KILIMO CHA MIHOGO CHAENDELEA KUBORESHWA MUSOMA VIJIJINI

WANACHAMA wa  Kikundi cha KILIMO cha TUMEJITAMBUA wakiwa kwenye kazi za UOTESHAJI wa MITI na kwenye mashamba yao ya MIHOGO. Hapo ni Kijijini Bwenda, Kata ya Rusoli 

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
MAZAO MAKUU ya CHAKULA yalimwayo Jimboni mwetu ni: Mihogo, Mahindi, Viazi Vitamu, Mtama,  Mpunga, Maharage na Kunde.
MBOGAMBOGA (k.m., mchicha, kabechi, nyanya, vitunguu) na MATUNDA (matikiti, maembe na machungwa) navyo vinalimwa Vijijini mwetu.
KIKUNDI cha KILIMO kiitwacho TUMEJITAMBUA cha Kijijini Bwenda, Kata ya Rusoli kinajishughulisha na UBORESHAJI wa KILIMO cha MIHOGO.
KIKUNDI hiki kilianzishwa Mwaka 2018 na kina WANACHAMA 31.
Mbali ya kilimo cha MIHOGO, KIKUNDI hiki nacho kiko kwenye Kilimo cha Mahindi, Maharage, Viazi Lishe, Uoteshaji wa Miti, na WANACHAMA wake wanakopeshana fedha.
UBORESHAJI WA KILIMO CHA MIHOGO
KIKUNDI cha TUMEJITAMBUA kimeanzisha SHAMBA DARASA la   kilimo cha MIHOGO ambalo limekuwa kivutio kikubwa kwa wakulima wa eneo hilo na Vijiji vingine.
LENGO KUU la KIKUNDI hiki cha KILIMO ni:
*Kufanya biashara ya mazao ya chakula, ikiwemo biashara ya  VIJITI vya MIHOGO
*Kuanzisha KIWANDA kitakachozalisha bidhaa zitokanzo na ZAO LA la MIHOGO kama vile, unga, wanga na biskuti.
KATIBU wa KIKUNDI hicho, Ndugu Festo Obed ameeleza jinsi KIKUNDI hicho kilivyopata mafunzo ya uzalishaji wa MBEGU za MIHOGO kutoka Shirika la MEDA (Mennonite Economic Development Associate)
KIKUNDI hicho kimelima aina mbili za Mbegu za Mihogo, yaani wamepanda Vijiti 4,000 vya Mbegu ya TARICAS 4 (Tz 130) na wanategemea kuvuna Vijiti 48,000 ya aina hii ya Mbegu.
Vilevile, kwa Mbegu ya pili ya MKURANGA 1, wamepanda Vijiti 7,000 na wanategemea kuvuna Vijiti 42,000.
MBEGU zote hizi zinachukua muda wa MIEZI 9 kupata mavuno mazuri ya  MIHOGO.
Baada ya Mbegu mbili hizo kutoa MAFANIKIO mazuri,
Mtaalam wa MEDA, Ndugu Isaack Musa ameshawishi KIKUNDI hicho kuchukua MBEGU nyingine ambazo nazo zinastahimili magonjwa ya mimea na mabadiliko ya tabianchi.
MBEGU nyingine za MIHOGO zilizotolewa na MEDA ni aina ya Mkuranga, Mkumba, Kizimbani, Taricas 2 (F10) na Kiroba.
MIKOPO NA MISAADA ILIYOTOLEWA KWA KIKUNDI CHA KILIMO CHA TUMEJITAMBUA
MAFANIKIO ya Kikundi cha KILIMO cha TUMEJITAMBUA
yanatolewa shukrani nyingi kwa wafuatao:
*MEDA kwa kuwapatia MBEGU mbalimbali za MIHOGO.
*JAMII IMPACT kwa kuwapatia Mkopo wa SHILINGI MILIONI 5 (awamu ya kwanza) na SHILINGI MILIONI 10 (awamu ya pili), na  hivi karibuni watapokea mkopo mwingine.
*PCI Tanzania kwa kuwapatia Mbegu za Mahindi, Maharage, Alizeti na magunia ya kuhifadhia chakula
*SHIMAKIUMU kwa kuwapatia Mbegu za Mahindi, Dawa za Mimea na Viroba vya kupandia miche
*MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo kwa kuwapatia Mbegu za Mihogo, Mtama na Alizeti
MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo alishagawa bure Mbegu (Vijiti) aina ya Mkombozi kwa Wakulima wa Jimboni mwetu kama ifuatavyo:
*MSIMU wa Kilimo wa Mwaka 2016/2017:
Magunia 446
*MSIMU wa Kilimo wa Mwaka 2017/2018:
Magunia 350
KARIBUNI KIJIJINI BWENDA (Kata ya Rusoli) MNUNUE VIJITI VYA MBEGU ZA MIHOGO
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

WANAKIJIJI  WASHIRIKIANA NA SERIKALI KUJENGA VYUMBA VIPYA VYA MADARASA

WANAKIJIJI wakiwa kwenye ujenzi wa Vyumba vipya 2 vya Madarasa na Ofisi 1 ya Walimu wa S/M Nyamwiru ya Kijijini Maneke, Kata ya Busambara.

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
SHULE ya MSINGI NYAMWIRU yenye WANAFUNZI 886 inaupungufu mkubwa wa MIUNDOMBINU ya ELIMU.
SHULE hii iko Kijijini Maneke, Kata ya Busambara. Kijiji hiki kina Shule za Msingi mbili (S/M Maneke & S/M Nyamwiru).
MWALIMU MKUU, Mwl Masilingi Maira ameleza yafuatayo kuhusu S/M Nyamwiru iliyoanzishwa Mwaka 1997:
*Mahitaji ya Vyumba vya Madarasa ni 17, vilivyopo ni vyumba 10.
*Darasa la Awali ndilo lenye Wanafunzi wengi ndani ya chumba kimoja cha Darasa –  wako 185
*Mahitaji ya Vyoo vya Wanafunzi ni Matundu 24, yaliyopo ni 12
*Matundu 4 yanahitajika kwa Vyoo vya Walimu, hakuna tundu hata moja.
*Mahitaji ya Walimu ni 17, waliopo ni 8
*Mahitaji ya Nyumba za Walimu ni 17, ipo nyumba moja tu.
SERIKALI YATOA SHILINGI MILIONI 40
SERIKALI kupitia Mradi wake wa EP4R imetoa Tsh Milioni 40 kwa ajili ya ujenzi wa:
*Vyumba vipya Viwili (2) vya Madarasa
*Ofisi moja (1) ya Walimu
MWENYEKITI wa Serikali ya Kijiji cha Maneke, Ndugu Rupago Loya, kwa niaba ya WANAKIJIJI wa MANEKE, ameishukuru sana SERIKALI kwa kutoa MCHANGO huo na amesema kwamba WANAKIJIJI watachangia NGUVUKAZI zao (kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji ya ujenzi) kukamilisha ujenzi huo.
MICHANGO MINGINE ILIYOTOLEWA KWENYE S/M NYAMWIRU
*KIKUNDI cha BUSARA
Kinachangia chakula cha Wanafunzi
*MBUNGE wa JIMBO
Prof Sospeter Muhongo amechangia:
(i) Madawati 115
(ii) Vitabu zaidi ya 1,000 vya Maktaba
MATOKEO YA MITIHANI YA TAIFA YA S/M NYAMWIRU
DARASA la IV (2020)
*Watahiniwa: 127
*Waliofaulu: 127
DARASA la VII (2020)
*Watahiniwa: 101
*Waliofaulu: 67
OMBI KUTOKA KIJIJINI MANEKE
*WAZALIWA wa Kijiji cha Maneke wanaombwa sana WAJITOKEZE kuchangia MAENDELEO ya nyumbani kwao, ikiwemo ujenzi wa Miundombinu ya ELIMU ya S/M Nyamwiru.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

A VERY SPECIAL BIRTHDAY (25 June 2021)

Today is my birthday… what a special birthday!
*The Uhuru Toch is in my District. I am among the Musoma District leaders who have just received it and will take it around.
*My staff (Office of the Member of Parliament of the Musoma Rural Constituency) surprised me with a birthday cake!
Let me share with you some documented episodes of today (25 June).
Sospeter Muhongo
25.6.2021

TARURA YAENDELEA KUFANYA KAZI NZURI MUSOMA VIJIJINI

ULIMAJI na UKARABATI wa baadhi ya BARABARA za Jimbo la Musoma Vijijini unaofanywa na TARURA (W).

MENEJA TARURA (W), Injinia Abbas Hussein amesema kwamba UKARABATI wa barabara zenye urefu wa jumla ya KILOMITA 30 umepagwa ukamilike tarehe 30.6.2021
KIONGOZI huyo amezitaja barabara hizo kuwa ni zile zinazopita kwenye VIJIJI na VITONGOJI vya:
*Bukima – Bulinga – Bwasi
*Nyegugu – Rusoli – Makojo
*Busungu – Bulinga – Bujaga
*Butata – Kastam
*Kastam – Kumsoma
GHARAMA za MRADI huu ni Tsh MILIONI 90.5 (Tsh 90.5M)
BAJETI YA MWAKA 2021/2022
Barabara nyingi za Vijijini mwetu, zikiwemo za:
*MASINONO-KINYANG’ERERE
*MKIRIRA-KWANGWA HOSPITAL
zitalimwa na kukarabatiwa kwa kutumia FEDHA zilizoongezwa kwenye BAJETI ya awali ya TARURA ya Mwaka 2021/2022.
WANAVIJIJI wa Jimbo la Musoma Vijijini wanatoa SHUKRANI NYINGI mno kwa SERIKALI yetu kwa kuhakikisha kwamba BARABARA zetu zote za VIJIJINI zinapitika Mwaka mzima.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

KASI YAONGEZEKA KWENYE UTEKELEZAJI WA MIRADI YA USAMBAZAJI WA MAJI YA BOMBA KUTOKA ZIWA VIKTORIA

hatua mbalimbali zilizofikiwa kwenye  utekelezaji wa MRADI wa MAJI ya BOMBA kutoka Ziwa Viktoria ya VIJIJI vya Makojo na Chitare.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
JIMBO la MUSOMA VIJIJINI lina KATA 21 zenye VIJIJI 68 na VITONGOJI 374
VIJIJI vyote 68 vina MIRADI ya MAJI ya BOMBA ya kutoka Ziwa Viktoria inayoendelea kutekelezwa kwa Mwaka huu wa Fedha (2020/2021) na Mwaka ujao (2021/2022).
FEDHA ZILIZOTUFIKIA HIVI KARIBUNI KUKAMILISHA BAADHI YA MIRADI
(1) Ukamilishaji wa Mradi wa Maji wa Suguti/Kusenyi
Tsh 84,000,000.
(2) Upanuzi wa Mradi wa Maji kutoka Suguti kwenda  Kwikonero, Rwanga na Kasoma
Tsh 80,000,000
(3) Mradi wa Maji wa Butata/Kastamu
Tsh 286,184,476
Jumla zimeletwa
Tsh 450,184,476
MRADI WA MAJI WA VIJIJI VYA CHITARE NA MAKOJO (Wanavijiji 10,178)
Mradi huu, kama ilivyo mingine unatekelezwa kwa kutumia Fedha za Mfuko wa Maji (National Water Fund, NWF)
MENEJA wa RUWASA (W), Injinia Edward Sironga  amesema kwamba jumla ya gharama za Mradi huu ni Tsh 1,071,154,700.00/= (Tsh bilioni 1.07), na kwamba ulianza kutekelezwa Mwaka 2014. MKANDARASI ni Interelty Builders Ltd.
KIONGOZI huyo wa RUWASA ameelezea kuwa MRADI huo UMETEKELEZWA kwa ASILIMIA 90 (90%), na utakamilishwa kabla ya tarehe 30 Juni 2021.
KAZI ZILIZOKAMILIKA ni:
*Ujenzi wa Mitambo ya kusukuma Maji kutoka kwenye chanzo, na kuweka Mtandao wa Mabomba yenye urefu wa km 18.
*Ufungaji wa Mfumo wa Umeme
*Ujenzi wa Vitekea Maji (DP) 18
*Ujenzi wa Vioski 4
*Ujenzi wa Manteki 2 ya Maji
   (i) Tank 1: Lita 100,000
   (ii) Tank 2 Lita 75,000
DIWANI wa Viti Maalum wa Kata ya Makojo, Mhe Tabu Machumu amesema kukamilika kwa MRADI huu  kutaondoa matatizo ya upatikanaji wa MAJI kwenye VIJIJI vya Chitare na Makojo.
DIWANI huyo, kwa niaba ya WANAVIJIJI  watakaonufaika na MAJI hayo ya BOMBA, ametoa SHUKRANI nyingi kwa SERIKALI kwa uamuzi wake wakutoa fedha za ujenzi na ukamilishaji wake.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

WANAKIJIJI WAPATA MICHANGO YA SERIKALI KWENYE UJENZI NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU

ujenzi wa Vyumba vipya vya Madarasa na Ofisi ya Walimu unaotekelezwa na WANAKIJIJI kwenye Shule yao ya Msingi, S/M KOME B, iliyoko Kijijini Kome, Kata ya Bwasi. 

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
SHULE ya MSINGI KOME B ilifunguliwa Mwaka 2015, Kijijini Kome, Kata ya Bwasi.
KATA ya BWASI ina Vijiji 3 (Bugunda, Bwasi na Kome) na kila Kijiji kina Shule za Msingi mbili (yaani shule moja kila kijiji yenye A&B).
MWALIMU MKUU wa S/M BWASI B,  Mwl Yoel Peter ametoa maelezo ya Shule hiyo kama ifuatavyo:
*Jumla ya Wanafunzi ni 565
*Mahitaji ya Vyumba vya Madarasa ni 10, vilivyopo ni 6
*Mirundikano ya Wanafunzi madarasani ni mikubwa, kwa mfano Darasa la III lenye Wanafunzi 160 wana chumba kimoja cha darasa.
*Wapo Wanafunzi wenye madarasa chini ya MITI.
MICHANGO YA UJENZI NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU KWENYE S/M KOME B
MTENDAJI wa KIJIJI (VEO) cha Kome, Ndugu Fredrick Jeremia amesema WANAKIJIJI WAMEAMUA kuanza ujenzi wa Vyumba vipya vya Madarasa na Ofisi ya Walimu kwenye Shule yao (S/M Kome B).
WANAKIJIJI wanachangia:
*NGUVUKAZI zao kwa kuchimba misingi ya majengo, na kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji ya ujenzi.
*FEDHA taslimu Tsh 2,300/= kutoka kila kaya.
*SERIKALI, kupitia Mradi wake wa PEDP (Primary Education Development Programme) imetoa Tsh MILIONI 12.5 kwa ajili ya kukamilisha Chumba 1 cha Darasa na kununua madawati na meza.
MICHANGO MINGINE ILIYOKWISHA KUTOLEWA SHULENI HAPO
*SERIKALI kupitia Mradi wake wa  EP4R ilitoa Tsh MILIONI 5
*PCI Tanzania imejenga Choo chenye Matundu 10
*MBUNGE wa JIMBO, Profesa Sospeter Muhongo ameishachangia:
 (i) Madawati 62
 (ii) Saruji Mifuko 120
(iii) Vitabu zaidi ya 1,000 vya Maktaba
*MFUKO wa JIMBO ulinunua Mabati 126
UFAULU WA MITIHANI KWENYE S/M KOME B
*Darasa la IV  (2020)
Watahiniwa 36
Waliofaulu  36
*Darasa la VII (2020)
Watahiniwa 33
 Waliofaulu  30
WAZALIWA wa Kijiji cha Kome na Kata ya Bwasi WANAOMBWA wachangie MAENDELEO ya nyumbani kwao – OMBI kutoka kwa ndugu zao.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

WANAKIJIJI WAANZA KUTEKELEZA MRADI WA UJENZI WA VYUMBA VIPYA 17 VYA MADARASA YA SHULE YAO YA MSINGI

Viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Nyambono na Mwalimu Mkuu wa S/M Nyetasyo wakishiriki kwenye Mradi wa ujenzi wa VYUMBA VIPYA 17 vya Shule hiyo iliyoko Kijijini Nyambono, Kata ya Nyambono.

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
UONGOZI wa Serikali ya Kijiji cha Nyambono kwa kushirikiana na Wananchi wa Kijiji hicho wameanza kutekeleza MRADI wa ujenzi wa VYUMBA VIPYA 17  vya Madarasa kwenye Shule yao ya Msingi, S/M NYETASYO.
Shule ya Msingi Nyetasyo ni moja kati ya Shule mbili za Msingi zilizopo Kijijini Nyambono.
Shule hii ilianzishwa Mwaka 1944 ikiwa inamilikiwa na Kanisa la Mennonite. Mwaka 1978, Shule ilitaifishwa na Serikali.
MWALIMU MKUU wa S/M Nyetasyo, Mwl Rutoryo Hitra ameelezea MAHITAJI ya Shule hiyo kama ifuatavyo:
*Jumla ya Wanafunzi ni 873
*Vyumba vya Madarasa vinavyohitajika ni 23, vilivyopo ni 6
*Madarasa yanayosomea nje ni mawili (Darasa la Awali na Darasa la II).
MIRUNDIKANO ya Wanafunzi madarasani ni mikubwa:
*Darasa la III lina chumba kimoja chenye Wanafunzi 121
*WALIMU wanaohitajika ni 23, waliopo ni 9
*NYUMBA za Walimu zinahitajika 23, zilizopo ni 4
*VYOO vya Wanafunzi –  yanahitajika Matundu 39, yaliyopo ni 10
*CHOO cha Walimu  –   yanahitajika Matundu 2, hakuna hata tundu moja.
UFAULU wa MITIHANI kwenye S/M NYETASYO:
*DARASA la IV (2020)
Watahiniwa: 113
Waliofaulu: 110
*DARASA la VII (2020)
*Watahiniwa: 62 *Waliofaulu: 45
WANAKIJIJI WAFANYA MAAMUZI YA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU KWENYE SHULE YAO
AFISA MTENDAJI (VEO) wa Kijiji cha Nyambono, Ndugu Mugeta Kaitira amesema SERIKALI ya KIJIJI chao imekubaliana na WANAKIJIJI  kuanza kutekeleza MRADI wa ujenzi wa Vyumba vipya 17 vya Madarasa ya Shule yao, na kwamba WANAKIJIJI watachangia:
*FEDHA taslimu, Tsh 11,500/= kutoka kila kaya
*NGUVUKAZI ya kusomba mchanga, mawe, kokoto na maji ya ujenzi.
MICHANGO ILIYOKWISHATOLEA
*MBUNGE wa JIMBO, Prof Sospeter Muhongo ameishatoa michango yake kama ifuatavyo:
(i) Madawati 60
(ii) Vitabu zaidi ya 1,000 vya Maktaba
*MFUKO wa JIMBO
(i) Tsh Milioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba vipya vitatu (3) vya Madarasa.
OMBI KUTOKA KIJIJI CHA NYAMBONO
Wananchi wa Kijiji cha Nyambono wanawaomba WAZALIWA wa Kijiji hicho, na  WADAU mbalimbali wa MAENDELEO wawaunge kwenye MIRADI ya ujenzi na uboreshaji wa MIUNDOMBINU ya ELIMU kwenye S/M NYETASYO
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma  Vijijini

WANAKIJIJI WASHIRIKIANA NA SERIKALI KUONGEZA VYUMBA VYA MADARASA KWENYE S/M BULINGA

MATUNDA ya USHIRIKIANO wa WANAKIJIJI na SERIKALI kwenye ujenzi na ukamilishaji wa Vyumba vipya 3 vya Madarasa na Choo chenye Matundu 6 kwenye S/M BULINGA B ya Kijijini Bugunda, Kata ya Bwasi.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
SHULE ya MSINGI BULINGA B ilifunguliwa Mwaka 2014. Shule hii ipo Kijiji cha Bugunda, Kata ya Bwasi.
MWALIMU MKUU wa Shule hii, Mwalimu Marwa James ameelezea yafuatayo kuhusu Vyumba vya Madarasa vya Shule hiyo:
*Idadi ya Wanafunzi ni 672
*Vyumba vya Madarasa vinavyohitajika ni 15, vilivyopo ni 6.
*Mirundikano ya Wanafunzi madarasani ni mikubwa. Kwa mfano, Darasa la IV lina Wanafunzi 145 kwenye chumba kimoja cha darasa.
MCHANGO WA SERIKALI WA KUTATUA TATIZO LA UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MADARASA
Serikali kupitia Mradi wake wa EP4R imetoa Tsh MILION 65.5 kwa ajili ya ujenzi wa:
*Vyumba vipya 3 vya Madarasa
*Choo chenye Matundu 6
*Ununuzi wa Madawati 69
*Ununuzi wa Matenki 3 ya Maji
MTENDAJI KATA wa Kata ya Bwasi,  Ndugu Mashaka Kagere amesema WANAKIJIJI wameshiriki vizuri sana kwenye MRADI huu kwa kufanya yafuatayo:
*kuchimba msingi wa Vyumba vipya 3 vya Madarasa
*kuchimba shimo la choo
*kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji ya ujenzi
VIONGOZI na WANAKIJIJI wa Kijiji cha Bugunda wanaishukuru sana SERIKALI kwa mchango wake ambao utapunguza tatizo la uhaba wa Vyumba vya Madarasa kwenye Shule ya Kijijini mwao.
MICHANGO MINGINE ILIYOTOLEWA KWENYE S/M BULINGA B
*PCI Tanzania imechangia:
(i) Ujenzi wa Matundu 6 ya choo
(ii) Huduma ya chakula shuleni hapo
*MBUNGE wa Jimbo,  Profesa Sospeter Muhongo ameishachangia:
(i) Saruji Mifuko 60
(ii) Madawati 70
(iii) Vitabu vingi vya Maktaba
OMBI KUTOKA KIJIJI CHA BUGUNDA
WAZALIWA wa Kijiji cha Bugunda na Kata ya Bwasi kwa ujumla wake, WANAOMBWA  wachangie MAENDELEO na nyumbani kwao.
UFAULU WA MITIHANI KWENYE S/M BULINGA B
*MATOKEO ya Darasa IV (2020)
Watahiniwa 82
Waliofaulu 70
MATOKEO ya Darasa la VII (2020)
Watahiniwa 55
Waliofaulu   27
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

WANAKIJIJI WANAENDELEA KUTATUA TATIZO LA UPUNGUFU WA MIUNDOMBINU YA ELIMU KWENYE SHULE YAO

Ukamilishaji wa Vyumba vipya vya Madarasa na Ofisi ya Walimu kwenye S/M Etaro ya Kijiji cha Etaro, Kata ya Etaro

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge

SHULE ya MSINGI ETARO ilifunguliwa Mwaka 1995. Shule hii iko Kijijini Etaro, Kata ya Etaro.

MWALIMU MKUU wa Shule hii, Mwl Mangire Mahombwe ameeleza yafuatayo:

*Shule ina jumla ya Wanafunzi 1,079 na ina Walimu 14.

*Shule ina Vyumba vya Madarasa 9, vinavyohitajika ni 23.

*Mirundikano madarasani ni mikubwa mno. Kwa mfano, Darasa la Saba (VII), Wanafunzi wote 154 wanasomea kwenye chumba kimoja (1) cha darasa.

*Shule ina matundu 30 ya choo, yanayohitajika ni 48.

UONGEZAJI WA VYUMBA VIPYA VYA MADARASA NA OFISI YA WALIMU

UJENZI wa Vyumba vipya vitano (5) vya Madarasa na Ofisi moja (1) ya Walimu wa Shule hii ulianza Mwaka 2017.

MICHANGO YA UJENZI WA VYUMBA VIPYA 5 VYA MADARASA & OFISI 1 YA WALIMU

MTENDAJI wa KIJIJI cha Etaro (VEO), Ndugu Sophia Anthony ameelezea uchangiaji wa ujenzi unaondelea kwenye S/M ETARO ni kama ifuatavyo:

*NGUVUKAZI za Wanakijiji cha Etaro: wanasomba mawe, kokoto, mchanga na maji

*FEDHA taslimu, Tsh 10,000/= (elfu kumi) zinachangwa kutoka kila KAYA. Kijiji kina KAYA 556.

*PCI Tanzania imejenga matundu 10 ya choo – Ahsante sana PCI Tanzania!

*MNARA wa SIMU, HALOTEL umechangia
(i) Saruji Mifuko 60
(ii) Mabati 54
(Ahsante sana HALOTEL)

*MBUNGE wa JIMBO, Prof Sospeter Muhongo, amechangia:
(i) Saruji Mifuko 60
(ii) Mabati 54
(iii) Madawati 227
(iv) Vitabu vya Maktaba zaidi ya 1, 000 (elfu moja)

*MFUKO wa JIMBO umechangia:
(i) Mabati 244

*MKUU wa MKOA, Marehemu Mhe Tupa: Mwaka 2012, alitoa Tsh. MILIONI 10 kwa ajili ya Mradi wa Maji Kata ya Etaro.

Kata hiyo ilipopata Mradi mwingine wa Maji, fedha hizo zimetumika kwenye ujenzi huu.

UFAULU WA S/M ETARO

Mbali ya upungufu mkubwa wa MIUNDOMBINU ya ELIMU kwenye Shule hii, UFAULU wake ni wa kuridhisha:

MATOKEO YA DARASA LA IV (2020):

* Watahiniwa 96
* Waliofaulu 93

MATOKEO YA DARASA LA VII (2020):

* Watahiniwa 90
* Waliofaulu 72

OMBI KUTOKA KWA WANAKIJIJI CHA ETARO

WAZALIWA wa Kijiji cha Etaro na Kata ya Etaro kwa ujumla, na WADAU wengine wa MAENDELEO, wanaombwa KUCHANGIA ujenzi na uboreshaji wa MIUNDOMBINU ya ELIMU kwenye Shule yao (S/M Etaro).

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Attachments area

KATA YA KIRIBA YAANZA UJENZI WA SEKONDARI YA PILI

Picha zilizoko hapa zinaonesha baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Bwai Kumsoma wakiwa kwenye ujenzi wa Sekondari yao mpya, BWAI SEKONDARI, inayotarajiwa kufunguliwa mwakani (Januari 2022). Hii itakuwa SEKONDARI ya PILI ya Kata ya Kiriba.

Tarehe 21.5.2021
Jimbo la Musoma Vijijini
Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
UMBALI MREFU wa kutembea na MIRUNDIKANO ya Wanafunzi madarasani ni sababu kuu zinazofanya baadhi ya KATA za Jimbo la Musoma Vijijini KUAMUA kuwa SEKONDARI zaidi ya moja.
KATA ya KIRIBA inayoundwa na Vijiji vitatu (3) ambavyo ni Bwai Kwitururu, Bwai Kumsoma, na Kiriba ina Sekondari moja ya Kata (KIRIBA SEKONDARI) iliyojengwa Kijijini Bwai Kwitururu.
SEKONDARI hii ilifunguliwa Mwaka 2006, na ina jumla ya WANAFUNZI 731 (Kidato cha 1-4).
WANAFUNZI wa Vijiji vya Bwai Kumsoma na Kiriba wanalazimika kutembea umbali wa kati ya KILOMITA 5 hadi 12 kwenda masomoni KIRIBA SEKONDARI.
Vilevile, kuna MIRUNDIKANO mikubwa ya Wanafunzi madarasani. Kwa mfano, Wanafunzi wa KIDATO cha KWANZA wako sitini (60) ndani ya chumba kimoja cha darasa
WANANCHI WAAMUA KUJENGA SEKONDARI YA PILI YA KATA
KIJIJI cha  Bwai Kumsoma chenye WAKAZI 10,500 KIMEAMUA kujenga SEKONDARI yake ili KUTATUA MATATIZO yaliyotajwa hapo juu.
SEKONDARI inayojegwa na KIJIJI kimoja hiki, chenye VITONGOJI NANE (8), itaitwa BWAI SEKONDARI na inajengwa ndani ya KITONGOJI cha BUSIKWA
WANAFUNZI wa kujiunga na SEKONDARI inayojengwa wapo wa kutosha kwani Kijiji cha Bwai Kumsoma kina SHULE za MSINGI TATU (3), na Wanafunzi wa Vijiji vingine viwili vya Kata hii watakaribishwa kujiunga na BWAI SEKONDARI inayotarajiwa kufunguliwa mwakani (Januari 2022).
MAOTEO ya WANAFUNZI watakaojiunga na  Kidato cha Kwanza mwakani (Januari 2022) kwenye Sekondari hii mpya ni kati ya 150 na 170.
MABOMA YANAYOJENGWA KWENYE SEKONDARI MPYA
Mwenyekiti wa Serikali ya  Kijiji cha Bwai Kumsoma, Ndugu PIMA MASINDE KITUNDU  ameeleza kwamba
ujenzi wa Shule hii ulianza rasmi mwezi uliopita (Aprili 2021), na unatekelezwa kwa mpangilio ufuatayo:
*Boma la Vyumba 3 vya Madarasa
*Vyoo vya Wanafunzi na Walimu
*Boma la Jengo la Utawala
*Maabara 3 (Fizikia, Kemia na Bailojia)
*Boma la Nyumba ya Mkuu wa Shule
MTENDAJI KATA, Ndugu  Pendo Isaach Mwita, na MRATIBU ELIMU KATA, Mwl Beatrice Ndosi, wanafuatilia kwa karibu sana ujenzi wa Sekondari hii mpya  – TUNAWASHUKURU SANA!
WACHANGIAJI WA MRADI HUU WA UJENZI.
MICHANGO itatolewa kwa awamu mbalimbali na kwa kuanzia:
*NGUVUKAZI za Wanakijiji zitatumika kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji.
*FEDHA taslimu, Tsh 10,000/= kwa kila mkazi mwenye umri kati ya miaka 18 na 59
*DIWANI wa Viti Maalum, Ndugu FLORA MAGWA ameanza kuchangia kwa kutoa SARUJI MIFUKO 5 (mitano)
*MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ameanza kuchangia kwa kutoa SARUJI MIFUKO 50 (hamsini)
ELIMU NI KIPAUMBELE CHA KWANZA MUSOMA VIJIJINI (KATA 21)
*Tunazo Sekondari 21 za Kata
*Tunazo Sekondari 2 za Binafsi
*Tunajenga Sekondari Mpya 8
WANAKIJIJI WANAOMBA TUSHIRIKIANE NAO KUJENGA SEKONDARI MPYA
MWENYEKITI Ndugu Pima Masinde Kitundu kwa niaba ya Wananchi na Serikali ya Kijiji cha Bwai Kumsoma anaomba WADAU wa MAENDELEO wakiwemo WAZALIWA wa KATA ya KIRIBA wajitokeze kuchangia MRADI huu wa ujenzi wa SEKONDARI ya pili ya Kata yao.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

WANAVIJIJI WAENDELEA NA UJENZI WA ZAHANATI MPYA VIJIJINI MWAO

baadhi ya WANANCHI wa Kijiji cha NYABAENGERE, Kata ya MUSANJA, wakishirikiana na MAFUNDI wao kujenga msingi (foundation) wa ZAHANATI ya Kijiji chao.

Tarehe 17.5.2021
Jimbo la Musoma Vijijini
Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
HUDUMA za AFYA ndani ya Halmashauri ya  Wilaya ya Musoma (Musoma DC) yenye Jimbo moja la Uchaguzi (Jimbo la Musoma Vijijini) ni hizi zifuatazo:
*Hospitali ya Wilaya ya Serikali: ujenzi unakamilishwa
*Vituo vya Afya 3 vya Serikali vinatoa huduma za Afya. Vituo hivi ni: Murangi, Mugango na Bugwema (Bugwema – ujenzi ni wa upanuzi wa Zahanati ya  Masinono kuwa Kituo cha Afya, ujenzi unakamilishwa)
*Zahanati 23 za Serikali zinatoa huduma za Afya
*Zahati 4 za Binafsi zinatoa huduma za Afya.
*Zahanati Mpya 15 zinajengwa na Wanavijiji. Serikali imeanza kuchangia baadhi ya ujenzi wa Zahanati hizo.
JIMBO la Musoma Vijijini lina KATA 21 zenye VIJIJI 68 na VITONGOJI 374.
KIJIJI CHA NYABAENGERE CHAAMUA KUJENGA ZAHANATI YAKE
Wananchi wa Kijiji cha Nyabaengere kilichopo Kata ya Musanja wameanza ujenzi wa ZAHANATI yao wakiwa na LENGO KUU la kutatua tatizo lao la  kutembea umbali mrefu wa zaidi ya KILOMITA 10 kwenda kutafuta HUDUMA za AFYA zilizoko Kata ya jirani ya Murangi – Kituo cha Afya Murangi.
DIWANI wa Kata ya Musanja, Mhe Ernest Mwira amesema ZAHANATI inayojengwa Kijijini hapo itakuwa na jumla ya VYUMBA 14.
HUDUMA za AFYA zitakazotolewa ni pamoja na:
*Kliniki ya Wajawazito na Huduma za Uzazi wa Mpango
*Huduma za Mama & Mtoto
*Matibabu mbalimbali na huduma nyingine za Afya
Diwani huyo amesema LENGO lao ni kukamilisha ujenzi wa ZAHANATI ya KIJIJI cha NYABAENGERE ndani ya MWAKA MMOJA.
MAMA Sophia Otieno, Mkazi Kijiji cha Nyabaengere amesema kukamilika kwa Zahanati hiyo kutaondoa adha wanayoipata AKINA MAMA kujifungulia nyumbani na njiani, na wengine kupoteza maisha wakienda kujifungulia mbali kwenye Kituo cha Afya cha Murangi.
MICHANGO YA UJENZI
MTENDAJI wa Kata ya Musanja, Ndugu Michael Tafuna amesema ujenzi wa Zahanati hiyo utafanikishwa kwa MICHANGO ifuatayo:
*NGUVUKAZI za Wanakijiji za kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji ya ujenzi.
*Tsh 24,000 kutoka kwa kila Mwanakijiji mwenye nguvu za kufanya kazi
*MAPATO ya Kijiji yanatokana na uuzaji wa rasilimali zao ambazo ni mchanga, mawe na kifusi.
*MAPATO kutoka kwenye ushuru wa mifugo.
*MICHANGO ya DIWANI, Mhe Ernest Mwira  – atachangia SARUJI MIFUKO 20. Ameanza kwa kuchangia Saruji Mifuko 5.
*MICHANGO ya Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo.
Mbunge huyu atatumia mtindo wake wa kuchangia hatua zote za ujenzi kama afanyavyo kwingine Jimboni mwao, na kwa Zahanati hii ameanza kwa kuchangia ujenzi wa msingi kwa kutoa SARUJI MIFUKO 50.
OMBI KUTOKA KIJIJI CHA NYABAENGERE
Diwani na Wananchi wa Kijiji cha Nyabaengere wanawaomba WAZALIWA wa KIJIJI hicho na KATA ya MUSANJA kwa ujumla waungane na ndugu zao kuchangia ujenzi wa ZAHANATI hii. WADAU wengine wa MAENDELEO nao wanakaribishwa kutoa MICHANGO yao.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

SHEREHE ZA EID AL FITR NA MIRADI YA MAENDELEO YA MUSOMA VIJIJINI

EID AL FITR ya Musoma Vijijini iliyofanyika kwenye MISIKITI 3 ya VIJIJI vya Bukima, Kiriba na Kakisheri/Kigera.

Tarehe, 15.5.2021
Jimbo la Musoma Vijijini
EID AL FITR ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini husherehekewa KILA MWAKA kwa MISIKITI 3 kuandaa sikukuu hiyo. Jumla ya Misikiti Jimboni mwetu ni 37.
Kwa MWAKA HUU (2021) mzunguko wa MISIKITI 3 wa kila Mwaka umetua kwenye MISIKITI ya VIJIJI vya:
*Bukima
*Kiriba
*Kakisheri/Kigera
MADHEHEBU YA KIKIRISTO nayo husherehekea KRISMASI na PASAKA kwa mtindo huu huu wa mzunguko ndani ya VIJIJI 68 vya JIMBO la Musoma Vijijini.
UTARATIBU huu wa kuwaweka WANANCHI pamoja wakati wa SHEREHE za KIDINI na wakati wa KAZI za kujiletea MAENDELEO yao ni sehemu ya MPANGOKAZI wa MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo.
MASHINDANO YA KUHIFADHI QURAAN
*WAISLAMU wa Jimbo la Musoma Vijijini wameamua kutayarisha MASHINDANO hayo kwa kushirikiana na Mbunge wao wa Jimbo. Tarehe itapangwa.
SHEREHE za KIDINI, mbali ya kufanyika kwa TAFRIJA za pamoja, hutumika KUKUMBUSHANA UTEKELEZAJI ya MIRADI ya MAENDELEO ya KATA iliyoandaa SHEREHE kwa Mwaka huo.
(1) EID AL FITR KWENYE MSIKITI WA KIJIJI CHA BUKIMA
WANANCHI wamekumbushwa na kuhimizwa kukamilisha MIRADI ifuatayo:
(a) Wodi ya Mama&Mtoto ya Zahanati ya Bukima
(b) Ujenzi wa Vyumba vipya vya Madarasa kwenye Shule zote za Msingi na Sekondari yao.
(c) Kasi iongezwe kwenye ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Butata
(2) EID AL FITR KWENYE MSIKITI WA KIJIJI CHA KIRIBA
WANANCHI wamekumbushwa na kuhimizwa kukamilisha MIRADI ifuatayo:
(a) Ujenzi wa Vyumba vipya vya Madarasa na Ofisi za Walimu wa S/M Kiriba B. Shule hii inahama kutoka kwenye eneo la pamoja na S/M Kiriba A
(b) Kasi ya ukamilishaji wa Maabara, Vyumba vipya vya Madarasa na Jengo la Utawala la Kiriba Sekondari iongezeke.
(c) Kitongoji cha Kubuingi cha Kijiji cha Kiriba kianze ujenzi wa SHULE SHIKIZI. Watoto wao wanatembea umbali mrefu kwenda masomoni kwenye S/M Kiriba A&B
(3) EID AL FITR KWENYE MSIKITI WA VIJIJI VYA KAKISHERI NA KIGERA
*Vijiji 2 hivi vinatumia Msikiti mmoja ambao unaendelea kujengwa kwa msaada mkubwa wa MAMA DIBOGO wa Musoma Mjini.
*Ujenzi wa Jengo la Madrasa utaanza hivi karibuni.
*KASWIDA iliyoambatanishwa hapa imeimbwa na vijana wa Msikiti huu.
WANANCHI wamekumbushwa na kuhimizwa kukamilisha MIRADI ifuatayo:
(a) Kuongeza kasi ya ujenzi na ukamilishaji wa SEKONDARI MPYA, ya kisasa, (imefunguliwa mwaka huu – Kigera Secondary School) inayojengwa na Vijiji hivi viwili.
(b) Kasi iongezwe kwenye ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kakisheri
MIRADI INAYOFADHILIWA NA SERIKALI
Mbali ya kutoa mkono wa EID AL FITR, Mbunge wa Jimbo hilo ameongea na WANANCHI na kuwaelezea MIRADI mbalimbali (k.m. elimu, afya, maji, umeme, barabara za TARURA & TANROADS) itakayotekelezwa na SERIKALI kwa kutumia BAJETI ya  Mwaka wa Fedha ujao, Mwaka 2021/2022.
Vilevile, MBUNGE huyo amesikiliza kero za Wananchi na kuzitatua.
SHEREHE NA MAENDELEO MUSOMA VIJIJINI:
TUENDELEE KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YETU KUCHANGIA MAENDELEO YETU –  TUTAFANIKIWA!
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

WANANCHI NA SERIKALI WASHIRIKIANA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA RUSOLI SEKONDARI

WANAVIJIJI na VIONGOZI wao (akiwemo Diwani wao Mhe Boaz Nyeura) washiriki kwenye ujenzi wa Chumba kimoja cha Darasa cha RUSOLI SEKONDARI

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
RUSOLI SEKONDARI ni Shule ya Kata ya Rusoli iliyofunguliwa Mwaka 2010. Kata hii ina Vijiji 3 ambavyo ni: Buanga,  Kwikerege na Rusoli.
IDADI YA VYUMBA VYA MADARASA
MWALIMU MKUU wa Sekondari hii, Mwalimu Tausi Juma amesema kuwa Shule ina jumla ya WANAFUNZI 444. Mahitaji ya Vyumba vya Madarasa ni 12 vilivyopo ni 10.
Kutokana na Ufaulu wa Wanafunzi wa Kidato cha kwanza  kuongezeka, kuna MIRUNDIKANO mikubwa ya WANAFUNZI madarasani. Kwa mfano, KIDATO cha KWANZA chumba kimoja cha Darasa kina WANAFUNZI 54 badala ya 40!
MAABARA 3 (Fizikia, Kemia & Bailojia)
SEKONDARI hii inazo MAABARA zote tatu ambazo Vyumba vyake vimo ndani ya JENGO moja.
SERIKALI ilitoa Tsh MILIONI 20 kuboresha na kukamilisha Maabara ya Kemia, na hivi karibuni SERIKALI imetoa Tsh MILIONI 30 kuboresha na kukamilisha Maabara ya Fizikia.
UJENZI WA VYUMBA VIPYA VYA DARASA
MTENDAJI KATA ya Rusoli, Ndugu Goodluck Mazige amesema WANANCHI WAMEAMUA kujenga VYUMBA VIPYA 3 VYA MADARASA ili kuondoa MIRUNDIKANO ya WANAFUNZI madarasani.
KIONGOZI huyo, na DIWANI wa Kata hiyo, Mhe Boaz Nyeura wamesema wanaanza na ujenzi wa Chumba kimoja cha Darasa ambacho kitakamilika kabla ya tarehe 30.5.2021
MICHANGO YA WANAVIJIJI
*NGUVUKAZI ya kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji.
*Tsh 5,000 kuchangwa na kila KAYA ndani ya KATA hiyo ya Rusoli.
DIWANI Mhe Boaz Nyeura anaomba WADAU wa MAENDELEO wakiwemo WAZALIWA na Kata hiyo wajitokeze na kuchangia ujenzi wa Vyumba Vipya 3 vya Madarasa ya Sekondari yao.
DIWANI huyo anatoa SHUKRANI nyingi sana kwa wanaochangia UBORESHAJI wa MIUNDOMBINU ya RUSOLI SEKONDARI ambao ni:
*WANAVIJIJI wa Kata yao
*SERIKALI yetu
*WAZALIWA wa Kata hiyo ambao ni: Profesa Mselu, William Makunja, Berias Mkama, Jeff Makongo, Laiton Samamba, Robert Masige, Majura Maingu, Feada Manyiri na Stephan Kaema.
*YEBHE CHIKOMESHE ni Kikundi cha WAZALIWA wa Kijiji cha Rusoli ambacho KINACHANGIA MAENDELEO ya kwao nyumbani yakiwemo ya Rusoli Sekondari. Kikundi hiki kimechimba KISIMA cha MAJI ya Kijijini kwao.
Vilevile, Kikundi hiki kilinunua VIFAA vya MAABARA vya Rusoli Sekondari na hivi karibuni kimenunua Computer na Photocopy ya Sekondari hiyo –  HONGERENI SANA SANA.
MICHANGO YA MBUNGE WA JIMBO
*Saruji Mifuko 70
*Kuchangia kulipa POSHO ya Mwalimu wa Kujitolea wa Masomo ya Sayansi kwa Mwaka mmoja.
*Vitabu vingi vya Maktaba
KARIBUNI TUCHANGIE MAENDELEO YA RUSOLI SEKONDARI
*MATOKEO ya KIDATO cha  II (2020)
Jumla ya Watahiniwa: 107
Div I = 6     Div II= 9
Div III = 26 Div IV= 66
*MATOKEO ya KIDATO cha IV (2020)
Jumla ya Watahiniwa: 64
Div = 1      Div II = 6
Div III = 7  Div IV = 44
Div O = 6
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or. tz

SEKONDARI MPYA ILIYOFUNGULIWA MWAKA HUU (2021) YAANZA UJENZI WA MADARASA MAPYA YATAKAYOHITAJIKA MWAKANI (2022)

ujenzi unaoendelea wa Vyumba vipya vya Madarasa vitakavyohitajika Mwakani (Januari 2022) kwenye SEKONDARI MPYA iliyofunguliwa Mwaka huu (tarehe 22.2.2021).

