EID EL FITR NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI –  SHEREHE NA MAENDELEO VIJIJINI

Mbunge wa Jimbo akiwa na Waumini wa Dini ya Kiislamu na Wegeni wengine waalikwa kwenye eneo la Sherehe ya Eid el Fitr Kijijini Kome.

I – MASJID KOME
Kijiji cha Kome, Kata ya Bwasi
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo AMEWAKARIBISHA WAISLAMU wa Kijiji cha Kome na kutoka Vijiji jirani KIFUNGUA KINYWA (Eid el Fitr Breakfast) na CHAKULA CHA MCHANA (Eid el Fitr Lunch) kwenye ENEO ambalo MSIKITI wa Kijiji UTAJENGWA.
Wananchi walipata fursa ya kueleza KERO zao ambazo zilijibiwa na Mbunge huyo.
II – CHEMISTRY LABORATORY OF NYANJA SECONDARY SCHOOL
Baada ya kupata KIFUNGUA KINYWA Msikitini, Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo ALIENDA KUKAGUA ujenzi wa MAABARA za Nyanja Secondary School iliyoko hapo Kijijini.
Sekondari ya Kata ya Bwasi (Nyanja Secondary School). Inakamilisha ujenzi wa MAABARA 3 za Chemistry, Physics na Biology. BOMA lenye Vyumba 3 vya Maabara hizo limekamilika. Kinachoendelea kwa sasa ni kuweka MIUNDOMBINU ya ndani ya MAABARA hizo. Wameanza na Maabara ya Kemia (Chemistry Laboratory).
Ujenzi huu unasimamiwa na BODI ya Shule, Mwenyekiti ni Ndugu Abel Bohohe na Mwalimu Mkuu, Mwl Charles Ndebele. Viongozi hawa WACHAPAKAZI WAZURI wamesema kwamba LENGO lao ni kukamilisha Maabara ya Kemia ifikapo tarehe 30.08.2019.
Mbunge Prof Sospeter Muhongo alipokuwa Shuleni hapo alipata fursa ya kuongea na Wanafunzi wanaosoma Masomo ya Sayansi na baadae ALICHANGIA UJENZI huo wa ndani ya Maabara kwa KUNUNUA NONDO 35 zilizokuwa zinahitajika kwa hatua hii ya ujenzi. Nondo zilinunuliwa hapo Kijijini.
Mbunge Prof Muhongo akiwa  Nyanja Secondary School alikagua UJENZI wa MIUNDOMBINU wa Maabara ya KEMIA. Mbunge huyo aliongea na Wanafunzi na baadae akaenda Kijijini kununua NONDO 35 zilizoombwa kwa ajili ya hatua hii ya ujenzi.
Baada ya kushiriki Eid el Fitr Kijijini Kome (Masjid Kome), Mbunge Prof Muhongo aliendelea kuungana na Waislamu wa Misikiti ya Vijiji vya Mayani – Masjid Ququ bin Amri (Kata ya Tegeruka) na Nyegina – Masjid Othman (Kata ya Nyegina).

UKAGUZI WA UJENZI WA HOSPITAL YA WILAYA 

UJENZI wa MAJENGO 8 ya Hospital ya Wilaya inayojengwa ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.

04.06.2019
Jimbo la Musoma Vijijini
SERIKALI yetu imetoa Tsh Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospital ya Wilaya ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.
Hospital hiyo inajengwa kwenye Kitongoji cha Kwikonero, Kijijini Suguti, Kata ya Suguti.
WANANCHI wa Kata 21, Vijiji 68 na Vitongoji vyote 374 vya Jimbo la Musoma Vijijini WAMEKUBALI KUCHANGIA ujenzi huu kwa Kila KATA kuchangia Tsh Milioni 7.5.  MADIWANI na WATENDAJI wa Kata na Vijiji wanasimamia UKUSANYAJI wa MICHANGO hiyo. Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo ataungana na WANANCHI na SERIKALI kuchangia ujenzi huo.
Jana, Jumatatu, 03.06.2019 Mbunge wa Jimbo akifuatana na VIONGOZI wa CCM Wilaya (M/Kiti WAZAZI, Katibu, Ma-Katibu wa Jumuiya za Chama- UWT, WAZAZI na UVCCM) WALIKAGUA UJENZI wa Hospitali hiyo ya Wilaya.
MAJENGO 8 yanayojengwa kwa sasa ni:
(1) Jengo la Utawala: Linakamilishwa usawa wa lenta
(2) Jengo la Mapokezi (OPD): Lipo hatua ya  kumwaga Jamvi
(3) Jengo la Maabara: Boma limekamilika tayari kwa kuezekwa
(4) Jengo la Mionzi (Radiology): Lipo hatua ya kumwaga Jamvi
(5) Jengo la Mama na Mtoto: Lipo hatua ya kumwaga Jamvi
(6) Jengo la Ufuaji (Laundry): Lipo hatua ya kumwaga Jamvi
(7) Jengo la Madawa (Pharmacy): Lunamwagwa Jamvi
(8) Jengo la Kichomea Taka: Lipo hatua ya Msingi
Mkuu wa Wilaya (DC) Dr Vicent Naayo Anney na Mkurugenzi wa Halmashauri (DED) Ndugu John Kayombo WANASIMAMIA ujenzi huu kwa UBUNIFU na UFANISI  mkubwa.

SHIRIKA LA BMZ LAENDELEA KUWAWEZESHA WATU WENYE ULEMAVU NA WANAFUNZI WA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

WATU wenye ULEMAVU na WANAFUNZI wakipokea VIFAA mbalimbali kutoka kwenye MIRADI ya BMZ yenye Ofisi yake pale HOSPITAL ya SHIRATI (DDH Shirati), Wilaya ya Rorya, Mkoa wa Mara

Jumanne 04.06. 2019
Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
MIRADI ya Shirika la UJERUMANI la BMZ yaendelea kutekelezwa kwenye  Jimbo la Musoma Vijijini. MIRADI hii inawalenga WANAFUNZI na WATU wenye ULEMAVU kwenye KATA 10 za Jimboni ambazo ni: Bugwema, Bukima, Bukumi, Bwasi, Kiriba, Makojo, Murangi, Nyambono, Nyamrandirira na Suguti – tukifanya vizuri BMZ huenda itapanua MIRADI yake itekelezwe kwenye Kata nyingine za Jimbo letu!
BMZ kirefu chake ni: Bundesministerium Fűr Wirtschaftliche Zusammenarbeit (German Federal Ministry for Economic Development and Cooperation).
Kati ya tarehe 28 Mei na 30 Mei 2019, MIRADI ya BMZ imekabidhi VIFAA mbalimbali kwa WATU wenye ULEMAVU na WANAFUNZI Jimboni mwetu.
Meneja wa Mradi wa BMZ, Ndugu Niwaely Sand, amekabidhi jumla ya:
(1) Mabegi ya Shule 50
(2) Daftari 100
(3) Kalamu 500
(4) Penseli 500
(5) Fimbo 10 kwa wenye ulemavu wa macho
(6) Cherehani 2
(7) Wheelchairs/Tricycles 12
(8) Miwani jozi 6
(9) Miguu Bandia 10
(10) Hearing Devices 6
Vifaa vilivyotajwa hapo juu vilikabidhiwa kwa WANAFUNZI na WATU wenye ULEMAVU ambao mahitaji yao ni MAALUM na ambao walishakamilisha VIPIMO vya kupatiwa mahitaji hayo.
Aidha Meneja huyo amewataka WATUMIAJI wa vifaa hivyo kuwa makini na waangalifu wakati watakapokuwa wanavitumia ili vidumu kwa manufaa yao.
Jimbo la Musoma Vijijini linatoa SHUKRANI za kipekee kwa BMZ na MIRADI yake yenye manufaa makubwa Jimboni mwetu – Vielen herzlichen Dank!
Let us take all plausible opportunities at Full Throttle!

 KITONGOJI CHA RWANGA CHAENDELEA KWA KASI KUBWA KUJENGA SHULE YAKE YA MSINGI 

Kikao cha Walimu wa S/M Rwanga, Wananchi wa Kitongoji cha Rwanga, Viongozi mbalimbali wa Kijiji/Kata, CCM Wilaya na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.

Jumatatu, 03.06.2019
Jimbo la Musoma Vijijini
Shule ya Msingi Rwanga iliyoko kwenye Kitongoji cha Rwanga, Kijijini Kasoma, Kata ya Nyamrandirira ilianza kujengwa na kufunguliwa Mwaka huo huo wa 2016.
Shule ina Madarasa 4 (Std I-IV), Walimu 5 na Mwalimu 1 wa Kujitolea. Vipo Vyumba 4 vya Madarasa, Ofisi 2 za Walimu na Choo chenye Matundu 6. Nyumba ya Mwalimu Mkuu imejengwa kwenye eneo la Shule.
Mwalimu Mkuu wa Shule, Mwl David Lawrent Swedi, Mtendaji wa Kijiji, Ndugu Phaustine Augustine na Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji, Ndugu Fedson Msalama kwa PAMOJA WANASIMAMIA kwa umakini na mafanikio makubwa ujenzi wa hiyo Shule.
Wakazi wa Kitongoji cha Rwanga WANACHANGIA NGUVUKAZI zao kwa kusomba mchanga, mawe, kokoto na maji. Vilevile, kila KAYA inachangia fedha taslim, Tshs 15,000.
Mradi wa EQUIP wa Ushirika kati ya Serikali yetu na ya Uingereza (DfID) ulitoa Tsh Milioni 25.2 kwa ajili ya ujenzi huo na kuunga mkono Wananchi waliojitolea kuboresha ubora wa ELIMU hapo Kijijini.
Mbunge wa Jimbo ameishatoa MICHANGO yake kwa S/M Rwanga kama ifuatavyo: (i) SARUJI MIFUKO 110, (ii) MADAWATI 41.
Leo, 03.06. 2019, baada ya Mbunge huyo kukagua ujenzi unaoendelea hapo Shuleni, amechangia SARUJI MIFUKO 50 ambayo itatumika kwenye ujenzi Mpya wa Vyumba vingine 2  vya Madarasa ambavyo WANANCHI wameahidi kuvikamilisha ifikapo 30.06.2019.
MFUKO wa JIMBO umechangia MABATI 150 kwenye ujenzi wa Vyumba 2 vipya vya Madarasa na Ofisi 1 ya Walimu hapo Shuleni.
Kwa kuwa Shule sasa inazo Ofisi za Walimu, Mbunge wa Jimbo amewapatia VITABU vya Elimu ya Shule ya Msingi. Vilevile Mbunge huyo  AMECHANGIA sehemu ya posho ya Mwalimu wa Kujitolea wa S/M Rwanga.
Viongozi wa CCM Wilaya ya Musoma Vijijini (Makatibu: UWT, WAZAZI na UVCCM) na Mwenyekiti WAZAZI Wilaya wameshiriki kwenye UKAGUZI wa ujenzi huo. Wameongozwa na Katibu wa CCM Wilaya, Ndugu Stephen Koyo,
Diwani wa Kata ya Nyamrandirira, Mhe Maregesi,  AMEWASHUKURU sana Wananchi na Wadau wa Maendeleo, ikiwemo Serikali yetu, kwa KUCHANGIA ujenzi wa Shule hiyo Mpya kwenye Kata yao. Amewaomba Wazaliwa wa Kata ya Nyamrandirira yenye Vijiji 5, WAJITOKEZE kuchangia ujenzi wa Seka Secondary School unaoendelea Kijijini Seka.

WANAKAZI WA KIJIJI CHA KAKISHERI WACHOSHWA KUTEMBEA UMBALI MREFU KUFUATA HUDUMA ZA AFYA

Kikao cha Tarehe 01.06.2019 cha WANANCHI, Mbunge wa Jimbo, Viongozi wa CCM Wilaya, kwenye eneo la ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kakisheri, Kata ya Nyakatende.

Jumamosi 01.06.2019
Jimbo la Musoma Vijijini
Wakazi wa Kijiji cha Kakisheri, Kata ya Nyakatende WANALAZIMIKA kutembea umbali wa kilomita 4 kwenda kwenye Zahanati ya Kijiji jirani cha Kiemba kupata MATIBABU wanapoyahitaji. HUDUMA za Afya nyingine zinapatikana Musoma Mjini, umbali wa kilomita 15 kutoka Kijijini Kakisheri.
Kutokana na kero hiyo SUGU ya upatinakanaji wa HUDUMA za AFYA, Wakazi wa Kijiji cha Kakisheri WAMEAMUA kujenga Zahanati Kijijini mwao.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji, Ndugu Msafiri Kolesi ameeleza kwamba WANANCHI wamekubali KUJITOLEA kutumia NGUVUKAZI zao kujenga Zahanati yao. Wanasomba mawe, kokoto, mchanga na maji. Vilevile kila KAYA inachangia Tshs 23,000 kwa ujenzi huu unaosimamiwa na Viongozi wa Kijiji na Kaimu Mtendaji wa Kijiji, Ndugu Antony Ndege.
Diwani wa Kata hiyo, Mhe Rufumbo Mugini Rufumbo amesema ujenzi wa Zahanati hiyo UTAENDA KWA KASI kubwa zaidi baada ya Wana-Kakisheri kukamilisha UJENZI wao wa Vyumba 2 vya Madarasa kwenye Sekondari yao ya Kata (Nyakatende Secondary School). Ujenzi huu wa Vyumba vya Madarasa ulikuwa muhimu ili kuhakikisha Wanafunzi wa Kijiji cha Kakisheri WALIOFAULU na KUCHAGULIWA kuanza Form I kwenye Sekondari ya Nyakatende WANAANZA MASOMO yao bila kuchelewa.
MBUNGE WA JIMBO ATIMIZA AHADI YAKE LEO
Baada ya kukagua ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kakisheri, Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo amechangia leo SARUJI MIFUKO 50 kama alivyoahidi.
Mbunge huyo alitembelea eneo la ujenzi akiwa amefuatana na Katibu ya CCM Wilaya, Ndugu Stephen Koyo na Viongozi wengine wa Chama (CCM)

UJENZI WA SHULE SHIKIZI YA KIJIJI CHA BUANGA WAFIKIA HATUA NZURI

Ujenzi wa Miundombinu ya Shule Shikizi ya Kijiji cha Buanga, Kata ya Rusoli

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
Ijumaa 31.05.2019
Watoto wa Kijiji cha Buanga, Kata ya Rusoli, wanalazimika kutembea umbali usiopungua kilomita 3-5 kwenda masomoni kwenye Shule ya Msingi Bwenda iliyoko Kijiji jirani – utoro, mimba na matokeo hafifu ya mitihani ni baadhi ya athari zinazotokana na mazingira hayo ya Elimu Kijijini Bwanga  – hayo yamesemwa na Mwl James William ambae ni Mlezi wa Shule Shikizi inayojengwa na ndie Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bwenda.
Kwa hiyo, Wananchi wa Kijiji cha Buanga WAMEAMUA kujenga Shule SHIKIZI Kijijini mwao wakikusudia hapo mbeleni kuipanua na kuwa Shule kamili ya Msingi inayojitegemea.
Ujenzi wa Shule Shikizi ya Buanga umefikia hatua nzuri ambapo Boma moja la Vyumba Viwili (2) vya Madarasa na Ofisi moja (1) ya Walimu liko kwenye hatua ya ukamilishwaji.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Buanga, Ndugu Kejire Eyembe ameelezea MAFANIKIO ya ujenzi huo kuwa, mbali na MICHANGO ya Wadau mbalimbali na Diwani wao, WANANCHI wa Kijiji cha Buanga wanachangia Nguvukazi kwa kusomba Mawe, Mchanga na Maji. Vilevile kila KAYA inachangia fedha taslimu, Tsh 10,000/= (elfu kumi).
Mwenyekiti huyo ameendelea na kusema kwamba kazi iliyoko mbele yao ni: kupaua na kukamilisha ujenzi wa BOMA hilo na kujenga matundu 10 ya CHOO ya Wanafunzi, na matundu 2 ya CHOO ya Walimu. Vilevile kuna ujenzi wa nyumba ya Mwalimu.
Diwani wa Kata ya Rusoli Mhe Boaz M. Nyeula amewashukuru WADAU mbalimbali wanaochangia ujenzi wa Shule ya Buanga akiwemo Mbunge wa Jimbo lao Prof Muhongo kwa MCHANGO wake binafsi wa SARUJI MIFUKO 50 na MCHANGO na Mfuko wa Jimbo SARUJI MIFUKO 50.
WAZALIWA na WADAU wa Maendeleo waliokwisha CHANGIA ujenzi huu ni:-
1. Jackison Songora
2. Nyabwira Mugonya
3. Jeremia Mugonya
4. Lawrance Wegoro
5. Samson Mbogora
6. Hamis Mgaya
7. Nyang’ura Masatu
8. Shida Samamba
9. Masau Mashauri
10. Emanuel Kusaga
Diwani wa Kata Mhe Nyeula na Mwenyekiti wa Kijiji Ndugu Eyembe wanaomba WAZALIWA wa Kata ya Rusoli na WADAU wengine wa Maendeleo KUJITOKEZA na KUCHANGIA ukamilishaji wa Shule Shikizi ya Kijiji cha Buanga.
Viongozi hao wanaendelea KUMSHUKURU sana Mbunge wa Jimbo, Prof Muhongo kwa kubaini MICHANGO yake mingine  katika Sekta ya Elimu kwenye S/M Bwenda A&B ambapo hadi sasa amechangia  SARUJI MIFUKO 120, MADAWATI 162 na VITABU vingi.

DAN MAPIGANO MEMORIAL SECONDARY SCHOOL – KUANZA KUCHUKUA WANAFUNZI WA FORM I JANUARY 2020

Ujenzi wa Dan Mapigano Memorial Secondary School inayojengwa Kijijini Bugoji.

Alhamisi, 30.05.2019
Jimbo la Musoma Vijijini
*Ujenzi wa Sekondari  hiyo ya Kata ya Bugoji ulianza Disemba 2018
MALENGO:
(1) Ifikapo tarehe 01  Agosti 2019 MAJENGO yanayohitajika Sekondari KUSAJILIWA na Serikali yawe yamekamilika.
(2) January 2020 Wanafunzi wa Form I waanze MASOMO yao hapo. Wengi wao watatoka kwenye Kata ya Bugoji yenye Vijiji 3 –  Kanderema, Kaburabura na Bugoji.
WACHANGIAJI wa UJENZI wa Sekondari hii kupitia HARAMBEE za Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo ni:
A- WANANCHI wa Vijiji 3 vya Bugoji, Kanderema na Kaburabura. Wanasomba maji, mchanga, mawe na kokoto. Vilevile wanachangia Fedha Taslimu – Tsh 17,000  kutoka kila KAYA. Wanalipa MAFUNDI ujenzi.
  B-WAZALIWA wa Kata ya Bugoji na WADAU wengine wa Maendeleo wakiongozwa na Diwani wa Kata Mhe Ibrahimund Malima. Wengine ni:
Mkwaya Toto, Musyangi Kaitira, Chiguti Mwesa, Petro Mufungo, Mafuru Kaitira, Munepo Machumu, Palapala Burenga, Martha Antoni, Mwalimu Morelia, Mwalimu Onesimo, Ndugu Nashoni, Raphael Magoti, Sostenes Ruhumbika, Alfred Majani, Evarist Maganga
C- FAMILIA ya Marehemu Jaji Dan Petro Mapigano
D-MFUKO wa Jimbo la Musoma Vijijini
E- MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo
SHEREHE za uwekaji wa Jiwe la Msingi la Dan Mapigano Memorial Secondary School zilifanywa tarehe 22.04.2019 Gharama za Sherehe hizo zilibebwa na Mbunge wa Jimbo Prof Muhongo, Diwani wa Kata, Mhe Ibrahimund Malima na  Viongozi wengine wa Kata na Vijiji.
MIPANGILIO YA UJENZI NA MAFANIKIO YAKE
(i) Ujenzi wa Vyumba 5 vya Madarasa na Ofisi 2 za Walimu UMEKAMILIKA. Angalia picha hapo chini.
(b) HALMASHAURI inasubiriwa ikamilishe MICHORO ya MAABARA (zitajengwa wa Kijiji cha Kanderema), Vyumba vingine 3 vya Madarasa (vitajengwa na Kijiji cha Bugoji) na Nyumba ya Walimu (itajengwa na Kijiji cha Kaburabura).

BUSAMBARA SECONDARY SCHOOL

Baadhi ya MAJENGO (yanayokamilishwa) ya Busambara Secondary School

Jumanne, 28.05.2019
Jimbo la Musoma Vijijini
LENGO:
*August 2019 Secondary IANDIKISHWE na kutambuliwa na Serikali.
*January 2020  Secondary IANZE kuchukua Wanafunzi wa FORM I wengi wao wakitoka Vijiji vya Maneke, Kwikuba na Mwiringo (Kata ya Busambara)
WACHANGIAJI WA UJENZI WA BUSAMBARA SECONDARY SCHOOL
(1) WANAVIJIJI:
(a) kutoka VIJIJI  vyote 3 wanasomba mawe, kokoto, mchanga na maji. Wanatengeneza tofali na kusaidia MAFUNDI kwenye ujenzi.
(b) Kila KAYA au kila NGUVUKAZI ndani ya Kata ya  Busambara IMECHANGIA na inaendelea KUCHANGIA Fedha taslimu kati ya Tsh 3,000 na 10,000 kwa ajili ya ujenzi huu.
(c) Harambee 2 zilishapigwa kwenye eneo la ujenzi wa Sekondari.
(2) VIONGOZI wa CCM wa Kata na Vijiji na DIWANI wa Kata (CHADEMA) wanachangia ujenzi huu.
(3) VIONGOZI wa Serikali wakiwemo Watendaji wa Vijiji na Kata wanachangia ujenzi huu.
(4) HALMASHAURI YETU inachangia ujenzi huu.
*DED wetu Ndugu John Kayombo anasimamia kwa umakini mkubwa ujenzi huu.
(5) MFUKO wa JIMBO: umechangia MABATI 75
(6) MBUNGE wa JIMBO Prof Sospeter Muhongo anachangia ujenzi huu na ameishatoa: SARUJI MIFUKO 150 na MABATI BANDO 8 (Mabati 96)
(7) NMB (Benki): itachangia MEZA 80 na VITI 80
(8) WAZALIWA wa KATA ya BUSAMBARA: Ndugu zetu waliozaliwa au WAZAZI/UKOO wao wana/una chimbuko la Kata ya Busambara WAMEAMUA KUCHANGIA ujenzi huu na  AHADI ZINATIMIZWA kama ifuatavyo:
(8a) Ndugu Joseph Chikongoye amechangia Tsh 500,000
(8b) ACP Nyakulinga amechangia Tsh 1,000,000
(8c) Wakili/Mchumi Saidi Chiguma amechangia Tsh 500,000.
*DC wetu Dr Vicent Naano Anney ANASIMAMIA VIZURI sana Michango yote inayotolewa.
Hadi sasa MAJENGO yaliyoezekwa na yanayokamilishwa ujenzi ni:
(i) Vyumba vya Madarasa 4 na Ofisi 2 za Walimu
(ii) Jengo la Utawala
TUNAOMBWA TUCHANGIE UJENZI wa SEKONDARI YETU IKAMILIKE kabla ya tarehe 01.08. 2019.

UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI CHA MKIRIRA WAENDELEA VIZURI

FUNDI akiendelea na ujenzi wa Boma la Zahanati ya Kijiji cha Mkirira

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
Jumamosi 25.05. 2019
UJENZI wa Zahanati ya Kijiji cha Mkirira, Kata ya Nyegina unaendelea vizuri baada ya kusuasua kwa miezi michache ya nyuma. Boma linapandishwa vizuri kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini. Maendeleo hayo mazuri yanazidi kuwapa MATUMAINI makubwa Wananchi wa Kijiji cha Mkirira kwani LENGO LAO KUU la upatikanaji wa Huduma ya Afya Kijijini mwao litafikiwa hivi karibuni.
Diwani wa Kata ya Nyegina, Mhe Majira Mchele amemueleza Msaidizi wa Mbunge, Ndugu Fedson Masawa kuwa mafanikio ya ujenzi wa Zahanati hiyo yanatokana na UMOJA na MSHIKAMANO kati ya Wazaliwa wa Kijiji cha Mkirira waishio nje ya Kijiji hicho na  Wazazi, Ndugu na Jamaa zao walioko hapo Kijijini (nyumbani kwao).
Wazaliwa wa Kijiji cha Mkirira walioanza kuchangia Ujenzi wa Zahanati hiyo ni:
(1) Joackim Masumbuko Nyarigo
(2) Dr med Happy Lisso
(3) Beatus John Malima
(4) Boko Dioniz Majinge
(5) Hamis Mbagati Nyarigo
(6) Joseph Nyerere
(7) Rose Nyarigo
(8) Juma Madibi
(9) Nyabise Mbagati Nyarigo
(10) Hasira Masige
(11) Zitta Dioniz Majinge
(12) Fikiri Jumanne Wantai
(13) Gwabhala Msira
Wadau wengine wa Maendeleo nao WANACHANGIA ujenzi huu. Mhe Diwani Majira amewashukuru sana, ambao ni:
(14) Wananchi wa Kijiji cha Mkirira na Diwani (yeye) kwa kusomba Maji, Mchanga, Mawe na kuchanga Fedha za kumlipa Fundi.
(15) Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo amechangia SARUJI MIFUKO 200
(16) Mbunge Viti Maalum, Mhe Amina Makiragi amechangia SARUJI MIFUKO 180
(17) Kampuni ya Nyanza Road imechangia SARUJI MIFUKO 50 na TRIPU 7 za KOKOTO.
Kaimu Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mkirira, Ndugu Pascal Eliga ambae ndiye Msimamizi Mkuu wa ujenzi wa Zahanati hiyo  amesema bado wana ukosefu wa NONDO 100 ili waweze kuharakisha ukamilikaji wa BOMA hilo mapema kabla tarehe 30 June 2019.
UONGOZI wa Serikali ya Kijiji cha Mkirira, kwa niaba ya Wananchi wa Kijiji hicho wanathamini sana MICHANGO ya NDUGU ZAO waishio nje ya Mkoa wa Mara na Wadau wengine wote wa Maendeleo kwa kuchangia ujenzi huo. WANAWAOMBA wazidi KUJITOLEA kutoa MICHANGO YAO ili kukamilisha ujenzi wa Zahanati hiyo mapema iwezekanavyo, kabla ya Januari 2020.

WAZALIWA WA KATA YA NYAMBONO WATEKELEZA AHADI ZAO KWA VITENDO: JENGO LA OPD LA KITUO CHA AFYA NYAMBONO LAKARIBIA KUEZEKWA

Mafundi wakiwa kwenye Ukamilishaji wa Renta ya Jengo la OPD la Kituo cha Afya Nyambono

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
WAZALIWA wa Kata ya Nyambono yenye Vijiji 2 (Nyambono na Saragana) wameendelea kushirikiana na Wazazi, Ndugu na  Jamaa zao huko nyumbani kwako KUJENGA KITUO CHA AFYA cha Kata ya NYAMBONO kwa njia ya KUJITOLEA.
WANANCHI wa Kijiji cha Nyambono wamekubali KUJITOLEA kusomba maji, mawe, mchanga na kokoto na michango ya fedha taslimu ambayo kila KAYA inachangia Tsh. 11,000/= (elfu kumi na moja).
Sambamba na Jitihada hizo za WANANCHI, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof Sospeter Muhongo ameunga mkono Jitihada zao kwa kuchangia SARUJI MIFUKO 100 na NONDO 18.
WAZALIWA au wenye chimbuko la Kijiji cha Nyambono ambao kwa sasa wanaishi nje ya Kijiji hicho ndio walioanzisha MRADI huu wa ujenzi. WAMEANZA KUCHANGIA tokea hatua za awali kabisa (foundation) za UJENZI wa Kituo hiki cha Afya.
Hivi karibuni wamechanga Tsh  5,954,000/= kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya ujenzi vya kukamilisha renta ya Jengo la OPD.
Aidha Uongozi wa Kijiji na Kata ya Nyambono, ukiongozwa na Diwani wa Kata ya Nyambono Mhe Mkoyongi Masatu Nyanjaba umetoa shukrani za pekee kwa WADAU WOTE wanaochangia ujenzi wa Kituo cha Afya Nyambono ambao ni: Wananchi, Wazaliwa wa Nyambono na Mbunge wa Jimbo.
Orodha ya WADAU WACHANGIAJI kwa upande wa WAZALIWA wa Nyambono ni:
1. Mkama Manyama
2. Nice Kuleba
3. Majura Songo
4. Eliud Kwabira
5. Shida Mlegi
6. Beredy Maregesi
7. Maganira Daudi
8. Malenya Sambu
9. David Alal
10. Bunyata Mkama
11. Adonias Mkama
12. Japhet Maganira
13. Mch. Yeremia Magomba
14. Ominde John
15. Albinus Manumbu
16. Benedict Mkama
17. Dickson Mufungo
18. Ching’oro Ebanda, na wengine wote wanaoendelea kutoa ushirikiano na michango yao kwenye ujenzi wa Kituo cha Afya cha Nyambono.
“Kazi bado ni kubwa, MCHANGO wako ni muhimu.” Karibu Tujenge Kituo cha Afya Nyambono.

KILIMO CHA UMWAGILIAJI CHAANZA KUWEKEWA MKAZO JIMBONI MWETU

Wanachama wa Kikundi cha No Sweat No Sweet wakipalilia Shamba lao la VITUNGUU

 Jumatatu, 20.05.2019
Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21, Vijiji 68 na Vitongoji 374 LIMEAMUA KUKUZA KILIMO CHA UMWAGILIAJI
(A) BONDE LA BUGWEMA
Halmashauri ya Wilaya ya Musoma yenye Jimbo la Musoma Vijijini IMEWEKEANA MKATABA na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kuanza KILIMO KIKUBWA cha UMWAGIALIAJI kwenye Bonde la Bugwema. MAZAO Makuu yatakayolimwa ni Pamba, Alizeti, Mpunga, Mahindi na Kunde. Taarifa za Mradi huu zilishatolewa.
(B) KILIMO CHA UMWAGILIAJI CHA WAKULIMA WADOGO WADOGO
Vikundi vya Kilimo cha Umwagiliaji vimeweka wazi Mipango yao ya kushirikiana na Serikali za Vijiji na Kata zao ili kuongeza kasi ya UKUAJI wa Kilimo cha Umwagiliaji Vijijini mwao.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kikundi  cha No Sweat No Sweet, Ndugu Goodluck Wambwe. Kikundi hiki kipo Kijiji cha Bugunda, Kata ya Bwasi.
Ndugu Wambwe alieleza kwamba wamepata mafanikio makubwa ambayo ni pamoja na kujihakikishia kipato cha kutosha kukidhi mahitaji ya kifamilia na mahitaji ya watoto shuleni. Ameendelea na kusema sasa wanalenga kushirikiana na Serikali za Vijiji na Kata kushawishi Wanavijiji wengine nao waanze Kilimo cha Umwagiliaji.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Bugunda,  Ndugu Manyama Bulerwa amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof Sospeter Muhongo kwa kukiwezesha Kikundi hicho (No Sweat No Sweet) kupata Vifaa vya Umwagiliaji kwa kutumia Fedha za Mfuko wa Jimbo. Aliendelea na kusema kuwa Kikundi hicho (No Sweat No Sweet) kimetoa hamasa kubwa, hadi sasa Kijiji chake kina jumla ya Vikundi 15 vya Kilimo cha Umwagiliaji.
Kikundi cha No Sweat No Sweet kimejikita zaidi katika Kilimo cha Mahindi, Matikiti Maji, Nyanya na Vitunguu.
FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO NA KILIMO CHA UMWAGIALIAJI JIMBONI
Kati ya Vikundi 15 vilivyokabidhiwa PAMPU, MIPIRA, MBEGU, n.k. kwa kutumia Fedha za Mfuko wa Jimbo, Kikundi cha No Sweat No Sweet ni moja kati ya Vikundi Vitano (5) tu vilivyoonekana vinafanya kazi vizuri na kukubaliwa kubaki na Vifaa vya Umwagiliaji.  Vikundi vingine 10 vilinyang’anywa vifaa hivyo baada ya kuthibitika kwamba vimeshindwa kabisa  kutumia vifaa hivyo ipasavyo. Vifaa hivyo vinatumika sehemu nyingine Jimboni penye mahitaji ya PAMPU za MAJI.
Vikundi vilivyofanikiwa kubaki na Vifaa vya Umwagiliaji ni: (1) Mwanga Farmers (Kata ya Nyambono), (2) KEUMA (Kata ya Busambara), (3) Angaza (Kata ya Bukumi), (4) Mkulima Jembe (Kata ya Bukima) na (5) No Sweat No Sweet (Kata ya Bwasi).
VIKUNDI hivi vinaomba Halmashauri iwapatie Wataalamu wa Kilimo cha Umwagiliaji na iwasaidie kupata MASOKO mazuri na ya uhakika ya bidhaa zao.

UJENZI WA KITUO CHA AFYA MUGANGO: SERIKALI NA WANANCHI WAENDELEA KUSHIRIKIANA KWENYE UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

Moja kati ya Majengo ya kituo cha afya cha Mugango

15.05.2019
Jimbo la Musoma Vijijini
Wananchi wa Kata ya Mugango WANAENDELEA kutoa SHUKRANI za DHATI kwa SERIKALI yao kwa kuwapatia Tsh Milioni 400 kwa ajili ya kupanua ZAHANATI yao na kuwa KITUO CHA AFYA chenye MAJENGO MAPYA yafuatayo:
(i) Jengo la Upasuaji (Theatre)
(ii) Jengo la Maabara
(iii) Jengo la Wadi ya Mama na Mtoto
(iv) Jengo la Maiti (Mortuary)
(v) Nyumba ya kuishi Daktari
MASHIMO 8 ya MAJI MACHAFU nayo yamejengwa.
Diwani wa Kata ya Mugango, Mhe Charles Magoma (CCM) na Mhe Kadogo Kapi, Diwani Viti Maalum (CCM) wamefanikiwa KUWASHAWISHI Wananchi Wakazi wa Kata ya Mugango KUJITOLEA kusomba MAWE (tripu 60) na MCHANGA (tripu 234) kwa ajili ya ujenzi huu ambao makadirio hadi sasa ya MICHANGO ya Wananchi na Viongozi wao (Madiwani 2 na wengine) wa Kata hiyo ni zaidi ya Tsh Milioni 32.
Daktari Kiongozi wa ZAHANATI ya Mugango, Dr. med. Marwa Saliro Mwita alieleza kwamba Zahanati yenyewe IMECHANGIA ujenzi huo kwa kulipia GHARAMA (Tsh Milioni 3.87) za usombaji wa MAJI na ununuzi wa MAFUTA ya Pampu ya Maji.
HALMASHAURI imechangia Tsh Milioni 8.
Mbunge wa Jimbo, Prof Muhongo alianza kushiriki kwenye upanuzi wa Zahanati hii kuwa KITUO CHA AFYA kwa kuchangia SARUJI MIFUKO 400.
Juzi Jumatatu, 13.05.2019, Mhe DC wa Wilaya Dr Vicent Naano Anney na Mkurugenzi wa Halmashauri Ndugu John Kayombo WALIKAGUA UJENZI wa Kituo hiki cha Afya na kutoa MAAGIZO kwa WAKANDARASI KUKAMILISHA na KUKABIDHI Majengo ifikapo Ijumaa, 17.05.2019.

UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA KIJIJINI SUGUTI WAENDELEA VIZURI

Maendeleo ya ujenzi wa HOSPITALI ya WILAYA Kijijini SUGUTI

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea KUISHUKURU SERIKALI yao kwa kutoa Tsh Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ndani ya Jimbo lao.
HOSPITALI hiyo inajengwa kwenye Kitongoji cha KWIKONERO, Kijijini SUGUTI.
Misingi (foundations) ya MAJENGO NANE (8)  yapo hatua ya kumwaga jamvi na tayari kuanza ujenzi wa  majengo hayo ambayo ni:
(1) Jengo la Maabara
(2) Jengo la OPD
(3) Jengo la Mama na Mtoto
(4) Jengo la Madawa
(5) Jengo la Mionzi
(6) Jengo la Utawala
(7) Jengo la  Kufua Nguo
(8) Jengo la Kuchomea Taka
MATOFALI:
*Ufyatuaji wa matofali unaendelea vizuri hadi sasa yapo matofali 75,000 kati ya 85,990 yanayohitajika.
UCHANGIAJI WA MRADI:
*Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini (Kata 21, Vijiji 68 na Vitongoji 374) WAMEKUBALI KUCHANGIA MRADI huu. Taratibu za Uchangiaji zimewekwa na Viongozi wa ngazi mbalimbali wanahamasisha UCHAGIAJI huu.
KARIBU NAWE UCHANGIE UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA inayojengwa ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.

WANANCHI WA KIJIJI CHA ETARO WAMEDHAMIRIA KUKAMILISHA UJENZI VYUMBA 5 VYA MADARASA IFIKAPO MWISHONI MWA MEI 2019 

Wananchi wa Kijiji cha Etaro wakiendelea na Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa ya S/M Etaro

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
Wananchi wa Kijiji cha Etaro Kata ya Etaro, wanakamilisha Ujenzi wa Vyumba 3 vya Madarasa na tayari wameanza hatua za ujenzi wa Vyumba vingine Viwili (2) vya Madarasa kwenye Shule ya Msingi Etaro.
Awali akizungumza na Msaidizi wa Mbunge wa Jimbo, Ndugu Fedson Masawa, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Ndugu Mangire Stephano Mahombwe alisema, “Shule ya Msingi Etaro ina Mahitaji ya Vyumba vya Madarasa 22, Vilivyopo 10 na kwa wakati huu tunakamilisha Vyumba 3, na baadae tunaanza ujenzi wa Vyumba vingine Viwili (2) ambavyo misingi (foundations) yake tumeishaiweka.”
Mwalimu Mkuu huyo aliendelea kueleza kwamba ifikapo mwishoni mwa Mei hii (Mei 2019), Vyumba vyote vitakuwa vimekamilika.
Mtendaji wa Kijiji cha Etaro Bi Sophia Charles Antone amewashukuru WADAU wa Maendeleo waliofanikisha kuchangia UJENZI wa Miundombinu ya Shule na Upatikanaji wa VIFAA muhimu vya Shule. WADAU hao ni pamoja na WANAKIJIJI wenyewe wa Kijiji cha Etaro waliosomba MAWE, KOKOTO, MCHANGA na MAJI. Mbunge wa Jimbo, Prof Muhongo alichangia MADAWATI 227 (walikuwa na upungufu wa Madawati 249), SARUJI MIFUKO 60, MABATI 54, na kutoa VITABU vingi.
Mkuu wa Wilaya (DC) Dr Vicent Naano Anney alichangia SARUJI MIFUKO 30, na Mchango wa Fedha za Mfuko wa Jimbo ni MABATI 144.
Wananchi wanategemea kwamba uboreshaji wa Miundombinu ya Shule yao, utaboresha ufaulu wa Mitihani ya Darasa la Saba (VII) na kuongezeka kutoka ule wa 33.11% wa Mwaka jana (2018). Wanatamani ufaulu uvuke Asilimia 50 (50%) na kufikia Asilimia 75 (75%).
KARIBU UCHANGIE UJENZI WA MIUNDOMBINU YA SHULE YA MSINGI ETARO.

UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA YA  MRADI WA SERIKALI WA EP4R WATEKELEZWA KIJIJINI CHIRORWE

Mafundi wakiwa kazini wakitekeleza Mradi wa EP4R kwenye Shule ya Msingi Chirorwe.

Alhamisi, 02.05.2019
Jimbo la Musoma Vijijini
Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
Wananchi wa Kijiji cha Chirorwe kilichoko Kata ya Suguti hivi karibuni wameanza UTEKELEZAJI wa MRADI wa EP4R {Education Programme for Results} wa Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa ya Shule ya Msingi Chirorwe.
Ujenzi huo wa Vyumba Viwili (2) na Ofisi 1, pamoja na Matundu Saba (7)  ya Vyoo unaoendelea Shuleni Chirorwe umewapatia Tsh Milioni 46.6 kutoka Serikalini.
Diwani wa Kata ya Suguti, Mhe Denis Ekwabi ANAISHUKURU sana SERIKALI kwa kuchangia ujenzi huu  na ameongeza kwa kusema MCHANGO wa Wananchi kwenye Mradi huu ni KUJITOLEA kufanya kazi ikiwa ni njia ya KUSHIRIKIANA na SERIKALI kuboresha MIUNDOMBINU ya ELIMU Shuleni hapo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Chirorwe, Ndugu Msai Maingu amesema kuwa WANANCHI wameishachangia
Mawe tripu 22, Mchanga tripu 28,  Kokoto tripu 4 na wanasomba Maji ya ujenzi.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Chirorwe Ndugu Martha H. John ameeleza kuwa ujenzi huo utakamilika na MAJENGO kukabidhiwa mwanzoni mwa Mwezi ujao, Juni 2019.
Aidha, Uongozi wa Kijiji cha Chirorwe na Kata ya Suguti kwa ujumla wanatoa shukrani za pekee kwa Mbunge wao Prof Muhongo kwa Jitihada za Maendeleo anazozifanya Jimboni.
MICHANGO ambayo Mbunge wao alishatoa Kijijini Chirorwe, na S/M Chirorwe inajumuisha:
(i) Saruji Mifuko 60 – ambayo iliyotumika kwenye ujenzi wa awali wa Boma la Vyumba  2 vya Madarasa na Ofisi 1.
(ii) Box 10 za Vitabu, zaidi ya Vitabu 1,000
(iii) Madawati 60
(iv) Kijiji cha Chirorwe kilishapokea Mbegu za Alizeti, Mihogo na Mtama kutoka kwa Mbunge wao Prof Muhongo.
Wazaliwa wa Kijiji cha Chirorwe na WADAU wengine wa Maendeleo WANAOMBWA kuchangia UBORESHAJI wa Miundombinu ya ELIMU na AFYA ya Kijiji cha Chirorwe.
“Kutoa ni Moyo, karibuni Tuchangie Maendeleo ya Kijiji cha Chirorwe”.

WANAFUNZI 133 WA FORM I WA SHULE YA SEKONDARI BUKIMA WALIOSUBIRI UPATIKANAJI WA VYUMBA VYA MADARASA  WAANZA MASOMO

Wanafunzi wa Form I wa Bukima Secondary School wakiwa masomoni Shuleni hapo

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
Jumamosi, 28.04.2019
Wanafunzi 133 wa Shule ya Sekondari Bukima waliokuwa wamekosa nafasi ya kujiunga na Kidato cha Kwanza (Form I) kutokana na uhaba wa Vyumba vya Madarasa tayari WAMEANZA Masomo yao ya Form I baada ya kukamilika kwa Vyumba 2 vya Madarasa Shuleni hapo.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Elbert Deogratias amesema, “Kukamilika kwa Vyumba viwili vya Madarasa Shuleni hapa kumewezesha Wanafunzi waliokuwa nyumbani sasa wameanza Masomo yao ya Form I.”
Mwalimu Mkuu huyo aliendelea kueleza kwamba hadi sasa wanavyo Vyumba vya Madarasa vitatu (3) kwa Form I na kila Darasa wanakaa Wanafunzi 62.
Diwani wa Kata ya Bukima, Mhe January Simula anamshukuru sana Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo kwa kutoa KIPAUMBELE cha kuboresha Miundombinu ya  Shule za Msingi na  Sekondari Jimboni mwao, na kubwa zaidi ni lile la Mbunge wa Jimbo kushirikiana na Wananchi na Wadau wa Maendeleo  kukamilisha Vyumba vya Madarasa ili kila Mwanafunzi aliyefaulu na kuchaguliwa kuendelea na Masomo ya Sekondari (Form I) anaenda Shuleni si kubaki nyumbani.
Diwani Simula amebainisha kwamba kwa Ukamilishaji wa ujenzi wa Vyumba vya Madarasa kwenye Sekondari ya Bukima, Mbunge wao amewachangia SARUJI MIFUKO 50.
Fedha za MFUKO wa Jimbo zimewapatia SARUJI MIFUKO 100 na MABATI 58
Vijiji  3 vya Kata ya Bukima, yaani Kijiji cha Kastam, Butata na Bukima vimeshirikiana vizuri sana kuhakikisha ujenzi huo unakamilika mapema na Wanafunzi wanaenda kuanza Masomo ya Sekondari (Form I) badala ya kukaa nyumbani kwa ukosefu wa Vyumba vya Madarasa.
Mafanikio haya yamechangiwa na DC, Dr Vicent Anney na DED, Ndugu John Kayombo – Diwani, kwa niaba ya Kata ya Bukima, anatoa shukrani nyingi kwa Viongozi hawa wawili ambao nao walihakikisha Wanafunzi waliofaulu na kuchaguliwa kwenda Sekondari wanaenda masomoni badala ya kukaa nyumbani kwa ukosefu wa Vyumba vya Madarasa.
Diwani Mhe January Simula ameendelea kumshukuruku Mbunge wao kwa MICHANGO MIKUBWA ya MBEGU (Alizeti, Mihogo, Mtama), SARUJI, MABATI, MADAWATI na VITABU aliyotoa   kwenye Kata hiyo ikiwemo ya kuchangia ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Butata na Wadi la Mama na Mtoto kwenye Zahanati ya Bukima.
UONGOZI na WANANCHI wa Kata ya Bukima bado wanakaribisha MICHANGO ya Uboreshaji wa Miundombinu ya Elimu na Afya kwenye Kata yao.

MAKTABA YAZINDULIWA KISIWANI RUKUBA – ZAWADI YA PASAKA KWA WAKAZI WA KISIWA HICHO 

Safari za BOTI za kwenda na kurudi kutoka Kisiwani Rukuba

Shule ya Msingi ya Rukuba iliyoko Kisiwani Rukuba, Kata ya Etaro imesherehekea UZINDUZI wa MAKTABA ya Shule yao. Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo ndiye aliyezindua Maktaba hiyo.
Maktaba hiyo ina VITABU mchanganyiko vikiwemo vya ngazi zote za Shule na vingine vya kuongeza MAARIFA (knowledge) ya aina mbalimbali. Hii Maktaba itatumiwa na Wanafunzi, Walimu, Wananchi na hata Wageni wanaotembelea Kisiwa cha Rukuba. Kwa hiyo ni Maktaba ya Jamii (Community Library). Mbunge Prof Muhongo AMEHAIDI kuendelea kuipatia MAKTABA hiyo VITABU zaidi.
S/M Rukuba ni MFANO WA KUIGWA – ina Vyumba 11 vya Madarasa (hawapo Wanafunzi wanaosomea chini ya MITI). Walimu wanayo Ofisi yao. Mwalimu Mkuu anayo Ofisi yake peke yake. Walimu wote wanazo nyumba nzuri za kuishi, n.k. na sasa wamepata  MAKTABA!
Kisiwa cha Rukuba kinafungia UMEME wa SOLA.
VIONGOZI wa CHAMA na SERIKALI wa ngazi mbalimbali wamehudhuria uzinduzi huu, akiwemo Katibu wa Chama (CCM) wa Wilaya Ndugu Stephen Koyo.
WANANCHI wakiwemo WANAFUNZI wameshiriki kwenye Chakula cha pamoja cha PASAKA (Easter Lunch).

