, Mwl Robertious Wanjara Bwire amesema kwamba MATOKEO YA MITIHANI YA MASOMO YA SAYANSI ya Mwaka jana (2019) ni MABAYA SANA. Fizikia (Physics) ilikuwa na Watahiniwa 4, mmoja (1) pekee alipata D. Kemia (Chemistry) ilikuwa na Watahiniwa 12, watatu (3) pekee walipata C. Biolojia (Biology) watahiniwa 99, waliopata B ni watatu (3) tu. Baadhi ya SABABU za msingi za MATOKEO MABAYA HAYO ni: (i) KUTOKUWEPO MAABARA yenye Miundombinu ya kujifunzia sayansi kwa vitendo (PRACTICALS)  na (ii) MIRUNDIKANO ya Wanafunzi madarasani.
WANANCHI NA SERIKALI WASHIRIKIANA KUTATUA MATATIZO HAYO
*MIRUNDIKANO Madarasani
Wananchi kutoka Vijiji 3 (Bwai Kwitururu, Bwai Kumusoma na Kiriba) vya Kata ya Kiriba WAMEKUBALIANA kuchangia NGUVUKAZI na FEDHA kujenga Vyumba 3 Vipya vya Madarasa. Kila Kijiji kinajenga jengo lake na kabla ya tarehe 30 March 2020, ujenzi huo uwe umekamilika na kutatua tatizo la MIRUNDIKANO madarasani.
SERIKALI Ilishachangia Tsh 37.5 Milioni kwa ajili ya ujenzi  na uboreshaji wa awali wa Vyumba vya Madarasa na ununuzi wa madawati na viti.
Jana, Jumatano, tarehe 4.3.2020, Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo alikagua ujenzi mpya huo wa Vyumba 3 vipya na KUCHANGIA Jumla ya SARUJI MIFUKO 150 (kila Kijiji kimechangiwa Mifuko 50).
*MAABARA BORA YA KI-SAYANSI
Kiriba Sekondari inavyo Vyumba 3 vya MAABARA ya Fizikia, Kemia na Biolojia LAKINI MIUNDOMBINU ya NDANI ni hafifu sana au haipo. Kwa hiyo, Mbunge wa Jimbo AMEWASHAWISHI Wananchi wa Kata ya Kiriba KUANZA ujenzi wa KUBORESHA MAABARA 3 hizo.
SARUJI MIFUKO 60 inahitajika kujenga MEZA za TOFALI/BLOCK ndani ya Maabara hizi tatu (3). Mdau wa Maendeleo ya Kiriba amechangia SARUJI MIFUKO 35 na Mbunge wa Jimbo amechangia SARUJI MIFUKO 25. Uboreshaji wa Miundombinu ya ndani ya Maabara tatu (3) za Sekondari hii umepangwa UKAMILIKE kabla ya tarehe 30 April 2020.
WAZALIWA wa Kata ya KIRIBA na WALIOSOMA Kiriba Sekondari wanaombwa WAJITOKEZE KUCHANGIA UBORESHAJI wa miundombinu ya ndani ya MAABARA hizi tatu
Mawasiliano ya MICHANGO
Headmaster:
0787 015 489
Mtendaji Kata (WEO):
0758 023 124
0629 537 798
SAYANSI NI CHIMBUKO LA UCHUMI WA KISASA NA USTAWI WA JAMII ZOTE DUNIANI KOTE

SEKONDARI MPYA JIMBONI KUONGEZA KASI KWENYE UJENZI WA MIUNDOMBINU MIPYA 

VIKAO vya Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo na WANAVIJIJI wa Kata ya Bugoji

DAN MAPIGANO MEMORIAL SECONDARY SCHOOL ya Kata ya Bugoji yenye Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza na iliyofunguliwa Mwaka huu (2020) ITAHITAJI VYUMBA VIPYA 5 VYA MADARASA kwa ajili ya Kidato cha Kwanza cha Mwakani (2021, Maoteo ni Wanafunzi 218). Vipo Vyumba vipya 2 vilivyokamilishwa ujenzi
BUSAMBARA SECONDARY SCHOOL ya Kata ya Busambara yenye Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza na iliyofunguliwa Mwaka huu (2020) ITAHITAJI VYUMBA VIPYA 7 VYA MADARASA kwa ajili ya Kidato cha Kwanza cha Mwakani (2021, Maoteo ni Wanafunzi 270). Lipo Boma la Vyumba 2 vya Madarasa linalojengwa.
UAMUZI WA WANANCHI WA KATA YA BUGOJI
(Dan Mapigano Memorial Secondary School)
* Ujenzi wa Maabara,  Vyoo Matundu 10, Nyumba ya Walimu (two in one) UKAMILIKE kabla ya tarehe 30 JULAI 2020.
* Ujenzi MPYA wa Vyumba 6 vya Madarasa na Nyumba ya pili ya Walimu (two in one) UKAMILIKE kabla ya tarehe 30 AGOSTI 2020.
* FAMILIA MAPIGANO imehudhuria Kikao cha leo (6.3.2020) cha Kijijini Bugoji na  kuhaidi KUJENGA CHUMBA 1 cha Darasa. Baadae watachangia COMPUTERS. Ujumbe wa Familia Mapigano uliongozwa na Ndugu Jarled Lisso.
* Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo aliyeitisha Kikao hicho cha Wananchi wa Kata ya Bugoji. amechangia MBAO za kutengeneza MEZA 6 na VITI 6 (Tsh 2 Million)
UAMUZI WA WANANCHI WA KATA YA BUSAMBARA
(Busambara Secondary School)
* Ifikapo tarehe 30 APRIL 2020 Kijiji cha Maneke kikamilishe ujenzi wa Boma la Vyumba 2 vya Madarasa.
* Ifikapo tarehe 30 APRIL 2020, Vijiji vya Mwiringo na Kwikuba, kila kimoja  kikamilishe ujenzi wa Vyumba vipya 2 vya Madarasa.
* Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo aliyeitisha Kikao cha leo (6.3.2020) Kijijini Kwikuba amechangia RANGI za KUPAKA Ofisi ya Walimu, na Vyoo vya Wanafunzi na Walimu.
WANAVIJIJI WA KATA ZA BUSAMBARA NA BUGOJI WANAWAOMBA WAZALIWA WA KATA HIZO WAUNGANE NAO KWENYE UJENZI WA SEKONDARI MPYA HIZO

ZAHANATI YA KIJIJI CHA MASINONO KUPANULIWA NA KUWA KITUO CHA AFYA CHA KATA YA BUGWEMA

MKUTANO wa WANANCHI wa Kata ya Bugwema na MBUNGE wao, Prof Sospeter Muhongo kwenye eneo la (ujenzi) Zahanati ya Masinono, Kata ya Bugwema.

SERIKALI imetoa Tsh Milioni 400 kupanua ZAHANATI ya Kijiji cha Masinono na kuwa KITUO CHA AFYA cha Kata ya Bugwema.
WANANCHI na VONGOZI wa Kata ya Bugwena na Halmashauri yao WANAISHUKURU sana SERIKALI yao na WAMEHAIDI kushirikiana nayo kukamilisha MRADI huu.
Jana, Jumatatu, tarehe 2.3.2020, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, ALITEMBELEA Zahanati ya Masinono na KUONGEA na WANANCHI kuhusu UPANUAJI wa Zahanati hiyo.
Diwani wa Kata ya Bugwema, Mhe Ernest Maghembe amesema, MAJENGO MAPYA yatakayojengwa ni: (i) Wadi la Mama & Mtoto, (ii) Jengo la Upasuaji (theatre) (iii) Maabara, (iv) Jengo la kufulia nguo, (v) Kichomea taka na (vi) Nyumba ya kutunza maiti (mortuary). Mindombinu mizuri ya Maji Safi na Taka itawekwa.
MICHANGO YA WANANCHI
Kata ya Bugwema inaundwa na VIJIJI 4 vya Bugwema, Kinyang’erere,  Masinono na Muhoji.
* NGUVUKAZI – kila Kijiji kimepangiwa siku za kusomba mawe, mchanga, maji, n.k.
* Kila Kijiji kitachangia Tsh 33, 437, 500 ili kupata Jumla ya Tsh 133,750,000 kwa ajili ya ujenzi huu.
MICHANGO YA MBUNGE WA JIMBO
* Prof Sospeter Muhongo, Mbunge wa Jimbo ametoa AHADI ya KUCHANGIA UJENZI huo Mwezi ujao (April, 2020) atakaporudi hapo KUKAGUA ujenzi wa KITUO hicho cha AFYA.
Mbunge huyo amewaeleza Wananchi wa Kata ya Bugwema kwamba alichangia SARUJI MIFUKO 400 wakati wa UBORESHAJI wa Miundombinu ya  KITUO cha AFYA MURANGI na kukipatia Gari la Wagonjwa  (Ambulance) la kisasa sana. Vilevile, alichangia SARUJI MIFUKO 400 wakati wa upanuaji wa Zahanati ya Mugango kuwa KITUO cha AFYA MUGANGO. Na hapa napo, Mbunge huyo alitoa Gari la Wagonjwa (Ambulance).
ZAHANATI ya Masinono inayopanuliwa kuwa Kituo cha Afya tayari Mbunge wa Jimbo aliishaipatia Gari la Wagonjwa (Ambulance).
MIUNDOMBINU YA HUDUMA ZA AFYA NA MAGARI YA WAGONJWA JIMBONI MWETU.
* HOSPITAL ya Wilaya: inajengwa kwenye Kitongoji cha Kwikonero, Kijiji cha Suguti.
* VITUO VYA AFYA vinavyotoa huduma ni viwili (2): Kata za Murangi na Mugango
* VITUO VYA AFYA vinavyojengwa ni viwili (2). Kata za Bugwema na Nyambono
* ZAHANATI zinazotoa huduma: 24 za Serikali na 4 za Binafsi
* ZAHANATI MPYA zinazojengwa ni kumi na tatu (13).
* MAGARI YA WAGONJWA (Ambulances) ni matano (5). Yote yalitolewa na Mbunge wa Jimbo.

SHEREHE ZA UZINDUZI WA BUSAMBARA SECONDARY SCHOOL ZAFANA SANA

Wananchi na Mbunge wa Jimbo katika Sherehe za Uzinduzi wa Busambara Secondary School

Jumamosi, 29.2.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
HATIMAE Kata ya Busambara iliyokuwa haina Sekondari yake IMEFANIKIWA KUJENGA na tayari Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza wameanza MASOMO yao Shuleni hapo.
KATA MOJA tu kati ya Kata 21 za Jimbo la Musoma Vijijini ndiyo haina Sekondari yake. Hata hivyo, Kata hiyo (IFULIFU) inajenga Sekondari mbili (Nyasaungu & Ifulifu Secondary Schools) kwa wakati mmoja na zitakuwa tayari kuchukua Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza ifikapo Juni 2020.
Kwa sasa, Jimbo lina Sekondari 20 za Kata/Serikali na 2 za Binafsi. Sekondari Mpya zinazojengwa ni 5: (i) Kigera (Kata ya Nyakatende), (ii) Nyasaungu (Kata ya Ifulifu), (iii) Ifulifu (Kata ya Ifulifu inajengwa Kijijini Kabegi), (iv) Bukwaya (Kata ya Nyegina) na (v) Seka (Kata ya Nyamrandirira). Kata (3) nyingine nazo zimepanga kutatua matatizo ya umbali mrefu na mirundikano madarasani kwa kujenga Sekondari mpya ndani ya Kata zao.
Leo, Jumamosi, tarehe 29.2.2020 JIWE LA MSINGI na UZINDUZI wa Busambara Secondary School umefanyika Kijijini Kwikuba na MGENI RASMI alikuwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo. Hii SEKONDARI MPYA ni ya Vijiji 3 (Kwikuba, Maneke na Mwiringo).
MAOTEO ni kwamba mwakani (2021) takribani WANAFUNZI 270 wanategemewa kuanza Kidato cha Kwanza Shuleni hapo. Kwa hiyo ujenzi kwa kasi kubwa ni muhimu.
Wananchi na Mbunge wa Jimbo watafanya KIKAO cha MUENDELEZO WA UJENZI wa Miundombinu ya Sekondari hii tarehe 6 Machi 2020, Saa 10 Alasiri, Shuleni hapo.

KIRIBA SEKONDARI – UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MADARASA KUTATULIWA KWA USHIRIKIANO WA  WANANCHI NA SERIKALI

Ujenzi wa Vyumba VIPYA 3 vya KIRIBA SECONDARY SCHOOL ya Kata ya Kiriba

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
Mkuu wa Kiriba Sekondari, Mwalimu Robertious Wanjara Bwire amesema kwamba Sekondari hiyo ilianzishwa Mwaka 2006 na ina jumla ya WANAFUNZI 672 na WALIMU 21. Mahitaji ya Vyumba vya Madarasa ni 18, vilivyopo ni 16 kwa hiyo UPUNGUFU ni VYUMBA 2.
WANANCHI wa Kata ya Kiriba inayoundwa na Vijiji vitatatu (3) vya Bwai Kumusoma, Bwai Kwitururu na Kiriba wameanza ujenzi wa Vyumba VIPYA vitatu (3) vya Madarasa ili KUTOKOMEZA KABISA tatizo la MIRUNDIKANO ya WANAFUNZI madarasani.
Akizungumza na Msaidizi wa Mbunge katika eneo la ujezi shuleni hapo, Mtendaji Kata (WEO) ya Kiriba, Ndugu Pendo Isack amesema ujenzi wa VYUMBA VIPYA hivyo unaendeshwa na Vijiji vyote vitatu ambapo kila Kijiji kinajenga Chumba kimoja (1) cha Darasa.
Mtendaji Kata huyo ameongezea kuwa, ujenzi huo unatarajiwa kukamilika mwezi ujao (30 March 2020) ili kuharakisha matumizi yake na KUONDOA MIRUNDIKANO ya Wanafunzi madarasani
Aidha Mkuu wa Sekondari hiyo AMEISHUKURU sana SERIKALI iliyochangia Tsh 37.5 Milioni kwa ujenzi huo (na ununuzi wa madawati na viti). Vilevile, anawashukuru sana Wanavijiji wa Kata ya Kiriba, Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri na Mbunge wa Jimbo kwa USHIRIKIANO wao na MICHANGO yao inayokusudia kuondoa kabisa kero ya MISONGAMANO ya Wanafunzi madarasani.
Kwenye ujenzi huu wa Vyumba Vipya 3 vya Madarasa, Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo atachangia Jumla ya SARUJI MIFUKO 150, yaani kila Kijiji kitakabidhiwa Saruji Mifuko 50. Makabidhiano hayo yatafanyika tarehe 4.3.2020, siku ambayo Mbunge huyo atakagua ujenzi wa Maabara na Vyumba VIPYA vya Madarasa Shuleni hapo.
MICHANGO YA AWALI YA MBUNGE WA JIMBO ni:
(i) Vitabu vingi vya Maktaba
(ii) Saruji Mifuko 100
(iii) Mabati 54
(iv) Rangi Ndoo 20
WAZALIWA WA KATA YA KIRIBA wanaombwa waendelee KUCHANGIA UJENZI NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA KIRIBA SECONDARY SCHOOL

MADARASA CHINI YA MITI LAZIMA YATOWEKE – KIJIJI CHA BWASI KIMEAMUA

WANANCHI wa VITONGOJI 5 vyote (Buruma, Kamtimba, Masonge na Mtakuja na Rugongo) vya KIJIJI CHA BWASI wakiwa kwenye UJENZI wa Vyumba Vipya vya Madarasa ya S/M Bwasi B.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini lenye VITONGOJI 374,  VIJIJI 68 na KATA 21 lina Jumla ya SHULE za MSINGI 111 za SERIKALI, 3 za BINAFSI na SHULE SHIKIZA 11 zinajengwa na nyingine tayari zimekamilika na kuanza kutumiwa.
TATIZO kubwa kwenye Shule za Msingi ni UKOSEFU na UPUNGUFU wa Vyumba vya MADARASA kunakosababisha MIRUNDIKANO Madarasani na kuwepo kwa MADARASA CHINI YA MITI. Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini WAMEDHAMIRIA KUTATUA TATIZO la kuwepo kwa Madarasa CHINI YA MITI.
Kijiji cha Bwasi kilichopo Kata ya Bwasi chenye VITONGOJI 5 na KAYA 450 wameanza ujenzi wa  Vyumba vipya vya Madarasa kutokana na upungufu mkubwa wa Madarasa unaozikabili S/M Bwasi (ilifunguliwa Mwaka 1952) na S/M Bwasi B (ilifunguliwa Mwaka 2015)
Mwalimu Mkuu wa S/M Bwasi B, Mwl Masillingi Maira amesema shule yake ina jumla ya Wanafunzi 508 (uandikishaji bado unaendelea),  wana Vyumba 4 vya Madarasa na UPUNGUFU wa Vyumba 8 vya Madarasa. Mwalimu Mkuu huyo ameeleza kwamba Darasa lenye WANAFUNZI WENGI linao 136 kwenye Chumba kimoja na lisilokuwa na MRUNDIKANO darasani lina Wanafunzi 34. Kwa hiyo, Madarasa 4 YANASOMEA NJE, CHINI YA MITI.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Bwasi, Ndugu Mbeli Mkama Majinge ameeleza  kuwa walifanya KIKAO na kuafikiana kwamba KILA KITONGOJI kijenga CHUMBA KIMOJA kwa kutumia MICHANGO YA WANAVIJIJI ya kila Kitongoji. Kwa mfano, Kitongoji cha Mtakuja kila KAYA inachangia Tsh 58,000, hatua kwa hatua, hadi ukamilishaji wa ujenzi wao.
Mtendaji Kata, Ndugu Mashaka Kagere amesema WANAVIJIJI WAMEHASIKA kujenga Vyumba vipya 5 vya Madarasa na Ofisi 3 za Walimu. Ndugu Kagera amesema VYUMBA 4  vya Madarasa VITAKAMILIKA kabla ya tarehe 29.2.2020 na MAJENGO mengine yatakamilishwa ifikapo tarehe 30.5.2020
VIONGOZI wa Kata ya Bwasi WANAMSHUKURU SANA Mkuu wa Wilaya,  Dr Vicent Naano Anney kwa KUHAMASISHA Wananchi wa Kata hiyo (hasa Vijiji vya Bugunda na Bwasi) KUANZA UJENZI wa Vyumba Vipya vya Madarasa. Ujenzi ULIKUWA UMEKWAMA kwa muda mrefu.
Aidha Diwani wa Kata hiyo, Mhe Masatu Nyaonge anatoa shukrani za dhati kwa  Mkuu wa Wilaya na Mbunge wa Jimbo kwa KUENDELEA KUHAMASISHA WANAVIJIJI kwenye masuala la MAENDELEO kwenye Kata yao likiwemo hili la UJENZI wa Vyumba Vipya vya Madarasa na KUACHANA na MADARASA CHINI YA MITI.
Katika UBORESHAJI wa ELIMU kwenye Kijiji cha Bwasi, Mbunge wa Jimbo, Profesa Muhongo aliwahi kuchangia vifuatavyo:
S/M Bwasi
*Madawati 39
*Vitabu vingi vya Maktaba
S/M  Bwasi B
*Madawati 36
*Saruji  Mifuko 70
*Vitabu vingi vya Maktaba
WAZALIWA WA KATA YA BWASI, WATU WALIOSOMA S/M BWASI na BWASI Sekondari WANAOMBWA KUCHANGIA UJENZI wa KUTOKOMEZA MADARASA CHINI YA MITI! KARIBU UCHANGIE.

KATA YENYE VIJIJI 4 YAAMUA KUJENGA SEKONDARI YA PILI

Viongozi wa Serikali ya Vijiji vya Kigera na Kakisheri, na baadhi ya Wananchi wakiendelea na kazi za ujenzi wa KIGERA SEKONDARI.

Jumatatu, 17.2.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
KATA ya NYAKATENDE ina Vijiji 4, ambavyo ni: Kamguruki, Kakisheri, Kigera na Nyakatende.
NYAKATENDE SEKONDARI iliyoanzishwa Mwaka 2006 inahudumia Wanafunzi wa kutoka Kata 2 za Nyakatende (Vijiji 4)  na Ifulifu (Vijiji 3). Sekondari hii ina jumla ya WANAFUNZI 573 na WALIMU 23.
Mwalimu Mkuu wa Nyaketende Sekondari, Mwalimu Halima Selemani Yusufu amesema kwamba DARASA lenye WANAFUNZI WENGI linao 68 na lenye wachache linao 55.
Mtendaji wa Kata (WEO) Ndugu Martha Omahe Gagiri ameeleza kwamba wapo Wanafunzi wanaotembea umbali usiopungua kilomita 10 kwenda  masomoni kwenye Sekondari hiyo (kurudi nyumbani ni umbali huo huo)!
UJENZI WA SEKONDARI YA PILI
Kutokana na MATATIZO ya UMBALI na MISONGAMANO MADARASANI, Vijiji 2 vya Kigera na Kakisheri VIMEAMUA kujenga Sekondari yao kwenye Kitongoji cha Kati, Kijijini Kigera.
WAZALIWA wa Vijiji 2 hivi ambao kwa sasa wanaishi na kufanya kazi na biashara NJE ya Vijiji hivi (nje ya kwao) wameanzisha UMOJA wao wenye lengo la kusaidiana na ndugu na jamaa zao VIJIJINI kujenga SEKONDARI hii. Mwenyekiti ni Ndugu Malele Eugen Kisha na Katibu ni Ndugu Joseph Mnibhi.
HATUA NZURI IMEFIKIWA
* BOMA la Vyumba viwili (2) vya Madarasa limekamilika
* Jengo la Utawala linakaribia kukamilishwa, liko kwenye renta.
* Jengo la Maabara tatu (3) linakaribia kukamilishwa
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kigera, Ndugu Magafu Katura amesema ujenzi ulioelezwa hapo juu utakamilika kabla ya mwisho wa Mwezi huu (Februari 2020).
Mwenyekiti huyo amesema kwamba baada ya kukamilika kwa MAJENGO hayo, ujenzi unaofuata ni wa: Vyoo Matundu manne (4) ya Wasichana, manne (4) ya Wavulana na mawili (2) ya Walimu, na Nyumba ya kuishi Mwalimu Mkuu.
Diwani wa Kata ya Nyakatende, Mhe Rufumbo Rufumbo, kwa niaba ya WANANCHI wa Vijiji vya Kigera na Kakisheri ANATOA SHUKRANI nyingi kwa WADAU wote wa Maendeleo wanaochangia ujenzi wa KIGERA SEKONDARI.
MICHANGO ILIYOKWISHATOLEWA
* NGUVUKAZI za Wakazi wa Vijiji vya Kigera na Kakisheri (kusomba maji, mchanga, mawe na kokoto)
* Michango ya awali: Shilingi 2,000 kwa kila mkazi (vijiji 2) mwenye umri kati ya miaka 18 na 59.
* WAZALIWA wa Vijiji  2 wanalipa MAFUNDI na fedha nyingine zinanunua vifaa vya ujenzi.
* SARUJI MIFUKO 100 ya Mbunge wa Jimbo, Profesa Muhongo.
* SARUJI MIFUKO 100 ya Mfuko wa Jimbo
TUJIKUMBUSHE MICHANGO YA MBUNGE WA JIMBO KWA SHULE ZA MISINGI ZA VIJIJI HIVI VIWILI
S/M KIGERA
(i) Madawati 43
(ii) Vitabu vingi vya Maktaba
(iii) Saruji Mifuko 60
S/M KIGERA B
(i) Madawati 70
(ii) Vitabu vingi vya Maktaba
(iii) Saruji Mifuko 60
S/M KAMBARAGE
(Kijiji cha Kakisheri)
(i) Madawati 99
(ii) Vitabu vingi vya Maktaba
(iii) Mabati 54
(iv) Saruji Mifuko 60
(v) Saruji Mifuko 100 (Mfuko wa Jimbo)
(vi) Mbao 100 (rafiki ya Mbunge wa Jimbo)
KARIBU TUCHANGIE UJENZI WA KIGERA SEKONDARI
(Kata jirani ya IFULIFU imeanza kujenga Sekondari zake 2 kwa ajili ya Wanafunzi wa Sekondari wa Kata hiyo).

WANAVIJIJI WADHAMIRIA KUACHANA NA JEMBE LA MKONO

baadhi ya Wanachama wa KIKUNDI cha KILIMO cha Kijijini Butata, Kata ya Bukima, kiitwacho, “FUKUZA NJAA”, kikiwa kazini kikitumia PLAU badala ya JEMBE la MKONO.

Na: Veredian Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
VIKUNDI VYA KILIMO 20 kutoka VIJIJI 20 vimeanza kurahisisha KILIMO chao kwa kutumia PLAU (jembe linalokokotwa na ng’ombe) badala ya kutumia JEMBE LA MKONO.
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo alitoa ZAWADI YA MWAKA MPYA (2020) ya PLAU 20 kwa VIKUNDI hivyo 20.
Ndugu Makuke Mnubi ni Mkulima wa Kijiji cha Chimati, Kata ya Makojo ambae KIKUNDI chake kilipewa zawadi ya PLAU moja. Kwa muda mfupi sana na bila kutumia nguvu nyingi waliweza kulima EKARI 6 kwa kutumia PLAU hiyo na wamepanda MPUNGA  na   MAHINDI.
Ndugu George Tole ni mkulima wa Kijiji cha Butata, Kata ya Bukima na yuko kwenye KIKUNDI CHA FUKUZA NJAA. Mkulima huyo amesema WANAVIJIJI wamevutiwa sana na  KILIMO cha kutumia PLAU na wengine  wameanza kutumia  PUNDA wao (mbali ya ng’ombe) kukokota PLAU yao na hadi sasa wamelima EKARI 7 za MAJARUBA ya MPUNGA na wamelima EKARI 5 nyingine ambazo wamepanda MAHINDI, MIHOGO na VIAZI LISHE.
Kwa nyakati tofauti VIONGOZI wa VIKUNDI vya KILIMO vilivyopewa PLAU, wanamshukuru sana Mbunge wao Profesa Muhongo kwa kushirikiana na WAKULIMA kuboresha SEKTA ya KILIMO Jimboni mwao.
KAMPENI YA  ZAO JIPYA LA BIASHARA NA UTUMIAJI WA PLAU
WAKULIMA wa Jimbo la Musoma Vijijini WAMEDHAMIRIA kuachana na JEMBE LA MKONO la mababu zao. VIKUNDI VYA KILIMO vinaendelea kuundwa kwa ajili ya MATUMIZI ya pamoja ya PLAU na Vikundi vingine (AMCOS) vinashawishiwa vichukue mikopo ya MATREKETA.
Mbali ya KAMPENI ya kutokomeza JEMBE la MKONO, Mbunge huyo kwa kushirikiana na MAAFISA KILIMO wanaendelea kushawishi WAKULIMA walime zao JIPYA la ALIZETI  Vijijini mwao. Kwa MISIMU 3 mfululizo Mbunge huyo AMEGAWA BURE TANI 9.7 za Mbegu za ALIZETI na Wizara ya Kilimo ilitoa bure TANI 10 za Mbegu za ALIZETI kwa WAKULIMA wa Jimbo hilo.
KILIMO CHA MIHOGO nacho kinaboreshwa Jimboni humo kwa kutumia MBEGU ya aina ya MKOMBOZI inayopendekezwa na WATAALAMU wa KILIMO. Mbunge wa Jimbo aligawa bure MAGUNIA 796 ya Mbegu ya Mkombozi kwa Wakulima wa Jimbo hilo. Vilevile, kwa kupambana na athari za tabianchi, Mbunge huyo aligawa bure TANI 7.7 za MTAMA Jimboni humo.
Kwa kuendelea kuboresha Kilimo ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini, FEDHA za MFUKO WA JIMBO zilitumika kununua VIFAA VYA UMWAGILIAJI na MBEGU kwa VIKUNDI 15 vya Vijana na Wanawake.
VIKUNDI VYA KILIMO VYA VIJIJI 20
Vikundi 20 vilivyopewa zawadi ya PLAU vinatoka Vijiji vifuatavyo:
Bukima, Butata, Chimati, Chitare, Chumwi, Mabui Merafuru, Masinono, Mikuyu, Kaburabura, Kamguruki, Kwibara, Maneke, Mwiringo, Nyakatende, Nyasaungu, Nyegina, Rusoli, Suguti, Tegeruka na Wanyere
WAZALIWA wa Vijiji vya Jimbo hili wanaombwa kuchangia UNUNUZI WA PLAU kwa Wakulima wa Vijijini mwao.
KUTOKOMEZA UTUMIAJI MKUBWA WA JEMBE LA MKONO  INAWEZEKANA, JITOKEZE NA CHANGIA KIJIJI CHAKO!