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
KIGERA SEKONDARI ni Shule mpya iliyoanza ujenzi wake Mwaka 2019 kwa NGUVU za WANANCHI wa Vijiji 2 wakishirikiana na WADAU wa MAENDELEO (Wazaliwa wa Vijiji hivyo viwili) na VIONGOZI wao (Madiwani 2 kwa nyakati tofauti, na Mbunge wa Jimbo)
SEKONDARI hii ni ya Vijiji 2 vya Kakisheri na Kigera vyote vya Kata ya Nyakatende. Hii ni SEKONDARI ya PILI ya Kata hii. Sekondari yake ya KWANZA (Nyakatende Sekondari) iko Kijijini Nyakatende.
MIUNDOMBINU ILIYOKWISHAKAMILISHWA
*Vyumba Vipya 2 vya Madarasa vinavyotumiwa na Kidato cha Kwanza
*Choo chenye Matundu 11
*Jengo la Utawala lenye Ofisi 9
SHULE KUFUNGULIWA
KIGERA Sekondari ilifunguliwa rasmi tarehe 22.2.2021 na tayari WANAFUNZI 122 wa KIDATO cha KWANZA wameanza masomo shuleni hapo.
IDADI YA WALIMU
*SEKONDARI hii mpya ina WALIMU 5 wa kuajiriwa na MWALIMU 1 wa kujitolea.
UJENZI UNAONDELEA
*Nyumba ya Mwalimu (inakamilishwa)
*Maabara 3 (zinakamilishwa)
WACHANGIAJI WA AWAMU YA KWANZA YA UJENZI (2019-2021):
*WANAVIJIJI – Nguvukazi (kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji)
*WANAVIJIJI – Fedha taslimu Shilingi 2,000 kwa kila Mkazi (ndani ya Vijiji hivyo viwili) mwenye umri wa zaidi ya Miaka 18
*WAZALIWA wa Vijiji 2 – kulipa gharama za Mafundi
*MBUNGE wa JIMBO, Prof Sospeter Muhongo
^Saruji Mifuko 150
^Mabati 108
*MBUNGE huyo wa JIMBO amelipia PANGO la miezi 6 (Februari – Julai 2021) ili WALIMU 2 wapate makazi Kijijini Kigera karibu na Sekondari hiyo.
*MFUKO wa JIMBO
^Saruji Mifuko 300
^Mabati 216
*HALMASHAURI
(Musoma DC)
 ^Tsh Milioni 5
MADAWATI NA SAMANI ZA OFISI ZA WALIMU
*WAZAZI wa WANAFUNZI 122 wa Kidato cha kwanza
^Madawati
*DIWANI wa Kata ya Nyakatende, Mhe Marere Kisha
^Samani za Ofisi za Walimu (Viti 8 na Meza 4)
MAJI YA BOMBA
*RUWASA WILAYA inakamilisha ujenzi wa Miundombinu ya MAJI ya BOMBA (kutoka Ziwa Victoria) ya Sekondari hii.
UJENZI WA VYUMBA VIPYA 3 VYA MADARASA YA MWAKANI (2022)
MAOTEO ya WANAFUNZI wa KIDATO cha KWANZA wa Mwakani (2022) ni kupokea WANAFUNZI kati ya 132 na 150 kwenye Sekondari hii.
Kwa hiyo, vinahitajika VYUMBA (vingine) VIPYA 3 vya Madarasa.
UJENZI WA AWAMU YA PILI (kuanzia April 2021 na kuendelea)
WANAVIJIJI wenye Sekondari hii (Vijiji 2 – Kakisheri & Kigera) WAMEANZA ujenzi wa VYUMBA hivyo 3 vitakavyohitajika mwakani (Januari 2022) na BOMA la CHUMBA kipya cha kwanza litakamilika kabla ya tarehe 30.4.2021.
Ujenzi utaendelea na kuhakikisha ifikapo Septemba 2021, MABOMA mengine mawili (2) yatakuwa yamekamilishwa.
WACHANGIAJI WA UJENZI WA AWAMU YA PILI
*WANAVIJIJI wa Vijiji 2 wanaendelea kujitolea (NGUVUKAZI) kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji.
*WANAVIJIJI hao wanachangia fedha taslimu Shilingi 1,000 kwa kila mwenye umri wa zaidi ya miaka 18.
*MZALIWA wa Kijiji cha Kigera, Ndugu Lucas Mashauri – ameanza kuchangia ujenzi huu mpya kwa kutoa Saruji Mifuko 10.
*Ndugu Lucas Mashauri ni MCHANGIAJI MKUU wa Miradi ya Maendeleo ya Kata ya kwao ya Nyakatende – HONGERA SANA NDUGU YETU!
TUNAKARIBISHWA KUCHANGIA UJENZI WA SEKONDARI MPYA YA KIGERA
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kigera, Ndugu Magafu Katura anaendelea KUWAKARABISHA WADAU wa MAENDELEO kuchangia ujenzi huu unaoenda kwa KASI kubwa na UBORA wa juu.
Aidha, MWENYEKITI huyo anatoa shukrani za dhati kwa WANAVIJIJI na WAZALIWA wa Vijiji vya Kakisheri na Kigera, DIWANI na MBUNGE wao kwa MICHANGO yao kwenye Mradi huu wa Maendeleo ya Wananchi wa Kata ya Nyakatende.
SHUKRANI za kipekee wanapewa Mkuu wa Wilaya (DC), Dr Vicent Naano Anney na Mkurugenzi (DED), Ndugu John Kayombo kwa usimamiaji mzuri na makini wa ujenzi wa KIGERA SEKONDARI.
Hii ni KIGERA SEKONDARI inayojengwa na WANANCHI wa Vijiji 2 vya Kakisheri na Kigera vyote vya Kata ya Nyakatende ambayo sasa inazo SEKONDARI MBILI (2) za Kata.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

VIKUNDI VYA KILIMO VYAENDELEA KUNEEMEKA KWA KILIMO CHA UMWAGILIAJI NA KWA KUTUMIA PLAU 

WANACHAMA wa Kikundi cha JIPE MOYO cha Kijijini Kome, Kata ya Bwasi, wakitayarisha SHAMBA lao la MIHOGO.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
KIKUNDI cha KILIMO  cha JIPE MOYO cha Kijijini Kome, Kata ya Bwasi kinajishughulisha na KILIMO cha UMWAGILIAJI.
KATIBU wa Kikundi hiki, Ndugu Deborah Isaack, amesema kuwa KIKUNDI chao kina WANACHAMA 35 na kilianzishwa Mwaka 2015.
KIKUNDI hiki (JIPE MOYO) kinaundwa na WANAWAKE tu na wanajishughulisha na KILIMO kwa MPANGILIO ufuatao:
MAZAO YA UMWAGILIAJI (bustani): Wanalima matikiti, nyanya, vitunguu na kabeji
MAZAO YA KUTEGEMEA MVUA: Wanalima mahindi, mihogo, maharage na alizeti (majaribio)
ZANA & MBEGU ZA KILIMO
Kikundi cha JIPE MOYO kimepewa misaada na mikopo kutoka kwa : HALMASHAURI yetu (Musoma DC) imetoa MIKOPO kwa awamu mbili, yaani, MILIONI tano (5) na MILIONI saba (7).
PCI (TANZANIA) imechangia: *MASHINE ya UMWAGILIAJI, *MBEGU za mahindi na mihogo
MBUNGE wa Jimbo lao, Prof Sospeter Muhongo amechangia:
*Jembe la kukokotwa na ng’ombe (PLAU)
*MBEGU za mihogo, mtama na alizeti.
MAFANIKIO YA KIKUNDI CHA JIPE MOYO
MWANACHAMA, Ndugu Bilenjo Mangano, amesema tayari yeye AMEJENGA NYUMBA BORA na anasomesha vizuri WATOTO wake kutokana na  MAPATO mazuri ya Kikundi chao.
VIlevile, MWANACHAMA huyo amesema wenzake wengine wamefanikiwa kufungua MADUKA kutokana na MAPATO mazuri ya Kikundi chao.
SHULE YA MSINGI KOME YAPEWA CHAKULA
Kikundi cha JIPE MOYO kimegawa sehemu ya MAVUNO yake ya hivi karibuni na kuipatia S/M Kome:
*MAHINDI Magunia 4
*MAHARAGE kilo 80
AFISA KILIMO wa  Kata ya Bwasi, Ndugu Alex Mihambo, amekuwa akifuatilia kazi za KILIMO za Kikundi hikil na kuhakikisha kuwa SOKO la MAZAO yao linapatikana bila usumbufu.
AFISA Kilimo huyo  amesema kwamba WANAVIJIJI wengine wamehamasika sana na KUANZISHA VIKUNDI vya KILIMO na kwa sasa kuna VIKUNDI vipya 15 Kijijini Kome.
KIKUNDI CHA JIPE MOYO CHATAYARISHA MIRADI MIPYA
Kwa siku za usoni, Kikundi hiki kimepanga kufanya yafuatayo:
*Kuongeza HISA za MFUKO wao wa FEDHA za kukopeshana
*Uoteshaji wa MITI ya msitu
*Ufugaji wa NYUKI kwa ajili ya biashara ya ASALI
*Kuanzisha KIWANDA kidogo cha kukamua MAFUTA ya ALIZETI.
DC, DED, MBUNGE, MADIWANI na VONGOZI wengine wanawashawishi WANAVIJIJI wa Jimbo la Musoma Vijijini KUANZISHA VIKUNDI VYA UCHUMI, yaani, vya Kilimo cha Umwagiliaji, Uvuvi wa samaki, Ufugaji wa nyuki, n.k.
MWITIKIO wa uanzishwaji wa VIKUNDI vya UCHUMI ni mzuri na Mbunge wa Jimbo anaendelea kugawa bure MAJEMBE ya kukokotwa na ng’ombe (PLAU) kwenye VIKUNDI vya KILIMO.
Taratibu za VIKUNDI vya UVUVI kupewa MIKOPO ya RIBA NAFUU unaendelea.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU KWENYE SHULE ZA MUSOMA VIJIJINI UNAENDELEA: VYOO VIPYA VYAJENGWA SHULENI LYASEMBE

MAJENGO na UKAMILISHAJI wa MATUNDU 22 ya CHOO KIPYA cha S/M Lyasembe ya Kijijini Lyasembe, Kata ya Murangi.

Tarehe 7.4.2021
Musoma Vijijini

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge

SERIKALI yetu imetoa SHILINGI 31,936,072.11 (Tsh Milioni 31.94) kuchangia ujenzi wa VYOO VIPYA kwenye Shule ya Msingi LYASEMBE ya Kijijini Lyasembe, Kata ya Murangi.

WANAKIJIJI wamejitolea kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji (NGUVUKAZI) kwa ajili ya ujenzi wa MATUNDU MAPYA 22 ya CHOO KIPYA cha Shule yao ya Msingi.

MWALIMU MKUU wa Shule hiyo, Mwl Athuman Mnkende amesema Shule ilianza Mwaka 1975 na ina jumla ya WANAFUNZI 872.

SHULE hiyo inapaswa kuwa na MATUNDU 40 ya CHOO. Ujenzi wa kutumia FEDHA zilizotolewa na SERIKALI, na NGUVUKAZI za WANAKIJIJI, umewezesha kukamilisha CHOO KIPYA chenye MATUNDU 22 na kufanya Shule hiyo kuwa na VYOO 2 vyenye jumla ya MATUNDU 28 (13 Wasichana, 13 Wavulana na 2 Walimu).

MWALIMU MKUU huyo anaishukuru sana SERIKALI yetu kwani vyoo vilivyokuwa vinatumiwa ni vya muda mrefu (1975) na vilikaribia kujaa. Kwa hiyo, bila msaada wa SERIKALI, Shule ingalifungwa kwa kukosa Vyoo vya Wanafunzi.

MTENDAJI wa Kijiji cha Lyasembe, Ndugu Chikonya Chikonya anawashukuru sana WANAKIJIJI kwa MCHANGO wa NGUVUKAZI zao uliowezesha ujenzi kukamilika ndani ya muda uliopangwa.

DIWANI wa Kata ya Murangi, Mhe Hamisi Nyamamu amewasihi wanafunzi na walimu kutunza na kudumisha usafi wa choo hicho kipya ambacho kimejengwa kwa USHIRIKIANO wa Serikali yetu na Wananchi wa Kijiji cha Lyasembe.

MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ameishaichangia S/M Lyasembe:
*Madawati 80
*Vitabu vingi vya Maktaba

TUCHANGIE UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA S/M LYASEMBE

*Madarasa yanayohitajika ni 20 yaliyopo ni 10

MATOKEO YA MITIHANI YA MWAKA JANA (2020)

*STD IV (2020)
Watahiniwa 104
Waliofaulu 99 (95.2%)

*STD VII (2020)
Watahiniwa 70
Waliofaulu 43 (61.4%)

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

MAJI SAFI NA SALAMA YA BOMBA NA SHEREHE ZA PASAKA NDANI YA VIJIJI VITATU

WANANCHI wa Vijiji vya Busungu (Kata ya Bulinga) na Kwikerege (Kata ya Rusoli) wakiteka MAJI ya BOMBA kutoka Ziwa Victoria.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge

WANANCHI wa Vijiji vya Busungu (Kata ya Bulinga), Bukima (Kata ya Bukima) na Kwikerege (Kata ya Rusoli) WAMEFURAHI sana kuanza kupata MAJI ya BOMBA ya Ziwa Victoria.

WANANCHI hao, hasa akina MAMA na WATOTO wamefurahishwa sana na upatikanaji wa maji katika maeneo yao, kwani hapo awali walilazimika kutembea umbali mrefu na kutumia muda mwingi kutafuta maji kutoka kwenye visima vya asili.

Mama Nyamburi Mafuru, Mkazi wa Kijiji cha Busungu amesema kuwa amefurahishwa sana na neema ya upatikanaji wa maji kijijini mwao maana walitumia muda mwingi kutafuta maji na kupelekea shughuli za kujitafutia kipato kuzorota.

Mama huyo amesema, “Tunaishukuru sana Serikali yetu kwa kutuondolea kero hii hasa sisi wanawake.”

MKANDARASI wa Mradi huu, EDM NETWORK LTD, Ndugu Adiel Mushi amethibitisha kukamilika kwa mradi huo kwa zaidi ya 90% na VITUO 23 vimeanza kutumika ambavyo ni:
* Vioski 2
*Maltwater 1
*Vituo 2 vya kunyweshea mifugo
*Vituo 18 vya kuchotea maji.

Mkandarasi huyo ameeleza kwamba TANKI la BUSUNGU lina uwezo wa kujaza LITA 225,000 za kuhudumia Vijiji 3 hivyo.

DIWANI wa Kata ya Bulinga, Mhe Abel Mafuru amewataka WANANCHI kutunza vizuri MIUNDOMBINU ya usambazaji wa maji ya bomba kwenye Vijiji vyao.

DIWANI huyo ametoa SHUKRANI nyingi sana kwa SERIKALI yetu kwa kuwapatia MAJI SAFI na SALAMA ya BOMBA, na vilevile amemshukuru Mbunge wao, Prof Sospeter Muhongo kwa UFUATILIAJI mzuri wa Miradi ya Maji na Miradi mingine ndani ya Jimbo lao.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijni.or.tz

UBORESHAJI WA MAZINGIRA YA KUJIFUNZA NA KUFUNDISHIA – MAKTABA ZAENDELEA KUJENGWA KWENYE SHULE ZA MSINGI

 

Katika MATUKIO mbalimbali kwenye S/M KARUBUGU ya Kijijini Kurwaki, Kata ya Mugango, Prof Sospeter Muhongo alitembelea Darasa la III la Shule hiyo kushuhudia Mirundikano ya Wanafunzi madarasani.

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge

WANANCHI wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kushirikiana na SERIKALI kuboresha mazingira ya KUJIFUNZA na KUFUNDISHIA kwenye SHULE za MSINGI na SEKONDARI za Jimboni mwetu.

UJENZI WA MAKTABA KWENYE S/M KARUBUGU

KIJIJI cha KURWAKI kimeamua kujenga MAKTABA kwenye Shule yao ya Msingi, S/M KARUBUGU, iliyofunguliwa Mwaka 1963.

MWALIMU MKUU wa Shule hii, Mwl Rehema Ramadhan amesema kwamba Shule ina jumla ya WANAFUNZI 830 na WALIMU 5.

UFAULU WA MITIHANI YA MWAKA JANA (2020)

MWALIMU MKUU huyo ameeleza UFAULU huo kama ifuatavyo:

STD IV (2020)
*Watahiniwa: 82
*Waliofaulu: 82

STD VII (2020)
*Watahiniwa: 73
*Waliofaulu: 60

UJENZI WA MAKTABA YA KISASA

MTENDAJI wa Kijiji cha Kurwaki, Ndugu Abeid Makamba Ndagala amesema kwamba ujenzi wa MAKTABA ya S/M KARUBUGU ulianza Jumatatu, 8.3.2021 na wanakusudia kukamilisha ujenzi wa BOMA la MAKTABA kabla ya tarehe 30.3.2021.

WACHANGIAJI WA UJENZI HUU

*WANAKIJIJI:
Wanachangia NGUVUKAZI kwa kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji.

*WANAKIJIJI wanachangia FEDHA taslimu Tsh. 5,000/= kwa kila KAYA.

*MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo anachangia SARUJI ya UJENZI wa BOMA la MAKTABA hii. Leo,16.3.2021 amechangia SARUJI MIFUKO 50 ataendelea kuchangia hadi Boma likamilike.

*PCI (TANZANIA) itafadhili umaliziaji wa ujenzi wa MAKTABA hiyo baada ya kukabidhiwa BOMA linalojengwa na WANAKIJIJI. Aidha, PCI (TANZANIA) itaweka SAMANI zinazohitajika kwenye MAKTABA hiyo.

VITABU VYA MAKTABA YA S/M KARUBUGU

Wachangiaji wa VITABU vya MAKTABA hiyo ni:

*PCI (Tanzania)
*MBUNGE wa Jimbo

MATUKIO mbalimbali kwenye S/M KARUBUGU ya Kijijini Kurwaki, Kata ya Mugango.

*Ufyatuaji wa matofali ya ujenzi wa Maktaba.
*Uchimbaji wa Msingi wa Boma la Maktaba
*Ujenzi wa Msingi wa Boma la Maktaba
*Mirundikano ya Wanafunzi madarasani. Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo alitembelea Darasa la III la Shule hiyo kushuhudia Mirundikano ya Wanafunzi madarasani.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

SERIKALI YASHIRIKIANA NA WANAKIJIJI KUTATUA MATATIZO YA UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MADARASA

Ujenzi unaondelea (Vyumba vya Madarasa & Vyoo) kwenye S/M BUSEKERA ya Kijijini Busekera, Kata ya Bukumi.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge

SHULE YA MSINGI BUSEKERA ilifunguliwa Mwaka 1954. Shule hii iko Kijijini Busekera, Kata ya Bukumi.

MWALIMU MKUU wa Shule hii, Mwl Kevin Majogoro amesema kwamba Shule ina jumla ya WANAFUNZI 1,271.

MAHITAJI ya Madarasa ni Vyumba 24, vilivyopo ni 10!

MIRUNDIKANO ya WANAFUNZI madarasana ni mikubwa. Kwa mfano, Darasa la AWALI lina Wanafunzi 234 kwenye chumba kimoja na Darasa la VII lina Wanafunzi 111 ndani ya chumba kimoja!

SERIKALI YATOA MCHANGO WA KUJENGA MADARASA NA VYOO

SERIKALI kupitia MRADI wake wa EP4R imetoa Tsh MILIONI 47.7 kwa ajili ya ujenzi wa VYUMBA 2 vya MADARASA na CHOO chenye MATUNDU 7 ya S/M Busekera.

MICHANGO YA WANAKIJIJI

MTENDAJI wa Kijiji cha Busekera, Ndugu Faustine Majura amesema WANAKIJIJI wameshirikishwa kwa:

*kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji

*kuchimba shimo la choo

*kuchimba msingi wa Vyumba 2 vya madarasa.

SHUKRANI KWA SERIKALI YETU

Wananchi na Viongozi wa Kijiji cha Busekera WANAISHUKURU sana SERIKALI kwa kuwachangia Tsh Milioni 47.7.

MICHANGO YA MBUNGE WA JIMBO

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo amekuwa akihamasisha na kuchangia uboreshaji wa MAZINGIRA ya KUJIFUNZA na KUFUNDISHIA kwenye SHULE zote za Jimboni mwao.

MICHANGO ya Mbunge huyo kwenye S/M Busekera ni:

*Saruji Mifuko 60
*Mabati 54
*Madawati 94
*Vitabu vingi vya Maktaba

TUCHANGIE KUBORESHA UFAULU WA S/M BUSEKERA

MATOKEO ya DARASA la IV (2020):

*Watahiniwa 123
*Waliofaulu 120

MATOKEO ya DARASA la VII (2020):

*Watahiniwa 69
*Waliofaulu 45

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijni. or. tz

WASAIDIZI 6 WA MBUNGE WA JIMBO WANUNULIWA PIKIPIKI MPYA 6

Tukio la ununuaji na upokeaji wa PIKIPIKI MPYA 6 za Wasaidizi wa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.

Leo, Jumatano, tarehe 3 Machi 2021, MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo AMEWANUNULIA WASAIDIZI wake PIKIPIKI MPYA 6 na kuwazawadia PIKIPIKI za ZAMANI walizokuwa wanazitumia.

JIMBO la Musoma Vijijini lina KATA 21 zenye VIJIJI 68 na VITONGOJI 374.

WASAIDIZI wa MBUNGE wamegawiwa maeneo yao ya kazi na KILA JUMAMOSI Ripoti za kazi zao za wiki lazima Mbunge huyo apewe.

Kwa hiyo, WANAVIJIJI wanafuatwa huko huko VIJIJINI mwao na hawana sababu ya KUFUNGA SAFARI kwenda kumtafuta Mbunge, badala yake wao (wanavijiji) ndio wanatembelewa kwenye makazi yao au sehemu zao za kazi za kiuchumi na kwenye miradi ya maendeleo.

Mbunge huyo ametoa VITENDEA KAZI vifuatavyo:

*Pikipiki tokea Mwaka 2015
*Mafuta ya Pikipiki kila wiki
*Smartphone & Bando
*Laptop
*GPS

Vilevile, Wasaidizi wa Mbunge huyo wanapewa BONUS ya kila mwisho wa Mwaka.

KARIBUNI TUJENGE MUSOMA VIJIJINI

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

KASI IONGEZEKE KWENYE UJENZI WA BARABARA YA LAMI YA MUSOMA-MAKOJO-BUSEKERA

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini akiwa na WATAALAAMU wa TANROADS na MKANDARASI Kijijini Kusenyi kwenye ukaguzi wa barabara ya Musoma-Makojo-Busekera inayojengwa kwa kiwango cha LAMI.

Jumatatu, tarehe 1.3.2021, MBUNGE wa JIMBO la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo alikagua ujenzi wa BARABARA KUU ya Jimbo hilo inayojengwa kwa kiwango cha LAMI – barabara ya KILOMITA 92 ya Musoma-Makojo-Busekera.

Mbunge huyo alifuatana na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mara, Injinia Felix Ngaile na MKANDARASI wa Mradi, Injinia Getanyeri Nyantori.

Wataalamu wengine wa TANROADS walikuwepo na VIONGOZI wa Kijiji cha KUSENYI nao walikuwepo.

USHAURI ULIOTOLEWA

(1) Kasi ya ujenzi iongezeke na AGIZO la RAIS Mhe Dkt John Joseph Pombe Magufuli LITEKELEZWE, yaani ujenzi wa awali wa KILOMITA 40.

(2) Kazi kubwa ya awali kwenye kipande cha Kusenyi-Kwikonero imefanyika, yaani kunyanyua tuta na kudhibiti udongo mweusi uliochukua sehemu kubwa ya kipande hiki ambacho ni mkondo wa maji yaingiayo Ziwa Victoria.

Vilevile, ujenzi wa madaraja kwenye maeneo korofi umekaribia kukamilika, kwa hiyo kasi ya ujenzi wa barabara hii MUHIMU SANA kwa UCHUMI wa Jimbo letu na kwa Taifa letu kwa ujumla (madini, samaki, pamba, mihogo, maziwa, n.k.) iongezeke.

(3) Fedha za Mradi zitolewe kwa wakati baada ya maombi yote kutimiza masharti yaliyowekwa.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

SEKONDARI YA KATA YAJENGA MAABARA YA KIWANGO KIZURI

MBUNGE wa JIMBO, Prof Sospeter Muhongo akikakugua MAABARA ya KEMIA na VYUMBA VIPYA 4 vya MADARASA ya Dan Mapigano Memorial Secondary School ya Kata ya Bugoji.

JIMBO la Musoma Vijijini lina KATA 21 lenye jumla ya VIJIJI 68.

IDADI YA SEKONDARI JIMBONI

*21 za Kata/Serikali
*2 Binafsi
*4 MPYA zinajengwa Kabegi, Nyasaungu, Nyegina na Seka
*7 MPYA zimepangwa kuanza kujengwa Mwaka huu (2021): Bukumi, Busamba, Bwai, Kataryo/Mayani, Kurwaki/Nyang’oma, Muhoji na Wanyere.

UJENZI WA MAABARA KWENYE SEKONDARI ZA JIMBONI

*Kila SEKONDARI iko kwenye hatua mbalimbali za ujenzi wa MAABARA 3 – Biology, Chemistry and Physics

DAN MAPIGANO MEMORIAL SECONDARY SCHOOL

SEKONDARI ilifunguliwa Mwaka jana (2020) na ina jumla ya WANAFUNZI 265 (139 Form I & 126 Form II). WALIMU wapo 6 na wote wameajiriwa na SERIKALI.

WANAOTOA MICHANGO YA UJENZI WAKE
*Wanavijiji
*Serikali
*Diwani wa Kata
*Mbunge wa Jimbo
*Wazaliwa wa baadhi ya Vijiji

UJENZI uliokwishakamilika:
*Vyumba 5 vya Madarasa
*Ofisi 2 za Walimu
*Choo chenye Matundu 8

UJENZI unaondelea:
*Vyumba 4 vya Madarasa
*Maabara 3
*Ofisi 1 ya Walimu
*Choo chenye Matundu 8
*Nyumba 1 ya Walimu

Jumamosi, 27.2.2021, MBUNGE wa JIMBO, Prof Sospeter Muhongo alikagua ujenzi unaondelea kwenye SEKONDARI hii ya KATA ya BUGOJI yenye Vijiji 3 – Bugoji, Kaburabura na Kanderema.

MAABARA ZINAZOJENGWA

SERIKALI imetoa Tsh MILIONI 50 kuchangia ujenzi wa MAABARA Shuleni hapo – TUNAISHUKURU SANA SERIKALI YETU KWA MCHANGO HUU MUHIMU SANA!

WANAVIJIJI wanachangia NGUVUKAZI kwenye ujenzi wa MAABARA hizi.

MAABARA YA KEMIA

UBORA wa MAABARA hii ni wa kiwango kizuri, na ujenzi wake utakamilika kabla ya tarehe 15 Machi 2021.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

MBUNGE WA JIMBO AWATOA WANAFUNZI WANAOJIFUNZIA MCHANGANI NA AKODISHIA NYUMBA KIJIJINI ITUMIWE NA WALIMU WA SEKONDARI MPYA

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, alipokuwa Kigera Sekondari (Kata ya Nyakatende) na Shule Shikizi Egenge (Kata ya Etaro)

 

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo anakagua ujenzi unaoendelea kwenye SHULE za MSINGI na SEKONDARI za Jimbo hilo.

SHULE SHIKIZI EGENGE

Shule hii iko kwenye Kitongoji cha Egenge, Kijiji cha Busamba, Kata ya Etaro.

IDADI ya WANAFUNZI wa Shule hii ni kama ifuatavyo: 60 Awali, 30 Darasa la I na 60 Darasa la II.

Prof Sospeter MUHONGO ameamua KUNUNUA VIBAO vya KUJIFUNZIA vya Wanafunzi wa DARASA LA AWALI na wa DARASA LA KWANZA baada ya kuambiwa kwamba Wanafunzi hao wanajifunza kwa KUANDIKA MCHANGANI.

Vilevile, Mbunge huyo amekubali KUEZEKA PAA la Vyumba 2 vya Madarasa vinavyojengwa hapo.

Shule ina Vyumba 4 vya Madarasa vilivyojengwa na SERIKALI (Miradi ya EQUIP & EP4R) kwa kushirikiana na WANANCHI wa Kitongoji cha Egenge.

Vilevile, WANANCHI hao hao wanajenga Vyumba vingine 4 kwa kushirikiana na DIWANI na MBUNGE wao wa Jimbo.

LEO KUU ni Shule SHIKIZI EGENGE iwe na MIUNDOMBINU ya Shule kamili ya Msingi kabla ya tarehe 30 Disemba 2021.

SEKONDARI MPYA YAFUNGULIWA KIJIJINI KIGERA

KIGERA Sekondari imefunguliwa Jumatatu, tarehe 22.2.2021 na tayari WANAFUNZI 103 kati ya 122 wa Kidato cha Kwanza wameanza masomo.

WALIMU 5 ni wa kuajiriwa na Serikali na 1 ni wa kujitolea.

UJENZI unaendelea kwa kasi na MAABARA zitakamilika kabla ya tarehe 1.6.2021.

SEKONDARI hii MPYA ni kati ya Sekondari mpya 5 zinazojengwa Jimboni mwetu, na nyingine 4 zitaanza kujengwa mwaka huu.

MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ametembelea Sekondari hiyo mpya na kutatua tatizo la MAKAZI ya WALIMU hapo Kijijini.

MBUNGE huyo ameamua kulipia PANGO la MIEZI 6 ili WALIMU 2 waweze kupata MAKAZI hapo Kijijini, karibu na Sekondari hiyo.

ELIMU NDIYO INJINI KUU YA MAENDELEO NA USTAWI WA JAMII

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

WANAFUNZI WASIOJUA KUSOMA, KUANDIKA NA KUHESABU (KKK) WAPUNGUA KWA KASI KUBWA NA UTORO WATOWEKA BAADA YA KITONGOJI CHA MWIKOKO KUJENGA SHULE YAKE

Ujenzi unavyoendelea kwenye Shule Shikizi MWIKOKO ya Kitongoji cha Mwikoko, Kijijini Chitare, Kata ya Makojo.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge

WANAVIJIJI wa JIMBO la Musoma Vijijini wanaendelea KUSHIRIKIANA na SERIKALI kuboresha MAZINGIRA ya kujifunzia na kufundishia WANAFUNZI wa SHULE za Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC) yenye Jimbo la Musoma Vijijini.

UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA
ELIMU YA MSINGI

*VYUMBA vipya 395 vya Madarasa vimejengwa kwenye Shule za Msingi za Serikali (111) ndani ya Miaka 5 (2015-2020)

MICHANGO ya ujenzi huo imetolewa na Wanavijiji, Serikali, Madiwani, Mbunge wa Jimbo na baadhi ya Wazaliwa wa Vijiji husika.

*SHULE SHIKIZI 12 zinajengwa na kupanuliwa kuwa Shule za Msingi kamili

MICHANGO ya ujenzi huo inatolewa na Wanavijiji, Serikali, Madiwani, Mbunge wa Jimbo na baadhi ya Wazaliwa wa Vijiji husika.

*MAKTABA za Shule za Msingi zinaendelea kujengwa na kufunguliwa

MICHANGO ya ujenzi wa MAKTABA inatolewa na Wanavijiji, PCI TANZANIA, Madiwani, Mbunge wa Jimbo na baadhi ya Wazaliwa wa Vijiji husika.

*VYOO vya kutosha vimejengwa kwa wingi kwenye Shule za Msingi – ahsante sana PCI TANZANIA kwa mchango wenu mkubwa kwenye ujenzi wa vyoo mashuleni. Wanavijiji wamechangia nguvukazi.

SHULE SHIKIZI MWIKOKO

Shule Shikizi Mwikoko ipo kwenye Kitongoji cha Mwikoko, Kijijini Chitare, Kata ya Makojo

WANAFUNZI 299 wa chini ya miaka minane (8), yaani Darasa la CHEKECHEA hadi la PILI wameacha kutembea umbali wa zaidi ya KILOMITA 4 kwenda masomoni kwenye Shule za Msingi za CHITARE A & B.

MWALIMU Magige Simon, Msimamizi na Mlezi wa Shule Shikizi Mwikoko amesema uwepo wa Shule hiyo kwenye Kitongoji hicho, umezaa matunda mazuri:

(i) UTORO unatoweka na Wanafunzi wanazidi kupenda shule

(ii) IDADI ya WANAFUNZI wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) INAPUNGUA kwa kasi kubwa mno kwa Wanafunzi wa Darasa la I & II wa Kitongoji hicho

MWENYEKITI wa Kitongoji cha Mwikoko, Ndugu Athuman Mtembela anawashukuru wale wote wanaochangia ujenzi wa shule yao.

MICHANGO YA UJENZI WA SHULE SHIKIZI MWIKOKO

(i) WANAKIJIJI – nguvukazi (kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji) na fedha taslimu Tsh 10,300 kutoka kwa kila KAYA.

(ii) SERIKALI kupitia Mradi wake wa EQUIP umechangia Tsh Milioni 60.

(iii) DIWANI wa Kata, Mhe Kuyenga Masatu amechangia Tsh 500,000

(iv) MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo amechangia SARUJI MIFUKO 100.

(v) MFUKO wa JIMBO umechangia SARUJI MIFUKO 80 na MABATI 108.

MALENGO ya Wakazi wa Mwikoko ni kwamba ifikapo Mwakani (2022) Shule Shikizi yao iwe Shule kamili ya Msingi yenye MADARASA 7.

KUMBUKA:
Kwa miaka 2 mfululizo (2019 & 2020) WANAFUNZI wa Darasa la IV wa Musoma Vijijini WAMEONGOZA Mkoa wa Mara kwenye MITIHANI ya Darasa la IV.

*Tuendelee kuboresha MAZINGIRA ya kujifunzia na kufundishia WANAFUNZI wetu – TUTAFANIKIWA!

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

UBORESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA MUSOMA VIJIJINI UNAENDELEA – KIJIJI CHA NYABAENGERE CHAANZA KUJENGA ZAHANATI YAKE

WANAVIJIJI wakisomba mawe kwa ajili ya ujenzi wa ZAHANATI ya Kijiji chao cha NYABAENGERE, Kata ya Musanja.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge

WANAVIJIJI wa Jimbo la Musoma Vijijini kwa kushirikiana na SERIKALI, wameamua kujenga na kuboresha MIUNDOMBINU ya HUDUMA za AFYA ndani ya Vijiji vyao na Kata zao.

Mbunge wa Jimbo, Madiwani na Wazaliwa wa baadhi ya Vijiji wanachangia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu hiyo.

ZAHANATI ZILIZOPO NA ZINATOA HUDUMA

*Zahanati 24 za Serikali
*Zahanati 4 za Binafsi

ZAHANATI MPYA ZINAZOJENGWA

*Zahanati 14 zinajengwa

WODI ZA MAMA & MTOTO ZINAZOJENGWA

*Wodi 3 za Mama & Mtoto zinajengwa kwenye Zahanati za Bukima, Kisiwani Rukuba na Nyegina.