WANANCHI WA KIJIJI CHA KABEGI  WAAMUA KUJENGA SHULE SHIKIZI KWENYE KITONGOJI CHA BINYAGO

Maboma ya Vyumba vya Madarasa ya Shule SHIKIZI kwenye Kitongoji cha Binyago, Kijijini Kabegi.

Na:Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
Jumatatu, 15.04.2019
Jimbo la Musoma Vijijini
Wananchi wa Kijiji cha Kabegi, Kata ya Ifulifu WAMEAU  KUJITOLEA na KUCHANGIA ujenzi wa Shule SHIKIZI kwenye Kitongoji cha Binyago.
Mradi huu ulianzishwa na WAKAZI wa Kitongoji cha Binyago. Baadae Serikali ya Kijiji cha Kabegi yenye Shule ya Msingi moja tu ILIAMUA MRADI huu upanuliwe kwa lengo la kujenga Shule ya Msingi ya pili. Kwa hiyo hatua ya kwanza ni kuanza na ujenzi wa Shule Shikizi na hatua ya pili ni kujenga Shule ya Msingi inayojitegemea.
Watoto wadogo wa Kitongoji cha Binyago hutembea umbali mrefu wa takribani kilomita sita (6) kwenda Kijiji jirani masomoni kwenye  Shule ya Msingi Nyasurura.
Mtendaji wa Kijiji cha Kabegi, Ndugu Pili Thomas amesema kwamba Kijiji cha Kabegi kina Kaya 390 na kila Kaya IMEKUBALI KUCHANGIA Shilingi Elfu Kumi (Tsh 10,000) kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba vya Madarasa vya Shule SHIKIZI yao.
Maboma ya Vyumba Viwili (2) na Ofisi ya Walimu yako tayari KUEZEKWA.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kabegi, Ndugu Charles Toto amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo kwa kuwaunga mkono Wananchi kwa kuchangia SARUJI MIFUKO 50.
Vilevile wanashukuru kupokea SARUJI MIFUKO 50 kutoka Fedha za Mfuko wa Jimbo.
Ndugu Toto amesema kwamba Mifuko hiyo 100 ya Saruji imeongeza hamasa yao ya kuchangia ujenzi wa Shule Shikizi kwenye Kitongoji chao.
Kiongozi huyo aliendelea kusema kuwa wana MPANGO  wa kuongeza  Vyumba vya Madarasa, kujenga Choo chenye Matundu nane (8) na Nyumba ya kuishi Walimu.
Wananchi wa Kijiji cha Kabegi WANAOMBA Wadau wa Maendeleo wawaunge mkono na kuwachangia, SARUJI, MABATI na MBAO za kukamilisha ujenzi wa Shule hiyo SHIKIZI ambayo hatimae itakuwa Shule ya Msingi inayojitegemea na kufanya Kijiji cha Kabegi kuwa na Shule za Msingi mbili (2).

WANANCHI WA KISIWA CHA RUKUBA WAANZA MAANDALIZI YA UJENZI WA WODI YA MAMA NA WATOTO

Wanachi wa Kisiwa Rukuba wakiendelea na Usombaji wa Mchanga wa kujengea Wodi ya Mama na Watoto.

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
Wakazi wa Kisiwa cha Rukuba kilichopo Kata ya Etaro wameanza maandalizi ya ujenzi wa Wodi ya MAMA na WATOTO kwenye Zahanati ya Kisiwa/ Kijiji chao. Wameanza kusomba MCHANGA na MAWE ya ujenzi huo.
Muuguzi wa Zahanati ya Rukuba Ndugu Jovin Mafuru alimweleza Msaidizi wa Mbunge (Ndugu Fedson Masawa) kwamba UAMUZI wa kujenga Wodi ya MAMA na WATOTO umefanywa na Wananchi wenyewe ikiwa ni muendelezo wa UBORESHAJI wa HUDUMA za AFYA katika Kisiwa cha Rukuba.
Ndugu Jovin ameongezea kuwa, Wodi hiyo ikikamilika itaondoa usumbufu wa kuwapeleka akina MAMA WAZAZI na WATOTO Hospitali ya Mkoa iliyopo Musoma Mjini. Hiyo ni SAFARI ya BOTI ya takribani masaa wawili (2) kwenye Ziwa Viktoria.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji/Kisiwa cha Rukuba Ndugu Japhary Ibrahim Kibhasa alisema ujenzi huo utaanza Mwezi huu (April 2019) na wanatarajia kuukamilisha ifikapo Mwezi Novemba 2019.
Ndugu Kibhasa ameongeza na kusema kwa niaba ya Wananchi wa Kijiji/Kisiwa cha Rukuba kwamba wanatambua na kushukuru sana kupokea Michango ya Wadau wa Maendeleo ya Kisiwa cha Rukuba wakiwemo Mbunge wao Prof Sospeter Muhongo, Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dr Vincent Naano Anney na Mkurugenzi Halmashauri ya Musoma Ndugu John Kayombo.
Aidha, Ndugu Kibhasa amewaomba Wadau wengine na wapenda Maendeleo kuungana na Viongozi hao ili kuunga mkono jitihada za Wananchi wa Rukuba katika ujenzi wa Wodi hilo.
OFISI YA MBUNGE WA JIMBO inawakumbusha kwamba:
(i) Sherehe za PASAKA za Jimbo la Musoma Vijijini zitafanyika Kisiwani Rukuba (20-21.04.2019). Wote mnakaribishwa.
(ii) Maktaba ya Shule ya Msingi Rukuba ITAZINDULIWA tarehe 21.04.2019. Mbunge Prof Muhongo ataipatia MAKTABA hiyo VITABU vingi siku hiyo.

WANAVIJIJI WALIKUBALI ZAO JIPYA LA BIASHARA LA ALIZETI JIMBONI MWAO

Moja ya SHAMBA BORA la ALIZETI Kijijini Masinono, Kata ya Bugwema

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
Wananchi Jimboni Musoma Vijijini wamenufaika na Kilimo cha zao Jipya la ALIZETI lililoanzishwa Jimboni humo na Mbunge wao, Prof Sospeter Muhongo
Akibainisha mafanikio haya mmoja ya WAKULIMA wa ALIZETI Jimboni, Ndugu Tewasa Makunza ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Masinono, Kata ya Bugwema, ameeleza kuwa zao hili la ALIZETI ni zao zuri la BIASHARA lisilo hitaji gharama kubwa kwa Wakulima na kwamba linastahimili UKAME hivyo kuwa na uhakika wa MAVUNO mazuri ukilinganisha na mazao mengine kama Pamba na mengineyo.
Ndugu Makunza ambaye amekuwa akijishughulisha na Kilimo cha zao hili kwa MISIMU MIWILI  iliyopita ameeleza kuwa zao hilo limemuinua zaidi kiuchumi kuliko mazao  mengine ambayo amekuwa akilima, na manufaa zaidi anapokamua MAFUTA, anapata MASHUDU kwa ajili ya MALISHO ya MIFUGO yake.
Ndugu Makunza ameendelea kusema kuwa Idadi ya Mifugo yake hususani, KUKU wameongezeka zaidi katika uzalishaji na ukuaji tangu walipotumia MASHUDU kuwalisha KUKU hao.
Aidha Mkulima huyu (Ndugu Makunza) wa ZAO JIPYA la ALIZETI Musoma Vijijini amekuwa akivuna zaidi ya KILO  1,000 (zaidi ya tani moja) kwa kila msimu. Kwenye Msimu huu amelima EKARI TANO (5) za ALIZETI akitegemea kupata mavuno mazuri.
Zao la ALIZETI ambalo linalimwa Jimboni Musoma Vijijini takribani kwa miaka mitatu (3) sasa, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini amekuwa akitoa MBEGU za ALIZETI BURE kwa Wananchi wa Jimbo lake kama ifuatavyo:
(i) MSIMU WA I: 2016/2017 – Mbunge aligawa kg 4, 682 (Tani 4.68).
(ii) MSIMU WA II: 2017/2018 – Mbunge aligawa kg 4,974 (Tani 4.97).
(iii) MSIMU WA III: 2018/2019 – Mbunge aligawa kg 1, 243.5 (Tani 1.24)
Kwa hiyo kwa ujumla wake Mbunge wa Jimbo Prof Muhongo amegawa bure MBEGU za ALIZETI za jumla ya Kg 9,656 (Tani 9.66) kwa MISIMU 3 mfululizo.
Aidha tunatoa Shukrani kwa Serikali yetu kupitia Wizara ya Kilimo kutupatia TANI KUMI (10) za MBEGU  za ALIZETI kwa ajili ya MSIMU wa Mwaka 2018/2019.
Shukrani za pekee pia zinatolewa kwa Viwanda Vidogo viwili (2) vya Watu Binafsi vilivyokwisha funga MITAMBO yao kwa ajili ya kukamua MBEGU za ALIZETI. Viwanda hivyo ni: SARAGANA OIL MILL kilichojengwa Kijijini Saragana na KUSENYI OIL MILL kilichojengwa Kijijini Kusenyi. Kwa hiyo  SOKO la uhakika liko ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini na kwingineko Mkoani Mara (Bunda na Kiabakari).
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Jitirora cha Kijiji cha Masinono, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji, Ndugu Simion Akito, ametoa Shukrani nyingi kwa Mbunge wao Prof Muhongo kwa namna anavyojitolea kwa MAENDELEO ya Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini.
Kata ya Bugwema ndiyo inayoongoza Kata zote 21 kwenye Kilimo cha ALIZETI.
Kilimo ni Uhai
Kilimo ni Biashara
Kilimo ni Ajira

PAROKIA YA BUKIMA YAJENGA MAABARA YA KISASA YA VIPIMO VYA AFYA

Msaidizi wa Mbunge Fedson Masawa akimkabidhi Saruji Paroko Haule katika Parokia ya Bukima

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof Sospeter Muhongo ametimiza ahadi yake, leo tarehe 06.04.2019, ya kuchangia SARUJI MIFUKO 50 kwa ajili ya Ujenzi wa MAABARA  kubwa ya KISASA ya VIPIMO vya AFYA  inayojengwa katika PAROKIA ya BUKIMA iliyopo Kata ya Bukima.
Awali akifafanua kuhusu ujenzi wa MAABARA hiyo, Kiongozi wa Parokia ya Bukima Padre Haule Emmanuel amesema, MAABARA hiyo itakapokamilika itatoa HUDUMA za KISASA za VIPIMO vya AFYA katika KATA 6 – ambazo ni za Bukima, Bukumi, Bulinga, Bwasi Makojo na Rusoli.
Padre Haule amesema kwa sasa SAMPULI za WAGONJWA za kufanyiwa VIPIMO zinasafirishwa kwenye MABASI kutoka Zahanati za Vijijini hadi kwenye HOSPITAL kubwa ya Musoma Mjini. Huu ni mwendo wa kati ya kilomita 50 na 90 kufika Musoma Mjini.
Padre Haule ameongezea kuwa, kutokana na uhitaji mkubwa wa huduma hiyo, Jengo hilo litakuwa limekamilika kabla ya PASAKA, April 21, 2019 na anamshukuru sana Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof Muhongo kwa MCHANGO wake wa SARUJI MIFUKO 50  itakayosaidia kufanikisha ujenzi huo.

 WANANCHI WA KATA YA MUGANGO WAWA MFANO WA KUIGWA KWA  KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO

Ujenzi unaoendelea kwenye Shule ya Sekondari Mugango

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
Wananchi wa Kata ya Mugango waendelea kuwa MFANO WA KUIGWA kwenye Miradi ya Maendeleo inayopokea MICHANGO ya SERIKALI kwa ajili ya UTEKELEZAJI wake.
Taarifa ya Ujenzi na Uboreshaji wa Miundombinu kwenye Sekondari yao ya Kata (Mugango Secondary School) INATIA MATUMAINI  makubwa.
Sekondari imepokea Tshs Milioni 66.6 kutoka SERIKALINI kwa ajili ya UJENZI wa Vyumba 3 vya Madarasa, Ofisi 1 na Choo chenye Matundu 7 (moja likiwa la Wanafunzi Walemavu).
Wanavijiji, Walimu na Wanafunzi WAMECHANGIA UJENZI huo kama ifuatavyo:
(A) SHULE YENYEWE Walimu na Wanafunzi: (i) wamesomba MORAMU trip 18 (thamani: Tsh 900,000), (ii) wamechangi MITI ya mbao (vipande 88: thamani Tsh 176,000, wameokoa Tsh 1,144,000), (iii) Wamesomba mawe trip 10 (thamani: Tsh 350,000), (iv) Wamesomba maji ya  ujenzi yenye thamani ya Tsh 500,000.
Mwalimu Mkuu Chacha Rugita anatoa makadirio ya Tsh 2,894,000 kuwa thamani ya MCHANGO uliotolewa na WALIMU na WANAFUNZI kwenye ujenzi huu unaoendelea kwenye shule yao.
(B) WANAVIJIJI wakiongozwa na Madiwani wao, Mhe Charles Magoma na Mhe Kadogo Kapi wamechangia: (v) Mchanga trip 40, (vi) Mawe trip 15 na (vii) Kokoto trip 9
MAFANIKIO haya yanatokana na USHIRIKIAKANO MZURI uliopo kati ya WANANCHI (chini ya Uongozi wa Madiwani wao 2 waliotajwa hapo juu), BODI ya Shule (Mwenyekiti Ndugu  Peter Kazimili), na Uongozi wa Shule (Mwalimu Mkuu Ndugu Chacha Rugita).
Mwenyekiti wa BODI ya Shule Ndugu Kazimili ameongezea kuwa, baada ya kukamilisha MRADI huu, wataanza ujenzi wa Miundombinu kwenye Chumba cha Maabara ya BIOLOJIA kwa kutumia SARUJI MIFUKO 50 iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo.
Vilevile Sekondari Mugango wanamshukuru Mbunge wao kwa kuwapatia VITABU vingi na MADAWATI. Wadau wengine wanaoendelea kuchangia Ujenzi na Uboreshaji wa Miundombinu ya Mugango Secondary School ni WANANCHI wakiongozwa na Serikali za Vijiji vyao na Kata yao, kwa kushirikiana kwa karibu sana na Madiwani wao 2, Mhe Charles Magoma na Mhe Kadogo Kapi

SERIKALI YATOA SHILINGI MILIONI 146 KWENYE SHULE YA SEKONDARI KIRIBA

UPAUAJI wa Vyumba vya Madarasa ya Kiriba Secondary School

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi  wa Mbunge
Shule ya Sekondari Kiriba iliyoko Kata ya Kiriba imepokea FEDHA kiasi cha SHILINGI MILIONI 146 kwa ajili ya UPAUAJI wa Vyumba Vitatu (3) vya Madarasa. SERIKALI kupitia TAMISEMI imetoa fedha hizo.
Mkuu wa Sekondari hiyo Mwalimu Revocatus Nyesela amesema kuwa Sekondari hiyo ina UPUNGUFU wa Vyumba Vinne (4) vya Madarasa. Kutokana na upungufu huo WANAFUNZI 190 waliochaguliwa kujiunga na KIDATO cha Kwanza (I) kwa sasa wanasomea katika CHUMBA cha MAABARA.
Mwalimu Nyasela AMESHUKURU SANA SERIKALI na kusema kwamba FEDHA HIZO zitaondoa tatizo la upungufu wa Vyumba vya Madarasa shuleni hapo na Chumba cha MAABARA kitatumika kama ilivyokusudiwa.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Kiriba, Ndugu Pendo Isack amesema kuwa kwa sasa WANANCHI wa Kata ya Kiriba WANASHIRIKI VYEMA katika Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa ya Sekondari yao na WAMEKUBALI  ya kuchangia Shilingi Elfu Kumi na Tano (15,000) kwa KILA KAYA.
MICHANGO hiyo ya WANANCHI imesaidia kukamilisha Maboma Matatu (3) ya Madarasa na Ofisi moja (1) ya Walimu ambayo ndiyo yanaezekwa kwa kutumia fedha hizo za Serikali.
Aidha Mtendaji huyo wa Kata hakusita kumpongeza  Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof Muhongo kwa MICHANGO yake ya  kuboresha SEKTA ya ELIMU kwa kuchangia VITABU kwa Shule za Msingi 8 na Sekondari 1,  MADAWATI 362 kwa Shule za Kata hiyo.
Mtendaji aliendelea kutaja MICHANGO ya Mbunge wao ikiwemo SARUJI MIFUKO 120 kwa S/M Kiriba, MIFUKO 120  kwa S/M Chanyauru, MIFUKO 60 kwa S/M Nyamiyenga, na MABATI 54 S/M Bwai.
Fedha za MFUKO wa JIMBO  zilinunua MABATI 106 kwa  S/M Nyamiyenga na S/M Chanyauru.
Aidha  katika kuboresha utoaji wa elimu katika Kata hiyo Afisa Mtendaji huyo amewaomba WADAU wa Maendeleo  kuchangia UJENZI wa HOSTELI unaotarajiwa kuanza hivi karibuni kwa ajili ya WANAFUNZI  wa KIKE ambapo mpaka sasa Wananchi wameanza kujitolea kusomba mawe na mchanga.

UJENZI NA UKAMILISHAJI WA MAABARA KWENYE SEKONDARI ZA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI 

Ujenzi wa Miundombimu kwenye Maabara ya Sekondari Nyanja ya Kata ya Bwasi

25 March 2019
Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini lina Kata 21, Vijiji 68 na Vitongoji 374.
Jimbo hili kwa sasa lina Shule za Sekondari za Serikali/Kata 18 na Binafsi 2. Kutokana na Ujenzi unaoendelea wa Sekondari Mpya, ifikapo Januari 2020, Jimbo linatarajia kuwa na Jumla ya Sekondari 25 (23 za Serikali/Kata na 2 za Binafsi).
UJENZI WA MAABARA KWENYE SEKONDARI JIMBONI
Sekondari za Serikali/Kata zenye Maabara 3 (Chemistry, Physics and Biology) ZINAZOTUMIKA ni: (i) Mkirira(Maabara 3), (ii) Nyakatende(2) na (iii) Bugwema (1, yenye kutumika kwa masomo yote 3)
Sekondari zote 2 za Binafsi (RC Nyegina na SDA Bwasi) zina Maabara za masomo yote 3.
SEKONDARI ZA NYANJA  NA MUGANGO ZAANZA UKALIMISHAJI WA MIUNDOMBINU YA MAABARA ZAO
SHULE ya Sekondari Nyanja iliyopo Kata ya Bwasi imeanza ujenzi wa Miundombinu ya Maabara zao 3. Sekondari ya Mugango ya Kata ya Mugango nayo iko kwenye zoezi hilo.
Maabara ya Sekondari Nyanja ina Jumla ya Vyumba vitatu ambavyo Bodi ya Shule hiyo imeamua kukamilisha Chumba kimoja ili kiwe ni cha Mfano na badae waendelea na ukamilishwaji wa Vyumba vingine viwili.
Ujenzi huu wa Miundombinu ya Maabara unafanikishwa kwa NGUVU za WANANCHI
WADAU wa MAENDELEO mbalimbali WANAOMBWA WACHANGIE UJENZI na UKAMILISHAJI WA MAABARA HIZI.
Mwezi Januari 2019, Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo alitembelea MAABARA za Sekondari Nyanja na Mugango na atazitembelea tena mwezi ujao, April 2019 na kuendelea kuchangia ukamilishwaji wa MAABARA hizo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Nyanja Mwl Charles F. Ndebele  amesema Sekondari ya Nyanja ina Jumla ya Wanafunzi 510. Wanafunzi wanaosoma Masomo ya Sayansi ni WACHACHE MNO – Form IV ni 11 na Form III ni 15.
Mwalimu Mkuu huyo  amewashukuru Wananchi, Wadau wa Maendeleo wakiwemo Diwani wa Kata yao, Mbunge wa Jimbo, Mkurugenzi wa Halmashauri na Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dr. Vincent Naano kwa kuchangia na kusimamia Maendeleo ya Elimu Musoma Vijijini
Mbali na Maabara hiyo, Mbunge wa Musoma Vijijini Prof Muhongo amewahi kuchangia Saruji, Mabati, Madawati, Vitabu kwa Shule za Kata ya Bwasi na Mbegu za Alizeti, Mihogo na Mtama. Pampu kwa ajili ya Kilimo cha Umwagiliaji ilinunuliwa kutoka kwenye Fedha za Mfuko wa Jimbo.
Iwapo unapenda kuchangia ujenzi wa Maabara hizo, Wasiliana na:
Headmaster
Nyanja Secondary School
+255 754 404 349
+255 679 359 957

JIWE LA MSINGI LA “DAN MAPIGANO MEMORIAL SECONDARY SCHOOL” KUWEKWA TAREHE 18.04.2019

MAJENGO ya Dan Mapigano Memorial Secondary School ya Kata ya Bugoji. yamefikia hatua nzuri.