VYUMBA VIPYA VYA MADARASA VINAVYOJENGWA VITAWATOA WANAFUNZI CHINI YA MITI

ujenzi wa Vyumba VIPYA vya Madarasa ya S/M Wanyere B, Kijijini Wanyere, Kata ya Suguti

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
Jimbo la Musoma Vijiji lenye Vitongoji 374, Vijiji 68 na Kata 21 lina jumla ya SHULE za MSINGI 111 za Serikali na 3 za Binafsi. Kuna UPUNGUFU mkubwa wa Vyumba vya Madarasa kwa baadhi ya Shule hizi za Msingi.
Kutokana na umbali mrefu wa kutembea na mirundikano madarasani, WANAVIJIJI kwa kushirikiana na SERIKALI, MADIWANI, MBUNGE wa Jimbo na WADAU wengine wa Maendeleo WAMEAMUA kujenga SHULE SHIKIZI MPYA 11 ambazo hapo baadae zitapanuliwa na kuwa SHULE za MSINGI kamili na zinazojitegemea.
KIJIJI CHA WANYERE CHAFUFUA MIRADI YA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA
Kijiji cha Wanyere, Kata ya Suguti KIMEAMUA kuendeleza MIRADI ya ujenzi wa MIUNDOMBINU ya SHULE zake za MSINGI baada ya kusuasua kwa zaidi ya miaka miwili – UONGOZI MPYA wa Serikali ya Kijiji ndio unafufua miradi hii.
Kijiji cha Wanyere kina VITONGOJI 6, ambavyo ni:
Mwikoro, Komesi, Mururangu, Miulu, Murugee na Ambagai. Kijiji hiki kina jumla ya Shule za Msingi 3 ambazo ni: S/M Wanyere, S/M Wanyere B, na S/M Murugee.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Wanyere, Ndugu Thomas Musiba amesema ujenzi wa Vyumba VIPYA vya Madarasa umeanza kwa MPANGILIO ufuatao:
 S/M WANYERE B
(i) Vitongoji vya Mwikoro na Komesi  wanaezeka Boma la Vyumba Vipya 2 vya Madarasa na Ofisi 1 ya Walimu.
(ii) Vitongoji vya Mururangu na Miulu  wanajenga Boma la Vyumba Vipya  2 vya Madarasa na tayari limefika kwenye renta.
UJENZI WA NYUMBA ZA WALIMU
S/M MURUGEE
Vitongoji vya Murugee na Ambagai vinajenga NYUMBA MPYA 2 za WALIMU.
Mwenyekiti huyo wa Kijiji cha Wanyere amesema kuwa ujenzi wote huo utakamilika ifikapo tarehe 1 Machi 2020.
Diwani wa Kata hiyo ya Suguti, Mhe Denis Ekwabi amemshukuru sana Mbunge wa Jimbo lao kwa jitihada kubwa anazozifanya Jimboni katika kutekeleza ILANI YA UCHAGUZI YA CCM (2015-2020). Diwani huyo ameomba WADAU wa Maendeleo wakiwemo WAZALIWA wa Kata ya Suguti kujitokeza kuchangia ujenzi huo.
MICHANGO ALIYOKWISHATOA MBUNGE WA JIMBO
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ametoa MICHANGO ifuatayo kwa Shule zote (3) za Msingi za Kijiji cha Wanyere:
(i) VITABU vingi vya MAKTABA kwa Shule zote 3.
S/M WANYERE
(ii) Madawati 71
(iii) Saruji Mifuko 25
S/M WANYERE B
(iv) Madawati 100
(v) Saruji Mifuko 85
(vi) Mabati 108 (Mfuko wa Jimbo)
S/M MURUGEE
(vii) Madawati 122
(viii) Saruji Mifuko 50  (Mfuko wa Jimbo)
WANYERE WAMEAMUA KUTATUA TATIZO LA MIUNDOMBINU YA ELIMU KWENYE SHULE ZAO – KARIBU USHIRIKIANE NAO.

KIJIJI CHA BUTATA CHAENDELEA KUTEKELEZA ILANI YA CCM – ZAHANATI MOJA KILA KIJIJI 

baadhi ya WANANCHI wa Kijiji cha Butata, Kata ya Bukima wakisomba mchanga wa ujenzi wa ZAHANATI ya Kijiji chao.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
Mtendaji wa Kijiji (VEO) cha Butata, Ndugu Charles Bulemo ameeleza kwamba WAKAZI wa Kijiji cha Butata wanalazimika kutembea umbali wa kilomita kati ya 3 na 6 kwenda kupata MATIBABU na HUDUMA nyingine za AFYA kwenye Zahanati ya Kijiji jirani cha Bukima.
Kata ya Bukima ina Vijiji 3 (Bukima, Butata na Kastamu). Diwani wa Kata hii, Mhe January Simula anasisitiza umuhimu wa KUTEKELEZA ILANI YA CCM (2015-2020) kwa VITENDO. Hivyo, kila KIJIJI kinashawishiwa kijenge Zahanati yake.
Diwani huyo amesema kwa sasa Vijiji vyote 3 vinatumia Zahanati moja iliyoko Kijijini Bukima. Zahanati hiyo inapanuliwa kwa kujenga WADI ya Mama na Mtoto ambapo Mbunge wao, Prof Sospeter Muhongo tayari amechangia SARUJI MIFUKO 100.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Butata, Ndugu William Mbasa  amesema ujenzi wa Zahanati ya Kijiji chao ulianza Mwaka 2018, ukasuasua, lakini kwa sasa WANANCHI WAMEAMUA kuendelea na kukamilisha ujenzi wa Zahanati hiyo.
MICHANGO inaendelea kutolewa na WANAVIJIJI, ambayo ni NGUVUKAZI (kusomba mawe, mchanga na maji) na SHILINGI 5,000/= kwa kila KAYA. Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo alishachangia SARUJI MIFUKO 50 kwa ajili ya ujenzi wa msingi wa BOMA la Zahanati hiyo.
MIUNDOMBINU YA HUDUMA ZA AFYA JIMBONI
Jimbo la Musoma Vijijini lina Vijiji 68 na kwa sasa WANAVIJIJI wanajenga ZAHANATI MPYA 13 na KITUO CHA AFYA 1. Ujenzi mwingine ni wa HOSPITALI ya WILAYA na upanuzi wa Zahanati ya Kijiji cha Masinono kuwa KITUO CHA AFYA cha Kata ya Bugwema.
Kwa sasa HUDUMA ZA AFYA ndani ya Jimbo zinatolewa na ZAHANATI 24 za Serikali na VITUO VYA AFYA 2 vya Serikali. Zahanati za BINAFSI ni 4.

SEKONDARI MPYA ZAENDELEA KUJENGWA JIMBONI MWETU

Viongozi wa Kata na Kamati ya Ujenzi wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa IFULIFU SECONDARY SCHOOL inayojengwa kwenye Kijiji cha Kabegi, Kata ya Ifulifu.

KATA ya IFULIFU ndiyo Kata pekee ISIYOKUWA na Sekondari yake. Kata hii yenye VIJIJI 3 (Kabegi, Kiemba na Nyasaungu) IMEAMUA kutatua tatizo hilo kwa kuanza ujenzi SEKONDARI 2 kwa wakati mmoja.
UMBALI mrefu wa kutembea, MISONGAMANO madarasani na JIOGRAFIA (k.m. Mto Nyasaungu unatenganisha vijiji hivyo) ni SABABU nilizotumiwa kufanya UAMUZI wa kuanza kujenga SEKONDARI zaidi ya moja ndani ya Kata hiyo ambayo watoto wake wanalazimika kutembea umbali mrefu kwenda Sekondari za Kata jirani za Mugango (Mugango Secondari) na Nyakatende (Nyakatende Sekondari).
Diwani wa Kata ya Ifulifu, Mhe Manyama Meru (CHADEMA) na Mtendaji Kata, Ndugu Fred Yona wamethibitisha UAMUZI wa WANANCHI wa kuamua kujenga Sekondari zaidi ya moja ndani ya Kata ya Ifulifu kwa wakati mmoja.
UJENZI WA NYASAUNGU SECONDARY SCHOOL
Hii Sekondari inajengwa na Kijiji kimoja cha Nyasaungu.
MICHANGO ya Wanakijiji wa Nyasaungu ni ya AINA YAKE kwani inategemea WINGI wa Ng’ombe alionao Mwanakijiji. Vyumba VIPYA 3 vya Madarasa vinaezekwa na Matundu 12 ya Vyoo yanachimbwa.
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo amewachangia SARUJI MIFUKO 35 na NONDO 20. Mfuko wa Jimbo umechangia MABATI 54. MIUNDOMBINU ya kuweza kuchukua Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza itakuwa tayari kabla ya tarehe 30 Juni 2020.
UJENZI WA IFULIFU SECONDARY SCHOOL
Ujenzi umeanza hivi karibuni Kijijini Kabegi.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kabegi, Ndugu Charles Choto kwa niaba ya Kamati ya ujenzi wa Ifulifu Sekondari, alifafanua na kusema kwamba  baada ya kukamilika kwa ujenzi wa  Vyumba VIPYA viwili vya Madarasa, kazi kitakayofuata ni ujenzi wa Jengo la Utawala, Vyoo vya Wanafunzi na Walimu, Maabara na baadae nyumba ya Mwalimu Mkuu.
MICHANGO kutoka kwa Wananchi ni NGUVUKAZI na FEDHA, Shilingi 33,000/= kwa kila KAYA
HARAMBEE YA MBUNGE WA JIMBO itafanyika Jumatatu, 2 Machi 2020 kwa ajili ya KUCHANGIA ujenzi wa IFULIFU SECONDARY SCHOOL.
VIONGOZI na WANANCHI wanasema MIUNDOMBINU ya IFULIFU SekondarI ya kuweza kuchukua Wanafunzi wa Kidato cha kwanza itakuwa tayari kabla ya tarehe 30 Juni 2020.
SEKONDARI MOJA AU ZAIDI KWA KILA KATA
Hadi leo hii (9.2.2020) Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21, lina SEKONDARI 20 za Kata/Serikali, na 2 za Binafsi. Sekondari MPYA zinazojengwa na zitakuwa tayari kutumiwa ifikapo Juni 2020 ni 5 (Kigera, Nyegina, Seka, Nyasaungu na Ifulifu). MIPANGO inakamilishwa ya ujenzi wa SEKONDARI MPYA kwenye Kata 3 za Etaro, Mugango na Suguti.

SHULE YA MSINGI ILIYOFUNGULIWA MWAKA 1942 YAOMBA MICHANGO ZAIDI KUTOKA KWA MBUNGE WA JIMBO

ufyatuaji wa matofali ya Shule ya Msingi BUTATA iliyoanza KUTATUA TATIZO la UKOSEFU wa Vyumba vya Madarasa na Ofisi za Walimu Shuleni hapo.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
SHULE YA MSINGI BUTATA ya Kijiji cha Butata, Kata ya Bukima iliyofunguliwa Mwaka 1942 kwa sasa ina WANAFUNZI 551, ambapo Wanafunzi wa Darasa la Kwanza (2020) ni 62 na uandikishaji unaendelea.
S/M BUTATA (B) iliyofunguliwa Mwaka 2014 ina Jumla ya WANAFUNZI 620, ambapo Darasa la Kwanza (2020) ni 80 na uandikishaji unaendelea.
Mwalimu Mkuu wa S/M Butata, Mwl Nancy Lema amesema WANAFUNZI 210 wanasomea nje CHINI YA MITI kwa sababu ya UKOSEFU wa Vyumba 6 vya Madarasa. Mwl Zablon Sehaba, Mwalimu Mkuu S/M Butata B amesema WANAFUNZI ZAIDI ya 221 wanasomea nje CHINI YA MITI kwa sababu hiyo hiyo. MVUA zinaponyeesha MISONGAMANO MADARASANI inakuwa mikubwa mno hadi kufikia Wanafunzi zaidi ya 100 kwenye Chumba kimoja cha Darasa.
UAMUZI WA KUTATUA TATIZO LA UKOSEFU WA VYUMBA VYA MADARASA KWENYE SHULE ZOTE MBILI ZA KIJIJI CHA BUTATA
S/M BUTATA
*Uongozi wa Shule UMEAMUA kuanza ujenzi wa Vyumba 2 VIPYA vya Madarasa na Ofisi 1 ya Walimu kwa kutumia na kufuata TARATIBU zilizowekwa za RUZUKU (Elimu bila Malipo) wanayopewa na Serikali. Wanaomba WANANCHI na  Mbunge wao Prof Sospeter Muhongo WAUNGANE nao kwenye ujenzi huu. Mbunge huyo AMEKUBALI kuungana nao na ataanza kwa kuchangia SARUJI MIFUKO 50.
S/M BUTATA B
* Shule inasubiri Serikali ya Kijiji iwapatie ENEO LA UJENZI na wao waanze. Vilevile, Wananchi na Mbunge wao wanaombwa washirikiane nao muda ukiwadia.
MICHANGO iliyokwishatolewa na Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo kwa Shule zote mbili za Kijijini Butata ni kama ifuatavyo:
 S/M BUTATA:
*Madawati 21
*Vitabu vingi vya Maktaba
*Mfuko wa Jimbo – Mabati 54
S/M BUTATA B
*Madawati 65
*Vitabu vingi vya Maktaba
*Saruji Mifuko 60
*Mfuko wa Jimbo – Mabati 54
WADAU WA MAENDELEO WANAOMBWA KUCHAGIA UJENZI WA VYUMBA VIPYA VYA MADARASA
*WAZALIWA wa Kijiji cha Butata WANAOMBWA WACHANGIE ujenzi wa Vyumba VIPYA vya Madarasa na Ofisi za Walimu za  Shule 2 hizo za Kijijini mwao.
*WADAU wengine wa Maendeleo nao wanaombwa wachangie ujenzi huo.

MRADI WA BMZ (UJERUMANI) WASAIDIA WATOTO WENYE ULEMAVU KWENYE KATA 10 ZA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

MRADI wa BMZ (Ujerumani) wa UGAWAJI wa Vifaa vya Shule na Chakula kwa Wanafunzi wenye ULEMAVU kutoka kwenye Kata 10 za Jimbo la Musoma Vijijini.

WATOTO WENYE ULEMAVU ndani ya Kata 10 za Jimbo la Musoma Vijijini  WAMEPEWA VIFAA VYA SHULE kutoka Mradi wa BMZ (Ujerumani) ulio na Ofisi zake kwenye Hospitali Teule ya SHIRATI, Wilaya ya Rorya.
BMZ (The Federal Ministry of Economic Cooperation and Development, formed in 1961) ya UJERUMANI ina MRADI wa KUHUDUMIA na KUTOA MATIBABU kwa Watu wenye ULEMAVU kwenye Wilaya 2 za Mkoa wa Mara.
MRADI huu ni wa USHIRIKIANO kati ya BMZ (Ujerumani) na Hospitali Teule ya Kanisa la Mennonite (KMT) la SHIRATI ambao unasaidia na kuwezesha WATU WENYE ULEMAVU kutoka KATA 10 za Wilaya ya Rorya na KATA 10 za Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC) yenye Jimbo la Musoma Vijijini.
MRADI HUU hutoa Vifaa vya Kimatibabu vinavyohitajika kwa Watu wenye ULAMAVU, MITAJI ya kuwawezesha kiuchumi na VIFAA vya SHULE kwa Wanafunzi wenye ULEMAVU. Hayo yameelezwa na Meneja wa Mradi wa BMZ, Ndugu Niwaely Sandy.
Hivi karibuni, kama ilivyo kawaida ya MRADI huu mara tu SHULE ZINAPOFUNGULIWA, Wanafunzi wenye ULEMAVU wamepewa:
*Vifaa vya Shule vikiwemo mabegi, madaftari na kalamu
* Vyakula – mchele, maharage na sukari
* Baadhi ya Wanafunzi hao watafanyiwa UPASUAJI wa MAREKEBISHO kwenye Hospitali Teule ya Shirati.
Wanafunzi wenye ULEMAVU waliopewa vifaa na chakula kutoka MRADI wa BMZ ni wa kutoka KATA za Bugwema, Bukima, Bukumi, Bwasi, Kiriba, Makojo, Murangi, Nyambono, Nyamrandirira na Suguti.
WANANCHI na VIONGOZI wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea KUSHUKURU SANA Mradi wa BMZ (Ujerumani)  kwa kutoa MISAADA ya Vifaa, Vyakula, Matibabu ya bure na MITAJI kwa Watu wenye ULEMAVU ndani ya Kata 10 zilizoko kwenye MRADI huu.

KATA 2 ZA NYAKATENDE NA IFULIFU ZAWEKA NGUVU PAMOJA KUTATUA UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MADARASA HUKU MOJA IKIJENGA SEKONDARI ZAKE MPYA MBILI

MAFUNDI wakiendelea na ujenzi wa Chumba kilichopungua kwa Wanafunzi wa Form I wa Nyakatende Secondary School

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge

SEKONDARI YA NYAKATENDE ilianzishwa Mwaka 2006 na kwa sasa ina Jumla ya Wanafunzi 737 na Walimu 23, akiwemo mmoja wa kujitolea. Jumla ya Walimu wa MASOMO ya SAYANSI ni 5.

Sekondari hii inahudumia KATA 2 za NYAKATENDE (Vijiji 4 – Kakisheri, Kamguruki, Kigera na Nyakatende) na IFULIFU (Vijiji 3 – Kabegi, Kiemba na Nyasaungu).

Mwalimu Mkuu wa Nyakatende Secondary School, Mwalimu Halima Yusuph Suleiman amesema jumla ya WANAFUNZI 269 wamechaguliwa kutoka VIJIJI 7 hivyo kuendelea na Masomo ya Kidato cha Kwanza (Form I) Shuleni hapo. Hadi sasa WANAFUNZI 213 wameisharipoti shuleni na tayari wako masomoni.

Mwalimu Mkuu huyo amesema kwamba vipo jumla ya Vyumba 5 kwa ajili ya Wanafunzi ya FORM I na kuna UPUNGUFU ya Chumba kimoja.

Mtendaji Kata (WEO) ya Nyakatende, Ndugu Martha Omahe Gagiri amesema kuwa Kata zote 2 (Nyakatende na Ifulifu) na Vijiji vyake vyote 7 wameamua kuunganisha nguvu ili kuharakisha ujenzi wa chumba hicho kimoja ambacho wanatarajia kukikamilisha kabla ya tarehe 15 Februari 2020.

Akiwa katika ZIARA ya uhamasishaji wa ujenzi wa Vyumba Vipya vya Madarasa Katani Nyakatende (6.1.2020), Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo alisema atachangia SARUJI MIFUKO 50 na MABATI 27 ili kukamilisha ujenzi wa chumba hicho kimoja.

Wakati huo huo, Kata pekee ndani ya Jimbo isiyokuwa na Sekondari yake, yaani Kata ya IFULIFU, WANANCHI wake WAMEAMUA KUJITEGEMEA kwa kujenga Sekondari zao MPYA, yaani NYASAUNGU SECONDARY SCHOOL (inajengwa na Kijiji kimoja cha Nyasaungu) na IFULIFU SECONDARY SCHOOL (inajengwa na Vijiji 2 vya Kabegi na Kiemba). Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo anaendelea KUCHANGIA VIFAA VYA UJENZI kwenye ujenzi huu. Sekondari MPYA hizi zitakamilishwa kwa ajili ya kuchukua Wanafunzi wa Form I kabla ya Juni 2020.

Kwa upande wake, Kata ya Nyakatende inajenga SEKONDARI YA PILI kwenye Kijiji cha Kigera ambayo
inajengwa na Vijiji 2 vya Kigera na Kakisheri. Itakuwa tayari kuchukua Wanafunzi wa Form I mwakani (Jan 2021).

UJENZI HUO HAPO JUU UKIKAMILIKA utatatua matatizo ya UMBALI MREFU wa kutembea (Wanafunzi & Walimu) na MIRUNDIKANO madarasani kwenye Kata za Nyakatende na Ifulifu.

WANAVIJIJI WAITIKIA MWITO WA KUTATUA TATIZO LA MIRUNDIKANO MADARASANI

Ujenzi wa chumba kimoja cha Darasa (Form I) cha Rusoli Secondary School kitakachokamilishwa kabla ya tarehe 15 Februari 2020.

Jumatano, 29.1.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
Na: Veredian Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
SEKONDARI zote za  Jimboni zenye UPUNGUFU wa Vyumba vya Madarasa ZITATATUA tatatizo hilo kabla ya tarehe 30 Machi 2020. Sekondari hizo ni  Bugwema (Vyumba 3), Bulinga (3), Kasoma (3), Nyakatende (2) na Rusoli (1).
Kwa sasa Jimbo letu lina Sekondari 20 za Kata/Serikali na 2 za Binafsi. Kata pekee (IFULIFU) isiyokuwa na Sekondari yake, kwa sasa inajenga SEKONDARI 2 (zinajengwa kwenye Vijiji vya Nyasaungu na Kabegi).
RUSOLI SECONDARY SCHOOL ya Kata ya Rusoli (Vijiji 3 – Buanga, Kwikerege na Rusoli) ilianzishwa Mwaka 2010 ina Jumla ya Wanafunzi 422 na Walimu 13 akiwemo H/M Mwalimu Tatu Juma.
Jumla ya WANAFUNZI 132 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha kwanza hapo Rusoli Sekondari. Mwalimu Mkuu huyo amesema hadi leo, WANAFUNZI 113 wameripoti Shuleni na 2 wamehama.
UPUNGUFU WA MIUNDOMBINU NA UPATIKANAJI WAKE
* WANAFUNZI 132 wa Form I wanahitaji Vyumba 3 vya Madarasa. Vipo 2 na kimoja kinajengwa na kitakamilishwa kabla ya tarehe 15 Februari 2020.
VIFAA VYA UJENZI wa Chumba kimoja hicho vimetolewa na WAZALIWA wa Kata ya Rusoli ambao ni: (1) Profesa Lawrence Mseru (2) Ndugu William Makunja (3) Belias Mkama na (4) Ndugu Laitoni Samamba. Vilevile, (5) Kanisa la Wasabato Rusoli nalo limechangia
Mbunge Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo atachangia SARUJI MIFUKO 50 ya kupigia lipu Jengo hilo.
UPANUAJI WA VYOO VYA WANAFUNZI
*Wazazi WAMEKUBALI kuongeza Matundu ya Vyoo vya Wasichana kufikia 10 (toka manne) na Wavulana kufikia 10 (toka manne). Kazi hii itakamilika kabla ya tarehe 30 Mai 2020.
Diwani wa Kata ya Rusoli, Mhe Boaz Nyeula na VIONGOZI wengine wa Kata na Vijiji wanaendelea kuwashawishi na kuwahimiza WANANCHI washiriki ipasavyo kwenye ujenzi na uboreshaji wa Miundombinu ya Rusoli Sekondari.
MICHANGO YA WAZALIWA WA KATA YA RUSOLI
Kikundi cha WAZALIWA wa Kata ya Rusoli kijulikanajo kwa jina la “YEBHE CHIKOMESHE” kimetoa MICHANGO MIKUBWA kwa ustwai wa ELIMU na MAENDELEO ndani ya Kata hiyo. Kimechangia KISIMA CHA MAJI kwa Shule za Sekondari na Msingi, Ujenzi wa Nyumba ya Walimu (two in one), Uboreshaji wa Maabara, Computer, Printer, Photocopier, Projector, n.k.
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini alishachangia SARUJI MIFUKO 70 kwa ajili ujenzi wa Vyumba vya Madarasa ya Rusoli Sekondari. Vilevile, Mbunge huyo amewapatia VITABU vingi vya Maktaba yao.

WANAFUNZI WENGINE NAO WAEPUKA KUTEMBEA UMBALI UNAOZIDI KM 10 KWENDA MASOMONI KATA YA JIRANI

Wanafunzi wa Form I wa DAN MAPIGANO MRMORIAL SECONDARY SCHOOL wakiwa ndani na nje ya Vyumba vyao vya Madarasa.

WANAFUNZI wa Kitongoji cha Kwisayenge, Kijiji cha Kaburabura mpakani na Wilaya jirani ya Bunda WANALAZIMIKA kutembea umbali wa kilomita usiopungua KM 15 kwenda (na kurudi umbali huo huo) MASOMONI Nyambono Sekondari ya Kata jirani ya Nyambono.
Alhamisi, 16.1.2020 SEKONDARI MPYA, DAN MAPIGANO MEMORIAL SECONDARY SCHOOL ya Kata ya Bugoji IMEANZA kutoa ELIMU ya SEKONDARI ndani ya Kata hiyo.
WANAFUNZI 141wa Kata ya Bugoji waliochaguliwa kuendelea na MASOMO ya Sekondari HAWATATEMBEA TENA UMBALI MREFU kwenda masomoni.
MAFANIKIO ya kuipata Dan Mapigano Memorial Secondary School yametokana na USHIRIKIANO MZURI wa SERIKALI na WANANCHI WA KATA YA BUGOJI yenye Vijiji 3 (Kaburabura, Kanderema na Bugoji)
* Wanavijiji wa Vijiji 3 wamechangia NGUVUKAZI na FEDHA.
* Viongozi mbalimbali akiwemo Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini wamechangia FEDHA na USHAURI
* Wazaliwa wa Kata ya Bugoji. Baadhi yao walichangia FEDHA na USHAURI. Majina yataandikwa kwenye ubao na kutunzwa shuleni hapo.
*Serikali ikiwemo  Halmashauri ya Wilaya ya Musoma imechangia FEDHA, USHAURI na UONGOZI chini ya Mkuu wa Wilaya ya Musoma (Dr Vicent Naano Anney) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri yetu (Ndg John Lipesi Kayumbo). PONGEZI za dhati kwa Viongozi hao na TIMU zao za kazi.
*Diwani wa Kata ya Bugoji, Mhe Ibrahimund Malima na TIMU zake za UJENZI na UONGOZI zinapewa PONGEZI nyingi za dhati kwa kazi nzuri mno. Vilevile, Mtendaji Kata, Ndugu Edna Edward Kurata na TIMU yake ya kazi wanastahili PONGEZI nyingi kwa UTEKELEZAJI mzuri wa majukumu yao.
UJENZI ULIOVUNJA REKODI
*Ujenzi wa Dan Mapigano Memorial Secondary School ulianza DISEMBA 2018 na kufikia NOVEMBA 2019 tayari MIUNDOMBINU muhimu ilishakamilishwa (k.m. Vyumba 5 vya Madarasa, Madawati, Ofisi 2 za Walimu, Vyoo matundu 10, misingi ya ujenzi wa Maabara na Nyumba ya Walimu)
HAKUNA MISANGAMANO MADARASANI
*Wanafunzi 141 wa Form I wanatumia VYUMBA 3 vya MADARASA (kwa sasa vipo 2 vya ziada). Kila Mwanafunzi analo DAWATI lake na KITI chake.
OFISI 2 ZA WALIMU
* Kwa sasa wapo WALIMU 5, yaani Headmaster na Walimu wake 4. Ofisi na samani zinatosha.
VYOO VYA WANAFUNZI & WALIMU
* Mashimo 10 ya Wasichana, 10 ya Wavulana na 2 ya Walimu yanatosha.
UJENZI WA VIWANGO BORA UNAENDELEA
* Ujenzi wa Maabara, Madarasa mengine, Maktaba, Nyumba za Walimu na Viwanja vya Michezo UNAENDELEA.
KUJIPONGEZA NA KUENDELEA NA UJENZI KWA KASI na UMAKINI MPYA
*Jumanne, tarehe 25 Februari 2020, Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo kwa kushirikiana na WAZALIWA wa Kata ya Bugoji WALIFANYA TAFRIJA Shuleni hapo (Dan Mapigano Memorial Secondary School) ya KUWAPONGEZA WANAVIJIJI wa Kata ya Bugoji kwa hatua hiyo waliyoifikia kwenye ujenzi wa Sekondari yao ya Kata – hawakuwa nayo!

SEKONDARI MPYA ZAONYESHA UBORA WA MIUNDOMBINU YA ELIMU VIJIJINI MWETU

Wanafunzi wa Form I wa Busambara Secondary School wakiwa ndani ya moja kati ya Vyumba vyao vya Madarasa.

Ijumaa, 24.1.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
Hatimae USHIRIKIANO kati ya WANANCHI  na SERIKALI wazaa MATUNDA MAZURI kwenye Sekta ya Elimu – Sekondari Mpya za VIWANGO vizuri ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.
Tarehe 14 Januari 2020, WANAFUNZI wa Kidato cha kwanza wa  BUSAMBARA SEKONDARY SCHOOL walianza MASOMO yao.
BUSAMBARA SECONDARY SCHOOL imejengwa kwa USHIRIKIANO wa:
* Wanavijiji wa Vijiji 3 vya Kata ya Busambara ambavyo ni Kwikuba, Maneke na Mwiringo. Hawa walichangia NGUVUKAZI na FEDHA.
* Viongozi mbalimbali akiwemo Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini. Hawa walichangia FEDHA na USHAURI
* Wazaliwa wa Kata ya Busambara. Baadhi yao walichangia FEDHA na USHAURI. Majina yataandikwa kwenye ubao na kutunzwa shuleni hapo.
*Serikali ikiwemo  Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. MICHANGO hapa ni FEDHA, USHAURI na UONGOZI chini ya Mkuu wa Wilaya ya Musoma (Dr Vicent Naano Anney) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri yetu (Ndg John Lipesi Kayumbo). HONGERENI sana Viongozi wetu.
*Mtendaji Kata ya Busambara, Ndugu Victor Kasyupa na TIMU yake ya Watendaji wa Vijiji na Afisa Elimu Kata WANASTAHILI PONGEZI kwa kazi kubwa yenye UBUNIFU na UTELEKEZAJI wa uhakika.
MICHANGO YA MADAWATI
* Benki ya NMB inapewa SHUKRANI NYINGI za dhati kwa KUCHANGIA Madawati 80 na Viti 80. AHSANTENI SANA.
HAKUNA MISANGAMANO MADARASANI
*Wanafunzi 142 wa Form I wanatumia VYUMBA 3 vya MADARASA. Kila mmoja analo DAWATI lake na KITI chake.
OFISI 2 ZA WALIMU
* Kwa sasa wapo WALIMU 6, yaani Headmaster na Walimu wake 5. Ofisi 2 zenye meza, viti na kabati zinawatosha.
WALIMU WA KUJITOLEA
* Wazaliwa wa Kata ya Busambara WAMEJITOLEA kuchangia POSHO za Walimu wa KUJITOLEA. Ndugu zetu hawa, Ndugu Joseph Chikongoye, Saidi Chiguma na Robert Cheumbe wanapewa PONGEZI NYINGI na SHUKRANI za dhati.
VYOO VYA WANAFUNZI
* Mashimo 8 ya Wasichana, 6 ya Wavulana na 2 ya Walimu yanatosha kwa idadi ya sasa ya Wanafunzi na Walimu.
UJENZI WA VIWANGO BORA UNAENDELEA
* Ujenzi wa Maabara, Madarasa mengine, Maktaba, Nyumba za Walimu na Viwanja vya Michezo UNAENDELEA.
KUJIPONGEZA NA KUENDELEA NA UJENZI KWA ARI MPYA
*Jumamosi, tarehe 29 Februari 2020, Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo kwa kushirikiana na WAZALIWA wa Kata ya Busambara WATAFANYA TAFRIJA Shuleni hapo (Busambara Secondary School) ya KUWAPONGEZA WANAVIJIJI wa Kata ya Busambara kwa hatua hiyo waliyoifikia kwenye ujenzi wa Sekondari yao ya Kata – hawakuwa nayo!
Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 kwa sasa (Jan 2020) lina Sekondari 20 za Kata/Serikali, 2 za Binafsi (SDA & KATOLIKI)  na zinajengwa 9 mpya.