VITUO VYA AFYA VINAVYOTOA HUDUMA

*Vituo 2 vya Afya vya Murangi na Mugango vinatoa huduma.

*Zahanati ya Masinono inapanuliwa iwe Kituo cha Afya cha Kata hiyo ya Bugwema.

HOSPITALI YA WILAYA INAJENGWA

*Hospitali ya Wilaya inajengwa kwenye Kitongoji cha Kwikonero, Kijijini Suguti.

KIJIJI CHA NYABAENGERE CHAAMUA KUJENGA ZAHANATI YAKE

DIWANI wa Kata ya MUSANJA, Mhe Ernest Mwira amesema VIJIJI 3 vya Kata hiyo havina ZAHANATI hata moja na vyote vinahudumiwa na KITUO cha AFYA cha Kata jirani ya Murangi.

KIONGOZI huyo ameendelea kueleza kwamba baadhi ya WAGONJWA wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya KILOMITA 10 kwenda kupata matibabu kwenye Kituo hicho cha Afya.

Kwa hiyo, Kijiji cha NYABAENGERE kimeamua kujenga ZAHANATI yake ambayo imepangwa ikamilike ndani ya mwaka mmoja.

MTENDAJI wa Kijiji (VEO) cha Nyabaengere, Ndugu Emmanuel Eswaga amesema utekelezaji wa MPANGOKAZI wa Mradi huo, unamtaka KILA MWANAKIJIJI mwenye uwezo wa kufanya kazi, ATACHANGIE Tsh 24,000, na kila KITONGOJI kitasomba mawe, mchanga na maji.

MCHANGO WA DIWANI

Diwani, Mhe Ernest Mwira ataanza kutoa MICHANGO yake kwa kuchangia SARUJI MIFUKO 20

MCHANGO WA MBUNGE
WA JIMBO

Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo, AMEKUBALI kuanza kuchangia ujenzi huo na ataanza kwa kuchangia SARUJI MIFUKO 100.

OMBI KWA WAZALIWA WA KATA YA MUSANJA

Zahanati inayoanza kujengwa Kijijini Nyabaengera itatoa HUDUMA za Afya kwa Vijiji jirani vya Mabui Merafuru na Musanja vyote vya Kata hiyo.

Kwa hiyo, WAZALIWA wa Kata ya MUSANJA wanaombwa wachangie MRADI huu kwa kutuma MICHANGO yao kwa DIWANI au VIONGOZI wengine wa Kata hiyo.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

WANAVIJIJI WASHIRIKIANA NA SERIKALI KUBORESHA MAZINGIRA YA ELIMU – KITONGOJI CHAJENGA SHULE SHIKIZI

Miundombinu ya SHULE SHIKIZI EGENGE inayojengwa ndani ya Kitongoji cha Egenge, Kijiji cha Busamba, Kata ya Etaro.

 

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge

JIMBO la MUSOMA laendelea kushirikiana na SERIKALI kutatua MATATIZO ya muda mrefu yaliyoko kwenye SEKTA ya ELIMU.

MATATIZO hayo ni:

*UMBALI mrefu wanaotembea WANAFUNZI kwenda masomoni

*MIRUNDIKANO ya WANAFUNZI Madarasani

SULUHISHO:

*UJENZI wa SHULE karibu na MAKAZI ya WANAVIJIJI

*UJENZI wa VYUMBA VIPYA vya MADARASA kwenye Shule zilizopo.

TAKWIMU: SHULE ZA MSINGI

*JIMBO lina KATA 21 zenye jumla ya VIJIJI 68

*SHULE za MSINGI za SERIKALI zipo 111

*SHULE SHIKIZI 12 zinajengwa na kupanuliwa kuwa Shule za Msingi kamili.

*SHULE za MSINGI za Binafsi zipo 3

*VYUMBA VIPYA 395 vya Madarasa vimejengwa ndani ya miaka mitano (2015-2020)

KITONGOJI CHA EGENGE CHAJENGA SHULE SHIKIZI

Kitongoji cha EGENGE ni moja kati ya VITONGOJI vinne (4) vya Kijiji cha BUSAMBA.

Kijiji hicho ni moja ya Vijiji 4 vya Kata ya ETARO. Vijiji vingine ni: Mmahare, Rukuba (Kisiwa) na Etaro.

WANAFUNZI wa Kitongoji cha EGENGE wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya KILOMITA 7 kwenda masomoni kwenye Shule ya Msingi Busamba.

UMBALI mrefu na MIRUNDIKANO ya Wanafunzi madarasani ni sababu kuu zilizofanya KITONGOJI cha EGENGE kiamue kujenga SHULE SHIKIZI yake, na ujenzi ulianza rasmi Mwaka 2016.

MRATIBU wa ELIMU wa Kata ya Etaro, Ndugu Samwel Samike ameeleza kwamba Shule Shikizi hiyo ILIFUNGULIWA Mwaka 2019 na inao WANAFUNZI wa Madarasa matatu, yaani, Darasa la Awali hadi Darasa la Pili.

WINGI wa WANAFUNZI wa Shule Shikizi hiyo ni kama ifuatavyo

*Darasa la AWALI, Wanafunzi 50
*Darasa la KWANZA, 40
*Darasa la PILI, 33.

WANAFUNZI wa Darasa la TATU wa Kitongoji hicho bado wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilomita saba (7) kwenda masomoni kwenye S/M Busamba.

UJENZI WA MIUNDOMBINU YA SHULE SHIKIZI

*Vyumba 2 na Ofisi 1 vimejengwa na SERIKALI kupitia Mradi wake wa EQUIP

*Matundu 4 ya choo cha Wanafunzi (EQUIP)

*Matundu 2 ya choo cha Walimu (EQUIP)

*Vyumba 2 na Ofisi 1, SERIKALI kupitia Mradi wa EP4R

*Vyumba 4 na Ofisi 1 vinajengwa na WANAVIJIJI na VIONGOZI wao.

MICHANGO INAYOTOLEWA KWENYE UJENZI HUU

(i) WANAVIJIJI

*Nguvukazi – kusomba mawe, kokoto, maji na mchanga.

*Fedha taslimu – kila KAYA kuchangia Tsh 10,000/=

(ii) SERIKALI – WIZARA ZA ELIMU & TAMISEMI

*Mradi wa EQUIP umechangia Tsh Milioni 60

*Mradi wa EP4R umechangia Tsh Milioni 47.7

(iii) MBUNGE wa JIMBO, Prof Sospeter Muhongo ameanza kutoa MICHANGO yake kwa kuchangia SARUJI MIFUKO 50.

MWENYEKITI wa Kitongoji cha EGENGE, Ndugu Nkuyu Mururi ametoa SHUKRANI nyingi kwa WACHANGIAJI wote ikiwemo SERIKALI yetu.

KIONGOZI huyo anaomba WADAU wa MAENDELEO waendelee kuwachangia VIFAA VYA UJENZI, ambapo MAHITAJI yao kwa sasa ni MABATI 216 na SARUJI MIFUKO 200.

UFAULU WA WATOTO KUTOKA KITONGOJI CHA EGENGE (Darasa la VII 2020)

Kati ya Wanafunzi 53 waliofaulu kutoka S/ M Busamba, Watoto kutoka Kitongoji cha EGENGE wamefaulu saba (7) tu.

Hivyo ni muhimu sana kuboresha mazingira ya kufundisha na kujifunza kwa watoto wa Kitongoji cha Egenge – ujenzi wa SHULE SHIKIZI EGENGE ukamilike!

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

WANAVIJIJI  WANAJENGA VYUMBA 2 VYA MADARASA NA MATUNDU 28 YA VYOO VYA WANAFUNZI

Hatua ya ujenzi iliyofikiwa kwa MABOMA ya Vyumba viwili vya Madarasa, na MASHIMO 28 ya VYOO vya Wanafunzi wa BUGWEMA SEKONDARI ya Kata ya Bugwema.

 

Na: Fedson Masawa

Msaidizi wa Mbunge

WANAVIJIJI wa Kata ya Bungwema yenye Vijiji 4 (Bugwema, Kinyang’erere, Masinono na Muhoji)  wanashirikiana na VIONGOZI wao kujenga Vyumba viwili (2) vya Madarasa, Ofisi moja (1) ya Walimu na Matundu 28 ya VYOO vya Wanafunzi kwenye SEKONDARI yao (Bugwema Secondary School).

Akishuhudia ujenzi unaoendelea shuleni hapo, MSAIDIZI wa MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Ndugu Fedson Masawa, amejiridhisha na maendeleo mazuri kwenye ujenzi huo.

 

MICHANGO YA UJENZI KUTOKA KWA WANAVIJIJI

MTENDAJI KATA (WEO) hiyo, Ndugu Josephat Phinias amesema WANAVIJIJI wamekubaliana kuchanga Tsh 5,000 kutoka kila KAYA kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba vya Madarasa.

Vilevile, kila KAYA inachanga Tsh 15,000/= kwa ajili ya ujenzi wa MATUNDU 28 ya VYOO vya Wanafunzi.

KIONGOZI huyo anaomba WADAU wa MAENDELEO wawachangie MABATI 108 kwa ajili ya kuezeka MABOMA wanayoyajenga.

 

MICHANGO YA

MBUNGE WA JIMBO

Prof Sospeter Muhongo, Mbunge wa Jimbo lenye Bugwema Sekondari ameishaichangia shule hii kama ifuatavyo:

*VITABU vingi vya Maktaba

*POSHO ya Mwalimu 1 wa MASOMO ya SAYANSI kwa kipindi cha MIAKA MIWILI (2).

*SARUJI MIFUKO 70

*Kupeleka WAFADHILI wa ujenzi wa MAABARA

 

MWALIMU MKUU wa Bugwema Sekondari, Mwl Joseph Emmanuel Ndaro ameeleza kwamba SEKONDARI hiyo ilianzishwa MWAKA 2006, ina WANAFUNZI 556. Shule ina Vyumba vinane (8) vya Madarasa, na inapungukiwa vinne (4)

 

MWALIMU MKUU huyo ameeeleza UFAULU wa Shule yao wa Mwaka jana (2020) wa Kidato cha PILI (II) na NNE (IV) kama ifuatavyo:

 

KIDATO CHA II MWAKA 2020

Daraja la I = Wanafunzi 5 (ME 4 na KE 1)

Daraja II = 7 (ME 6, KE 1)

Daraja III = 13 (ME 10, KE 3)

Daraja IV = 51 (ME 24, 27

Daraja 0 = 7 (ME 5, KE 2)

 

KIDATO CHA IV MWAKA 2020

Daraja I = Wanafunzi 3 (ME 3, KE 0)

Daraja II = 4 (ME 4, KE 0)

Daraja III = 8 (ME 7, KE 1)

Daraja IV = 50 (ME 28, KE 12)

Daraja 0 = 24 (ME 7, KE 17)

 

Ofisi ya Mbunge

Jimbo la Musoma Vijijini

www.musomavijijini.or.tz

UJENZI WA VIWANGO VIZURI VYA SEKONDARI MPYA YA KATA: MIUNDOMBINU YA MAJI INAJENGWA

MIUNDOMBINU ya KIGERA SEKONDARI ambayo itafunguliwa Mwezi huu (Februari 2021)

Tarehe 8.2.2021.
Jimbo la Musoma Vijijini

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge

KATA ya NYAKATENDE inayoundwa na Vijiji 4 vya Kakisheri, Kamguruki, Kigera na Nyakatende ina SEKONDARI MOJA inayohudumia VIJIJI hivyo na Vijiji vya Kata jirani ya IFULIFU.

Kwa hiyo SEKONDARI moja hiyo inakabiliwa na MATATIZO ya MIRUNDIKANO ya WANAFUNZI madarasani, na wengine wanatembea umbali wa zaidi ya KILOMITA 10 kwenda masomoni.

WANANCHI wa Vijiji 2 (Kigera na Kakisheri) wameamua KUJENGA SEKONDARI yao ambayo itakuwa ni Sekondari ya pili ndani ya Kata hiyo (Nyakatende), na inaitwa KIGERA SECONDARY SCHOOL.

UJENZI WA UBORA WA JUU

AFISA ELIMU na WATAALAMU wa ujenzi wa Halmashauri yetu wanakiri kwamba KIGERA SEKONDARI inajengwa kwa kuzingatia matakwa ya ujenzi yanayotolewa na SERIKALI yetu.

PONGEZI nyingi ziende kwa WANAVIJIJI na WAZALIWA wa Vijiji hivyo, na UONGOZI mzuri na madhubuti wa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kigera, Ndugu Magafu Katura.

MICHANGO YA UJENZI

Michango ya ujenzi wa Sekondari hii inatolewa na:

*WANAVIJIJI – Nguvukazi, yaani kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji.

*WANAVIJIJI – Fedha taslimu, Shilingi 2,000 kwa kila MKAZI wa Vijiji hivyo viwili na mwenye umri wa zaidi ya miaka 18.

*WAZALIWA wa Vijiji 2 hivyo. Hawa wanalipa gharama za mafundi na wananunua baadhi ya vifaa vya ujenzi.

*MBUNGE wa JIMBO, Prof Sospeter Muhongo amekwishachangia SARUJI MIFUKO 150 na MABATI 108

*MFUKO wa JIMBO umechangia SARUJI MIFUKO 300 na MABATI 216.

*HALMASHAURI yetu imechangia Shillingi 5,000,000/= (Tshs 5M)

MADAWATI NA SAMANI ZA OFISI

*WAZAZI wa WANAFUNZI 124 watakaoanza masomo KIGERA SEKONDARI wametengeneza Madawati.

*DIWANI wa Kata ya Nyakatende, Mhe Marere Kisha amechangia Samani za Ofisi za Walimu (Viti 8 na meza 4)

MIUNDOMBINU YA MAJI INAJENGWA

*RUWASA inakamilisha ujenzi wa MIUNDOMBINU ya MAJI kwa ajili ya matumizi ya Sekondari hiyo mpya – hii ni sehemu ya MRADI wa RUWASA wa USAMBAZAJI MAJI (kutoka Ziwa Victoria) kwenye Kata ya Nyakatende.

MIUNDOMBINU INAYOKAMILISHWA ILI SEKONDARI IFUNGULIWE

*Vyumba 2 vya Madarasa vimekamilika

*Jengo la Utawala lenye Ofisi 9 limekamilika.

*Boma la CHOO cha Matundu 11. Tundu 1 la choo ni kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum – limekamilika

*Ujenzi wa CHOO cha WALIMU umeanza.

*Boma la MAABARA 3 linakamilishwa

*Nyumba 1 ya MWALIMU imeanza kujengwa

WANAFUNZI WALIOFAULU KUINGIA KIDATO CHA KWANZA

WANAFUNZI 191 wa Kata ya Nyakatende wamefaulu kujiunga na Kidato cha Kwanza. Hivyo, WANAFUNZI hao 191 watagawanywa kwenye SEKONDARI 2 za Kata hiyo yaani, Nyakatende Sekondari na Kigera Sekondari (itakayofunguliwa Mwezi huu, Februari 2021)

*Vyumba vya Madarasa
*Choo chenye Matundu 11
*Madawati ya Wanafunzi
*Viti na Meza za Walimu
*Miundombinu ya Maji ya RUWASA

ELIMU NI INJINI YA UCHUMI, MAENDELEO NA USITAWI IMARA WA KILA TAIFA

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

ZAHANATI ZA MUSOMA VIJIJINI ZAPANULIWA KWA KUONGEZA WODI ZA MAMA & MTOTO

BOMA la Jengo la Mama & Mtoto la Zahanati ya Kisiwani Rukuba, Musoma Vijijini.

Tarehe 2.2.2021
Jimbo la Musoma Vijijini

HALMASHAURI ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC) yenye Jimbo la Musoma Vijijini (Kata 21, Vijiji 68) lina:

*Magari ya Wagonjwa (Ambulances) 5
*Zahanati 24 za Serikali zinazotoa huduma za Afya
*Zahanati 4 za Binafsi zinazotoa huduma za Afya
*Zahanati mpya 14 zinajengwa
*Vituo vya Afya 3 vinatoa huduma za Afya
*Hospitali ya Wilaya 1 – ujenzi unakamilishwa

WANAVIJIJI wa Jimbo la Musoma Vijijini wameamua kuboresha HUDUMA za AFYA zitolewazo kwenye ZAHANATI zao kwa kujenga WODI za Mama & Mtoto.

UJENZI wa MIUNDOMBINU hii mipya unachangiwa na:

*Serikali
*Wanavijiji
*Mbunge wa Jimbo
*Madiwani
*Wazaliwa wa Musoma Vijijini
*Wadau wengine wa Maendeleo

UJENZI WA WODI ZA MAMA & MTOTO

Baadhi ya ZAHANATI zilizojengwa zamani zimeanza kuboresha HUDUMA za AFYA wanazozitoa kwa kujenga WODI za Mama & Mtoto.

KISIWA cha RUKUBA ni Kijiji cha Kata ya Etaro. Kijiji hiki kimeamua kujenga WODI ya Mama & Mtoto inayotarajiwa kukamilika kabla ya tarehe 1 Machi 2021.

Zahanati nyingine zilizoanza ujenzi wa Wodi za Mama & Mtoto ni Zahanati za Bukima na Nyegina.

JENGO la WODI ya Mama & Mtoto la Zahanati ya Kisiwani Rukuba lina VYUMBA 13. Michango ya ujenzi imetolewa na:

*WANAVIJIJI – nguvukazi
*FEDHA zinazorudishwa (20% ya Makusanyo ya ushuru) kutoka Halmashauri yetu
*MBUNGE wa JIMBO – ameanza kwa kuchangia SARUJI MIFUKO 200.

WADAU wa MAENDELEO wanaombwa kuanza kuchangia VIFAA vinavyohitajika kwenye WODI hiyo, vikiwemo, vitanda, magodoro, n.k.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

MUSOMA VIJIJINI – RUWASA YAONGEZA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA USAMBAZAJI MAJI YA ZIWA VIKTORIA

Jumamosi, 30.1.2021 RUWASA (W) ilifanya majaribio ya MRADI wa MAJI wa BULINGA-BUJAGA kwenye KITUO cha SWEDI

INJINIA Saidi Nyamlinga, Meneja wa RUWASA wa Wilaya ya Musoma amesema kwamba kwenye Mradi huu wamejenga MATENKI 2:

(i) Tenki la Kijijini BULINGA lina uwezo wa kujaza LITA 150,000. VITUO 14 vimejengwa na leo (30.1.2021) majaribio yamefanywa kwenye KITUO cha Swedi – PICHA 3 za hapa zinaonesha WANAVIJIJI wakiteka MAJI kutoka Kituo cha Swedi.

Hili ni BOMBA la MAJI la Bujaga-Bulinga ndani ya Kata ya Bulinga

(ii) Tenki la Kijijini BUSUNGU lina uwezo wa kujaza LITA 225,000. Ujenzi wa VITUO 15 vya Vijiji 3 vya Busungu, Bukima na Kwikerege unakamilishwa na majaribio yatafanywa ndani ya wiki 2 zijazo.

Hili ni BOMBA la MAJI la Busungu-Bukima-Kwikerege ndani ya Kata za Bulinga, Bukima na Rusoli.

MAJARIBIO yakikamilika, WANAVIJIJI watakaribishwa kutuma MAOMBI ya kufungiwa maji majumbani mwao au kwenye maeneo ya biashara zao.

HONGERENI SANA RUWASA

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

UJENZI NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU WAPANDISHA UFAULU WA SHULE ZA MSINGI

Matokeo ya Darasa la Nne ya Mwaka jana (SFNA 2020) ya Halmashauri 9 za Mkoa wa Mara.

Matokeo ya Darasa la Nne ya Mwaka jana (SFNA 2020) ya Halmashauri 9 za Mkoa wa Mara.

Jumatano, 27.1.2021
Jimbo la Musoma Vijijini

MICHANGO ya WANAVIJIJI, SERIKALI, MBUNGE wa JIMBO na MADIWANI yawezesha Jimbo la Musoma Vijijini na Halmashauri yake kujenga VYUMBA VIPYA 395 vya MADARASA kati ya Mwaka 2015 na 2020.

VYUMBA VIPYA hivyo 395 vimejengwa kwenye SHULE za MSINGI 111 na SHULE SHIKIZI 14.

MUSOMA VIJIJINI YAONGOZA MKOA

Kwa miaka miwili mfululizo (2019 & 2020) Shule za Msingi za Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC) ZIMEFANYA VIZURI na kuongoza Mkoa wa Mara kwenye MITIHANI ya DARASA la NNE (SFNA, standard four national assessment) na Mwaka jana (2020) ufaulu ulikuwa wa kiwango cha 98.04% – PONGEZI NYINGI ziende kwa Wanafunzi, Walimu, Wazazi, DC Dr Anney Naano & Timu yake, na DED Ndugu John Kayombo & Timu yake.

Kwa miaka ya nyuma, Halmashauri yetu ilikuwa inashikilia mkia Mkoani Mara. Haya ni MABADILIKO MAKUBWA yaliyochangiwa na UJENZI na UBORESHAJI wa MIUNDOMBINU ya ELIMU kwenye Shule za MSINGI za Halmashauri hii.

VYUMBA VIPYA VYA MADARASA VYAENDELEA KUJENGWA

Mbali ya ujenzi wa Vyumba vipya 395 ndani ya miaka 5, MBUNGE wa JIMBO na MADIWANI wa Kata zote 21 WAMEAMUA kwamba ifikapo tarehe 1.7.2021, SHULE zote za MSINGI hazitakuwa na MADARASA CHINI ya MITI.

Vilevile, MIRUNDIKANO ya Wanafunzi madarasani itapungua kwa kiasi kikubwa.

WANAVIJIJI wanaomba SERIKALI yao iendelee kuchangia ujenzi wa Vyumba vipya vya Madarasa kwenye Shule zao.

UJENZI WA MAKTABA KWENYE SHULE ZA MSINGI

JIMBO la Musoma Vijijini LINAENDELEA kujenga MAKTABA kwenye Shule zake za Msingi.

MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo anaendelea kugawa VITABU kwenye Shule zote za Msingi na Sekondari. VITABU hivi ni vya Maktaba za Shule na vingi ni vya Masomo ya Sayansi na Lugha ya Kiingereza.

PCI TANZANIA YATOA MICHANGO MIKUBWA

PCI Tanzania inaendelea kuchangia ujenzi wa MAKTABA na utoaji wa VITABU kwenye Maktaba hizo – Ahsante sana PCI Tanzania.

PICHA za hapa zinaonesha:

*Maktaba ya S/M Butata (Jengo lenye rangi ya krimu) – Wanafunzi wakiwa ndani ya Maktaba hiyo.

*Maktaba ya S/M Rukuba (Jengo lenye rangi nyeupe). Hii Maktaba iko Kisiwani Rukuba

*Matokeo ya Darasa la Nne ya Mwaka jana (SFNA 2020) ya Halmashauri 9 za Mkoa wa Mara.

wanafunzi wakiwa ndai ya Maktaba ya S/M Butata

Maktaba ya S/M Butata (Jengo lenye rangi ya krimu) – Wanafunzi wakiwa ndani ya Maktaba hiyo.

Maktaba ya S/M Rukuba (Jengo lenye rangi nyeupe). Hii Maktaba iko Kisiwani Rukuba

FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO ZACHANGIA UKAMILISHAJI WA MIUNDOMBINU YA SHULE  ZA MUSOMA VIJIJINI

baadhi ya MIUNDOMBINU inayojengwa kwenye SEKONDARI MPYA ya VIJIJI 2 (Kakisheri & Kigera) vya Kata ya Nyakatende. SEKONDARI hii itafunguliwa Mwezi huu, Januari 2021.

UJENZI na UBORESHAJI wa MIUNDOMBINU ya SHULE zote za Jimboni mwetu unachangiwa na:
* Wanavijiji
* Serikali
* Mbunge wa Jimbo
* Wadau wa Maendeleo, k.m. PCI Tanzania, na Benki za NMB, CRDB na TPB
* Wazaliwa wa baadhi ya Vijiji
IDADI YA SHULE NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI
(Jimbo lina Vijiji 68, Kata 21)
(i) SHULE SHIKIZI: 12
Ujenzi na upanuzi wa Shule hizi unaendelea. Baadhi ya Shule hizo tayari zinatoa ELIMU ya AWALI ya WATOTO wa chini ya MIAKA 6.
(ii) SHULE ZA MSINGI: 111
Vyumba vipya vya Madarasa  vinaendelea kujengwa na kuboreshwa kwenye Shule hizi.
Vyumba VIPYA 380 vimejengwa kwenye Shule hizi ndani ya miaka mitano (2016-2020).
MAKTABA zinaendelewa kujengwa (nyingine tayari zimekamilika na zinatumika) kwenye baadhi ya Shule hizi
MIUNDOMBINU mingine inaendelea kujengwa na kuboreshwa, hasa NYUMBA mpya za WALIMU na VYOO vipya.
(iii) SHULE ZA MSINGI ZA BINAFSI: 3
*Zipo Shule za Binafsi 3 ndani ya Jimbo letu.
(iv) SEKONDARI ZA KATA:
20 + 5 mpya
SEKONDARI MPYA zilizofunguliwa Mwaka jana (2020) ni mbili:
 * Dan Mapigano Memorial Secondary School ya Kata ya Bugoji
* Busambara Secondary School ya Kata ya Busambara
Vyumba VIPYA 120 vimejengwa kwenye Sekondari zetu 20 ndani ya miaka mitano (2016-2020).
(v) SEKONDARI
 ZA BINAFSI: 2
* Zipo Sekondari 2 za Madhehebu ya Dini ya Katoliki (RC) na Wasabato (SDA)
(vi) SEKONDARI MPYA ZA KATA ZINAZOJENGWA
SEKONDARI zinazojengwa na zitakazofunguliwa Mwaka huu (2021) ni:
* Seka Secondary School ya Kata ya Nyamrandirira (Sekondari ya pili ya Kata)
* Nyasaungu Secondary School ya Kata ya Ifulifu (Sekondari ya kwanza ya Kata)
* Kigera Secondary School, Kata ya Nyakatende (Sekondari ya pili ya Kata)
* Bukwaya Secondary School ya Kata ya Nyegina inakamilisha miundombinu (Sekondari ya pili ya Kata)
* Ifulifu Secondary School ya Kata ya Ifulifu inayojengwa Kijijini Kabegi. Inakamilisha miundombinu (Sekondari ya Kata ya pili)
USIMAMIAJI MZURI & MADHUBUTI
*MKUU wa Wilaya (DC), Dr Vicent Anney Naano anapongezwa sana kwa KUSIMAMIA ujenzi huu na mwingine, kwa MAFANIKIO makubwa, tokea Mwaka 2016.
* HALMASHAURI yetu chini ya Mkurugenzi (DED) John Lipesi Kayombo inafanya kazi vizuri.
MGAO WA FEDHA ZA
MFUKO WA JIMBO
(Jan 2021, Tshs 52.43M)
MANUNUZI & UGAWAJI:
*Mabati: 1,134
*Saruji Mifuko (supa):1,020
JUMLA: Tshs 52,176,378 (Tshs 52.18M)
* HALMASHAURI yetu ndiyo inayotunza FEDHA za MFUKO wa JIMBO, na ndiyo inafanya MANUNUZI ya VIFAA vya UJENZI baada ya kupewa MAELEKEZO kutoka kwenye Kamati ya Mfuko wa Jimbo chini ya Mwenyekiti wake, Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo
MGAO – MALENGO
* Kukamilisha MIUNDOMBINU ya SHULE MPYA ili zifunguliwe Mwaka huu (2021).
* Kuongeza idadi ya Vyumba VIPYA vya Madarasa kwenye Sekondari zilizofunguliwa Mwaka jana (2020)
SEKONDARI MPYA (2021):
(1) SEKA SECONDARY SCHOOL
(Kata ya Nyamrandirira)
* Mabati 216
* Saruji Mifuko 200
(2) KIGERA SECONDARY SCHOOL
(Kata ya Nyakatende)
* Mabati 216
* Saruji Mifuko 200
(3) NYASAUNGU SECONDARY SCHOOL
(Kata ya Ifulifu)
* Mabati 54
* Saruji Mifuko 80
SEKONDARI MPYA ZA MWAKA JANA (2020)
(4) DAN MAPIGANO MEMORIAL SECONDARY SCHOOL
(Kata ya Bugoji)
* Mabati 216
* Saruji Mifuko 180
(5) BUSAMBARA SECONDARY SCHOOL
(Kata ya Busambara)
* Mabati 216
* Saruji Mifuko 180
SHULE ZA MSINGI MPYA
(6) MWIKOKO SHULE SHIKIZI
(Kitongoji cha Mwikoko, Kijiji cha Chitare, Kata ya Makojo)
* Mabati 108
* Saruji Mifuko 80
(7) NYASAENGE SHULE SHIKIZI
(Kitongoji cha Nyasaenge, Kijiji cha Kataryo, Kata ya Nyakatende)
* Mabati 108
* Saruji Mifuko 100
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

KITONGOJI CHA NYASAENGE CHAAMUA KUJENGA SHULE YAKE YA MSINGI

MIUNDOMBINU ya  SHULE SHIKIZI NYASAENGE inayojengwa ndani ya Kitongoji cha Nyasaenge, Kijiji cha Kataryo, Kata ya Tegeruka.

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
WATOTO wa Kitongoji cha NYASAENGE wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya KILOMITA 10 kwenda masomoni kwenye SHULE ya Msingi KATARYO.
Kitongoji cha NYASAENGE ni moja kati ya VITONGOJI 6 (sita) vya Kijiji cha KATARYO. Kijiji hiki ni moja ya Vijiji 3 (Kataryo, Mayani na Tegeruka)  vya Kata ya TEGERUKA
Kijiji cha KATARYO kina SHULE 2 za MSINGI, yaani KATARYO na KATARYO B.
WANANCHI wa Kitongoji cha NYASAENGE wameamua kutatuta tatizo la umbali mrefu unaotembewa na WATOTO wao kwenda masomoni kwa KUJENGA SHULE yao ya MSINGI, ambayo itaanza ikiwa SHULE SHIKIZI NYASAENGE.
MIUNDOMBINU ya SHULE SHIKIZI hiyo inayokamilishwa ni:
*Vyumba 2 vya Madarasa
*Ofisi 1 ya Walimu
*Choo chenye Matundu 8
Kwa hiyo, WANANCHI wa KITONGOJI cha MYASAENGE wanaomba WATATO wao waanze MASOMO yao ya AWALI kwenye Shule Shikizi yao itakayotambuliwa na Halmashauri yetu.
MRATIBU wa Elimu Kata ya Tegeruka, Ndugu Modest Fadhili amesema kuwa jumla ya WANAFUNZI 149 wa Darasa la Awali wanasomea CHINI ya MTI hapo hapo Kitongojini Nyasaenge wakifundishwa na MWALIMU wa KUJITOLEA, Ndugu Mauna Rugeye.
KITONGOJI CHA NYASAENGE CHAFANYA VIZURI MASOMONI
Mbali ya umbali mrefu wa kutembea, WANAFUNZI wa kutoka Kitongoji cha NYASAENGE, wamefaulu vizuri Mitihani ya Darasa la VII (2020) wakishinda Vitongoji vingine vitano (5).
Matokeo ya Darasa la VII (2020) ni haya hapa:
*S/M Kataryo:*
Kati ya Wanafunzi 16 waliofaulu, jumla ya Wanafunzi 11 (Wasichana 6 na Wavulana 5) wametoka Kitongoji cha Nyasaenge
*S/M Kataryo B*
Kati ya Wanafunzi 37 waliofaulu, jumla ya Wanafunzi 13 (Wasichana 8 na Wavulana 5) wametoka Kitongoji cha Nyasaenge
WACHANGIAJI WA UJENZI HUU
(i) WANANCHI
*NGUVUKAZI  – kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji
*FEDHA taslimu – kila KAYA inachangia Tsh 30,000/=
(ii) WAZALIWA WA KITONGOJI CHA NYASAENGE
Fedha taslimu zimechangwa kutoka kwa:
*Saguda Paliga 100,000/=
*Madete Washuli 100,000/=
*Gubi Gong’oma 100,000/=
*Maiku Lyangeni 100,000/=
(ii) MBUNGE WA JIMBO
*Prof Sospeter Muhongo atachangia MABATI 54.
MBUNGE huyo ametoa MICHANGO mingi kwa SHULE 2 za Kijiji cha KATARYO ambayo ni:
S/M KATARYO
*Madawati 76
*Vitabu vya Maktaba
S/M KATARYO B
*Saruji Mifuko 60
*Mabati 108
*Madawati 73
*Vitabu vya Maktaba S/M
MFUKO WA JIMBO
*Mabati 54
(S/M Kataryo B)
MWENYEKITI wa Kitongoji cha Nyasaenge, Ndugu Kabole Mesogachura ametoa SHUKRANI nyingi kwa WACHANGIAJI wote wakiwemo WANANCHI wa Kitongoji cha NYASAENGE.
KIONGOZI huyo anaomba WADAU wa MAENDELEO waendelee kuwachangia VIFAA ZA UJENZI ili wakamilishe ujenzi wa SHULE SHIKIZI NYASAENGE ambayo itapanuliwa na kuwa SHULE YA MSINGI NYASAENGE.
WANAFUNZI 149 wa ELIMU ya AWALI wa Kitongoji cha NYASAENGE wataacha kusomea CHINI ya MTI baada ya kupata VYUMBA 2 vya Madarasa ya SHULE SHIKIZI NYASAENGE.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

KATA YA NYAMRANDIRIRA YADHAMIRIA KUPATA SEKONDARI YAKE YA PILI ITAKAYOFUNGULIWA JANUARI 2021

MIUNDOMBINU ya SEKA SEKONDARI inavyoendelea kujengwa Kijijini Seka, Kata ya Nyamrandirira.

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
Kata ya Nyamrandirira inaundwa na Vijiji Vitano (5) ambavyo ni: Chumwi, Kaboni, Kasoma, Mikuyu na Seka.
Kata hii ina Sekondari moja tu iliyoko Kijijini Kasoma (KASOMA SECONDARY SCHOOL) yenye Kidato cha kwanza hadi cha sita.
UMBALI MREFU wa zaidi ya km 10 wa kutembea kwa  Wanafunzi walio wengi, na MIRUNDIKANO yao  Madarasani ni sababu zilizowafanya WANANCHI wa Kata hii kuamua kujenga SEKONDARI ya pili Kijijini Seka (SEKA SECONDARY SCHOOL).
Akizungumza na Msaidizi wa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini,  Ndugu Fedson Masawa, DIWANI wa Kata ya Nyamrandirira, Mhe Nyeoja Wanjara amesema kuwa lengo lao ni kukamilisha ujenzi wa VYUMBA 5 vya MADARASA kabla ya tarehe 30 Januari 2021.
MIUNDOMBINU mingine muhimu inayohitajika ili SEKA SEKONDARI ifunguliwe itakamilishwa kabla ya tarehe 30 Januari 2021 ambayo ni:
* Choo chenye Matundu 8
* Jengo la Utawala
MAJENGO mengine yatakayojengwa ni: Maabara, Maktaba, Vyumba zaidi vya Madarasa, Nyumba za Walimu, n.k.
SEKA SEKONDARI ni moja ya Sekondari Mpya 5 zinazojengwa ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini lenye Sekondari 20 za Serikali/Kata na 2 za Binafsi.
*Wachangiaji wa Ujenzi huu ni:*
(i) WANANCHI kwa mpangilio huu:
*Kijiji cha Kaboni –  kila Kaya inachangia Tsh 10,000/=
* Kijiji cha Seka – kila Kaya inachangia kati ya Tsh 20,000/=  na 15,000/=
* Kijiji cha Kasoma – kila Kaya inachangia Tsh 10,000/=
* Kijiji cha Chumwi – kila Kaya inachangia Tsh 6,500/=
* Kijiji cha Mikuyu – kila Kaya inachangiya Tsh 20,000/=
(ii) NGUVUKAZI za Wanavijiji wa Vijiji vyote 5 – kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji.
(iii) MBUNGE WA JIMBO
Prof Sospeter Muhongo tayari amekwishachangia SARUJI MIFUKO 250 (mia mbili hamsini).
MBUNGE huyo ametoa AHADI ya kutoa MICHANGO zaidi iwapo KASI ya UJENZI itaongezeka, na hasa ya ujenzi wa VYOO vya Shule.
(iv) WAZALIWA WA KATA YA SEKA
*Wazaliwa 21 tayari wamechangia jumla ya Tsh 1,884,000/=
(v) WADAU WENGINE WA MAENDELEO
Mgodi wa MMG uliopo Kijijini Seka umechangia:
* Mawe tripu 20
* Molamu tripu 10
* Mchanga tripu 10
Vilevile, MMG imetoa AHADI ya kujenga Jengo moja la Shule.
MWENYEKITI wa Serikali ya Kijiji cha Seka, Ndugu Damian Mjara, kwa niaba ya Wananchi wa Kata Nyamrandirira, anawaomba WADAU wa MAENDELEO wajitokeze na kuwachangia MABATI, SARUJI, NONDO, MADAWATI, n.k. ili SEKA SEKONDARI ifunguliwe tarehe 30 Januari 2021.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

SEKONDARI NYINGINE MPYA INAYOJENGWA KWA NGUVU ZA WANANCHI NA MBUNGE WAO KUFUNGULIWA JANUARI 2021

ukamilishaji wa MIUNDOMBINU ya KIGERA SECONDARY SCHOOL itakayofunguliwa Januari 2021.

Tarehe 29.12.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
JIMBO la MUSOMA VIJIJINI lenye Kata 21na Vijiji 68 linajenga SEKONDARI MPYA 5 ili kutatua MATATIZO sugu mawili – mirundikano madarasani na umbali mrefu wanaotembea baadhi ya Wanafunzi.
Kwa hiyo, idadi ya SEKONDARI za Serikali Jimboni humo zitaongezeka kutoka 20 hadi 25. Vilevile, zipo Sekondari 2 za Madhehebu ya Dini.
MWAKA MPYA (2021): Kata nyingine 6 zitaanza ujenzi wa Sekondari ya pili ya Kata zao.
KATA ya NYAKATENDE yenye Vijiji 4 (Kakisheri, Kamguruki, Kigera na Nyakatende) ina Sekondari moja tu (NYAKATENDE SEKONDARI) ambayo imeelemewa na wingi wa Wanafunzi kutoka Vijiji 4 na wengine wanatoka Kata jirani ya Ifulifu.
Kwa hiyo, UJENZI wa SEKONDARI ya PILI ya Kata hiyo ni muhimu sana.
KIGERA SEKONDARI ITAFUNGULIWA JANUARI 2021
Vijiji 2 (Kakisheri na Kigera) vya Kata hiyo VIMEAMUA kujenga SEKONDARI yao ili watoto wao waachane kabisa na mirundikano madarasani na kutembea mwendo wa zaidi ya kilomita 10 kwenda masomoni.
WANAOCHANGIA UJENZI WA KIGERA SEKONDARI
(i) WANAVIJIJI wa Vijiji viwili wanachangia NGUVUKAZI zao – kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji.
 (ii) WANAVIJIJI hao hao wanachangia FEDHA taslimu: Shilingi 2,000 (elfu mbili) kwa kila mkazi mwenye umri wa kuanzia miaka 18.
(iii) WAZALIWA wa Vijiji hivyo viwili: wanalipa GHARAMA zote za MAFUNDI na wananunua baadhi ya VIFAA vya ujenzi.
(iv) DIWANI wa Kata ya Nyakatende, Mhe Marere J. Kisha ambae ni mmoja wa WAZALIWA na Vijiji 2 nae anachangia kama Wazaliwa wenzake.
*Vilevile, DIWANI huyu anatengeneza MADAWATI 130 ya WANAFUNZI watakaoanza Kidato cha kwanza shuleni hapo Januari 2021.
(v) MBUNGE wa JIMBO, Prof Sospeter Muhongo amekwishachangia:
*Saruji Mifuko 150
 *Mabati 108
MFUKO wa JIMBO
*Saruji Mifuko 100
*Mbunge huyo atachangia, Januari 2021, zaidi ya VITABU 1,000 (elfu moja) vya SAYANSI vya Maktaba ya Sekondari hiyo mpya.
MAJENGO YANAYOKAMILISHWA UJENZI
*VYUMBA 2 vya Madarasa vimeishaezekwa, frame za milango na madirisha zimewekwa, sasa wanapiga jamvi kwa ajili ya kuweka sakafu.
*JENGO la Utawala lenye Ofisi 9 limeezekwa na madirisha yamewekwa.
*BOMA la CHOO cha Matundu 11 limeishaezekwa . Tundu 1 la Choo ni kwa ajili ya Wanafunzi wenye mahitaji maalum.
*Boma la Maabara linajengwa
*Boma la Nyumba ya Mwalimu linajengwa
WANAFUNZI 191 WA KATA WAMEFAULU
Wanafunzi 191 wa Kata ya Nyakatende wamefaulu kujiunga na Kidato cha Kwanza Januari 2021.
Kwa hiyo, WANAFUNZI hao 191 watagawanywa kwenye SEKONDARI 2 za Kata – Nyakatende & Kigera Secondary Schools.
MWENYEKITI wa Serikali ya Kijiji cha Kigera, Ndugu Magafu Katura anatoa maombi yafuatayo ya  kuchangia ujenzi huu  kwa hatua waliyoifikia:
*Saruji Mifuko 100
*Topu 31 za Milango
*Frame 21 za Milango ya Choo na ya Jengo la Utawala
*Vitasa 31vya Milango
*Bawaba 31 (pair) za Milango
*Masinki 15 ya Choo
*Mabomba piece 5 ya Choo
*Rangi Lita 80
HALMASHAURI ya Wilaya ya Musoma IMECHANGIA Shilingi MILIONI TANO (5M) kwenye ukamilishaji wa ujenzi wa Miundombinu ya Sekondari hii mpya.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

WANANCHI WA KIJIJI CHA NYASAUNGU WASHIRIKIANA NA MBUNGE WAO KUJENGA SEKONDARI YA KIJIJI CHAO

ukamilishaji wa ujenzi wa MIUNDOMBINU ya NYASAUNGU SEKONDARI ya Kijiji cha Nyasaungu, Kata ya Ifulifu. 