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
Wananchi wa Kata ya Bugoji Jimboni Musoma Vijijini, wameendelea na ujenzi wa Sekondari yao ya Kata kwa kasi na umakini mkubwa sana.
Sekondari hiyo imepewa jina la “Dan Mapigano Memorial Secondary School”
kwa nia ya kumuenzi Msomi, Mwanasheria mahiri na Jaji wa Mahakama Kuu wa kwanza kutoka Jimbo la Musoma Vijijini. Marehemu Jaji Dan Mapigano alizaliwa Kijiji cha Bugoji.
Kwa sasa Wanafunzi wa Sekondari kutoka Kata ya Bugoji yenye Vijiji 3 (Kaburabura, Kanderema na Bugoji) na Kata ya Nyambono yenye Vijiji 2 (Saragana na Nyambono) wote wanasom kwenye Sekondari ya Nyambono – umbali wa kutembea ni mkubwa, Vyumba vya Madarasa havitoshi, Maabara haijakamilika.
Kwa hiyo Kata ya Bugoji imeamua kujenga Sekondari yake ili KUBORESHA MAZINGIRA ya kujifunza na kufundisha MASOMO ya Sekondari kwa Wanafunzi wa Kata zote mbili.
Akieleza juu ya Ujenzi wa Sekondari hiyo, Diwani wa Kata ya Bugoji,  Mhe Ibrahim Malima amesema tangu ujenzi huo ulipoanza rasmi Mwezi Desemba 2018, unaendeshwa kwa NGUVU za WANANCHI, SERIKALI, MBUNGE wa JIMBO na WADAU wengine wa  Maendeleo kwa mchanganuo ufuatao:
(i) SERIKALI (TAMISEMI):  imetoa Tsh 62.5 Milioni ambazo zitakamilisha Ujenzi wa Vyumba 5 vya Madarasa
(ii) MFUKO wa Jimbo: Saruji Mifuko 75
(iii) MBUNGE wa Jimbo: Saruji Mifuko 50 na anaendelea kuchangia
(iv) WAZALIWA wa Kata ya Bugoji nao wanachangia, orodha ni ndefu –  Diwani Malima, Injinia Nyamuhanga, Mkwaya Toto Songorwa, Mafuru Kaitira, Petro Mfungo, Raphael Magoti, Parapara Bulenga, Kabende Manyama,  Mshangi Kaitira, Munepo Machumu na wengine wanazidi kujitokeza kuchangia ujenzi wa Sekondari ya Kata yao.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Bugoji ambaye pia ni Kaimu WEO wa Kata ya BUGOJI, Ndugu Ernest Maregesi ametoa SHUKRANI NYINGI kwa Wananchi wa Kata hiyo kwa kuwa ndio waanzilishi wa ujenzi huo, Serikali, Mbunge na Wadau wengine wa Maendeleo kwa kuungana pamoja hadi kufikia hatua hiyo kama ifuatavyo:
(i) Boma la Vyumba viwili (2) limekamilika na hivi karibuni wanaanza kupaua baada ya kukamilisha ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Shule na Makamu wake. Ofisi hizi 2 ziko kwenye Jengo hilo.
(ii) Boma lingine la Vyumba viwili (2) na Ofisi 1 wanafunga renta, huku wakiendelea na ufyatuaji wa matofari ili kuanza ujenzi wa Vyumba vingine vya Madarasa na Nyumba ya kuishi Walimu.
Dan Mapigano Memorial Secondary School itafunguliwa rasmi Januari 2020 na kuanza kuchukua Wanafunzi wa Form I.
Jiwe la Msingi litawekwa siku ya Alhamisi, tarehe 18.04.2019, saa 4 asubuhi, Kijijini Bugoji. KARIBUNI WOTE

WANANCHI KIJIJI CHA CHIMATI WAAMUA KUJENGA ZAHANATI YA KIJIJI CHAO

Kazi za ujenzi wa ZAHANATI Kijiji cha Chimati

15.03.2019
Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
Wananchi Kijiji cha Chimati, Kata ya Makojo wameamua KUJITOLEA kujenga ZAHANATI ndani ya Kijiji chao. UAMUZI huu umefikiwa baada ya Wanakijiji hao kuchoshwa na adha ya kutembea umbali mrefu kufuata HUDUMA ya AFYA Kijiji cha Jirani cha Chitare.
Ndugu Juma Nyituga, Mtendaji wa Kijiji cha Chimati amesema kuwa jumla ya WAKAZI 535 wanalazimika kutembea umbali wa kilomita 10  kufuata HUDUMA ya AFYA katika Kijiji cha Chitare. Kwa hiyo wameamua kujenga Zahanati kijijini mwao ili kutatuta tatizo hilo.
Akizungumzia Ujenzi wa Zahanati hiyo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Chimati, Ndugu Masinde Bwire amesema kuwa  kukamilika kwa ZAHANATI hiyo kutaboresha HUDUMA za AFYA Kijijini hapo. Mama Wajawazito, Watoto na Wazee hawatapata usumbufu wa kutembelea umbali mkubwa kama ilivyo sasa.
Mkuu wa Wilaya ya  Musoma Dkt. Vicent Anney amewapongeza Wananchi wa Kijiji cha Chimati na kuwaomba wakamilishe ujenzi wa Zahanati yao mapema iwezekanavyo na vilevile amewashauri  waendelee kuunga mkono SERIKALI kwenye MIRADI ya MAENDELEO yao. Mkuu wa Wilaya huyo alisema Ujenzi wa ZAHANATI hiyo kwa mtindo wa KUJITOLEA ni mfano wa kuigwa na Vijiji vingine.
Aidha sambamba na jitihada hizo za Wananchi Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof Sospeter Muhongo ametoa MCHANGO wa SARUJI MIFUKO 50 akichangia ujenzi wa Msingi (foundation) na akatoa  ahadi ya kuchangia SARUJI MIFUKO mingine 50 wakati wa Ujenzi wa Boma la Zahanati hiyo.
MICHANGO MINGINE mikubwa  aliyokwishatoa Mbunge Prof Muhongo kwenye Kijiji cha Chimati na kwenye Vijiji vingine vya Kata ya Makojo ni: SARUJI, MABATI, MADAWATI, VITABU, MBEGU za Alizeti, Mihogo na Mtama.
Michango hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo ili kuunga mkono juhudi za Wanavijiji kwenye Utekelezaji wa MIRADI yao ya KIPAUMBELE ya ELIMU, AFYA na KILIMO.

UJENZI WA SHULE SHIKIZI BUSAMBARA UMEPATA MSUKUMO MPYA BAADA YA KUSUASUA KWA MIEZI KADHAA

UJENZI wa SHULE SHIKIZI BUSAMBARA unaoendelea na utakamilika ifikapo tarehe 30 Machi 2019.

Jumamosi, 09.03.2019
Jimbo la Musoma Vijijini
Ujenzi wa Shule SIHIKIZI BUSAMBARA iliyoko Kitongoji cha Ziwa, Kijiji cha Mwiringo umepata msukumo  na mwamuko mpya baada ya kushindwa kukamilika tarehe 28 Februari 2019.
Kamati ya Ujenzi na Fundi wao, wametoa AHADI ya kukamilisha ujenzi huo ifikapo tarehe 30 Machi 2019.
Tunaomba WANANCHI waendelee KUJITOLEA kukamilisha MRADI huu wakiweka maanani kwamba SERIKALI yetu imetoa MCHANGO MKUBWA wa Tsh 60 Milioni kwenye MRADI wa  Ujenzi wa Shule SHIKIZI BUSAMBARA.
TUNAENDELEA kutoa SHUKRANI ZETU za DHATI kwa SERIKALI yetu kwa kutoa MICHANGO MIKUBWA kwa UJENZI wa SHULE SHIKIZI za Vitongoji vya Egenge, Kijiji cha Busamba (Tsh 60 M ujenzi umekamilika), Kaguru, Kijiji cha Bugwema  (Tsh 60M, ujenzi unaendelea), Mwikoko, Kijiji cha Chitare (Tsh 60M, ujenzi unakaribia kukamilika).
Vilevile tunapenda kuendelea KUPONGEZA WANANCHI walioamua KUTATUA TATIZO la UMBALI MKUBWA (Km 2 hadi 5 au zaidi) ambao WATOTO WAO wanautembea kwenda Masomoni kwenye Shule za Jirani.
WANANCHI WAMEAMUA kujenga Shule Shikizi ambazo baadae zitapanuliwa na kuwa Shule za Msingi ndani ya Vitongoji na Vijiji vyao.
Mbali ya hizo zilizotajwa hapo juu, Shule Shikizi nyingine zinajengwa:
*Kitongoji cha Kiunda, Kijiji cha Kamguruki
*Kitongoji cha Binyago, Kijiji cha Kabegi
*Kitongoji cha Gomola, Kijiji cha Musanja
*Kitongoji cha Chirugwe, Kijiji cha Buanga
*Kitongoji cha Mwaloni, Kijiji cha Buraga
JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI LITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI kwa karibu sana KUJENGA na KUBORESHA MIUNDOMBINU ya ELIMU na AFYA kwa manufaa ya Wananchi wa Vijijini mwetu na kwa WATANZANIA wote.

S/M RUKUBA YAKARIBIA KUKAMILISHA UJENZI WA MAKTABA YAO – MFANO WA KUIGWA NA SHULE NYINGINE

Maktaba ya S/M Rukuba. Inakamilishwa ujenzi

Shule ya Msingi (S/M) Rukuba iliyoko Kisiwani Rukuba ina MAENDELEO MAZURI kwenye UJENZI na UBORESHAJI wa MIUNDOMBINU YA ELIMU kama ifuatavyo:
(1) Wanafunzi wote (465, March 2019) wanasomea ndani ya Vyumba vya Madarasa. Hawapo wanaosemea CHINI ya MITI.
(2) Shule ina Vyumba 7 vya Madarasa vinavyotumika na ujenzi wa VIPYA 3 unakamilishwa. Kwa hiyo ifikapo 30 March 2019, S/M Rukuba itakuwa na Vyumba 10 vya Madarasa.
(3) Wanafunzi wote 465 wanatumia MADAWATI wakati wakiwa Madarasani. Hayupo anaekaa sakafuni.
(4) Mwalimu Mkuu anayo Ofisi yake pekee. Walimu wengine wanayo Ofisi yao. Walimu hawana Ofisi chini ya Miti.
(5) Walimu wote wanaishi kwenye NYUMBA za SHULE – Makazi ya uhakika.
(6) Shule inakamilisha ujenzi wa MAKTABA itakayotumiwa na Wanafunzi, Walimu, Wakazi na Wageni Kisiwani hapo. Itafunguliwa April 2019 wakati wa Sherehe za PASAKA za Jimbo zitakazofanyika Kisiwani hapo.
(7) Wanafunzi wanapata CHAKULA shuleni kwa siku zote za masomo.
Kisiwa cha Rukuba kina ZAHANATI inayotoa Huduma za Afya.

UFAULU MDOGO NA UMBALI MKUBWA WA SHULE ZA JIRANI VIMEWAFANYA WAKAZI WA KITONGOJI CHA MWALONI KUAMUA KUJENGA SHULE YAO

Wananchi wakiwa kazini – Urekebishaji wa Msingi na Umwagiliaji Matofali.

Jumamosi, 02.03.2019
Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
Kitongoji cha Mwaloni kiko ukingoni mwa Ziwa Victoria ndani ya Kijiji cha Buraga, Kata ya Bukumi.
Wanafunzi wa Kitongoji cha Mwaloni wanasoma Shule za Msingi za jirani: S/M Buraga, mwendo km 3-4 na S/M Chitare, mwendo wa km 2-3.
Kwa Matokeo ya Mitihani ya Darasa la VII ya Mwaka jana (2018), Wanafunzi kutoka Kitongoji cha Mwaloni waliokuwa wanasoma S/M Buraga HAYUPO aliyefaulu Mitihani na kuchaguliwa kwenda Sekondari. Kwa wale waliokuwa wakisoma S/M Chitare ni WAWILI (2)  tu waliofaulu na kuchaguliwa kwenda Sekondari ya Makojo.
Kutokana na hali hiyo ya Elimu ya kutoridhisha kwenye Kitongoji cha Mwaloni, WAKAZI wa Kitongoji hicho WAMEAMUA kujenga Shule yao ya Msingi wakianzia kwa kujenga SHULE SHIKIZI ambayo itawatoa nje WANAFUNZI 34 wa Kitongoji hicho wanaosomea CHINI ya MITI.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Buraga, Ndugu Geliad Mageta ameeleza kamba tayari ufyatuaji wa awali wa MATOFALI umekamilika baada ya kupokea SARUJI MIFUKO 50 iliyonunuliwa na Halmashauri kutoka Fedha za MFUKO wa JIMBO.
MDAU wa Maendeleoa amechangia SARUJI MIFUKO 5 iliyonunuliwa Kijijini Chitare na kukabidhia tarehe 25.02.2019 kwa Viongozi wa Kitongoji cha Mwaloni.
Ndugu Nyajoge Chirya, Mwenyekiti Kamati ya Ujenzi wa Shule hiyo, alisema kuwa SARUJI MIFUKO 5 iliyopokelewa kutoka kwa Mdau wa Maendeleo Jimboni ni MCHANGO muhimu sana kwa ujenzi wa Shule yao ambayo sasa wanaanza kunyanyua BOMA.
Mbunge wao Prof Muhongo aliahidi kuwachangia SARUJI MIFUKO 100 iwapo Halmashauri itaridhia marekebisho ya ujenzi huo
Mbali ya MICHANGO ya Mbunge Prof Sospeter Muhongo ya Madawati, Vitabu, Saruji na Mbegu za Alizeti, Mihogo na Mtama kwa  Kata ya Bukumi, Mbunge huyo wa Jimbo amechangia HUDUMA za AFYA kama ifuatavyo:
(i) SARUJI MIFUKO 50 kwenye ujenzi wa Nyumba ya Mganga wa Zahanati ya Kurugee.
(ii) Gari la Wagonjwa (AMBULANCE) la Zahanati ya Kurugee.
Vilevile Fedha za MFUKO wa JIMBO zilitumika kununua VIFAA VYA KUMWAGILIA (Kilimo cha Bustani) kwa KIKUNDI cha ANGAZA –  Pampu, Mipira na Mbegu.

JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI – UJENZI WA ZAHANATI WAZIDI KUSHIKA KASI JIMBONI

Wananchi na Mafundi wakiendelea na Ujenzi wa Msingi wa Boma la Zahanati ya Kakisheri

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
*Tarehe 01.03.2019*
UJENZI wa Zahanati Mpya umezidi kushika kasi ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini ili kujihakikishia upatikanaji wa Huduma bora za Matibabu (Afya) Jimboni. Hii ni sehemu muhimu ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM (2015-2020).
Hali hii imedhihirika baada ya Vijiji mbalimbali kuongeza kasi zaidi na kushiriki kwa hali na mali katika ujenzi wa ZAHANATI za VIJIJI vyao.
Zahanati ya Kijiji cha Kakisheri kilichopo Kata ya Nyakatende ni moja kati ya Zahanati 13 ambazo ujenzi wake unaendelea kwa kasi kubwa. Hadi kufikia March 4, 2019 ujenzi wa Msingi wa Boma la Zahanati ya Kakisheri utakuwa umekamilika.
Zahanati nyingine zinazoendelea kujengwa Jimboni ni (ii) Zahanati ya Kijiji cha Bukumi inayojengwa kwenye Kitongoji cha Burungu. Vijiji vingine vinavyojenga Zahanati zao ni: (iii) Butata, (iv) Chimati, (v) Chirorwe, (vi) Kurwaki, (vii) Maneke, (viii) Mkirira, (ix) Mmahare, (x) Nyasaungu, (xi) Muhoji, (xii) Kurukerege na (xiii) Bwai Kwitururu.
Akizungumza na Msaidizi wa Mbunge, kwa niaba ya Wana-Kakisheri,  kwenye eneo la ujenzi huo, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji Ndugu Msafiri Corrence amesema, Wananchi wa Kakisheri WAMEAMUA KWA DHATI kuchangia ujenzi wa Zahanati yao ili ikamilike na kuanza kutoa huduma ifikapo January 2020.
Mwenyekiti pia ameshukuru jitihada za Mbunge Prof Muhongo za kuchangia shughuli za Maendeleo Kijijini Kakisheri, MICHANGO hiyo ni pamoja na:
(i) Madawati 99 kwa S/M Kambarage
(ii) Mabati 54 kwa S/M Kambarage
(iii) Saruji Mifuko 60 kwa S/M Kambarage
(iv) Vitabu vingi
(v) Mbegu za Mihogo, Mtama na Alizeti.
Pamoja na Michango hiyo, Wananchi wamezidi kuwaomba Ndugu na Jamaa, Wadau mbalimbali wa Maendeleo ndani na nje ya Jimbo washirikiane na WAKAZI wa Kijiji cha Kakisheri, Kata ya Nyakatende kuchangia ujenzi wa ZAHANATI ya Kijiji hicho ili kufikia malengo yao ya kuanza kuitumia ifikapo Januari mwakani (2020)

MIRADI YA TANROADS NA TARURA NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI YAKAGULIWA

Mhe Bupilipili akimsaidia Mama kwa kubeba Mtoto wa Mama huyo aliyekuwa akivuka Mto Nyamwifi kwenye eneo la Daraja lililokatika.

Jumatatu, 25.02.2019
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Barabara Mkoa wa Mara wametembelea na kukagua MIRADI inayotekelezwa na TANROADS na TARURA ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.
Kiongozi wa Wajumbe hao alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Mhe Lydia Simeon Bupilipili. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Mhe Charles Magoma na Mbunge Prof Sospeter Muhongo walikuwa kwenye ziara hiyo iliyoratibiwa na Wataalamu (Wahandisi) kutoka TANROADS Mkoa na TARURA Wilaya.
Barabara zinazosimamiwa na TANROADS zinafanyiwa matengenezo mazuri na zinapitika kwa MWAKA MZIMA hata wakati wa MSIMU WA MVUA. Barabara kuu ya Musoma-Mugango-Murangi-Makojo-Busekela (km 92) iko kwenye hali nzuri na matayarisho ya kuwekwa LAMI yamekamilika.
Picha Na. 1 na 2 hapo chini inaonyesha Wajumbe wa Bodi, Wataalamu/ Wahandisi wa TANROADS na TARURA wakiwa pamoja na Mhe Bupilipili (mwenye cap ya njano) kwenye Daraja la Kijijini Kusenyi, mahali ambapo ujenzi utaanzia na kuelekea Makojo hadi Busekela.
TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (TARURA Musoma DC) ina Jumla ya BARABARA 85 zenye urefu wa km 474.32 (ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini).
Usimamizi wa BARABARA zilizo chini ya TARURA ni mzuri na matengenezo yanayafanywa kwa kiwango kizuri.
Viongozi wa TARURA wamewaonyesha Daraja kwenye Mto Nyamwifi lilokatika. Hili liko kwenye Barabara ya Bukima-Bulinga- Bwasi. Usanifu wa awali imefanyika na gharama zimekadiriwa kuwa Tsh Milioni 350 ambazo zimeombwa kwenye Bajeti ya 2019/2020.
Viongozi wa TARURA wameeleza kwamba Barabara ya Wanyere – Kataryo, kwenye Mto Suguti nayo inahitaji Daraja jipya.
WAJUMBE wa BODI ya BARABARA Mkoa wa MARA WAMERIDHIKA na kupongeza TANROADS na TARURA kwa kazi nzuri.

MBUNGE ACHANGIA SARUJI KATIKA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA YA S/M RWANGA.

Majengo yanayojengwa kwa MICHANGO ya Wananchi, Mbunge wa Jimbo na Mradi wa EQUIP. Majengo haya yatakamilika tarehe 28.02.2019.

Jumapili 24. 2.2019
Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
Kijiji cha Kasoma ni kati ya Vijiji 5 vinavyounda Kata ya Nyamrandirira. Vijiji vingine ni Mikuyu, Seka, Chumwi na Kaboni
Leo Jumapili, tarehe 24.02.2019 Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo amekabidhi SARUJI MIFUKO 50, akiwa anatimiza AHADI YAKE aliyoitoa hivi karibuni wakati alipotembelea S/M Rwanga.
Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho Ndugu Faustin M. Majura amesema kuwa S/M RWANGA ni shule changa iliyoanzishwa Mwaka 2016, na hadi sasa ina jumla ya Wanafunzi 319 wa Darasa la I – IV. Ina  jumla ya Vyumba vya Madarasa viwili (2) kwa matumizi ya Madarasa 4, kwa hiyo Wanafunzi wanasoma kwa zamu kwa kuachana madasara hayo mawili.
Afisa Mtendaji huyo aliendelea kueleza kuwa Wananchi wa Kijiji cha Kasoma WAMEAMUA KUJITOLEA kujenga Vyumba vya kutosha  ili KUTATUA TATIZO hilo.
Wananchi wanaendelea kuchanga fedha, na kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji kwa ajili ya ujenzi huu.
Mbunge wa Jimbo Prof Muhongo aliwachangia SARUJI MIFUKO 60 iliyowasaidia kujenga Vyumba 2 vya Madarasa ambavyo vinakamilishwa. Mradi wa EQUIP (Mradi wa Ushirika wa Serikali yetu na DfID, UK) nao umechangia ujenzi wa Vyumba 2 vipya hapo shuleni.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Ndugu Fedson B. Msalama ametoa shukrani za pekee kwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini kwa moyo wake wa KUJITOLEA kuchangia  Maendeleo ya JIMBO ZIMA ikiwemo S/M Rwanga. Kiongozi huyo alibainisha MICHANGO ya Mbunge wao kwa Shule yao kwamba ni:
(i) Box 10 za Vitabu. Takribani Vtabu 500
(ii) Saruji Mifuko 60
(iii) Madawati 64
Mfuko wa Jimbo umechangia:
(iv) Mabati 54
(v) Mabati 150  yaliyogawiwa tarehe 20/2/2019 baada ya KIKAO cha WAZI cha kugawa FEDHA hizo kilichofanyika Kijijini Bugoji, Kata ya Bugoji.
SARUJI MIFUKO 50 zilizokabidhiwa leo tarehe 24/2/2019 kwa Viongozi wa Kijiji hicho, zitatumika kwenye UJENZI MPYA wa Vyumba vingine  viwili (2) vya Madarasa. Viongozi wa Kijiji wamesema kwamba ifikapo Jumatano ya tarehe 27.2.2019 Msingi (foundation) utakuwa umekamilika.
OMBI: Uongozi wa Kijiji cha Kasoma na wa S/M Kasoma wanaomba WADAU wa MAENDELEO waungane nao kuijenga S/M Kasoma.

WANANCHI WA KIJIJI CHA WANYERE WAENDELEA NA UJENZI WA VYUMBA VIPYA VYA MADARASA

Wananchi wa Vitongoji vya Mwikoro na Komesi wakiendelea na ujenzi wa Msingi wa Vyumba Vipya 2 vya Madarasa ya Shule ya Msingi ya Wanyere A.

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
Kata ya Suguti inaundwa na Vijiji vinne (4), ambavyo ni Kusenyi, Suguti, Chirorwe na Wanyere.
Kijiji cha Wanyere kina VITONGOJI SITA (6) na Shule za Msingi (S/M) tatu (3) – S/M Wanyere A, S/M Wanyere B, na S/M Murugee.
Kijiji cha Wanyere kimeanza ujenzi wa Vyumba Vipya vya MADARASA kwa Shule zake za  Msingi kwa  MPANGILIO na MGAWANYO ufuatao:
(i) S/M Wanyere A: Vitongoji vya Mihuru na Mururangu – Wananchi wa Vitongoji hivi wanaendelea na ujenzi wa Msingi wa Vyumba vya Madarasa, na wanataraji kukamilisha ujenzi huu ifikapo Alhamisi, 21.02.2019 (kesho)
(ii) S/M Wanyere B: Vitongoji vya Mwikoro na Komesi – Wananchi wa Vitongoji hivi tayari WANAPAUA Vyumba vya Madarasa.
(iii) S/M Mrugee: Vitongoji vya Ambagai na Mrugee yenyewe – Wananchi  wameanza uchimbaji wa Msingi, na matarajio yao ni kuanza ujenzi wa Msingi kabla ya Ijumaa ya wiki hii (kesho kutwa)
Mwenyekiti wa Kijiji cha Wanyere, Ndugu Charles Mtani alieleza kuwa wameamua kuendesha UJENZI huo kwa kugawanya kazi kwa VITONGOJI na hivyo kufanya USHINDANI kati ya Vitongoji ili KUHARAKISHA ujenzi wa Vyumba Vipya vya Madarasa. Lengo ni kuhakikisha kila Kitongoji HAKINA Shule ambayo WANAFUNZI wanasomea nje CHINI ya MITI kwa kukosa Vyumba vya MADARASA.
Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo ameishatoa MICHANGO kadhaa kwa Shule zote 3 kama ifuatavyo: (a) Jumla ya Madawati 293, (b) Jumla ya Vitabu Box 30 (zaidi ya vitabu 1,500), (c) Jumla ya SARUJI MIFUKO 145. Mfuko wa Jimbo umechangia Jumla ya SARUJI MIFUKO 100 na Mabati 58 (S/M Wanyere B).
Diwani wa Kata hiyo ya Suguti, Mhe Dennis Ekwabi ameendelea kusisitiza WANANCHI wa Kata hiyo kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana, kwa kujituma na bila Malumbano. Hii itasaidia kuyatimiza yale waliyojipangia. Aidha pia Mheshimiwa huyo, anaendelea kutoa shukrani za pekee kwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Mhe. Prof Muhongo kwa MIRADI anayoendelea kuitekeleza Jimboni, na pia kwa WANANCHI kwa KUJITOLEA kwao. Ameshukuru Mfuko wa Jimbo akiamini kuwa hizi ni jitihada za SERIKALI  kuunga mkono juhudi za Wananchi za kujitolea kujiletea MAENDELEO yao wenyewe.