WANAVIJIJI WA KATA YA BULINGA WAKUBALI KUTATUA TATIZO LA MRUNDIKANO WA WANAFUNZI MADARASANI

MKUTANO wa Mbunge Jimbo, Prof Sospeter Muhongo na WANANCHI wa Kata ya Bulinga.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
WANAFUNZI 157 wa Kata ya Bulinga wamechaguliwa kuendelea na MASOMO ya KIDATO cha KWANZA kwenye Sekondari ya Kata yao, yaani Bulinga Secondary School.
Hadi sasa, WANAFUNZI takribani 120 WAMERIPOTI Shuleni na wote WAMERUNDIKANA kwenye Chumba kimoja cha Darasa.
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo alitembelea Bulinga Sekondari na KUONGEA na WANANCHI akiwashawishi WASHIRIKIANE na SERIKALI yao kutatua TATIZO la UKOSEFU na UPUNGUFU wa Vyumba vya Madarasa kwenye Sekondari hiyo yenye Jumla ya WANAFUNZI 410.
Mwalimu Mkuu wa Bulinga Sekondari, Mwl Nyang’oso Chacha alisema Wanafunzi 157 wa Form I wanahitaji VYUMBA 3 VIPYA vya MADARASA na kwa sasa lipo BOMA la DARASA 1 liloezekwa tayari na linahitaji kukamilishwa. MABOMA 2 ya Vyumba 2 vya Madarasa hayajaezekwa.
Diwani wa Kata hiyo, Mhe Mambo Japan (CHADEMA) na Mwenyekiti  wa Serikali ya Kijiji cha Busungu, Ndugu Abel Mafuru (CCM) wamesema WANANCHI WAMEKUBALI kutoa NGUVUKAZI na KUCHANGA Shillingi 11,000/= kwa KILA KAYA ili KUKAMILISHA UJENZI wa VYUMBA 3 hivyo.
Aidha, Wananchi na Viongozi wa Kata ya Bulinga wanamshukuru sana Mbunge wao, Profesa Sospeter Muhongo kwa kushiriki na kuhamasisha shughuli za maendeleo kwenye Sekta ya Elimu na nyinginezo kwenye VIJIJI VYAO 3 – Bulinga, Bujaga na Busungu. Mbunge huyo alishachangia VITABU vingi, SARUJI MIFUKO 120 na MFUKO wa JIMBO ulishachangia MABATI 108.
UKAMILISHAJI WA VYUMBA 3 VIPYA VYA MADARASA
Wananchi wa Vijiji vyote 3 na Viongozi wao WAMEKUBALIANA kukamilisha ujenzi wa Vyumba hivyo 3 ifikapo tarehe 15 FEBRUARI 2020.
Kwa uharaka wa kupatikana CHUMBA cha PILI cha Form I ifikapo Jumatatu, 27.1.2020, Mbunge wa Jimbo amechangia, juzi (21.1.2020) SARUJI MIFUKO 35 ya kupiga lipu chumba kilichokwisha uzekwa.

PROF MUHONGO AWEZESHA UWEKAJI WA UMEME KWENYE JENGO LA CCM LA WILAYA YA MUSOMA VIJIJINI

MAFUNDI wa TANESCO wakiweka UMEME kwenye Jengo (Ukumbi na Vyumba 4) la CCM Kijijini Chumwi, Kata ya Nyamrandirira.

Jumatano, 22.1.2020
CCM Wilaya ya Musoma Vijijini
Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo ameombwa na Chama (CCM) na kukubali kugharamia uwekaji wa UMEME kwenye Jengo la Chama Cha Mapinduzi (CCM) lililopo Kijijini Chumwi, Kata ya Nyamrandirira.
JENGO hilo lina Ukumbi na Vyumba 4.
TANESCO wamekamilisha ZOEZI LA KUWEKA umeme ndani ya SIKU 2 tu! TANESCO Mkoa (Mara) wanapongezwa kwa KAZI NZURI waliyoifanya na kwa muda mfupi sana!
Akizungumza na Msaidizi wa Mbunge, Katibu wa CCM Wilaya ya Musoma Vijijini, Ndugu Steven Koyo ametoa shukrani zake za dhati kwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini kwa kukubali ombi la Chama la kuweka umeme katika Jengo la CCM ambalo litaanza kutumika rasmi wiki ijayo kama OFISI YA MUDA ya CCM Wilaya  ya Musoma Vijijini wakati Chama (CCM)  kikiwa kinajenga JENGO LAKE LA KUDUMU Kijijini Murangi. Ujenzi unaanza Mwezi ujao (Februari 2020).
Wanachama wa CCM na rafiki zao wanakaribishwa KUCHANGIA UJENZI wa Makao Makuu ya CCM ya Wilaya ya Musoma Vijijini KIJIJINI MURANGI – KARIBUNI.

VIJIJI VYAGAWANA KAZI KUHARAKISHA UJENZI WA VYUMBA VIPYA VYA MADARASA NA OFISI ZA WALIMU

KIKAO (ndani ya Bugwema Sekondari) cha Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo na Wanavijiji wa Kata ya Bugwema.

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
Wananchi wa Kata ya Bugwema WAMEAMUA kuharakisha UJENZI wa VYUMBA 4 VIPYA vya Madarasa na OFISI 2 za Walimu kwenye Sekondari yao ya Kata (Bugwema Secondary School) ndani ya MWEZI MMOJA (ifikapo tarehe 28.2.2020). UAMUZI huo ulitolewa na WANAVIJIJI wa Kata hiyo walipotembelewa na Mbunge wao Prof Sospeter Muhongo.
Kata ya Bugwena ina VIJIJI 4 – Bugwema, Kinyang’erere, Masinono na Muhoji.
Vijiji vya  Masinono na Kinyang’erere wako kwenye hatua ya UPAUAJI wa Vyumba 2 VIPYA vya Madarasa na OFISI 1 ya Walimu. Vijiji vya Bugwema na Muhoji navyo vinapaswa kukamilisha ujenzi wao unaofanana na ule wa Vijiji vya Masinono na Kinyang’erere.
Mwalimu Mkuu wa  Bugwema Sekondari, Mwl Ndaro Emmanuel amesizitiza kuwa Wananchi wa Kata ya Bugwema na Kata nyingine WANAPASWA kutatua mapema tatizo la UHABA wa Vyumba vya Madarasa ili WANAFUNZI ambao ni WATOTO wao waweze kupata ELIMU BORA wakisomea ndani ya Vyumba vizuri vya Madarasa vikiwa na idadi ya Wanafunzi wanaotakiwa badala ya KURUNDIKANA. Mwalimu huyo aliendelea kwa kusema kwamba tatizo la MIRUNDIKANO ya Wanafunzi madarasani likitatuliwa, UFAULU kwenye Mitihani ya Taifa ya  KIDATO CHA PILI NA CHA NNE utaongezeka.
Mwalimu Mkuu huyo  alieleza kuwa Jumla ya Wanafunzi wa Kata ya Bugwema waliochaguliwa kujiunga na masomo ya Kidato cha kwanza mwaka huu (2020) ni 249, na hadi sasa (wiki jana), Jumla ya Wanafunzi 114 (45.78%) walikuwa wameripoti shuleni na hao wote wamerundikana kwenye Chumba 1 cha Darasa la Form I.
Diwani wa Kata hiyo, Mhe Ernest Maghembe AMEOMBA WADAU mbalimbali WAJITOKEZE kuungana na Wananchi wa Kata ya Bugwema kujenga na kuboresha MIUNDOMBINU ya ELIMU kwenye Kata hiyo.
Diwani huyo na Wananchi kwa ujumla WANAMSHUKURU sana Mbunge wao wa Jimbo kwa kuisaidia Bugwema Sekondari kwa kutoa VITABU zaidi ya 1,000 (elfu moja), kuleta WADAU wa kuboresha MAABARA, kutoa POSHO ya Mwalimu wa Kujitolea wa Masomo ya Sayansi. MFUKO wa JIMBO umechangia Saruji Mifuko 70.

KATA YA NYAMRANDIRIRA YAAMUA KUJENGA SEKONDARI YAKE YA KATA

KIKAO kilichofanyika Kasoma Sekondari kilichohudhuriwa na Wananchi wa VIIJIJI 5 vya Kata ya Nyamrandirira, DC wa Wilaya ya Musoma na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.

Ijumaa, 17.1.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
Kata ya Nyamrandirira yenye Vijiji 5 ndiyo Kata kubwa kuliko nyingine zote Jimboni mwetu. Vijiji vyake ni: Chumwi, Kaboni, Kasoma, Mikuyu na Seka.
Kasoma Secondary School ndiyo inatumiwa na Kata hii. Kasoma Sekondari ilianzishwa Mwaka 1995 ikipanuliwa kutoka iliyokuwa “Middle School” ya Serikali iliyoanzishwa Mwaka 1956.
Kasoma Secondary School ina KIDATO V & VI (A-level) cha MASOMO YA SANAA. Jumla ya Wanafunzi wa “A-level” ni 220 ambao wanahitaji Vyumba 7 vya Madarasa. Jumla ya Wanafunzi wa “O-level (Kidato I-IV) ni 929 ambao wanahitaji Vyumba 23 vya Madarasa. Nyumba za Walimu zipo 8 tu kwa Walimu 26 waliopo. UPUNGUFU ni mkubwa (Vinahitajika jumla ya Vyumba 30 vya Madarasa, vipo 24)!
Wanafunzi wa Kata ya Nyamrandirira WALIOCHAGULIWA kujiunga na Masomo ya Kidato cha kwanza Mwaka huu (2020) ni 202. UFAULU huu ni mdogo ukilinganisha na Kata nyingine za Jimboni mwetu.
TAKWIMU hizo hapo juu ZIMESHAWISHI kupatikana  kwa UAMUZI wa kujenga SEKONDARI MPYA ndani ya Kata hiyo badala ya KUENDELEA kuongeza Vyumba VIPYA vya Madarasa hapo Kasoma Sekondari.
Wiki iliyopita, Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dr Vicent Naano Anney na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo WALISHIRIKI KIKAO cha WANAVIJIJI wa Kata hiyo kilichotoa UAMUZI wa kujenga SEKONDARI MPYA ndani ya Kata yao.
WANAVIJIJI kutoka VIJIJI 5 vyote vya Kata hiyo WALIKUBALIANA kujenga Sekondari mpya KIJIJINI SEKA.
UJENZI umeanza. DC huyo atasaidia upatikanaji na MAWE na MCHANGA na Mbunge huyo ataanza kutoa MICHANGO yake kwa kutoa SARUJI MIFUKO 100. WANANCHI wa VIJIJI 5 vyote watatoa NGUVUKAZI na MICHANGO mingine ya ujenzi huo.
Vyumba vipya 4 vya Madarasa vinapaswa KUKAMILIKA kabla ya tarehe 30 Machi 2020 ili baadhi WANAFUNZI wa Form I WALIORUNDIKANA Kasoma Sekondari wahamie kwenye Sekondari MPYA inayojengwa Kijijini Seka. Vilevile, kukamilika kwa Vyumba hivyo KUTARUHUSU Kasoma Sekondari kuendelea kutumia MAABARA zake 3 ipasavyo, kwani kwa sasa ndiyo Madarasa ya Form I.
KARIBU TUCHANGIE UJENZI WA SEKONDARI MPYA YA KATA YA NYAMRANDIRIRA.
Mawasiliano ya kutoa MICHANGO:
Mtendaji (WEO)
0683 573 808
M/K Kamati ya Ujenzi
0683 120 444
Katibu Kamati ya Ujenzi
0629 424 717
0767 334 023
SEKONDARI MPYA KUFUNGULIWA JAN 2020 – MAFANIKIO MAZURI
*Busambara Secondary School, Kata ya Busambara (Vijiji 3 – Kwikuba, Maneke na Mwiringo) imekubaliwa kuchukua Wanafunzi wa Form I (2020) wa Kata hiyo.
*Dan Mapigano Memorial Secondary School, Kata ya Bugoji (Vijiji – Bugoji, Kaburabura na Kanderema) imekubaliwa kuchukua Wanafunzi wa Form I (2020) wa Kata hiyo.

WASAGA FC YAENDELEZA MATUMAINI YA KUWA MABINGWA WA MKOA

WASAGA FC ya Kijijini Kasoma

Jumatano, 15.1.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
Timu ya WASAGA FC inayoshiriki Ligi  Daraja la Tatu Mkoani Mara imeendelea kufanya vizuri katika mashindano ya Ligi hiyo.
WASAGA FC ni Timu ya Kijiji cha Kasoma, Kata ya Nyamrandirira. Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo ametoa MCHANGO MKUBWA (usajiri/posho, jezi na viatu) kuiwezesha Timu hii kushiriki Ligi hiyo.
Katika Mchezo wa kwanza wa tarehe 6 Januari 2020, WASAGA FC ilishinda bao 1 – 0 dhidi ya Timu ya JK FC ya Manispaa ya Musoma na kutinga hatua ya nusu fainali.
Mchezo wa Nusu Fainali uliofanyika tarehe 13.01.2020 kati ya Timu ya WASAGA FC na TAGOTA ya Tarime, Timu ya WASAGA FC iliibuka na ushindi wa mabao 2 – 0. Ushindi huo ulitosha kuipeleka WASAGA FC fainali ambapo itacheza na NYAMONGO SC ya Tarime tarehe 16 Januari 2020 kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume Mjini Musoma

MBUNGE WA JIMBO AIWEZESHA TIMU YA KIJIJI CHA KASOMA KUSHIRIKI LIGI DARAJA LA 3

MSAIDIZI wa Mbunge, Ndugu Fedson Masawa (mwenye track suit) akikabidhi JEZI na VIATU kwa VIONGOZI na WACHEZAJI wa Wasaga FC., Kijijini Kasoma, Makao Makuu ya Wasaga FC.

MICHEZO na UTAMADUNI ni moja ya VIPAUMBELE vya Jimbo la Musoma Vijijini lenye Vitongoji 374, Vijiji 68 na Kata 21.
TIMU YA WASAGA FC ya Kijiji cha Kasoma, Kata ya Nyamrandirira inashiriki LIGI YA DARAJA LA 3 ya Mkoa wa Mara.
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo AMEIWEZESHA WASAGA FC kushiriki LIGI hiyo kwa kuchangia:
* USAJILI wa Wachezaji
* Jezi Mpya
* Viatu vya kuchezea Mpira wa Miguu
VIFAA hivyo vimekabidhiwa kwa TIMU hiyo tarehe 12.1.2020
Vilevile, Mbunge huyo wa Jimbo la Musoma Vijijini ni mmoja wa Wafadhili wa BIASHARA UNITED ya Mkoa wa Mara inayoshiriki LIGI KUU ya Taifa.

KIKUNDI CHA WAZALIWA WA KIJIJI CHA RUSOLI CHAENDELEA KUBORESHA  UBORA WA SHULE ZA KIJIJINI MWAO

TUKIO la kukabidhi Computers (Desktops 2 na Laptop 1), Photocopiers (2) na Projector (1) kwenye S/M Rusoli A&B na Rusoli Secondary School.

Kikundi cha YEBHE CHIKOMESHE kinachoundwa na baadhi ya WAZALIWA wa Kijiji cha Rusoli, Kata ya Rusoli KINAENDELEA KUCHANGIA UBORESHAJI wa Miundombinu na Vifaa vya ELIMU kwa Shule za Msingi Rusoli A&B na Rusoli Sekondari.
Jumatatu, tarehe 6.1.2020 YEBHE CHIKOMESHE kwa kushirikiana na WADAU wao wa Maendeleo wa nchini Denmark wametoa vifaa vifuatavyo:
* Computer (Desktop 1) na Photocopier 1 (+printer&scanner) kwa Rusoli Secondary School
* Vifaa kama hivyo kwa S/M Rusoli A
* Laptop na Projector kwa S/M Rusoli B.
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo aliombwa na kukubali kukabidhi vifaa hivyo kwenye Shule hizo 3 za Kijiji cha Rusoli.
TUREJEE MICHANGO KUTOKA YEBHE CHIKOMESHE
* Kisima cha Maji kwa ajili ya Shule zote 3 na Kijiji cha Rusoli
* Vifaa vya Maabara vya Tsh Milioni 5 na Kabati la Chuma kwa Rusoli Sekondari
* Nyumba ya Walimu (two in one) ya  Sekondari. Ukamilishwaji unaendelea.
* Utengenezaji wa Maktaba na Vifaa vyake kwa Shule 2 za Msingi
Wananchi, Viongozi wa Chama na Serikali wanaendelea KUKISHUKURU Kikundi cha YEBHE CHIKOMESHE kwa michango ya Maendeleo wanayoitoa kwa manufaa ya JAMII nzima ya Kijiji na Kata ya Rusoli.
TUREJEE MICHANGO KUTOKA KWA MBUNGE WA JIMBO KWA KIKIJI CHA RUSOLI
(i) Madawati 64 S/M Rusoli A
(ii) Madawati 97 S/M Rusoli B
(iii) Mabati 50 S/M Rusoli A
(iv) Mabati 54 S/M Rusoli B
(v) Mbao 107 S/M Rusoli A
(vi) Saruji Mifuko 60 S/M Rusoli B
(vii) Saruji  Mifuko 70 Rusoli Sekondari
(viii) Posho ya Mwalimu wa Kujitolea wa Masomo ya Sayansi wa Rusoli Sekondari
(ix) Vitabu vingi kwa Shule zote 3
(x) Vifaa vya Michezo (jezi na mipira ).
(xi) Mbegu za Alizeti, Mtama na Mihogo
Taarifa ijayo itaeleza vyanzo vya MICHANGO ya Ukamilishaji wa  Chumba 1 cha Darasa kinachohitajika Rusoli Sekondari.
TUENDELEA KUCHANGIA MAENDELEO YA VIJIJI VYETU

MZALIWA WA KIJIJI CHA BUKIMA AANZISHA SHULE YA MSINGI KIJIJINI MWAO – YAZINDULIWA RASMI LEO

UZINDUZI wa AGAPE PRIMARY SCHOOL Kijijini Bukima, Kata ya Bukima. Aliyeshika kipaza sauti ndiye MMILIKI wa Agape Primary School, Ndugu Andrew Kayola.

Wanafunzi, Walimu, Wazazi, Viongozi wa Serikali na Chama (CCM) wamehudhuria SHEREHE za UZINDUZI wa AGAPE Primary School zilizofanyila leo, Jumanne, 7.1.2020 Kijijini Bukima.
KIONGOZI na MMLIKI wa Shule hiyo, Ndugu ANDREW KAYOLE (32yr), mhitimu wa UDOM, Shahada ya Biashara  Bc(HRM) amesema Shule hiyo ilisajiliwa rasmi tarehe 21.6.2017 na tayari WAHITIMU wa kwanza wamemaliza Darasa la 7 (Std 7) Mwaka jana (2019) wakiwa wa KWANZA kwa Wilaya ya Musoma katika kundi lao. Wanafunzi wote walifaulu (A&B). Shule inafundisha kwa lugha ya KIINGEREZA na Mwakani lugha ya KIFARANSA itaanza kufundishwa Shuleni hapo.
MGENI RASMI, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo amesema kwamba kuwepo kwa Shule Binafsi (Private Schools) Jimboni mwao ni muhimu sana kwa UIMARIKAJI wa UBORA wa ELIMU kupitia USHINDANI KITAALUMA kwa Shule zote za Msingi zilizoko Jimboni humo (Shule 3 za Binafsi na 111 za Serikali).
Mbunge huyo amekuwa AKICHANGIA MAENDELEO ya Shule za Msingi na Sekondari za Serikali na Binafsi bila UBAGUZI wo wote. Aliwakumbusha WAGENI waalikwa kwamba Vyuo Vikuu bora Duniani vimo vya Binafsi (Private Universities) kama vile Harvard (USA),  MIT (USA), Yale (USA) Caltech (USA), na vilevile vimo vya umma (Public Universities) kama vile Oxford (UK) na Cambridge (UK).
Leo, Mbunge huyo amechangia box 10 za VITABU vya Maktaba ya Shule hiyo. Vilevile, amechangia SARUJI MIFUKO 50 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la TEHAMA. Ametoa ahadi ya kuchangia COMPUTER 1 na PRINTER 1 mara Jengo hilo litakapokamilika na kuanza kutumika.
Wakati akizindua AGAPE Primary School na kuweka Jiwe la Msingi la Jengo la TEHAMA la Shule hiyo, Mbunge huyo AMEMWOMBA MWANZILISHI wa Shule hiyo aendelee kuipanua hadi kuanza kutoa MASOMO ya SEKONDARI.
WAZALIWA KUWEKEZA VIJIJINI MWAO
MMILIKI (Ndugu ANDREW KAYOLE) wa Agape Primary School ni KIJANA (32yr) ALIYETHUBUTU na KUFANIKIWA kuwekeza Kijiji mwao. Mbunge wa Jimbo AMEMPONGEZA SANA na kusema JIMBO LINAJIVUNIA kuwa na WAWEKEZAJI wa aina hiyo – TUJIFUNZE KWAKE na TUWEKEZE Vijijini kwetu!

HAYUPO MWANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA 2020 (wamechaguliwa 3,502) ATAKAYEBAKI NYUMBANI

Mbunge wa Jimbo (mwenye T-shirt nyeupe) akiwa na Wananchi wa Kata ya Bugoji wakipiga HARAMBEE ya kukamilisha ujenzi wa Vyoo vya Dan Mapigano Memorial Secondary School.

SEKONDARI 2 MPYA ZINAZOJENGWA JIMBONI ZAOMBA ZIFUNGULIWE TAREHE 13.1.2020
(1) Busambara Secondary School ya Kata ya Busambara (Vijiji vya Maneke, Kwikuba na Mwiringo).
Vyumba vipya 3 vya Madarasa na madawati 40 kila darasa viko tayari. Jengo la Ofisi za Walimu linakamilishwa kwa kuwekwa milango na madirisha. Ujenzi wa Vyoo vya Wasichana, Wavulana na Walimu UTAKAMILIKA Alhamisi, 9.1.2020.
KIKAO cha HARAMBEE cha Wananchi na Mbunge wao, Prof Sospeter Muhongo, cha tarehe 2.1.2020 kimetoa msukumo mkubwa wa ukamilishaji wa ujenzi huo.
Mbali ya MICHANGO ya awali ya Mbunge huyo, amekubali KUNUNUA RANGI ya kupaka ndani na nje ya Majengo 3 hayo ya Vyoo na Jengo la Ofisi za Walimu. Baadhi ya WAZALIWA wa Kata ya Busambara  WANAENDELEA KUCHANGIA ujenzi wa Sekondari ya Kata yao – AHSANTENI SANA!
Wananchi wa Vijiji 3 vya Kata ya Busambara wameandika barua wakiiomba Serikali iwaruhusu Sekondari yao IFUNGULIWE tarehe 13.1.2020 na KUCHUKUA Wanafunzi 142 ya Kata yao waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha kwanza Januari 2020.
(2) Dan Mapigano Memorial Secondary School ya Kata ya Bugoji (Vijiji vya Kanderema, Kaburabura na Bugoji)
Vyumba vipya 5 vya Madarasa na madawati 40 ya kila darasa viko tayari. Ofisi za Walimu zimekamilika. Ujenzi wa VYOO vyote (wasichana, wavulana na walimu) vya shule utakamilika ifikapo Jumatano, 8.1.2020. Kwenye HARAMBEE ya ujenzi huu, Mbunge wao, mbali ya MICHANGO yake ya awali, amechangia tena utengenezaji wa MILANGO mipya 12 ya Vyoo hivyo. Baadhi ya WAZALIWA wa Kata ya Bugoji wamechangia ujenzi wa Sekondari ya Kata yao.
Vijiji 3 vya Kata ya Bugoji vimeiiomba Serikali iwaruhusu Sekondari yao ifunguliwe tarehe 13.1.2020 na KUCHUKUA WANAFUNZI 141 wa Kata hiyo waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza Januari 2020.
KUPUNGUZA MRUNDIKANO WA WANAFUNZI MADARASANI
Vyumba VIPYA vya Madarasa VIZIPOPATIKANA kwenye baadhi ya Sekondari patakuwepo na MRUNDIKANO MKUBWA wa Wanafunzi madarasani mwao:
Bugwema (vyumba vipya 3 vinahitajika), Bulinga (3), Kasoma (3), Nyakatende (2), Nyanja (1) na Rusoli (1).
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ANAFANYA VIKAO VYA HARAMBEE vya kukamilisha ujenzi wa Vyumba VIPYA vinavyohitajika kwenye Sekondari hizo. Baadhi ya WAZALIWA wa Kata zenye upungufu wa Vyumba vya madarasa WANACHANGIA ujenzi huu.
Kwa hiyo, kwa Jimbo la Musoma Vijijini, HAYUPO Mwanafunzi wa Kidato cha kwanza 2020 (3,480 Sekondari za Kata na 22 za Bweni) ATAKAYEBAKI nyumbani kwa sababu ya UKOSEFU wa Vyumba vya Madarasa – muhimu ni kupatikana kwa Vyumba vipya ili kila darasa lichukue Wanafunzi wasiozidi 40.

MICHEZO JIMBONI – UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM YA 2015-2020

Mashindano ya kupiga Kasia yaliyofanyika Kijijini Bukima, tarehe 30.12.2019.

Mashindano ya Kupiga Kasia (AINA MOJAWAPO YA MCHEZO) yaliyofanyika jana (30.12.2019) Kijijini Bukima ni sehemu ya UTEKELEZAJI wa ILANI ya CCM ya 2015-2020.
Mbunge wa Jimbo la la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo AMEAMUA KIVITENDO KUFUFUA Utamaduni na Michezo ya Jimboni mwao iliyokuwa INAFIFIA na kuanza KUTOWEKA.
Kila Mwaka, Mbunge huyo anatayarisha na kufadhili MASHINDANO ya KWAYA (nyimbo) na NGOMA ZA ASILI.
Vilevile, Mbunge huyo ni mmoja wa WAFADHILI wa Timu ya Mpira ya Mkoa wa Mara, BIASHARA UNITED inayoshiriki Ligi Kuu ya Taifa. Ameombwa na kukubali kuna mmoja wa Wafadhili wa WASAGA FC ya Kata ya Nyamrandirira itakayoshiriki Ligi ya Daraja III. Mbunge huyo alishagawa Vifaa vya Michezo Vijijini na Mashuleni.
MASHINDANO YA KUPIGA KASIA 2019 (The Annual Boat Race) – Washindi na Zawadi
Mbunge wa Jimbo ametoa ZAWADI hizi:
MSHINDI 1
Kata ya Murangi
Tsh Milioni 1 & Kikombe
MSHINDI 2
Kata ya Musanja
Tsh 700,000 & Kikombe
MSHINDI 3
Kata ya Suguti
Tsh 400,000 & Kikombe
Mshindi wa Nne
Kata ya Bukima
Mshindi wa Tano
Kata ya Rusoli
ZAWADI ndogo ndogo nazo zilitolewa.
Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wameomba Mbunge wa Jimbo lao AENDELEE kutayarisha MASHINDANO ya kupiga KASIA na ikiwezekana yafanyike mara mbili kwa Mwaka.

MASHINDANO YA KUPIGA KASIA 2019 (THE ANNUAL BOAT RACE)

VIKOMBE vya WASHINDI na T-SHIRT za Washiriki

Jumapili, 29.12.2019
Jimbo la Musoma Vijijini

KIPAUMBELE Na. 5 (Michezo na Utamaduni) cha Jimbo la Musoma Vijijini kinaendelea kutekelezwa na kesho, Jumatatu, 30.12.2019 kuna MASHINDANO YA KUPIGA KASIA Kijijini Bukima, Kata ya Bukima.

MASHINDANO hayo, kama yalivyo ya KWAYA (Nyimbo), NGOMA za ASILI na MPIRA wa MIGUU ni sehemu ya UTEKELEZAJI wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020, ndani ya Jimbo letu (Rejea Kitabu cha Kurasa 110 cha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani hiyo: Januari 2016 – Juni 2019, Jimbo la Musoma Vijijini).

Matayarisho ya MASHINDANO hayo yamekamilika.

MAHALI:
Mwalo (Ufukwe) wa Kijiji cha Bukima

SIKU:
Jumatatu, 30.12.2019

MUDA:
Timu zinazoshindana zitawasili MWALONI (ufukweni) Bukima Saa 2.30 Asubuhi

UKUBWA WA TIMU:
Wapiga kasia 5 kwa kila MTUMBWI (Timu)

USALAMA:
Taratibu za usalama majini (ziwani) zitazingatiwa.

KATA ZILIZOJIANDIKISHA kushiriki kwa ridhaa zao:

(1) Bugwema, (2) Bukima, (3) Bukumi, (4) Bwasi, (5) Etaro, (6) Mugango, (7) Murangi, (8) Musanja, (9) Nyakatende, (10) Rusoli na (11) Suguti

ZAWADI KWA WASHINDI

*Mshindi wa 1
Tsh Milioni 1 & Kikombe

*Mshindi wa 2
Tsh 700,000 & Kikombe

*Mshindi wa 3
Tsh 400,000 & Kikombe

*Kifuta jasho kwa WASHIRIKI ambao hawatashinda: Tsh 50,000 kwa Timu.