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
KATA ya IFULIFU ni Kata pekee kati ya Kata 21 za Jimbo la Musoma Vijijini ambayo HAINA SEKONDARI yake.
WANAFUNZI wa Sekondari kutoka VIJIJI 3 vya Kata hii, yaani, Kabegi, Kiemba na Nyasaungu wanasoma kwenye Sekondari za Kata jirani za Mugango na Nyakatende.
WANAVIJIJI wa Kata ya IFULIFU WAMEAMUA kujenga Sekondari zao za Kata kwa utaratibu huu:
*Kijiji cha Nyasaungu kinajenga Sekondari yake kwa kushirikiana na Mbunge wao wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo
*Vijiji vya Kabegi na Kiemba nao wanajenga  Sekondari yao kwa kushirikiana na Mbunge wao, Prof Muhongo
NYASAUNGU SEKONDARI
Ujenzi wa Sekondari hii ulianza Julai 2019.  WANANCHI wa Kijiji cha Nyasaungu waliamua kujenga Sekondari yao iitwayo NYASAUNGU SEKONDARI ili kutatua kero ya Watoto wao kutembea kilomita 24 kwenda masomoni kwenye Sekondari za Kata jirani.
MWENYEKITI wa Serikali ya Kijiji cha Nyasaungu, Ndugu Magesa Chacha Marera, amesema kuwa ujenzi huo hadi hapo ulipofikia unaendeshwa kwa NGUVU za WANANCHI wa Kijiji cha Nyasaungu pekee, na michango ya Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo.
MAKUNDI YANAYOCHANGIA UJENZI WA NYASAUNGU SEKONDARI
(i) KAYA zenye NG’OMBE zaidi ya 100, michango yao ni zaidi ya Tshs 200,000 (laki mbili)
(ii) KAYA zenye NG’OMBE kati ya 50 na 99, michango yao ni Tshs 100,000 (laki moja)
(iii) KAYA zenye NG’OMBE chini ya 50, michango yao ni Tshs 40,000 (elfu arobaini).
(iv) NGUVUKAZI za Wanakijiji za kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji.
(v) MICHANGO ya Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo
*MABATI 108
*SARUJI MIFUKO 35
*NONDO 20
MFUKO wa JIMBO
*Mabati 54
MIUNDOMBINU INAYOKAMILISHWA SEKONDARI IFUNGULIWE JANUARI 2021
*VYUMBA 2 vya Madarasa tayari vimeishaezekwa
*CHUMBA 1 cha Darasa tayari kimeishaezekwa na hiki kitatumika kwa muda kama OFISI ya WALIMU
*CHOO chenye MATUNDU 6 kinaezekwa kabla ya tarehe 1.1.2021
WANAFUNZI 124 WA KATA WAMEFAULU
NYASAUNGU Sekondari, yenye VYUMBA 2 vya MADARASA inategemea kupokea baadhi ya WANAFUNZI hao wa Kata
UONGOZI wa KIJIJI cha Nyasaungu unatoa maombi kwa WADAU wa MAENDELEO waungane wao kwenye ujenzi wa SEKONDARI yao – wanaendelea na ujenzi wa Vyumba vya Madarasa, Jengo la Utawala, Maabara, Maktaba, Nyumba za Walimu, Vyoo, n.k.
SEKONDARI hii MPYA itakuwa tayari kupokea Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza, Januari 2021.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

VIKUNDI VYA WANAVIJIJI VYA KUKUZA UCHUMI VINAZIDI KUSHAMIRI MUSOMA VIJIJINI

baadhi ya Wanachama wa Kikundi cha TUMETAMBUA wakipalilia MIHOGO shambani mwao, Kijijini KASTAM, Kata ya Bukima.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge

WANAVIJIJI ndani ya VIJIJI 68 vya Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kuanzisha VIKUNDI vya kustawisha na kukuza UCHUMI wao. VIKUNDI hivyo ni vya KILIMO, UVUVI, UFUGAJI na VICOBA.

KIKUNDI cha TUMETAMBUA kilichopo Kijiji cha Kastam, Kata ya Bukima kilianzishwa Mwaka 2017 na kina Wanachama 29.

KIKUNDI hiki kinajishughulisha na KILIMO, uoteshaji wa MITI, na KUKOPESHANA fedha.

MWENYEKITI wa Kikundi hiki, Ndugu Nyamisi Daniel anasema wao wamejikita zaidi kwenye KILIMO cha mihogo, mahindi, maharage na viazi lishe. Kwa hiyo, WANACHAMA wote wanacho CHAKULA cha kutosha kwa familia zao, na wanapeleka 20% ya MAVUNO yao ya mazao ya chakula kwenye S/M Mkapa ya Kijijini mwao.

Vilevile, Kikundi hiki chenye MAFANIKIO makubwa kinatoa msaada wa VIFAA vya SHULE kwa Wanafunzi wanaosoma wakiwa kwenye mazingira magumu.

MBEGU YA MIHOGO YA AINA YA MKOMBOZI YATOA MAVUNO MAZURI

MZALISHAJI MBEGU za MIHOGO, Ndugu Festo Obed ambae pia ni Mwanachama wa Kikundi cha TUMETAMBUA amepata MAFUNZO ya kuzalisha mbegu bora za mihogo kutoka Shirika la MEDA ambalo kwa sasa linafanya kazi kwenye Kata za Bugoji, Bukima, Kiriba, Murangi, Nyamrandirira, Rusoli na Suguti.

Ndugu Obed anasema alipanda VIJITI 4,000 vya mbegu ya MKOMBOZI akafanikiwa kuvuna VIJITI 38,400 ndani ya Miezi 12. Kwa sasa, yeye amekuwa Mfanyabiashara wa MBEGU (Vijiti) ya MIhogo ya aina ya MKOMBOZI ambapo kila KIJITI anauza Shilingi 30.

MTAALAMU wa MEDA, Ndugu Isaack Musa amesema lengo kuu la Shirika lao ni kuendeleza mbegu bora za mihogo zinazostahimili magonjwa. Baada ya kupata MAFANIKIO kwa Mbegu ya MKOMBOZI, MEDA imeanzisha MASHAMBA DARASA ya mbegu nyingine za mihogo za aina ya MKUMBA, MKURANGA 1, T130, ORERA, KIROBA, EYOPE na F-10-30R katika Kata za Ifulifu, Mugango, Nyambono na Rusoli.

KIKUNDI cha TUMETAMBUA kinasudia kupanua MASHAMBA yake ya MIHOGO ili wapate MAVUNO ya ziada ya biashara.

Aidha, mbali na MAFANIKIO hayo KIKUNDI hiki kinatarajia kuanzisha Mradi wa MASHINE ya KUSAGA, kununua CHAREHANI za kushona nguo, na kununua VIFAA vya USEREMALA.

WANACHAMA wa Kikundi cha TUMETAMBUA wanatoa SHUKRANI kwa WADAU wa MAFANIKIO yao ambao ni:

*PCI Tanzania kwa kuwapatia Mbegu za Mahindi, Maharage, Alizeti na magunia ya kuhifadhia chakula.

*Jamii Impact kwa kuwapatia MKOPO wa Shilingi Million 5 (awamu ya kwanza), na awamu ya pili walikopeshwa Shilingi Million 8.

*SHIMAKIUMU kwa kuwapatia Mbegu za Mahindi, Dawa za Mimea na Viroba vya kupandia miche.

*MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo kuwapatia Mbegu za Mihogo, Mtama na Alizeti.

Prof Muhongo aligawa bure Jimboni mwao MAGUNIA 796 ya MBEGU (Vijiti) ya mihogo aina ya MKOMBOZI kama ifuatavyo:

Mwaka 2016/2017: MAgunia 446

Mwaka 2017 /2018: Magunia 350

MFUKO wa JIMBO kwa kuwapatia mashine na mipira ya umwagiliaji, na mbegu za bustani za mbogamboga.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Attachments area

WANAVIJIJI WAMEDHAMIRIA WATOTO WAO WASITEMBEE UMBALI MREFU KWENDA MASOMONI

MIUNDOMBINU inayojengwa  KIGERA SEKONDARI itakayokuwa tayari kupokea WANAFUNZI wa KIDATO cha KWANZA Januari 2021.

Tarehe 18.12.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
KATA ya NYAKATENDE yenye Vijiji 4 (Kakisheri, Kamguruki, Kigera na Nyakatende) inayo SEKONDARI MOJA tu,  NYAKATENDE SEKONDARI ambayo ina MIRUNDIKANO ya WANAFUNZI madarasani. Vilevile, baadhi ya WANAFUNZI wanatembea zaidi ya KILOMITA 10 kwenda masomoni kwenye Sekondari hiyo iliyofunguliwa Mwaka 2006, yenye WANAFUNZI 784 na ina UPUNGUFU wa Vyumba 4 vya Madarasa.
SULUHISHO LA KERO ZA MIRUNDIKANO NA UMBALI MREFU WA KUTEMBEA
VIJIJI 2 vilivyoko mbali na Nyakatende Sekondari VIMEAMUA KUJENGA SEKONDARI yao wenyewe. VIJIJI hivyo ni Kakisheri na Kigera.
MICHANGO YA UJENZI WA SEKONDARI MPYA
MICHANGO ya ujenzi wa Sekondari ya Vijiji hivyo viwili inatolewa na:
*WANAVIJIJI wanachangia NGUVUKAZI zao kwa kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji.
*WANAVIJIJI wanachangia FEDHA taslimu, Shilingi 2,000 kwa kila mwenye umri wa miaka 18 na zaidi.
*WAZALIWA wa Vijiji vya Kakisheri na Kigera WANALIPA GHARAMA za MAFUNDI ujenzi na WANANUNUA  baadhi ya VIFAA vya ujenzi.
*DIWANI wa Kata ya Nyakatende, Mhe Marere John Kisha, ni mmoja wa WAZALIWA wanaochangia ujenzi huu. Vilevile, ameanza kutengeneza MADAWATI 130 ya Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza watakaoanza  MASOMO Januari 2021 kwenye Sekondari hiyo inayoitwa,” KIGERA SECONDARY SCHOOL.”
*MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo AMEISHACHANGIA:
^Saruji Mifuko 150
^Mabati 108
*MFUKO wa JIMBO umeishachangia:
^Saruji  Mifuko 100
MBUNGE wa JIMBO kwa KUSHIRIKIANA na WADAU wengine wa MAENDELEO ataendelea kuchangia ujenzi huu.
MAJENGO YANAYOKAMILISHWA UJENZI
*VYUMBA 2 vya Madarasa vimeishaezekwa na madirisha yamewekwa.
*JENGO la UTAWALA lenye Vyumba (Ofisi 9) limeishaezekwa na madirisha yamewekwa.
*BOMA la CHOO chenye MATUNDU 11 litaezekwa kabla ya tarehe 30.12.2020. Tundu 1 ni kwa Watu wenye ULEMAVU.
*BOMA la MAABARA 2 litaezekwa kabla ya tarehe 30.12.2020
*BOMA la NYUMBA 1 ya MWALIMU litaezekwa kabla ya tarehe 30.12.2020
WANAFUNZI WALIOFAULU
*WANAFUNZI 191 wa Kata ya Nyakatende WAMEFAULU kuendelea na MASOMO ya SEKONDARI.
Kwa hiyo, WANAFUNZI hao 191 watagawanywa kwenye SEKONDARI 2 za Kata, yaani NYAKATENDE SEKONDARI iliyoanza Mwaka 2006, na KIGERA SEKONDARI itakayoanza Januari 2021.
MWENYEKITI wa Serikali ya Kijiji cha Kigera, Ndugu Magafu Katura anatoa MAOMBI ya kuchangiwa SARUJI MIFUKO 300 na RANGI LITA 80 ili kukamilisha Maboma ya Sekondari yao.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

EQUITY BANK YAINGIA MUSOMA VIJIJINI: WAVUVI WAJIUNGA  KWENYE VIKUNDI KUOMBA MIKOPO

UHAMASISHAJI wa uundwaji wa VIKUNDI vya UVUVI ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
Tarehe, 16.12.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
WAVUVI walioko katika Mialo minne ya Busekera (Kata ya Bukumi), Bwai Kumusoma (Kata ya Kiriba) na Visiwa vya Iriga na Rukuba (Kata ya Etaro) wamepokea ELIMU ya kujiunga kwenye VIKUNDI vya UVUVI ili kutekeleza shughuli zao za UVUVI kwa UFANISI mkubwa zaidi, na uwezekano wa kupata MITAJI kupitia MIKOPO mbalimbali.
VIONGOZI wa HALMASHAURI ya WILAYA ya MUSOMA  waliwatembelea WAVUVI wa Kata hizo 3 na kufanya uhamasishwaji huo  kwa muda wa siku mbili mfululizo.
AFISA UVUVI wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Ndugu Augustine Constatine alisisita suala la UVUVI BORA unaozingatia SHERIA na KANUNI zake.
AFISA MAENDELEO ya JAMII wa Halmashauri hiyo, Ndugu Tanna Nyabange na Msaidizi wake Ndugu Nyanjara Majura walielezea umuhimu wa uundwaji wa VIKUNDI vya UVUVI kwa ajili ya kupata na MIKOPO kutoka kwenye HALMASHAURI yao na kutoka kwenye TAASISI za FEDHA, zikiwemo BENKI mbalimbali. Suala la upatikanaji wa SOKO ya UHAKIKA kupitia Vikundi vya Uvuvi lilisisitizwa.
WASAIDIZI 3 wa MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Ndugu Fedson Masawa, Ndugu Verediana Mgoma na Ndugu Hamisa Gamba WALISHIRIAKANA na VIONGOZI wa Halmashauri hiyo kuorodhesha VIKUNDI vya UVUVI vyenye nia ya kuomba MIKOPO  kutoka Equity Bank.
EQUITY BANK NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI
BANK hiyo imewakilishwa na Ndugu Bahati Dollo, Kemilembe Kabugumila na Peter Chuchu, kwenye ZIARA ya KIKAZI ya siku 2 na kuongea na VIKUNDI vya UVUVI vya Kata hizo tatu.
IDADI ya VIKUNDI
vilivyojitokeza kuomba MIKOPO kutoka Bank hiyo ni kama ifuatavyo:
(i) Kata Bukumi (Vijiji 4)
*Vikundi 17, Wanachama 203
(ii) Kata ya Kiriba (Vijiji 3)
*Vikundi 25, Wanachama 327
(iii) Kata ya Etaro (Vijiji 3)
*Kisiwa cha Rukuba
Vikundi 31, Wanachama 425
*Kisiwa cha Iriga
Vikundi 6, Wanachama 80
EQUITY BANK itaanza na VIKUNDI vya UVUVI 79, vyenye WANACHAMA 1,035
LEO, Jumatano, 16.12.2020, MAAFISA 3 wa EQUITY BANK wameonana na Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dr Vicent Naano Anney, na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo KUJADILI FURSA hiyo ya upatikanaji wa MIKOPO ya EQUITY BANK kwa VIKUNDI vya UVUVI vya Jimbo la Musoma Vijijini.
EQUITY BANK iko tayari kutoa MIKOPO kwa VIKUNDI vya UVUVI vya Jimbo la Musoma Vijijini – matayarisho yanaendelea.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

UFUGAJI WA NYUKI WAANZA KUCHANGAMKIWA MUSOMA VIJIJINI

KIKUNDI cha JIPE MOYO cha Kijijini Buanga, Kata ya Rusoli kikiwa kwenye SHAMBA lao lenye MIZINGA ya NYUKI.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
KIKUNDI cha JIPE MOYO cha Kijiji cha Buanga, Kata ya Rusoli kimeanzisha MRADI wa UFUGAJI NYUKI kwa ajili ya kupanua wigo wa shughuli za ki-uchumi za KIKUNDI hicho.
Kikundi hicho kimepata UTAALAMU wa UFUGAJI wa NYUKI kutoka kwenye MAFUNZO waliyopewa na SHIRIKA la SWISSCONTACT.
MWENYEKITI wa Kikundi cha JIPE MOYO, Ndugu Masamaki Girishom, amesema kwamba Kikundi chao kilianzishwa Mwaka 2018 na kina Wanachama 24. Kikundi hiki linashughulisha na KILIMO, na sasa kimeanza KUFUGA NYUKI.
Shirika la SWISSCONTACT limewapatia VIFAA vya awali vya Mradi huu ambavyo ni MIZINGA 10 na VAZI 1 la kuvunia ASALI.
MRATIBU wa Swiss Contact, Ndugu Nelson Bento amesema kwamba hadi sasa, JIMBONI mwetu, kuna VIKUNDI 7 vya UFUGAJI wa NYUKI, na WANAVIJIJI wengi wanaanza kupenda kufuga nyuki kwa ajili ya kuongeza vyanzo vya  mapato yao.
MRATIBU huyo amesema SOKO la ASALI itakayovunwa Vijijini mwetu lipo.
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo anaendelea kuhimiza WANAVIJIJI waanzishe VIKUNDI vya UCHUMI, vikiwemo vya kilimo cha umwagiliaji, uvuvi na ufugaji wa nyuki.
KARIBUNI TUFUGE NYUKI VIJIJINI MWETU
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

MIRADI MINGINE YA RUWASA – KATA ZA SUGUTI NA NYAMBONO ZAKARIBIA KUANZA KUTUMIA MAJI YA ZIWA VICTORIA

MIUNDOMBINU inajengwa kwa ajili ya usambazaji wa MAJI SAFI na SALAMA (maji ya bomba) kwenye KATA za SUGUTI na NYAMBONO.

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
Kata ya SUGUTI ina Vijiji 2 (Suguti na Kusenyi) vyenye ufukwe wa ZIWA VICTORIA, na vingine viwili (Wanyere na Chirorwe) viko mbali na Ziwa hilo.
Kata ya NYAMBONO, yenye Vijiji 2, yaani Nyambono na Saragana iko umbali wa zaidi ya kilomita 10 kutoka Ziwa Victoria.
SERIKALI imetoa Shilingi MILIONI 356  kwa Mradi wa MAJI wa Kata ya Suguti na Shilingi MILIONI 230 kwa Mradi wa  MAJI wa Kata ya Nyambono – hii ni MIRADI mingine ya RUWASA inaotekelezwa ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini kwa Mwaka huu wa Fedha (2020/2021).
MIUNDOMBINU inajengwa kuvuta na kusambaza MAJI kutoka ZIWA VICTORIA (Kijijini Suguti) ambapo PAMPU yenye uwezo wa kusukuma LITA 67,000 kwa saa itajengwa. VIFAA vyote vimeishanunuliwa.
MAJI ya kutoka Kijijini Suguti yatasambazwa kwenye Vijiji vya Kusenyi, Chirorwe na Wanyere (Kata ya Suguti).
TENKI la ujazo wa LITA 200,000 linajengwa Kijijini Chirorwe ambapo MAJI ya Kata ya Nyambono yatachukulia kupitia Mlima Nyabherango. TENKI jingine la ujazo wa LITA 200,000 linajengwa Kijijini Saragana kwa ajili ya MAJI ya Kijiji hicho na cha Nyambono.
Kwa hiyo, RUWASA kwa sasa inakamilisha ujenzi wa MIUNDOMBINU ya kusambaza MAJI SAFI na SALAMA kwenye Kata za SUGUTI na NYAMBONO. Hapo baadae, Kata ya BUGOJI yenye Vijiji 3 (Bugoji, Kaburabura na Kanderema) nayo itafikishiwa MAJI kutoka kwenye TENKI la Kijijini Saragana.
MENEJA wa MRADI huu wa RUWASA, Injinia Mohamed Said Yamlinga amesema kuwa MIRADI ya Kata za Suguti na Nyambono itakamilika Januari 2021.
WANAVIJIJI wa Kata za SUGUTI na NYAMBONO, na VIONGOZI wao, wanaishukuru sana SERIKALI yetu kwa kutoa FEDHA za kutekeleza MIRADI ya kusambaza MAJI ya BOMBA Vijijini mwao.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

RUWASA YAANZA KUTEKELEZA KWA KASI MRADI WA USAMBAZAJI MAJI KWENYE KATA YA NYAKATENDE

UTEKELEZAJI wa MRADI wa RUWASA wa kusambaza MAJI ya ZIWA VICTORIA kwenye Kata ya Nyakatende. 

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
RUWASA imeanza kujenga MIUNDOMBINU ya USAMBAZAJI wa MAJI ya ZIWA VICTORIA kwa Kata ya NYAKATENDE.
Kata ya NYAKATENDE ina Vijiji 4 ambavyo ni Kakisheri, Kamuguruki, Kigera na Nyakatende. Vijiji 2 (Kigera na Kakisheri) viko kwenye mwambao wa ZIWA VICTORIA na ndivyo vitaanza kusambaziwa MAJI ya Mradi huu, baadae Vijiji vya Kamuguruki na Nyakatende vitafuata.
MITAMBO ya kuvuta na kusafisha MAJI ya ZIWA inajengwa kwenye Kitongoji cha Kusenyi, Kijijini Kigera.
Sehemu ya Kijiji cha KURUKEREGE cha Kata jirani ya NYEGINA itapata MAJI ya Mradi huu, na sehemu nyingine ya Kijiji hicho itapewa MAJI ya MRADI wa MUWASA.
MENEJA wa MRADI huu wa RUWASA, Injinia Mohamed Said Yamlinga amesema MIUNDOMBINU inayojengwa kwa sasa ni:
*TENKI la MAJI lenye ujazo wa LITA 300,000 (laki tatu)
*OFISI ya Mradi
*VIOSKI vya kuzuia maji
*Kutandaza MABOMBA kwenye mitaro inayochimbwa.
MENEJA huyo amesema kuwa MRADI huu utakamilika Januari 2021.
WANANCHI na VIONGOZI wao wa Kata ya Nyakatende WANAISHUKURU sana SERIKALI yao kwa kutekeleza AHADI yake ya usambazaji wa MAJI SAFI na SALAMA Vijijini mwao.
Kata za jirani za ETARO, NYEGINA na IFULIFU zitapewa MAJI ya kutoka kwenye Mitambo ya MUWASA iliyoko Bukanga, Musoma Mjini. MRADI umeanza kutekelezwa.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

WANAKIJIJI WAUNGWA MKONO NA SERIKALI KUJENGA NYUMBA ZA WALIMU

ujenzi wa NYUMBA MOJA ya WALIMU (kuanzia msingi hadi nyumba kukamilika) S/M BUIRA ya Kijiji cha Buira, Kata ya Bukumi.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
7.12.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
MWALIMU MKUU wa SHULE ya MSINGI BUIRA, Mwl Yahya Mgika amesema Shule hiyo iliyoanzishwa Mwaka 1992 ina jumla ya WANAFUNZI 747, WALIMU 8, NYUMBA 5 za Walimu, na ina Vyumba 8 vya Madarasa – bado kuna UPUNGUFU wa Vyumba 9 vya Madarasa.
SERIKALI imetoa SHILINGI MILIONI 25 kuchangia ujenzi wa NYUMBA MOJA ya WALIMU kwenye Shule hii. Fedha hizo zimetoka kwenye MRADI wa SERIKALI uitwao, “Primary Education Development Project (PEDP)”.
WANAKIJIJI wa Kijiji cha BUIRA, Kata ya BUKUMI wanaishukuru sana SERIKALI yetu kwa kutoa FEDHA hizo, na wao wamechangia NGUVUKAZI kuhakikisha kwamba gharama za ujenzi wa nyumba hiyo zinapungua – wamejitolea kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji.
MWENYEKITI wa Kijiji cha BUIRA, Ndugu Donald Mafwere ameeleza kwamba, mbali ya MCHANGO wa NGUVUKAZI, Wanakijiji walichangia SARUJI MIFUKO 70, MBAO vipande 101 na MABATI 52 kwenye ujenzi huu.
MWENYEKITI huyo anawashukuru sana WANAKIJIJI hao kwa kuona umuhimu wa KUJITOLEA kwa ajili ya MAENDELEO yao wenyewe wakisaidiana na SERIKALI yetu. Wanavijiji hawa walishajenga NYUMBA 4 za WALIMU wa Shule hiyo.
MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo anapewa SHUKRANI nyingi kwa kuichangia Shule hiyo MADAWATI 60, VITABU zaidi ya 1,000 vya Maktaba, SARUJI MIFUKO 60, na MABATI 54.
VIONGOZI 2 hao, yaani Mwenyekiti wa Kijiji na Mwalimu Mkuu, kwa pamoja wanaomba WADAU wa MAENDELEO wakiwemo WAZALIWA wa Kata ya BUKUMI wajitokeze kuchangia ujenzi wa Vyumba Vipya vya Madarasa, Nyumba Mpya za Walimu na Maktaba – MPANGOKAZI wa ujenzi umeishatayarishwa.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

PROGRAMU YA WAKULIMA KUPUNGUZA MATUMIZI YA JEMBE LA MKONO INAENDELEA MUSOMA VIJIJINI

Kikundi cha Wakulima  wa Kijiji cha Buanga, Kata ya Rusoli, kiitwacho “NGUVUKAZI” kikiwa katika shambalao walilolima kwa kutumia PLAU waliyopewa na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.

Tarehe, 29.11.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo anaendelea KUGAWA bure PLAU (majembe ya kukokotwa na ng’ombe au punda) kwa VIKUNDI vya WAKULIMA wa Jimbo la Musoma Vijijini. MGAO mwingine utakuwa wa ZAWADI ya KRISMASI & MWAKA MPYA utafanyika tarehe 24 Disemba 2020.
Kikundi kiitwacho, “NGUVUKAZI”, cha Kijiji cha Buanga, Kata ya Rusoli ni moja ya VIKUNDI vilivyokwishapewa PLAU na MBEGU kutoka kwa Mbunge huyo.
Kikundi cha NGUVUKAZI kilianzishwa Mwaka 2015 na kina WANACHAMA 30 wanaolima MAZAO ya CHAKULA na BIASHARA. Kikundi hiki kinagawia SHULE za MSINGI Bwenda A&B 50% ya MAVUNO ya Mazao yake ya CHAKULA.
MWENYEKITI wa Kikundi hicho, Ndugu Tore Masamaki anasema MISAADA ya NYEZO zao za Kilimo imetolewa na PCI (Tanzania) na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo.
PCI (Tanzania) imewapatiwa MASHINE ya UMWAGILIAJI, MBEGU za Viazi Lishe, Mahindi na Alizeti.
Mbunge Prof Muhongo amewapatia PLAU 1 na MBEGU za Mihogo, Mtama, Ufuta na Alizeti
Vilevile, kwa Kata ya Rusoli, Mbunge huyo aligawa PLAU 1 kwa Kikundi kingine kiitwacho “MKULIMA JEMBE”.
Ndugu Anna Masange, MWANAKIKUNDI cha NGUVUKAZI amesema kwamba ameweza kujenga NYUMBA, ANASOMESHA WATOTO wake na kufungua BIASHARA ya DUKA dogo kutokana na MAPATO ya Kilimo cha Kikundi chao. Kwa hiyo, anawashawishi WANAWAKE na VIJANA wajiunge kwenye VIKUNDI vya KILIMO vina manufaa sana.
AFISA KILIMO wa Kata ya Rusoli, Ndugu Gervas Ngova. amesema WANAVIJIJI wa Kata hiyo wamechangamkia fursa za kuanzisha VIKUNDI vya KILIMO kwani vinawarahisishia kupata MAFUNZO na MISAADA ya Kilimo kutoka kwa WADAU wa MAENDELEO ikiwemo SERIKALI yetu.
Vilevile, hapo shambani, Afisa Kilimo wa Kata hiyo anatoa MAELEKEZO ya Kilimo bora kwa Kikundi cha “NGUVUKAZI”.
KILIMO NI UHAI
KILIMO NI AJIRA
KILIMO NI UCHUMI
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

CRDB YAUNGANA NA WANAKIJIJI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA SHULE YA MSINGI ILIYOFUNGULIWA MWAKA 1956

Baadhi ya MAJENGO yaliyokamilika ujenzi na MADARASA ya S/M MURUNYIGO ya Kijiji cha Kiemba, Kata ya Ifulifu.

Tarehe, 27.11.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
SHULE ya MSINGI MURUNYIGO ya Kijiji cha Kiemba, Kata ya Ifulifu ilianza kutoa ELIMU Mwaka 1956.
SHULE hii ina WANAFUNZI 949 na WALIMU 12. IDADI ya WANAFUNZI kwenye chumba kimoja cha DARASA ni kati ya 80 na 152. Kwa hiyo, MIRUNDIKANO Madarasani ipo!
AFISA MTENDAJI (VEO) wa Kijiji cha Kiemba. Ndugu Regina Chirabo amesema kuwa UBORESHAJI wa MIUNDOMBINU ya S/M MURUNYIGO umefanywa na:
*WANAKIJIJI:
Wamechangia NGUVUKAZI kwa kusomba mawe, mchanga, maji na FEDHA taslimu 2,200,000/= za malipo ya Fundi.
*BENKI YA CRDB
Imechangia Saruji Mifuko 60, Rangi Lita 40, Vifaa vya Mlango 1 na Dirisha 1 – SHUKRANI nyingi sana kwa CRDB.
*PCI (TANZANIA)
Imefadhili ujenzi wa Choo chenye Matundu 10 (Wasichana 5 na Wavulana 5 – kwenye picha zilizoko hapa utaona Jengo la rangi ya “light blue”) – SHUKRANI nyingi sana kwa PCI (Tanzania).
*MBUNGE WA JIMBO
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo amechangia Saruji Mifuko 60 na Mabati 54.
MICHANGO mingine ya MBUNGE huyo kwenye Shule hiyo ni pamoja na: Madawati 150 na Vitabu vya Maktaba zaidi ya 1,000 (elfu moja).
MWALIMU MKUU huyo amesema Jumla vya Vyumba vya Madarasa vinavyohitajika ni 18 na vilivyopo ni 9 tu!Mbali ya UPUNGUFU mkubwa huo WANAFUNZI 59 kati ya 64 wamefaulu kujiunga MASOMO ya KIDATO I mwakani!
MWALIMU MKUU huyo anaendelea KUTOA OMBI kwa WADAU wa MAENDELEO kujitokeza na KUCHANGIA uboreshaji na ujenzi wa MIUNDOMBINU kwenye Shule kongwe ya Msingi ya Kijiji cha Kiemba, S/M MURUNYIGO.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

WANAVIJIJI WASHIRIKIANA NA SERIKALI KUJENGA KITUO CHA AFYA CHA KATA YA BUGWEMA

baadhi ya MAJENGO yanayojengwa kwenye Mradi wa kupanua ZAHANATI ya KIJIJI cha Masinono kuwa KITUO cha AFYA cha KATA ya Bugwema.

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
Alhamisi, 26.11.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
SERIKALI imetoa TSH MILIONI 400 kupanua ZAHANATI ya Kijiji cha MASINONO iwe KITUO cha AFYA cha Kata ya BUGWEMA.
Kata ya BUGWEMA inaundwa na Vijiji vinne (4) ambavyo ni: Bugwema, Kinyang’erere, Masinono na Muhoji.  Vijiji vyote hivi vinatumia ZAHANATI moja (1) tu ya Kijijini Masinono.
UPANUZI WA ZAHANATI KUWA KITUO CHA AFYA
Michango ya ujenzi inatolewa na:
*SERIKALI:
Tsh Milioni 400 – SHUKRANI nyingi sana zinatolewa kwa Serikali yetu.
*WANAVIJIJI:
Wanavijiji kutoka Vijiji vyote 4 na Viongozi wao wa Vijiji na Vitongoji wanachangia NGUVUKAZI zao kwa kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji. Vilevile, wanachangia FEDHA taslimu.
*VIONGOZI wa KATA:
Diwani Mteule, Mhe Clifford Machumu na Diwani aliyemaliza muda wake, Mhe Ernest Maghembe wanaendelea kuchangia FEDHA taslimu na USAFIRI kwenye ujenzi huu.
*MBUNGE WA JIMBO:
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo, amechangia leo SARUJI MIFUKO 100  bado ataongezea Saruji Mifuko 300 kukamilisha AHADI yake.
MICHANGO mingine  ya Mbunge wa Jimbo kwenye ZAHANATI ya Masonono ni kama ifuatavyo:
(i) Gari 1 la Wagonjwa (Ambulance).
(ii) Nondo, Wavu na Masinki kwa ajili ya ukarabati wa choo cha Zahanati ya Masinono
MSIMAMIZI MKUU wa Mradi huu, Injinia Mrisho Shomari amesema, hadi sasa Mradi huo umetekelezwa kwa Asilimia 75 (75%) na kufikia mwishoni mwa mwezi Disemba, 2020  ujenzi utakuwa umekamilika kwa Asilimia 100 (100%).
Injinia Mrisho ametaja majengo ya KITUO hiki cha AFYA kuwa ni:
(i) Wodi ya Mama na Mtoto
(ii) Maabara
(iii) Jengo la Upasuaji
(iv) Jengo la Kufulia
(v) Jengo la Maiti (mortuary)
(vi) Vyoo vya nje, na
(vii) Miundombinu ya kutolea uchafu.
MGANGA MFAWIDHI wa Zahanati ya Masinono, Ndugu Mzalendo Wambura amewaomba WADAU wa MAENDELEO wakiwemo WAZALIWA wa KATA ya BUGWEMA kuwaunga mkono Wananchi wa Kata ya Bugwema na Serikali ili kukamilisha Mradi huu mapema iwezekanavyo.
MIUNDOMBINU YA HUDUMA ZA AFYA NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI
*Zahanati 24 za Serikali
*Zahanati 4 za Binafsi
*Zahanati Mpya 14 zinajengwa
*Vituo vya Afya 2
(Murangi & Mugango)
*Hospitali ya Wilaya inajengwa Kijijini Suguti
*VITENDO KWANZA
*MAENDELEO KWANZA
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

SERIKALI YATOA SHILINGI MILIONI 50 ZA KUUNGA MKONO JITIHADA ZA WANAVIJIJI ZA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA SEKONDARI YAO YA KATA

baadhi ya WANAVIJIJI wa Kata ya Kiriba na MAFUNDI wao wakiwa kwenye ujenzi wa JENGO la UTAWALA la Kiriba Sekondari.

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
23.11.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
JIMBO la Musoma Vijijini lenye Kata 21 na Vijiji 68 lina jumla ya SEKONDARI 20 za KATA, na SEKONDARI MPYA 5 za Kata zinatarajiwa kufunguliwa Januari 2021. Vilevile, Jimbo lina SEKONDARI 2 za BINAFSI za Madhehebu ya Dini.
KATA 5 – Etaro, Makojo, Mugango, Suguti na Tegeruka zimepanga kuanza kujenga SEKONDARI ya PILI ya Kata zao.
KIRIBA SEKONDARI:
VIJIJI 3 vya Kata ya KIRIBA ambavyo ni Bwai Kumusoma (Paris), Bwai Kwitururu (London) na Kiriba VIMEAMUA KUJITOLEA kuboresha MIUNDOMBINU ya Sekondari yao, KIRIBA SEKONDARI.
UBORESHAJI uko kwenye ujenzi wa MAABARA 3, MABWENI 2, JENGO la UTAWALA na NYUMBA za WALIMU.
SHILINGI MILIONI 50 ZA SERIKALI:
SERIKALI yetu inapewa SHUKRANI nyingi kwa kutoa Shilingi MILIONI 50 kuchangia ujenzi wa JENGO la UTAWALA la Sekondari hiyo.
WANAVIJIJI kutoka Vijiji 3 vya Kata hiyo wanachangia NGUVUKAZI kwa kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji. Hayo yamesemwa na Mwalimu Mkuu wa Sekondari hii, Mwl Paul Mtani.
DIWANI MTEULE wa Kata ya Kiriba, Mhe Hamisi Saire ametoa SHUKRANI nyingi kwa SERIKALI na kwa MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo kwa MICHANGO yao MINGI ya kuboresha MIUNDOMBIMU ya ELIMU ndani ya Kata yao.
MBUNGE huyo wa Jimbo la Musoma Vijijini alishachangia KIRIBA SEKONDARI jumla ya Saruji Mifuko 175, Rangi na Vitabu 1,000 vya Maktaba.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

SHULE ZA MSINGI ZA MUSOMA VIJIJINI ZAENDELEA KUJENGA NA KUTUMIA MAKTABA

WANAFUNZI wakijipatia vitabu ndani ya MAKTABA yao.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
Jumamosi, 21.11.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
SHULE YA MSINGI BUTATA, iliyoko Kijijini Butata, Kata ya Bukima imejenga MAKTABA MPYA kwa muda wa MIEZI 8 na tayari inatumika.
MWALIMU MKUU,  Mwl Nancy Lema amesema Shule hiyo iliyoanza Mwaka 1942, ina furaha nyingi sana ya KUPATA MAKTABA ambayo inatumiwa na WANAFUNZI wa Madarasa yote kujisomea na hasa kufanya kazi za ziada walizopewa na Walimu wao (homeworks)
MICHANGO YA UJENZI WA MAKTABA
Mwalimu Yohana Dawi, Mwalimu wa MIUNDOMBINU, aliyesimamia ujenzi wa Maktaba hii amesema MICHAGO ilitoka kwa:
*WAKIJIJI wa Kijiji cha Butata walichangia NGUVUKAZI – kusomba mawe, mchanga na maji.
* PCI (Tanzania) inapewa shukrani nyingi sana kwa kutoa Vifaa vingi vya ujenzi wa Maktaba  hii. MEZA, VITI na SHUBAKA vimetolewa na PCI (Tanzania)
* MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo alichangia Shule hii  SARUJI MIFUKO 100 (50 Maktaba & 50 Vyumba vipya vya Madarasa)
* WAZALIWA 2 wa Kijiji cha Butata, Ndugu Samson Masawa (Tsh 500,000) na Masawa Masawa (Tsh 500,000) walichangia
VITABU VYA MAKTABA
Mwl Yohana Dawi amesema VITABU vya MAKTABA hiyo vimetolewa na:
* PCI (Tanzania)
* MBUNGE wa Jimbo , Prof Sospeter Muhongo
WATUMIAJI WENGINE WA MAKTABA HII
Mbali ya WANAFUNZI wa S/M Butata, WANAFUNZI wa SHULE za MSINGI na SEKONDARI jirani, na WANANCHI wa Kata ya Bukima na wengine wote WANAKARIBISHWA kutumia MAKTABA ya S/M BUTATA – Karibuni Mjisomee!
JIMBO LA Musoma Vijijini lenye Kata 21, Vijiji 68 na Vitongoji 374 lina jumla ya SHULE za MSINGI 111 (za Serikali), 3 (za Binafsi) na linajenga Shule Mpya 14 za Msingi.
*ELIMU NI INJINI YA MAENDELEO*
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

KAMPENI YA UHIMILISHAJI (ARTIFICIAL INSEMINATION) YAZINDULIWA MUSOMA VIJIJINI

matukio mbalimbali ya UZINDUZI wa UHIMILISHAJI wa ng’ombe wa kienyeji uliofanyika Kijijini Bugwema tarehe 18.11.2020.