WANANCHI WA KIJIJI CHA BUSUNGU WAAMUA KUTOKOMEZA UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MADARASA KWENYE SHULE YAO YA MSINGI

Maendeleo ya Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa vya Shule ya Msingi Busungu

Na: Verediana Mgoma
Msadizi wa Mbunge
Upungufu wa Vyumba vya Madarasa MASHULENI ni tatizo ambalo WANANCHI wa Jimbo la Musoma Vijijini WAMEAMUA KULITATUA kwa kushirikiana na SERIKALI yao.
Wananchi wa Kijiji cha Busungu, Kata ya Bulinga wameamua na kuanza Ujenzi wa Vyumba VIPYA vya Madarasa kuondoa uhaba wa Vyumba vya Madarasa uliopo kwenye Shule ya Msingi Busungu.
Mtendaji wa Kijiji cha Busungu, Ndugu Charles Ndagile amesema kwamba Wananchi wamehamasika kuchangia NGUVUKAZI zao ili kuondoa MIRUNDIKANO ya Wanafunzi madarasani.
 “Tumefanikiwa kunyanyua Maboma ya Vyumba 3 na Ofisi ya Walimu, tukiwa na LENGO la kuondoa kabisa tatizo la UKOSEFU wa Vyumba vya Madarasa kwenye Shule yetu,” alisema Ndugu Charles Ndagile.
Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Ndugu Chacha Magogo alitoa taarifa ya Shule yake na kusema kwamba Shule ina Jumla ya  Wanafunzi 570, ina Madarasa 7 na ina upungufu wa Madarasa 5. S/M Busungu inamshukuru sana Mbunge Prof Muhongo kwa kuchangia SARUJI MIFUKO 110.
“Hatuna Wanafunzi wanaosomea nje chini ya MITI,  lengo letu ni KUONDOA MIRUNDIKANO ya Wanafunzi Madarasani ili kila Darasa lichukue Wanafunzi 45, ” alisema Mwalimu Mkuu, Ndugu Charles Magogo.
Aidha Diwani wa Kata ya Busungu, Ndugu Mambo Japani ameishukuru SERIKALI kwa MISAADA iliyotoa kwenye ujenzi wa Shule za Msingi na Sekondari kwenye Kata hiyo. Vilevile amemshukuru  Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo kwa MICHANGO aliyotoa kwenye Kata hiyo ikiwemo ya MADAWATI, VITABU na MBEGU za MAZAO (Alizeti, Mihogo na Mtama),.
Diwani wa Kata Mhe Mambo Japani anasisitiza na kusema kwamba WAMEAMUA kuboresha MIUNDOMBINU YA ELIMU kwenye Shule zote za Msingi zilizoko ndani ya Kata yao. Aliendelea kutoa SHUKRANI NYINGI kwa Halmashauri na SERIKALI kwa ujumla kwa kuungana na  Wananchi, yeye mwenyewe (Diwani) na Mbunge wa Jimbo kukamilisha ujenzi wa Sekondari Mpya iliyoanza kuchukua Wanafunzi wa Form I Mwaka huu (Jan 2019). Wanakamilisha usajili wa Sekondari hiyo ya Kata (Bulinga Secondary School).

KIJIJI CHA KAKISHERI CHAAMUA KUJENGA ZAHANATI YA KIJIJI CHAO

Uchimbaji (umekamilika) wa Msingi wa Zahanati ya Kijiji cha Kakisheri.

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini limechagua VIPAUMBELE 3 – ELIMU, AFYA na KILIMO. Maji, Umeme, Barabara, n.k. ni NYENZO zinazohitajika kutekeleza, kwa mafanikio makubwa, Miradi ya Vipaumbele hivyo vitatu.
Wananchi wa Kijiji cha Kakisheri, Kata ya Nyakatende, wameanza Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji chao. Uamuzi huu unatokana na Kikao cha Wanakijiji hao na Mbunge wao Prof Sospeter Muhongo uliofanyika kwenye eneo la ujenzi mwezi uliopita (Januari 2019).
Diwani wa Kata ya Nyakatende, Mhe Rufumbo Rufumbo na Ndugu Msafiri Matete Mwenyekiti wa Kijiji cha Kakisheri wamesema kwamba LENGO LAO KUU ni kuhakikisha ujenzi wa Zahanati hiyo unakamilika na kuanza kutoa huduma za matibabu  ndani ya mwaka mmoja kuanzia mwezi huu (Februari 2019 – Februari 2020).
Ujenzi wa Zahanati hii unafuata maelekezo ya Halmashauri yao ya Wilaya ya Musoma. Kila hatua ya ujenzi inakaguliwa na Wataalamu kutoka Halmashauri yao.
Wananchi wanachanga FEDHA, wanasomba mawe, kokoto, mchanga na maji ikiwa ni MICHANGO yao kwenye Mradi huu. Wameishanunua Saruji Mifuko 50 ya kuanzia ujenzi.
Mbunge wa Jimbo, Prof Muhongo atachangia kwa kila hatua itakayafikiwa kwenye ujenzi wa Zahanati hii. Kwa hatua ya msingi (foundation) atachangia Saruji Mifuko 50 na kwa hatua ya kusimamisha Boma atachangia tena Saruji Mifuko 50.
WADAU wa MAENDELEO wanaombwa kuwaunga mkono Wananchi wa Kijiji cha Kakisheri, Kata ya Nyakatende kwenye Mradi wa ujenzi wa Zahanati yao.
“Umoja ni Ushindi, tuungane kujenga Zahanati ya Kijiji cha Kakisheri.”

WANANCHI KIJIJI CHA NYABAENGERE  WAMEAMUA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU KWENYE SHULE YAO YA MSINGI – KILA KITONGOJI KUJENGA DARASA MOJA

Ujenzi na Ufungaji lenta wa Vyumba vya Madarasa na Ofisi za Walimu wa Shule ya Msingi Nyabaengere, Kijiji cha Nyabaengere, Kata ya Musanja

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
Kutokana na idadi kubwa ya Wanafunzi wanaojiunga na ELIMU ya Msingi  kumekuwa na tatizo kubwa la UHABA wa Vyumba vya Madarasa kwenye Shule ya Msingi Nyabaengere iliyoko kwenye Kijiji cha Nyabaengere.
Ndugu Nashoni Manji ambae ni Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyabaengere ameeleza kwamba Wanakijiji WAMEKIRI KWAMBA kuna TATIZO kubwa la UPUNGUFU wa Vyumba vya Madarasa. Kwa hiyo kwa kupitia Halmashauri ya Kijiji chao wamejiwekea UTARATIBU wa KILA KAYA kuchangia kiasi cha SHILINGI ELFU KUMI (10,000) na WAMEKUBALIANA kwamba KILA KITONGOJI kitajenga CHUMBA KIMOJA  cha Darasa.
Aliendelea na kusema, “Tumefanikiwa kunyanyua Maboma ya Vyumba Vinne na Ofisi mbili za Walimu kwa kushirikiana na Viongozi wenzangu wa Vitongoji vya Nyabaengere, Chakaroso, Kairo na Kamugea.”
Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Nyabaengere, Mwalimu Steve Kihoko ameeleza kwamba MATATIZO yaliyopo hapo shuleni yatapatiwa tiba baada ya  kukamilika kwa Vyumba Vinne vya Madarasa. Hakutakuwepo na  mrundikano wa Wanafunzi Madarasani na hawatakuwepo Wanafunzi wanaosomea CHINI YA MITI.
Aidha Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Musanja, Ndugu Elias Ndaro amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo kwa KUCHANGIA SARUJI MIFUKO 60 na Mabati 108. Hayo Mabati yamenunuliwa kutoka Mfuko wa Jimbo.
Mbunge wa Jimbo Profesa Muhongo ameishatoa MICHANGO ya Madawati, na Vitabu (mara tatu) kwenye Shule hii. Vilevile Profesa Muhongo amechangia Ustawi wa Kilimo kwenye Kata hii kwa Wanavijiji kuwapatia bure Mbegu za Alizeti (mara tatu), Mihogo na Mtama.
WADAU wa Maendeleo wakiwemo Wazaliwa wa Kata ya Musanja na Vijiji vyake WANAOMBWA WAJITOKEZE kuchangia ujenzi huu.

KATA YA BUKIMA WAAMUA KUTATUA TATIZO LA UKOSEFU WA VYUMBA VYA MADARASA KWA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MASOMO YA KIDATO CHA KWANZA

Maendeleo ya ujenzi wa Vyumba vya Madarasa vya Sekondari ya Bukima

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
Wananchi wa Vijiji Vitatu vya Kata ya Bukima – Butata,  Kastam na Bukima VIMEAMUA KWA KAULI MOJA na wamedhamilia kukamilisha ujenzi wa Vyumba vya Madarasa ya Kidato cha Kwanza, baada ya Wanafunzi waliofaulu kujiunga na Kidato cha Kwanza kwa Mwaka huu (2019) kukosa mahali pakusomea.
Akizungumzia tatizo hilo, Mkuu wa Shule ya Sekondari  Bukima, Mwalimu  Elberth Deogratias anaeleza kwamba jumla ya Wanafunzi WALIOCHAGULIWA  kujiunga na Kidato cha Kwanza ni 187,  WALIOANZA masomo ni 50, na WANAOSUBIRI uwepo wa Vyumba vya Madarasa (vikamilike kujengwa) ni WANAFUNZI 137
Nao Viongozi wa ngazi mbalimbali wa Kata ya Bukima na Vijiji vyake 3, wamesema kuwa  WANALAZAMIKA kujenga Vyumba Viwili  vya Madarasa  na Kukarabati chumba kimoja kwa lengo la kuepusha WATOTO wao KUKAA MTAANI kwa kukosa mahali pa kusomea!
Naye Mhe January Simula ambaye ni Diwani wa Kata ya Bukima amesema  MIPANGO iliyopo ni kuhakikisha kwamba ifikapo tarehe 01.02.2019, Wanafunzi WANAOSUBIRI Vyumba vya Madarasa kupatikana Bukima Sekondari, WANAANZA MASOMO YAO ya Form I.
 Mhe Diwani Simula amesema, “Tunawashukuru WANANCHI walioamua kujitolea kwenye ujenzi huu na Mbunge wa Jimbo Profesa Muhongo aliyechangia SARUJI MIFUKO 50 kuhakikisha uhaba wa Vyumba vya Madarasa unatatuliwa kwa manufaa ya watoto wetu.”
Aidha ujenzi wa VYUMBA VYA MADARASA ni MPANGOKAZI ENDELEVU  kwa Vijiji hivyo Vitatu kwa kusudio la kuondoa UKOSEFU wa upungufu wa Vyumba vya Madarasa kwenye Shule zote (Sekondari & Msingi) ndani ya Kata hiyo.

UJENZI NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU JIMBONI MWETU NI WA LAZIMA KUFANYIKA SASA NA KWA KASI KUBWA

Vikao vya Wanavijiji wa Kata ya Suguti (Vijiji 4) na Mbunge wao Prof Sospeter Muhongo

Mh. Mbunge Prof Sospeter Muhongo alikuwa kwenye Kata ya Suguti yenye Vijiji 4 (Wanyere, Chirorwe, Kusenyi na Suguti).
Hali ya Miundombinu ya Elimu kwenye Kata ya Suguti, yenye Vijiji 4 na Sekondari 1 ya Kata, inafanana na hali iliyoko kwenye Kata nyingine 18 alizozitembelea Mbunge wa Jimbo.
MIFANO YA KUHUZUNISHA:
(1) S/M Wanyere A iliyoanza kutoa elimu Mwaka 1954, yenye Wanafunzi 537 ina Vyumba vya Madarasa 5 na pungufu 7. Watahiniwa (2018) walikuwa 48, Waliofaulu na kuchaguliwa kwenda Form I ni 18.
(2) S/M Murugee (1996), Wanafunzi 350, Madarasa 6 na pungufu 4. Watahiniwa 36, Waliofaulu na kuchaguliwa 14.
(3) S/M Suguti A (1946), Wanafunzi 638, Madarasa 7 na  pungufu 5. Watahiniwa 62, Waliofaulu 30, Waliochaguliwa 11.
UAMUZI WA WANANCHI NA VIONGOZI WAO
(1) Ujenzi wa Vyumba Vipya vya Madarasa HAUKWEPIKI, NI WA LAZIMA!
(2) Maboma yanayojengwa YAKAMILISHWE KABLA ya Tarehe 30 January 2019. Ujenzi mpya utakaoanza wiki ijayo ukamilike ifikapo 28 February 2019… Marshall Plan of its kind?
HARAMBEE na MICHANGO YA MBUNGE
Utaratibu wa Mbunge wa Jimbo Prof Muhongo ni kwamba ANACHANGIA pale ambapo ujenzi UMEANZA na una RATIBA YA UJENZI inayotekelezeka.
Kwa leo, Jumanne, tarehe 08.01.2019, Mbunge wa Jimbo amechangia (kutegemeana na Ratiba zao za ujenzi zilizokubalika mbele ya Vikao na Mbunge wao):
(1) S/M Murugee
Saruji Mifuko 50
(2) S/M Wanyere B
Mabati 54
(3) S/M Wanyere A&B:
Saruji Mifuko 50
(4) S/M Kusenyi A
Mabati 54
(5) S/M Kusenyi B
Saruji Mifuko 20
(6) S/M Suguti A
Saruji Mifuko 50
(7) S/M Suguti B
Saruji Mifuko 50

WANAFUNZI 232 NDANI YA CHUMBA KIMOJA CHA DARASA – WANANACHI WAAMUA KUTATUA MATATIZO YA UKOSEFU WA VYUMBA VYA MADARASA MASHULEN

Kikao cha Wanakijiji na Mbunge wao Prof Muhongo wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa SHULE MPYA YA MSINGI kwenye Kitongoji cha Gomora, Kijiji cha Musanja, Kata ya Musanja.

Jumatatu, 07.01.2019, Mbunge Prof Sospeter Muhongo AMEENDELEA na Ziara zake za KUKAGUA na KUPIGA HARAMBEE  za Ujenzi na Uboreshaji wa Miundombinu ya ELIMU na AFYA Jimboni. Leo alikuwa kwenye Kata za Musanja na Murangi.
Matatizo ya Miundombinu ya Elimu yanafanana sana kwa karibu Kata zote 21, na Vijiji vyake 68.
MIFANO INAYOTULAZIMISHA SISI SOTE KUBADILIKA NI HII:
(1) UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MADARASA – (a) S/M Nyabaengere (ilianzishwa Mwaka 1996), pungufu vyumba 13,  (b) S/M Kanyega (1952), pungufu vyumba 11
(2) WANAFUNZI (STD VII, 2018) WALIOFAULU vs WALIOCHAGULIWA –
 (a) S/M Murangi B Waliofaulu 21
Waliochaguliwa 5
(b) S/M Lyasembe
Waliofaulu 33
Waliochaguliwa 9
(c) S/M Kanyega
Waliofaulu 61
Waliochaguliwa 30
MFANO WA MATOKEO KIDATO CHA IV (2017)
Mabui Merafuru Secondary School (35 in 2017)
(a) Division III: 3
(b) Division IV: 16
(c) Division 0: 16
Nyumba za Walimu – pungufu 15
Padre anakusudia KUFUNGA HOSTEL ya Wasichana wa Mabui Secondary kwa sababu WAZAZI HAWATAKI WATOTO WAO WAKAE HOSTEL WAKATI WA MASOMO – sababu kuu ni: hawataki kuchangia gunia moja la mahindi kwa mwaka mmoja wa masomo  n.k.
WANANCHI/WAZAZI WAMEKUBALI KUBADILIKA KAMA IFUATAVYO:
(1) Kujenga Vyumba vya Madarasa kwa kasi kubwa na kukamilisha ujenzi huo ifikapo tarehe 30 Jan 2019.
(2) Wanafunzi wote waliofaulu kuendelea na masomo ya Sekondari, wajiunge na Sekondari za Kata zao ifikapo 01.02.2019
(3) Ujenzi wa Vyumba VIPYA vya Madarasa kwenye Shule za Msingi na Sekondari UTAKUWA ENDELEVU KWA MIAKA KADHAA
(4) Msongamano ukiwa mkubwa SHULE MPYA ZIJENGWE, k.m. Mbunge ataweka (28.02.2019) Jiwe la Msingi  la Shule MPYA ya Msingi Kijijini Musanja.
HARAMBEE, MICHANGO & AHADI ZA MBUNGE ZA TAREHE 07.01.2019
(1) Vijiji ambavyo havijaanza ujenzi vianze haraka na Mbunge Prof Muhongo ATAPIGA HARAMBEE za ujenzi  wao.
(2) S/M Nyabaengere, Kata ya Musanja. (a) Saruji Mifuko 60, (b) Mabati 108 (wakiwa tayari kuezeka)
(3) S/M (Mpya) Sombero, Kata ya Musanja. Saruji Mifuko 100 (awamu 2)
(4) Murangi Sekondari. Saruji Mifuko 100 (awamu 2).  Vyumba  Vipya vya Madarasa 2 vikalike na kuanza kutumika ifikapo tarehe 01.02.2019.

WANAFUNZI WA DARASA LA 7 JIMBONI WANAFAULU LAKINI WANACHAGULIWA WACHACHE KUENDELEA NA MASOMO YA SEKONDARI KUTOKANA NA UPUNGUFU MKUBWA WA VYUMBA VYA MADARASA KWENYE SEKONDARI ZA KATA

Baadhi ya Matukio ya ziara ya tarehe 06.01.2019 ya Mbunge Prof Muhongo Kata za Bwasi na Bukima

Kwenye Vikao kati ya Wanavijiji/Wazazi na Mbunge wao Prof Sospeter Muhongo, TATIZO LA UKOSEFU/UPUNGUFU wa Vyumba vya Madarasa kwenye Sekondari za Kata LIMEPATIWA SULUHISHO – UJENZI WA VYUMBA VIPYA.
Ziara ya  Jumapili (06.01.2019) kwenye Kata za Bwasi na Bukima IMEWEKA MSUKUMO MKUBWA WA KUHAKIKISHA Wanafunzi Waliofaulu Mitihani ya Darasa la VII Mwaka Jana (2018), WANACHAGULIWA WOTE KUENDELEA NA MASOMO YA SEKONDARI IFIKAPO tarehe 30 Januari 2019.
Mfano: S/M Bukima A – Waliofaulu ni 41, Waliochaguliwa ni 11 (26.8% ya Waliofaulu). Wanafunzi 30 (73.2% ya Waliofaulu) wamebaki nyumbani wakisubiri nafasi kupatikana kwenye Sekondari ya Bukima ni 30!
UTATUAJI WA TATIZO LA UPUNGUFU/UKOSEFU WA VYUMBA VYA MADARASA KWENYE SEKONDARI ZA KATA –
(1) Jumla ya Sekondari za /Kata/Serikali (Jan 2019) ni: 19 ikiwemo Sekondari Mpya ya Bulinga –  Kila Sekondari ya Kata inajenga Vyumba vya Madarasa 2 (au zaidi) ambavyo vinatarajiwa kukamilika tarehe 15 Jan 2019 au tarehe 30 Jan 2019. Sekondari ya Bukima inaweza kukamilisha Vyumba 3.
(2) Sekondari Mpya zinajengwa kwa kasi kubwa ili zianze kutumika Mwaka huu (2019), ambazo ni 2: Sekondari za Busambara (Kata ya Busambara na Bugoji (Kata ya Bugoji, imependekezwa iitwe, “Dan Mapigano Memorial Secondary School”)
UPUNGUFU/UKOSEFU WA VYUMBA VYA MADARASA KWENYE SHULE ZA MSINGI  –
Tatizo la Wanafunzi kusomea CHINI ya MITI (zaidi ya 13,000) na Msongamano Madarasani (50-200) wa Wanafunzi wa Shule za Msingi nalo LINATATULIWA KWA KUJENGA VYUMBA VIPYA vya Madarasa kwenye Shule za Msingi za Jimboni (112, ikiwemo 1 ya Binafsi)
Mfano: Kijiji cha Bugunda – S/M Bulinga A&B: Wanafunzi wanaosomea CHINI YA MITI ni 615!
Hata S/M Bwasi iliyoanzishwa Mwaka 1952 bado inapungufu mkubwa wa Vyumba vya Madarasa!
MICHANGO YA UJENZI WA VYUMBA VIPYA VYA MADARASA KWENYE SHULE ZA MSINGI na SEKONDARI
Wanavijiji kwenye Vijiji vingi (jumla 68) WAMEAMUA KUJITOLEA kwenye ujenzi huu. Vipo vijiji vichache sana ambavyo MWITIKIO ni HAFIFU!
Wanavijiji wa Kata za Bwasi na Bukima wameendelea kuchangia fedha na kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji kwenye ujenzi huu.
Mbunge Prof Muhongo ameendelea na HARAMBEE kwa ajili ya ujenzi huu na tarehe (06.01.2019) alichangia kama ifuatavyo:
(i) S/M Bwasi – wanavijiji hawajahamasika kutoa michango. Wanajipanga na watamwita Mbunge apige Harambee.
(ii) S/M Kome, Kata ya Bwasi: Mabati 72
(iii) Nyanja Sec School, Kata ya Bwasi: vifaa vya ujenzi vya Maabara – ujenzi ukianza na kuvibainisha.
(iv) Bukima Sec School, Kata ya Bukima: Saruji Mifuko 50.
(v) S/M Mkapa, Kijiji cha Kastamu, Kata ya Bukima: Saruji Mifuko 100 (awamu 2) wakianza ujenzi wiki ijayo.