SIKUKUU YA KRISMASI KIJIJINI NYASAUNGU – WANAKIJIJI WASISITIZA SEKONDARI YAO KUFUNGULIWA MWAKANI (2020)

Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo akiendesha HARAMBEE ya ujenzi wa Nyasaungu Secondary School

SHEREHE YA KRISMASI Jimbo la Musoma Vijijini imetumika kuboresha UAMUZI  wa Wananchi wa Kijiji cha Nyasaungu wa kuhakikisha SEKONDARI MPYA inayojengwa Kijijini mwao INAFUNGULIWA Mwakani (Februari 2020).
SHEREHE za Eid al Fitr, Krismasi na Pasaka za Jimbo la Musoma Vijijini zinafanywa kwa mzunguko ndani ya Kata zote 21 za Jimbo hili.
Marafiki 2 (na wanafunzi wenzake) wa  Prof Muhongo wa kutoka Jijini Berlin,  Ujerumani (Magharibi) walihudhuria SHEREHE hiyo. Hao ni: Christa Werner (Dr.rer.nat.) na Wolfgang Zils (Dipl Ing, Dipl Geol).
Jimbo la Musoma Vijijini lina Jumla ya Kata 21. Kata 18 tayari zilishajenga Sekondari zao na zinatumika. Kata 3 (Bugoji, Busambara na Ifulifu) zisizokuwa na Sekondari zinakamilisha ujenzi wa Sekondari zao ili zianze kutumika mwakani (2020).
Kwa hiyo, ifikapo Februari 2020 KILA KATA Jimboni itakuwa inayo Sekondari yake. Kutokana na WINGI wa Wanafunzi na UMBALI wa kutembea, baadhi ya Kata zimeanza kujenga Sekondari ya pili kwenye Kata zao. Jumla ya Sekondari za Binafsi Jimboni ni mbili (2).
HARAMBEE YA KRISMASI – Nyasaungu Secondary School
Baada ya Ibada ya Krismasi, Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo aliendesha HARAMBEE ya kuchangia VIFAA VYA ujenzi vitakavyotumika ifuatavyo:
*Vyumba 3 vya Madarasa viezekwe ifikapo tarehe 15.1.2020
*Vyoo vya Wanafunzi  na Walimu vikamilishwe ujenzi wake kabla ya tarehe 30.1.2020
MFUKO wa JIMBO ulishachangia MABATI 54 ya kuezeka chumba kimoja cha darasa.
Tarehe 25.12.2019, Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo alichangia MABATI 54. Hapo awali, Mbunge huyo alishachangia SARUJI MIFUKO 35 na NONDO 20 kwa ajili ya ujenzi wa Sekondari hii.

KRISMASI 2019 – WANAVIJIJI WAFURAHIA ZAWADI YA MAJENBE YA KUKOKOTWA NA NG’OMBE (PLAU)

UTOAJI wa ZAWADI YA KRISMASI ya PLAU kwa VIKUNDI 20 vya KILIMO vya Jimbo la Musoma Vijijini

VIKUNDI 20 VYA KILIMO kutoka VIJIJI 20 ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini WAMEPOKEA KWA FURAHA KUBWA Zawadi ya Krismasi kutoka kwa Mbunge wao, Prof Sospeter Muhongo.
ZAWADI hiyo iliyotolewa tarehe 24.12.2019 kwa kila Kikundi ni PLAU MOJA – Jembe la kukokotwa na ng’ombe moja. Mbunge huyo AMETOA ZAWADI hiyo ikiwa ni ISHARA ya kuanza rasmi KAMPENI ya kupunguza matumizi ya JEMBE la MKONO Jimboni humo.
PLAU hizo zimegawiwa kwenye Vituo 2:
KITUO 1: CHUMWI SENTA – Vikundi kutoka Vijiji vya:
Bukima, Butata, Chimati, Chitare, Chumwi, Mabui Merafuru, Masinono, Mikuyu, Kaburabura, Rusoli, Suguti na Wanyere
KITUO 2: NYASURURA SENTA – Vikundi kutoka Vijiji vya: Kamguruki, Kwibara, Maneke, Mwiringo, Nyakatende, Nyasaungu, Nyegina na Tegeruka.
MADIWANI na Viongozi wengine wa Kata zenye Vijiji vilivyopewa ZAWADI hiyo ya KRISMASI walikuwepo.
Mbunge wa Jimbo aliambatana na rafiki zake wa miaka mingi kutoka Ujerumani ambao wamemtembelea huko Jimboni. Wageni hao, Christa Werner (Dr.rer.nat.) na Wolfgang Zils (Dipl Ing, Dipl Geol) walisoma na Prof Muhongo huko Ujerumani ya Magharibi miaka ya 80.
KRISMASI YA JIMBO (2019)
Itafanyika Kijijini Nyasaungu, Kata ya Ifulifu.
HARAMBEE ya ujenzi wa Nyasaungu Secondary School, IBADA KANISANI na Chakula cha Mchana cha Krismasi (CHRISTMAS LUNCH), vyote vimefanyika Kijijini Nyasaungu,  tarehe 25.12.2019.

VIKUNDI VYA KILIMO KUPEWA ZAWADI YA KRISMASI YA KUBORESHA KILIMO CHAO

Wakulima wa Vijiji vya Bukumi (Kata ya Bukumi) na Kamuguruki (Kata ya Nyakatende) wakiwa mashambani mwao, kwenye Kilimo cha MSIMU huu (2019/2020), kwa kutumia MAJEMBE ya KUKOKOTWA na NG’OMBE (PLAU).

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
Zimebaki siku 2 kabla Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo kukabidhi ZAWADI ya KRISMASI ya PLAU (Majembe ya kukokotwa na Ng’ombe) kwa VIKUNDI VYA KILIMO 18 vya Wakulima ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.
WAKULIMA Jimboni wanaendelea kuhamasika zaidi kwa kutambua umuhimu wa kutumia PLAU (na MATREKTA yakipatikana) badala ya JEMBE LA MKONO.
WAKULIMA wameeleza kuwa, tofauti na kipindi cha nyuma, ambacho Wakulima wengi walikuwa wakitumia Majembe ya Mkono  kwenye kilimo chao, kwa sasa Wakulima walio na MAJEMBE ya NG’OMBE (PLAU) wanatumia majembe hayo kulima eneo kubwa kwa muda mfupi.
Ndugu Majura Mbogora wa Kijiji cha Bukumi ameeleza kwamba Mkulima anaweza kulima EKARI MOJA kwa siku moja kwa kutumia PLAU MOJA wakati kulima shamba hilo hilo kwa kutumia JEMBE la MKONO, siku 5  hadi 7 zinahitajika kwa Familia ya watu wasiopungua watano (5). Hivyo, WAKULIMA wanaona kuna umuhimu wa KULIMA kwa kutumia PLAU ili kupanua ukubwa wa mashamba yao kwa kutumia muda mfupi zaidi.
ZAWADI ZA PLAU KWA VIKUNDI VYA KILIMO
Tarehe 24.12.2019, Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo atatoa ZAWADI YA KRISMASI YA PLAU kwa kila KIKUNDI cha KILIMO kutoka VIJIJI 18. Hii ni sehemu ya KAMPENI ya KUSHAWISHI Wakulima wapunguze kutumia JEMBE la MKONO na waanze kutumia PLAU kwa wingi.
VIONGOZI wa VIKUNDI vya KILIMO 18 vitakavyopewa ZAWADI YA PLAU kwa kila KIKUNDI wanatanguliza SHUKRANI zao za DHATI kwa Mbunge wa Jimbo lao kwa KUENDELEA KUBORESHA KILIMO Jimboni mwao.
Vilevile, WAKULIMA wanamshukuru sana Mbunge wao kwa kuwagawia bure MBEGU za mazao ya ALIZETI, MIHOGO, MTAMA na UFUTA kwa misimu kadhaa ya kilimo chao.
MATREKTA YA MKOPO
Jimbo la Musoma Vijijini lina jumla ya Vyama vya Ushirika vya Msingi vya Mazao (AMCOS) 35. Idara ya Kilimo ya Halmashauri (Musoma DC) yenye Jimbo hili IKO TAYARI kusaidia AMCOS hizo kutayarisha nyaraka za kutafuta MIKOPO ya kununua MATREKTA kwa manufaa ya Wanachama wao.

JUBILEE YA SHULE YA MSINGI MWIRINGO YAFANA NA WANANCHI WAAHIDI KUONGEZA KASI KWENYE UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO YAO

Burudani kutoka kwa Wanafunzi wa S/M Mwiringo katika kusherehekea Jubilee ya shule yao

WANANCHI wa Kijiji cha Mwiringo, Kata ya Busambara WAMEJIWEKEA MALENGO MAPYA YA KUONGEZA KASI YA MAENDELEO YAO:
* Wataongeza kasi ya USHIRIKIANO wao na Serikali kutekeleza Miradi ya Maendeleo kijijini mwao na kwenye Kata yao.
* Wataendelea KUBORESHA MIUNDOMBINU ya Shule ya Msingi Mwiringo. Wameanza kwa kuchanga fedha za kukamilisha ujenzi wa Vyumba 2 vya Madarasa na Ofisi ya Walimu.
* Wamechanga fedha za kukamilisha ujenzi wa Vyoo vya Wavulana kwenye SEKONDARI MPYA ya Kata yao (Busambara Secondary School). Ujenzi wa Vyoo hivyo utakamilika ifikapo tarehe 24.12.2019.

ZAO LA DENGU LAANZA KULIMWA KWENYE BONDE LA BUGWEMA

Ndugu Owiyo na Familia yake wakiwa kwenye palizi ya DENGU. Hapo ni Kijijini Masinono, Kata ya Bugwema.

Jumapili, 15.12.2019
Jimbo la Musoma Vijijini
Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
KATA ya BUGWEMA inayoundwa na Vijiji vinne (4) yaani Muhoji, Masinono, Kinyang’erere na Bugwema ina BONDWE kubwa kwa ajili ya Kilimo cha Mazao ya CHAKULA na BIASHARA. Kilimo kikubwa cha UMWAGILIAJI kitatekelezwa kwenye BONDE hili.
Bonde la BUGWEMA lina ukubwa wa EKARI 5,075 (hekta 2,054)
Mazao makuu ya CHAKULA yanayolimwa BUGWEMA ni: MAHINDI, MIHOGO, MTAMA, MPUNGA, VIAZI VITAMU, MATUNDA na MBOGAMBOGA.
Mazao Makuu ya BIASHARA yanayolimwa BUGWEMA ni: PAMBA, ALIZETI, MPUNGA, MAHINDI na DENGU.
DENGU ni zao JIPYA la CHAKULA na BIASHARA liloanzwa kulimwa BUGWEMA kwa miaka ya karibuni. Ni moja ya MAZAO yatakayoendelea kulimwa kwa wingi kwenye BONDE la BUGWEMA kwenye KILIMO CHA UMWAGILIAJI kitakachoendeshwa na MRADI mkubwa wa Benki ya Kilimo (Tanzania Agricultural Development Bank, TADB) kwa kushirikiana na WANAVIJIJI na HALMASHAURI ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC). Mazao mengine ya MRADI huo ni: MPUNGA, VITUNGUU, MAHINDI, ALIZETI na PAMBA.
Mmoja ya Wakulima wa DENGU kwenye Kijiji cha Masinono, Ndugu Francis Owiyo  amesema kwamba hivi karibuni ameanza kujishughulisha na Kilimo cha DENGU. Vilevile, hulima ALIZETI. Ndugu Owiyo ambaye kwa sasa ameanza kwa kulima Ekari 3 za DENGU, amesema  kuwa zao hilo kwa  kawaida linachukua takribani miezi mitatu  (3) kuwa tayari kwa kuvunwa.
Mkulima huyo amesema KILO 1 ya DENGU huuzwa kwa bei ya Shilingi 800 – 1,000. Ndugu Owiyo anasubiri kwa hamu kubwa MRADI wa Kilimo cha UMWAGILIAJI kwenye BONDE la BUGWEMA. Anakusudia kupanua mashamba yake kwa kutumia ZANA za KISASA za KILIMO zitakazotolewa na Benki ya Kilimo (TADB).
Diwani wa Kata ya Bugwema, Mhe Ernest Magembe ameendelea kushawishi na kushauri wananchi wa Kata hiyo kuhakikisha wanaongeza juhudi kubwa kwenye Kilimo ili kutokomeza NJAA kwenye Kata yao na Jimboni kwa ujumla.
Diwani huyo ameendelea kutoa shukrani za pekee kwa Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo kwa kugawa bure mbegu za MTAMA, MIHOGO, UFUTA na ALIZETI kwa Wakulima wa Kata ya Bugwema na Jimboni kote (Kata 21).
Diwani huyo ameongeza kwa kusema kwamba Wanavijiji wa Kata ya Bugwema ndio WAKULIMA MASHUHURI wa mazao ya ALIZETI na DENGU ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.
HATUTAKI NJAA NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI – TWENDENI SHAMBANI!

MAZAO YA VIKUNDI VYA KILIMO YAPATA KWA URAHISI MASOKO YA NDANI

Kikundi cha NO SWEAT NO SWEET wakiwa na mavuno yao ya MATIKITI. Mfanyabiashara, Ndugu Salha Mohamed ameenda Kijijini Bwasi kununua MATIKI ya Kikundi hicho.

Jumapili, 8.12.2019
Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
KIKUNDI cha NO SWEAT NO SWEET cha Kata ya Bwasi kinaendelea kunufaika na MRADI wa KILIMO baada ya kujifunza kulima mwaka mzima, yaani kwa vipindi vya kiangazi na masika.
Mwenyekiti wa KIKUNDI hiki, Ndugu Goodluck Wambwe ameeleza kuwa wako kwenye KILIMO cha BIASHARA cha Mazao ya MAHINDI, MATIKITI, VITUNGUU na NYANYA.
Kiongozi huyo ameongeza na kusema kwamba, WAMEFANIKIWA KUNUNUA MASHINE YA PILI ya Umwagiliaji.
Vilevile, KIKUNDI hiki KIMEFANIKIWA kufungua AKAUNTI BENKI, kununua SHAMBA jingine, kulipa ADA za masomo ya watoto wao na kuhudumia FAMILIA zao kwa ubora zaidi.
Ndugu Salha Mohamed (pichani), Mfanyabiashara kutoka Kijiji cha Bukima anashukuru sana kwa VIKUNDI vya KILIMO hasa vya UMWAGILIAJI kujitokeza kwa wingi JIMBONI humo na  kulima MAZAO ya BIASHARA.
“Kwa sasa tumepunguza sana gharama za kusafiri nje ya Jimbo letu kwenda kununua MAZAO ya BIASHARA. Bidhaa nyingi tunazipata ndani ya Jimbo letu”, alisema Mfanyabiashara huyo, Ndugu Salha Mohamed.
Ndugu Gustavu Tesha, Kaimu Afisa Kilimo wa Kata ya Bwasi amekuwa akitoa elimu juu ya KILIMO cha UMWAGILIAJI na kufanikiwa kuongeza idadi ya VIKUNDI vya KILIMO cha  UMWAGILIAJI ndani na nje ya Kata hiyo.
Wanachama na Viongozi wa Kikundi cha NO SWEAT NO SWEET wanamshukuru sana Mbunge wao  Profesa Sospeter Muhongo kwa kuwapatia MASHINE ya kwanza ya UMWAGILIAJI. Hiki Kikundi ni moja ya VIKUNDI 15 vilivyopewa MASHINE za UMWAGILIAJI na mbegu Mwaka 2016. Vifaa hivi vilinunuliwa kutoka kwenye Fedha za MFUKO wa JIMBO.
VIKUNDI VYA KILIMO CHA UMWAGILIAJI vinazidi kuongezeka ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.
Tarehe 24.12.2019 (Christmas Eve) Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ATATOA ZAWADI YA KRISMASI ya PLAU (jembe la kukokotwa na ng’ombe) kwa VIKUNDI 14 kutoka VIJIJI 14 vya Jimbo la Musoma Vijijini.

BARAZA LA MADIWANI LAFANYA UAMUZI WA KUJENGA VETA KWENYE HALMASHAURI YAO

Wajumbe wa BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Kikao kilifanyika tarehe (6.12.2019) kwenye Ukumbi wa Kanisa Katoliki Mugango.

BARAZA la MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma  LIMEFANYA UAMUZI MUHIMU kwa Maendeleo ya Wananchi wa Halmashauri hiyo yenye Jimbo la Musoma Vijijini.
JIMBO hilo lina Kata 21, Vijiji 68 na Vitongoji 374.
Shule za Msingi za Serikali ni 111, za Binafsi ni 3 na Shule Shikizi ni 10. Jimbo lina Sekondari za Serikali/Kata 18, za Binafsi 2 na Sekondari Mpya zinazojengwa ni 9. WINGI wa WAHITIMU wa Shule zote hizi WANAHITAJI FURSA ZAIDI za kujiendeleza kiuchumi.
WILAYA ya Musoma yenye Jimbo la Musoma Vijijini na Jimbo la Musoma Mjini inayo VETA MOJA iliyoko Musoma Mjini. Kwa hiyo UAMUZI wa leo (6.12.2019) wa BARAZA la MADIWANI wa Jimbo la Musoma Vijijini UNASTAHILI PONGEZI NYINGI sana – KUPANUA WIGO WA FURSA ZA  WAHITIMU kujiendeleza kiuchumi.
VETA itakayojengwa itazingatia hali halisi ya Sekta Kuu za Uchumi (k.m. Uvuvi, Kilimo na Ufugaji) wa Jimbo la Musoma Vijijini.

WANAVIJIJI WATATHMINI MAENDELEO YA VIJIJI VYAO YA MWAKA HUU (2019)

KIKAO cha tarehe 4.12.2019 cha Viongozi wa MABARAZA ya WAZEE kijijini Suguti. TATHMINI za WANAVIJIJI za UCHUMI na MAENDELEO ya VIJIJI vyao kwa MWAKA huu (2019) ziliwasilishwa.

Jumatano, tarehe 4.12.2019, VIONGOZI wa MABARAZA ya WAZEE ya Ushauri, Ushawishi, Utamaduni na Maadili ya VIJIJI waliwasilisha TATHMINI za MIRADI YA UCHUMI na MAENDELEO ya VIJIJI vyao.
KIKAO hicho kilifanyika Kijijini SUGUTI chini ya Uenyekiti wa Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo.
TATHMINI za Vijiji zimewasilishwa na Mwenyekiti na Katibu wa Baraza la kila Kijiji. Jimbo lina Kata 21 na Vijiji 68. KIKAO cha VIONGOZI wa MABARAZA ya KATA kitakafanyika baadae.
TATHMINI zilifanyika kwenye SEKTA za: (i) Elimu, (ii) Afya, (iii) Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, (iv) Mazingira na (v) Michezo na Utamaduni. Vilevile, TATHMINI zimeongelea MIRADI ya maji, umeme, barabara, vyombo vya  usafirishaji na mawasiliano.
MAAZIMIO:
Baada ya uwasilishi na mjadala kukamilika, yafuatayo ni MAAZIMIO yatakayofikishwa Vijijini kwa UTEKELEZAJI:
(1) Hakuna Wanafunzi kusomea CHINI ya MITI. Kila Shule kijijini iwe na Vyumba vya Madarasa ya kutosha. MABARAZA yatashawishi na kushauri kazi hii ikamilike ifikapo 30 Juni 2020.
(2) MABARAZA yatashawishi na kushauri UPANDAJI wa MITI kwa WINGI kwa kila Kijiji. MICHE ya BURE inapatikana kwa Mkuu wa Wilaya (DC) ya Musoma.
(3) MABARAZA yatashawishi na kushauri Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kuunda VIKUNDI vya UCHUMI na kuomba MIKOPO kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Musoma yenye Jimbo la Musoma Vijijini.
(4) MABARAZA yatashawishi na kushauri WAKULIMA na WAFUGAJI kuunda VIKUNDI VYA KILIMO vya kutumia PLAU (majembe ya kulimia yanayokokotwa na ng’ombe).
ZAWADI YA KRISMASI YA PLAU KWA VIKUNDI VYA KILIMO
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ATATOA ZAWADI YA PLAU (tarehe 24.12.2019) kwa VIKUNDI VYA KILIMO vilivyokuwa vya kwanza kuundwa na kuanza kazi.
VIKUNDI hivyo vinatoka Vijiji (14) vya: Bukima, Butata, Chitare, Chumwi, Kamguruki, Kwibara, Mabui Merafuru, Nyakatende,  Nyegina, Mikuyu, Rusoli, Suguti, Tegeruka na Wanyere.

SEMINA ELEKEZI NA MIKOPO ISIYOKUWA NA RIBA YA TSH 116.5 MILIONI VYATOLEWA KWENYE HALMASHAURI YA WILAYA YA MUSOMA (MUSOMA DC)

Jumatatu, tarehe 2.12.2019 HALMASHAURI YA WILAYA YA MUSOMA yenye Jimbo la Musoma Vijijini ILITOA SEMINA ELEKEZI kwa WENYEVITI WAPYA wa Vijiji juu ya UENDESHAJI WA SERIKALI ZA VIJIJI.
SEMINA hiyo imehudhuriwa na Wenyeviti 64 kati ya 68 (Mahudhurio 94.12%, Wenyeviti 4 wameomba udhuru).
Baadhi ya masuala muhimu yaliyotolewa MAFUNZO ni juu ya: Sheria ya Serikali za Mitaa, Muundo wa Serikali (Halmashauri) ya  Kijiji, Kamati za Halmashauri ya Kijiji na Majukumu yake, Vikao/Mikutano (Wajumbe wake na Kazi zake), Utungaji wa Sheria ndogo ndogo za Kijiji, Vyanzo vya Mapato, Majukumu ya Mwenyekiti, Taratibu za kumuondoa madarakani Mwenyekiti wa Halmashauri wa Kijiji, n.k. Fursa iliyotolewa ya KUULIZA MASWALI.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Musoma Vijijini, Ndugu Nyabukika Bwire Nyabukika ALIKARIBISHWA kutoa salamu za CHAMA kwa WENYEVITI hao. MGENI RASMI alikuwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo.
SEMINA ELEKEZI kwa WENYEVITI wa VITONGOJI 374 wa Halmashauri hii itatolewa siku chache zijazo.
TSH 116.5 MILIONI – MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WATU WENYE ELEMAVU, VIJANA NA WANAWAKE
Halmashauri ya Wilaya ya Musoma chini UONGOZI WENYE UBUNIFU MKUBWA wa Mkurugenzi Mtendaji (DED), Ndugu John Kayombo, leo (2.12.2019) IMETOA MIKOPO YA TSH MILIONI 116.5 kwa Makundi hayo matatu.
IKUMBUKWE kwamba hii ROBO YA KWANZA YA MWAKA WA FEDHA wa 2019/2020 na tayari HALMASHAURI hii INATEKELEZA KWA VITENDO UTOAJI wa MIKOPO kama ilivyoagizwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020.
*MIKOPO KWA WATU WENYE ULEMAVU
Vikundi 3 vyenye Jumla ya Wanachama 45 vimepewa Jumla ya  Tsh Milioni 15. Vikundi hivyo vinatoka Vijiji vya Bukima, Murangi na Nyambono.
*MIKOPO KWA VIKUNDI VYA VIJANA
Vikundi 4 vyenye Jumla ya Wanachama 78 vimepewa Jumla ya Tsh Milioni 21. Vikundi hivyo vinatoka Vijiji vya Lyasembe, Maneke, Kataryo na Kisiwa cha Rukuba.
*MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANANAWAKE
Vikundi 16 vyenye Jumla ya Wanachama 285 vimepewa Jumla ya Tsh Milioni 80.5. Vikundi hivyo vinatoka Vijiji vya Murangi (3), Tegeruka (2), Kwikuba (2), Bukima (1), Bujaga (1),  Saragana (1), Kwibara (1), Kataryo (1), Bwai Kwitururu (1), Busungu (1), Mayani (1) na Kome (1). MGENI RASMI alikuwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo.
Utoaji wa MIKOPO ISIYOKUWA NA RIBA ni endelevu. Vipo VIKUNDI vilivyopewa Mikopo Mwaka wa Fedha wa 2018/2019 na vingine BADO VITAPEWA mikopo ndani ya Mwaka huu wa Fedha (2019/2020)
WENYEVITI wa Serikali ya Vijiji, VIKUNDI vilivyopokea MIKOPO isiyokuwa na RIBA, na VIONGOZI mbalimbali Waliohudhuria shughuli hizi mbili WAMETOA SHUKRANi nyingi za dhati kwa Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt John Pombe Joseph Magufuki na Viongozi wengine wa Chama na Serikali kwa kuunga mkono juhudi za Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini kwenye Utekelezaji wenye MAFANIKIO MAKUBWA wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM (2015-2020) ndani ya Jimbo lao.

KUANZA KWA MRADI WA UJENZI WA BARABARA YA LAMI YA MUSOMA-MAKOJO- BUSEKELA

kazi zinazoendelea kwenye ujenzi wa Barabara ya LAMI ya Musoma-Makojo-Busekela

AHADI ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt John Pombe Joseph Magufuli yaanza kutekelezwa kwenye Jimbo la Musoma Vijijini. Mhe Rais alitoa AHADI hii wakati wa Kampeni za UCHAGUZI wa 2015 akiwa Kijijini Kabegi, Kata ya Ifulifu.
BARABARA ya Musoma-Makojo-Busekela yenye urefu wa kilomita 92 imeanza KUJENGWA kwa kiwango cha LAMI. Ujenzi umeanzia kwenye LOT II (Kusenyi-Makojo -Busekela). LOT I ni Musoma-Mugango-Kusenyi.
Kuanza kwa MRADI wa ujenzi wa Barabara hii muhimu sana kwa UCHUMI na MAENDELEO ya Wilaya ya Musoma ni kielelezo na kithibitisho kingine cha MAFANIKIO ya UTEKELEZAJI wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020 ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.
Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21, Vijiji 68 na Vitongoji 374 linajishughulisha na KILIMO (mazao makuu: mihogo, mahindi, mpunga, viazi vitamu, matunda, mbogamboga,  pamba na alizeti), UVUVI (sangara, sato, dagaa, n.k.), UFUGAJI (ng’ombe, mbuzi, kondoo na kuku) na UCHIMBAJI MADINI (dhahabu).
Kwa hiyo BIDHAA za aina mbalimbali za kutoka Musoma Vijijini zitafika kwa uharaka na ubora wake kwenye MASOKO tarajiwa.
WANANCHI na VIONGOZI wa Wilaya ya Musoma yenye Jimbo la Musoma Vijijini WANAENDELEA kutoa SHUKRANI zao za DHATI kwa Mhe Rais wao, Mhe Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa kutimiza AHADI aliyoitoa Jimboni mwao – ujenzi wa barabara ya LAMI.

MBUNGE MLEZI APANGA HARAMBEE ZA MIRADI YA MAENDELEO

MATUKIO mbalimbali ya KAMPENI za leo (21.11.2019) Jimboni BUTIAMA kwenye Kata za Busegwe na Nyankanga. MGENI RASMI alikuwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo ambae ni Mlezi wa Jimbo la Butiama.

Leo, Alhamisi, 21.11.2019, MLEZI wa Jimbo la BUTIAMA, Prof Sospeter Muhongo AMESHIRIKI KAMPENI kwenye Kata 2 za Jimbo la BUTIAMA. Viongozi wa CCM (na Jumuiya zake) wa ngazi za Wilaya, Kata na Vijiji wameshiriki Kampeni hizo wakiongozwa na Ndugu Yohana Mirumbi, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Butiama.
KAMPENI hizo zimefanyika kwenye Kata za BUSEGWE (Vijiji 3) na NYANKANGA (Vijiji 2).
MLEZI wa Jimbo hilo ambae ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini amewakumbusha WAGOMBEA wa CCM na WANANCHI VIPAUMBELE vilivyo kwenye DIRA yetu ya MAENDELEO na umuhimu wa KUTEKELEZA ILANI ya Uchaguzi ya CCM (2015-2020) kwa umakini mkubwa.
WAGOMBEA wa CCM wakiongozwa na Wenyeviti wa Vijiji 5 vya Kata hizo mbili, WAMEAHIDI kuanza na kuendeleza utekelezaji wa MIRADI ya MAENDELEO kwa kasi kubwa baada ya Uchaguzi wa tarehe 24.11.2019.
WANANCHI na WAGOMBEA wa CCM wamepanga kupiga HARAMBEE, tarehe 28.11.2019 ya kuendeleza ujenzi wa SEKONDARI ya Kata ya Busegwe.
Tarehe 30.11.2019, WANANCHI na WAGOMBEA wa CCM wamepanga kupiga HARAMBEE ya kupanua Shule SHIKIZI ya Nyabange iwe SHULE ya MSINGI yenye Shule ya Awali hadi Darasa la VII.

MBUNGE WA JIMBO ATUMIA SIKU ZA KAMPENI KUHAMASISHA UKAMILISHWAJI WA UJENZI WA SEKONDARI MPYA

Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo akieleza MAFANIKIO kutoka kwenye UTEKELEZAJI wa Ilani ya CCM kwa muda wa MIAKA 3 na NUSU (Jan 2016-Juni 2019). Alitumia FURSA hiyo kuhimiza ukamilishwaji wa ujenzi wa Sekondari MPYA za Kata za Bugoji na Busambara.