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
Tarehe, 18.11.2020
KATIBU MKUU wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Idara ya MIFUGO, Prof Elisante Ole Gabliel amezindua Kampeini ya UHIMILISHAJI wa NG’OMBE (Artificial  Insemination) kwa WAFUGAJI wa Musoma Vijijini.
Tukio hilo lililofanyika Kijijini Bugwema, lilihudhuriwa na WAFUGAJI na VIONGOZI mbalimbali wakiwemo Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dr Vincent Naano Anney, Madiwani Wateule na Wasaidizi wa Mbunge. WANANCHI wasio Wafugaji nao walihudhuria uzinduzi huo.
Prof Elisante ole Gabriel alieleza kwamba LENGO KUU la UHIMILISHAJI ni UPANDIKIZAJI wa MIMBA kwenye NG’OMBE (wakiwemo wa kienyeji) kwa kuweka MBEGU ya NG’OMBE wa KISASA kwa njia ya MRIJA ili kuongeza UBORA na WINGI wa MIFUGO (ng’ombe) hiyo.
KATIBU MKUU huyo alisisitiza kuwa MIFUGO ni UTAJIRI, na kwamba WAFUGAJI wanapaswa kuwa tayari kutoa USHIRIKIANO mkubwa kwa WIZARA ili kuanzisha Miradi ya UFUGAJI wa KISASA wenye NG’OMBE BORA (maziwa mengi, nyama laini, ngozi nzuri, n.k.).
WAFUGAJI wa Kata ya Bugwema, kwa niaba ya Wafugaji wa Musoma Vijijini, wameishukuru sana SERIKALI kwa kuwasogezea huduma hiyo ya UHIMILISHAJI na wameahidi kutoa USHIRIKIANO mkubwa wa kuboresha UFUGAJI wao kwa njia hii ya UHIMILISHAJI wa ng’ombe wa kienyeji.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

KIGERA SEKONDARI KUFUNGULIWA JANUARI 2021 – SEKONDARI YA PILI YA KATA

baadhi ya MABOMA ya KIGERA SEKONDARI itakayofunguliwa Januari 2021 – KARIBU UCHANGIE ujenzi huu.

Kata ya Nyakatende yenye Vijiji 4 ina Sekondari 1 ambayo imeelemewa na wingi wa Wanafunzi na baadhi yao wanatembea umbali mrefu (zaidi ya kilomita 5) kwenda masomoni.

Vijiji 2 vya KIGERA na KAKISHERI vimeamua kujenga SEKONDARI yao (KIGERA SEKONDARI) kwani WATOTO wao ndio wanatembea umbali mrefu kwenda NYAKATENDE SEKONDARI.

MICHANGO YA UJENZI ILIYOKWISHATOLEWA

*NGUVUKAZI za Wakazi wa Vijiji vya Kigera na Kakisheri (kusomba maji, mchanga, mawe na kokoto)

*MICHANGO ya FEDHA taslimu ya awali: Shilingi 2,000 kwa kila mkazi (vijiji 2) mwenye umri kati ya miaka 18 na 59.

*WAZALIWA wa Vijiji 2 wanawalipa MAFUNDI na fedha nyingine zinanunua vifaa vya ujenzi.

*SARUJI MIFUKO 150 ya Mbunge wa Jimbo, Profesa Muhongo*

*SARUJI MIFUKO 100 ya Mfuko wa Jimbo*

MAJENGO YANAYOHITAJIKA KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA (2021)

*Maoteo ya Wanafunzi wa Kata ya Nyakatende watakaojiunga na Kidato I ni 190.

*Maoteo ya Wanafunzi watakaojiunga na Kidato I KIGERA SEKONDARI ni 120.

*Maoteo ya Wanafunzi wa Kidato I watakaoenda NYAKATENDE SEKONDARI ni 70.

MICHANGO MINGINE YA MBUNGE WA JIMBO NA DIWANI MTEULE

*Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo atachangia MABATI 108 (bando 9, geji 28)

*Diwani Mteule, Mhe Marere John Kisha atatengeneza MADAWATI 120 ya Wanafunzi wa Kidato I.

*ELIMU KWANZA*

Jimbo la Musoma Vijijini lenye KATA 21, lina:

*Sekondari 20 za Kata/Serikali

*Sekondari 2 za Binafsi

*Sekondari Mpya 5 zinazotarajiwa kufunguliwa Januari 2021 (Bukwaya, Kigera, Nyasaungu, Ifulifu na Seka)

*Sekondari Mpya 5 zitakazoanza kujengwa mwakani (2021) za Kata za: Etaro, Makojo, Mugango, Suguti na Tegeruka.

*HIGH SCHOOLS zitaongezeka kutoka 2 (1 Serikali & 1 Binafsi) hadi 6 ndani ya miaka 5.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

MICHANGO INAHITAJIKA ILI SEKA SEKONDARI IFUNGULIWE JANUARI 2021

Baadhi ya MABOMA ya SEKA SEKONDARI yanayopaswa kukamilishwa kabla ya tarehe 30.12.2020 – UNAKARIBISHWA SANA UCHANGIE ujenzi huu

KATA ya NYAMRANDIRIRA ina Vijiji 5 (Chumwi, Kaboni, Kasoma, Mikuyu na Seka) na Sekondari moja, KASOMA SEKONDARI. Sekondari hii imeelemewa na WINGI wa WANAFUNZI wa kutoka Vijiji 5 WANAORUNDIKANA madarasani.

Baadhi ya Wanafunzi hao wanatembea UMBALI MREFU wa zaidi ya kilomita 10 kwenda masomoni kwenye Sekondari hiyo.

SULUHISHO: kujenga Sekondari ya pili ya Kata hiyo. Ujenzi umeanza na lengo kuu ni kuifungua mwakani (Januari 2021).

MAJENGO YANAYOJENGWA KWA SASA

* Vyumba 8 vya Madarasa
* Jengo la Utawala
* Vyoo vya Wanafunzi & Walimu
* Maabara
* Maktaba
* Nyumba za Walimu

MAJENGO YANAYOHITAJIKA KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA MWAKANI

IDADI YA WANAFUNZI:

* Maoteo: Wanafunzi 250 wa Kata ya Nyamrandirira watafaulu kujiunga na Kidato I mwakani, Januari 2021

* Maoteo: Wanafunzi 100 watajiunga na SEKA SEKONDARI

* Wanafunzi 150 watajiunga na KASOMA SEKONDARI

MAJENGO YANAYOPASWA KUKAMILISHWA KABLA YA TAREHE 30 DISEMBA 2020:

(1) Vyumba 3 vya Madarasa
(2) Ofisi 1 ya Walimu
(3) Choo chenye Matundu 8

WANAOCHANGIA UJENZI HUU (hadi leo hii):

(1) Wanavijiji wa Vijiji 5
(2) Viongozi wa Vijiji/Kata
(3) Mgodi Mdogo wa Dhahabu wa Seka
(4) Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo (alishachangia Saruji Mifuko 150)

MABATI 54:
Tarehe 24.11.2020, Mbunge wa Jimbo, Prof S Muhongo atachangia MABATI 54 ya kuezeka Chumba 1 cha Darasa.

WAZALIWA WA KATA YA NYAMRANDIRIRA:
* Wanavijiji bado wanasubiri kwa shauku kubwa AHADI za MICHANGO ya WAZALIWA (na marafiki zao) wa Kata hiyo.

MICHANGO IPELEKWE kwa:
* Mtendaji: 0756 680 887
* DC wa Wilaya ya Musoma
* Mkurugenzi wa Halmashauri (Musoma DC)

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

KAMPENI ZA CCM – PROF MUHONGO ARUDI VIJIJINI KUSISITIZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO YA CHAGUO LAO 

Jumamosi, 24.10.2020, MGOMBEA UBUNGE wa CCM wa Jimbo la Musoma Vijijini, PROF MUHONGO amerudi kwenye Kata ya MAKOJO na kupiga KAMPENI kwenye Vijiji vya CHITARE na CHIMATI.
UTEKELEZAJI WA ILANI MPYA YA CCM (2020-2025) NDANI YA KATA YA MAKOJO
(1) MAJI VIJIJINI
* Miradi wa MAJI kutoka ZIWA VICTORIA unatekelezwa ndani ya Kata hii – kukamilisha Mradi wa Bomba la Maji la Chitare-Makojo na baadae kusambaza Maji ya Bomba hili hadi Kijiji cha Chimati
(2) UMEME VIJIJINI
*Vijiji vyote 3 vya Kata hii (Chimati, Chitare & Makojo) vinayo MIUNDOMBINU ya usambazaji wa UMEME, na baadhi ya Vitongoji vyake tayari vimepewa UMEME wa REA. Vitongoji vilivyosalia vitapewa UMEME, kama ilivyoelezwa ndani ya ILANI ya UCHAGUZI ya CCM (2020-2025)
VIPAUMBELE VYA KILA KIJIJI
(1) KIJIJI CHA CHIMATI
*Kukamilisha ujenzi wa ZAHANATI ya Kijiji chao
*Kujenga SEKONDARI ya Kijiji chao kwani SEKONDARI ya Kata iko mbali Kijijini Makojo.
(2) KIJIJI CHA CHITARE
*Kujenga SEKONDARI ya Kijiji chao kwani SEKONDARI ya Kata iko mbali Kijijini Makojo
*WADI ya MAMA & MTOTO kujengwa kwenye ZAHANATI yao
(3) KIJIJI CHA MAKOJO
*Kujenga ZAHANATI ya Kijiji chao
*VITENDO KWANZA
*MAENDELEO KWANZA
KATA YA MAKOJO imeahidi KUTOA KURA ZOTE kwa CCM – sababu – ILANI ya UCHAGUZI ya CCM (2020-2025) ina VIPAUMBELE vya MIRADI ya MAENDELEO yao
VIAMBATANISHO – Matukio ya leo ya KAMPENI za CCM kwenye Kijiji cha Chimati, Kata ya Makojo
“TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE PAMOJA”
Sospeter Muhongo
Jimbo la Musoma Vijijini
24.10.2020

WANAVIJIJI WA KATA YA NYEGINA WAAINISHA VIPAUMBELE VYAO VYA UTEKELEZAJI WA ILANI MPYA YA CCM

MIKUTANO ya KAMPENI za CCM ndani ya Kata ya Nyegina.

Alhamisi, 15.10.2020, MGOMBEA UBUNGE wa CCM wa Jimbo la Musoma Vijijini, PROF MUHONGO, amefanya MIKUTANO 3 ya KAMPENI za CCM ndani ya Kata ya Nyegina.
MIKUTANO 3 imefanywa kwenye VIJIJI vya Kurukerege, Nyegina na Mkirira.
WANAVIJIJI wa Kata hii wamesema KURA ZOTE watazipeleka CCM kwenye nafasi ya URAIS, UBUNGE na UDIWANI.
WANAVIJIJI wameamua hivyo baada ya kuvutiwa na ILANI MPYA YA CCM ya 2020-2025 na VIPAUMBELE vyao vya MAENDELEO vimo ndani ya ILANI hii.
*VITENDO KWANZA
*MAENDELEO KWANZA
VIPAUMBELE VYA KIJIJI CHA KURUKEREGE
* Kukamilisha ujenzi wa ZAHANATI ya Kijiji chao
* Kukamilisha ujenzi wa Vyumba Vipya vya Madarasa vya SHULE ya MSINGI BUKWAYA ambayo ni mpya yenye Madarasa 5.
VIPAUMBELE VYA KIJIJI CHA NYEGINA
* Kukamilisha WODI ya Mama & Mtoto inayojengwa kwenye ZAHANATI ya Nyegina.
VIPAUMBELE VYA KIJIJI CHA MKIRIRA
* Kukamilisha ZAHANATI ya Kijiji chao
VIPAUMBELE VYA KATA (Vijiji vyote 3)
* ELIMU: Kukamilisha ujenzi wa SEKONDARI ya PILI (Bukwaya Secondary School) itakayofunguliwa Januari 2021. Inajengwa Kijijini Nyegina
* MAJI VIJIJINI: Kata iko kwenye MIRADI 2 ya MAJI kutoka Ziwa Victoria –
(i) MAJI ya MUWASA
Maji ya Mji wa Musoma YAMEANZA kusambazwa kwenye VIJIJI jirani na Mji huo vikiwemo VIJIJI vyote vya Kata za Etaro, Nyegina, Nyakatende na Ifulifu.
(ii) MRADI wa MAZIWA MAKUU
* Vijiji vyote 3 vya Kata hii ni miongoni mwa VIJIJI 33 vya Jimboni mwetu vilivyoko kwenye Mradi huu.
* UMEME VIJIJINI: Baadhi ya Vitongoji vya Vijiji vyote 3 vimeishapatiwa umeme na USAMBAZAJI unaendelea hadi kukamilisha upelekaji wa UMEME kwenye Vitongoji vyote.
UTAMADUNI, MICHEZO NA SANAA
* ILANI mpya ya CCM ya 2020-2025 inaeleza umuhimu wa Utamaduni, Michezo na Sanaa kwa TAIFA letu
*Jimbo letu LINAENDELEA kustawisha ukuaji na uimarikaji wa KWAYA na  NGOMA zetu za ASILI.
MICHANGO ya PROF MUHONGO kwenye MIRADI yote ya MAENDELEO ya Kata hii inatambuliwa na kutolewa shukrani nyingi.
“TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE PAMOJA”
Sospeter Muhongo
Jimbo la Musoma Vijijini
15 Oktoba 2020

MIRADI YA MAENDELEO YAING’ARISHA CCM NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

WanaMusoma Vijijini wakisikiliza kwa makini Katika mkutano mmojawapo wa Kampeni.

MALENGO ya KAMPENI za CCM ndani ya Vijiji 68 vya Jimbo la Musoma Vijijini ni MAENDELEO (kwa ujumla wake) & USTAWI wa JAMII. Hivyo, USHINDI wa kishindo kizito.
WANANCHI wa kila KIJIJI na kila KATA, kwa kutumia ILANI ya UCHAGUZI ya CCM (2020-2025), wanabainisha VIPAUMBELE vyake vya MIRADI ya MAENDELEO.
KATA YA BUSAMBARA
Kata hii ina VIJIJI 3 (Kwikuba, Maneke na Mwiringo) na VIPAUMBELE vyake ni:
(1) ELIMU & MAFUNZO
Kata ya Busambara inayo SEKONDARI MPYA (Busambara Secondary School) iliyofunguliwa Januari 2020.
Ujenzi wa Vyumba vipya vya Madarasa, Maabara, Maktaba, Nyumba za Walimu, n.k. unaendelea.
MICHANGO ya ujenzi wa SEKONDARI hii inatolewa na WANANCHI, SERIKALI, PROF MUHONGO na WAZALIWA wa Kata hii.
(2) MAJI VIJIJINI
 MIRADI 2 ya MAJI ya kutoka Ziwa Victoria itatekelezwa ndani ya Kata hii:
 (i) Vijiji vyote vitatu vimo ndani ya Mradi wa Maziwa Makuu
(ii) Vijiji vyote vitatu vimo ndani ya Mradi wa Mugango-Kiabakari- Butiama.
(3) UMEME VIJIJINI
Vijiji vyote vitatu vinayo miundombinu ya umeme na baadhi ya Vitongoji vimeishapatiwa umeme. Vitongoji vilivyosalia navyo vitapewa umeme kama inavyoelezwa ndani ya ILANI ya CCM ya 2020-2025
KIJIJI CHA MWIRINGO
* Kukamilisha ujenzi wa SHULE SHIKIZI iliyoko Kitongoji cha Ziwa. Shule itapanuliwa hadi  kufikia Darasa la VII (Shule ya Msingi kamili).
KIJIJI CHA KWIKUBA
* Nyumba za Wafanyakazi wa ZAHANATI yao.
KIJIJI CHA MANEKE
* Kukamilisha ujenzi wa ZAHANATI ya Kijiji chao
UTEKELEZAJI wa MIRADI hiyo hapo juu unaanza tarehe 1.11.2020
WANANCHI wa Kata ya BUSAMBARA wanasema KURA ZOTE watapewa WAGOMBEA WATATU wa CCM (Urais, Ubunge na Udiwani)
*VITENDO KWANZA
*MAENDELEO KWANZA
VIAMBATANISHO (Picha hapo juu) ni Kampeni za CCM ndani ya Kata ya Usambara.
“TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE PAMOJA”
Sospeter Muhongo
Jimbo la Musoma Vijijini
14.10.2020

KAMPENI ZA CCM NI ZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO: KATA YA NYAKATENDE INAYO MIRADI 5 YA KIPAUMBELE

Jumatatu, 12.10.2020 MGOMBEA UBUNGE wa CCM wa Jimbo la Musoma Vijijini, PROF MUHONGO amefanya KAMPENI 3 na kukamilisha UOMBAJI wa KURA kwenye VIJIJI vyote 4 vya Kata ya Nyakatende (Kakisheri, Kamuguruki, Kigera na Nyakatende).
MIRADI yote ya KIPAUMBELE ya Kata ya Nyakatende CHIMBUKO LAKE ni ILANI za CCM za 2015-2020 na 2020-2025
(1) MAJI VIJIJINI
*Vijiji vyote 4 vya Kata hii vitapata MAJI kutoka Ziwa Victoria. Ipo MIRADI 3 ya Ziwa Victoria na unaotekelezwa SASA HIVI ni wa MAJI kutoka MUWASA (Maji ya Mji wa Musoma). SERIKALI ya CCM inatekeleza AHADI yake ya kusambaza MAJI VIJIJINI.
(2) UMEME VIJIJINI
* Vijiji vyote 4 vinayo Miundombinu ya kuendelea na usambazaji wa UMEME VIJIJINI kwenye Vitongoji vilivyosalia.
MIRADI INAYOHITAJI MICHANGO YA WANANCHI & KUTOKA SERIKALINI
(3) ELIMU & MAFUNZO
* SEKONDARI ya PILI (Kigera Secondary School) inajengwa na Vijiji 2 itafunguliwa JANUARI 2021. MICHANGO inatoka kwa Wanavijiji, Wazaliwa wa Vijiji 2 (Kakisheri & Kigera) na Prof Muhongo.
* SHULE SHIKIZI KIHUNDA inajengwa Kijijini Kamuguruki kwa kutumia MICHANGO ya Wananchi na Prof Muhongo
(4) HUDUMA ZA AFYA
* ZAHANATI mpya ya Kijiji cha Kakisheri tayari imeanza kujengwa
* ZAHANATI mpya ya Kijiji cha Kamuguruki itaanza kujengwa baada ya tarehe 28.10.2020
* KITUO cha AFYA cha Kata ya Nyakatende kitajengwa Kijijini Kigera.
KAMPEZI za CCM ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini ni KAMPENI za UTEKELEZAJI wa ILANI MPYA ya CCM ya 2020-2025
WAPIGA KURA WA KATA YA NYAKATENDE wanasema:
*Dkt Magufuli: 100%
*Prof Muhongo: 100%
*Ndugu Kishe: 100%
“TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE PAMOJA”
Picha hapo juu ni moja kati ya MATUKIO mbalimbali ya KAMPENI 3 za leo za CCM ndani ya Kata ya Nyakatende
*VITENDO KWANZA
* MAENDELEO KWANZA
Sospeter Muhongo
Jimbo la Musoma Vijijini
12 Oktoba 2020

KISIWA CHA RUKUBA CHAIKUBALI ILANI MPYA YA CCM NA KUAMUA KUJENGA KITUO CHA AFYA

Kisiwa cha RUKUBA kiko ndani ya Kata ya ETARO yenye VIJIJI 4 (Busamba, Etaro, Mmahare na Rukuba).
Leo, Jumapili, 11.10.2020 MGOMBEA UBUNGE wa CCM wa Jimbo la Musoma Vijijini, PROF MUHONGO, alifanya MIKUTANO 4 ya KAMPENI za CCM ndani ya Kata hiyo – akianzia Kisiwani RUKUBA.
VIPAUMBELE VIKUU VYA UTEKELEZAJI WA ILANI MPYA YA CCM NDANI YA KATA YA ETARO
(1) MAJI SAFI & SALAMA
* Vijiji vya Mmahare, Etaro na Busamba vinasambaziwa MAJI ya MUWASA (Maji ya Mji wa Musoma kutoka Ziwa Victoria) na tayari uchimbaji wa mitaro na utandikaji wa mabomba umeanza. SERIKALI ya CCM inatekeleza AHADI yake ya USAMBAZAJI wa MAJI VIJIJINI.
* Kisiwa cha RUKUBA kiko kwenye Mradi wa Maziwa Makuu – kutumia Maji ya Ziwa Victoria.
(2) UMEME VIJIJINI
* Kisiwa cha RUKUBA kimeanza kutumia UMEME wa JUA (solar)
* VITONGOJI vya Vijiji 3 vilivyosalia vitapewa UMEME wa REA kama ilivyoainishwa ndani ya ILANI MPYA ya CCM ya 2020-2025.
(3) ELIMU & MAFUNZO
* Kata ya ETARO inayo SEKONDARI MOJA inayotumiwa na Vijiji 4. Haitoshi! SEKONDARI ya PILI ya Kata hiyo itajengwa Kijijini Busamba.
(4) HUDUMA ZA AFYA
* Kisiwa cha RUKUBA kitapanua ZAHANATI yake na kuwa KITUO cha AFYA. WODI ya MAMA & MTOTO inayojengwa Kisiwani hapo kwa kutumia MICHANGO ya WANANCHI & PROF MUHONGO, litakuwa (WODI) sehemu ya KITUO cha AFYA hicho.
* Kijiji cha MMAHARE kitakamilisha ujenzi wa ZAHANATI ya Kijiji chake. WADAU wengi wa MAENDELEO, akiwemo PROF MUHONGO, wanachangia ujenzi wa ZAHANATI hii.
KURA ZA KATA YA ETARO – Wananchi wanasema:
* Dkt Magufuli: 100%
* Prof Muhongo:100%
* Ndg Kigwa: 100%
VIAMBATANISHO vya hapa: matukio mbalimbali ya KAMPENI za CCM ndani ya Kata ya ETARO
“TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE PAMOJA”
Sospeter Muhongo
Jimbo la Musoma Vijijini
11 Oktoba 2020

ILANI MPYA YA CCM IMEBEBA VIPAUMBELE VYA MAENDELEO YA KATA YA TEGERUKA

Tarehe 9.10.2020, MGOMBEA UBUNGE wa CCM wa Jimbo la Musoma Vijijini, PROF MUHONGO, alikuwa na MIKUTANO ya KAMPENI kwenye VIJIJI 2 (Mayani & Tegeruka) vya Kata ya TEGERUKA. Hapo awali alishafanya MKUTANO wa KAMPENI kwenye KIJIJI cha Kataryo.
VIPAUMBELE vya MAENDELEO ya Vijiji hivyo 3 vya Kata hiyo vimo kwenye ILANI MPYA ya UCHAGUZI ya CCM ya 2020-2025. Kwa hiyo, UTEKELEZAJI unaanza mara moja baada ya UCHAGUZI wa tarehe 28.10.2020.
MAJI KWA VIJIJI VYOTE VYA KATA YA TEGERUKA
* SERIKALI ya CCM inao MRADI wa Tsh BILIONI 70 wa MAJI ya BOMBA ya Ziwa Victoria – Mugango – Kiabakari – Butiama. VIJIJI vyote 3 vya Kata ya TEGERUKA nitapata MAJI kutoka kwenye Bomba hili.
* FEDHA za MRADI huu zimetolewa na Serikali ya Saudi Arabia, BADEA (Khartoum, Sudan) na Serikali yetu. Mradi utaanza Januari 2021 au kabla.
UMEME KWA VIJIJI VYOTE VYA KATA YA TEGERUKA
* Kwa kuwa UMEME tayari unatumiwa na baadhi ya WAKAZI wa VIJIJI 3 vya Kata hii, WANANCHI wana imani kubwa na SERIKALI ya CCM kukamilisha USAMBAZAJI uliosalia – na hili nalo limo ndani ya ILANI MPYA ya CCM.
KUBORESHA MIUNDOMBINU YA SEKONDARI YA KATA
* Ujenzi wa MAABARA, MAKTABA, n.k  kwenye Tegeruka Sekondari unaendelea.
KIJIJI CHA KATARYO:
WANANCHI wameamua kujenga:
* ZAHANATI ya Kijiji chao
* SHULE SHIKIZI Nyasaenge
VIJIJI VYA MAYANI & KATARYO:
* WANANCHI wameamua kujenga SEKONDARI ya PILI ya Kata itakayojengwa katikati ya Vijiji hivyo viwili. Ujenzi unaanza tarehe 1.11.2020
KAMPENI ZA UCHAGUZI za Jimbo la Musoma Vijijini ni KAMPENI za MATAYARISHO ya UTEKELEZAJI wa ILANI MPYA ya CCM (2020-2025)
* VITENDO KWANZA
* MAENDELEO KWANZA
KURA ZA KATA YA TEGERUKA – Wananchi wamesema:
* Dkt Magufuli: 100%
* Prof Muhongo: 100%
* Ndg Mashauri: 100%
VIAMBATANISHO vya hapa: baadhi ya Matukio ya KAMPENI za UCHAGUZI ndani ya Kata ya Tegeruka.
“TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE PAMOJA”
Sospeter Muhongo
Jimbo la Musoma Vijijini
10.10.2020

ARI KUBWA YA WANAVIJIJI KUCHANGIA MAENDELEO YAO WAIWEKA PAZURI KATA YA MUGANGO – WANAANZA UJENZI WA MABWENI WAWE NA “HIGH SCHOOL” MWAKANI

Tarehe 8.10.2020, MGOMBEA UBUNGE wa CCM wa Jimbo la Musoma Vijijini, PROF MUHONGO, alifanya MIKUTANO 2 ya KAMPENI ndani ya Kata ya Mugango.
Mbali ya kunadi SERA za CCM, Prof Muhongo alijadili UTEKELEZAJI wa MIRADI ya KIPAUMBELE ya Kata hiyo – hii ikiwa ni sehemu ya matayarisho ya UTEKELEZAJI wa ILANI MPYA ya CCM baada ya UCHAGUZI wa tarehe 28.10.2020.
KIPAUMBELE CHA ELIMU:
KATA ya MUGANGO yenye Vijiji 3 (Kwibara, Kurwaki, Nyang’oma) inaanza KUTEKELEZA ILANI MPYA ya CCM (2020-2025) kwa KUJENGA MABWENI 3 ili mwakani (Julai 2021) iwe na Kidato cha V & VI.
Vilevile, Kata hiyo imeamua kujenga SEKONDARI ya PILI kwenye eneo la katikati ya Vijiji vya Kurwaki na Nyang’oma.
MAFANIKIO makubwa ya WANANCHI kukubali  KUCHANGIA MAENDELEO YAO (nguvukazi & michango ya fedha taslimu) yako dhahiri:
* Vyumba vya Madarasa ya Shule zao za Msingi  na Sekondari ya Mugango havina mirundikano ya Wanafunzi.
* MAABARA za Mugango Sekondari zinajengwa
* Vyoo vya kutosha vipo mashuleni
* Bustani za shule zipo
KIPAUMBELE CHA AFYA:
* KITUO cha AFYA cha Mugango tayari kimekamilika kwa USHIRIKIANO MZURI wa WANANCHI na SERIKALI yao ya CCM
* ZAHANATI ya Kijiji cha Kurwaki itakamilishwa ikiwa ni moja ya MAFANIKIO ya UTEKELEZAJI wa ILANI MPYA ya CCM.
* VITENDO KWANZA
* MAENDELEO KWANZA
ILANI MPYA YA CCM YAKUBALIKA SANA
* MAJI VIJIJINI – Kata ya Mugango yenye CHANZO (Ziwa Victoria) cha BOMBA la MAJI ya Kiabakari na Butiama, itaendelea kupata MAJI kutoka kwenye BOMBA hilo la zamani ambalo limechakaa!
MRADI mkubwa wa Tsh Bilioni 70 wa BOMBA la MAJI la Mugango – Kiabakari – Butiama utaanza kutekelezwa hivi karibuni na VIJIJI vya Kata za MUGANGO na TEGERUKA vitapewa MAJI safi na salama kutoka kwenye BOMBA hili jipya.
* UMEME VIJIJINI – Kama ilivyoandikwa ndani ya ILANI MPYA ya CCM, WANANCHI wa Kata ya Mugango wana imani kubwa sana na SERIKALI ya CCM kukamilisha USAMBAZAJI wa UMEME kwenye Vitongoji vilivyosalia.
IDADI YA KURA KUTOKA KATA YA MUGANGO
* Dkt Magufuli: 100%
* Prof Muhongo: 100%
* Ndg Charles Magoma: 100%
VIAMBATANISHO vya hapa:
* Kwaya ya Mugango
* Matukio mengine ya Mikutano 2 ya Kampeni
“TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE PAMOJA”
Sospeter Muhongo
Jimbo la Musoma Vijijini
9 Oktoba 2020

ILANI MPYA YA CCM INATOA MAJIBU YA KERO & VIPAUMBELE VYA WANANCHI WA KATA YA NYAMRANDIRIRA

Kata ya Nyamrandirira ina Vijiji 5 (Chumwi, Kaboni, Kasoma, Mikuyu na Seka) na kila KIJIJI kinakiri kwamba ILANI MPYA ya UCHAGUZI ya CCM (2020-2025) ndiyo pekee inatoa MAJIBU ya Kero na Vipaumbele vya MAENDELEO na USTAWI wa Vijiji vyao.
Hayo yamebainika wakati wa MIKUTANO 4 ya KAMPENI ya Mgombea Ubunge wa CCM wa Jimbo la Musoma Vijijini, PROF MUHONGO.
* ELIMU – SEKONDARI MPYA YA KATA
Vijiji vyote 5 vinachangia ujenzi wa SEKONDARI ya PILI ya Kata yao. SEKONDARI hii (Seka Secondary School) itafunguliwa Januari 2021.
*KIJIJI CHA MIKUYU
VIPAUMBELE vya Kijiji hiki ni MAJI, UMEME na ZAHANATI.
Ujenzi wa ZAHANATI ya Kijiji chao utaanza  baada ya UCHAGUZI wa tarehe 28.10 2020 kwa kutumia NGUVUKAZI na MICHANGO ya Wanakijiji na Viongozi wao.
MAJI – Kijiji hiki kiko kwenye Mradi wa BOMBA la Maji ya kutoka Ziwa Victoria (Kijijini Chumwi) kwenda Mabui Merafuru na Mikuyu. USANIFU wa awali unapitiwa upya na RUWASA kwani awali Vijiji vya Nyambono na Saragana vilikuwa ndani ya Mradi huu. Kwa sasa vijiji hivyo vimepelekwa kwenye  Mradi wa Suguti – Wanyere/Chirorwe.
UMEME- Miundombinu ya Usambazaji wa UMEME ipo na baadhi ya Wanavijiji tayari wameunganishiwa umeme. Kazi inaendelea na itakamilika kama isemavyo ILANI MPYA ya CCM.
* KIJIJI CHA CHUMWI
VIPAUMBELE vya Kijiji hiki vinafanana na vile vya Kijiji cha Mikuyu kasoro  Zahanati. UTEKELEZAJI wa Miradi yake ya MAJI & UMEME unafana na ule wa Kijiji cha Mikuyu.
* KIJIJI CHA KASOMA
MAJI ya Kijiji hiki yatatolewa Ziwa Victoria. Kijiji hiki kiko kwenye orodha ya Vijiji 33 vya Jimboni mwetu vilivyo kwenye Mradi wa MAZIWA MAKUU.
UMEME – ni kama ilivyoelezwa hapo juu kwenye Kijiji cha Mikuyu.
* VIJIJI VYA KABONI & SEKA
MAJI ya Vijiji hivi yatatolewa kwenye BOMBA la MAJI la MGODI wa SEKA ambalo chanzo chake kiko Kijijini Kaboni. Baadhi ya Wanavijiji tayari wanahudumiwa na Bomba hili.
UMEME – Baadhi ya Wanaviviji ndani ya Vijiji hivi viwili tayari wameunganishiwa umeme. Vitongoji vilivyosalia vitapewa UMEME na kazi ya usambazaji inaendelea.
ELIMU – Kijiji cha KABONI kinashughulikia suala ya ardhi kwa ajili ya ujenzi wa SHULE ya MSINGI yao. Kijiji hakina Shule ya Msingi.
MGOMBEA URAIS WA CCM (DKT MAGUFULI) ameahidiwa KURA ZOTE (100%) kutoka Kata Nyamrandirira
VIAMBATANISHO vya hapa:
Kwaya, Shairi, Igizo kutoka Kata ya Nyamrandirira
“TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE PAMOJA”
Sospeter Muhongo
Jimbo la Musoma Vijijini
8 Oktoba 2020

MIKUTANO 3 YA KAMPENI NDANI YA KATA YA NYAMBONO YAMKUBALI SANA DKT MAGUFULI

Leo, Jumanne, 6.10.2020 MGOMBEA UBUNGE wa CCM wa Jimbo la Musoma Vijijini, PROF MUHONGO ameenda Kijijini Nyambono, Kijijini Saragana na kwenye Kitongoji cha Nyabherango KUOMBA KURA za WAGOMBEA  wa CCM wa nafasi za Urais, Ubunge na Udiwani.

DKT MAGUFULI anakubalika kwa Asilimia Miamoja  (100%). SABABU KUU zikiwa:

(i) MAJI ya ZIWA VICTORIA

Vijiji 2 vya Kata ya Nyambono (Saragana & Nyambono) viko mbali na Ziwa Victoria na hivi karibuni vitapata MAJI ya Ziwa hilo kupitia MRADI wa BOMBA la MAJI wa Suguti-Wanyere/Chirorwe ambapo BOMBA hilo litapaleka MAJI kwenye Vijiji hivyo. Ujenzi wa TENKI kubwa la MAJI kwenye Mlima Nyabherango utaanza hivi karibuni (Bajeti ya Mwaka huu).

(ii) UMEME wa REA:

Vitongoji vya Kata hiyo vilivyosalia vitapewa umeme – ILANI MPYA ya CCM (2020-2025) imebainisha hivyo.

VIPAUMBELE MAALUM

* KIJIJI CHA NYAMBONO

WANANCHI wa Kijiji hiki WAMEAMUA kwa KAULI moja kwamba kwa MIAKA 5 ya UTEKELEZAJI wa ILANI ya CCM (2020-2025) watajenga SEKONDARI yao. Kwa sasa WATOTO wao wanatembea umbali wa zaidi ya KILOMITA 6 kwenda  masomoni kwenye SEKONDARI ya NYAMBONO iliyoko Kijijini Saragana.

Vilevile, WANANCHI hawa  na WADAU  wao wa MAENDELEO watakamilisha ujenzi wa ZAHANATI ya Kijiji chao.

WATOTO wa Kitongoji cha Nyabherango wanaenda  masomoni kwenye SHULE za MSINGI za mbali na kwao (zaidi ya kilomita 5).  Kitongoji hicho kinatafuta ardhi kianze kujenga SHULE SHIKIZI.

* KIJIJI CHA SARAGANA

Kitongoji cha Kabise kitajenga SHULE SHIKIZI kutatua tatizo sugu la mwendo mrefu ambao WATOTO wao wanatembea kwenda masomoni kwenye SHULE za MSINGI za Vitongoji vingine.

* MIRADI MINGINE ni kama ilivyoainishwa kwenye ILANI MPYA ya CCM ya 2020-2025.

“TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE PAMOJA”

Sospeter Muhongo

Jimbo la Musoma Vijijini

6 Oktoba 2020

KAMPENI ZA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI NI KAMPENI ZA UCHUMI & MAENDELEO – KATA YA BUGWEMA ITAENDELEA KUPANUA KILIMO CHA ALIZETI

KATA ya BUGWEMA yenye VIJIJI 4 (Bugwema, Masinono, Muhoji na Kinyang’erere) ndiyo inayoongoza kwenye KILIMO cha MAZAO MCHANGANYIKO (alizeti, pamba, mahindi, mihogo, mpunga, mtama, dengu, vitunguu, nyanya, viazi, n.k.) ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.

Jana, wakati wa KAMPENI za CCM kwenye Vijiji vya Bugwema na Masinono, KILIMO kiliwekewa mkazo sana.

Matayarisho ya MRADI mkubwa wa KILIMO cha UMWAGILIAJI kwenye BONDE LA BUGWEMA unaendelea ndani ya SERIKALI yetu.

ELIMU & MAFUNZO ni KIPAUMBELE kingine cha Kata hii ambayo VIJIJI vyake 4 viko mbalimbali. Kwa mfano, kutoka Muhoji hadi Masinono (kwenye SEKONDARI yao ya Kata) ni mwendo usiopungua kilomita 11. Kwa hiyo, SEKONDARI MOJA haitoshi. WANANCHI wamependekeza SEKONDARI 2 MPYA zijengwe kwenye VIJIJI vya Muhoji na Bugwema ndani ya MIAKA 5 ya UTEKELEZAJI wa ILANI MPYA ya CCM (2020-2025).

BARAZA LA MADIWANI liliishaamua kupanua BUGWEMA SEKONDARI na kuwa na “HIGH SCHOOL” ya Wasichana (Bugwema Girls High School). Uamuzi huu UTATEKELEZWA ndani ya MIAKA 5 ya UTEKELEZAJI wa ILANI MPYA ya CCM.

WANANCHI wanayo imani kubwa na SERIKALI ya CCM kuendelea kusambaza UMEME kwenye Vitongoji vilivyosalia.

Ndani ya MIAKA 5 (2020-2025), RUWASA imeahaidi kusambaza MAJI kutoka Ziwa Victoria kwenda kwenye VIJIJI 4 vya Kata hii.

ZAHANATI ya Masinono, yenye GARI la WAGONJWA (Ambulance) walilopewa na Prof Muhongo, IMEPOKEA Tsh MILIONI 400 kutoka SERIKALINI kwa ajili ya upanuzi wake wa kuwa KITUO cha AFYA  – KURA za DKT MAGUFULI ni NYINGI kweli kweli!

MASUALA ya UKABILA yamekewa sana na WANANCHI wa KATA ya BUGWEMA wamehaidi kutoa KURA zaidi ya 98% kwa WAGOMBEA wa CCM kwenye nafasi za URAIS (Dkt Magufuli), UBUNGE (Prof Muhongo) na UDIWANI (Ndugu Clifford Machumu).