WANANCHI WA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI WAMEAMUA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU JIMBONI MWAO

Mbunge Prof Muhongo akizungumza na WANAVIJIJI wa Kata za Nyamurandirira na Nyakatende

UKAGUZI na HARAMBEE za Ujenzi  na Uboreshaji wa MIUNDOMBINU ya ELIMU Jimboni – Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo AMEENDELEA KUSISITIZA UMUHIMU wa Upatikanaji wa kutosha na unaokubalika wa Vyumba vya Madarasa kwenye Shule za Msingi na Sekondari.
Msisitizo huo aliendelea kuutoa wakati wa ziara zake  kwenye Kata za Nyamurandirira na Nyakatende.
Kuna TOFAUTI KUBWA SANA za MWITIKIO na USHIRIKI wa Kata na Vijiji vyake kwenye masuala ya MAENDELEO. Mifano ni hiyo hapo chini:
(1) Vyumba vya Madarasa kwenye Shule za Msingi vina wanafunzi kati ya 50 na 150 au zaidi kwenye chumba kimoja. Hii ni hali halisi kwenye kila Kata (tunazo Kata 21, Vijiji 68).
(2) Bado wapo Wanafunzi (zaidi ya 13,000) ndani ya Jimbo letu wanaosemea chini ya miti.
(3) Shule nyingi za Msingi zina upungufu mkubwa wa Vyumba vya Madarasa, kwa hiyo kuna Madarasa yanasoma kwa zamu (shift), asubuhi/mchana.
(4) Kata ya Nyamurandirira yenye Vijiji 5 (Mikuyu, Seka, Chumwi, Kasoma na Rwanga) inayo Sekondari 1 (Kasoma) ambayo ni ya Serikali. Sekondari ya Kasoma yenye Kidato cha I hadi VI ilianza kama Middle School Mwaka 1956. Kwa hiyo Vijiji vyote 5 vya Kata ya Nyamurandirira vinategemea Sekondari moja ya Serikali.
Matokeo yake, kwa Mwaka huu (Jan 2019):
(a) S/M Mikuyu: Wanafunzi 1 tu amechaguliwa kwenda Form I Kasoma Sekondari.
(b) S/M Nyamurandirira: wanafunzi 3 tu ndio wamechaguliwa kwenda Kasoma Sekondari
(c) S/M Chumwi A:
Wanafunzi 19 kati ya 33 Waliofaulu ndio wamechaguliwa kwenda Kasoma Sekondari.
SULUHISHO:
Mbunge Prof Muhongo ameshauri: (a) Vijiji vya Seka, Chumwi na Rwanga VIJENGE Sekondari zao KUPUNGUZA msongamano kwenye Sekondari ya Kasoma.
(b) Wananchi waendelee kujenga kwa kasi kubwa  Vyumba Vipya vya Madarasa kwenye Shule za Msingi na Sekondari.
(c) Mbunge wa Jimbo Prof Muhongo AMEPIGA HARAMBEE ya Ujenzi wa Vyumba Vipya vya Madarasa kwenye Maboma yanayokusudiwa kukamilika kabla ya tarehe 30 Januari 2019.
(d) HARAMBEE na MICHANGO YA UJENZI
Wanavijiji wanaendelea kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji. Vilele wanachangia fedha za ununuzi wa vifaa vya ujenzi.
Mbunge wa Jimbo Prof Muhongo ameendelea kupiga HARAMBEE na yeye mwenyewe kuchangia kama ifuatavyo:
(i) S/M Mikuyu, Kata ya Nyamurandirira Mabati 87
(ii) S/M Rwanga, Kata ya Nyamundarira, Saruji Mifuko 100
(iii) S/M Kigera, Kata ya Nyakatende, Mabati 90
(iv) Zahanati ya Kijiji cha Kakisheri, Kata ya Nyakatende, Saruji Mifuko 100
Vifaa hivyo vya ujenzi kutoka kwa Mbunge VITANUNULIWA SIKU ambayo Wanavijiji watakuwa wako tayari (vifaa vingine vikiwepo) kukamilisha ujenzi wao kwa hatua iliyopangwa.

MBUNGE WA MUSOMA VIJIJINI AENDELEA KUSHIRIKIANA NA WANAVIJIJI JIMBONI KUJENGA NA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU

Prof Sospeter Muhongo AMETIMIZA AHADI YAKE YA KUCHANGIA MABATI BANDO 8, yaani Mabati 112 ya kuezekea Vyumba vya Madarasa 2 katika SEKONDARI MPYA YA KATA YA BUSAMBARA

Matokeo ya Mitihani ya Shule za Msingi na Sekondari kwenye Jimbo la Musoma Vijijini HAYARIDHISHI KABISA – ni tatizo la miaka takribani 10 iliyopita.
Matatizo ya ufaulu mbaya yanajulikana. Moja kati ya hayo ni MAZINGIRA YA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA YASIYOKUWA MAZURI kwa Walimu na Wanafunzi, hasa UKOSEFU au UPUNGUFU wa VYUMBA vya MADARASA.
Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo ANAENDELEA KUSHIRIKIANA na WANAVIJIJI kutatua tatizo la upungufu/ukosefu wa Vyumba vya Madarasa kwenye Shule za Msingi (112, moja ikiwa ya Binafsi) na Sekondari 20 (2 zikiwa za Binafsi).
Januari 2019, Sekondari Mpya ya Bulinga itafunguliwa.
Kata ya Busambara yenye Vijiji 3 (Mwiringo, Kwikuba na Maneke), WIKI IJAYO, ITAANZA KUEZEKA VYUMBA VYA MADARASA 4 ya SEKONDARI MPYA YA KATA HIYO. Kusudio muhimu ni Sekondari hiyo kuanza Masomo ya Form I ifikapo tarehe 01 Februari 2019. Hii itakuwa Sekondari ya 21 ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini (19 za Serikali/Kata na 2 Binafsi).
Mtendaji wa Kata ya Busambara, Bi Sabine Peter Chacha amesema kwamba WANAFUNZI 98 wa Kata ya Busambara WAMEFAULU KUENDELEA na Masomo ya Sekondari lakini WATABAKI NYUMBANI hadi hapo nafasi kwenye Vyumba vya Madarasa itakapopatikana kwenye Sekondari za jirani (zimejaa) au kwenye hiyo ya Kata inayojengwa Kijijini Kwikuba.
Ndugu Kubega, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kwikuba amesema kwamba dhamira ya Wanavijiji wa Kata ya Busambara ni kujenga na kukamilisha baadhi ya majengo muhimu ya awali ili watoto wao 98 waanze Form I ifikapo tarehe 01 Februari 2019.
Leo, Ijumaa tarehe 04.01.2019, Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo AMETIMIZA AHADI YAKE YA KUCHANGIA MABATI BANDO 8, yaani Mabati 112 ya kuezekea Vyumba vya Madarasa 2.
Wanavijiji nao wamenununua Mabati Bando 8 kuezekea Vyumba vya Madarasa 2. Kwa hiyo ndani ya Wiki 2 zijazo, Vyumba vya Madarasa 4 vya Sekondari ya Busambara vitakuwa vimeezekwa.
Wanavijiji wa Kata ya Busambara WANAENDELEA KUOMBA WADAU WA MAENDELEO wachangie angalau Mabati 54 ya kuezeka Ofisi 1ya Walimu. Wao wanaendelea kuchangia ujenzi wa Sekondari yao ya Kata.

KIJIJI CHA BUIRA CHAONYESHA NJIA, CHAJENGA MAKTABA KWENYE SHULE YAKE YA MSINGI

Maboma ya S/M Buira, Kata ya Bukumi, ikiwemo Maktaba yatakayoezekwa kuanzia Jumatatu, 07.01.2019.

Wananchi na Viongozi wa Kijiji cha Buira, Kata ya Bukumi wamejenga MAKTABA kwenye S/M Buira. Uezekaji wake utafanyika wiki ijayo.
Leo, Jumatano, tarehe 02.01.2019 Kijiji cha Buira KIMEPOKEA MREJESHO WA 20% ya Makusanyo yake kutoka kwenye Mwalo wa Buira. Hizi ni takribani Sh Milioni 6. PONGEZI ZA DHATI ZINATOLEWA KWA MKURUGENZI WA HALMASHAURI, Ndugu John Kayombo na Halmashauri yote kwa kuwezesha fedha hizo kupatikana na kurudishwa Kijijini Buira (kupitia Benki).
Sehemu ya fedha hizo imenunua Mabati 57, Saruji Mifuko 20, Mbao na Misumari kwa ajili ya KUEZEKEA: (a) Vyumba vya Madarasa 2, (b) Ofisi ya Walimu,1 na (c) Maktaba 1.
Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo AMETIMIZA AHADI YAKE leo (02.01.2019) kwa kununua MABATI 54 kwa ajili ya ujenzi huo kwenye S/M Buira.
Vilevile Mbunge Prof Muhongo AMEHAIDI KUIGAWIA VITABU Maktaba Mpya hiyo kutoka kwenye Kontena la Vitabu kutoka USA ambavyo bado hajaanza kuvigawa Jimboni. Shule zote za Msingi na Sekondari ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini zimeishagawiwa mara tatu VITABU kutoka USA na UK.
Wananchi na Viongozi kwenye Vijiji vyote 68 WAMEAMUA kutatua TATIZO SUGU la UPUNGUFU wa Vyumba vya Madarasa kwenye Shule za Msingi 112 (ikiwemo 1 ya binafsi) na Sekondari  20 (zikiwemo 2 za binafsi).
JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI – HATUTAKI BAADHI YA WANAFUNZI WAENDELEE KUSOMEA CHINI YA MITI au WABANANE MADARASANI – TUTAFANIKIWA, TUJITUME KWA VITENDO!

WANAVIJIJI WA KATA YA KIRIBA – WASEMA – “HAKUNA MTOTO ALIYECHAGULIWA KWENDA FORM I ATAKAYEBAKI NYUMBANI KWA SABABU YA UKOSEFU WA VYUMBA VYA MADARASA KWENYE SEKONDARI YAO YA KATA.”

Baadhi ya Matukio ya tarehe 31.12.2018 Kijijini Bwai Kwitururu nyumbani kwa Familia ya Prof Muhongo.

Wanafunzi 236 wa Kata ya Kiriba yenye Vijiji 3 wamefaulu na kuchaguliwa kujiunga na Masomo ya Sekondari.
Kutokana na UPUNGUFU MKUBWA wa Vyumba vya Madarasa ni WANAFUNZI 50 tu, watajiunga (07.01.2019) na Masomo ya Sekondari kwenye Sekondari ya Kata ya Kiriba (Kiriba Secondary School).
Wanafunzi 186 WATABAKI NYUMBANI wakisubiri upatikanaji wa Vyumba vya Madarasa kwenye Sekondari ya Kata yao.
UAMUZI WA WANANCHI na VIONGOZI WAO
Tarehe 31.12.2018, wakati wa CHAKULA CHA KUAGA Mwaka (2018) na KUKARIBISHA Mwaka Mpya (2019), Wananchi walitumia fursa hiyo kujadiliana na Mbunge wao Prof Muhongo namna ya KUTATUA TATIZO HILO SUGU LA UKOSEFU WA VYUMBA VYA MADARASA.
Chakula hicho kilitayarishwa na Familia ya Prof Muhongo ya Kijijini Bwai Kwitururu, Kata ya Kiriba.
Tarehe 01.01.2019, UONGOZI WA KATA uliweka RATIBA YA KAZI YA UJENZI WA VYUMBA 4 VYA MADARASA MAPYA yanayohitajika na kazi ya ujenzi inaanza Jumatatu, tarehe 07.01.2019 na kukamilika tarehe 30.01.2019. Ujenzi ukiaanza KWA UAMUZI na MATAKWA ya WANAVIJIJI wa KATA YA KIRIBA, Mbunge wao wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo ataenda kwenye eneo la ujenzi KUPIGA HARAMBEE.
Vilevile Wananchi wamesisitiziwa umuhimu wa kuendelea kuboresha Miundombinu ya Elimu kwenye Shule zao za Msingi na hiyo Sekondari ya Kata.
MWAKA HUU MPYA (2019) NI MWAKA WA VITENDO – KINACHOHITAJIKA NI UTEKELEZAJI WA MIRADI KWA VITENDO.

SHEREHE ZA KRISMASI ZA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI ZIMEFANYIKA KWENYE KANISA LA KATOLIKI KIJIJINI BUKUMI

Sherehe za Krismasi Parokiani Bukima (Miradi ya Ujenzi) na kwenye Kigango cha Bukumi

Leo, Jumanne, tarehe 25.12.2018 Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo kwa kushirikiana na Paroko Emmanuel Sylvester Haule wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bukima WAMEKARIBISHA WANANCHI kwenye Chakula cha Mchana cha Krismasi (Christmas Lunch) kwenye Kigango cha  Bukumi.
Mbunge alipata fursa ya kutembelea MIRADI YA KANISA Parokiani Bukima na amevutiwa sana na MRADI wa UJENZI MAABARA YA AFYA. Kanisa linajenga Maabara ambayo itarahisisha matibabu (vipimo vya sampuli za damu, n.k.) kwenye Zahanati za Kata za Bukima, Bukumi, Bulinga, Makojo na Rusoli. Mbunge amehaidi kuchangia ujenzi huo ifikapo Februari 2019, na amependekeza kwamba Maabara hiyo ianze kutumiwa kabla ya Juni 2019.
Mahubiri ya Paroko Haule yamekazia umuhimu wa: (a) unyenyekevu, (b) upendo, (c) ufanyaji wa kazi kwa bidii, na kuwasihi waumini na wananchi kwa ujumla kuanza Mwaka Mpya wakiwa “watu wapya” wenye unyenyekevu, upendo, na wakiwa wachapa kazi.
Baada ya Ibada, Wanakijiji, Viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa, na Waalikwa  kutoka Madhehebu mengine (wakiwemo Waislamu) walikaribishwa kwenye chakula cha mchana ikiwa ndicho kilele cha Sherehe za Krismasi za Mwaka huu (2018) ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.

KATA ZASHINDANA KUJENGA MIUNDOMBINU YA ELIMU NA AFYA NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Boma la Zahanati ya Kijiji cha Kurwaki, Kata ya Mugango litakaloezekwa na kukamilika Machi 2019

Kwenye ziara za Ukaguzi wa Ujenzi na Uboreshaji wa Miundombinu ya Elimu na Afya, Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo, ameshuhudia USHINDANI MKUBWA kati ya KATA 21 za Jimbo la Musoma Vijijini.
Leo Jumatatu, 24.12.2018 Mbunge alitembelea Kata 2 za Mugango na Nyegina na Vijiji vyake vyote.
(1) KATA YA MUGANGO
(a) Kijiji cha Kurwaki kimekamilisha Ujenzi wa Boma la Zahanati ya Kijiji chao.
Wananchi wa Kijiji cha Kurwaki WAMEDHAMIRIWA kukamilisha Uezekaji wa Jengo la Zahanati yao ifikapo tarehe 30 Machi 2019. Wanaendelea kuchangia ujenzi wa Zahanati yao. Kwenye Harambee ya leo (24.12.2018) WANANCHI wamechangia mbao, misumari na vifaa vingine vya kuezekea Jengo lao. Diwani wao, Mhe Charles Magoma amechangia BANDO 5 za MABATI. Mbunge wao, Prof Sospeter Muhongo amechangia BANDO 12 za MABATI. Kijiji cha Kurwaki kinajenga kwa kasi kubwa Zahanati yao.
(2) KATA YA NYEGINA
(a) Kijiji cha Mkiririra kilichoanza ujenzi wa Zahanati yake wakati mmoja na Kijiji cha Kurwaki, KINAENDA KWA KASI NDOGO kwa sababu ya matatizo ya Uongozi wa Mradi wa Ujenzi wa Zahanati yao. Imeamuliwa kwamba tarehe 28.12.2018 KIKAO CHA WANAKIJIJI kitakaa kutatua matatizo ya Uongozi wa Mradi wao wa Zahanati. Mbunge Prof Muhongo alishachangia SARUJI MIFUKO 200 kwenye Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mkirira. WAZALIWA wa Kijiji cha Mkiririra na WADAU wengine alishachangia kokoto na saruji kwenye Mradi huu.
(b) Kijiji cha  Kurukerege, Kata ya Nyegina kimeamua  kuanza kujenga Zahanati ya Kijiji chao na kuikamilisha ifikapo Juni 2019.
Wananchi wameanza kukusanya vifaa vya ujenzi na watakapoanza Ujenzi wa Msingi wa Boma la Zahanati watamkaribisha Mbunge wao, Prof Muhongo, kupiga HARAMBEE YA UJENZI wa Zahanati ya Kijiji chao cha Kurukerege.

PROF MUHONGO AOMBA JINA LAKE LIACHWE NA BADALA YAKE LICHUKULIWE JINA LA MAREHEMU JAJI DAN MAPIGANO

HARAMBEE (akiwemo mbuzi) ya ujenzi wa Sekondari ya Kata ya Bugoji itakayopewa jina la Marehemu Jaji Dan Mapigano.

Jimbo la Musoma lenye Kata 21, lina Kata 3 ambazo hazina Shule za Sekondari, ikiwemo Kata ya Bugoji. Nyingine zisizokuwa na Shule za Sekondari ni Kata za Ifulifu na Busambara.
Kata za Busambara na Bugoji zimeanza kujenga kwa kasi kubwa Sekondari zao za Kata ambazo zitafunguliwa mwakani (2019).
Leo, Jumamosi, tarehe 22.12.2018 Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo ameendelea na  ziara zake za KUKAGUA na KUPIGA HARAMBEE za Ujenzi na Uboreshaji wa Miundombinu ya Elimu na Afya kwenye Kata za Bugoji (Vijiji 3 – Karenderema, Kaburabura na Bugoji) na Nyambono (Vijiji 2 – Saragana na Nyambono)
Wananchi wa Kata ya Bugoji wameanza ujezi wa Sekondari ya Kata yao. Ujenzi unaenda kwa kasi kubwa sana kwa kusudio la Sekondari hiyo kufunguliwa na kuanzia kutumika ifikapo April 2019.
HARAMBEE ya ujenzi wa Sekondari ya Kata hiyo imekuwa ya mafanikio makubwa. Wakazi wa Vijiji 3 vya Kata  hiyo WAMEKUBALIANA KUCHANGA Tsh 17,500 kutoka kila KAYA. Wanajitolea kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji.
WAZALIWA na WAKAZI wa Kata ya Bugoji WAISHIO NJE ya KATA wameanza KUCHANGA KWA KASI nzuri, MICHANGO ikianzia Saruji Mifuko 50 hadi 5, na fedha kati ya Sh 500,000 (laki 5) na 50,000 (elfu 50). Baadhi ya Wachangiaji hao ni (11) –  Ndugu G Nyamohanga, S Evarist, M Kaitira, K Zakayo, A Mfungo, C  Mwesa,  M Kaitira,  M Burenga, Songorwa na M Kassim.
Mbunge Prof Muhongo amechangia SARUJI MIFUKO 100 kwenye hatua hiyo ya ujenzi.
JINA LA SEKONDARI YA KATA YA BUGOJI
Wananchi wa Kata ya Bugoji, kupitia VIKAO VYAO vinavyotambuliwa kisheria, WALIPENDEKEZA Sekondari hiyo iitwe Jina la Mbunge wa Jimbo – Prof Muhongo Secondary School – sababu kubwa ikiwa ni mchango mkubwa wa maendeleo (Elimu, Afya, Kilimo, n.k.) ambao Mbunge Prof Muhongo anautoa ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.
Prof Sospeter Muhongo kwa HESHIMA na UNYENYEKEVU MKUBWA alipokea OMBI HILO na yeye AKAWASHAURI na KUWAOMBA waache jina lake na kuchukua Jina la Marehemu Jaji Dan Mapigano.
Prof Muhongo kwenye ushawishi wake aliwakumbusha kwamba Marehemu Jaji Dan Mapigani alizaliwa Kijijini Bugoji, alikuwa Msomi wa Kwanza kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania wa kutoka Jimbo la Musoma Vijijini. Vilevile aliwakumbusha utendaji kazi wake (hukumu zake) uliokuwa wa kiwango cha juu ambao bado UNAHESHIMIKA hadi leo hii.
Wananchi wa Kata ya Bugoji WAMELIKUBALI PENDEKEZO la Prof  Muhongo, kwa hiyo Sekondari ya Kata ya Bugoji itapewa jina la Marehemu Jaji Dan Mapigano. Utaratibu utafuatwa.
Mbunge wa Jimbo alitembelea na kukagua Kituo cha Afya cha Nyambono kinachojengwa kwa Mchango Mkubwa kutoka kwa WAZALIWA wa Kijiji cha Nyambono. Mbali ya Mchango wake (Mbunge) wa awali wa SARUJI MIFUKO 100, leo amechangia NONDO 18 ili ufungaji wa renta ukamilike ndani ya siku 10.
Vilevile Mbunge aliongea na kusikiliza kero za Wakazi wa Kijiji cha Saragana.
Mvua zilizokuwa zinanyeesha kwa nguvu sana na kwa muda mrefu zilimzuia Mbunge kufika kwenye Shule za Msingi Kanderema, Bugoji na Kamatondo. Atazitembelea Februari 2019

WANAFUNZI WAWILI  TU WA KUTOKA KITONGOJI CHA BURAGA MWALONI NDIO WAMECHAGULIWA KUENDELEA NA MASOMO YA SEKONDARI – WAZAZI WACHARUKA NA KUAMUA  KUJENGA SHULE YAO YA MSINGI

Wananchi wa Kitongoji cha Buraga Mwaloni wakiwa na Mbunge wao Prof Muhongo kwenye eneo la Ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi, Buraga Mwaloni.

Wanafunzi wa Kitongoji cha Buraga Mwaloni wanalazimika kutembea umbali wa kilomita kati ya 3 na 5, wakipita porini, kwenda masomoni kwenye S/M Buraga.
Kitongoji hicho chenye wavuvi wengi kina KAYA zaidi ya 100. Kwa sasa Darasa la Chekechea (Utayari) la Kitongoji hicho linasomea chini ya mti. Mwaka huu (2018) WANAFUNZI 2 tu ndio WAMEFAULU kuendelea na masomo ya Sekondari.
Matokeo hayo mabaya na umbali mkubwa wanaotembea watoto wa Kitongoji hicho kwenda masomoni, ni sababu nzito zilizowalamisha WAKAZI wa Kitongoji hicho KUAMUA kuanza ujenzi wa Shule yao ya Msingi ambayo wamekusudia ikamilike ifikapo Julai 2019.
Wananchi wanachanga fedha, wanasomba mawe, kokoto, mchanga na maji kwa ajili ya ujenzi huo. Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo ametembelea Kitongoji hicho na kufika kwenye eneo la ujenzi, ameongea na wananchi na hatimae amechangia SARUJI MIFUKO 100 kwa hatua hiyo ya ujenzi. HARAMBEE kubwa itapigwa mwakani.
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ameendelea na ziara zake za KUKAGUA na KUPIGA HARAMBEE za KUCHANGIA Ujenzi na Uboreshaji wa Miundombinu ya Elimu na Afya ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini. Ameendelea kuongea na wanavijiji na kutatua kero zao.
Ukaguzi na Harambee za leo (21.12.2018) imefanyika kwenye Kata 2: Bukumi na Rusoli. Prof Muhongo ametembelea MIRADI kwenye Kata 2 hizo na kuchangia MABATI na SARUJI.
(1) KATA YA BUKUMI
*Kijiji cha Bukumi
(a) Ujenzi wa Zahanati ya Burungu
*Kijiji cha Busekera
(a) Ujenzi wa Maabara, Sekondari ya Mtiro
(b) Vyumba vya Madarasa, S/M Busekera
*Kijiji cha Buira
(a) Vyumba vya Madarasa, S/M Buira
*Kijiji cha Buraga
(a) Vyumba vya Madarasa, S/M Buraga
(b) Ujenzi (mpya) S/M Buraga Mwaloni
(2) KATA YA RUSOLI
*Kijiji cha Kwikerege
(a) Kuzungumza na Wananchi
*Kijiji cha Rusoli
(b) Vyumba vya Madarasa, S/M Rusoli
*Kijiji cha Buanga
(a) Ujenzi (mpya) S/M ya Buanga

UBORESHAJI WA KILIMO CHA ZAO LA MIHOGO NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

KIKAO CHA WATAALAMU WA KILIMO NA WAKULIMA STADI (WAWAKILISHI WA WAKULIMA VIJIJINI), MADIWANI NA MBUNGE WA JIMBO

Washiriki wa Kikao cha, “Kilimo cha Kisasa cha Mihogo ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.