WANAVIJIJI wa Kata za BUGOJI na BUSAMBARA wamehimizwa kukamilisha ujenzi wa Sekondari zao ili zianze kuchukua Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza (Form I) mwakani, Januari 2020.
Hadi kufikia leo (20.11.2019). Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo tayari ametembelea Kata 20 kati ya Kata 21 za Jimbo hilo AKIELEZA MAFANIKIO yaliyokwishapatikana kutoka kwenye UTEKELEZAJI wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM (2015-2020). Amefanya VIKAO vya ndani (na nje kwa baadhi ya Kata) na WAGOMBEA wa CCM wa ngazi zote kwenye Kata zote hizo 20 na moja iliyobaki ataikamilisha baada ya kutoka kazini kwenye Jimbo la Butiama.
DAN MAPIGANO MEMORIAL SECONDARY SCHOOL (Kata ya Bugoji)
VILIVYOKAMILIKA:
*Vyumba 5 vya Madarasa
*Madawati 40 kila Darasa
*Ofisi 2 za Walimu
*Viti na Meza za Ofisi za Walimu
UJENZI UTAKAOKAMILIKA KABLA YA TAREHE 15 DEC 2019:
*Matundu 10 ya Vyoo vya Wasichana
*Matundu 10 ya Vyoo vya Wavulana
*Matundu 2 ya Vyoo vya Walimu
*MAABARA 3 (Physics, Chemistry & Biology)
*NYUMBA ya Mwalimu Mkuu
NB: Mfuko wa Jimbo umechangia ujenzi huo (Kata  ya Bugoji) SARUJI MIFUKO 290 na NONDO 100.
BUSAMBARA SECONDARY SCHOOL (Kata ya Busambara)
VILIVYOKAMILIKA:
*Vyumba 4 vya Madarasa
*Madawati 40 kila Darasa
UJENZI UTAKAOKAMILIKA KABLA YA TAREHE 15 DEC 2019
*Ofisi 3 za Walimu (Viti na Meza zake)
*Matundu 8 ya Vyoo vya Wasichana
*Matundu 6 ya Vyoo vya Wavulana
*Matundu 2 ya Vyoo vya Walimu
*MAABARA 3 (Physics, Chemistry & Biology)
*NYUMBA ya Mwalimu Mkuu
NB: Mfuko wa Jimbo umechangia ujenzi huo (Kata ya Busambara) SARUJI MIFUKO 290 na NONDO 100.

PROF MUHONGO AZINDUA KAMPENI ZA UCHAGUZI NA KUSISITIZA UKAMILISHWAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

Jumapili, tarehe 17.11.2019, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo AMEZINDUA Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwenye KATA ya KIRIBA yenye Vijiji 3.
Mbali ya kuelezea MAFANIKIO yaliyopatikana kwa UTEKELEZAJI MZURI wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM (2015-2020) ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Muhongo AMEWASHAWISHI Wananchi wa Kata ya Kiriba KUONGEZA KASI ya kutekeleza Miradi yao ya Maendeleo kwa kushirikiana na SERIKALI yao na Wadau wengine wa Maendeleo.
WAGOMBEA wa CCM wa nafasi mbalimbali za uongozi wa Serikali za Mitaa WAMEAHIDI kushirikiana vizuri na WANANCHI, SERIKALI na WADAU wengine wa Maendeleo KUKAMILISHA Miradi iliyopo na KUANZA Miradi mipya.
VIONGOZI Wateule wa Kata ya Kiriba WAMEAHIDI kuongeza kasi ya Ukamilishwaji wa MAABARA 3 (Physics, Chemistry and Biology) za Kiriba Secondary School. Kila Kijiji kitakamilisha Maabara moja.
VIONGOZI Wateule wa Kata ya Kiriba WAMEAHIDI kuharakisha ujenzi wa Vyumba VIPYA vya Madarasa na kwamba HAKUNA WANAFUNZI KUSOMEA CHINI YA MITI ndani ya Kata hiyo.
Kijiji cha Chanyauru ndicho pekee hakina Zahanati ndani ya Kata ya Kiriba. VIONGOZI Wateule wa Kijiji hicho WAMEAHIDI kuongeza kasi ya ujenzi wa Zahanati yao.
UZINDUZI wa Kampeni wa Kata ya Kiriba UMEFANIKIWA SANA kwani VIONGOZI mbalimbali wa CCM na WAGOMBEA wateule wa CCM wamesisitiza umuhimu wa USHIRIKIANO MZURI kwenye UTEKELEZAJI wa Miradi yao ya Maendeleo.

WANANCHI WAAMUA KUUNGANA NA SERIKALI KWENYE UJENZI WA HOSPITAL YA  WILAYA

SARUJI (Mifuko 100) iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo kwaajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya

Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea KUTOA SHUKRANI  zao za DHATI kwa SERIKALI yao kwa kuwapatia Tsh Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Kijijini Suguti kwenye Kitongoji cha Kwikonero.
WANANCHI wa Vijiji vyote 68 vya Jimbo la Musoma Vijijini WAMEKUBALI kuchangia Tsh Milioni 2 kila KIJIJI ili kuharakisha ukamilishwaji wa ujenzi wa HOSPITALI hiyo.
Hadi leo hii, 13.11.2019 MAJENGO yafutayo yako kwenye hatua ya ukamilishwaji:
(i) OPD, (ii) Pharmacy, (iii) X-Ray, (iv) Maabara, (v) Wadi la Mama&Mtoto, (vi) Utawala, (vii) Ufuaji (laundry)
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ameungana na WANANCHI wenzake wa Jimboni mwao kuchangia ujenzi huu na leo amechangia SARUJI MIFUKO 100.
MAFANIKIO ya kazi nzuri za MRADI huu yanatokana na UONGOZI na USIMAMIZI mzuri na wenye ubunifu mkubwa wa Mkuu wa Wilaya, Dr Vicent Anney Naano, Mkurugenzi Mtendaji (DED), Ndugu John Lipesi Kayombo pamoja Wafanyakazi kwenye Ofisi zao.
HONGERENI SANA WANANCHI NA VIONGOZI WA MUSOMA DC.

SEKONDARI MPYA MBILI (2) NI LAZIMA ZIKAMILIKE LA SIVYO MSONGAMANO MADARASANI HAUTAEPUKIKA

DAN MAPIGANO MEMORIAL SECONDARY SCHOOL ya Kata ya BUGOJI (Vijiji vya Kaburabura, Kanderema na Bugoji) kazi ya ufyatuaji wa MATOFALI kwaajili ya ujenzi wa MATUNDU ya VYOO na VYUMBA vya MAABARA 3 inaendelea.

Jimbo la Musoma Vijijini lenye Vijiji 68 na Vitongoji 374 lina SEKONDARI 18 za Kata /Serikali na SEKONDARI 2 za Binafsi (Madhahebu ya Katoliki & SDA).
WANAVIJIJI kwa kushirikiana na SERIKALI yao na WADAU wengine wa Maendeleo wanajenga SEKONDARI MPYA 9.
MATOKEO ya MITIHANI ya Darasa la VII ya Mwaka huu (2019) YANATULAZIMISHA KUONGEZA SEKONDARI MPYA 2-3 ili KUEPUKA MSONGAMANO wa Wanafunzi wa Kidato  cha Kwanza (Form I) kwenye SEKONDARI 18 zilizopo.
UFAULU WA KATA ZISIZOKUWA NA SEKONDARI ZAO
*Kata ya BUGOJI 141
*Kata ya NYAMBONO 149
(Nyambono Secondary School ni ya Kata 2: Nyambono & Bugoji)
*Kata ya BUSAMBARA 142
*Kata ya IFULIFU 130
(Kijiji cha Nyasaungu, Kata ya Ifulifu kinajenga Sekondari yake chenyewe, Wamefaulu 55)
WANAFUNZI wa Sekondari wa Kata ya BUGOJI (Vijiji 3) WANAENDA masomoni kwenye Sekondari ya Kata ya NYAMBONO (Vijiji 3). Kwa hiyo Mwakani (Januari 2020) JUMLA YA WANAFUNZI 290 wanapaswa kuanza Form I hapo Nyambono Secondary School! MSONGAMANO na MRUNDIKANO wa HALI JUU! TUSIKUBALI!
SULUHISHO: Dan Mapigano Memorial Secondary School IKAMILIKE HARAKA na Januari 2020 ichukue Wanafunzi wa Form I:
(i) Vyumba Vipya 5 vya Madarasa vimeishakamilika
(ii) Madawati  200 tayari yamewekwa Madarasani
(iii) Ofisi Mpya 2 za Walimu zimekamilika
(iv) Ujenzi wa Vyoo Matundu 10 ya Wanafunzi na 2 ya Walimu UTAKAMILIKA ndani ya WIKI MOJA ijayo.
(v) Ujenzi wa Maabara 3 (Physics, Chemistry na Biology) UNAENDA KWA KASI..msingi umejengwa na matofali yanafyatuliwa. Ujenzi utakamilika Disemba 2019.
(vi) Ujenzi wa Nyumba ya Walimu (two in one) umeanza, utakamilika Disemba 2019.
FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO (Saruji Mifuko 290 na Nondo 100) umeongeza kasi ya UKAMILISHAJI wa MAJENGO ya Dan Mapigano Memorial Secondary School.
MAKTABA ya KISASA itajengwa hapo Shuleni Mwakani (2020). Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo AMEAHIDI kuendesha HARAMBEE ya ujenzi huo na AMEAHIDI kujaza VITABU kwenye MAKTABA hiyo ya MFANO.
WALIOTOA AHADI YA KUCHANGIA ujenzi wa Dan Mapigano Memorial Secondary School WANAOMBWA WAKAMILISHE AHADI ZAO.
TAARIFA za ujenzi wa Sekondari Mpya za BUSAMBARA (inajengwa na Kata yenye Vijiji 3) na  NYASAUNGU (inajengwa na Kijiji kimoja cha Nyasaungu), nazo ZITATOLEWA.

VIKUNDI VYA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI VYACHANGAMKIA MIKOPO KUTOKA JAMII IMPACT LIMITED

UZINDUZI wa OFISI ya JAMII IMPACT LIMITED kwenye eneo la Kanisa la Mennonite (KMT), Nyabange.

Taasisi ya JAMII IMPACT Limited inatoa huduma ya MIKOPO kwa VIKUNDI vinavyojishughulisha na MIRADI ya KI-UCHUMI vikiwemo VICOBA vilivyo na utaratibu wa kununua hisa na kukopeshana.
VIKUNDI kadhaa vya Jimbo la Musoma Vijijijini kutoka Kata za Nyambono, Suguti, Kiriba, Ifulifu na Nyakatende VIMEJITOKEZA na kutuma maombi yao.
Kikundi cha TUMAINI VICOBA GROUP cha Kata ya Kiriba KIMETIMIZA MASHARTI ya Ombi la MKOPO wao. Kikundi hiki chenye WANACHAMA 30 kinajihusisha na shughuli za kilimo, ufugaji, uvuvi na biashara. Fedha za MKOPO zitatolewa kwa ajili ya shughuli za ki-uchumi za Kikundi hiki.
JAMII IMPACT LIMITED inakaribisha  VIKUNDI vingine kupeleka MAOMBI yao ya MIKOPO kwenye OFISI zao  zilizopo NYABANGE KMT Mission, Musoma.
Kwa MAELEZO zaidi, Wasiliana na:
Ndugu William Mdemu
Namba: 0658218673 / 0758208673
Afisa Mikopo (Jamii Impact Limited)

MBUNGE WA JIMBO AENDELEA KUCHANGIA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

MAKABIDHIANO ya PRINTER MPYA Ofisini kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Musoma Vijijini. Msaidizi wa Mbunge, Ndugu Fedson Masawa (kushoto) alimkabidhi Katibu wa CCM Wilaya, Ndugu Stephen Koyo (wa pili kushoto) PRINTER MPYA iliyonunuliwa na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.

Leo, Jumatano, tarehe 23.10.2019, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, AMENUNUA PRINTER MPYA kwa ajili ya matumizi kwenye OFISI ya CCM ya Wilaya ya MUSOMA VIJIJINI. Hapo awali aliinunulia Ofisi hii COMPUTER MPYA.
Vifaa hivyo ni muhimu sana kwa wakati huu wa matayarisho ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 24.11.2019.
Vilevile, Mbunge huyo AMECHANGIA JUMLA ya LITA 400 (mia nne) za Dizeli kwa ajili ya ZIARA za shughuli za UCHAGUZI za Kamati ya Siasa na Sekretariati ya CCM ya Wilaya ya Musoma Vijijini.
CCM Wilaya ya BUTIAMA imepokea JUMLA ya LITA 300 za Dizeli kutoka kwa Prof Sospeter Muhongo ikiwa ni MCHANGO wake kwa ajili ya matayarisho ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Wilayani BUTIAMA.
CCM Mkoa imechangiwa LITA 200 za Diseli na Prof Sospeter Muhongo. MAFUTA haya ni kwa ajili ya Ziara za Viongozi wa Mkoa kwenye shughuli za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

MAHAFALI YA DARASA LA VII YATUMIKA KUBORESHA MIUNDOMBIMU YA SHULE 2 ZA MSINGI

Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo AKIKABIDHI Saruji Mifuko 100 na Fedha taslimu na Milango 2 (Tsh 300,000) kwenye S/M Nyaminya A & B Kijijini Tegeruka, Kata ya Tegeruka.

23 Oktoba 2019
Jimbo la Musoma Vijijini
MAHAFALI ya Darasa la VII ya tarehe 23.08.2019 ya Shule za Msingi Nyaminya A na B yametumika kuharakisha ujenzi wa Vyumba vipya vya Madarasa na Ofisi za Walimu za Shule hizo mbili zilizoko Kijijini Tegeruka, Kata ya Tegeruka.
MGENI RASMI wa MAHAFALI hiyo alikuwa Ndugu SHAIBU NGETICHA, Katibu wa CCM wa Mkoa wa Mara.
MATOKEO YA MITIHANI ya Wahitimu hao ni haya hapa – haya ni kwa Watahiniwa wasiozidi 40 ndani ya Darasa (S/M Nyaminya A&B zilikuwa na Watahiniwa chini ya 40).
(i) S/M Nyaminya A
*Imeshika nafasi ya KWANZA (1) kwenye Kata yao yenye Jumla ya Shule za Msingi 6.
*Imeshika nafasi ya 3 kati ya Shule za Msingi 26 za Halmashauri ya Musoma yenye Jimbo la Musoma Vijijini
*Imeshika nafasi ya 44 kati ya Shule 158 za Mkoa wa Mara
*Imeshika nafasi ya 2,576 kati ya Shule 7,102 Taifa
Kumbuka haya MATOKEO ni kwa Watahiniwa wasiozidi 40 ndani ya Darasa.
(ii) S/M Nyaminya B
*Imeshika nafasi ya 3 kwenye Kata yao.
*Imeshika nafasi ya 14 Wilayani
*Imeshika nafasi ya 120 Mkoani Mara
“Imeshika nafasi ya 5,562 Taifa
Kumbuka haya MATOKEO ni kwa Watahiniwa wasiozidi 40 ndani ya Darasa.
Jana, tarehe 23.10.2019, Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ALITIMIZA AHADI yake ILIYOTOLEWA kwenye HARAMBEE ya tarehe 23.08.2019 iliyofanyika wakati wa MAHAFALI ya Darasa la VII wa Shule hizo mbili.
Mbunge huyo ALITOA SARUJI MIFUKO 100 (kila Shule Mifuko 50) na MLANGO 2 yenye thamani ya Tsh 300,000 (kila Shule Mlango 1)

SERIKALI YATOA TSH MILIONI 100 KUJENGA NYUMBA ZA WALIMU KWA KUSHIRIKIANA NA NGUVUKAZI ZA WANAVIJIJI

Ujenzi wa Nyumba 4 za Walimu kwenye Sekondari ya Tegeruka

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
UJENZI wa Nyumba nne (4) za Walimu katika Shule ya Sekondari Tegeruka iliyopo Kata ya Tegeruka umefikia hatua nzuri.
SERIKALI yetu ilitoa Tsh Milioni 100 na Wananchi wa Kata ya Tegeruka, yenye Vijiji vya Kataryo, Mayani na Tegeruka wanachangia NGUVUKAZI zao kwenye MRADI huu. Wanasomba mawe, kokoto, mchanga na maji ya ujenzi.
Nyumba mbili (2) zimeezekwa bado kupiga lipu na sakafu. Nyumba moja (1) imepauliwa tayari kwa kuezekwa na nyumba ya nne mafundi wanamimina lenta ya juu. Vyoo navyo vinajengwa.
Akizungumza na Msaidizi wa Mbunge, Mkuu wa Shule ya Sekondari Tegeruka, Mwalimu Anton Helege James alisema Sekondari yake ina uhitaji wa Nyumba 17, za Walimu, zilizopo ni 3 na inaupungufu wa Nyumba 14. Hivyo kukamilika kwa Nyumba hizo 4 kutasaidia kupunguza idadi ya Walimu wa Sekondari hiyo wanaofundisha na kuishi mbali na Shule.
WANANCHI na VIONGOZI wao wa ngazi zote hadi Wilayani na Mkoani, akiwemo Mbunge wao, WANAISHUKURU sana SERIKALI yao kwa msaada huu mkubwa wa kuanza kutatua kero ya MAKAZI ya WALIMU wa Sekondari yao.
Kuna UPUNGUFU wa Walimu wa Masomo ya Sayansi kwani kwa sasa Shule ina Walimu wa:- Physics 1, Biology 1, Chemistry 2 na Maths 2.
Mwalimu Mkuu huyo ameendelea kueleza na kusema kwamba wapo Walimu wengine 3 wa Kujitolea wa Masomo ya Sayansi – hawa wanalipwa POSHO na Wazazi wenye Watoto hapo Shuleni. Bado kuna upungufu wa Walimu wa English Geography na Maths.
Mbali ya kumshukuru Mbunge wa Jimbo kwa kuwapatia Vitabu vingi vya Masomo ya Sayansi na Kiingereza, Mwalimu Mkuu huyo amemuomba Mbunge huyo awasaidie kupata Walimu wengine wa kujitolea. Vilevile, ameomba HARAMBEE ifanyike Disemba 2019 kwa ajili ya ujenzi wa Maabara 3 za Masomo ya Sayansi. Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo amekubali kushirikiana na Shule na Wananchi wa Kata ya Tegeruka kwenye ujenzi na uboreshaji wa Miundombinu ya Elimu ya Tegeruka Secondary School.

RATIBA YA KUMBUKIZI YA BABA WA TAIFA 

Mgeni Rasmi, Mhe Jaji Joseph Sinde Warioba akitoa zawadi mbalimbali kwa Washindi wa Ngojera na Hotuba za Baba wa Taifa

Kila siku, kuanzia tarehe 08 Okt hadi 14 Okt kuna MASHINDANO ya Michezo mbalimbali ikiwemo riadha, mpira wa pete na miguu, bao na baiskeli. Kwaya na Ngoma za Asili nazo zipo.
Jumamosi, 12.10.2019, Makumbusho ya Mwalimu Nyerere Butiama chini ya Uongozi wa Mkurugenzi wake, Ndugu Emmanuel Kiondo walitayarisha MASHINDANO ya Shule za Msingi na Sekondari ya NGONJERA na HOTUBA ZA BABA WA TAIFA yakipima viwango vya vipaji vya Wanafunzi hao kwenye KUMBUKUMBUKU ya kazi za Baba wa Taifa. Vilevile kwenye kuelezea WASIFU wake.
Mgeni Rasmi wa Mwaka huu (2019) ni Jaji Joseph Sinde Warioba. Wageni wengine ni Ndugu Philip Mangula na Ndugu Stephen Masato Wasira.
 MATUKIO mbalimbali yamefanyika Mwitongo, eneo la Makumbusho ya Mwalimu Nyerere.

SERIKALI YAENDELEA NA MATAYARISHO YA MRADI MKUBWA WA MAJI NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Wataalamu wakipima Eneo ambalo TANKI la usambazaji MAJI litajengwa.

MRADI WA MAJI WA MAZIWA MAKUU
Timu ya WATAALAMU wa MAJI kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Ofisi ya Wilaya ya RUWASA (Wakala wa Maji Vijijini) WAMEANZA HATUA YA PILI ya Utekelezaji wa MRADI  huu, ambayo ni UPIMAJI wa Maeneo ambapo MIUNDOMBINU ya USAMBAZAJI MAJI itajengwa ndani ya VIJIJI 33 vya Jimbo la Musoma Vijijini.
VIJIJI hivyo 33  vilivyoko karibu na Ziwa Viktoria ndivyo vitakuwa vya kwanza
kusambaziwa MAJI ya MRADI huu.
WATAALAMU hao wameanza kazi zao kwenye Vijiji vya Kurukerege na Mkirira, Kata ya Nyegina. Diwani wa Kata hiyo, Mhe Rajabu Majira Mchele aliambatana na Wataalamu hao walipokuwa kazini kwenye Kata yake.
Kazi zinaendelea kwenye Vijiji 33 vya Jimbo la Musoma Vijijini vilivyoko kwenye MRADI wa MAJI wa MAZIWA MAKUU.
SERIKALI INATIMIZA AHADI YAKE YA KUSAMBAZA MAJI SAFI NA SALAMA VIJIJINI – Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kuiomba SERIKALI yao ikamilishe MRADI huo mapema iwezekanavyo.

KARIBU TUKAMILISHE MAJENGO YA DAN MAPIGANO MEMORIAL SECONDARY SCHOOL

Moja ya majengo yanayokamilishwa sasa ni pamoja na Vyoo vya Wanafunzi na Waalimu

Wananchi wa Kata ya Bugoji WANASHIRIKIANA vizuri sana na SERIKALI yao, na WADAU wengine wa Maendeleo, akiwemo Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo,  KUHAKIKISHA kwamba Sekondari yao ya Kata inafunguliwa Januari 2020.
Vilevile, WAZALIWA wa Kata ya Bugoji yenye Vijiji 3 (Kaburabura, Kanderema na Bugoji) WANAENDELEA KUCHANGIA ujenzi wa Sekondari hiyo iliyoanza kujengwa Disemba 2018.
Kata hiyo HAINA SEKONDARI, kwa hiyo Watoto wao wanatembea umbali usiopungua kilomita 4 kwenda masomoni kwenye Sekondari ya Kata jirani (Nyambono). Hivyo, Nyambono Secondary School ina msongamano mkubwa madarasani kwa Wanafunzi kutoka Kata 2 hizo (Nyambono na Bugoji).
MAJENGO YALIYOKAMILISHWA
* Vyumba 5 vya Madarasa
* Ofisi 2: Mwalimu Mkuu (1) na Walimu (1)
MAJENGO YANAYOKAMILISHWA
* Vyoo vya Wanafunzi na Walimu (misingi tayari imejengwa)
* Maabara:  (misingi inachimbwa)
Diwani wa Kata Mhe Ibrahimund Malima, Mtendaji wa Kata, Ndugu Edina Kurata na Kamati ya Ujenzi WAMEFANIKIWA SANA kuhamasisha Wananchi wa Kata ya Bugoji kushiriki kwa hamasa kubwa kwenye MRADI huu unaotekelezwa kwa kasi kubwa.
KARIBU TUKAMILISHE Majengo ya “Dan Mapigano Memorial Secondary School” ili IFUNGULIWE na kuanza kutoa ELIMU ya SEKONDARI Januari 2020.

KARIBUNI TUKAMILISHE UJENZI WA BUSAMBARA SECONDARY SCHOOL

ujenzi wa Vyoo vya Wanafunzi. Majengo ya rangi nyeupe ni Vyumba vya Madarasa, na kulia ni Jengo la Utawala.

Leo, Jumatano, 09.10.2019, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo AMEFANYA UKAGUZI MWINGINE ndani ya mwezi mmoja, wa ujenzi wa Busambara Secondary School ya Kata ya Busambara.
MAJENGO YANAYOPASWA KUKAMILISHWA
* Vyoo vya Wanafunzi na Walimu
* Maabara za Physics, Chemistry and Biology
* Nyumba ya kuishi Mwalimu Mkuu
SHUKRANI:
Tokea jana, Jumanne, 08.10.2019, naona WAZALIWA  wa Vijiji vya Maneke, Kwikuba na Mwiringo, yaani Kata ya Busambara, WANAHIMIZANA KUTOA MICHANGO ili Busambara Secondary School ifunguliwe na ianze kutoa Elimu ya Sekondari Januari 2020.
KARIBU UCHANGIE UJENZI WA BUSAMBARA SECONDARY SCHOOL

SEKONDARI ZAJITAYARISHA KWA ONGEZEKO LA WANAFUNZI MWAKANI (JAN 2020): VYUMBA VIPYA VYA MADARASA VINAHITAJIKA

Wajumbe wa Baraza la Maendeleo la Kata ya Musanja wakiwa kwenye Kikao cha WDC

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini lina Jumla ya Sekondari za Kata/Serikali 18 na za Binafsi 2.
Wananchi kwa kushirikiana na Serikali yao  WANAJENGA Sekondari Mpya 9.
Wananchi WAMEDHAMIRIA kwamba ifikapo Januari 2020, Sekondari Mpya zitakazochukua Wanafunzi wa Kidato cha I (FORM I) ni:
(1) Dan Mapigano Memorial Secondary School ya Kata ya Bugoji yenye Vijiji 3.
(2) Busambara Secondary School ya Kata ya Busambara yenye Vijiji 3.
(3) Nyasaungu Secondary School inayojengwa na Kijiji 1 cha Nyasaungu ndani ya Kata ya Ifulifu.
HAYO HAPO JUU NI MATAYARISHO MAZURI ya kupunguza umbali wa kutembea na msongamano madarasani wa Wanafunzi.
Vilevile, MABARAZA ya Maendeleo ya Kata (WDC) yameweka mipango maalumu ya ujenzi wa Vyumba VIPYA vya Madarasa kwa Shule za Sekondari zilizopo ili kukabiliana na mahitaji sahihi ya Januari 2020.
Oktoba 7, 2019 Wajumbe wa Baraza la Maendeleo la Kata ya Musanja (WDC) walifanya MAJADILIANO ya uharakishaji wa ujenzi wa Vyumba Vipya vitatu (3) vya Madarasa katika Sekondari yao ya Kata, Mabui Secondary School. Kikao hicho kilifanyika chini ya Mwenyekiti wa WDC, Mhe Diwani Elias Majura Ndaro.
Awali akitoa taarifa ya Shule hiyo, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mabui, Mwalimu Generose Severine alisema kuwa shule ina jumla ya Wanafunzi 304 na ina Vyumba 7 vya Madarasa.
Mwalimu Mkuu huyo alisema Sekondari hiyo inatarajia kupokea takribani Wanafunzi Wapya 157 (Form I). Kwa hiyo, patakuwepo na UPUNGUFU wa Vyumba 3 vya Madarasa. Hivyo, kuna haja ya kujenga Vyumba Vipya vitatu (3).
Kutokana na taarifa hiyo, Wajumbe wa Baraza la Maendeleo la Kata ya Musanja kwa pamoja WAMEAMUA kwamba Vijiji vyote vitatu vya Kata hiyo (Musanja, Mabui na Nyabaengere) vitaanza ujenzi huo Oktoba 16, 2019 ambapo kila Kijiji kitajenga chumba kimoja (1) cha Darasa
Katika kuboresha Miundombinu ya Shule ya Sekondari Mabui, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof Sospeter Muhongo, alishachangia  Mabati 54 kwa ajili ya kuezeka chumba kimoja (1) cha darasa. Vilevile, Mbunge huyo aliwapatia Vitabu vingi vya Masomo ya Sayansi na Kiingereza.
UJENZI wa Vyumba Vipya 3 ukianza, Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ataenda hapo Shuleni kupiga HARAMBEE na yeye mwenyewe kuchangia ujenzi huo.

WANAVIJIJI NA MBUNGE WAO WA JIMBO WAAMUA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUHARAKISHA UJENZI WA HOSPITAL YA WILAYA YAO

Moja kati ya MAJENGO 7 ya Hospitali ya Wilaya yanayojengwa kwenye Kitongoji cha Kwikonero, Kijijini Suguti:

Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini WANAENDELEA kutoa SHUKRANI zao za dhati kwa SERIKALI yao kwa kutoa Tsh Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya kwenye eneo lao.
Wananchi wa Vijiji 68 wa Jimbo la Musoma Vijijini, wakiongozwa na MADIWANI wao wa Kata 21, WAMEAMUA KUTOA MICHANGO ya FEDHA ili kushirikiana na SERIKALI yao kuharakisha ujenzi wa Hospitali yao ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC) inayojengwa kwenye Kitongoji cha Kwikonero, Kijijini Suguti, Kata ya Suguti.
Kila KIJIJI kinachangia Tsh Milioni 2 kutoka kwenye Michango ya Fedha Taslimu na/au kutoka kwenye 20% ya Fedha zinazorejeshwa na Halmashauri yao kutoka kwenye Makusanyo ya Mapato yao ya ndani (own source).
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ameanza kuchangia kwa kutoa SARUJI MIFUKO 100 na amesema ataitoa wakati wo wote itakapohitajika.
MIUNDOMBINU ya AFYA ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.
(1) Hospitali ya Wilaya: inajengwa
(2) Vituo vya Afya 2 (Murangi na Mugango)
(3) Zahanati:
 (a) Za Serikali: 24 zinatoa huduma
 (b) Za Binafsi: 4 zinatoa huduma
(4) Zahanati zinazojengwa Vijijini: 13 (NGUVUKAZI za Wanavijiji, Serikali, Mbunge wa Jimbo na Wadau wengine wa Maendeleo)
(5) Kituo cha Afya 1: kinajengwa Kijijini Nyambono (Wazaliwa wa Nyambono, Mbunge wa Jimbo na Wadau wengine wa Maendeleo)
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM (2015-2020): Inatekelezwa kwa kasi kubwa – kila Kijiji kiwe na Zahanati moja, TUTAFIKA!
SHUKRANI KWA UONGOZI MZURI
DC wa Musoma, Dr Vicent Naano Anney  na DED, Ndugu John Kayombo WANAPONGEZWA SANA kwa Uongozi wao mzuri unaoleta MAFANIKIO makubwa kwenye UTEKELEZAJI wa Miradi ya Maendeleo kwenye Jimbo la Musoma Vijijini.

MWITONGO, BUTIAMA: KABURI (MAUSOLEUM) LA BABA WA TAIFA LINAPAKWA RANGI NA KUSAFISHWA

Prof Sospeter Mwijarubi Muhongo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini ametekeleza KAZI aliyojipangia ya kila Mwaka kupaka rangi KABURI la Baba wa Taifa, Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere.