UTAMADUNI, MICHEZO & SANAA – ILANI MPYA CCM – Kata ya Bugwema iko tayari kwenye UTEKELEZAJI wake

“TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE PAMOJA”

Sospeter Muhongo

Jimbo la Musoma Vijijini

4 Oktoba 2020

WANANCHI WA KATA YA MUSANJA WATOA VIPAUMBELE VYAO KWA MIAKA 5 YA UTEKELEZAJI WA ILANI MPYA YA CCM (2020-2025)

Ijumaa, tarehe 2.10.2020, KATA ya MUSANJA yenye VIJIJI 3 (Mabui Merafuru, Musanja na Nyabaengere) ilikuwa kwenye KAMPENI za UCHAGUZI za Chama cha Mapinduzi (CCM)

WAGOMBEA UBUNGE (Prof Muhongo) na UDIWANI (Ndugu Mwira) wa CCM walinadi SERA na MIRADI ya MAENDELEO iliyoko kwenye ILANI MPYA (2020-2025) ya Chama chao.

MIKUTANO 2 ya KAMPENI ilifanywa kwenye VIJIJI 2 (Musanja & Mabui Merafuru).

WANANCHI  WALIVUTIWA SANA na SERA za CCM na kuahidi kutoa KURA ZOTE kwa WAGOMBEA wa CCM kwa nafasi ya URAIS (Dkt Magufuli), UBUNGE (Prof Muhongo) na UDIWANI (Ndg Ernest John Mwira).

MIRADI ya KIPAUMBELE ya KATA ya MUSANJA ni:

*Kukamilishwa kwa usambazaji wa UMEME kwenye Vitongoji vilivyosalia

*Kuanza kwa utekelezaji wa Mradi wa MAJI ya kutoka Ziwa Victoria (Chumwi, Kata ya Nyamrandirira) hadi Mabui Merafuru (Kata ya Musanja). Wataalamu walishakamilisha USANIFU wa Mradi huu.

*Ukamilishaji wa ujenzi wa SHULE Shikizi Gomora na kuipanua iwe Shule ya Msingi inayojitegemea.

*Kujenga ZAHANATI 1 kwenye Kijiji 1 kati ya Vijiji 3. Kwa sasa Kata ya Musanja inatumia Kituo cha Afya ya Murangi.

*SEKONDARI kwenye Kijiji cha Musanja ambacho kiko mbali na Sekondari ya Kata iliyoko Kijiji cha Mabui Merafuru

*VITENDO KWANZA

*MAENDELEO KWANZA

VIAMBATANISHO vya hapa:

*Kwaya ya Musanja

*Matukio mengine ya Kampeni

“TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE KWA PAMOJA”

Sospeter Muhongo

Jimbo la Musoma Vijijini

3 Oktoba 2020

MIRADI YA UJENZI WA SEKONDARI MPYA TISA (9) ZA KATA ITAKAMILISHWA NA WANANCHI WAKISHIRIKIANA NA SERIKALI YA CCM

 

Jimbo la Musoma Vijijini lina JUMLA ya SEKONDARI 20 za KATA. Sekondari zote hizi ziko kwenye UJENZI wa MAABARA, MAKTABA, VYUMBA VIPYA VYA MADARASA, OFISI & NYUMBA ZA WALIMU, n.k.

Jimbo la Musoma Vijijini lina UJENZI wa SEKONDARI MPYA TANO (5) za Kata zilizopangwa zifunguliwe mwakani (Januari 2021). SEKONDARI MPYA hizo ni:

(i) Kigera, Kata ya Nyakatende,

(ii) Nyasaungu, Kata ya Ifulifu,

(iii) Ifulifu (inajengwa Kijijini Kabegi), Kata ya Ifulifu,

(iv) Seka, Kata ya Nyamrandirira, na

(v) Bukwaya, Kata ya Nyegina.

Kata hizo 5 zitakuwa na SEKONDARI zaidi ya MOJA ndani ya Kata zao.

*VITENDO KWANZA*

Kata nyingine za Jimbo la Musoma Vijijini nazo zimepanga kuwa na SEKONDARI zaidi ya MOJA ndani ya Kata zao. Kwa hiyo, zimeishafanya maamuzi ya kuanza kujenga SEKONDARI MPYA. Kata hizo ni:

(vi) Suguti, itajenga Sekondari mpya Kijijini Wanyere,

(vii) Tegeruka, Sekondari mpya itajengwa katikati ya Vijiji vya Kataryo na Mayani,

(viii) Etaro, itajenga Sekondari mpya Kijijini Busamba, na

(ix) Mugango, Sekondari mpya itajengwa katikati ya Vijiji vya Kurwaki na Nyang’oma

Ifikapo MWAKA 2025, Jimbo la Musoma Vijijini, lenye Kata 21 litakuwa na:

* SEKONDARI 29 za Kata (Serikali)

* SEKONDARI 2 za Binafsi (SDA & KATOLIKI)

* VETA 1 – maombi yameishapelekwa Serikalini

*MAENDELEO KWANZA*

*CHAGUENI CCM  TUKAMILISHE MIRADI YETU

*CHAGUENI DKT MAGUFULI ili TUKAMILISHE MIRADI YETU*

* CHAGUENI PROF MUHONGO & MADIWANI 21 WA CCM wa KATA 21 za Jimbo letu ili TUKAMILISHE MIRADI YETU

PICHA zilizopo hapa zinaonesha ujenzi unaoendelea kwa baadhi ya SEKONDARI MPYA za KATA za Jimbo la Musoma Vijijini.

“TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE PAMOJA”

Sospeter Muhongo

Jimbo la Musoma Vijijini

29 Sept 2020

 

 

SHULE MPYA 11 ZA MSINGI KUKAMILISHWA NDANI YA MIAKA 5 (2020-2025) – CHAGUA CCM, CHAGUA DKT MAGUFULI MIRADI IKAMILIKE

 

MWAKA jana (2019) SHULE za MSINGI za  Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC), yenye Jimbo la Musoma Vijijini, ziliongoza (NAMBA MOJA) Mkoa wa Mara kwenye MITIHANI ya Darasa la Nne (Std IV).

WANANCHI wa VIJIJI 11 ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini WAMEAMUA kujenga SHULE MPYA 11 za MSINGI kwa madhumuni ya kuongeza UBORA wa ELIMU itolewayo kwenye SHULE za MSINGI za maeneo yao.

Baadhi ya WANAFUNZI wa Shule za Msingi wanatembea umbali mrefu (kati ya kilomita 2 na 5) kwenda masomoni, na kwenye baadhi ya SHULE za MSINGI kuna MIRUNDIKANO mikubwa MADARASANI.

Kwa hiyo, WANANCHI, kwa kutumia NGUVUKAZI zao na kwa KUSHIRIKIANA na SERIKALI ya CCM, wameamua kutatua matatizo haya!

SHULE SHIKIZI 11 zinajengwa kwenye VIJIJI 11 vya Jimbo hili. Baadhi ya SHULE hizi tayari zina MADARASA ya AWALI na zimeanza kutoa MASOMO ya Darasa la Kwanza na Pili (Std I & II).

Ndani ya MIAKA 5 ya UTEKELEZAJI wa ILANI ya CCM (2020-2025), SHULE hizi 11 zitaendelea kujengwa na kukamilishwa, yaani kuwa SHULE za MSINGI kamili.

*CHAGUA CCM,

*CHAGUA MAENDELEO KWA VITENDO

ORODHA YA SHULE SHIKIZI ZINAZOJENGWA:

(1) Binyango: Kijijini Kabegi, Kata ya Ifulifu

(2) Buanga: Kijijini Buanga, Kata ya Rusoli

(3) Buraga Mwaloni: Kijijini Buraga, Kata ya Bukumi

(4) Egenge: Kijijini Busamba, Kata ya Etaro

(5) Gomora: Kijijini Musanja, Kata ya Musanja

(6) Kaguru: Kijijini Bugwema, Kata ya Bugwema

(7)  Karusenyi: Kijijini Mikuyu, Kata ya Nyamradirira

(8) Rwanga: Kijijini Kasoma, Kata ya Nyamradirira

(9) Mwikoko: Kijijini Chitare, Kata ya Makojo

(10) Kihunda: Kijijini Kamguruki, Kata ya Nyakatende

(11) Ziwa: Kijijini Mwiringo, Kata ya Busambara

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, PROF MUHONGO ni sehemu ya MAFANIKIO ya UJENZI wa SHULE SHIKIZI hizi. Baada ya UCHAGUZI ataendelea KUSHIRIKIANA na WANANCHI na SERIKALI ya CCM kukamilisha ujenzi wa SHULE hizi.

PICHA zilizoko hapa zinaonyesha baadhi ya SHULE SHIKIZI zinazojengwa ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.

“TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE PAMOJA.”

Sospeter Muhongo

Jimbo la Musoma Vijijini

28 Sept 2020

ELIMU & MAFUNZO – MAKTABA ZAJENGWA KWENYE SHULE ZA MSINGI ZA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

JENGO LA TEHAMA – AGAPE PRIMARY SCHOOL

JIMBO la Musoma Vijijini tayari linatekeleza ILANI MPYA ya CCM (2020-2025) kwa SHULE za MSINGI kujenga MAKTABA zao.

(1) SHULE YA MSINGI RUKUBA

Hii iko Kata ya Etaro. MAKTABA imekamilika na inatumika. Ujenzi wake ni mafanikio ya USHIRIKIANO wa WANANCHI, PCI (USA – vifaa vingi vya ujenzi), PROF MUHONGO (Saruji Mifuko 50) na UONGOZI wa SHULE. VITABU vya Maktaba vilitolewa na Prof Muhongo.

VIAMBATANISHO – Picha za Jengo lenye Mabati Meupe (Maktaba)  baadhi ya vitabu vimeshakabidhiwa

 

(2) SHULE YA MSINGI BUTATA

Hii iko Kata ya Bukima. Ujenzi wake ni mafanikio ya USHIRIKIANO wa  MiCHANGO ya WANANCHI, PCI (USA – vifaa vingi vya ujenzi), PROF MUHONGO (Saruji Mifuko 50) na UONGOZI wa SHULE. VITABU vya Maktaba vitatolewa na Prof Muhongo na PCI (USA).

(3) SHULE YA MSINGI BUSAMBA

Hii iko Kata ya Etaro na inajengwa kwa USHIRIKIANO wa WANANCHI, PROF MUHONGO (Saruji Mifuko 60) na UONGOZI wa SHULE

(4) SHULE YA MSINGI BURAGA

Hii iko Kata ya Bukumi. WANANCHI wamemuomba MGOMBEA UBUNGE wa CCM (Prof Muhongo) achangie ujenzi wake baada ya Uchaguzi wa tarehe 28.10.2020. Amepokea OMBI hilo na kukubali kushirikiana na Wananchi hao.

(5) SHULE YA MSINGI BUIRA

Hii iko Kata ya Bukumi. Ujenzi wake unafanana na ule wa S/M BURAGA (soma hapo juu).

(6) AGAPE PRIMARY SCHOOL

Hii ni SHULE ya PRIVATE (Binafsi) iliyoko kwenye Kata ya Bukima na inajenga JENGO la TEHAMA (angalia Kiambatanisho –  Picha za Jengo lenye mabati ya rangi ya kijani).

PROF MUHONGO alishachangia VITABU vya MAKTABA na Saruji Mifuko 50 ya ujenzi wa Jengo la Tehama la Shule hii, na alihaidi kuchangia COMPUTERS.

SHULE NYINGINE za MSINGI za JIMBO la Musoma Vijijini zimeweka MIPANGO ya ujenzi wa MAKTABA zao.

PROF MUHONGO aligawa VITABU vingi vya MAKTABA kwenye SHULE zote za MSINGI za JIMBO hili (111 za Serikali & Agape ya Binafsi).

ILANI MPYA CCM (Elimu & Mafunzo) TAYARI INATEKELEZWA ndani ya JIMBO la Musoma Vijijini

*VITENDO KWANZA

*MAENDELEO KWANZA

Sospeter Muhongo

Jimbo la Musoma Vijijini

27 Sept 2020

JENGO LA MAKTABA SHULE YA MSINGI RUKUBA

CHAGUENI CCM NCHI IZIDI KUNG’ARA – SHAIRI KUTOKA KIJIJI CHA KASOMA

WANANCHI wa Kata ya Nyamrandirira yenye VIJIJI 5 wamewaomba Prof SOSPETER MUHONGO (Mgombea Ubunge) na Mwl NYEOJA WANJARA (Mgombea Udiwani) waungane nao tarehe 5 Novemba 2020 kukamilisha MAJENGO ya AWALI yanayohitajika ili SEKA SEKONDARI ifungiliwe Januari 2021.

 

VIJIJI 5 (Chumwi, Kaboni, Kasoma, Mikuyu na Seka) vya Kata ya Nyamrandirira vinayo SEKONDARI MOJA (Kasoma Secondary School) ambayo kwa sasa imeelemewa na WINGI wa WANAFUNZI kutoka kwenye vijiji hivyo. WANAFUNZI wengine wanatembea mwendo wa zaidi ya kilomita 10 kwenda masomoni Kasoma Sekondari.

 

Kwa hiyo, KATA hiyo imeamua kuanza KUTEKELEZA ILANI MPYA YA CCM (2020-2025) kwa KUKAMILISHA UJENZI wa MIUNDOMBINU INAYOHITAJIKA kwa ufunguzi wa SEKONDARI yao mpya (Seka Secondary School) inayojengwa Kijijini Seka.

 

Sospeter Muhongo

Jimbo la Musoma Vijijini

25.9.2020

MIRADI YA MAENDELEO YA KATA YA NYAKATENDE ITAKAMILISHWA NA CCM

Kampeni za CCM kwenye Kata ya Nyakatende.

Jumanne, 22.9.2020, WANANCHI wa Kata ya NYAKATENDE waliamua wazi wazi kwamba kwenye Kata yao yenye VIJIJI VINNE (Kakisheri, Kamuguruki, Kigera na Nyakatende) KURA zote zitaenda CCM.
SEKONDARI ya PILI (Kigera Secondary School) inayojengwa Kijijini Kigera imepangwa ifunguliwe mwakani (Januari 2021). MAJENGO muhimu ya awali yanaezekwa na WANANCHI wanayo imani kubwa sana na WAGOMBEA wa CCM wa nafasi za URAIS, UBUNGE na UDIWANI kwamba ndio wenye uwezo na kutoa ushirikiano wa SEKONDARI hiyo mpya ifunguliwe Januari 2021.
KIJIJI cha Kakisheri kinajenga ZAHANATI yake. HALMASHAURI ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC) imepanga kujenga KITUO cha AFYA kwenye Kata hiyo kwa kutumia MICHANGO na NGUVUKAZI ya WANANCHI wa Kata hiyo.
WANANCHI wanasema MIRADI hii na mingine ya MAENDELEO (k.m. usambazaji wa MAJI na UMEME) itakamilishwa kwa ushirikiano na SERIKALI ya CCM.
UAMUZI wa KATA ya NYAKATENDE ni huu – “KURA ZOTE kwa MAGUFULI (Urais), MUHONGO (Ubunge) na MARERE (Udiwani).”
*VITENDO KWANZA
*MAENDELEO KWANZA

CCM YAENDELEA KUNG’ARA NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa akiteta jambo na Prof Muhongo

Jumatatu, 21.9.2020, Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa MAJALIWA amepiga KAMPENI yenye MAFANIKIO MAKUBWA ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.
Mhe Waziri Mkuu ameelezea MAFANIKIO MAKUBWA yaliyopatikana kwenye UTEKELEZAJI wa ILANI ya CCM ya 2015-2020 chini ya UONGOZI na USIMAMIZI wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt John Joseph Pombe MAGUFULI
Mhe Waziri Mkuu ametoa maelezo ya kina juu ya UTEKELEZAJI wa ILANI mpya ya CCM ya 2020-2025 na kuwadhibitishia WANANCHI wa Jimbo la Musoma Vijijini kwamba MIRADI ya MAENDELEO ya Jimbo hilo ITATEKELEZWA na KUKAMILISHWA na SERIKALI ya CCM chini ya UONGOZI wa Mhe Dkt John Joseph Pombe MAGUFULI.
MIRADI ya MAENDELEO ya Jimbo la Musoma Vijijini INAYOTEKELEZWA kwa USHIRIKIANO wa SERIKALI na WANANCHI wa Jimbo hilo ni mingi mno ikiwemo ya ujenzi wa barabara ya lami ya Musoma-Makojo-Busekera, Hospital ya Wilaya, Zahanati mpya na Vituo vya Afya vipya, Sekondari mpya, ukamilishaji wa usambazaji wa MAJI na UMEME vijijini, upanuzi wa kilimo cha umwagiliaji, n.k. MIRADI mipya imo ya ujenzi wa VETA, Makao Makuu ya Halmashauri Kijijini Murangi, n.k.
Waziri Mkuu amekabidhi ILANI ya UCHAGUZI ya CCM ya 2020-2025 kwa Mgombea Ubunge (Prof Muhongo) wa CCM wa Jimbo la Musoma Vijijini.
Prof Muhongo amesema kwamba WANANCHI wa Jimbo la Musoma Vijijini, kwa KUSHIRIKIANA na SERIKALI yao ya CCM, wataanza KUTEKELEZA ILANI mpya ya CCM ya 2020-2025 kuanzia tarehe 1.11.2020. Muhtasari wa MIRADI ya Jimbo hilo imekabidhiwa kwa Mhe Waziri Mkuu.
Mhe Waziri Mkuu ameshuhudia UTAYARI na MWITIKIO mkubwa wa WANANCHI wa Jimbo la Musoma Vijijini wa KUTOA KURA NYINGI SANA kwa MGOMBEA URAIS wa CCM, Mhe Dkt John Joseph Pombe MAGUFULI.
SHUKRANI nyingi zimetolewa kwa WAZIRI MKUU, Mhe Kassim Majaliwa MAJALIWA kwa kuwahutubia WANANCHI Kijijini Bukima, Kijijini Suguti (Kusenyi), Kijijini Kwikuba, Kijijini Mugango na Kijijini Mkirira. AMEFANIKIWA SANA kuwaombea KURA WAGOMBEA wa CCM wa nafasi za URAIS, UBUNGE na UDIWANI.
WANANCHI wa JIMBO la Musoma Vijijini WAMEAHIDI kupiga kura, bila kukosa, tarehe 28.10.2020 na kupata USHINDI MKUBWA MNO MNO kwa CHAMA cha MAPINDUZI (CCM).
Sospeter Muhongo
21 Sept 2020

JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI – ILANI MPYA YA UCHAGUZI YA CCM (2020-2025) KUANZA KUTEKELEZWA TAREHE 1 NOVEMBA 2020

Prof MUHONGO akiwa na BODABODA wa Kijiji cha Kataryo

WANANCHI wa Kata ya TEGERUKA WAMEAMUA kujenga SEKONDARI ya PILI ili kutatua tatizo la mwendo mrefu wanaotembea WANAFUNZI wa SEKONDARI wa Kata hiyo.
KATA hiyo yenye VIJIJI 3 (Kataryo, Mayani & Tegeruka) vilivyo mbali mbali ina SEKONDARI moja. WANAFUNZI kutoka Vijiji vya Kataryo na Mayani wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya KILOMITA 15 kwenda masomoni TEGERUKA SEKONDARI.
Tarehe 1.11.2020, WANANCHI wanaanza ujenzi wa SEKONDARI ya PILI ya Kata yao itakayojengwa eneo lililo katikati ya Vijiji vya Kataryo na Mayani. WAGOMBEA UBUNGE (Prof S Muhongo) na UDIWANI (Askofu A M Mashauri) WAMEKUBALI KUSHIRIKIANA na WANANCHI hao kujenga Sekondari hiyo.
WANANCHI wa Kata ya Kataryo WAMEFURAHI na KUSHUKURU sana SERIKALI yao baada ya kuambiwa kwamba MRADI wa BOMBA la MAJI kutoka Ziwa Victoria (Mugango) kwenda Kiabakari na Butiama litakuwa na MATOLEO ya MAJI ndani ya VIJIJI vyote VITATU vya Kata hiyo. MRADI huo utagharimu TSH BILIONI 71 (bilioni sabini na moja) ambazo ZIMEISHATOLEWA na Serikali ya SAUDI ARABIA, BADEA na SERIKALI yetu. Utekelezaji wake unaanza hivi karibuni.
Sospeter Muhongo
Jimbo la Musoma Vijijini
19.9.2020

JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI – USAMBAZAJI WA MABANGO,  VIPEPERUSHI & VITABU VYA TAARIFA ZA UTEKELEZAJI WA ILANI ILIYOPITA

usambazaji wa MABANGO & VIPEPERUSHI ndani ya Vijiji vyote 68 vya Jimbo la Musoma Vijijini.

(1) MABANGO 4,000 (elfu nne) ya MGOMBEA URAIS wa CCM, Mhe Rais Dkt John Joseph Pombe MAGUFULI yanasambazwa ndani ya Vijiji vyote 68.
(2) VIPEPERUSHI 5,000 (elfu tano) vyenye Muhtasari wa MIRADI itakayotekelezwa (2020-2025), vinasambazwa. MIRADI hii inatokana na ILANI mpya ya UCHAGUZI ya CCM ya 2020-2025.
(3) VIPEPERUSHI 5,000 (elfu tano) vya Muhtasari wa WASIFU wa MGOMBE UBUNGE, Prof Sospeter Mwijarubi MUHONGO, vinasambazwa.
(4) VITABU 10,000 (Volume I & II) vyenye TAARIFA za Utekelezaji wa ILANI ya UCHAGUZI ya CCM ya 2015-2020,  usambazaji wake utafikia tamati tarehe 1.10.2020
(5) VIPEPERUSHI 4,200 (elfu nne mia mbili) vya kuvaa shingoni vya WAGOMBEA UDIWANI 21 (@200) wa CCM vinaanza kusambazwa kesho (9.9.2020). Mgombea Ubunge, Prof Muhongo amewatengenezea vipeperushi hivyo.
(6) BENDERA za CCM 500 (400 kutoka Chamani Dodoma & 100 za Mgombea Ubunge) zinagawiwa.
UZINDUZI WA KAMPENI ZA CCM ZA WILAYA YA CCM YA MUSOMA VIJIJINI
Mahali:
Bwai Kwitururu
Kata ya Kiriba
Siku:
Ijumaa, 11.9.2020

PROF. MUHONGO ARUDISHA FOMU ZA MAOMBI YA KUGOMBEA NAFASI YA UBUNGE WA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Ijumaa, 17.7.2020, Katibu wa CCM wa Wilaya ya Musoma Vijijini, Ndugu Peter Francis Mashenji ALIPOKEA FOMU za Prof Sospeter Muhongo za kuomba kugombea nafasi ya UBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini.
Prof Muhongo alisindikizwa na WASAIDIZI wake 5 {4 wanaotembelea Wanavijiji kila siku wakitumia PIKIPIKI na Dreva 1}. Wasaidizi wengine 3 wako masomoni ambao ni: Webmaster (1) na Wasoma taarifa kwenye On-line Radio (2).

PLAU NYINGINE 50 KUGAWIWA KWA VIKUNDI VINGINE 50 VYA WAKULIMA WA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Wakulima wakitumia PLAU walizopewa bure na Prof Sospeter Muhongo

Jumatatu, tarehe 13 Julai 2020, Prof Sospeter Muhongo alinunua PLAU 50 (majembe ya kukokotwa na ng’ombe) kwa ajili ya kuzigawa siku ya Sherehe za WAKULIMA (8.8.2020, NANENANE).
Prof Muhongo amefanya hivyo kwa kuzingatia TARATIBU za UCHAGUZI ambapo ltarehe 13 Julai 2020 ndiyo siku ya mwisho ya kutekeleza AHADI za waliokuwa WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. PLAU hizo zitagawiwa tarehe 8.8.2020 (NANENANE) na Mkuu wa Wilaya (DC) ya Musoma.
PROGRAMU YA KUPUNGUZA MATUMIZI MAKUBWA YA JEMBE LA MKONO
Prof Muhongo AMEANZISHA PROGRAMU hiyo ikiwa ni sehemu ya  LENGO kuu la KUBORESHA KILIMO ndani ya VIJIJI 68 vya Jimbo la Musoma Vijijini.
JUMLA YA PLAU 85 zimeishagawiwa kwa VIKUNDI 85 vya WAKULIMA wa Jimbo la Musoma Vijijini. LENGO KUU ni kuwa na angalau  PLAU 20 kwa kila Kijiji.
WAKULIMA wameelezwa mara kadhaa namna ya kupata MIKOPO ya KUNUNUA MATREKITA. Ofisi ya Kilimo ya HALMASHAURI yetu (Musoma DC) ipo tayari kuwasaidia kutuma MAOMBI ya MIKOPO yao.
MBEGU BORA zimeishagawiwa kwa WAKULIMA wa Jimbo la Musoma Vijijini. Hizo ni: Mbegu za ALIZETI (tani 20), MIHOGO, MTAMA na UFUTA.
KARIBUNI TUCHANGIE UBORESHAJI wa KILIMO ndani ya VIJIJI 68 vya Jimbo la Musoma Vijijini.

WATOTO CHINI YA MIAKA 6 WAJENGEWA SHULE VIJIJINI MWAO

WANAVIJIJI wakiwa kwenye ujenzi wa Shule SHIKIZI KARUSENYI, Kijijini Mikuyu, Kata ya Nyamrandirira, na Jengo lilokamilishwa la Shule SHIKIZI EGENGE, Kijijini Busamba, Kata ya Etaro

Prof Sospeter Muhongo ameendelea KUCHANGIA UJENZI wa SHULE SHIKIZI ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.
Leo, Ijumaa, tarehe 10 Julai 2020, Prof Muhongo AMETOA MICHANGO ifuatayo:
* MABATI 54 ya Geji 28 ya kuezekea Darasa moja kwenye Shule SHIKIZI KARUSENYI ya Kitongoji cha Mtakuja, Kijiji cha Mikuyu, Kata ya Nyamrandirira
* SARUJI MIFUKO 100 kwa ujenzi wa Vyumba bora vya Madarasa ya Shule SHIKIZI KIUNDA ya Kijijini Kamuguruki, Kata ya Nyakatende. Darasa linalotumiwa ni la matofali ya tope.
JIMBO la Musoma Vijijini linajenga SHULE SHIKIZI 11 kwa ajili ya kutatua MATATIZO sugu ya:
* Wanafunzi wa Madarasa ya Awali (chini ya miaka 6) kusomea chini ya miti.
* Wanafunzi chini ya umri wa miaka 6 kutembea umbali mrefu kwenda masomoni
* Mirundikano madarasani
IDADI YA SHULE ZA MSINGI MUSOMA VIJIJINI (Vijiji 68)
* Shule SHIKIZI 11 zinajengwa, zikiwemo hizo zilizochangiwa leo vifaa vya ujenzi. Nyingine zimeanza kupokea Wanafunzi.
* Shule za Msingi za SERIKALI ni 111
* Shule za Msingi za BINAFSI ni 3
UJENZI NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU & VIFAA VYA SHULE KWENYE SHULE ZA MSINGI
* MADAWATI zaidi 10,000 yalishagawiwa mashuleni
* VITABU vingi vya Maktaba vilishagawiwa
* VYUMBA vipya zaidi ya 450 vya Madarasa vilishajengwa
* PCI (USA) na WADAU wengine wa Maendeleo wanaendelea kuchangia ujenzi MAKTABA na VYOO kwenye baadhi ya Shule za Msingi
MATOKEO MAZURI YAANZA KUPATIKANA
* Uboreshaji wa MIUNDOMBINU & VIFAA vya Shule kwenye Shule za Msingi za Musoma Vijijini UMEANZA KUZAA MATUNDA MAZURI kwa mfano:
Mwaka jana (2019), Shule za Msingi za MUSOMA VIJIJINI zilishika NAMBA ya KWANZA kwenye MITIHANI ya DARASA LA NNE (IV) ndani ya Mkoa wa Mara – huko nyuma nafasi yao ilikuwa mkiani!
KARIBUNI TUJENGE SHULE ZA MSINGI zenye MIUNDOMBINU mizuri & VIFAA vizuri vya Shule vijijini mwetu.

SEKONDARI MPYA ZINADAIWA VYUMBA VIPYA VYA MADARASA KWA AJILI YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA CHA MWAKANI (2021)

Wanafunzi wa Dan Mapigano Memorial Secondary School, wakiwa Darasani.

JIMBO la Musoma Vijijini lina SEKONDARI MPYA 2 (Dan Mapigano Memorial Secondary School, Kata ya Bugoji) & Busambara Secondary School, Kata ya Busambara) zilizofunguliwa Mwaka huu (2020). MIUNDOMBINU ILIYOPO inatosheleza MAHITAJI ya sasa ya KIDATO CHA KWANZA (Form I).
MAOTEO ya Wanafunzi wa FORM I mwakani (2021) ni haya:
(i) Dan Mapigano Memorial Secondary School ya Kata ya Bugoji INATARAJIA KUPOKEA Wanafunzi 250 wa Form I (Jan 2021)
Vyumba Vipya vinavyohitajika ni 5,  vilivyopo ni 2. UJENZI wa Vyumba Vipya 3 umeanza na unapaswa kukamilika kabla ya tarehe 1.10.2020.
Prof Sospeter Muhongo ATACHANGIA MABATI 54 ya Geji 28 (yanayotosha kuezeka darasa moja) kabla ya tarehe 14.7.2020
(ii) Busambara Secondary School  ya Kata ya Busambara INATARAJIA KUPOKEA Wanafunzi 270 wa Form I (Jan 2021)
Vyumba Vipya vinavyohitajika ni 7,  vilivyopo ni 1. UJENZI wa Vyumba Vipya 6 umeanza na unapaswa kukamilika kabla ya tarehe 1.10.2020.
Prof Sospeter Muhongo ATACHANGIA MABATI 54 ya Geji 28 (yanayotosha kuezeka darasa moja) kabla ya tarehe 14.7.2020
SEKONDARI NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI
* Sekondari za Serikali au Kata ni 20.
Ujenzi wa MAABARA kwenye Sekondari zote 20 HAUJAKAMILIKA!
* Sekondari za Binafsi ni 2
* Sekondari zinazojengwa na zimepagwa zifunguliwe mwakani (2021) ni 5: Seka (Kata ya Nyamrandirira), Nyasaungu, Kabegi (zote za Kata ya Ifulifu), Kigera (Kata ya Nyakatende) na Bukwaya (Kata ya Nyegina). Kata nyingine zilizopanga kuanza kujenga Sekondari ya pili ni Etaro, Mugango na Suguti.
UAMUZI WA KUONGEZA HIGH SCHOOLS JIMBONI MWETU
Tunayo MOJA TU, KASOMA High School, Arts subjects (Kata ya Nyamrandirira)
Baraza la Madiwani lilishaamua KUONGEZA High Schools (hasa za MASOMO ya SAYANSI) kwenye Sekondari zifuatazo: (i) Bugwema, (ii) Mtiro, (iii) Mugango na (iv) Mkirira.
KARIBUNI TUCHANGIE ujenzi wa Secondary & High Schools Jimboni mwetu

UJENZI WA WODI YA MAMA NA MTOTO KISIWANI RUKUBA

Ujenzi wa Wodi ya Mama na Mtoto kwenye Zahanati ya Kisiwa cha Rukuba – hatua hiyo ya ujenzi imefikiwa ndani ya muda wa wiki 2 (kasi kubwa)

Jumamosi, tarehe 4.7.2020, Prof Sospeter Muhongo, alikamilisha AHADI  yake ya KUCHANGIA SARUJI MIFUKO 200 (mia mbili) kwa ajili ya ujenzi wa Wodi ya Mama & Mtoto kwenye Zahanati ya Kisiwa cha Rukuba. Prof Muhongo alitoa AHADI hiyo kabla muda wake wa UBUNGE kufikia tamati.
HALI YA HUDUMA YA AFYA MUSOMA VIJIJINI
* Zahanati 24 za Serikali
* Zahanati 4 za Bunafsi
* Zahanati 14 zinajengwa kwa nguvu za WANANCHI kwa kushirikiana na Serikali
* Wodi za Mama na Mtoto zinajengwa kwenye Zahanati za Bukima, Nyegina na Kisiwa cha Rukuba.
* Vituo vya Afya 2 (Murangi & Mugango)
* Kituo cha Afya Bugwema – Zahanati  ya Kijiji cha Masinono inapanuliwa iwe Kituo cha Afya cha Kata ya Bugwema.
* Hospitali ya Wilaya inajengwa Kijijini Suguti, Kitongoji cha Kwikonero.
MAGARI YA WAGONJWA (Ambulances):
Yapo 5: Kwenye Zahanati za Masinono, Kurugee na Nyakatende, na kwenye Vituo vya Afya vya Murangi na Mugango.
Jimbo la Musoma Vijijini lina Kata 21, Vijiji 68 na Vitongoji 374.
KARIBUNI TUCHANGIE UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA AFYA MUSOMA VIJIJINI

WANANCHI KISIWANI RUKUBA  WAJENGA MSINGI WA JENGO LA WODI YA MAMA NA MTOTO LENYE VYUMBA 13 KWA MUDA WA WIKI MOJA 

ujenzi wa WODI ya MAMA na MTOTO kwenye ZAHANATI ya KISIWA cha RUKUBA, Kata ya Etaro. WODI hiyo itakamilika na kutumika kabla ya tarehe 1 Disemba 2020.

KISIWA cha RUKUBA kimo ndani ya Kata ya Etaro ambayo ni moja ya Kata 21 za Jimbo la Musoma Vijijini.
Baadhi ya MAFANIKIO makubwa ya KISIWA cha RUKUBA ni haya hapa:
SHULE YA MSINGI RUKUBA ina:
* Wanafunzi 434
* Walimu 7
* Maktaba yenye Vitabu mbalimbali
* Vyumba vya Madarasa 10 – Vyumba 2 vinahitaji matengenezo
* Nyumba za Walimu 8 – Nyumba 2 zinahitaji matengenezo
* Wanafunzi na Walimu wanapata chakula cha mchana hapo Shuleni
UMEMEJUA (SOLAR):
Umeanza kufungwa hapo Kisiwani. Wakazi wanaomba kasi iongezeke.
MAJI YA BOMBA:
Kisiwa cha Rukuba ni moja kati ya VIJIJI 33 vilivyoko kwenye MRADI wa MAZIWA MAKUU. Serikali inajitayarisha kuanza kuutekeleza Mradi huu.
ZAHANATI YA KISIWA CHA RUKUBA
* Wafanyakazi 4
* Nyumba 1 ya Wafanyakazi (two in one)
* Maabara yenye Darubini 1
UJENZI WA WODI YA MAMA NA MTOTO
WANANCHI wa Kisiwa cha Rukuba wameamua kuongeza HUDUMA za AFYA kwenye ZAHANATI yao kwa kujenga WODI ya MAMA na MTOTO. Jengo hill lina Jumla ya VYUMBA 13 na MSINGI wake umejengwa kwa KASI KUBWA sana na kukamilika ndani ya muda wa WIKI MOJA!
WANANCHI hao wanachangia NGUVUKAZI (kusomba mawe, mchanga na maji). FEDHA zinazotumika kwa sasa ni zile za MAKUSANYO yao (20%) zinazorudishwa na HALMASHAURI yetu (Musoma DC).
MBUNGE wa JIMBO, Prof Sospeter Muhongo atachangia SARUJI MIFUKO 200 kulingana na KASI ya ujenzi wa WODI hiyo na tayari ameishachangia Saruji Mifuko 100 kufikia leo (13.6.2020).

UBORESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA VIJIJINI UNAFANYWA KWA USHIRIKIANO MZURI WA SERIKALI NA WANAVIJIJI

ujenzi unaoendelea kwenye WODI ya MAMA na MTOTO kwenye ZAHANATI ya Kijiji cha Bukima, Kata ya Bukima.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
ZAHANATI za Vijiji vya Jimbo la Musoma Vijijini ZAANZA kupanua ZAHANATI zao kwa kujenga WODI za MAMA na MTOTO
Jimbo la Musoma Vijijini lenye KATA 21 na VIJIJI 68 lina jumla ya ZAHANATI 28 (24 za Serikali na 4 za Binafsi). ZAHANATI MPYA 14 zinajengwa kwa ushirikiano wa SERIKALI na WANANCHI.
Jimbo hili lina VITUO vya AFYA 2 (Murangi & Mugango) na cha tatu (Bugwema) kitapatikana kabla ya Disemba 2020. SERIKALI, WANAVIJIJI na MBUNGE wa Jimbo hili, Prof Sospeter Muhongo, WAMECHANGIA ujenzi na uboreshaji wa MIUNDOMBINU kwenye VITUO hivi vya AFYA.
Jimbo hili litapata HOSPITALI ya Wilaya, yenye ufadhili mkubwa wa Serikali (Tsh bilioni 1.5), inayojengwa Kijijini Suguti, Kata ya Suguti. WANAVIJIJI na MBUNGE wao nao wanachangia ujenzi huu.
WODI ZA MAMA NA MTOTO
ZAHANATI 3 (Bukima, Nyegina na Kisiwa cha Rukuba) za Jimboni mwetu zimeanza ujenzi wa WODI za MAMA na MTOTO kwa lengo la kuboresha HUDUMA za AFYA zitolewazo kwenye Zahanati hizo.
UJENZI WA WODI YA MAMA NA MTOTO KWENYE ZAHANATI YA BUKIMA
Kata ya Bukima yenye Vijiji vitatu (Bukima, Butata na Kastam) ina Zahanati moja inayohudumia wakazi wote wa Vijiji hivyo.
WANANCHI wa Kijiji ya Bukima wameamua KUFUFUA ujenzi wa WODI ya MAMA na MTOTO uliosimama kwa takribani miaka minne. Uamuzi wa ujenzi huu ni muhimu sana kwani MAMA WAJAWAZITO wa Kijiji na Kata yote ya Bukima wanalazimika kutembea umbali ya zaidi ya kilomita 7 kwenda kupata matibabu kwenye Kituo cha Afya cha Murangi.
MTENDAJI  wa KIJIJI cha Bukima, Ndugu Josephat Phinias amesema WANAWAKE wamejitokeza kwa wingi kuchangia NGUVUKAZI zao kwenye ujenzi huu. WANAVIJIJI wanasomba mchanga, kokoto, mawe na maji.
Vilevile, Kiongozi huyo amesema, “Tumepokea RUZUKU ya Kijiji kutoka HALMASHAURI yetu, kiasi cha Tsh 6,075,000/= ambayo imesaidia kuharakisha ujenzi wetu.”
MGANGA MKUU wa Zahanati hiyo, Ndugu Malisha John ameeleza kuwa kukamilika kwa JENGO hilo kutasaidia kuboresha HUDUMA za AFYA ya UZAZI na ufuatiliaji wa MAKUZI ya WATOTO kwenye Kata hiyo na Kata za jirani zisizokuwa na huduma hizo.
DIWANI wa KATA, Mhe January Simula amesema WANANCHI wameamua kukamilisha ujenzi wa WODI hiyo na vilevile, ZAHANATI MPYA inaendelea kujengwa kwenye Kijiji cha Butata. Kwa hiyo, Kata ya Bukima yenye Vijiji 3 itakuwa na ZAHANATI 2 ifikapo Disemba 2020.
MICHANGO YA MBUNGE WA JIMBO
Prof Sospeter Muhongo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini AMEANZA KUCHANGIA ujenzi wa WODI ZA MAMA na MTOTO kwenye ZAHANATI zote tatu.
ZAHANATI ya Bukima imeshachangiwa SARUJI MIFUKO 100 bado mingine 100 itakayotolewa kulingana na kasi ya ujenzi huo. Mbunge huyo ameishachangia SARUJI MIFUKO 50 kwa ZAHANATI MPYA inaojengwa Kijijini Butata.
ZAHANATI ya Nyegina imeishachangiwa SARUJI MIFUKO 50, bado 150 itakayotolewa kwa utaratibu ule ule – kasi ya ujenzi.
ZAHANATI ya Kisiwa cha Rukuba imepewa SARUJI MIFUKO 50, imebaki 150. Kasi yao ya ujenzi ni kubwa.
MICHANGO YA WADAU WENGINE WA MAENDELEO
Jhpiego (Johns Hopkins Program for International Education in Gynaecology and Obstetrics,  USA) wanasaidia kutoa Huduma za Afya ya Mama na Mtoto kwa kutoa chanjo na madawa kwenye Zahanati ya Bukima na nyingine zote Jimboni mwetu.
 ICAP (International Centre for AIDS Care and Treatment Programs, USA) inatoa Huduma ya upimaji wa VVU katika jamii kwenye Zahanati ya Bukima na nyingine zote Jimboni mwetu.
AGPAHI (Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiatives, USA) inasaidia kutoa Huduma za matibabu endelevu kwa wanaoishi na VVU ndani ya Jimbo letu.
* Tunawashakuru sana WADAU hao wa MAENDELEO kwa kuendelea KUCHANGIA UBORESHAJI wa HUDUMA za AFYA Jimboni mwetu.
OMBI KUTOKA KWA WANAVIJIJI WA KATA YA BUKIMA
WANAVIJIJI wanawaomba WAZALIWA wa Kata ya Bukima washirikiane nao kwa kutoa MICHANGO ya kukamilisha WODI ya MAMA na MTOTO kwenye ZAHANATI ya Kijiji cha Bukima. Vilevile, wanaombwa wachangie ukamilishaji wa ZAHANATI MPYA inayojengwa Kijijini Butata.