Leo Jumatatu, tarehe 17.12.2018 KIKAO cha MATAYARISHO ya Kilimo cha KISASA cha MIHOGO ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini kimefanyika Kijijini Maneke chini ya Uenyekiti wa Mbunge wa Jimbo Prof Dr Sospeter Muhongo
YALIYOKUBALIWA:
(1) Matayarisho haya ni ya Kilimo cha kuanzia Msimu wa Masika, Machi- Mai 2019
(2) Kilimo cha Zao la Mihogo ndani ya Jimbo (Kata 21, Vijiji 68, Vitongoji 374) liendeshwe kwa Muongozo wa Sheria Ndogo kama ilivyo kwenye Kilimo cha Pamba.
(3) Zao la Mihogo liwe zao la CHAKULA na BIASHARA kwa Jimbo la Musoma Vijijini
AGIZO:
Wataalamu wa Kilimo watawasilisha Andiko hilo kwa Baraza la Madiwani kabla ya tarehe 31.12.2018
Takwimu zinazoonyesha MAHITAJI ya WINGI wa MBEGU ziwakilishwe na Wataalamu kabla ya tarehe 30.01.2019
(4) Mbegu ya MKOMBOZI ndiyo imependekezwa na Wataalamu wa Kilimo kuwa CHAGUO la wakati huu wa MBEGU BORA Jimboni.
(5) ANDIKO LA KUELEKEZA WAKULIMA WA MIHOGO Jimboni litatolewa na Wataalamu wa Kilimo ifikapo tarehe 24.12.2018. Andiko litakuwa la Ukurasa mmoja – aina ya mbegu na upatikanaji wake, mbolea, madawa, upandaji & uvunaji, n.k.
(6) Halmashauri ITUNGE SHERIA ndogo zinazowalinda Wakulima na Wafugaji. Sheria Ndogo za kulinda Mazingira.. miti itakayopandwa nayo ilindwe na Sheria Ndogo za Halmashauri.
(7) ZANA ZA KILIMO
(a) Fursa za Mikopo ya MATREKETA IPO kwa Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS), Vikundi na Watu Binafsi. Halmashauri INASUBIRI KUWASAIDIA WAOMBAJI
(b) PLAU – Ofisi ya Mbunge INASUBIRI KUPOKEA orodha ya Vikundi vya Kilimo VINAVYOOMBA PLAU. Wenye MIFUGO ya kutumiwa kwenye Kilimo cha kutumia PLAU wawemo kwenye Vikundi hivyo.

MIUNDOMBINU YA ELIMU – UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MADARASA NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Wananchi na Viongozi waliohudhuria HARAMBEE ya KUPAUA Maboma 3 ya Sekondari ya Busambara

TUJIKUMBUSHE:
(a) Jumla ya Shule za Sekondari (Jan 2019): 20 (18 Serikali, 2 Binafsi)
* Chumba kimoja cha Darasa KINAPASWA kutumiwa na Wanafunzi 40
(b) Jumla ya Shule za Msingi (Jan 2019): 112 (111 Serikali, 1 Binafsi)
*Chumba kimoja cha Darasa KINAPASWA kutumiwa na Wanafunzi 45.
MATOKEO YA MITIHANI YA STD VII MWAKA HUU (2018)
(a) Wanafunzi Waliofaulu: 3,117
(b) Wanafunzi Waliochaguliwa: 1,649 (52.90%)
(c) Wanafunzi Waliokosa Nafasi: 1,468 (47.10%)
USHAURI/OMBI
(a) TUKIJENGA VYUMBA VINGI ZAIDI kwenye Sekondari zetu, Wanafunzi Waliokosa Nafasi (1,468) WATAPATA NAFASI ZA KUJIUNGA na Form I mwakani (Jan 2019)
(b)Wanafunzi wa Shule za Msingi 13,570 WANASOMEA CHINI YA MITI
WANANCHI WAMEAMUA TUTATUA TATIZO SUGU LA UKOSEFU/UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MADARASA
(a) Wanavijiji WAMEKUBALI KUCHANGA Shilingi 15,000 kutoka kila KAYA.
(b) Wanavijiji WAMEKUBALI KUCHANGIA NGUVU ZAO kwa kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji ya ujenzi.
Jumamosi, tarehe 15.12.2018 Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo AMETEMBELEA na KUKAGUA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA VYA KATA 2 za KIRIBA na BUSAMBARA kama alivyofanya jana (14.12.2018 kwenye Kata za Makojo na Bulinga).
* Sekondari Mpya ya Bulinga itafungiliwa Januari 2019.
HARAMBEE (15.12.2018)
Lengo ni kupiga Harambee ili Shule ya Sekondari Busambara ikamilike na kufunguliwa January 2019.
Wananchi wamejenga na KUKAMILISHA VYUMBA vya MADARASA SITA (6) na OFISI YA WALIMU MOJA (1).
HARAMBEE ya Leo, 15.12.2018 IMEFANIKISHA kupatikana MABATI YA KUEZEKA BOMA MOJA lenye Vyumba vya Madarasa 2.
(a) Mabati ya kuezeka BOMA 1: 216
(b) Bei ya BATI 1: Shilingi 27,000
(c) Michango ya Wananchi (Harambee): Mabati 135
(d) Mchango wa Mbunge wa Jimbo (Harambee): Mabati 96 (bundle 8)

WANANCHI WA KIJIJI CHA CHIMATI WAMEAMUA KUPUNGUZA UHABA WA VYUMBA VYA MADARASA

UJENZI wa Vyumba vya Madarasa kwa njia ya KUJITOLEA, katika Shule za Msingi Chimati A na Chimati B

Na: Verediana Mgoma, Msaidizi wa Mbunge
19.11.2018
WANANCHI wa Kijiji cha Chimati,  Kata ya Makojo wameendelea KUTATUA TATIZO SUGU LA UPUNGUFU wa Vyumba vya Madarasa katika Shule za Msingi mbili (2) za Kijijini mwao, yaani S/M Chimati A na S/M Chimati B, kwa kuboresha Miundombinu ya Elimu ikiwa ni pamoja na UJENZI wa Vyumba vya Madarasa kwa njia ya KUJITOLEA.
Akitoa taarifa za UJENZI wa Vyumba vya Madarasa Shuleni hapo, Mtendaji wa  Kijiji cha Chimati, Ndugu Juma Chacha alimueleza Msaidizi wa Mbunge kuwa WANANCHI wa Kijiji cha Chimati WAMEAMUA KUJITOLEA KUJENGA Vyumba vya Madarasa ili kupunguza na hatimae KUTATUA TATIZO la UPUNGUFU wa Vyumba vya Madarasa kwenye Shule zao mbili (2) za Msingi.
Ndugu Chacha ameongezea kuwa, kutokana na MPANGOKAZI wa UJENZI huo, wamekubaliana KILA KITONGOJI kujenga chumba kimoja cha Darasa ambapo mpaka sasa WAMEFANIKIWA kujenga Vyumba 4 kwa MICHANGO na NGUVU zao wakisaidiwa na WAFADHILI mbalimbali.
Nae Mwenyekiti wa Kijiji, Ndugu Masinde Ndege alimshukuru sana Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo  kwa MCHANGO wake wa SARUJI MIFUKO 60 iliyotumika kwenye UJENZI wa Vyumba Vitatu (3) vya Madarasa
MCHANGO mwingine ulitoka kwenye MFUKO wa JIMBO (fedha zake zinatunzwa na Halmashauri) uliochangia MABATI 54 yaliyotumika kuezeka Chumba kimoja cha Darasa.
Wananchi wa Kijiji cha Chimati wanaendelea kumshukuru Mbunge wao kwa KUCHANGIA MADAWATI 146 kwa Shule zote mbili (2) za Msingi.
Mwenyekiti wa Kijiji  cha Chimati, Ndugu  Masinde Ndege ANAWAOMBA WADAU wa MAENDELEO na WAZALIWA wa Kijiji cha Chimati waishio nje ya Kijiji hicho KUJITOLEA KUCHANGIA ujenzi huo ili ukamilike mapema.
KARIBUNI TUCHANGIE MAENDELEO YETU KWA VITENDO na kwa KUSHIRIKIANA na SERIKALI YETU

SHULE SHIKIZI EGENGE YAKAMILIKA

JENGO la SHULE SHIKIZI EGENGE, Kijiji cha Busamba, Kata ya Etaro.

SERIKALI kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Musoma  INAZIDI KUBORESHA MIUNDOMBIMU YA ELIMU kwenye Jimbo la Musoma Vijijini.
Shule SHIKIZI Egenge ya Kijiji cha Busamba, Kata ya Etaro IMEKAMILIKA.
Mradi wa EQUIP umetoa fedha za ujenzi na WANANCHI wamechangia NGUVU ZAO ili kupunguza gharama za ujenzi.
MAJENGO YA SHULE SHIKIZI EGENGE ni: (i) Vyumba 2 vya Madarasa, (ii) Ofisi 1 ya Walimu, (iii) Vyoo 2 (Wanafunzi 1 & Walimu 1)
Fundi Mkuu, Ndugu Metai Makamba  (kutoka Kijiji cha Lyasembe, Kata ya Murangi: Simu 0743 282 595) anakaribisha WANANCHI na Viongozi mbalimbali waende kujifunza ujenzi bora wa Miundombinu ya Shule kutoka Shule Shikizi Egenge.

BMZ WAKAMILISHA ZOEZI LA UGAWAJI WA VIFAA VYA ELIMU KWA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU

Makabidhiano ya Vifaa vya Elimu Kutoka BMZ Kwenye Kata ya Nyamurandirira na Kiriba.

Na Fedson Masawa, Msaidizi wa Mbunge
MRADI wa BMZ (The Federal Ministry of Economic Cooperation and Development) wa UJERUMANI leo tarehe 8.11.2018 umekamilisha zoezi la Ugawaji wa Vifaa vya Elimu kwa Wanafunzi wenye Ulemavu katika Kata ya Murangi, Nyamurandirira na Kiriba zote za Jimbo la Musoma Vijijini.
Awali akizungumza na WAZAZI wa WATOTO wenye ULEMAVU, Wasaidizi wa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, wawakilishi wa WALIMU na Viongozi wa Serikali ngazi ya Kata na Vijiji, Meneja wa BMZ Mkoa wa Mara, Bi Niwaely Sandy alizitaja Kata 10 zilizo kwenye Mradi kuwa ni Nyambono, Bugwema, Bukumi, Makojo, Bwasi, Bukima, Murangi, Nyamurandirira, Suguti na Kiriba.
Ndugu Niwaely aliendelea kuulezea Mradi huu na kusema, “Vifaa tulivyovigawa ni MADAFTARI, KALAMU na  BEGI za kubebea vifaa vya shule.
Vilevile Mradi wa BMZ umegawa T-shirt kwa Viongozi wa Kata na Wawakilishi wa Walimu kutoka Shule zilizo na Watoto wenye Ulemavu.
Mwenyekiti wa SHIVYAWATA Wilaya, Ndugu Yohana Magai alitoa pendekezo kwa Viongozi wa Serikali la kuwachukulia hatua Wazazi ambao hawataki kuandikisha shuleni watoto wenye ulemavu kwani kufanya hivyo ni kuwanyima haki yao ya msingi ya kupata elimu.
Vilevile Kiongozi huyo amewashauri Viongozi Wahusika wahakikishe MIUNDOMBINU ya MAJENGO ya Taasisi zote iwe rafiki kwa watu wenye ulemavu.
Naye Mtendaji wa Kata ya Kiriba, Bi  Pendo Isack Mwita aliwapongeza BMZ kwa kazi nzuri wanayoifanya katika Jamii na kuahidi kupambana na wazazi wote watakaokataa kuwaandikisha shuleni watoto wenye ulemavu.
Kwa upande wake Mratibu Elimu Kata ya Nyamurandirira, Ndugu Rehema Mateko alisema atahakikisha TAARIFA za Wanafunzi wenye ULEMAVU zinahifadhiwa na kuwasilishwa kwenye Mamlaka husika kwa msaada zaidi pale itakapotokea.
Aidha, mmoja wa Wanafunzi waliogawiwa Vifaa vya Elimu kutoka BMZ, Nyawaye Magesa Kamenge anayesoma Darasa la tatu katika Shule ya Msingi Nyamiyenga, Kijiji cha Kiriba, Kata ya Kiriba alishukuru kwa msaada alioupokea na kuahidi kufanya vizuri zaidi katika masomo yake.
Ofisi ya Mbunge wa Musoma Vijijini imesema itaendelea kushirikiana na BMZ kuhakikisha MRADI wao wa KUSAIDIA na KUWAWEZESHA KI- UCHUMI WALEMAVU unafanikiwa.
TUENDELEE KUWASAIDIA NA KUWAWEZESHA KI-UCHUMI WALEMAVU JIMBONI MWETU – SHUKURANI NYINGI KWA MRADI WA BMZ

UJENZI WA VYUMBA VINNE VYA MADARASA YA SHULE SHIKIZI YA MWIKOKO WAFIKIA HATUA NZURI

Moja kati ya Majengo ya Madarasa Mapya katika Shule SHIKIZI ya Mwikoko ya Kijiji cha Chitare.

Na Verediana Mgoma, Msaidizi wa Mbunge
10.11.2018
Ujenzi wa Vyumba Vinne (4) vya Madarasa na Ofisi Mbili (2) za Walimu katika Shule SHIKIZI ya Mwikoko ya Kijiji cha Chitare, Kata ya Makojo umefikia hatua nzuri ambapo Vyumba Viwili, Ofisi ya Walimu na Choo 1 vinavyojengwa kwa Mchango wa Mradi wa EQUIP (Tsh Milioni 60) vipo katika hatua ya mwisho ya ukamilishwaji. WANANCHI wanachangia NGUVU ZAO kupunguza gharama za ujenzi huu.
Kwa upande wa Vyumba Viwili (2) na Ofisi moja (1) ya Walimu vinavyojengwa kwa MICHANGO ya WANANCHI na WADAU wengine wa Maendeleo akiwemo Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo, vipo hatua ya ukamilishaji wa kozi mbili za mwisho.
Akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi, Mwalimu wa Shule ya Msingi Chitare, Ndugu Charles Amon ambaye pia ni Msimamizi na Mlezi wa Shule Shikizi ya Mwikoko alisema kuwa, UMOJA wa WANANCHI wa Kijiji cha Chitare ndio umeleta mafanikio ya ukamilishaji wa shughuli hizo za ujenzi ili kuwaokoa watoto wao wanaotembea umbali mrefu kufika zilipo Shule za Chitare A na Chitare B.
Ndugu Amon aliongezea na kusema kwamba kukamilika kwa SHULE SHIKIZI hiyo  kutaboresha mahudhurio ya watoto waliokuwa hawafiki shuleni kwa ajili ya umbali mrefu wa kutembea kwenda Shule za mbali.
Aidha Mtendaji wa Kijiji cha Chitare, Ndugu Alex Masija aliwapongeza WANANCHI wa Kijiji cha Chitare katika ujenzi wa shule hiyo pamoja na WADAU mbalimbali waliowaunga mkono hadi kufikia hatua hiyo.
Ili kufanikisha ujenzi wa Shule SHIKIZI ya Mwikoko, Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo alichangia SARUJI MIFUKO 100. Ameridhishwa na matumizi ya Mifuko 50 ya awali na atakapokagua ujenzi huo Mwezi ujao (Disemba 2018) atatoa Mifuko 50 iliyobakia.
MAENDELEO NDANI YA VIJIJI 68 VYA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI YATELETWA KWA VITENDO NA SIYO KWA MANENO MATUPU – TUCHANGIE KWA VITENDO MAENDELEO YA VIJIJI VYETU!

 PROF MUHONGO ACHANGIA SARUJI SIKU YA MAHAFARI YA SHULE YA SEKONDARI SUGUTI

Prof Sospeter Muhongo amechangia Saruji Mifuko 50 kwenye Harambee ya kuchangia ukamilishaji wa ujenzi wa Jengo la Utawala wa Shule ya Sekondari Suguti.

Na Hamisa Gamba, Msaidizi wa Mbunge
Tarehe 23.10.2018
MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof Sospeter Muhongo  amechangia Saruji Mifuko 50  iliyokabidhiwa na Msaidizi wake kwenye Harambee iliyoendeshwa ili kuchangia ukamilishaji wa ujenzi wa Jengo la Utawala wa Shule ya Sekondari Suguti. Haya yalifanyika tarehe 19.10.2018, siku ya Mahafari ya 10 ya Kidato cha IV shuleni hapo.
Awali, akisoma Risala kwa Mgeni Rasmi, Mkuu wa Shule ya Sekondari Suguti,  Ndugu Pendo Kaponoke alitaja changamoto zinazoikabili Sekondari hiyo kuwa ni pamoja na ukosefu wa Maktaba, Maabara, Nyumba za Waalimu za kukidhi mahitaji na Jengo la Utawala.
Akitoa Hotuba kwenye Mahafali hiyo,  Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Musoma, aliyewakilishwa na Ndugu Raymond Romuli ambae ni Katibu Tarafa, aliwaasa Wahitimu, na Wanafunzi wote kutilia mkazo Elimu, na kufanya kwa umakini mitihani yao, na kuwa waadilifu sehemu yoyote wawapo.
Mgeni Rasmi alichangia Tsh 300,000/= ili kufanikisha ujenzi wa Jengo la Utawala huku akiwahamasisha WAZAZI na JAMII kujituma zaidi katika kushiriki na kuchangia shughuli za maendeleo.
Msaidizi wa Mbunge, akiongea kwa niaba ya Mbunge, aliwahimiza Wanafunzi wote kuzingatia sana Elimu kwa kufanya mitihani yao vizuri ili kupata matokeo mazuri. Pia aliwaomba Wazazi wajitume kwa hali na mali kushiriki katika shughuli za Maendeleo kwenye Sekta za Elimu, Afya na Kilimo.
Saruji Mifuko 50 iliyotolewa na Mbunge Prof Muhongo itatumiwa kukamilisha Jengo la Utawala wa Sekondari hii.
Kwa siku za nyuma Mbunge Prof Muhongo alishatoa misaada ya VITABU, MADAWATI, MBEGU ZA ALIZETI, SARUJI MIFUKO 50, n.k kwenye Shule ya Sekondari Suguti.
NDUGU ZANGU WA MUSOMA VIJIJINI – MATOKEO YA MITIHANI YA SHULE ZETU ZA MSINGI NI MABAYA…. naomba tujikumbushe:
(1) “Education comes from within; you get it by struggle and effort and thought.” Napoleon Hill (1883-1970).
(2) “An investment in knowledge pays the best interest.” President Benjamin Franklin (1706-1790)
KARIBUNI TUCHANGIE UBORA WA ELIMU MUSOMA VIJIJINI

WANANCHI WA KIJIJI CHA BUANGA KUKAMILISHA UJENZI WA SHULE JANUARI 2019

Baadhi ya Wananchi na Viongozi wakiendelea na ufyatuaji wa matofali Kijijini Buanga.

Na Verediana Mgoma, Msaidizi wa Mbunge
Oktoba 18, 2018
Wananchi wa Kijiji cha Buanga kwa kushirikiana na Viongozi wa Serikali ya Kijiji hicho wamesema wamejipanga kuhakikisha ifikapo mwezi Januari 2019 watakuwa wamekamilisha zoezi la ujenzi wa Shule mpya ya UTAYARI inayojengwa Kijijini humo.
Hayo yalisemwa na Viongozi wa Kijiji cha Buanga kwa niaba ya Wananchi wao jana tarehe 17. 10. 2018 wakati wakiendelea na zoezi la ufyatuaji wa matofali kwenye eneo la ujenzi wa Shule ya UTAYARI Mpya Buanga.
Awali, akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Buanga Ndugu Kejile M. Eyembe alisema, “tunashukuru sana kwa mchango wa Mbunge wa jumla ya Saruji Mifuko 100. Tayari ametupatia Saruji Mifuko 50 leo itakamilika katika hatua ya ufyatuaji wa matofali na kesho tutakabidhiwa  Saruji Mifuko 50 iliyobakia kama alivyoahidi Mbunge alipoendesha Harambee ya ujenzi huu tarehe 9.10.2018. Ujenzi wa boma utaenda kwa kasi kubwa sana.”
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Rusoli Mhe Boazi M. Nyeula amezidi kumshukuru Mbunge kwa dhamira yake ya kujitolea katika kufanikisha Maendeleo Vijijini mwetu.
Mhe Diwani Boazi ameongezea kuwa ana imani na kasi ya Wananchi wa Buanga kwani muda mwingi wapo kazini na kusema, “sisi kama viongozi tutaendelea kuwashirikisha kwa karibu sana Wazawa wa Kata yetu na Kijiji chetu kufanikisha ujenzi huu kabla ya Februari 2019.”
NJOONI TUCHANGIE MAENDELEO KWA VITENDO

PROF MUHONGO ASHIRIKI HARAMBEE UJENZI WA BWENI LA WASICHANA LA SEKONDARI YA BWASI

Viongozi mbalimbali walioshiriki katika Harambee ya kuchangia Ujenzi wa Bweni la Wasichana katika Shule ya Sekondari Bwasi

Na Verediana Mugoma, Msaidizi wa Mbunge
OFISI ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini imekabidhi mchango SARUJI MIFUKO  50 ya kutoka kwa Mbunge wa Jimbo hilo Prof Sospeter Muhongo kwa ajili ya kuchangia ukarabati wa Bweni la Wasichana katika Shule ya Sekondari Bwasi iliyopo Kijijini Bwasi, Kata ya Bwasi.
Akizungumza kabla ya kukabidhi Mchango huo kwa niaba ya Mbunge, Msaidizi wa Mbunge Verediana Mgoma alisema,
“Ili kuharakisha shughuli za maendeleo Jimboni, WANANCHI VIJIJINI, WADAU WA MAENDELEO,  WAZAWA wa Jimbo la Musoma Vijijini na RAFIKI ZAO hawana budi kujitolea na  kushiriki kikamilifu kuchangia MAENDELEO YA VIJIJI VYETU kwa KUSHIRIKIANA na SERIKALI, Madiwani na Mbunge wa Jimbo  kufikia malengo yaliyowekwa kwa wakati.”
Naye Mgeni Rasmi katika Harambee hiyo Dr. Fredy J. Gamba, amemshukuru Prof Muhongo kwa kuipa kipaumbele Sekta ya Elimu na kusema kama WANANCHI wataungana pamoja na kumuunga mkono Mbunge, Musoma Vijijini itapiga hatua nzuri ya maendeleo ya Elimu na itakuwa ya mfano wa kuigwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Bwasi Ibrahim Chacha ametoa shukrani zake za dhati kwa WACHANGIAJI WOTE walioshiriki katika kufanikisha HARAMBEE hiyo na kuahidi kuitumia SARUJI iliyotoka kwa Mbunge ndani ya kipindi kifupi kama ulivyo utaratibu wa matumizi ya vifaa vinavyotoka kwa Mbunge wa Jimbo.
Sekondari ya Bwasi imeishapokea VITABU VYA MASOMO YA SEKONDARI kutoka kwa Mbunge Prof Muhongo. Vitabu hivyo vinatoka USA na UK. January 2019, Mbunge amepanga kugawa vitabu kwa mara ya nne (4) kwa Shule zote za Sekondari na Msingi za Jimboni.
JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI – QUALITY EDUCATION AT ALL LEVELS

VIKUNDI VYA BUSTANI KUTOA FURSA ZAIDI ZA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

Vijana wa Kikundi cha No Sweat No Sweet cha Kijijini Bugunda wakiwa wanaendelea na kazi za Uzalishaji kwenye bustani yao

Na Verediana Mgoma, Msaidizi wa Mbunge
VIKUNDI vya Kilimo cha Umwagiliaji ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini vimejipanga kutoa ELIMU itakayohamasisha VIJANA na AKINA MAMA  kuchangamkia fursa za KILIMO cha UMWAGILIAJI hasa kwa jamii zinazoishi karibu na vyanzo vya maji mengi yanayoweza kutumika kwenye umwagiliaji.
Hayo yamezungumzwa mapema wiki hii na Ndugu Gudluck Wambwe ambaye ni Mwenyekiti wa Kikundi cha NO SWEAT NO SWEET cha Kijijini Bugunda, Kata ya Bwasi.
Kikundi hicho cha Kijijini Bugunda, kwa kipindi kirefu kimekuwa kikijishughulisha na Kilimo cha Bustani za Mbogamboga na Matunda.
Ndugu Gudluck Wambwe alisema kuwa, wamekuwa wakipata maarifa ya Kilimo cha Umwagiliaji kutoka kwa  Mtaalamu wa Kilimo wa Kata yao.
Ameongezea kuwa “Kupitia Kilimo cha Umwagiliaji tayari wamekwishanufaika na faida za Kilimo hicho ni nyingi zikiwemo: kuwa na uwezo wa kifedha wa kugharimia mahitaji ya shule ya watoto wao, na kujipatia mahitaji mbalimbali ya kifamilia.”
Aidha, Kiongozi huyo alisema kuwa, malengo yao ya sasa ni kuielimisha jamii kuhusu Kilimo cha Umwagiliaji tofauti na ilivyozoeleka hapo awali kujikita kwenye Kilimo cha Asili (msimu wa mvua) peke yake.
Kwa upande wake Afisa Kilimo wa Kata, Ndugu Gustav Tesha alieleza kuwa, anaendelea kuwapa elimu wakazi wa Kata za Bulinga na Bwasi juu ya Kilimo cha Umwagiliaji na anakiri kwamba jamii imekubali kubadilika na kuwa na mtazamo mpya wa kushiriki katika Kilimo cha Umwagiliaji.
Ikumbukwe kuwa, Kikundi cha NO SWEAT NO SWEET ni moja kati ya Vikundi 15 vilivyofadhiliwa Pampu, Mipira ya umwagiliaji na Mbegu kutoka kwenye Mgao wa FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO awamu ya kwanza.
Wanakikundi na Washiriki wa Kikundi cha NO SWEAT NO SWEET wanamshukuru Mbunge wao Prof. Muhongo kwa juhudi zake za kuipa kipaumbele Sekta ya Kilimo cha Kisasa na chenye Manufaa ili kuinua Uchumi wa Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini na wanasema kwao Kilimo ni Ajira.