Prof Sospeter Mwijarubi Muhongo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini anaendelea KUTEKELEZA KAZI aliyojipangia ya kila Mwaka ya kupaka rangi KABURI la Baba wa Taifa, Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere. Kazi hii inafanywa kwa ushirikiano na Familia ya Baba wa Taifa.
Leo, Jumatano, 02.10.2019, Msaidizi wa Mbunge, Ndugu Fedson Masawa, amekabidhi rangi za kupaka KABURI (Mausoleum) la BABA wa TAIFA. Kazi zinaendelea hapo Mwitongo (angalia picha).
WANANCHI wanakaribishwa kwenye KUMBUKUMBUKU za BABA wa TAIFA nyumbani kwake Mwitongo, Butiama.
Ratiba inaonesha shughuli zitaanza tarehe 08.10.2019 na kufikia kilele chake tarehe 14.10.2019. Mashindano ya Mchezo wa Bao (Mchezo alioupenda sana Baba wa Taifa) yapo. Jimbo la Musoma Vijijini litawakilishwa na Kikundi 1 cha KWAYA na Kikundi 1 cha NGOMA za ASILI.
Mgeni Rasmi ni Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe Jaji Sinde Warioba. Viongozi wengine waliofanya kazi kwa karibu sana sana na Baba wa Taifa watakuwepo. KARIBUNI.

JAMII IMPACT LIMITED YAKARIBISHA USHIRIKIANO NA VIKUNDI VYA UZALISHAJI

Hafla ya Uzinduzi wa Jamii Impact Limited Nyabange Mission (KMT), Musoma.

Jumatatu, 23.09.2019
Jimbo la Musoma Vijijini
Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
JAMII IMPACT LIMITED ni Taasisi isiyokuwa ya Serikali inayoshirikiana na Kanisa la Mennonite UJERUMANI kupitia Mennonitisches Hilfswerk e.V. (MH) na Kanisa la Mennonite TANZANIA (KMT), na imefungua Ofisi zake Nyabangi Mission (KMT), Musoma
VIKUNDI na VICOBA  vinavyofanya KAZI za  UZALISHAJI kama vile Kilimo, Biashara, Utoaji wa Huduma za Kijamii, vinakaribishwa na JAMII IMPACT LTD kuwasilisha MAOMBI ya MIKOPO kwenye Ofisi zake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Impact Ltd, Ndugu Mesika Mongitta, ameeleza  kwamba, “Taasisi hiyo iko tayari kufanya kazi na VIKUNDI ambavyo vinafanya MIRADI ya UZALISHAJI na vile ambavyo vinasaidia kutoa Huduma mbalimbali kwa Jamii.
MASHARTI: Waombaji wawe WANATAMBULIKA na wawe WAMEJIANDIKISHA  kwenye HALMASHAURI zao.
Ndugu Mesika Mongitta aliongezea kuwa, tayari Jamii Impact Limited imefungua Ofisi zake katika Viwanja vya Kanisa la Mennonite vilivyopo Nyabange Mission (KMT), Musoma. Hivyo, kwa maelekezo zaidi juu ya upatikanaji wa MIKOPO kutoka kwenye Taasisi hiyo.
WAOMBAJI kutoka nchini kote wanakaribishwa kuwasiliana na:
William Marcus Mdemu
Simu: 0658218673 / 0758208673
Mch John Wambura, ambae pia ni Katibu Mkuu Kanisa la Mennonite Tanzania (KMT),  anawahimiza Wana – Vikundi kutumia fursa zinazopatikana kwenye maeneo yao ili kuanzisha MIRADI inayoweza kupata MIKOPO kutoka Jamii Impact Ltd.
Hafla ya uzinduzi wa Ofisi ya Jamii Impact Ltd ilifanyika tarehe 06.09.2019 Nyabange Mission. Jimbo la Musoma Vijijini liliwakilishwa na Msaidizi wa Mbunge,  Ndugu Fedson Masawa na Wajumbe 2 (Wana-Vikundi) –  mmoja kutoka Kata ya Bugoji na mwingine kutoka Kata ya Nyakatende

PROF MUHONGO AKAMILISHA AHADI YAKE YA SARUJI MIFUKO 100

Msaidizi wa Mbunge, Ndugu Fedson Masawa akikabidhi SARUJI MIFUKO 50

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof Sospeter Muhongo, Septemba 20, 2019 alikamilisha AHADI yake ya kuchangia SARUJI MIFUKO 100 kwa ajili ya Ujenzi wa Sekondari Mpya ya Kigera inayojengwa na Vijiji viwili vya Kigera Etuma na Kakisheri vyote vya Kata ya Nyakatende.
AHADI hiyo imekamilika baada ya Msaidizi wa Mbunge, Ndugu Fedson Masawa kukabidhi Kamati ya Ujenzi wa Sekondari hiyo SARUJI MIFUKO 50 kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo.
Kwa hiyo, idadi hiyo inakamilisha jumla ya SARUJI MIFUKO 100. Hapo awali, Mbunge wa Jimbo alikabidhi SARUJI MIFUKO 50 alipotembelea Kijiji cha Kigera Etuma na  kukagua Mradi huo wa Ujenzi.
Sekondari hii ikikamilika, Kata ya Nyakatende itakuwa na Jumla ya SEKONDARI 2 za Kata.
Akizungumza mara baada ya kupokea Saruji hiyo, Mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Kigera Etuma, Ndugu Charles Manyonyi, akiongea kwa niaba ya Wananchi wa Vijiji vya Kigera Etuma na Kakisheri, amemshukuru sana Mbunge wa Jimbo lao, Prof Muhongo kwa MICHANGO yake MIKUBWA anayoitoa Kijijini hapo na ndani ya Jimbo zima la Musoma Vijijini.
Katibu wa Kamati ya Ujenzi wa Sekondari ya Kigera, Ndugu James Majengo amesema Wananchi wa Kigera Etuma na Kakisheri wataendelea na ujenzi kwa kasi kubwa ili kuhakikisha  Sekondari hiyo inafunguliwa January 2020.

KIKUNDI KINGINE CHA NGOMA ZA ASILI KUTOKA MKOA WA MARA CHAENDA KUSHINDANA NJE YA MKOA WAO

Msaidiyi wa Mbunge, Ndugu Hamisa Gamba akimkabidhi TIKETI ZA USAFIRI Kiongozi wa LIRANDI, Ndugu Mtatiro Ijanja.

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, AMECHANGIA USAFIRI wa Kikundi cha LIRANDI cha Kijiji cha Masinono, Kata ya Bugwema kwenda mashindanoni Tukuyu, Mkoani Mbeya.
MASHINDANO haya yanajulikana kwa jina la, “TULIA TRADITIONAL DANCES FESTIVAL”, yatafanyika TUKUYU Mjini, tarehe 26-28.09.2019.
Mashindano haya yanatayarishwa na Mhe Dkt Tulia Ackson, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kikundi cha LIRANDI cha Kata ya Bugwema ndicho kilichukua ushindi wa kwanza kwa Mashindano ya NANENANE ya Ngoma za Asili ya Jimbo la Musoma Vijijini yaliyofanyika tarehe 10.08.2019 Kijijini Suguti.
MKOA WA MARA UNAWAOMBEA SANA WAWAKILISHI WAO WARUDI NA USHINDI WA KWANZA
*EGUMBA (Jimbo la Butiama) ichukue ushindi wa kwanza (kimataifa) huko Dar Es Salaam
*LIRANDI (Jimbo la Musoma Vijijini) ichukue ushindi wa kwanza huko Tukuyu, Mbeya

MATUMIZI YA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO YAJADILIWA HADHARANI

KIKAO cha KUGAWA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO cha Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo kilichofanyika Kijijini Busamba, Kata ya Etaro.

 Jumanne, 17.09.2019, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, ALIITISHA KIKAO kwenye Kijiji cha Busamba, Kata ya Etaro KUJADILI na KUGAWA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO.
Mbunge wa Jimbo hilo AMEWEKA UTARATIBU wa kufanya VIKAO vya pamoja vya Wananchi na Viongozi wao wa Serikali na Vyama vya Siasa wa ngazi mbalimbali WAKATI WA KUGAWA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO. Vikao hivyo vinafanywa kwa mzunguko ndani ya Kata 21 ya Jimbo hilo. Safari hii KIKAO kimefanyika kwenye KATA YA ETARO.
Wananchi na Viongozi wao wa Kata ya Etaro yenye Vijiji 4 walishiriki.
MADIWANI wa Vyama vyote vya Siasa, yaani, CCM na CHADEMA walishiriki.
CCM iliwakilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Musoma Vijijini wakiwemo, Mwenyekiti wa Wilaya, Ndugu Nyabukika Bwire Nyabukika na Katibu wa Wilaya, Ndugu Stephene Koyo. Viongozi wengine wa CCM na Jumuiya zake walikuwepo.
TAARIFA YA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO
*Fedha hizi ni za Serikali na zinatunzwa na Halmashauri yetu.
*MIUNDOMBINU YA ELIMU kwenye Shule za Msingi na Sekondari bado zinahitaji KUBORESHWA sana, kwa hiyo Fedha za Mfuko wa Jimbo ZITACHANGIA juhudi za WANANCHI za kuboresha MIUNDOMBINU ya ELIMU Jimboni mwetu.
*Fedha taslimu HAZITOLEWI kwa WALENGWA na badala yake WALENGWA wanapewa VIFAA VYA UJENZI VILIVYOOMBWA na kununuliwa na Halmashauri.
*Mwaka wa Fedha wa 2018/2019, Tsh 50.43M zilipokelewa kwenye MFUKO wa JIMBO. Fedha zilizobakia Mwaka 2017/2018  zilikuwa Tsh 4.23M. JUMLA: Tsh 54.66M
*Fedha za MFUKO wa JIMBO kwa Mwaka 2018/2019 (Tsh 54.66M) ZILITUMIKA KUNUNUA: (i) MABATI 931 na (ii) SARUJI MIFUKO 1,155. VIFAA hivyo viligawiwa mashuleni na kila KATA ilipata MGAO wake.
* Fedha zilizopokelewa kwa Mwaka wa Fedha wa  2019/2020 ni Tsh 52.43M. Zilizobakia Mwaka jana ni Tsh 1.46M. JUMLA: Tsh 53.89M
MGAO WA Tsh 53.89M
*Kipaumbele cha kwanza ni Sekondari 2 zitakazofunguliwa Januari 2020.
*Sekondari hizo ni Dan Mapigano Memorial Secondary School ya Kata ya Bugoji na Busambara Secondary School ya Kata ya Busambara.
*Kata nyingine 19 nazo zimepata MGAO wa VIFAA VYA UJENZI kulingana na maombi yaliyowasilishwa.
FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO kwa Mwaka 2018/2019 (Tsh 53.89M) zitatumika kununua na kugawa jumla ya: (i) NONDO 200, (ii) MABATI 1,026, (iii) SARUJI MIFUKO 1,150 na (iv) Iwapo bei zitakuwa nzuri na fedha kusalia, fedha hizo zinunue vifaa vya ujenzi na kuendelea kuvigawa ipasavyo.

BUSAMBARA SECONDARY SCHOOL – WANAVIJIJI WAKUBALIANA KUONGEZA KASI YA UJENZI

Ziara ya M/Kiti wa CCM wilaya Ndugu Nyabukika Bwire Nyabukika na Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo kwenye eneo la ujenzi wa Busambara Secondary School, Kijijini Kwikuba, Kata ya Busambara

Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 na Vijiji 68 lina Sekondari za Kata/ Serikali 18 na za Binafsi 2.
Wanavijiji WAMEAMUA kujenga SEKONDARI MPYA 9 ili kupunguza umbali watembeao Wanafunzi na Walimu, na kupunguza msongamano madarasani.
Kata ya Busambara yenye Vijiji 3 (Maneke, Kwikuba na Mwiringo) inakaribia kukamilisha Awamu ya Kwanza ya ujenzi wa Sekondari ya Kata yao.
Ujenzi wa Vyumba 4 vya Madarasa umekamilika na kila Darasa lina Madawati 40.
Wanavijiji na Viongozi wao wa ngazi mbalimbali wanaishukuru sana Benki ya NMB kwa kuwapatia Madawati 80 na Viti 80.
Ujenzi wa Ofisi ya Mwalimu Mkuu na ya Walimu wengine  unakamilishwa.
Wananchi wa Vijiji 3 vya Kata hiyo WAMEGAWANA KAZI za Ujenzi wa Vyoo, Maabara na Nyumba ya Mwalimu Mkuu. Kazi zimeanza.
Jana, Jumatatu, 16.09.2019, Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Musoma Vijijini, Ndugu Nyabukika Bwire Nyabukika WALIKAGUA MAENDELEO YA UJENZI wa Sekondari ya Busambara.
Vilevile walitumia fursa hiyo kuongea na Wanavijiji wa Kata ya Busambara. Maswali yaliulizwa na kujibiwa.
FEDHA na VIFAA vya ujenzi wa Busambara Secondary School vimetoka: (i) Serikalini (TAMISEMI)  Tsh 37.5M, na Halmashauri, Tsh 2 M, (ii) Mbunge wa Jimbo-Saruji Mifuko 150 na Bando 8 za Mabati, (iii) Wazaliwa wa Kata ya Busambara (Afande Nyakulinga, Joseph Chikongowe na Advocate Said Chiguma), (iv) Michango ya Wanavijiji wa Tsh 15,000 kutoka kila Kaya, (v) Michango ya WADAU wengine wa Maendeleo.
UAMUZI WA WANAVIJIJI
*NGUVUKAZI kutoka Vijijini iongezeke
*Ujenzi wa Vyoo ukamilike kabla ya tarehe 30 Oktoba 2019
*Ujenzi wa MAABARA ukamilike kabla ya tarehe 30 Novemba 2019
*Ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu Mkuu ukamilike ifikapo tarehe 30 Disemba 2019
*Busambara Secondary School IFUNGULIWE na kuchukua WANAFUNZI wa FORM Januari 2020.

UJENZI WA DAN MAPIGANO MEMORIAL SECONDARY SCHOOL WAENDELEA VIZURI

Ziara ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Ndugu Nyabukika Bwire Nyabukika na Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo wakiwa eneo la ujenzi wa Dan Mapigano Memorial Secondary School, Kijijini Bugoji, Kata ya Bugoji.

 
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijijini, Prof Sospeter Muhongo akiambatana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Ndugu Nyabukika Bwire Nyabukika WAMEFANYA ZIARA Kijijini Bugoji KUKAGUA UJENZI wa Dan Mapigano Memorial Secondary School.
 
Serikali, Wanavijiji na Viongozi wao, Mbunge wa Jimbo, na Wadau wengine  wa Maendeleo ya Kata ya Bugoji WANACHANGIA UJENZI WA SEKONDARI hii.
 
NGUVUKAZI ya Wanavijiji wa Vijiji vya Kaburabura, Kanderema na Bugiji IMESAIDIA SANA kuharakisha ujenzi huu ulioanza Disemba 2018.
 
Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa  vitano (5) umekamilika na kila Chumba (Darasa) kina MADAWATI 40. Ofisi za Mwalimu Mkuu na Naibu wake zimekamilika.
 
Ujenzi wa Vyoo, Maabara na Nyumba ya Mwalimu Mkuu UMEANZA na unaendelea.
 
LENGO KUU: Dan Mapigano Memorial Secondary School ifunguliwe Januari 2020 na Wanafunzi wengi wa Form I watoke Vijiji vya Kaburabura, Kanderema na Bugoji (Kata ya Bugoji).

PROF MUHONGO ATUNUKIWA HATI YA HESHIMA

Msaidizi wa Mbunge, Ndugu Fedson Masawa akipokea HATI ya HESHIMA kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo Prof Muhongo. Mbunge wa Jimbo hakuwepo kwani alikuwa kwenye maziko ya Marehemu Mhe Balozi Paul James Ndobho.

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge

JUMUIYA ya Wazazi Wilaya ya Musoma Vijijini leo September 14, 2019 imemtunuku HATI ya HESHIMA Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof Sospeter Muhongo.

Ndugu Julius Kambarage Masubo, Mjumbe wa Baraza la Wazazi Taifa kutoka Mkoa wa Mara ndiye aliyekuwa MGENI RASMI wa Baraza la Wazazi Wilaya ya Musoma Vijijini lililokutana leo Kijijini Chumwi

Akikabidhi HATI hiyo, MGENI RASMI amesema, “HATI hii ni Ishara ya kipekee ya kutambua Mchango na Utendaji kazi mzuri na uliotukuka wa Mbunge wa Jimbo katika kuitekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2015 – 2020 ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini na Halmashauri ya Wilaya ya Musoma.

Mgeni Rasmi huyo aliendelea kusema kwamba, HATI hiyo ni kielelezo cha kutambua MCHANGO MKUBWA wa Mbunge huyo kwenye Chama (CCM) na Jumuiya zake zote.

Ndugu Kambarage Masubo ametoa pongezi nyingi kwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof Muhongo kwa Uongozi Shirikishi unaowaunganisha Wananchi wa Musoma Vijijini katika kuharakisa Maendeleo Jimboni mwao.

Jimbo hili halina malumbano ya kisiasa wala halina mivutano ya kikabila – Mbunge wa Jimbo wanawaunganisha Wananchi wote kwenye MIRADI ya Maendeleo bila ubaguzi wa aina yo yote ile.

Wengine waliotunukiwa HATI ya HESHIMA na Jumuiya ya Wazazi ni pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Musoma, Mhe Charles Magoma Nyambita pamoja na Diwani wa Kata ya Bukima Mhe January Simula.

Ndugu Kambarage Masubo ameikumbusha Jumuiya ya Wazazi wawe kitu kimoja kuhakikisha Ilani ya Chama cha Mapinduzi inatekelezwa kwa kasi kubwa chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt John Joseph Pombe Magufuli.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Musoma Vijijini, Ndugu Phares Maghubu amesisitiza kuwa Jumuiya ya Wazazi inaendelea kuimarisha mipango yao ya utunzaji wa Mazingira, kuhamasisha uboreshaji wa elimu na kuimarisha nidhamu na maadili kwa Vijana ili kuwa na kizazi chenye maadili mazuri na chenye kujituma katika shughuli za ki-uchumi na maendeleo.

CHAMA CHA MAPINDUZI KATA YA RUSOLI YAMTUNUKU MHE. MBUNGE WA JIMBO HATI YA HESHIMA.

Msaidizi wa Mbunge akionesha hati ya HESHIMA aliyokabidhiwa Mh. Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo

HATI hii ya HESHIMA  ni kielelezo cha WANA-RUSOLI kutambua MCHANGO MKUBWA wa MAENDELEO anaoutoa Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo kwenye Kata ya Rusoli.
HATI imekabidhiwa na M/kiti wa CCM Kata ya Rusoli Ndugu Sabato Mkome, kwa Msaidizi wa Mbunge Hamisa Gamba, leo tarehe 6/9/2019, kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Mhe. Prof. Sospeter Muhongo.
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo
ameishukuru sana CCM  Kata ya Rusoli, kwa kutambua MCHANGO WAKE MKUBWA kwenye Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM (2015-2020) kwenye Kata hiyo na ndani ya Kata zote za Jimbo la Musoma Vijijini.

WANANCHI WA KIJIJI CHA KABURABURA NAO WAAMUA KUJENGA ZAHANATI YAO

Wananchi wa Kijiji cha Kaburabura, Kata ya Bugoji wakisomba MCHANGA, kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati yao.

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
Wananchi wa Kijiji cha Kaburabura kilichoko Kata ya Bugoji WAMEAMUA na KUANZA UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI chao.
HUDUMA za AFYA kwa WAKAZI wa Kijiji cha Kaburabura ZINAFUATWA kwenye VIJIJI JIRANI, yaani Kijiji cha Bugoji, umbali wa kilomita 4 au Kijiji cha Kangetutya, umbali wa kilomita 5, kwenye Wilaya nyingine, Wilaya ya Bunda.
Jumatano, tarehe 4.9.2019 WANAVIJIJI hao wameanza ujenzi wa Zahanati ya Kijiji chao baada ya KUFANYA UAMUZI wa pamoja.
Aidha hatua za ujenzi wa Zahanati hiyo umeanza chini ya Usimamizi wa Mwenyekiti wa Kijiji cha Kaburabura Ndugu Chriphord Masatu, na Kaimu VEO Ndugu Majura Magambo.
Akifafanua juu ya ujenzi huo, Ndugu Chriphord Masatu ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji hicho, amesema kuwa, kazi za Ujenzi wa Zahanati hiyo zitafanyika JUMANNE na ALHAMIS ya kila wiki, huku wakitaraji kukamilisha ujenzi huo ndani ya takribani MIEZI 4 na ifikapo Januari 2020, ujenzi uwe umekamilika.
Ndugu Masatu ameendelea kufafanua kuwa mbali na NGUVUKAZI za WANANCHI za kusomba Mawe, Kokoto, Mchanga na Maji ya ujenzi,  WAMEKUBALIANA kwamba KILA KAYA ichangie Tsh. 50,000/= (Elfu hamsini) ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika mapema.
Kazi hizo za  AWALI za usombaji wa mchanga, zimeongozwa na Katibu wa CCM wa Tawi la Kaburabura Ndugu Juma Magoti.
Diwani wa Kata ya Bugoji, Mhe Ibrahimund Malima wamewaomba Wananchi wa Kijiji hicho kushirikiana vema ili kuhakikisha ujenzi unakamilika kama ulivyopangwa.
Diwani huyo pia ametoa wito kwa WAZALIWA wa Kijiji cha Kaburabura walioko nje ya Kijiji hicho, KUSHIRIKIANA na  Ndugu, Jamaa na Marafiki zao walioko Kijijini hapo, KUKAMILISHA MRADI huu muhimu sana kwa Huduma Bora za Afya zao.
Diwani huyo ametoa taarifa kwamba Group la WhatsApp liitwalo, “KABURABURA NI KWETU,” ndilo Group LINALOWAUNGANISHA Wazaliwa wa Kijiji cha Kaburabura na Rafiki zao kwenye UTEKELEZAJI wa Mradi huu na mingineyo.
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo AMETOA PONGEZI nyingi kwa WANA- KABURABURA kwa UAMUZI wao huo mzuri na ATAENDA KUPIGA HARAMBEE ya ujenzi huo na yeye mwenyewe atachangia SARUJI MIFUKO 100.
ILANI YA CCM ya UCHAGUZI ya 2015-2020 INATEKELEZWA kwa KASI kubwa kwenye Jimbo la Musoma Vijijini:
*Zahanati Mpya 14 zinajengwa Jimboni kwa NGUVUKAZI za Wananchi na Michango ya SERIKALI na WADAU wengine wa Maendeleo
*Kituo cha Afya 1 (Kata ya Nyambono) kinajengwa.
*Hospitali 1 ya Wilaya, Kitongoji cha Kwikonero, Kijiji cha Suguti inajengwa.
HUDUMA ZA AFYA ZITOLEWAZO JIMBONI
*Zahati 24 za Serikali
*Zahanati 4 za Binafsi
*Vituo vya Afya 2 (Murangi na Mugango)
ILANI YA CCM: Kila Kijiji kiwe na Zahanati Moja – Jimbo la Musoma Vijijini lenye Vijiji 68 linatekeleza KWA VITENDO.

VIKUNDI VYA WATU WENYE ULEMAVU VYANUFAIKA NA MIKOPO KUTOKA HALMASHAURI NA BMZ

Baadhi ya Wanachama wa SHIVYAWATA ERUSULI wakiwa kazini kwenye MRADI wao wa UFUGAJI wa kuku wa kienyeji Kijijini Bwai Kumusoma, Kata ya Kiriba.

Jumatatu, 02.09.2019
Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
HALMASHAURI ya Wilaya ya Musoma yenye Jimbo la Musoma Vijijini INAENDELEA kutekeleza AGIZO la SERIKALI la kutoa MIKOPO kwenye MAKUNDI 3, yaani VIJANA, WANAWAKE na WATU WENYE ULEMAVU. Mikopo inatolewa kila Mwaka.
Baadhi ya WATU WENYE ULEMAVU ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini WANAENDELEA kupokea MISAADA ya aina mbalimbali kutoka kwenye MRADI wa BMZ wa Serikali ya Ujerumani.
BMZ (Bundesministerium fuer wirtschaftliche Zusammenarbeit und Entwicklung, in English: The Federal Ministry of Economic Cooperation and Development) ina MRADI wa KUSAIDIA WATU WENYE ULEMAVU, wakiwemo WANAFUNZI, kwenye  Kata 10 za Jimbo la Musoma Vijijini. MISAADA hiyo ni pamoja na: Matibabu kwenye Hospitali Teule ya Wilaya ya Rorya, KMT SHIRATI, Vifaa Maalum vya Kujimudu, Vifaa vya Shule kwa Wanafunzi, na Mikopo midogo midogo kwa Watu Wenye Ulemavu.
Kikundi cha Watu wenye Ulemavu cha SHIVYAWATA ERUSULI (Wanachama 15) kilichoko Kijijini Bwai Kumusoma, Kata ya Kiriba, kimeanzisha MRADI wa UFUGAJI wa KUKU wa kienyeji baada ya kupokea MKOPO wa Shilingi Milioni 2 kutoka HALMASHAURI ya Wilaya ya Musoma.
Akizungumza na Msaidizi wa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Msimamizi wa Mradi huo, Ndugu Malandala Titi Masau ameeleza kwamba wametumia FEDHA za MKOPO huo kujenga banda la kuku, kununua vifaa vya kulishia kuku, chakula na madawa ya kuku. Malengo ni kuanza kufuga kuku 100 na hadi juzi walikuwa wameishanunua kuku 64.
Ndugu Titi Masau ameongezea kuwa, mbali ya MKOPO wa Halmashauri yao, SHIVYAWATA ni miongoni mwa Vikundi vya Watu Wenye Ulemavu vilivyo ndani ya MRADI wa BMZ ambao tayari  umetoa MKOPO wa Tsh 575,000/= kwenye Kikundi hicho. VIKUNDI vingine 9 navyo vimepokea MIKOPO kutoka kwenye MRADI huu.
Ndugu Hawa Daniel, Mwanachama wa Kikundi cha SHIVYWATA ERUSULI, kwa niaba ya Wanachama wenzake, ameshukuru sana HALMASHAURI yao na MRADI wa BMZ kwa kuwawezesha Watu Wenye Ulemavu kuanzisha MIRADI itakayowafanya WAJITEGEMEE ki-uchumi.

VIJANA WANUFAIKA NA KILIMO CHA BUSTANI KWA KUTUMIA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO

baadhi ya Wanakikundi cha NYAKABHUNGO wakiwa kazini kwenye BUSTANI yao ya MBOGAMBOGA iliyoko Kijijini Kanderema, Kata ya Bugoji.

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
KILIMO CHA UMWAGILIAJI, kikiwemo cha BUSTANI za mbogamboga na mazao mengine kinazidi kushamiri ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.
VIJANA na Wananchi wengine kwa ujumla wameendelea kunufaika na aina hii ya KILIMO tofauti na kile kilichozoeleka cha kutegemea MVUA.
VIJANA wa Kikundi cha NYAKABHUNGO GROUP kilichoko kwenye Kijiji cha Kanderema, Kata ya Bugoji ni moja ya Vikundi vilivyopewa MASHINE/PAMPU za Kilimo cha Umwagiliaji na MBEGU kutoka MFUKO wa JIMBO ambao Mwenyekiti wake ni Mbunge wa Jimbo.
KIKUNDI hiki kinanufaika na MSAADA huo kutoka Serikalini (Mfuko wa Jimbo) na VIKUNDI vingine vinavyofanya vizuri ni:
(ii) Angaza, Kata ya Bukumi
(iii) Mwanga Farmers, Kata ya Nyambono
(iv) No Sweat No Sweet, Kata ya Bwasi
(v) Mkulima Jembe, Kata ya Bukima
(vi) Keuma, Kata ya Busambara
(vii) Jitume, Kata ya Suguti
Mwenyekiti wa Kikundi cha NYAKABHUNGO,  Ndugu Mtaka Mwenura,
ameeleza kuwa Kikundi chao kinajishughulisha na Kilimo cha NYANYA, VITUNGUU, MBOGAMBOGA, MAHINDI na VIAZI VITAMU na kwamba wanataraji kuingia sokoni hivi karibuni.
Mwenyekiti huyo,  kwa niaba ya VIJANA wa Kikundi hicho wameishukuru sana SERIKALI kupitia Mbunge wao wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo na HALMASHAURI yao, kwa kutoa Vifaa hivyo vya Kilimo cha Umwagiliaji.
Diwani wa Kata hiyo,  Mhe Ibrahimund Malima ametoa shukrani za kipekee kwa Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo, Mkuu wa Wilaya, Dr Vicent Naano Anney na Mkurugenzi wa Halmashauri yao, Ndugu John Kayombo kwa UTEKELEZAJI mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM (2015 – 2020).
Diwani huyo anamshukuru sana Mbunge wao wa Jimbo kwa KUGAWA BURE Mbegu za ALIZETI kwa misimu 3 mfululizo. Kwa sasa ALIZETI ni zao jipya la BIASHARA linalolimwa Jimboni humo.
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, anaendelea kutoa wito kwa VIJANA, KINAMAMA na WATU WENYE ULEMAVU waendelee kuunda VIKUNDI vinavyotambulika kwa ajili ya kupata MIKOPO, pale fursa inapotokea.

UJENZI, UKAMILISHAJI NA UBORESHAJI WA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI KWENYE SEKONDARI ZA KATA

Ufyatuaji wa Matofali 1,200 kwa ajili ya UKAMILISHAJI wa ujenzi wa BOMA lenye Maabara za Masomo ya Sayansi ya Sekondari ya Murangi.