SERIKALI YATOA SHILINGI MILIONI 400 KUJENGA KITUO CHA AFYA NA WANANCHI WAJIONGEZA ILI KUPATA  MIUNDOMBINU ZAIDI

WANAVIJIJI wakiwa kwenye kazi za upanuzi wa ZAHANATI ya Masinono kuwa KITUO cha AFYA cha Kata ya Bugwema.

Jumamosi, 30.5.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge.
HALMASHAURI ya Musoma (Musoma DC) ina Jumla ya VITUO VYA AFYA 2 (Murangi & Mugango) na sasa inapanua ZAHANATI ya MASINONO kiwe KITUO CHA AFYA cha Kata ya Bugwema.
WANANCHI na VIONGOZI wa Kata ya Bugwema wakiongozwa na Diwani wao, Mhe Ernest Maghembe, na Halmashauri yote wanatoa SHUKRANI nyingi na za dhati kwa SERIKALI yao kwa kutoa Tsh MILIONI 400 kwa ajili ya MRADI wa kupanua Zahanati hiyo iwe KITUO cha AFYA cha TATU ndani ya Halmashauri yetu yenye Jimbo la Musoma Vijijini.
MIUNDOMBINU YA HUDUMA ZA AFYA JIMBONI MWETU
* HOSPITALI ya WILAYA inajengwa. Serikali imetoa Tsh BILIONI 1.5. Wananchi na Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo, nao wanachangia ujenzi huu.
* VITUO vya AFYA 2 (Murangi na Muganga). Kituo cha tatu (Bugwema) kinajengwa.
* ZAHANATI 24 za Serikali na 4 za Binafsi zipo zinatoa huduma.
* ZAHANATI MPYA 14 zinajengwa kwa ushirikiano wa Serikali, Wanavijiji, Wazaliwa wa Jimboni na Mbunge wa Jimbo.
KITUO CHA AFYA KIPYA CHA BUGWEMA
Kata ya Bugwema inaundwa na Vijiji vinne: Bugwema, Kinyang’erere, Masinono na Muhoji. Vijiji hivi 4 vina ZAHANATI moja tu ya Kijijini Masinono ambayo Mbunge wa Jimbo aliipatia GARI la WAGONJWA (Ambulance).
MGANGA MFAWIDHI wa Zahanati ya Masinono, Ndugu Mzalendo Wambura, ameeleza kuwa Zahanati yao imekuwa ikitoa huduma kwa jumla ya Wagonjwa wa Nje (OP) wapatao 17,000 (elfu kumi na saba) kwa mwaka. Kwa siku moja wamekuwa wakipokea Wagonjwa wa Nje kati ya 70 na 100.
Aidha, Mganga huyo ameendelea kufafanua kuwa katika shughuli za Ujenzi wa kupanua hiyo Zahanati kuwa Kituo cha Afya, wamepanga kujenga MAJENGO SABA (7):  (i) Wodi ya Mama na Mtoto, (ii) Maabara, (iii) Jengo la Upasuaji, (iv) Jengo la Kufulia, (v) Jengo la Maiti (mortuary), (vi) Vyoo vya nje, na (vii) Miundombinu/Mfumo wa kutolea Taka. Ujenzi umeanza kwa kasi kubwa.
AFISA MTENDAJI Kata ya Bugwema, Ndugu Alphonce Nyamgambwa  amesema kuwa Wananchi wa Kata hiyo wameupokea MRADI huo kwa furaha tele na utayari mkubwa wa kuutekeleza.
WANAVIJIJI wanachangia NGUVUKAZI (kusomba maji, mawe na mchanga) na FEDHA taslimu ambapo KILA KIJIJI kitachangia jumla ya Tsh MILIONI 33.5.
WANAVIJIJI watachangia TRIPU 600 za MCHANGA na nusu yake tayari imepatikana. MAWE yanapatika kwenye kimlima jirani na Zahanati inayopanuliwa.
MICHANGO YA MBUNGE WA JIMBO
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo atachangia SARUJI MIFUKO 400 kwa MRADI huu wa Kata ya Bugwema. Mbunge huyo amechangia kiasi cha SARUJI kama hicho kwenye uboreshaji na upanuzi wa VITUO vya AFYA vya Murangi na Mugango.
Vilevile, Mbunge huyo ametoa MAGARI YA WAGONJWA (Ambulances) kwa VITUO vya AFYA vya Murangi na Mugango. Ambulance ya Murangi ni ya kisasa sana kwani UPASUAJI (operation) unaweza kufanyika ndani ya gari hilo.

ZAWADI YA EID AL FITR: PLAU 40 KWA VIKUNDI 40

Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo akitoa ZAWADI yake ya Eid al Fitr ya PLAU 40 kwa VIKUNDI 40 vya Jimbo la Musoma Vijijini. Katibu wa CCM Wilaya ya Musoma Vijijini, Ndugu Peter Francis Mashenji aliambatana na Mbunge huyo kwenye zoezi hilo la kugawa PLAU hizo lilofanyika jana (24.5.2020) Vijijini Kusenyi (Kata ya Suguti), Kwibara (Kata ya Mugango) na Mkirira (Kata ya Nyegina).

PROGRAMU YA KUBORESHA KILIMO NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI
* ZANA ZA KILIMO: Programu ya kupunguza UTUMIAJI wa JEMBE la MKONO kwenye kilimo chetu  inaendelea vizuri.
ZAWADI MUHIMU ya Eid al Fitr (2020) ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo aliyoitoa kwa WANAVIJIJI wa Jimbo letu ni PLAU 40 (MAJEMBE 40 ya kukokotwa na ng’ombe au punda).
LENGO KUU: kuongeza MATUMIZI ya PLAU badala ya JEMBE la MKONO ndani ya VIJIJI vyetu vyote 68. Hadi sasa (25.5.2020), Mbunge huyo ameishagawa bure jumla ya PLAU 85 kwa VIKUNDI 85 kutoka Vijiji vyote 68.
MGAO mwingine utafanyika wakati wa Sherehe za WAKULIMA, yaani NANENANE 2020.
Tumejiwekea MALENGO ya kuwa na PLAU zaidi ya 20 ndani ya KILA KIJIJI kwa kipindi cha Miaka 2 (2020 & 2021).
* MAZAO MAKUU YA CHAKULA: Mihogo, Mahindi, Mtama, Viazi vitamu, Mpunga, Mbogamboga na Matunda. Malengo yetu ni kuongeza UZALISHAJI kwenye MAZAO hayo ili yatumike kama MAZAO ya CHAKULA na MAZAO ya BIASHARA. Kilimo cha UMWAGILIAJI kinawekewa msisitizo mkubwa na kimeanza kuzaa matunda mazuri.
* MAZAO MAKUU YA BIASHARA: Pamba na Alizeti. Tumeongeza ZAO la ALIZETI na kwa misimu 3 mfulilizo ya Kilimo, takribani TANI 20 za MBEGU za ALIZETI zimegawawiwa bure kwa WAKULIMA ndani ya Kata zote 21. Mbunge Jimbo alichangia takribani TANI 10 na SERIKALI kupitia Wizara ya Kilimo ilichangia TANI 10.
MITAMBO 2 ya Watu Binafsi ya kukamua Mbegu za ALIZETI (viwanda vidogo) imefungwa Jimboni mwetu –  Vijijini Saragana na Kusenyi. MITAMBO mingine ya kukamua ALIZETI iko maeneo jirani, k.m. kwenye Miji ya Bunda na Musoma.

UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM (2015-2020) NA UJENZI WA OFISI YA CCM WILAYA YA MUSOMA VIJIJINI

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Mh. Prof Sospeter Muhongo akikagua ujenzi wa Ofisi ya CCM Wilaya ya Musoma Vijijini inayojengwa Kijijini Murangi.

TAARIFA ZA UTEKELEZAJI WA ILANI: Jimbo la Musoma Vijijini
VOLUME I:
(Jan 2016-Juni 2020)
Ilichapishwa tarehe 7.7.2019, Kurasa 110, Rangi, Nakala 5,000 (elfu tano), zimegawiwa bure
VOLUME II:
(Julai 2019-Juni 2020), itachapishwa tarehe 30 Juni 2020
NAKALA KWENYE TOVUTI YA JIMBO
Tovuti:
Volume I: ipo
Volume II: itawekwa
UJENZI WA OFISI YA CCM WILAYA YA MUSOMA VIJIJINI
Leo, Jumamosi, 23.5.2020, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo AMEKAGUA UJENZI wa Ofisi hiyo inayojengwa Kijijini Murangi.
Maendeleo ya ujenzi ni MAZURI na hadi kufikia hatua hiyo ya ujenzi, Mbunge huyo ameishachangia Tsh MILIONI 12 (Milioni kumi na mbili).
SHUKRANI nyingi zinatolewa kwa KAMATI ya UJENZI kwa usimamizi mzuri wa Mradi huu. Kamati hiyo inaongozwa na Mkuu wa Wilaya (DC) ya Musoma, Dr Vicent Naano Anney.
Vilevile, SHUKRANI nyingi zinatolewa kwa WACHANGIAJI wengine wa Mradi huu (Kamati ya Ujenzi inayo majina ya wachangiaji wote)

 WANAVIJIJI WAAMUA KUJENGA VYUMBA VIPYA 5 VYA MADARASA NA SERIKALI YACHANGIA UJENZI HUO

MAFUNDI wakiwa kwenye kazi za ujenzi wa VYUMBA VIPYA vya Madarasa ya S/M BWASI B ya Kijiji cha Bwasi, Kata ya Bwasi.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
UBORESHAJI wa MIUNDOMBINU ya ELIMU umetiliwa MKAZO mkubwa sana Mkoani Mara. UBORESHAJI huu umebainika kuwa njia mojawapo ya KUINUA KIWANGO cha UBORA wa ELIMU ndani ya Mkoa huu.
HALMASHAURI ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC) imechanga Tsh MILIONI 5 kwa ajili ya ujenzi wa VYUMBA VIPYA 5 kwenye S/M BWASI B.
S/M BWASI B iko Kijijini Bwasi ndani ya Kata ya Bwasi. Shule hii ilianza Mwaka 2015, ina jumla ya WANAFUNZI 512 na WALIMU 7.
MWALIMU MKUU wa Shule hii, Mwl Masilingi Maira amesema Shule ina VYUMBA 4 vya Madarasa huku MAHITAJI ni VYUMBA 8. Kwa hiyo, WANAFUNZI wa Madarasa 3 WANASOMEA chini ya MITI, huku Darasa moja likiwa na MRUNDIKANO wa WANAFUNZI 118.
MTENDAJI wa Kijiji cha Bwasi, Ndugu Gabriel Chacha ameeleza kwamba, kwa sasa, WANAKIJIJI   wamekubali na kuhamasika KUTATUA MATATIZO SUGU la kutokuwepo Vyumba vya Madarasa na Ofisi za Walimu za kutosha Shuleni hapo.
KIONGOZI huyo amesema WANANCHI wameanza ujenzi wa VYUMBA VIPYA 5 vya Madarasa na OFISI 3 za WALIMU. Mbali ya kuchangia NGUVUKAZI zao (kusomba mawe, mchanga na maji ya ujenzi), WANAVIJIJI hao wanachangia Tsh 14,000/= kutoka kila KAYA.
SERIKALI ya Kijiji cha Bwasi IMECHANGIA fedha za kununua MBAO za UPAUAJI wa VYUMBA VIPYA 4 vya Madarasa na HALMASHAURI yetu (Musoma DC) imechangia Tsh MILIONI 5 kwa ajili ya UPAUAJI huo  – HONGERENI sana VIONGOZI wa Serikali ya Kijiji cha Bwasi na VIONGOZI wa HALMASHAURI yetu.
WANANCHI wa KIJIJI cha BWASI na Kata nzima ya Bwasi WANATOA SHUKRANI nyingi sana kwa:
PCI (Project Concern International, USA) kwa kujenga vyoo, tanki la maji na kuwezesha MRADI wa CHAKULA cha Wanafunzi kwenye S/M Bwasi B na nyingine ndani ya Kata ya Bwasi – Ahsante sana PCI.
BMZ (The Federal Ministry of Economic Development and Cooperation, Germany)  – Mradi huu umetoa madaftari, kalamu, mabegi ya kubebea vifaa vya shule, miwani na matibabu maalumu kwa WANAFUNZI wenye ULEMAVU kwa Shule zote za msingi ndani ya Kata ya Bwasi –  Ahsante sana BMZ.
MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo ametoa MICHANGO ifuatavyo:
(i) S/M BWASI B:
Saruji Mifuko 70, Madawati 36, Vitabu vingi vya Maktaba
(ii) S/M BWASI:
Saruji Mifuko 50, Madawati 39 na Vitabu vingi vya Maktaba.
OMBI KUTOKA KWA WANAKIJIJI wa Kijiji cha Bwasi
WAZALIWA wa  Kijiji cha Bwasi na WADAU wengine wa MAENDELEO wanaombwa kuchangia MABATI 162 ili UPAUAJI wa VYUMBA VIPYA vya Madarasa UKAMILIKE kabla ya WANAFUNZI kurudi Shuleni hapo (S/M Bwasi B) kuendelea na masomo yao.

KATA YA BWASI YAENDELEA KUBORESHA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

baadhi ya WANAKIKUNDI cha NO SWEAT NO SWEET wakiwa kazini kwenye MASHAMBA yao ya MPUNGA na MATIKITI Kijijini Bugunda, Kata ya Bwasi.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
KATA ya BWASI ina Vijiji 3 ambavyo ni Bugunda, Bwasi na Kome. Vijiji 2 –  Bugunda na Bwasi viko kwenye mwambao wa Ziwa Victoria.
KIKUNDI cha NO SWEAT NO SWEET cha Kijiji cha Bugunda kinajishughulisha na KILIMO cha BUSTANI (nyanya, vitunguu na matikiti)  na KILIMO cha MAZAO ya CHAKULA na BIASHARA (mahindi, maharage, viazi lishe na mpunga)
KATIBU wa KIKUNDI hicho, Ndugu Daudi Silas ameeleza kwamba kwa sasa HAWASUBIRI MVUA KUNYEESHA kwani KILIMO chao ni cha UMWAGILIAJI hata kwenye kilimo cha MPUNGA.
KIKUNDI hiki kina MASHINE 2 za UMWAGILIAJI. Mashine ya kwanza ilinunuliwa kwa kutumia FEDHA za MFUKO wa JIMBO na Mashine ya pili WAMEJINUNULIA WENYEWE  – hongereni sana Wanachama wa NO SWEAT NO SWEET!
Vilevile, KIKUNDI hiki tayari kimenunua NG’OMBE 2 kwa ajili ya KILIMO cha kutumia PLAU. Mbunge wao, Prof Sospeter Muhongo amekubali maombi yao ya kupewa PLAU (jembe la kukokotwa na ng’ombe) ikiwa ni ZAWADI ya EID al FITR
MBUNGE huyo ATAGAWA BURE PLAU 40 ikiwa ni ZAWADI yake ya EID al FITR (2020) kwa VIKUNDI 40 kutoka VIJIJI 40 vya Jimbo la Musoma Vijijini. MGAO huo wa tatu utafikisha jumla ya PLAU 85 ambazo Mbunge huyo atakuwa amegawa bure kwenye VIKUNDI 85 vya Jimbo la Musoma Vijijini lenye Vijiji 68 – PROGRAMU hii ya UBORESHAJI wa KILIMO Jimboni humo ni ENDELEVU!
Kwa sasa, WANACHAMA wa KIKUNDI CHA KILIMO cha NO SWEAT NO SWEET wanasomesha watoto wao bila matatizo na wameanza kujenga bora za kisasa za kuishi – hongereni sana ndugu zetu kwa MAFANIKIO hayo.
KIKUNDI cha KILIMO cha JIPE MOYO cha Kijijini Kome kinaendelea kuboresha kilimo chao kwa kutumia PLAU waliyopewa na Mbunge wao, Prof Sospeter Muhongo.
AFISA KILIMO wa Kata ya Bwasi, Ndugu Alex Mihambo anaendelea KUSHAWISHI na KUHAMASISHA Wanavijiji waunde VIKUNDI vya KILIMO kurahisisha UTOAJI wa MAFUNZO ya KILIMO na utafutaji wa MASOKO ya MAZAO yao.
SHUKRANI kutoka kwa VIKUNDI VYA KILIMO vya Vijiji vya Bugunda na Kome zinapelekwa kwa:
* SERIKALI yetu kwa kuwapatia WATAALAMU wa KILIMO walioko kwenye Halmashauri yetu.
* PCI (Project Concern International, USA) kwa kutoa bure MBEGU za MAHINDI kwa Kikundi cha JIPE MOYO cha Kijijini Kome. PCI imepanga kukipatia Kikundi hiki MASHINE ya UMWAGILIAJI.
* MBUNGE wa JIMBO, Prof Sospeter Muhongo kwa kugawa bure ZANA za KILIMO (plau na mashine ya umwagiliaji) na MBEGU za MIHOGO, MTAMA na ALIZETI kwa Wakulima wa Kata ya Bwasi.

WANAKIJIJI WANAJENGA MAKTABA, VYUMBA VIPYA VYA MADARASA NA OFISI YA WALIMU KWA WAKATI MMOJA

WANAVIJIJI wakiwa kwenye ujenzi wa MAKTABA ya S/M BUTATA, Kijijini Butata. Kata ya Bukima. Ujenzi huo umepangwa kukamilika kabla ya tarehe 15 Juni 2020.

USHIRIKIANO MZURI kati ya WANANCHI, SERIKALI, VIONGOZI wa Kata na Kijiji, na WADAU wa MAENDELEO unazaa matunda mazuri kwenye ujenzi na uboreshaji wa MIUNDOMBINU ya ELIMU kwenye Kijiji cha Butata, Kata ya Bukima.
WANAKIJIJI wa Kijiji cha Butata wanachangia NGUVUKAZI (kusomba mchanga, mawe, kokoto na maji) na Tsh 4,000 (elfu nne) kutoka kila KAYA kwenye ujenzi wa MAKTABA, VYUMBA 2 VIPYA vya MADARASA na OFISI 1 ya WALIMU ya S/M BUTATA. DIWANI wao, Mhe January Simula amechangia Saruji Mifuko 5. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji, Ndugu William Kugosora – HONGERENI SANA WANA-BUTATA!
Leo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo amechanga SARUJI MIFUKO 50 na kukamilisha AHADI yake ya SARUJI MIFUKO 100 kwa ajili ya ujenzi unaondelea Shuleni hapo.
Baada ya kukamilika kwa MAKTABA ya Shule hiyo, Mbunge huyo ataiongezea Shule hiyo VITABU vingine vya MAKTABA.
Leo, PCI (Plan Concern International),  IMETHIBITISHA AHADI yake ya kukamilisha ujenzi wa MAKTABA hiyo kama ifuatavyo: kuezeka jengo, kukamilisha jengo ndani na nje (finishing) na kuweka samani za maktaba – AHSANTE SANA PCI!
WADAU wengine wa MAENDELEO wanaochangia UJENZI kwenye Shule hiyo ni: Ndugu Samson Masawa (USA) na Ndugu Muya Essero – hawa ni WAZALIWA wa Kijiji cha Butata  – AHSANTENI SANA!
MWALIMU MKUU wa Shule hiyo,  Mwl Yohani Dawi amesema kwamba FEDHA zitokazo SERIKALINI kwa ajili ya ukarabati wa MIUNDOMBINU zimechangia sana ujenzi huu. Vilevile, HALMASHAURI yetu inakusudia kuchangia ujenzi huu  – AHSANTE SANA SERIKALI na HALMASHAURI yetu!
DIWANI wa Kata ya Bukima yenye VIJIJI 3 vya Butata, Kastamu na Bukima, Mhe January Simula ANAWASHUKURU sana WANANCHI wa Kijiji cha Butata kwa kupata ARI MPYA ya kukamilisha MIRADI ya ujenzi wa MAKTABA, VYUMBA vipya vya Madarasa, OFISI ya Walimu, ZAHANATI, OFISI ya Kijiji na Shule MPYA ya Msingi.
DIWANI huyo ameishukuru sana SERIKALI na HALMASHAURI yetu kwa kuendelea kuchangia UBORESHAJI wa MIUNDOMBINU ya ELIMU kwenye Kata ya Bukima.
WADAU wengine wa Maendeleo kwenye SEKTA ya ELIMU ndani ya Kata hiyo ni: PCI, USA (vitabu, ujenzi wa vyoo, matenki ya maji, kilimo cha chakula cha wanafunzi,  na mafunzo mbalimbali), BMZ, Ujerumani (vifaa vya elimu kwa wanafunzi wenye ulemavu), na baadhi ya WAZALIWA wa Kata ya Bukima.
MBUNGE wa JIMBO, Prof Sospeter Muhongo ametoa MICHANGO mingi kwenye SEKTA ya ELIMU ndani ya Kata hiyo ikiwemo ya: (i) Madawati kwa Shule zote za Msingi, (ii) Vitabu vya Maktaba kwa Shule zote za Msingi na Sekondari (iii) Saruji na Mabati.
MFUKO wa JIMBO nao umechangia Saruji na Mabati kwenye Sekta ya Elimu ndani ya Kata ya Bukima.
KARIBUNI TUCHANGIE UJENZI na UBORESHAJI wa MIUNDOMBINU YA ELIMU KWENYE KATA YA BUKIMA

UJENZI WA SHULE MPYA SHIKIZI KUTATUA MATATIZO YA UMBALI MREFU WA KUTEMBEA NA MIRUNDIKANO   MADARASANI

WANANCHI na VIONGOZI wao wa Kijiji cha Buanga, Kata ya Rusoli wakiendelea na UJENZI wa VYUMBA vya MADARASA ya SHULE SHIKIZI yao.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
KIJIJI cha BUANGA cha Kata ya RUSOLI kina Jumla ya VITONGOJI 9 na SHULE za MSINGI 2 (S/M Bwenda na S/M Bwenda B).
MWALIMU MKUU wa S/M Bwenda B, Mwl Christopher Cosmas  amesema Shule hiyo iliyofunguliwa Mwaka 2015 ina jumla ya WANAFUNZI 482, VYUMBA vya MADARASA 4 na inao UPUNGUFU wa Vyumba 5 vya Madarasa. Kwa hiyo MADARASA 4 yanasomea CHINI ya MITI na kipo Chumba cha Darasa kina WANAFUNZI 99.
MATATIZO ya UMBALI MREFU wa kutembea na MIRUNDIKANO madarasani ya WANAFUNZI wa kutoka VITONGOJI 9 vya Kijiji cha Buanga,  yamewalazimisha WANANCHI WAAMUE kuyatatua kwa kujenga SHULE SHIKIZI MPYA kwenye KITONGOJI cha CHIRUGWE.
MWENYEKITI wa Kijiji cha Buanga, Ndugu Kejile Eyembe amesema WATOTO WAO wanatembea umbali wa KILOMITA 5 kwenda masomoni kwenye Shule Mama ya Bwenda (S/M Bwenda & S/M Bwenda B). Kwa hiyo, WAMEAMUA kujenga Shule MPYA, yaani SHULE SHIKIZI na WANANCHI WAMEKUBALIANA kuchanga Tsh 10,000 (elfu kumi) kutoka kila KAYA, na tayari ujenzi umeanza.
DIWANI wa Kata ya RUSOLI, Mhe Boaz Nyeula amesema UJENZI wa SHULE hiyo unachangiwa na NGUVUKAZI na FEDHA za WANAKIJIJI, na WADAU wengine wa MAENDELEO wakiwemo WAZALIWA wa Kijiji cha Buanga.
MALENGO ya UJENZI ni kukamilisha VYUMBA 7 vya MADARASA, OFISI 1 ya Walimu na VYOO vya Wanafunzi na Walimu.
SHUKRANI KUTOKA KIJIJI CHA BUANGA
Wananchi na Viongozi wa Kijiji cha Buanga wakiongozwa na Diwani wao huyo wanatoa SHUKRANI nyingi kwa:
* SERIKALI na HALMASHAURI yake kwa kushirikiana na WANANCHI kujenga na kuboresha MIUNDOMBINU ya Shule za Msingi za Kijiji cha Buanga na Kata yao yote ya Rusoli.
* PLAN CONCERN INTERNATIONAL (PCI) kwa kujenga VYOO, kugawa VITABU na CHAKULA kwa Wanafunzi.
* MBUNGE wa JIMBO, Prof Sospeter Muhongo kwa MICHANGO yake ya:
(i) S/M Bwenda –
Madawati 92, Saruji Mifuko 60 na Vitabu vingi vya Maktaba
(ii) S/M Bwenda B –
Madawati 70, Saruji Mifuko 60, Mabati 50 na Vitabu vingi vya Maktaba
(iii) Shule SHIKIZI inayojengwa: SARUJI MIFUKO 100.
OMBI KUTOKA KWA WANAKIJIJI
WAZALIWA wa Kijiji cha Buanga na Kata ya RUSOLI wanaombwa WAJITOKEZE KUCHANGIA UJENZI wa SHULE SHIKIZI ya Kijiji cha Buanga iliyopangwa kufunguliwa mwakani (Januari 2021).
SHULE ZA MSINGI NDANI YA JIMBO LETU
HALMASHAURI ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC) na JIMBO lake la Musoma Vijijini (Vijiji 68, Kata 21) ina jumla ya:
* Shule za Msingi za Serikali 111
* Shule za Msingi za Binafsi 3
* Shule Shikizi 11 (nyingine zimeishafunguliwa na nyingine zinakamilisha ujenzi)
* MAKTABA kwenye Shule za Msingi zipo chache na ujenzi unaendelea.

WANAVIJIJI WAENDELEA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI, PCI NA CRDB KUBORESHA MIUNDOMBINU YA SHULE ILIYOFUNGULIWA MWAKA 1956

baadhi ya WANANCHI wa KIJIJI cha KIEMBA, Kata ya Ifulifu wakiwa kwenye kazi za ujenzi wa MIUNDOMBINU ya S/M MURUNYIGO

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
WANAKIJIJI cha Kijiji cha Kiemba, Kata ya Ifulifu wameendelea kushirikiana na WADAU wa MAENDELEO kuboresha MIUNDOMBINU ya SHULE YA MSINGI MURUNYIGO iliyofunguliwa Mwaka 1956.
Hivi karibuni BENKI ya CRDB imechangia ukamilishaji wa ujenzi wa chumba kimoja cha DARASA kwenye Shule hiyo.
MWALIMU MKUU wa Shule hiyo, Mwl Grace Majinge amesema kwamba jumla ya WANAFUNZI Shuleni hapo ni 846, na mahitaji ya VYUMBA vya MADARASA ni 21, vilivyopo ni 9 na UPUNGUFU ni 12.
BENKI ya CRDB imechangia kupunguza UPUNGUFU huo kwa kutoa VIFAA vya UJENZI vya kukamilisha CHUMBA kimoja (1) cha DARASA.
AFISA MTENDAJI wa Kijiji hicho, Ndugu Regina Mafuru Chirabo ameorodhesha VIFAA vilivyochangwa na CRDB kuwa ni: SARUJI MIFUKO 60, RANGI NDOO 2 na KOPO 1, SQUARE PIPE 5, FLAT BAR 10, SHEET 1, KOMEO na BAWABA.
AFISA MTENDAJI huyo na WANANCHI wa Kijiji cha Kiemba na VIONGOZI wengine, wakiwemo DC, DED na MBUNGE wa Jimbo WAMEISHUKURU sana BENKI ya CRDB kwa MCHANGO huo na kwa pamoja wameahidi kukamilisha ujenzi huo kabla ya tarehe 30 Mei 2020.
MWENYEKITI wa Serikali ya Kijiji cha  Kiemba, Ndugu  Rocket Mauna Rukiko ameungana na WANAKIJIJI wenzake KUSHUKURU WADAU wengine wa MAENDELEO waliokwishachangia UJENZI kwenye Shule hiyo, ambao ni: SERIKALI, PCI na MBUNGE wa JIMBO lao.
SERIKALI inaendelea kugharamia UBORESHAJI wa Elimu kwenye Shule hiyo. MRADI wa EQUIP wa SERIKALI yetu nao umechangia sana UBORESHAJI wa Elimu Shuleni hapo.
PROJECT CONCERN INTERNATIONAL (PCI) imejenga VYOO vya S/M Murunyigo. Imetoa CHAKULA cha WANAFUNZI, VITABU, ELIMU ya AFYA na inaendelea kuchangia UBORESHAJI wa ELIMU kwenye Shule hiyo.
MBUNGE wa JIMBO la Musoma Vijijini,  Prof Sospeter Muhongo amechangia Shule hiyo ifuatavyo: SARUJI MIFUKO 60, MADAWATI 106 na VITABU vingi vya MAKTABA.
OMBI KUTOKA KWA WANAVIJIJI
KIJIJI cha Kiemba, Kata ya Ifulifu kinawaomba WADAU wa MAENDELEO wakiwemo WAZALIWA wa Kijiji na Kata hiyo KUCHANGIA ujenzi wa Miundombinu ya Shule yao ya Msingi iliyoanzishwa Mwaka  1956.

UTUMIAJI WA MAJEMBE YA KUKOKOTWA NA NG’OMBE (PLAU) WAONGEZA UFANISI KWENYE KILIMO VIJIJINI

WANAKIKUNDI cha KILIMO KWANZA wakiandaa SHAMBA la DENGU (kwa kutumia PLAU badala ya JEMBE la MKONO) kijijini kwao Lyasembe, Kata ya Murangi.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo anatekeleza PROGRAMU ya UBORESHAJI wa KILIMO Jimboni humo kwa KUCHANGIA UPATIKANAJI wa PLAU na MBEGU BORA za mazao mbalimbali.
VIKUNDI VYA KILIMO vimeanzishwa ndani ya VIJIJI vyote 68 na tayari vimeanza kugawiwa PLAU huku MBEGU bora za MAZAO ya ALIZETI, MIHOGO, MTAMA na UFUTA zilianza kugawiwa na MBUNGE huyo tokea Mwaka 2016.
VIKUNDI VYA KILIMO VYA KATA YA MURANGI
DIWANI wa Kata ya Murangi, Mhe Kujerwa Simion Kujerwa amesema Kata hiyo ina VIJIJI viwili (Lyasembe na Murangi) na hadi sasa vipo VIKUNDI 15 vya KILIMO ambayo vinajishughulisha na KILIMO cha BUSTANI za mbogamboga, matunda na mazao mengine.
DIWANI huyo ameeleza kwamba VIKUNDI vya KILIMO 2 viitwavyo KILIMO KWANZA (cha Kijiji cha Lyasembe) na IFAD (cha Kijiji cha Murangi) VIMEGAWIWA PLAU za Mbunge wa Jimbo. Aliongeza kwa kusema kwamba KIKUNDI cha WANAWAKE kiitwacho TUPENDANE (cha Kijiji  cha Lyasembe) kilipewa MASHINE ya UMWAGILIAJI, mbegu na dawa za mimea.
KIKUNDI cha KILIMO KWANZA cha Kijijini Lyasembe kilianzishwa Mwaka 2018 kikiwa kinatumia MAJEMBE ya MKONO, na sasa kinatumia  JEMBE la kukokotwa na NG’OMBE walilogawiwa na MBUNGE wao wa Jimbo – hayo yamesemwa na Ndugu MANYAMA MAKUYU ambae ni Mwenyekiti wa Kikundi hicho chenye WANACHAMA 16 wanaojishughulisha na KILIMO cha MAHINDI na DENGU.
WANACHAMA wa Kikundi hicho wanamshukuru sana MBUNGE wao wa Jimbo kwa kuwaboreshea UFANISI kwenye KILIMO chao.
PROGRAMU ya kuongeza MATUMIZI ya PLAU ndani ya JIMBO la Musoma Vijijini INAENDELEA KUTEKELEZWA kwa mpangilio mzuri unawaohamasishwa na kushirikisha WANAVIJIJI wenyewe. MBUNGE wa Jimbo ameishagawa PLAU 45 na atagawa tena PLAU 40 wakati wa Sikukuku ya Eid al Fitr, tarehe 24 Mei 2020
Zoezi la UGAWAJI wa PLAU (zana bora kuliko jembe la mkono) ndani ya VIJIJI 68 vya Jimbo la Musoma Vijijini ni ENDELEVU na ni sehemu ya MPANGO wa UBORESHAJI wa KILIMO ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.

SHULE YENYE WANAFUNZI 187 KWENYE CHUMBA KIMOJA CHA DARASA YACHANGIWA KUJENGA VYUMBA VIPYA VYA MADARASA

Kazi za ujenzi zinazofanyika kwenye S/M NYAMIYENGA ya Kijijini Bwai Kumusoma, Kata ya Kiriba.

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
MIUNDOMBINU ya ELIMU inaendelea KUJENGWA na KUBORESHWA kwenye SHULE ZOTE za  MSINGI (111 za Serikali, 3 za Binafsi na 11 Shule Shikizi), na SEKONDARI (20 za Serikali, 2 za Binafsi na 5 Mpya zinajengwa) ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.
UJENZI na UBORESHAJI huo UNATEKELEZWA kwa USHIRIKIANO wa WANANCHI na SERIKALI yao.
SHULE YA MSINGI NYAMIYENGA
Shule hii ilifunguliwa Mwaka 2016 na iko kwenye Kijiji cha Bwai Kumusoma, Kata ya Kiriba.
S/M NYAMIYENGA ina Jumla ya WANAFUNZI 411 (Awali hadi Darasa la V) na WANAFUNZI 187 wa Darasa la III WAMERUNDIKANA kwenye Chumba kimoja cha Darasa. Walimu (jumla ni 6) hawana Ofisi na hawana Vyoo vyao.
KUTATUA MATATIZO YA S/M NYAMIYENGA
MWALIMU Heriel Joseph ambaye ni Mwalimu Mkuu Msaidizi wa S/M Nyamiyenga amesema kuwa HAKIPO CHUMBA CHA DARASA kwa ajili ya Darasa la VI litakalopanda kutoka Darasa la V mwakani (Januari 2021)
WANANCHI wa Kijiji cha Bwai Kumusoma   WAMEAMUA kutatua  MATATIZO hayo kabla ya kufika tarehe 30 Julai 2020.
* Kwa sasa KAMATI ya UJENZI ya Shule hiyo inasimamia UJENZI wa VYUMBA VIPYA 3 vya Madarasa, OFISI ya WALIMU na CHOO yenye MATUNDU 10.
 MICHANGO YA KUKAMILISHA UJENZI
* WANAVIJIJI wanachangia NGUVUKAZI (kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji) na FEDHA Taslimu (Tsh 5,000 kwa kila mwenye umri wa zaidi ya miaka 18) – haya yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi, Ndugu Sikudhani Juma Maanya.
* HALMASHAURI yetu ulishachangia Tsh Milioni 4.
* MBUNGE WA JIMBO leo (23.4.2020) amechangia SARUJI MIFUKO 50. Hapo awali alishachangia SARUJI MIFUKO 60, MADAWATI 65 na VITABU 1,000 vya MAKTABA.
OMBI KUTOKA KWA WANAVIJIJI
WADAU wa MAENDELEO wakiwemo WAZALIWA wa KATA YA KIRIBA wanaombwa KUCHANGIA UJENZI wa MIUNDOMBINU ya ELIMU kwenye S/M NYAMIYENGA.

SHULE ZA MSINGI ZA MUSOMA VIJIJINI ZAANZA KUJENGA MAKTABA

MAKTABA ya S/M RUKUBA

UBORESHAJI WA kiwango cha ELIMU ndani ya JIMBO la Musoma Vijijini na HALMASHAURI yake UNAENDELEA kwa KUJENGA na KUBORESHA MIUNDOMBINU ya ELIMU kwa SHULE zote za Msingi na Sekondari.
Mbali ya kuwepo MIRADI ya ujenzi wa  VYUMBA VIPYA vya MADARASA kwenye SHULE za MSINGI za SERIKALI (jumla: 111 za Msingi & 11 Shikizi), UJENZI WA MAKTABA UMEANZA kutiliwa mkazo.
MAKTABA MPYA KWENYE SHULE ZA MSINGI
S/M RUKUBA ya Kisiwani Rukuba ndiyo ya kwanza kujengwa na kuanza kutumiwa. Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo,  ameweka VITABU VINGI vya kutumiwa na WANAFUNZI, WALIMU, WAKAZI na WAGENI wa hapo Kisiwani.
WANANCHI wa Kisiwani Rukuba na baadhi ya WADAU wao wa Maendeleo WALICHANGIA ujenzi wa MAKTABA hiyo. Mbunge wa Jimbo alichangia MABATI 57 ya kuezekea Jengo la MAKTABA hiyo.
MAKTABA MPYA ZINAZOJENGWA
MAKTABA za S/M BURAGA (Kijiji cha Buraga, Kata ya Bukumi) na S/M BUIRA (Kijiji cha Buira, Kata ya Bukumi) zinajengwa kwa kutumia MICHANGO ya  WANAVIJIJI wenyewe. MICHANGO ya kukamilisha MIRADI hii ya ujenzi inakaribishwa.
BAADHI ya SHULE ZA MSINGI za Jimboni mwetu, k.m. S/M BUSEKELA na S/M RUSOLI zimetumia MAJENGO yaliyopo Shuleni mwao kutengeneza MAKTABA za SHULE zao. Mbunge wa Jimbo amegawa VITABU VINGI vya MAKTABA kwa SHULE ZOTE za Msingi na Sekondari za Jimbo la Musoma Vijijini.
MATOKEO MAZURI yaanza kuonekana ambapo MWAKA JANA (2019) HALMASHAURI ya WILAYA ya MUSOMA (Musoma DC) yenye JIMBO la Musoma Vijijini ILIKUWA YA KWANZA MKOANI MARA kwenye Mitihani ya Darasa la Nne (IV).
KARIBUNI TUJENGE MAKTABA KWENYE SHULE ZETU

SEKONDARI MPYA ILIYOFUNGULIWA MWAKA HUU (2020) YAJITAYARISHA KUPOKEA WANAFUNZI WAPYA MWAKANI (2021)

AWAMU YA PILI ya ujenzi wa MIUNDOMBINU ya Busambara Sekondari ya Kata ya Busambara Inaendelea vizuri.

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
BUSAMBARA SEKONDARI ya Kata ya Busambara imefunguliwa Januari 2020 na inao WANAFUNZI 130 wa KIDATO cha KWANZA ambao wana VYUMBA 3 vya MADARASA na kila Mwanafunzi analo DAWATI lake na KITI chake – HAKUNA MIRUNDIKANO MADARASANI –  SHUKRANI nyingi ziende kwa Benki ya NMB kwa kuchangia Madawati na Viti hivyo.
WANANCHI wa VIJIJI 3 vya Kata ya Busambara (VIJIJI: Kwikuba, Maneke na Mwiringo), wameanza UJENZI MPYA kwa ajili ya  kupokea WANAFUNZI wa KIDATO cha KWANZA mwakani (Januari 2021)
WAZALIWA wa VIJIJI  hivyo WANAENDELEA KUCHANGIA ujenzi wa SEKONDARI ya Kata yao.
AFISA MTENDAJI wa Kata ya Busambara, Ndugu Victor Kasyupa ameeleza kuwa SEKONDARI hiyo mwakani (Januari 2021) inataraji kupokea WANAFUNZI 270 wa KIDATO cha KWANZA (2021).
Kwa hiyo, SEKONDARI hiyo ina MAHITAJI ya VYUMBA VIPYA 7 vya MADARASA. Kipo chumba kimoja,  na vinahitajika 6 vingine.
MGAWANYO WA KAZI VIJIJINI ni kama ifuatavyo:
(i) KIJIJI CHA MANEKE:
* Kumalizia Boma la Vyumba 2 vya Madarasa
(ii) KIJIJI CHA KWIKUBA:
* Kuanza ujenzi wa Vyumba 2 vya Madarasa. Tayari wameanza kufyatua MATOFALI kwa kutumia SARUJI MIFUKO 50 iliyotolewa na Ndugu JUMA RAMADHAN, Mzaliwa wa Kijiji hicho – Tunamshukuru sana ndugu yetu huyu kwa MCHANGO wake.
(iii) KIJIJI CHA MWIRINGO:
* Kuanza ujenzi wa Vyumba 2. Tayari wameishanza kusomba mchanga.
UCHANGIAJI WA AWAMU YA KWANZA ya ujenzi wa BUSAMBARA SEKONDARI ulikuwa hivi:
(i) WANAVIJIJI
* Nguvukazi na Fedha Taslimu vyenye thamani ya Tsh 45M – HONGERENI SANA WANAVIJIJI.
(ii) FEDHA ZA SERIKALI KUU: Tsh 37.5M – SHUKRANI NYINGI KWA SERIKALI YETU.
(iii) HALMASHAURI: mbali ya kusimamia MANUNUZI ya Fedha za MFUKO wa JIMBO, Halmashauri yetu ilichangia MASINKI 14 na Fedha Taslimu Tsh 2M – Tunamshukuru sana MKURUGENZI wetu (Ndugu John Kayombo) na WAFANYAKAZI wote wa HALMASHAURI yetu.
(iv) MBUNGE WA JIMBO, Prof Sospeter Muhongo,  alichangia:
* SARUJI MIFUKO 150
* MABATI BANDO 8 (Mabati 112)
* RANGI ya kupaka Vyoo vyote
* VITABU vya Maktaba
MFUKO wa JIMBO ulichangia:
 * SARUJI MIFUKO 365
* NONDO 100
(v) WATAALAMU NGAZI YA KATA: walichangia SARUJI MIFUKO 10 – AHSANTENI SANA!
(vi) WAZALIWA 13 wa VIJIJI hivyo WALIOCHANGA kati ya Tsh 1.2M na 100,000 ni: Diwani (Chadema, amejiuzulu), Mhe Ngero Antony Kibuyu, Mwenyekiti wa Wazazi (W) Ndugu Phares Nguruti, ACP Sulemain Nyakulinga, Ndugu Joseph Chikongoye, Wakili Saidi Chiguma, Simon Songe, James Nyamanda, Alfaxad Kajanja, Obadia Nyangiro, Nyetango Kajanja, Monica Chikongoye, P Maregesi, Masondore Isarael na Michael Saire – AHSANTENI SANA!
WALIMU 2 WA KUJITOLEA: Ndugu Joseph Chikongoye,  Wakili Saidi Chiguma, Ndugu Richard Cheumbe na Thadeo Makindu WANACHANGIA POSHO za kila Mwezi za Walimu hao – AHSANTENI SANA KWA KUCHANGIA POSHO ZA WALIMU WETU!
MICHANGO YA AWAMU YA PILI YA MBUNGE WA JIMBO
MWEZI UJAO (Mei, 2020), Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ATAANZA KUCHANGIA AWAMU ya PILI ya UJENZI kwa Sekondari Mpya 2 zilizofunguliwa Januari 2020, ambazo ni: Busambara Secondary School (Kata ya Busambara) na Dan Mapigano Memorial Secondary School (Kata ya Bugoji).
OMBI KUTOKA KWA WANAVIJIJI:
TUENDELEE KUCHANGIA UJENZI WA BUSAMBARA SEKONDARI

MATATIZO SUGU YA MIRUNDIKANO MADARASANI NA UMBALI MREFU WA KUTEMBEA YAENDELEA KUTATULIWA MUSOMA VIJIJINI

Ujenzi wa SEKA SEKONDARI ya Kata ya Nyamrandirira. Hii ni Sekondari ya pili ya Kata hiyo.

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
JIMBO la Musoma Vijijini na HALMASHAURI yake (Musoma DC) linaendelea kutatua MATATIZO SUGU ya Mirundikano Madarasani na Umbali mrefu wa kutembea kwa WANAFUNZI na WALIMU. Utatuzi huu unafanywa kwenye SHULE zote za Msingi na Sekondari.
SEKONDARI ZILIZOPO
*Sekondari 20 za Serikali/Kata
*Sekondari 2 za Binafsi
*Sekondari MPYA zinazojengwa na ZITAFUNGULIWA Januari 2021ni:
(i) Kigera (inajengwa na Vijiji vya Kakisheri na Kigera, Kata ya Nyakatende – Sekondari ya PILI ya Kata)
(ii) Nyasaungu (inajengwa na Kijiji cha Nyasaungu, Kata ya Ifulifu – Sekondari ya KWANZA ya Kata)
(iii) Ifulifu (inajengwa na Kijiji cha Kabegi, Kata ya Ifulifu – Sekondari ya PILI ya Kata)
(iv) Nyegina (inajengwa na Vijiji vyote 3 vya Kata ya Nyegina – Sekondari ya PILI ya Kata), na
(v) Seka (inajengwa na Vijiji vyote 5 vya Kata ya Nyamrandirira – Sekondari ya PILI ya Kata)
Kwa hiyo ifikapo Januari 2021, JIMBO la Musoma Vijijini lenye Kata 21 na Vijiji 68 litakuwa na:
(i) SEKONDARI 25 za Serikali/Kata
(ii) SEKONDARI 2 za Binafsi
UJENZI WA KUSHIRIKISHA WANANCHI
Ujenzi wa SEKONDARI hizo MPYA unaendeshwa kwa USHIRIKIANO wa: SERIKALI na HALMASHAURI yake (Musoma DC), WANAVIJIJI, MBUNGE wa JIMBO, WAZALIWA (baadhi) wa KATA zinazojenga na WADAU wengine wa MAENDELEO.
UJENZI WA SEKONDARI MPYA KIJIJINI SEKA
WANANCHI wa Kata ya Nyamrandirira yenye VIJIJI 5 (Chumwi, Kaboni, Kasoma, Mikuyu na Seka) IMEAMUA KUJENGA SEKONDARI YA PILI ili kutatua MIRUNDIKANO iliyopo Kasoma Sekondari. Vilevile, SEKA SEKONDARI ITAPUNGUMZA UMBALI wa kutembea kwa WANAFUNZI wa kutoka VIJIJI vya Seka, Mikuyu na Chumwi.
AFISA MTENDAJI wa Kata ya Nyamrandirira, Ndugu Muswaga Itra, amesema kwamba WANANCHI ndani ya VIJIJI vyote 5 wanachangia NGUVUKAZI na FEDHA taslimu ambazo zimeamuliwa na VIJIJI vyenyewe (kati ya Tsh 20,000 na 5,000 kutoka kila KAYA).
MICHANGO mingine imetolewa na MGODI wa SEKA ikiwa ni TRIPU 23 za MAWE na TRIPU 1 ya MCHANGA.
MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ameishachangia SARUJI MIFUKO 250.
DIWANI wa Kata hiyo, Mhe Obadia Maregesi amesema kwamba kwa sasa UJENZI ni wa MASHINDANO kati ya VIJIJI vyote vitano (5) na amesisitiza kwamba UJENZI wa VYUMBA 8 vya Madarasa ya Sekondari hiyo vitakamilika hivi karibu na MIUNDOMBINU mingine muhimu itakamilika kabla ya tarehe 30 Septemba 2020.
OMBI KUTOKA VIJIJINI
WANANCHI wanawaomba sana WAZALIWA wa VIJIJI 5 vya Kata yao WAJITOKEZE KUCHANGIA UJENZI huu.

PROGRAMU YA KUBORESHA KILIMO NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

UGAWAJI WA PLAU kwa VIKUNDI 25 kutoka VIJIJI 25 vya JIMBO la Musoma Vijijini.

ZAWADI YA PASAKA
JIMBO la Musoma Vijijini HUSHEREHEKEA Sikukuu za PASAKA, EID AL FITR na KRISMASI kwa  NGAZI ya JIMBO kwa WANAVIJIJI kuwa na TAFRIJA za CHAKULA cha PAMOJA wakiwa na Mbunge wao wa Jimbo.
HADHARI ZA VIRUSI VYA KORONA zinazuia TAFRIJA hizi kufanyika kwa WAKATI HUU na badala yake PROGRAMU YA KUONDOA JEMBE LA MKONO VIJIJINI mwetu inaendelea KUTEKELEZWA.
UBORESHAJI WA KILIMO JIMBONI MWETU
Tunaendelea KUTEKELEZA PROGRAMU hii kwa kufanya yafuatayo:
(1) KUONDOA JEMBE LA MKONO: Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ANAENDELEA KUGAWA PLAU (jembe la kukokotwa na ng’ombe au punda) kwenye VIKUNDI VYA KILIMO.
PASAKA (12.4.2020) Mbunge huyo amegawa PLAU 25 kwa VIKUNDI 25 kutoka VIJIJI 25.
Mbunge huyo aligawa PLAU 20 kutoka VIJIJI 20 ikiwa ni ZAWADI ya Mwaka Mpya (2020).
ZAWADI YA EID AL FITR (2020) itakuwa ya kugawa PLAU 40 kutoka VIKUNDI 40 vya VIJIJI 40.
Hatua kwa hatua PLAU zitatumika kwa wingi zaidi VIJIJINI mwetu badala ya JEMBE LA MKONO
(2) KUONGEZA IDADI YA MAZAO YA BIASHARA
Mbunge huyo wa Jimbo la Musoma Vijijini kwa MISIMU 3 mfululizo AMEGAWA BURE Tani 9.66 za MBEGU za ALIZETI ikiwa ni MPANGO wa kuongeza IDADI ya MAZAO ya BIASHARA Jimboni humo. SERIKALI kupitia Wizara ya Kilimo ilichangia Tani 10 za MBEGU za ALIZETI
Prof Muhongo, Mbunge wa JIMBO la Musoma ameendelea KUWASHAWISHI Wakulima wa Jimboni humo KUPANUA KILIMO cha MAZAO ya CHAKULA ili KUJITOSHELEZA kwa CHAKULA na kuyafanya MAZAO hayo nayo kuwa sehemu ya MAZAO ya BIASHARA. Mbunge huyo AMEGAWA BURE Mbegu bora za MIHOGO, MTAMA na ULEZI.
(3) KILIMO CHA UMWAGILIAJI
MFUKO wa JIMBO ulitoa FEDHA, Mwaka 2016, za kununua VIFAA vya UMWAGILIAJI kwa baadhi ya VIKUNDI vya KILIMO. Kilimo hiki kinawekewa MKAZO na MRADI mkubwa wa KILIMO cha UMWAGILIAJI kwenye Bonde la BUGWEMA uko kwenye matayarisho.
VIPAUMBELE VYA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM (2015-2020)
JIMBO la Musoma Vijijini na Halmashauri yake ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC) limechagua VIPAUMBELE 5 kwenye UTEKELEZAJI wa ILANI hiyo.
VIPAUMBELE Vikuu vitano ni: (i) ELIMU, (ii) AFYA, (iii) KILIMO (+ Uvuvi na Ufugaji), (iv) MAZINGIRA, na (v) MICHEZO na UTAMADUNI. Maji, Umeme, Barabara, Vyombo vya Usafirishaji na Mawasiliano ni NYENZO MUHIMU za kufanikisha UTEKELEZAJI wa MIRADI ya VIPAUMBELE hivyo vitano.
TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM
Tarehe 7 Julai 2019, KITABU cha Kurasa 110 (cha rangi) cha TAARIFA ya UTEKELEZAJI WA ILANI hiyo kati ya Mwezi Januari 2016 na Juni 2019 kilichapishwa na NAKALA 5,000 kusambazwa VIJIJINI (Jimboni) na kwingineko ndani ya CHAMA na SERIKALI.
Tarehe 7 Julai 2020, KITABU kidogo kinachotoa TAARIFA ya UTEKELEZAJI wa ILANI  wa 1 Julai 2019 – 30 Julai 2020 (kikiwa na MIRADI inayoendelea hadi tarehe 30 Disemba 2020) kitachapishwa na kusambazwa.
Vilevile, KITABU chenye TAARIFA ya UTEKELEZAJI wa ILANI ya CCM ndani ya JIMBO la Musoma Vijijini, kimeambatanishwa hapa.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

BENKI YA CRDB YACHANGIA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA S/M MURUNYIGO

Mkuu wa Wilaya (DC) ya Musoma, Dr Vicent Naano Anney (pichani – mwenye Kaunda Suti ya kijivu) akipokea VIFAA VYA UJENZI kutoka Benki ya CRDB kwa ajili ya S/M Murunyigo ya Kijiji cha Kiemba, Kata ya Ifulifu.

Jumamosi, 4.4.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
AZIMIO LA MKOA WA MARA la kujenga na kuboresha MIUNDOMBINU YA ELIMU kwenye Shule zake za MSINGI na SEKONDARI unaendelea kutekelezwa kwa kasi ya kuridhisha ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma yenye Jimbo la MUSOMA VIJIJINI.
Jana, Ijumaa, 3.4.2020, Mkuu wa Wilaya (DC) ya Musoma, Dr Vicent Naano Anney alipokea VIFAA VYA UJENZI kutoka Benki ya CRDB, Tawi la Musoma.
Ndugu Solomon Marwa, Meneja wa Benki ya CRDB, Tawi la Musoma alikabidhi VIFAA hivyo ambavyo ni: SARUJI MIFUKO 60 na VIFAA vya kutengeneza MILANGO na MADIRISHA. Vifaa vyote vinagharimu Tsh Milioni 2.
WANANCHI wa Kijiji cha Kiemba chenye S/M Murunyigo na VONGOZI wao wanaishukuru sana Benki ya CRDB kwa MCHANGO huo uliopatikana kwa muda muafaka.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dr Vicent Naano Anney, Mkurugenzi Mtendaji (DED) wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Ndugu John Kayombo na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo WANAISHUKURU sana Benki ya CRDB kwa MCHANGO huo na mingine waliyokwishaitoa ndani ya Wilaya yao.

WANAFUNZI 157 WA KIDATO CHA KWANZA  HAWATARUNDIKANA MADARASANI 

Kazi za upauaji na upigaji lipu wa VYUMBA VIPYA vya MADARASA ya KIDATO cha KWANZA (2020) cha BULINGA SEKONDARI ya Kata ya Bulinga.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
BULINGA SEKONDARI ya Kata ya Bulinga ilisajiliwa Mwaka jana (2019) na kabla ya hapo ilikuwa SEKONDARI SHIKIZI ya Nyanja Sekondari ya Kata jirani ya Bwasi.
KATA YA BULINGA yenye Vijiji 3 vya Bujaga, Bulinga na Busungu imekamilisha ujenzi wa VYUMBA 3 VIPYA vya MADARASA kwa ajili ya WANAFUNZI wa KIDATO cha KWANZA (Form I) wa Sekondari yao ya Kata.
MWALIMU MKUU wa Sekondari hiyo, Mwl Nyang’oso Chacha Munyera ameeleza kwamba jumla ya WANAFUNZI waliochaguliwa kujiunga KIDATO cha KWANZA Mwaka huu (Januari 2020) ni 157 na hadi sasa WANAFUNZI 134 ndio WAMEANZA MASOMO Shuleni hapo.
CHUMBA kimoja cha Darasa kilikuwa kinachukua WANAFUNZI 67, na baada ya KUKAMILISHA ujenzi wa VYUMBA 3 VIPYA, sasa kila CHUMBA kimoja cha Darasa kitachukua WANAFUNZI 45 – hakuna mirundikano madarasani!
MTENDAJI KATA hiyo, Ndugu Pima  Mengere amesema upauaji na upigaji lipu VYUMBA VIPYA 2 ulikamilika tarehe 25 Machi 2020 na muda mfupi ujao watakamilisha kazi ya kupiga lipu Chumba cha tatu. Kwa hiyo, WANAFUNZI 134 wa KIDATO cha KWANZA watakaporudi Shuleni (baada ya likizo ya CORONAVIRUS) watakuwa na VYUMBA VIPYA 3 vya Madarasa yao – hakuna mirundikano madarasani.
WANAVIJIJI wamechangia NGUVUKAZI zao na FEDHA taslimu Tsh 10,500 kutoka kila KAYA.
DIWANI wa KATA ya Bulinga, Mhe Mambo Japani (CHADEMA) amesema kwamba kuna MIPANGO imewekwa na WANAVIJIJI ya KUSHIRIKIANA na SERIKALI kupitia HALMASHAURI yao na MBUNGE wao wa Jimbo, KUBORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU kwenye SEKONDARI hiyo na SHULE zote za MSINGI ndani ya Kata yao.
DIWANI huyo amesema ifikapo Januari 2021, MADARASA CHINI YA MITI yatatoweka kabisa. Ameishukuru sana SERIKALI kwa MICHANGO yake kwenye SEKTA YA ELIMU ndani ya Kata yao.
MICHANGO YA MBUNGE WA JIMBO
Mbunge Prof Sospeter Muhongo amechangia:
* MADAWATI, VITABU vingi vya MAKTABA, SARUJI na MABATI kwa Shule zote za Msingi za Kata ya Bulinga.
* BULINGA SEKONDARI: Mbunge huyo amechangia Saruji Mifuko 192 na Vitabu vingi vya Maktaba. MFUKO wa JIMBO umechangia Mabati 108.
WAZALIWA wa KATA ya BULINGA wanaombwa wajitokeze kuchangia MIRADI ya MAENDELEO ya KATA yao ikiwemo ya UBORESHAJI wa Miundombinu ya Elimu kwenye Shule za Msingi na Sekondari.

 ZAHANATI KWA KILA KIJIJI – KATA YA NYEGINA YATEKELEZA ILANI YA CCM

MAFUNDI na VONGOZI wa Kata ya Nyegina wakiwa kwenye eneo la Ujenzi wa ZAHANATI ya KIJIJI cha MKIRIRA, Kata ya NYEGINA.

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
KATA YA NYEGINA ina Vijiji 3 ambavyo ni Kurukerege, Mkirira na Nyegina.
KIJIJI cha NYEGINA kinayo ZAHANATI ambayo inapanuliwa kwa kuongeza WADI ya MAMA na MTOTO. Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo amechangia SARUJI MIFUKO 200 kwenye ujenzi wa WADI hiyo.
KIJIJI CHA KURUKEREGE kilisimamisha kwa muda ujenzi wa ZAHANATI yake baada ya kupata fedha kutoka PIC kujenga VYOO vya S/M Kurukerege. Kazi hiyo imekamilika na sasa wanaendelea na ujenzi wa ZAHANATI ya Kijiji chao. Mbunge wao wa Jimbo atakagua ujenzi huo na kuchangia ipasavyo.
KIJIJI CHA MKIRIRA
kinajenga ZAHANATI yake kwa kushirikisha WAZALIWA wa Kijiji hicho na WADAU wengine wa MAENDELEO.
UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI CHA MKIRIRA
Afisa Mtendaji wa Serikali ya Kijiji cha Mkirira, Ndugu  Sabina  Chacha amesema kuwa WANAKIJIJI wamekusudia kukamilisha ujenzi wa BOMA la ZAHANATI yao ifikapo mwishoni mwa Mwezi huu (April 2020).
WANAVIJIJI wakiongozwa na DIWANI wao, Mhe Majira Mchele, wanachangia NGUVUKAZI na FEDHA taslimu kwenye ujenzi wa ZAHANATI ya Kijiji cha MKIRIRA.
DIWANI huyo ametoa SHUKRANI nyingi kwa WAZALIWA na Kijiji hicho kwa MICHANGO yao iliyofanikisha ujenzi kufikia hatua hiyo. Vilevile, amesema baadhi ya WAZALIWA wa Kijiji hicho wameanzisha UMOJA wao uitwao, “MKIRIRA MAENDELEO” kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa ZAHATI ya Kijiji chao.
DIWANI huyo ameendelea kutoa SHUKRANI zake kwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo kwa kuchangia SARUJI MIFUKO 200 kwenye ujenzi wa ZAHANATI hiyo na kwa MICHANGO yake mingi ndani ya KATA hiyo kwenye SEKTA za Elimu, Afya, Kilimo, Mazingira, Michezo na Utamaduni.
SHUKRANI ZA KIPEKEE zinapelekwa NMB kwa kuchangia MABATI 182. Mhe Amina Makilagi (Mb)  anapewa SHUKRANI nyingi kwa MICHANGO yake.
Aidha, MWENYEKITI wa Serikali ya Kijiji hiki, Ndugu Magogwa Majinge alisema bado kuna UPUNGUFU wa VIFAA VYA UJENZI wa nondo 12 na Saruji Mifuko 40 kukamilisha ujenzi wa BOMA hilo.
UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM (2015-2020) kwenye SEKTA YA AFYA unaendelea vizuri ndani ya JIMBO la Musoma Vijijini kwa USHIRIKA wa SERIKALI na WANANCHI:
* Zahanati Mpya 14
zinajengwa
* Hospitali ya Wilaya moja (1) inajengwa
* Zahanati moja (1) ya Masinono inapanuliwa kuwa Kituo cha Afya
* Zahanati zinazotoa HUDUMA ni 28 (24 za Serikali & 4 za Binafsi)
*Vituo vya Afya vinavyotoa HUDUMA ni viwili (2)
KARIBUNI TUKAMILISHE UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI CHA MKIRIRA NA NYINGINE 13 ZINAZOJENGWA KWENYE VIJIJI VINGINE 13 JIMBONI MWETU

WALEMAVU KWIKUBA GROUP WAPOKEA MKOPO USIOKUWA NA RIBA KUTOKA HALMASHAURI YAO

Baadhi ya Wana-Kikundi cha WALEMAVU KWIKUBA GROUP wakiwa kwenye MRADI wao wa UFUGAJI wa KONDOO na MBUZI, Kijijini Kwikuba, Kata ya Busambara.

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
KIKUNDI cha Watu wenye ULEMAVU kiitwacho, “WALEMAVU KWIKUBA GROUP” kilianzishwa Februari 2019 kikiwa na WANACHAMA 26 ambao kwa sasa wamefika 41.
WALEMAVU KWIKUBA GROUP yenye maskani yake Kijijini Kwikuba, Kata ya Busambara ilianza kwa KUUZA NAFAKA na wamepanua biashara yao na kuanza KUFUGA KONDOO na MBUZI baada ya kupata MKOPO usiokuwa na RIBA wa Tsh 2,400,000 kutoka HALMASHAURI ya Wilaya ya Musoma yenye Jimbo la Musoma Vijijini.
MWENYEKITI wa Kikundi hiki, Ndugu John Ndaro Musulubhi alisema kuwa Kikundi chao KIMESAJILIWA na HALMASHAURI yao na LENGO lao kuu ni KUJITEGEMEA KIUCHUMI kutokana na MAPATO ya BIASHARA zao za NAFAKA na MIFUGO.
MWENYEKITI huyo anaishukuru sana HALMASHAURI ya Wilaya ya Musoma na VIONGOZI wake kwa kutoa MIKOPO isiyokuwa na RIBA kwa WATU wenye ULEMAVU walioko ndani ya Halmashauri hiyo.
MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ametunisha MTAJI wao wa biashara ya NAFAKA kwa kuwanunulia MAGUNIA KUMI (10) ya MAHINDI na amesema watawasaidia kutafuta WADAU wengine wa Maendeleo watakaowatunishia MTAJI wao wa biashara.
Sambamba na MAFANIKIO hayo, WALEMAVU KWIKUBA GROUP  wanataraji kuanzisha  MRADI wa USEREMALA, na wanaomba WADAU wa MAENDELEO na hasa kwa WATU wenye ULEMAVU, wajitokeze kuwasaidia wapate VIFAA VYA USEREMALA.
WALEMAVU KWIKUBA GROUP wanawashauri na kuwashawishi WATU WENYE ULEMAVU po pote walipo kutumia FURSA zinazotolewa na SERIKALI yetu ya kuwafanya WAJITEGEMEE KIUCHUMI.

SHULE YA MSINGI MURANGI B YAKARIBIA KUACHANA NA DARASA NA OFISI CHINI YA MITI

UPAUAJI wa CHUMBA kimoja cha Darasa S/M MURANGI B ya Kijijini Lyasembe, Kata ya Murangi

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
MWALIMU MKUU wa S/M Murangi B, Mwl Kerango Msakambi ameeleza kwamba SHULE hiyo ina jumla ya WANAFUNZI 544, WALIMU 6. Vyumba vya Madarasa vilivyopo ni 7 na UPUNGUFU ni 9. Shule ilifunguliwa Mwaka 2014 na iko Kijijini Lyasembe, Kata ya Murangi.
Chumba cha Darasa lenye WANAFUNZI WENGI kinao 124 (Std III) na chenye wachache ni 59 (Std II).
WANAFUNZI wa Darasa la II hawana Chumba chao cha Darasa, kwa hiyo WANASOMEA chini ya MTI au ikibidi wanapokezana (kusoma kwa zamu) na Darasa la I lenye Wanafunzi 71.
WALIMU hawana OFISI, wanakaa CHINI YA MITI na mvua ikinyeesha wanahamia MADARASANI.
Diwani wa Kata ya Murangi, Mhe Simion Kujerwa amesema kwamba KATA imedhamiria kutatuta TATIZO SUGU la MIRUNDIKANO YA WANAFUNZI Madarasani. WANAVIJIJI na WAZALIWA wa Kata hiyo wameanza kuchangia ujenzi wa MIUNDOMBINU bora kwenye Shule zilizoko ndani ya Kata yao.
KATA ya Murangi, yenye VIJIJI 2 (Lyasembe na Murangi) inazo SHULE ZA MSINGI 4 na SEKONDARI 1.
DIWANI huyo anaishukuru sana SERIKALI kupitia Halmashauri yao na Mbunge wao, Profesa Sospeter Muhongo kwa  MICHANGO ya MIRADI ya MAENDELEO kwenye Kata yao. Ameeleza kwamba MBUNGE wao wa JIMBO amechangia SARUJI, MADAWATI na VITABU vingi kwa SHULE zote nne (4) za MSINGI. MURANGI SECONDARY School imepewa VITABU VINGI vya MAKTABA
UKAMILISHAJI WA DARASA LA S/M MURANGI B
Njia pekee ya kuwatoa WANAFUNZI (Std II) CHINI ya MTI ni KUKAMILISHA Chumba kimoja cha Darasa kinachoezekwa kwa MABATI 54 yaliyonunuliwa na FEDHA za MFUKO wa JIMBO.
MBUNGO wa Jimbo anachangia SARUJI MIFUKO 50 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Chumba hicho. SARUJI hiyo itachukuliwa tarehe 2.4.2020.
Baada ya JENGO hilo kukamilika, Mbunge wa Jimbo atapiga HARAMBEE ya kujenga VYUMBA 2 VIPYA vya Madarasa vyenye OFISI ya WALIMU katikati.
WAZALIWA wa KATA ya MURANGI wanaombwa wajitokeze KUCHANGIA UJENZI huu na MIRADI mingine ya MAENDELEO inayotekelezwa ndani ya Kata yao.
Kwa muda wa takribani MIAKA MINNE na NUSU (4.5 yrs), JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI limeendelea KUJENGA na KUBORESHA MIUNDOMBINU ya ELIMU kwenye SHULE zake zote za MSINGI (114 – 111 za Serikali na 3 za Binafsi) na SEKONDARI (22 – 20 za Serikali na 2 za Binafsi). MADAWATI na VITABU VINGI vya MAKTABA vimegawiwa. Sekondari Mpya 5 zinajengwa zifunguliwe mwakani  (Januari 2021).
WADAU WA MAENDELEO wakiwemo PCI, NMB, CRDB na baadhi ya WAZALIWA wa Vijiji vya Jimbo hili WANAENDELEA KUCHANGIA MIRADI muhimu kwenye SEKTA YA ELIMU ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini – TUNAWASHUKURU SANA!
Picha zilizoko hapa zinaonesha UPAUAJI wa CHUMBA kimoja cha Darasa ya S/M MURANGI B ya Kijijini Lyasembe, Kata ya Murangi.

MATATIZO YA UMBALI MREFU WA KUTEMBEA NA MIRUNDIKANO YA WANAFUNZI MADARASANI YAENDELEA KUTATULIWA

Ujenzi wa Vyumba vipya vya Madarasa unaoendelea kwenye SHULE SHIKIZI BURAGA MWALONI inayojengwa kwenye Kitongoji cha Mwaloni, Kijijini Buraga, Kata ya Bukumi.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
AZIMIO NA. 1 LA UBORESHAJI WA KIWANGO CHA ELIMU NDANI YA MKOA WA MARA
(1) Uboreshaji wa MIUNDOMBINU ya ELIMU ya aina zote katika Shule za Msingi na Sekondari
JIMBO la Musoma Vijijini LINATEKELEZA AZIMIO hilo na mengine matano (5) kwa USHIRIKA wa WANANCHI, VIONGOZI na SERIKALI yao – MATUNDA MAZURI yameanza kuonekana.
SHULE ZA MSINGI JIMBONI
* 111 za Serikali
* 3 za Binafsi
UJENZI unaendelea kwenye SHULE zote za MSINGI ili kuboresha MIUNDOMBINU yao ya ELIMU.
MATUNDA YA AWALI yaliyopatikana tokea UBORESHAJI wa MIUNDOMBINU ya SHULE ZA MSINGI uanze, miaka minne (4) iliyopita ni HALMASHAURI YA WILAYA YA MUSOMA (yenye Jimbo la Musoma Vijijini) kuwa ya KWANZA MKOANI MARA Mwaka jana (2019) kwenye MITIHANI YA DARASA LA NNE (IV).
SHULE SHIKIZI JIMBONI
* 11 zinaendelea kujengwa na baadhi tayari zina WANAFUNZI wa Darasa la AWALI na la kwanza (Std I).
Ujenzi wa SHULE MPYA hizi unazingatia UBORA unaotakiwa kwa MIUNDOMBINU yake.
UJENZI WA SHULE SHIKIZI BURAGA MWALONI
SHULE MPYA hii inajengwa na WAKAZI wa Kitongoji cha Buraga Mwaloni ili KUTATUA TATIZO la WATOTO wao wenye UMRI wa chini ya MIAKA 10 kutembea umbali wa kilometa 5-7 kwenda masomoni kwenye SHULE za MSINGI za vitongoji jirani.
MWALIMU WA KUJITOLEA, Ndugu Dickson Maregesi ndie MSIMAMIZI wa SHULE SHIKIZI Buraga Mwaloni. Amesema SHULE hiyo ilianza rasmi Mwaka 2015 ikiwa na jumla ya WANAFUNZI 117 waliokuwa wanasomea CHINI YA MTI na baada ya kuhitimu hapo WALIENDA kuanza MASOMO ya Darasa la kwanza (Std I) kwenye SHULE ZA MSINGI za Buraga na Chitare ambazo ziko mbali na Kitongoji cha Mwaloni.
Kwa wakati huu, WANAFUNZI 41 wa Darasa la Awali wa SHULE SHIKIZI hiyo wanasomea chini ya MTI.
Ndugu Nyajoge Wanjara, Mwenyekiti wa KAMATI ya ujenzi wa Shule hiyo amesema WANA-KITONGOJI wameanza KUCHANGIA UJENZI wa Shule yao kwa kutoa NGUVUKAZI na Fedha taslimu kiasi cha Tsh 5,000/= kutoka kila KAYA. Kiongozi huyo amesisitiza kwamba  SHULE yao hiyo ujenzi utakamilika na kufunguliwa Januari 2021.
MICHANGO MINGINE
* Saruji Mifuko 50 kutoka MFUKO wa JIMBO
* Saruji Mifuko 100 kutoka kwa Mbunge wao, Prof Sospeter Muhongo
WAZALIWA wa Kata ya Bukumi na hasa wa Kijiji cha Buraga wanaombwa KUTOA MICHAGO ya ujenzi wa Shule hiyo ambayo inahitaji VYUMBA vipya vya Madarasa, Ofisi ya Walimu, Vyoo na Nyumba ya Walimu.
WADAU wengine wa Maendeleo nao wanaombwa KUCHANGIA.

OFISI YA CCM YA WILAYA YA MUSOMA YAANZA KUJENGWA

Uanzaji wa ujenzi wa OFISI YA CCM ya Wilaya ya Musoma Vijijini, yaani UCHIMBAJI wa MSINGI na UFYATUAJI wa MATOFALI.

OFISI YA MUDA ya CCM ya Wilaya ya Musoma Vijijini iko kwenye Kijiji cha Chumwi, Kata ya Nyamrandirira.
Wana-CCM wa Musoma Vijijini (kwenye Vitongoji 374, Vijiji 68, Kata 21) wakiongozwa na KAMATI YA UJENZI wameanza rasmi kujenga OFISI YA CCM ya Wilaya yao.
MWENYEKITI wa KAMATI ya Ujenzi ni Dr Vicent Anney Naano, Mkuu wa Wilaya (DC) ya Musoma na MAKAMU MWENYEKITI ni Mhe Diwani Charles Magoma Nyambita, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma.
Ndugu John Lipesi Kayombo, Mkurugenzi Mtendaji (DED) wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ANASHIRIKI vizuri sana kwenye UTEKELEZAJI wa MRADI huu.
HATUA ZA AWALI ZA UJENZI
Mwenyekiti wa Kamati ya ujenzi amewezesha upatikanaji wa MAWE na MCHANGA wa kuanzia ujenzi. FUNDI ameanza kuchimba MSINGI.
AHADI ZA MICHANGO ILIYOTOLEWA KWENYE HARAMBEE YA UJENZI
KAMATI ya ujenzi INASUBIRI WALIOTOA AHADI za VIFAA VYA UJENZI na FEDHA TASLIMU watimize AHADI zao ili ujenzi uende kwa kasi kubwa.
AHADI YA MBUNGE WA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo alihaidi kutoa MCHANGO wa awali wa MATOFALI 5,000 (elfu tano). Alianza kwa kununua MATOFALI 1,000 kutoka Kanisa Katoliki Nyegina.
KAMATI YA UJENZI imependekeza MATOFALI yatengenezewe karibu na eneo la ujenzi ili kuachana kabisa na GHARAMA za kusafirisha MATOFALI. Kwa hiyo, Mbunge huyo ameanza kununua SARUJI hapo hapo Kijijini (Murangi) ya kutengenezea MATOFALI 5,000.
Vilevile, Mbunge huyo atachangia FEDHA za kumlipa FUNDI ujenzi.
Diwani wa Kata ya Murangi, Mwenyeji wa MRADI huu, Mhe Simion Kujerwa ANAFANYA KAZI NZURI ya kusimamia ujenzi wa OFISI hii  ya CCM Wilaya.

SHULE YA MSINGI MKAPA YA KIJIJINI KASTAM IMEAMUA KUTATUA TATIZO LA MIRUNDIKANO MADARASANI

Kazi inaendelea ya ujenzi wa Vyumba VIPYA vya Madarasa ya S/M MKAPA ya Kijiji cha Kastam, Kata ya Bukima.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
SHULE YA MSINGI MKAPA ilianzishwa Mwaka 2009 na iko Kijijini Kastam, Kata ya Bukima.
Mwalimu Mkuu wake, Mwl
Nyakusanja David Mkangara amesema Shule hiyo ina jumla ya WANAFUNZI 972. Vyumba vya Madarasa VILIVYOPO ni nane (8) na UPUNGUFU ni kumi na nne (14).
Mwalimu Mkuu huyo anasema, “Hawapo Wanafunzi WANAOSOMEA NJE chini ya MITI lakini kuna MIRUNDIKANO MIKUBWA Madarasani ambapo Chumba kimoja cha Darasa chenye WANAFUNZI WENGI kinao 204 (Std III) na chenye WACHACHE kinao 87 (Std VI).”
TATIZO LA MIRUNDIKANO mikubwa Madarasani LINATATULIWA kwa KUJENGA Vyumba Vipya vya Madarasa.
Ndugu Adonias Matijo, Mtendaji wa Serikali ya Kijiji cha Kastam amesema kuwa Kijiji hicho kilipokea Tsh 2,030,000/= ambayo ni RUZUKU (20%) kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Fedha hizo zilitumika KUNUNUA SARUJI na kuanza kufyatua MATOFALI  ya ujenzi wa Vyumba Vipya vya Madarasa.
Mbali ya FEDHA kutoka kwenye HALMASHAURI yao, KILA KAYA ya Kijiji cha Kastam inachangia  NGUVUKAZI na FEDHA Taslimu ya kiasi cha Tsh 6,200/=
VYANZO hivyo vya FEDHA na NGUVUKAZI vimefanya WANAKIJIJI kufanikiwa KUJENGA Vyumba viwili (2) vya Madarasa na Ofisi moja (1) ya Walimu.
KAZI BADO KUBWA, Wanakijiji hao wanaomba WADAU wa Maendeleo na WAZALIWA na Kijiji cha Kastam na Kata ya Bukima kwa ujumla, WAJITOKEZE KUCHANGIA ujenzi wa Vyumba VIPYA vya Madarasa ya S/M MKAPA. HARAMBEE ya Mbunge wa Jimbo itafanyika hivi karibuni.
MICHANGO YA MBUNGE WA JIMBO KWENYE S/M MKAPA
Mbunge wao wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ameishachangia:
* Madawati 160
* Vitabu vingi vya Maktaba
* Saruji Mifuko 60
* Mabati 54
MICHANGO YA MFUKO WA JIMBO KWENYE S/M MKAPA
* Saruji Mifuko 50
* Mabati 54
Diwani wa Kata hiyo (Bukima), Mhe January Simula amesema kwamba KATA YAO  imejipanga kuhakikisha kwamba WANAFUNZI wa SHULE zote za  MSINGI ndani ya Kata yao HAWATASOMEA NJE CHINI YA MITI ifikapo mwakani (Januari 2021).
Diwani huyo anawashukuru Viongozi wa Wilaya na Halmashauri yao, na Mbunge wao wa Jimbo kwa MICHANGO wanayoitoa kwenye MIRADI ya MAENDELEO (Elimu, Afya, Kilimo, Mazingira, Michezo, n.k.) ya Kata yao yenye VIJIJI 3 (Bukima, Butata na Kastam).
JIMBO la Musoma Vijijini LINAJENGA na KUBORESHA MIUNDOMBINU ya ELIMU kwenye SHULE zake zote za MSINGI 114 (111 za Serikali na 3 za Binafsi), SHULE SHIKIZI 11 (kati ya hizi zipo zilizofunguliwa).
Jimbo hili lenye KATA 21 na VIJIJI 68 lina SEKONDARI 22 zenye Wanafunzi (20 za Serikali/Kata na 2 za Binafsi). Sekondari MPYA 5 zinajengwa na zitafunguliwa mwakani (Januari 2021).