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini lina jumla ya Sekondari 18 za Kata/Serikali na 2 za Binafsi (Katoliki & SDA). Sekondari Mpya 8 zinajengwa Jimboni mwetu.
Kazi mojawapo muhimu INAYOFANYWA kwa wakati huu ni UJENZI, UKAMILISHAJI na UBORESHAJI wa MAABARA za MASOMO ya Sayansi (Physics, Chemistry na Biology)  kwenye Sekondari zetu za Kata.
Sekondari zote 20 (za Serikali na Binafsi) zina VITABU vya kutosha vya Masomo ya SAYANSI vinavyogawiwa na Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo. Mbunge huyu anahimiza ujenzi wa Maktaba kwenye Shule zote za Sekondari na Msingi.
MAABARA ZA SEKONDARI YA MURANGI
VIJANA Wazaliwa wa Kata ya Murangi yenye Vijiji 2 (Lyasembe na Murangi), wakiongozwa na Diwani wa Kata hiyo, Mhe Kujerwa Simon Kujerwa, WAMEAMUA kuchangia SARUJI MIFUKO 70 kwa ajili ya kuanza kazi za UKAMILISHAJI  wa BOMA lenye Maabara 3 za Masomo ya SAYANSI kwenye Sekondari ya Kata yao, yaani Murangi Secondary School.
Ujenzi huu ulisimamia Mwaka 2016 na Diwani huyo ambae ameingia madarakani hivi karibuni, AMEFUFUA ujenzi huo na nia yao sasa ni kukamilisha Boma hilo lenye Maabara zote tatu.
Mwalimu Mkuu wa Secondari ya Murangi, Mwl Ernest Mazoya amemshukuru sana Mhe Diwani huyo KUFUFUA ujenzi wa Maabara zao. Sekondari hiyo ilifunguliwa Mwaka 2006.
Awali akitoa taarifa ya ujenzi huo, Diwani huyo amesema kwa SASA Wananchi wa Kata ya Murangi WAMEKUBALI kuchangia NGUVUKAZI zao kwa kusomba mchanga, mawe, kokoto na maji ya ujenzi. Vilevile, Wananchi hao WAMEKUBALI kuchangia gharama za MAFUNDI.
Mhe Kujerwa Simon Kujerwa anawashukuru sana Vijana wenzake waliojitokeza kuchangia ujenzi wa Maabara hizo. Kwa hatua hizi za awali MICHANGO imetolewa na VIJANA waishio ndani ya Kata hiyo ambao ni:
(1) Magesa Saile
(2) Kalii Saile
(3) Magoti Biswaro
(4) Robert Kainja
(5) Soti Mashenene
(6) Thomas Kujerwa
(7) Mea Nyang’ombe
(8) Nyandeka Gesi
(9) Sabina Nyamayugu, na
(10) Diwani mwenyewe
Ofisi ya Mbunge wa Jimbo INAENDELEA kuwashawishi WADAU mbalimbali na hasa WAZALIWA wa Jimbo la Musoma Vijijini KUENDELEA KUCHANGIA Maendeleo ya Kata zetu 21 na Vijiji vyetu 68. Kila Kijiji kina MRADI wa Maendeleo unaotekelezwa kwa wakati huu – KARIBU UCHANGIE.

WAZAZI WA KATA YA TEGERUKA WAAGA VIJANA WAO KWA ZAWADI YA KIPEKEE

baadhi ya MATUKIO ya MAHAFALI ya Wanafunzi wa Darasa la VII  wa S/M Nyaminya A&B, Kijijini Tegeruka, Kata ya Tegeruka.

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
WAZAZI wa Wanafunzi wa S/M Nyaminya A na B zote za Kijiji cha Tegeruka, Kata ya Tegeruka wamewaaga WATOTO wao watakaohitimu Elimu ya Msingi kwa kutoa ZAWADI ya uchangiaji wa UJENZI na UBORESHAJI wa MIUNDOMBINU ya ELIMU katika Shule hizo mbili.
Zoezi hilo limefanyika jana Agosti 23, 2019 kwenye MAHAFALI ya kuwaaga WANAFUNZI wa Darasa la VII wa Shule hizo.
ZAWADI hiyo imetokana na MGENI RASMI, Ndugu SHAIBU NGATICHE, Katibu wa CCM Mkoa wa Mara kupokea Changamoto za Shule ya Msingi Nyaminya B ambazo ziliwasilishwa na Mkuu wa Shule hiyo, Mwl Zerulia John Shana.
Changamoto hizo ni pamoja na ukosefu wa Ofisi ya Mwalimu Mkuu, Upungufu wa Vyumba vya Madarasa. Nyingine ni kutokuwepo SAKAFU kwenye  baadhi ya Vyumba vya Madarasa na upungufu wa Nyumba za kuishi Walimu.
Baada ya kupokea orodha ya Changamoto hizo, MGENI RASMI waliwasihi WAZAZI na WAGENI wengine kwenye MAHAFALI hiyo KUUNGANA nae KUTATUA baadhi ya matatizo hayo.
HARAMBEE ilipigwa na matokeo yake ni:
(1) Saruji  Mifuko: 140
(2) Misumari: Kg 10
(3) Milango ya Vyumba vya Madarasa: 2
(4) Fedha Tsh 2,175,100/=
(5) NGUVUKAZI: Wanavijiji WAMEKUBALI KUJITOLEA kusomba mchanga, mawe, kokoto na maji ya ujenzi.
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo alichangia SARUJI MIFUKO 100 (kila Shule Mifuko 50) na MILANGO 2 ya Vyumba vya Madarasa (kila Shule Mlango 1 wenye thamani ya Tsh 150,000).
Mara baada ya HARAMBEE hiyo, Mwl Mkuu wa S/M Nyaminya B,  mwenyeji wa Sherehe hizi, Mwl Zerulia John Shana, ALIMSHUKURU SANA MGENI RASMI, Ndugu SHAIBU NGATICHE kwa kuendesha HARAMBEE hiyo iliyokuwa ya MAFANIKIO mazuri.
Vilevile, Mwalimu Mkuu huyo ALIWASHUKURU  WAZAZI na Wananchi wengine waliotoa MICHANGO yao wakiwemo Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dr Vincent Naano, Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo na VIONGOZI wengine wa Chama (CCM) na Serikali.
Pamoja na HARAMBEE hiyo, Mwalimu Mkuu huyo aliendelea KUTAMBUA, kwa shukrani nyingi, MICHANGO ya AWALI iliyokwishatolewa Shuleni hapo kutoka kwa WADAU wengine wa Maendeleo wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo, Ndugu Juma Ramadhani, Mwl Masinde Bigambo na Ndugu Paschal Rutundwe.

MIRADI MIKUBWA YA MAJI INAYOTEKELEZWA NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJI

Kumbukumbu za Sherehe (15.08.2019) ya uwekaji wa SAINI (Serikali & Mkandarasi) wa Mradi wa ujenzi wa Bomba la Maji la Mugango-Kiabakari-Butiama. Serikali iliwakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof Kitila Mkumbo.

Wananchi wa Vijiji 68 vya Jimbo la Musoma Vijijini WANATOA SHUKRANI ZA DHATI kwa Serikali yao kwa kuanza KUTEKELEZA MIRADI ya USAMBAZAJI wa MAJI SAFI na SALAMA Vijijini mwao.
(1) SHUKRANI MAALUM zimetolewa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt John Joseph Pombe Magufuli KWA KUTIMIZA AHADI YAKE ya KUTEKELEZA Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Maji la Mugango-Kiabakari-Butiama. Maji yatatoka Ziwa Viktoria.
MRADI wa Mugango-Kiabakari-Butiama utagharimu Tsh bilioni 70 ( US$ 30.68) umefadhiliwa na Serikali ya Tanzania, Saudi Arabia na BADEA. Mradi huu utakamilika ndani ya MIEZI 24.
(2) MRADI WA MAZIWA MAKUU
Vijiji vyote vya Jimbo la Musoma Vijijini vilivyoko karibu na Ziwa Viktoria (Vijiji 33) vimo kwenye Mradi huu. USANIFU umefanyika na Serikali inajipanga ianze utekelezaji wake.
(3) MAJI YA MUWASA KUSAMBAZWA VIJIJINI
MAJI yanayozalishwa MUWASA kwa ajili ya Mji wa Musoma ni MENGI MNO na matumizi yake kwa sasa ni takribani 50% ya MAJI yanayozalishwa. Maji yanatoka Ziwa Viktoria.
Kwa hiyo Serikali imeamua Vijijini vya Jimbo la Musoma Vijijini na Jimbo la Butiama VISAMBAZIWE MAJI hayo ya ziada. Kwa upande wa Jimbo la Musoma Vijijini, VIJIJI VYOTE vya Kata za ETARO, NYEGINA, NYAKATENDE na IFULIFU vimo kwenye Mradi huu ambao UTEKELEZAJI wake tayari umeanza.
(4) MIRADI MINGINE INAYOTEKELEZWA na MAJI yake yanatoka Ziwa Viktoria ni:
(4a) Bujaga-Bulinga-Bukima-Kwikerege
(4b) Chitare-Makojo
(4c) Suguti-Kusenyi-Chirorwe-Wanyere
(5) MIRADI AMBAYO USANIFU UMEKAMILIKA
USANIFU kwenye VIJIJI vya Kata za Bugoji, Nyambono, Bugwema, Musanja na Nyamrandirira UMEFANYIKA na MAOMBI ya Fedha za utekelezaji wa Miradi ya usambazaji wa MAJI Vijijini humo YAMEFIKISHWA Serikalini na yanafuatiliwa kwa ukaribu sana.

VIJIJI VIWILI VYA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI VYAAMUA KUJENGA SEKONDARI YAO 

Mafundi na Wanavijiji wa Kigera Etuma na Kakisheri wakiendelea na Ujenzi wa Jengo la Utawala la Kigera Secondary School.

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
Vijiji vya Kigera Etuma na Kakisheri vyote vya Kata ya Nyakatende vimeanza kwa kasi kubwa kujenga Sekondari yao. Sababu kuu za UAMUZI huu ni UMBALI MREFU wa kutembea na MSONGAMANO Madarasani wa Wanafunzi kwenye Sekondari ya Kata iliyoko Kijijini Nyakatende.
Wanavijiji hawa tayari wamekamilisha ujenzi wa Boma la Vyumba viwili vya Madarasa ambavyo vimejengwa kwa kutumia MICHANGO ya WANAVIJIJI na WAZALIWA wa Vijiji hivyo viwili. HARAMBEE ya Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo imeongeza kasi ya ujenzi wa Jengo la Utawala.
MTINDO WA KUTOA MICHANGO
Wakazi wa Vijiji vya Kigera Etuma na Kakisheri WAMEKUBALIANA kwamba kila MWANAKIJIJI mwenye umri wa kuanzia MIAKA 18 achangie TOFALI MOJA. Mawe, kokoto, mchanga na maji ya kujengea vinasombwa kwa kutumia NGUVUKAZI  zao.
WADAU wengine wenye kuchangia ujenzi huu ni: WAVUVI na WACHIMBAJI Wadogo Wadogo wanaofanya shughuli zao Vijijini hapo.
Aidha, Katibu wa Kamati ya ujenzi wa Sekondari hiyo Ndugu James Majengo, kwa niaba ya Uongozi na Wananchi wa Vijiji vya Kigera Etuma na Kakisheri, anatoa SHUKRANI nyingi kwa WAZALIWA wa Vijiji vya Kakisheri na Kigera Etuma kwa MICHANGO yao mikubwa.
Vilevile, SHUKRANI nyingi zimetolewa kwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo aliyechangia SARUJI MIFUKO 100.
WAZALIWA wa Vijiji vya Kigera Etuma na Kakisheri WAMEUNDA UMOJA WAO kwa ajili ya kuchangia ujenzi huu. Hadi sasa waliochangia ni:
(1) Nyakiriga Kabende-Mwenyekiti
(2) Albinus Makanyaga-Mhasibu
(3)Joseph Mnibhi – Katibu
(4) Augostino Eugene
(5) Joseph Surusi
(6) Wambura Mujungu
(7) Marere Eugene
(8) Mareges Eugene
(9) Emmanuel Ekama
(10) Mareges Jela
(11) Kisha Charamba
(12) Garani Magafu
(13) Mugini Kibusi Marere
(14) Ngajeni Manumbu
(15) Lucas Mashauri
(16) Mutandu Kabende
(17) Boniphace Kitende
(18) Boniphace Changanya
Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 na Vijiji 68 lina Sekondari za Kata/Serikali 18 na 2 za Binafsi. Wanavijiji WAMEAMUA kujenga SEKONDARI MPYA NANE (8).

SHULE YA MSINGI MURANGI – SOMO LA STADI ZA KAZI LATUMIKA KUIMARISHA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

Wanafunzi wa S/M Murangi iliyoko Kijijini Lyasembe wakiwa kwenye SOMO la STADI za KAZI – ndani ya Shamba la Nyanya la Shule.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
Shule ya Msingi Murangi iliyopo Kijiji cha Lyasembe, Kata Murangi imeamua kufanya KILIMO cha UMWAGILIAJI kupitia SOMO la STADI za KAZI.
Lengo kuu hapa ni KUWATAYARISHA WAHITIMU waweze KUJIAJIRI na KUJITEGEMEA kupitia KILIMO hasa cha UMWAGILIAJI kwani makazi yao yako karibu sana na Ziwa Viktoria.
Mwalimu Maburugi Matiko wa Shule hiyo alipata MAFUNZO ya UFUNDISHAJI wa STADI za KAZI mbalimbali zikiwemo za KILIMO. Kwa hiyo, Shule imanzisha SHAMBA DARASA la mihogo, mahindi, vitunguu, nyanya na matikiti.
MAVUNO kutoka shamba hilo yamesaidia KUKUZA UCHUMI wa SHULE. Wanafunzi wameweza kupata uji wawapo masomoni. Vilevile MATUMIZI mengine ya Shule yameboreka kutokana na mapato ya Kilimo hiki.
Mwanafunzi Samwel Manyama wa Darasa la VII Shuleni hapo, amesema kwamba anafurahia SOMO la STADI za KAZI kwa sababu analisoma kwa VITENDO na yeye mwenyewe amekuwa ANAJITOLEA kuelimisha JAMII aliyomo juu ya aina hii ya Kilimo yenye faida kubwa zaidi kuliko ile ya Kilimo kilichozoeleka cha kutegemea MVUA.
Mtendaji wa Kijiji cha Lyasembe, Ndugu Chikonya Chikonya amesema MAPATO ya Kilimo ya Shule za Msingi mbili ziliko kwenye Kijiji hicho, yamesaidia KUBORESHA baadhi ya MIUNDOMBINU ya Shule zao.
Mtendaji huyo wa Kijiji anamshukuru sana Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo kwa juhudi zake za kuboresha Sekta ya Kilimo Jimboni mwao, ikiwemo kugawa bure MBEGU za ALIZETI, MIHOGO, MTAMA na ULEZI kwa Wanavijiji (Vijiji vyote 68) na kwenye Taasisi za Elimu zinazopenda kujishughulisha na KILIMO.
Vilevile, Wakulima wa Kijiji cha Lyasembe wanamshukuru Mbunge wao wa Jimbo kwa kuwapa PAMPU/MASHINE ya UMWAGILIAJI akina MAMA wa Kikundi cha TUPENDANE cha Kijiji hicho ambacho kimeleta hamasa kubwa ya KILIMO cha UMWAGILIAJI Kijijini hapo. PAMPU/MASHINE na vifaa vyake ilinunuliwa kwa kutumia Fedha za MFUKO wa JIMBO.

BOMBA LA MAJI SAFI NA SALAMA – MRADI WA MUGANGO-KIABAKARI-BUTIAMA

UWEKAJI wa SAINI za UTEKELEZAJI wa Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Maji la Mugango-Kiabakari- Butiama kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi ya Nyamisisi, Kata ya Kukirango, Kiabakari, Wilaya ya Butiama

AHADI ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt John Joseph Pombe Magufuli IMEANZA KUTEKELEZWA.
Mradi wa Bomba la Maji Safi na Salama la kutoka Ziwa Victoria (Mugango, Musoma Vijijini) hadi Wilaya ya Butiama (Kiabakari-Butiama) umeanza kutekelezwa kwa SERIKALI na MKANDARASI kuwekeana SAINI ya UTEKELEZAJI wa MRADI huu wenye Thamani ya US$ 30.69 million (Tshs 70 billion).
Maji kiasi cha LITA MILIONI 35 (35,000 cu.m.) yatazalishwa Kijijini Kwibara (Kata ya Mugango) na kusafirishwa na kusambazwa kwenye VIJIJI vya Jimbo la Musoma Vijijini (kwa kuanzia Vijiji vya Kata za Mugango na Tegeruka) na Vijiji vya Jimbo la Butiama. Mradi utakamilika ndani ya MIEZI 24.
Serikali iliwakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof Kitila Mkumbo. Mkoa uliongozwa na Mkuu wa Mkoa, Mhe Adam Malima. Wakuu wa Wilaya za Musoma na Butiama, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya 2 hizo, Madiwani na Viongozi wengine wa Chama na Serikali walihudhuria TUKIO hili muhimu kwa Mkoa wa Mara.
Chief Japhet Wanzagi Nyerere, Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Mkoa alihudhuria sherehe hizi.
Wabunge waliohudhuria ni Mhe Agnes Marwa, Mhe Amina Makilagi na Prof Sospeter Muhongo.
Wananchi na Viongozi wa Chama na Serikali wa Wilaya za Musoma na Butiama WANATOA SHUKRANI nyingi sana Mhe Rais Dkt John Joseph Pombe Magufuli na Viongozi wengine wote wa Serikali kwa KUKAMILISHA TARATIBU za UTEKELEZAJI wa Mradi huu.

MIRADI YA SEKTA YA AFYA NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

baadhi ya MAJENGO ya Hospitali ya Wilaya inayojengwa Jimboni mwetu (Kitongoji cha Kwikonero, Kijiji cha Suguti). DC, DED, MADIWANI na Wafanyakazi wa Halmashauri yetu WAPEWE PONGEZI nyingi sana kwa usimamiaji mzuri wa ujenzi wa Hospitali hii

Jimbo lina Kata 21, Vijiji 68, Vitongoji 374

ZAHANATI

* 24 za Serikali zinazotoa huduma

* 4 za Binafsi zinatoa huduma

* 13 MPYA zimeanza kujengwa na Wanavijiji wakishirikiana na Wadau wa Maendeleo yao

VITUO VYA AFYA

* 2 vya Serikali vinavyotoa huduma za Afya (Murangi & Mugango)

* 1 KIPYA kimeanza kujengwa na Wanavijiji (Kata ya Nyambono) wakishirikiana na Wadau wa Maendeleo yao

HOSPITALI YA WILAYA

* Inajengwa kwenye Kitongoji cha Kwikonero, Kijiji cha Suguti, Kata ya Suguti

* Serikali imetoa Tsh 1.5 bilioni kuanza ujenzi wake

* Kila Kijiji kimekubali kuchangia Tsh Milioni 2.

* Mbunge wa Jimbo amekubali kuchangia

ZAHANATI ZINAZOJENGWA NA WANAVIJIJI

(1) Kitongoji cha Burungu, Kijijini Bukumi, Kata ya Bukumi

(2) Kijijini Butata, Kata ya Bukima

(3) Kijijini Chimati, Kata ya Makojo

(4) Kijijini Chirorwe, Kata ya Suguti

(5) Kijijini Kakisheri, Kata ya Nyakatende

(6) Kijijini Kurwaki, Kata ya Mugango

(7) Kijijini Maneke, Kata ya Busambara

(8) Kijijini Mkirira, Kata ya Nyegina

(9) Kijijini Kurukerege, Kata ya Nyegina

(10) Kijijini Nyegina, Kata ya Nyegina

(11) Kijijini Mmahare, Kata ya Etaro

(12) Kijijini Bwai Kwitururu, Kata ya Kiriba

(13) Kijijini Nyasaungu, Kata ya Ifulifu

 

WANAFUNZI WA NYAMBONO SECONDARY SCHOOL WAFURAHIA MADAWATI YALIYOTOLEWA NA BENKI YA NMB

baadhi ya Wanafunzi, Walimu na Viongozi wa Kata ya Nyambono na Kijiji cha Saragana WAKIPOKEA MSAADA WA Benki ya NMB wa Madawati 50 na Viti 50. Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ALIWAKABIDHI Msaada huo wa Benki ya NMB.

Wanafunzi na Walimu wa Nyambono Secondary School iliyoko Kijijini Saragana, Kata ya Nyambono WANASHUKURU SANA SANA kwa MSAADA uliotolewa na Benki ya NMB wa MADAWATI 80 na VITI 80. Jana (07.08.2019), Shule iliyopokea Madawati 50 na Viti 50. Mengine yatapelekwa hivi karibuni.
Busambara Secondary School ya Kata ya Busambara itakayoanza kutoa Elimu ya Sekondari kuanzia Januari 2020 nayo IMEPOKEA MSAADA wa BENKI ya NMB wa MADAWATI na VITI ya idadi sawa na Nyambono Secondary School na kwa utaratibu huo huo.
WAZAZI na VIONGOZI wa Serikali na Chama (CCM) wa ngazi mbalimbali wa Kata ya Nyambono na Kijiji cha Saragana WAMETUMA SALAMU ZAO ZA SHUKRANI kwa BENKI YA NMB kupitia kwa Mbunge wao wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo.
Mwalimu Mkuu wa Nyambono Secondary School, Mwl Michael Mpasi, aliyekuwa mwenye furaha nyingi sana, amesema yeye mwenyewe ATATUMA SHUKRANI za KIPEKEE kwenye Benki ya NMB.
SHEREHE ZA UWEKAJI SAINI wa MRADI MKUBWA wa MAJI wa MUGANGO-KIABAKARI-BUTIAMA (BOMBA JIPYA LA MAJI)
Wananchi wanakaribishwa KUSHUHUDIA uwekaji SAINI kati ya SERIKALI na MKANDARASI wa UTEKELEZAJI wa Mradi huu. Gharama za Mradi ni US$ 30.69 (Takribani Tshs 70 bilioni).
Tukio hilo muhimu na kubwa litafanyika Kijijini Mugango (Mitambo ya Maji), tarehe 15.08.2019, saa 3 Asubuhi.
SHEREHE hiyo itatumbuizwa na KWAYA ya JIMBO na NGOMA ASILI ya JIMBO.
Vikundi hivi (Ngoma na Kwaya) vya Jimbo vitapatikana kwenye MASHINDANO ya NANENANE yatakayofanyika Jumamosi, 10.08.2019 kwenye Viwanja vya S/M Suguti, Kijijini Suguti.
Kata ipi itaibuka Mshindi wa Kwanza (Kikombe & Tsh Milioni 1) ya Ngoma za Asili? NGOMA ya Jimbo?
Kata ipi itaibuka Mshindi wa Kwanza (Kikombe & Tsh Milioni 1) wa KWAYA? KWAYA ya Jimbo?

UONGEZAJI WA HIGH SCHOOLS NA UBORESHAJI WA ELIMU YA SAYANSI KWENYE SEKONDARI ZETU

Moja wapo ya Vikao 2 vya Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo. Hapa anaonekana akiwa na BODI ya Nyegina Secondary School.

*IDADI YA SHULE ZA MSINGI
Jimbo lina Jumla ya Shule za Msingi 111 za  Serikali na 3 za Binafsi
Wananchi, Madiwani na Viongozi wao wengine, kwa kushirikiana na SERIKALI na Mbunge wao wa Jimbo wanajenga SHULE SHIKIZI mpya 10. Shule hizi hapo baadae zitapanuliwa na kuwa Shule za Msingi kamili zenye Darasa la I hadi VII.
* IDADI YA SHULE ZA SEKONDARI
Jimbo lina Jumla ya Sekondari 18 za Serikali na 2 za Binafsi.
Wananchi, Madiwani na Viongozi wao wengine, kwa kushirikiana na Serikali na Mbunge wao wa Jimbo wanajenga Sekondari mpya 8.
UAMUZI WA KUONGEZA HIGH SCHOOLS JIMBONI
Jimbo hili lina High Schools 2 tu, yaani Kasoma High School (Serikali) yenye MASOMO ya ARTS tu, na Nyegina High School (Binafsi, Katoliki) yenye MASOMO  ya SAYANSI  na ARTS.
MAPENDEKEZO YA KUONGEZA HIGH SCHOOLS ZA SERIKALI
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo amefanya VIKAO na Wananchi na Viongozi mbalimbali AKIWASHAWISHI kuboresha MIUNDOMBINU (k.m. Maabara, Ujenzi wa Mabweni) ya baadhi ya Sekondari zetu ili ZIPANULIWE na kuanza kutoa Elimu ya Kidato cha V na VI ya Masomo ya Sayansi.
Mapendekezo haya yanaungwa mkono na Wananchi na Viongozi wao wa ngazi mbalimbali wakiwemo MAAFISA ELIMU wa Halmashauri yetu.
Sekondari za BUGWEMA, MTIRO, MUGANGO na MKIRIRA ndizo ziko juu kwenye orodha ya kuweza KUANZISHA HIGH SCHOOLS za Masomo ya Sayansi. Sekondari nyingine nazo zina nafasi sawa na hizo iwapo Miundombinu ya Elimu ya kuanza High Schools itakuwepo. Kwa hiyo, kinachotakiwa ni KUWEKA MIUNDOMBINU INAYOHITAJIKA kukidhi MATAKWA ya uwepo wa High Schools.
Wananchi, MADIWANI,  Mbunge wa Jimbo kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Halmashauri, Ndugu John Kayombo na Mkuu wa Wilaya, Dr Vicent Naano Anney WATATEKELEZA MRADI huu wa Ongezeko la High Schools za Serikali kwenye Jimbo letu.
Njia ya pili ya kuongeza High Schools Jimboni mwetu ni kukaribisha uanzishwaji wa High Schools za Binafsi (Private High Schools).
Mbunge wa Jimbo amefanya KIKAO na BODI ya Secondary ya Nyegina (Binafsi, Katoliki) na KUKUBALIANA kuimarisha na kuboresha High School yao. Mipango ya Utekelezaji inatayarishwa ili KUONGEZA IDADI ya Wanafunzi wanaosoma Masomo ya Sayansi  ya Kidato cha V na VII Shuleni hapo.
Mbunge wa Jimbo hakuweza kufanya Kikao na BODI ya Bwasi Secondary School baada ya Shule hiyo kupata msiba. Kikao hicho kitafanyika baadae. Uongozi wa Bwasi Secondary School UNAKUBALIANA NA pendekezo la KUANZISHA High School yenye Masomo ya Sayansi.
MRADI WA KUBORESHA ELIMU YA SAYANSI KWENYE SEKONDARI ZETU
Mbunge wa Jimbo amefanya VIKAO 2, kimoja (06.08.2019) na BODI ya Nyegina Secondary School, na kingine (07.08.2019) na AFISA ELIMU (DEOs) na Viongozi wengine wa Idara ya Elimu ya Halmashauri yetu kuhusu suala hili.
IMEKUBALIWA kwamba MRADI uanzishwe kwa UTEKELEZAJI wa pendekezo hili na Kituo cha Utekelezaji kiwe Kijijini Nyegina kwenye Madaraka Nyerere Library and Community Resource Center. Idara ya Elimu ya Halmashauri yetu na Mbunge wa Jimbo watashiriki kwenye Mradi huu. Wataalamu wa Elimu wanatayarisha MIPANGO ya UTEKELEZAJI wake.
KWA NINI TUNASISITIZA KUBORESHA ELIMU YA SAYANSI?
*Taifa litakalokuwa na UBUNIFU (INNOVATION) mkubwa kwenye TEKNOLOJIA na SAYANSI ndilo LITATAWALA UCHUMI wa Dunia yetu kwenye Karne hii na zijazo. Wenzetu wameingia kwenye “4th Industrial Revolution” ambayo imejikita kwenye Cyber Space, Digital Codes, Internet of Things (IoT), Artificial Intelligence (AI), Robotics, Genetic Engineering, Nanotechnologies, n.k. Africa isiachwe nyuma sana, nasi tupate Wanasayansi Mahiri.

WAFUGAJI WAAMUA KUTUMIA MIFUGO YAO KUCHANGIA UJENZI WA SEKONDARI MPYA, ZAHANATI NA VYUMBA VYA MADARASA KWENYE SHULE YA MSINGI

HARAMBEE ya WANAKIJIJI na Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo ya ujenzi wa Nyasaungu Secondary School na Zahanati

Wakazi wengi wa Kijiji cha Nyasaungu ni WAFUGAJI. Kijiji hiki kiko ndani ya Kata ya Ifulifu, Musoma Vijijini.
Kata ya Ifulifuli haina Sekondari ya Kata. Watoto wa Kata hii wanatembea umbali usiopungua kilomita 3 kwenda kwenye Sekondari za Kata jirani – Mugango na Nyakatende Secondary Schools.
Kwa kuzingatia JIOGRAFIA (k.m. mito na mabonde) ya Kata ya Ifulifu, Wakazi wa Vijiji vya Kabegi na Kiemba (Kata ya Ifulifu) wanajenga Sekondari yao. Wakazi wa Kijiji cha Nyasaungu (Kata ya Ifulifu) nao wanajenga Sekondari yao.
MTINDO WA UCHANGIAJI WA KIJIJI CHA NYASAUNGU
Wanakijiji wa Kijiji hiki WAMEKUBALIANA kwamba MICHANGO yao kwenye MIRADI ya Maendeleo ITAZINGATIA WINGI  WA MIFUGO aliyonayo mchangiaji. Kwa MFANO kwenye kila awamu ya MCHANGO wenye NG’OMBE ZAIDI ya 51, wanachangia Tsh 200,000 (laki 2).
Kutokana na UTARATIBU huo wa uchangiaji, Kijiji kina MIRADI 3 inayotekelezwa kwa wakati mmoja – (i) Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji, (ii) Ujenzi wa Vyumba 2 vya Madarasa kwenye Shule ya Msingi Nyasaungu na (iii) Ujenzi wa Sekondari yao.
HARAMBEE ZA MBUNGE WA JIMBO
Leo, Jumatatu, 05.08.2019, Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo AMEPIGA HARAMBEE 2 Kijijini Nyasaungu na matokeo ni haya:
(i) HARAMBEE ya Ujenzi wa Nyasaungu Secondary School.
SARUJI:
*Wanakijiji na Viongozi wao wamechangia SARUJI MIFUKO 67
*Mbunge wa Jimbo amechangia SARUJI MIFUKO 35
NONDO
*Wanakijiji na Viongozi wao wamechangia NONDO 27
* Mbunge wa Jimbo amechangia NONDO 20
(ii) HARAMBEE ya Ujenzi wa Zahanati
*Mbunge wa Jimbo alishachangia SARUJI MIFUKO 100
*Leo, 05.08.2019, Wanakijiji na Viongozi wao wamechangia NONDO 20
*Leo, 05.08.2019, Mbunge wa Jimbo amechangia NONDO 20.

SEKONDARI MOJA YA KATA HAITOSHI – WANANCHI WAAMUA KUJENGA SEKONDARI YA PILI

Kikao cha Mbunge Prof Sospeter Muhongo na WANAVIJIJI kwenye eneo la ujenzi wa Sekondari MPYA ya PILI ya Kata ya Nyakatende

NYAKATENDE SECONDARY SCHOOL iliyo kwenye Kata ya Nyakatende inahudumia Kata 2 – Kata ya Nyakatende (Vijiji 4) na Kata ya Ifulifu (Vijiji 3). Kwa hiyo MSONGAMANO MADARASANI ni mkubwa.
Kata ya IFULIFU isiyokuwa na Sekondari, IMEAMUA kujenga Sekondari 2 kwa wakati mmoja. Kijiji cha Nyasaungu kinajenga Sekondari yake na Vijiji vingine 2 (Kabegi na Kiemba) vinajenga Sekondari yao.
Mbali ya Kata ya Ifulifu kujenga Sekondari zake, bado masuala ya UMBALI na WINGI wa Wanafunzi ndani ya Kata ya NYAKATENDE,  vimelazimisha Wananchi wa Kata hiyo KUAMUA kujenga Sekondari ya pili.
SEKONDARI MPYA ya Kata ya Nyakatende inajengwa kwenye Kijiji cha KIGERA ETUMA. Sekondari hii inajengwa na Vijiji 2 – Kigera Etuma na Kakisheri
MAENDELEO YA UJENZI
MABOMA ya Vyumba 2 vya Madarasa yamefikia hatua ya kuezekwa na MATOFALI ya kutosha ujenzi wa JENGO LA UTAWALA yapo tayari.
MICHANGO YA WANANCHI
Wananchi WAMEKUBALIANA kila mwenye umri wa kuanzia MIAKA 18 achangie TOFALI MOJA. Mawe, kokoto, mchanga na maji vinasombwa kwa zamu, Kitongoji kwa Kitongoji.
WADAU WANAOCHANGIA UJENZI HUU
Mbali ya MICHANGO ya thamani ya TOFALI MOJA ya Wanavijiji wenyewe, WAVUVI na WACHIMBAJI Wadogo Wadogo nao wanachangia ujenzi huu.
MICHANGO YA WAZALIWA WA VIJIJI VYA KIGERA ETUMA NA KAKISHERI
Hawa ni WADAU WAKUU wa Mradi huu na kwa sasa wafuatao wameunda KIKUNDI kwa ajili ya kuchangia ujenzi huu:
(1) Nyakiriga Kabende-Mwenyekiti
(2) Albinus Makanyaga-Mhasibu
(3)Joseph Mnibhi – Katibu
(4) Augostino Eugene
(5) Joseph Surusi
(6) Wambura Mujungu
(7) Marere Eugene
(8) Mareges Eugene
(9) Emmanuel Ekama
(10) Mareges Jela
(11) Kisha Charamba
(12) Garani Magafu
(13) Mugini Kibusi Marere
(14) Ngajeni Manumbu
(15) Lucas Mashauri
(16) Mutandu Kabende
(17) Boniphace Kitende
(18) Boniphace Changanya
HARAMBEE YA MBUNGE
Leo, Ijumaa, 02.08.2019, Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo AMEENDESHA HARAMBEE YA UJENZI wa Sekondarii hii MPYA inayojengwa Kijijini Kigera Etuma.
HARAMBEE imefanikisha kupata:
(i) Fedha: 324,000/= kutoka Wanavijiji waliokuwepo
(ii) SARUJI MIFUKO 68 kutoka kwa Wanavijiji waliokuwepo
(iii) SARUJI MIFUKO 100 kutoka kwa Mbunge Prof Sospeter Muhongo
UJENZI UNAENDELEA KWA KASI KUBWA – KARIBU TUCHANGIE UJENZI WA SEKONDARI MPYA INAYOJENGWA NA VIJIJI VIWILI.

UKARABATI WA MABWENI YA SEKONDARI YA BWASI

Ukarabati na Uboreshaji wa Mabweni ya Bwasi Secondary School (private, SDA) iliyoko Kijijini Bwasi, Kata ya Bwasi.

Jumatatu, 29.07.2019
Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
Shule ya Sekondari Bwasi ni moja ya Sekondari mbili za Binafsi (private) zilizopo kwenye Jimbo la Musoma Vijijini. Nyingine ni Nyegina Secondary School inayomilikiwa na Kanisa Katoliki.
Bwasi Secondary School INAMILIKIWA na Kanisa la Waadventista Wasabato na ipo kwenye Kijiji cha Bwasi. Ilianzishwa Mwaka 1987.
Matokeo ya Mitihani ya Mwaka jana (2018) ya Form IV yalikuwa ya KURIDHISHA: Division I walifaulu wawili (2), Division II kumi (10), Division III ishirini (20) na Division IV wanne (4).
MAABARA
Bwasi Secondary School ina MAABARA zote tatu, yaani za Physics, Chemistry na Biology. Maabara hizi zinahitaji UBORESHWAJI mkubwa.
MABWENI:
Kwa sasa ukarabati unaendelea kwenye MABWENI 2 yote yenye uwezo wa kuchukua WANAFUNZI 140 –  moja la Wasichana na jingine la Wavulana. Bado kuna upungufu wa BWENI MOJA la Wasichana.
Mkuu wa Sekondari hii, Mwalimu Ibrahim Chacha amesema kwamba Miundombinu ya Shule hiyo haijakarabatiwa kwa muda mrefu, kwa hiyo sasa Shule imeamua kufanya ukarabati na UBORESHAJI wa Miundombinu hiyo ili KUBORESHA MAZINGIRA ya Utoaji na Upokeaji/Upataji wa Elimu bora.
Mwalimu Mkuu huyo anawashukuru Wadau wa Elimu walioguswa na kuhamasika katika uchangiaji wa kukamilisha kazi hii.
Wanafunzi wa Sekondari hii  wamefurahishwa na ukarabati wa MABWENI yao na wamehaidi kusoma kwa bidii na kufaulu vizuri zaidi.
HARAMBEE iliyofanyika kwenye Mahafali ya Kidato cha IV (2018) iliwezesha Shule kuanza ukarabati wa Mabweni hayo mawili. Baadhi ya WALIOCHANGIA siku hiyo ni: (1) Prof Lawrence Museru, (2) Dr Freddy Jirabi Gamba, (3) Ndugu Misana Gamba, (4) Ndugu Shauri Makota, (5) Mara Conference of Seventh Day Adventist Church na (6) Watumishi wa Sekondari hiyo.
Mbunge wa Jimbo Profesa Sospeter Muhongo akishagawa VITABU vya SEKONDARI mara mbili kwenye Shule hiyo na kwenye HARAMBEE hiyo alichangia SARUJI MIFUKO 50 kwa ajili ya ukarabati wa Bweni la Wasichana.
Tarehe 05.08.2019, Mbunge huyo atafanya KIKAO na BODI ya Sekondari hii AKIWA na LENGO la KUWASHAWISHI kuanzisha BWASI HIGH SCHOOL yenye MASOMO ya SAYANSI.

MBEGU YA  MIHOGO YA AINA YA MKOMBOZI YANUFAISHA WAKULIMA JIMBONI

Ndugu Ladislaus Manumbu na familia yake wakipalilia SHAMBA lao la MIHOGO lililotumia Mbegu ya MKOMBOZI. Hapo ni Kijijini Bukima.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
UCHUMI na AJIRA kuu kwa Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini viko kwenye SEKTA za Kilimo, Uvuvi, Ufugaji na Biashara. Sekta ya KILIMO ndiyo uti wa mgongo wa UCHUMI na AJIRA kubwa zaidi kuliko hizo nyingine.
MAZAO Makuu ya CHAKULA ni MIHOGO, MAHINDI, MTAMA, VIAZI VITAMU na MPUNGA.
ZAO kuu la BIASHARA ni PAMBA  na kwa misimu mitatu hii ya kilimo (2016/17- 2018/19), zao la ALIZETI nalo limeanza kulimwa Jimboni mwetu. Kilimo cha MPUNGA na MIHOGO nacho kinasisitizwa kiwe kwa ajili ya CHAKULA na BIASHARA.
MRADI MKUBWA WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI WA BONDE LA BUGWEMA, ulionzishwa na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu J.K.Nyerere, UNAFUFULIWA.
KILIMO cha UMWAGILIAJI kwenye Bonde la BUGWEMA lenye ukubwa wa Ekari 5,075 utakuwa wa Ushirika kati ya WANAVIJIJI, HALMASHAURI na BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO TANZANIA (TADB). Mazao yatakayozalishwa kwenye Bonde hili ni: MPUNGA, MAHINDI, VITUNGUU, DENGU, ALIZETI na PAMBA.
Kijiji cha Bukima ni miongoni mwa Vijiji 68 vya Jimbo la Musoma Vijijini ambacho shughuli zake kuu za UCHUMI ni KILIMO na UVUVI.
Mazao cha Chakula ya Wakazi wa Kijiji cha Bukima ni: mihogo, viazi vitamu na viazi lishe, mahindi, mpunga, mtama na mbogamboga. Kilimo chao ni cha mazoea!
Ndugu Ladislaus Manumbu ni miongoni mwa Wakulima wachache maarufu wa ZAO la MIHOGO ambae AMEAMUA kutumia MBEGU ya MIHOGO ya aina ya MKOMBOZI.
Ndugu Manumbu anaeleza kwamba baada ya kupokea vijiti vya mihogo aina ya MKOMBOZI amefuata MAELEKEZO ya KILIMO BORA na kufanikisha kupata MAVUNO MAZURI kwa misimu mitatu mfululizo. Kila Ekari anavuna MAGUNIA kati ya 16 na 20. MBEGU za ASILI hutoa MAGUNIA kati ya 5 na 6 kwa Ekari moja. Vilevile, Mbegu ya MKOMBOZI inastahili MAGONJWA.
Baada ya MAVUNO mazuri kutoka Mbegu ya MKOMBOZI, Wanavijiji jirani wameomba na kupewa mbegu hiyo na Ndugu Manumbu. Mbegu hii ya MKOMBOZI kwa sasa inatumiwa na Wakulima wengi kwenye Jimbo la Musoma Vijijini.
Mtendaji wa Kijiji cha Bukima, Ndugu Josephat Phinehas amesema anashirikiana na Afisa Kilimo kukuza na kuboresha Kilimo cha Mihogo Kijijini Bukima.
Wananchi na Viongozi wa Kijiji cha Bukima na Vijiji vingine Jimboni wanamshukuru sana Mbunge wao, Profesa Sospeter Muhongo kwa juhudi zake za KUBORESHA  KILIMO cha Mazao ya CHAKULA na BIASHARA Jimboni mwao. Mbunge huyo AMEGAWA BURE Mbegu za ALIZETI, MTAMA, MIHOGO na ULEZI kwa Wakulima ndani ya Vijiji vyote 68 vya Jimbo hilo.

HALMASHAURI YASHIRIKIANA NA MRADI WA BMZ (Ujerumani) KUTOA HUDUMA KWA VITUO VYA ELIMU YA WATOTO WENYE ULEMAVU 

Wanafunzi wenye ULEMAVU wakiwa masomoni, baada ya kupata Kifungua Kinywa (breakfast) Shuleni kwao, S/M Nyambono B, Kijijini Saragana, Kata ya Nyambono.

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
Vituo vya Elimu ya Wanafunzi wenye ULEMAVU ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini vimeanza kuhudumiwa na Halmashauri yao kwenye Kata za Nyambono, Mugango na Nyegina.
Vituo hivi vya Elimu vinajumuisha WATOTO wenye ULEMAVU wa Akili, Bubu, Viwete, Viziwi,  Vipofu na Wagonjwa wa Ngozi (Albino).
Kwenye Kata ya  Nyambono, Wanafunzi 20 wenye Ulemavu wanapata ELIMU ya MSINGI kwenye S/M Nyambono B, Kijijini Saragana.
Mwalimu Mkuu wa S/M Nyambono B, Mwl Abel Paul ambae pia ni Mwalimu anaefundisha Watoto wenye Ulemavu na Uhitaji wa Elimu Maalum, amesema ELIMU MAALUM hiyo ilianza kutolewa hapo Shuleni Mwaka 2017, baada ya kufanikiwa  kuwatafuta majumbani na kuwaleta Shuleni Watoto wenye Ulemavu.
Mwalimu Mkuu huyo amesema Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (yenye Jimbo la Musoma Vijijini) imekuwa ikitoa Fedha zinazosaidia Wanafunzi hao kupata Kifungua Kinywa (breakfast) wafikapo Shuleni asubuhi.
MRADI wa BMZ (Ujerumani) unatoa VIFAA MBALIMBALI vinavyohitajika kwa WANAFUNZI hao kama vile,  baiskeli, miwani ya kusomea, madaftari, kalamu, mabegi, n.k.
WANAFUNZI wenye ULEMAVU wanashukuru HALMASHAURI yao na MRADI wa  BMZ wa UJERUMANI kwa MISAADA yao inayowawezesha kupata Elimu.
Baadhi ya Wanafunzi wenye Ulemavu wa S/M Nyambono B wanakiri na kusema: “Mimi Magesa Adonias nimepewa Baiskeli ya kutembelea inayomwezesha kufika Shuleni, na baadae napenda kuwa Mwalimu” – alijieleza kwa Kiingereza chenye ufasaha mzuri.
Mwl Abel ameomba WADAU wa Maendeleo kuchangia ujenzi wa Vyumba vya Madarasa kwa ajili ya Matumizi ya Wanafunzi hao wenye Ulemavu hapo Shuleni.
Mbunge wa Jimbo Prof Muhongo amepokea ombi la Shule hiyo na AMEKUBALI KUCHANGIA ujenzi wa Vyumba vya Madarasa ya WANAFUNZI wenye ULEMAVU – KARIBUNI TUCHANGIE!

UJENZI WA SHULE SHIKIZI MWALONI KIJIJINI BURAGA UNAENDELEA VIZURI

Ujenzi wa BOMA la Vyumba Viwili (2) vya Madarasa na Ofisi 1 ya Walimu kwenye Shule Shikizi Mwaloni, Kijijini Buraga, Kata ya Bukumi.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
Ujenzi wa Shule Shikizi Mwaloni  kwenye Kitongiji cha Mwaloni, Kijiji cha Buraga, Kata ya Bukumi umefikia hatua nzuri ambapo Boma la Vyumba Viwili (2) vya Madarasa na Ofisi moja (1) ya Walimu limeanza kunyanyuliwa.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Buraga, Ndugu Gerald Mageta ameelezea mafanikio ya ujenzi huo kuwa, mbali na MICHANGO ya WADAU wa Maendeleo, WAKAZI wa Kitongoji wa Buraga wanachangia NGUVUKAZI zao ikiwemo kusomba mawe, mchanga na maji ya ujenzi. Vilevile wanachanga  Tsh 5,000/- (elfu tano) kutoka kila Kaya.
Baada ya kukamilisha ujenzi wa BOMA hilo kifuatacho ni ujenzi wa Matundu 4 ya Choo, Nyumba moja  ya Mwalimu na baade kuongeza Vyumba vya Madarasa kwa ajili ya kuwa na Shule ya Msingi yenye Darasa la I hadi la VII.
WAKAZI wa Kitongoji cha Mwaloni na Kijiji cha Buraga kwa ujumla wao, WANAOMBA WAZALIWA na WADAU wa Maendeleo  wajitokeze KUCHANGIA ujenzi huu – hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Buraga, Ndugu Gerald Mageta.
Kwa upande wake, Mlezi wa Shule Shikizi Mwaloni, Mwl  Robart Marwa ameiomba SERIKALI na WADAU wengine wa Maendeleo waendelee kuunga mkono jitihada za Wanakijiji hao ili waweze kuondoa tatizo la Watoto zaidi ya 80 ambao hutembea umbali wa kilomita zaidi ya 4 kwenda masomoni kwenye Shule za Msingi za jirani zilizoko Vijiji vya Chitare na Buraga.
Aidha Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Shule hiyo, Ndugu Nyajoge Nyanjara amesema kwa sasa wana jumla ya WANAFUNZI 51 wa UTAYARI ambao wanasomea chini ya  MTI kwa sababu ya UKOSEFU wa Vyumba vya Madarasa.
Wananchi wa Kitongoji cha Mwaloni na wa Kijiji chote cha Buraga WANAMSHUKURU Mbunge wao Profesa Sospeter Muhongo kwa MCHANGO wake wa SARUJI MIFUKO 50. Vilevile MFUKO wa JIMBO umewachangia SARUJI MIFUKO 50.
Shule ya Shikizi Mwaloni ni kati ya  Shule Mpya 10 (kumi) za Msingi zinazojengwa (na nyingine zimekamilisha ujenzi) Jimboni mwetu. Kwa sasa Vijiji vyetu 68 vina jumla ya Shule za Msingi 113 (111 za Serikali na 2 za Binafsi).
Jimbo la Musoma Vijijini linaelekea kwenye KILA KIJIJI  kuwa na SHULE za MSINGI MBILI (2). TUMEDHAMIRIA, TUTAFANIKIWA!

WANAKIJIJI NA SERIKALI KUPITIA MRADI WA EQUIP  WAKAMILISHA UJENZI WA SHULE SHIKIZI MWIRINGO

Shule SHIKIZI Mwiringo ikiwa imekamilika na tayari kupokea Wanafunzi kutoka Kitongoji cha Ziwa na kwingineko Kijijini Mwiringo, Kata ya Busambara.

Jumanne, 09.07.2019
Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
Wananchi wa Kijiji cha MWIRINGO, Kata ya Busambara WAMESHIRIKIANA na SERIKALI yetu kupitia Mradi wake na Wafadhili wa EQUIP kufanikisha ujenzi wa Shule SHIKIZI Kijijini humo.
Shule hiyo imejengwa kwenye Kitongoji cha Ziwa ndani ya Kijiji cha Mwiringo.
Shule Shikizi Mwiringo ni kati ya SHULE KUMI (10)  MPYA za MSINGI zinazojengwa kwenye Jimbo la Musoma Vijijiji lenye Jumla ya Shule za Msingi 113 (111 za Serikali na 2 za Binafsi).
Ujenzi wa hizo Shule kumi (10) ukikamilika na baadae zikapanuliwa ili kuchukua Wanafunzi wa Darasa la I hadi VII, Jimbo letu litakuwa na Jumla ya Shule za Msingi 123 (121 za Serikali na 2 za Binafsi). Safari ya kuelekea kwenye SHULE ZA MSINGI MBILI (2) KWA KILA KIJIJI (Vijiji 68, Kata 21) inaenda vizuri!
EQUIP (The Education Quality Improvement Programme) ilitoa Shilingi MILIONI 60 kwa ajili ya ujenzi wa: (i) Vyumba viwili (2) vya Madarasa,  (ii) Ofisi moja (1) ya Walimu, na (iii) Matundu sita (6) ya Vyoo, yaani 4 ya Wanafunzi na 2 ya Walimu.
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Mwiringo, Mwl Surusi Mnene ambae ndie Mlezi wa Shule hiyo SHIKIZI, alieleza kuwa ujenzi huo ulianza Januari 2019 na hadi hivi sasa ujenzi umekamilika. Matenki mawili (2) ya kuvuna MAJI yako tayari na Mafundi wanakamilisha MADAWATI 50.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mwiringo, Ndugu Coletha Felix alieleza kuwa amefurahishwa sana na Jitihada za Wananchi wa Kijiji cha Mwiringo kwa NGUVUKAZI zao na ushirikiano wao mkubwa waliouonesha katika kuhakikisha ujenzi huo unakamilika haraka. Wananchi hao wamejitolea kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji kwa ajili ya ujenzi huu.
Wanakijiji cha Mwiringo na Viongozi wao wa Jimbo la Musoma Vijijini, kwa pamoja, wanaishukuru sana SERIKALI yetu kwa jitihada kubwa inazofanya kwa kuwaunga mkono kwenye MIRADI ya MAENDELEO ikiwemo Miradi ya ELIMU na AFYA Kijijini mwao.

MRADI WA USAMBAZAJI WA MAJI  WATEKELEZWA KWENYE VIJIJI VITANO (5)

Utekelezaji wa MRADI wa USAMBAZAJI MAJI kwenye Vijiji vya Busungu, Bukima na Kwikerege.

Jumapili, 07.07.2019
Jimbo la Musoma Vijijini
Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
MRADI wa USAMBAZAJI WA MAJI kwenye Vijiji vitano (5) umegawanywa kwenye Makundi mawili (2 LOTS) ili kuharakisha UTEKELEZAJI wake.
KUNDI I (Lot I)
Bulinga-Bujaga: Maji yatachukuliwa kutoka Kijijini Bujaga kwa ajili ya kusambaza kwenye Vijiji vya Bujaga na Bulinga, vyote vya Kata ya Bulinga. Mradi huu unatekelezwa na Mkandarasi MEDES COMPANY Ltd na gharama yake ni  Tsh.1,812,675,036 (Tsh 1.81 bilioni).
MRADI huo ulizinduliwa wakati wa Mbio za Mwenge kwenye Jimbo la Musoma Vijijini, tarehe 31.05.2019.
KUNDI II (Lot II)
Busungu-Bukima-Kwikerege: Maji yatachukuliwa kutoka Kijiji cha Bujaga na kusambazwa Vijijini Busungu (Kata ya Bulinga), Bukima (Kata ya Bukima) na Kwikerege (Kata ya Rusoli)
UTEKELEZAJI wa Mradi wa Usambazaji wa MAJI kwenye Vijiji hivyo vitano (5) unaendelea kwa kasi ya kuridhisha.
MRADI wa Busungu-Bukima-Kwikerege: unagharimu Tsh 1, 022, 531, 876 (Tsh 1.02 bilioni), unatekelezwa na Mkandarasi EDM NETWORK LTD JV FAU CONSTRUCTION LTD.
Kazi zinazotekelezwa ni pamoja na:
(i) Ujenzi wa Tenki lenye ujazo wa LITA 225,000, (ii) Ofisi ya Mradi, (iii) Vituo 18 vya kuchotea Maji, (iv) Viosk 2 vya kuuzia Maji, (v) Birika za kunyweshea MIFUGO na (vi) Utandazaji wa MABOMBA ya kusambaza MAJI.
Mkandarasi anayesimamia Mradi huu, Injinia Bosco Victor Sechu anasema kuwa hadi sasa wamejenga Vituo 18 vya maji, Ofisi, Viosk na Birika za kunyweshea MIFUGO. MRADI  unatekelezwa kwa muda wa MWAKA MMOJA na utakamilika ifikapo Septemba 2019.
Ndugu Charles Ndagile, Mtendaji wa Kijiji (VEO) cha Busungu ameeleza kwamba WANANCHI wa Eneo la MRADI wameupokea vizuri Mradi huu na KUKUBALI KUTOA MAENEO ya ARDHI yao ili kutandaza MABOMBA bila kudai fidia yo yote.
Aidha kukamilika kwa MRADI huu kutaondoa UKOSEFU wa upatikanaji na MAJI safi na salama kwa hivyo Vijiji na  akina MAMA hawatatembea tena umbali mkubwa kwenda kuteka MAJI.
Taratibu za kumpata Mkandarasi wa Mradi wa Vijiji vya Bugunda, Bwasi, Chimati na Kome zimeanza.
Kwa niaba ya WANANCHI wa Jimbo la Musoma Vijijini, Mbunge wa Jimbo, Profesa Sospeter Muhongo anaendelea KUISHUKURU SANA SERIKALI kwa juhudi zake za kuanzisha na kutekeleza MIRADI ya USAMBAZAJI wa MAJI Vijijini mwao.

KIKUNDI CHA NGUVUKAZI CHATOA MSAADA WA CHAKULA SHULENI

Kikundi cha NGUVUKAZI kikiwa na mavuno ya MAHINDI kutoka shambani mwao

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
Jumamosi, 29.06.2019
Kikundi cha NGUVUKAZI kilichopo Kijiji cha Buanga, Kata ya Rusoli kilianzishwa Mwaka jana (2018) wakiwa chini ya Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Jamii (PCI, Project Concern International) lililowapa MAFUNZO ya KILIMO Wanachama wa Kikundi hicho na baadae wakaanzisha KILIMO cha MAHINDI, VIAZI LISHE, na MPUNGA.
Afisa Kilimo wa Kata, Ndugu Sevas Ngova ameeleza kwamba Kikundi cha NGUVUKAZI kilipata MAFUNZO ya ZAO JIPYA JIMBONI la ALIZETI na baada ya MAFUNZO walianza na SHAMBA DARASA kwa kutumia Mbegu walizopewa na Mbunge wa Jimbo,
Profesa Sospeter Muhongo. Mavuno ya awali ya ALIZETI yalikuwa ya MAGUNIA 10. Mbegu nyingine walizopokea kutoka kwa Mbunge wao huyo ni za MTAMA, MIHOGO na UFUTA.
Ndugu Tore Masamaki, Mwenyekiti wa Kikundi cha NGUVUKAZI ameeleza kwamba Kikundi hicho kilianza na WANACHAMA 18 na baada ya MAFANIKIO ya kuridhisha kupatikana, Wanachama wameongezeka na kufikia 30 (thelathini).
Kikundi cha NGUVUKAZI kinaendelea kushirikiana na Shirika la PCI ambalo moja ya malengo yake makuu ni kutoa CHAKULA mashuleni, ikiwemo Shule ya Msingi Bwenda.
“Kupitia Kikundi hiki mavuno yanayopatikana hupelekwa shuleni hapo, na mengine ni kwa manufaa yao wenyewe na familia zao – Ndugu Masamaki aliyasema haya na kuongeza kwamba sasa wanatafuta VIFAA vya UMWAGILIAJI waanze Kilimo hicho.
Mwalimu Mkuu wa S/M Bwenda, Mwl Christopher Cosmas  amekiri kupokea jumla ya KILO 220  za MAHINDI kutoka Kikundi cha NGUVUKAZI  kwa ajili ya CHAKULA cha WANAFUNZI.
Mwalimu Mkuu huyo anasema CHAKULA kinachotelewa kwa WANAFUNZI wote hapo Shuleni kimefanya UTORO usiwepo na HAMASA ya Wanafunzi kupenda kupata ELIMU imeongezeka.
Aidha Diwani wa Kata ya Rusoli, Mhe Boaz Nyeura ameshukuru Kikundi cha NGUVUKAZI kwa jitihada zake na kupitia vikao vya hadhara ameomba VIKUNDI vingine kujitokeza kusaidia UPATIKANAJI wa CHAKULA kwa Shule nyingine ndani ya Kata yao ya Rusoli.

KILIMO CHA UMWAGILIAJI CHANUFAISHA KIUCHUMI KIKUNDI CHA MKULIMA JEMBE CHA KATA YA BUKIMA

WANACHAMA wa Kikundi cha MKULIMA JEMBE wakiwa kwenye SHAMBA lao la MATIKITI, Kijijini Kastam, Kata ya Bukima.

Jumapili, 23.06.2019
Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
Kikundi cha MKULIMA JEMBE kilichopo Kijiji cha Kastam, Kata ya Bukima kilianzishwa Mwaka 2014  kikijishughulisha na uoteshaji wa MICHE badaye  walifanikiwa kuanzisha KILIMO cha UMWAGILIAJI wakilima MBOGAMBOGA, MATUNDA pamoja na mazao ya CHAKULA – viazi vitamu, maharage na mahindi.
Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Ndugu Festo Obed ameeleza kuwa  kupitia KILIMO cha UMWAGILIAJI  wamefanikiwa kununua Mashine/Pampu ya Umwagiliaji ya SOLAR, kusomesha Watoto wao na kujikimu kwenye matumizi mengine ya kifamilia. Fedha zao zinatunzwa Benki.
Ndugu Obed ameendelea na kusema kwamba, Kikundi cha MKULIMA JEMBE kimefanikia kuanzisha Kikundi kingine kiitwacho “TUMETAMBUA” ambacho kinajishughulisha na Kilimo cha Umwagiliaji na kina Mradi wa KUWEKA na KUKOPESHANA.
Afisa Kilimo wa Kata ya Bukima, Ndugu Mushangi Salige ameeleza kuwa Kata hiyo  ina fursa kubwa ya kupanua KILIMO cha UMWAGILIAJI kwa sababu Wakazi wengi wapo kando kando mwa Ziwa Viktoria.
Afisa Kilimo huyo amemshukuru sana Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo kwa kuwezesha Kikundi cha MKULIMA JEMBE kupata Vifaa vya Umwagiliaji (pampu na mipira) kutoka MFUKO wa JIMBO. Kikundi hicho na vingine Jimboni viligawiwa bure MBEGU za Mbogamboga na  Matunda.
Vilevile Wanavijiji wa Kata hiyo ya Bukima wanamshukuru sana Mbunge wao Prof Muhongo kwa KUWAGAWIA BURE Mbegu za ALIZETI, MTAMA na MIHOGO, amesema Afisa Kilimo huyo.