KILIMO CHA KISASA CHA WANANCHI WENYEWE NDANI YA BONDE LA BUGWEMA

Wananchi wa kijiji cha Bugwema na vijiji jirani vya Kata ya Bugwema na Kata za jirani wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Mhe Dkt Vincent Naahano katika mkutano uliohusu MRADI wa UWEKEZAJI wa BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO Tanzania ndani ya Bonde la Bugwema.

Na Hamisa Gamba, Msaidizi wa Mbunge.
Alhamisi, tarehe 27.09.2018, saa 4 asubuhi, Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Mhe Dkt Vincent Naahano ALIFANYA MKUTANO  na WANANCHI wa Kijiji cha Bugwema, na kuongelea juu ya MRADI wa UWEKEZAJI wa  BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO Tanzania ndani ya Bonde la Bugwema.
Uwekezaji utakuwa wa KILIMO CHA UMWAGILIAJI kwenye SHAMBA LA BUGWEMA.
Mahudhurio kwenye Mkutano huo yalikuwa mazuri sana ambapo WANANCHI walitoka Kijiji cha Bugwema na VIJIJI JIRANI vya Kata ya Bugwema na Kata za jirani. Vilevile Watendaji wa Serikali Kata na Vijiji, na Viongozi wa Chama (CCM) walihudhuria Mkutano huu.
Imeelezwa kuwa moja ya shughuli kubwa zitakazoendeshwa na MRADI huu ni kwamba, Mwekezaji ambaye ni Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania ITAJENGA MIUNDOMBINU ya UMWAGILIAJI kwa ajili ya WANANCHI kufanya KILIMO cha UMWAGILIAJI ndani ya Bonde la Bugwema. Aidha Mwekezaji atatoa vifaa vya Kilimo kwa wananchi kwa MAKUBALIANO ya MKATABA baina ya pande zote mbili. Utaratibu wa kurejesha MIKOPO utahakikisha unawanufaisha WAKULIMA watakaokuwa ndani ya MRADI HUU.
Pembejeo zitakazotolewa na Benki ya Kilimo ni: ZANA za KISASA za Kilimo,  MBEGU, MBOLEA  na huduma nyiingine pale zitakapokuwa zinahitajika.
MAZAO MAKUU ya kuanzia yatakayolimwa kwa wingi ni MPUNGA, MAHINDI na VITUNGUU.
Kwa AWAMU YA KWANZA YA MRADI wanufaikaji watakuwa WANANCHI wa Bugwema na kadri MRADI utakapokuwa unaendelea, WANANCHI WENGINE (nje ya Bugwema) watakaribishwa kushiriki katika shughuli hizo za kilimo.  HATIMAE GHARAMA ZA MWEKEZAJI ZIKIRUDI MRADI UTAKABIDHIWA KWA WANANCHI chini ya usimamizi wa Halmashauri yao.
Kwa taarifa hiyo ya Mkuu wa Wilaya (DC),  wananchi wamekubali na kuupokea MRADI huo kwa furaha kubwa, huku wakithibitishiwa na Mhe DC kuendelea kuyatumia mashamba waliokuwa wamelima mwaka jana ndani ya BONDE HILO.
Eneo lingine katika BONDE (SHAMBA) hilo la Bugwema la  zaidi ya EKARI 800 WAMEPEWA WAKAZI wa Bugwema kwa ajili ya MALISHO ya mifugo yao, na KUJENGA Shule, Zahanati na Ofisi ya Serikali ya Kijiji na Taasisi nyingine za Serikali.
Bugwema mambo ni moto, wananchi wanafurahishwa na Uongozi mzuri unaofanywa na Viongozi wa Wilaya ya Musoma (Halmashauri, Jimbo, Kata na Vijiji) wa kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma stahiki na Maendeleo chanya.
Picha hapo chini zinaonyesha DC wa Wilaya ya Musoma akiwa na Wananchi na Viongozi mbalimbali waliokuwa kwenye Mkutano wa leo wa Kijijini Bugwema.

WAZIRI WA NISHATI AKAGUA UTEKELEZAJI WA MRADI WA REA III JIMBONI

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akikagua Utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini wa REA III ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini

Na Fedson Masawa, Msaidizi wa Mbunge

18 – 09 – 2018

WAZIRI wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amefanya ziara ya Ukaguzi wa Utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini wa REA III ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini ambapo pia ametumia fursa hiyo kuzungumza na wananchi wa Jimbo hilo kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo Umeme Vijijini.

Akizungumza katika Mkutano wa hadhara leo Agosti 18, 2019 Kijijini Nyakatende, Dkt. Kalemani amewahakikishia wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini kwamba TAASISI, maeneo mbalimbali ya UWEKEZAJI na VITONGOJI vyote 374 vya Jimbo VITAPATA UMEME.

Awali akieleza kuhusu kero ya Umeme Musoma Vijijini, Waziri Kalemani amesisitiza kuwa Prof Muhongo aliomba Umeme kwenye Vijiji vyake vyote 68 na amepewa Vijiji vyote katika Mradi wa REA III

Akisisitiza juu ya jambo hilo, Dkt. Kalemani amesema kuwa kazi ya Mkandarasa ni kuhakikisha anapeleka umeme Vijiji vyote 68 vyenye VITONGOJI 374 katika awamu hii ya REA III

“Hakuna kijiji, hakuna kitongoji na hakuna mwananchi atakayerukwa katika Mradi huu” Amesisitiza Mhe Dkt. Kalemani

Aidha Waziri Dkt Kalemani ametoa maelekezo ya Uboreshaji wa Utekelezaji wa Mradi wa REA III mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Madiwani na WANANCHI wa Musoma Vijijini.

Dkt. Kalemani amewaagiza watendaji wake kufanya kazi bila kuondoka saiti hadi watakapokamilisha kazi hiyo.

“Mkandarasi nataka usihamishe genge, peleka genge kila kijiji. Badala ya kuhamishahamisha,” alisema Waziri wa Nishati Mhe Dkt Kalemani.

Vilevile, Dkt. Kalemani ameshiriki Tukio la Kuwasha Umeme Kijijini Nyakatende kuashiria Uzinduzi rasmi wa Mradi wa REA III Musoma Vijijini.

Katika Ziara yake hiyo, Dkt Kalemani aliongozana viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Taasisi zake ambao ni pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu TANESCO, Kaimu Mtendaji Mkuu wa REA, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Mara, Engineer wa TANESCO Kanda ya Ziwa (Mwanza), Engineer wa Miradi ya REA Kutoka Makao Makuu, na Mkandarasi wa Mradi wa REA III Mkoa wa Mara.

Dkt. Kalemani amehitimisha ziara yake Jimboni kwa kutoa pongezi nyingi kwa Mbunge wa Jimbo, Prof Muhongo kwa Jitihada kubwa za Maendeleo anazozifanya. akishirikiana na Mkuu wa Wilaya, Dr. Vicent Naano na Viongozi wengine. Mhe Waziri amewataka Madiwani na Mkurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha Jimbo la Musoma Vijijini linapiga hatua kubwa za kimaendeleo.

KILA KIJIJI KINACHANGIWA KILO 100 ZA MBEGU YA MTAMA.

KILA KIJIJI KINACHANGIWA KILO 100 ZA MBEGU YA MTAMA. MBEGU ZA ALIZETI AMBAZO ZIKO KWENYE OFISI ZA KATA ZOTE 21 NAZO ZINAGAWAWIWA KWA WAKULIMA
Picha 5 hapo chini zinaonyesha upokeaji wa Mbegu za Mtama kwenye Kata 5 zilizogawiwa  siku ya Alhamisi  (30.08.2018).
Picha Na 1 Kata ya BUGOJI, Na 2 BUGWEMA,Na 3 MUSANJA,Na 4 MURANGI,Na 5 RUSOLI.

KIJIJI CHA BUTATA CHAEZEKA CHUMBA KINGINE CHA DARASA KWA KUTUMIA  MCHANGO WA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO

KAZI za Uezekaji wa Chumba cha DARASA la Shule ya Msingi Butata

Na Verediana Mgoma, Msaidizi wa Mbunge
Uongozi wa Shule ya Msingi Butata kwa kushirikiana na WANANCHI na Serikali ya Kijiji cha Butata wamefanikisha zoezi la uezekaji wa Chumba kingine cha DARASA baada ya kupokea Mchango wa Mabati 54 kutoka kwenye Fedha za Mfuko wa Jimbo ili kuendeleza jitihada za kupunguza tatizo la uhaba wa madarasa na MSONGAMANO wa WANAFUNZI madarasani.
Awali, akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Butata, Ndugu Cleophance Kasara alieleza kuwa
“Serikali ya Kijiji chetu kwa kushirikiana na WANANCHI inaendelea na zoezi la Ujenzi wa VYUMBA VYA MADARASA ili kupunguza tatizo hilo Shuleni hapo.”
Aidha, Mwenyekiti huyo ameongezea kuwa ataendelea KUHAMASISHA Wananchi wake kujitolea ili kufanikisha shughuli za MAENDELEO KIJIJINI humo.
Naye Kaimu Mtendaji wa Kijiji cha Butata, Ndugu Mushangi Salige amefafanua kuwa, MWAMKO wa WANANCHI wa Kijiji hicho katika Ujenzi wa Vyumba Viwili (2)  vya MADARASA umekuwa msaada mkubwa kwa WANAFUNZI ambao awali walikuwa wakisomea nje. Jua kali na mvua vilikuwa kero kubwa.
Diwani wa Kata ya Bukima, Mhe January Simula ameshukuru na kuiomba SERIKALI YETU iendelee kuwaunga mkono ili kufanikisha suala la MAENDELEO.
Mhe Diwani Simula ametoa shukrani zake kwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof Muhongo kwa msaada wa SARUJI MIFUKO 60 iliyojenga Vyumba Viwili (2) vya Madarasa na Mabati 108 (54 kutoka Mfuko wa Jimbo na 54 kutoka kwa Mbunge) ambayo yote yametumika kuezeka Vyumba hivyo vya Madarasa.
Sambamba na Michango hiyo, Shule ya Msingi Butata A na B zimeshapokea Jumla ya Madawati 86 kutoka kwa Mbunge Prof Muhongo, mchango uliomaliza kabisa uhaba wa Madawati Shuleni hapo kulingana na mahitaji ya wakati huo.

KASI YA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU JIMBONI YAONGEZEKA

Wananchi wakishiriki katika kazi ya kujaza kifusi kwenye Msingi wa SHULE MPYA ya MSINGI YA BUANGA

Na Verediana Mgoma, Msaidizi wa Mbunge
WANANCHI WA KIJIJI  CHA BUANGA WAANZA UJENZI WA SHULE MPYA
Wananchi wa Kijiji cha Buanga, Kata ya Rusoli WAMEAMUA KUJITOLEA kujenga Vyumba Vinne (4) vya MADARASA katika Shule  Mpya ya Msingi inayojengwa katika Kitongoji cha Chilugwe ili kuwapunguzia UMBALI WATOTO WANAOTEMBEA WA takribani Km 5 kwenda masomoni kwenye Shule ya Msingi Bwenda.
Ujenzi wa Shule Mpya katika Kijiji cha Buanga, ni hatua muhimu katika  KUINUA KIWANGO cha UBORA WA ELIMU itolewayo kwenye Kata ya Rusoli. WANAFUNZI  ambao wengi wao wamelazimika kukatisha masomo yao na wengine kuwa watoro sugu shuleni, SASA WAMEKUWA NA MATUMAINI MAPYA KIELIMU.
Awali wakizungumza na Mwandishi wa Habari hizi Kijijini Buanga, WANANCHI  hao wameeleza kwa namna ambavyo wamewiwa kwa kutoa maeneo yao, kuuza mifugo yao kwa ajili ya ujenzi wa SHULE hiyo MPYA ili kuokoa na kuinua taaluma kwa WATOTO WAO hasa wenye umri wa kuanza SHULE, likiwemo DARASA la AWALI.
Akitoa taarifa ya ujenzi huo, Mtendaji wa Kijiji cha Buanga,  Ndugu Tumaini Rugembe, ameeleza kwamba, “umbali umekuwa kisababishi cha watoto wao kupotea, na kutofika shuleni kwa muda muafaka.”  Aliongezea kuwa hadi kufikia January 2019, wanatarajia SHULE hiyo iwe IMEFUNGULIWA.”
Diwani wa Kata ya Rusoli, Mhe Boazi M. Nyeura kwa niaba ya wananchi wake amesema kuwa, ANAUTAMBUA MCHANGO mkubwa wa SERIKALI na VIONGOZI mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mbunge Prof Sospeter Muhongo kwa mchango wake wa MADAWATI 162 katika Shule ya Msingi Bwenda A na B, SARUJI MIFUKO 120 na MABATI 50.
MFUKO WA JIMBO ulichangia MABATI 54 na Halmashauri ilichangia Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya ukamilishaji wa Vyumba Vinne (4) vya Madarasa katika Shule ya Bwenda A na B, Kijijini Buanga.
Aidha Diwani alimpongeza Mkuu wa Wilaya(DC) Dr. Vincent Naano Anney  kwa UHAMASISHAJI wake kwa WANANCHI ili kuwezesha ujenzi wa Vyumba vya MADARASA na MAABARA ndani ya Kata ya Rusoli.
Mhe Diwani  Boazi Nyeura AMEENDELEA KUWAOMBA WADAU WA MAENDELEO WAJITOKEZE kushirikiana na Wananchi wa Kata ya Rusoli KUBORESHA MIUNDOMBINU ya ELIMU na AFYA NDANI YA KATA HIYO.

KILIMO CHA MAZAO MAPYA YA ALIZETI NA UFUTA CHAFUFUA MATUMAINI YA UCHUMI IMARA JIMBONI

Kilimo cha ALIZETI na UFUTA ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini kimefufua matumaini ya kuinua uchumi wa wananchi, shule kadhaa   na vikundi vya maendeleo.
Kwa misimu mitatu mfululizo, mbegu za ALIZETI zimegawiwa bure na Mbunge wa Jimbo wakati mbegu za UFUTA ziligawiwa bure na Halmashauri ya Musoma.
Mkuu wa Wilaya na Afisa Kilimo wa Halmashauri, wamesimamia ugawaji wa mbegu zote na utoaji elimu kuhusu kilimo cha ALIZETI na UFUTA ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.
Awali, akizungumza na Msaidizi wa Mbunge, Mwalimu wa Somo la Kilimo katika Shule ya Msingi Mkirira A, Neema Manyama amesema, “ALIZETI ni zao pekee ambalo tangu lilimwe kijijini hapo limekuwa likistawi na kutoa uhakika wa mavuno mazuri. Hivyo ni vyema jamii zikachangamkia zao hili, ikiwezekana lilimwe na kila kaya kwa ajili ya uhakika wa kipato kizuri.”
 Mwalimu Manyama ameongezea kuwa, Kilimo cha ALIZETI na UFUTA ndio mradi mkuu na wa uhakika shuleni hapo ambapo zaidi ya ekari 2 kwa kila zao zimelimwa na wana matarajio ya kuvuna kwa wingi zaidi huku akizidi kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof Muhongo kwa kuwathamini na kuwajali wananchi wa Jimbo lake kwa kubuni kilimo bora na chenye manufaa.
Kwa upande wa Shule ya Msingi Busekera, ambayo  ni msimu wa kwanza kwao kulima ALIZETI wamesema, ALIZETI ni zao pekee lililostawi bila tatizo lo lote na tayari limefikia hatua nzuri. Hayo yalielezwa na  Mwalimu Paschal Abel wa shule hiyo.
Ndugu Godilisten Kenny wa Kijiji cha Saragana, amekiri kwamba kilimo cha ALIZETI kitaongeza kipato cha wakulima ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.
Mazao ya biashara ya Jimbo la Musoma ni: (i) pamba, (ii) alizeti,  na (iii) ufuta. Mihogo na mahindi yatalimwa kwa wingi kwa ajili ya chakula na biashara.

ZAHANATI YA KISIWA CHA RUKUBA YAPATA DARUBINI

Wakazi wa Kisiwa cha Rukuba wanalazimika kusafiri kwa boti na mitumbwi kutoka Kisiwani hadi Musoma Mjini kwenda kufanyiwa VIPIMO VYA MATIBABU kwa sababu Zahanati yao haina DARUBINI.

Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo AMEMWOMBA DAKTARI BINGWA, Dr Derick Davis Nyasebwa wa Uhuru Hospital ya Mwanza
ATOE MSAADA WA DARUBINI MOJA YA KISASA YA KUTUMIWA KUFANYA VIPIMO VYA MATIBABU. Daktari Bingwa huyo amekubali.

DARUBINI hiyo itapelekwa Kisiwani Rukuba hivi karibuni.

Vilevile Mbunge Prof Muhongo ataenda hapo Kisiwani KUZINDUA MAJENGO yaliyojengwa na MFADHILI MKUU (MFARANSA) WA MAENDELEO wa Kisiwa cha Rukuba.

KARIBUNI TUJENGE UCHUMI WA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

DR DERRICK NYASEBWA HONGERA KWA KUTEKELEZA AHADI ZAKO KWA VITENDO.

WANANCHI WA KATA YA RUSOLI WAHAMASIKA NA UJENZI WA MAABARA KWENYE SEKONDARI YA KIJIJINI MWAO

UPAUAJI wa  JENGO la MAABARA unaendelea kwenye Shule ya Sekondari Rusoli. Aliyevaa kofia kwenye picha ni Mhe Diwani Boaz Nyeula alipotembelea Maabara ya Sekondari ya Rusoli.

Na. Verediana Mgoma, Msaidizi wa Mbunge
Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wameendelea kuhamasika katika Ujenzi wa Maabara kwenye Shule za Sekondari za Kata zao.
Wakazi wa Kijiji cha Rusoli wameendelea KUJITOLEA kuweka NGUVU ZAO kwenye Sekondari ya Rusoli ili kukamilisha JENGO la MAABARA litakalotumika kujifunza MASOMO YA SAYANSI kwa VITENDO.
Sekondari hiyo imepata msaada wa VIFAA vya MAABARA kutoka kwa Ndugu Japhet Makongo mzaliwa wa Kijijini hapo na MDAU MKUBWA wa ustawi na maendeleo ya Sekondari ya Kijijini kwao Rusoli.
WANAFUNZI wa Sekondari ya Rusoli wamekuwa wakipata shida katika MASOMO YA SAYANSI ya VITENDO kwa kukosa vifaa vya maabara kwa muda mrefu hivyo kupatikana kwake kutaondoa adha waliyokuwa wakiipata Wanafunzi hao.
Bi.Tausi Juma ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Rusoli alisema licha ya kupatikana kwa vifaa hivyo tatizo kubwa linalowakabili ni KUTOKUWEPO JENGO LA MAABARA na kupelekea VIFAA VYA MAABARA VILIVYOPATIKANA kuhifadhiwa DARASANI.
Wanafunzi na Walimu wamefurahia sana kuona UJENZI WA MAABARA umeanza shuleni hapo.
HALMASHAURI YA WILAYA YA MUSOMA IMETOA Tshs MILIONI 25 kwa ajili ya UEZEKAJI WA JENGO HILO na ukamilishaji wa chumba kimoja huku Shule ikiwa na changamoto ya ukamilishaji wa Vyumba vingine viwili vya Maabara vinavyohitaji Saruji Mifuko 400, madirisha na milango.
Wanakijiji, Wanafunzi na Walimu wa Sekondari WANAOMBA WAFADHILI wajitokeze kukamilisha ujenzi huu muhimu sana kwa MASOMO YA SAYANSI shuleni hapo.
Kwa upande wake, Mwalimu anayesimamia Maabara katika Shule hiyo, Mwalimu Joseph Kasili alisema uwepo wa Vifaa hivyo vya Maabara umetoa hamasa kubwa kwa WANAFUNZI  kupenda Masomo ya Sayansi.
Sekondari ya Rusoli inashukuru kupokea mara mbili VITABU VYA MASOMO YA SAYANSI kutoka kwa Mbunge Prof Sospeter Muhongo aliyeletewa vitabu hivyo kutoka USA na UK.
Diwani wa Kata hiyo Mhe Boaz Nyeula  amewashukuru ndugu, jamaa na marafiki wanaoendelea KUJITOLEA kwenye suala zima la maendeleo kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo kuipa ELIMU kipaumbele na kuwaomba Wadau wengine mbalimbali kuwaunga mkono ili kukamilisha UJENZI wa MAABARA hapo shuleni.
Aidha, Diwani huyo ameishukuru Ofisi ya Mbunge kwa msaada wa Saruji Mifuko 70  iliyotolewa hapo Shuleni  na kutumika kukarabati Vyumba vya Madarasa huku lengo likiwa ni kujenga Mazingira bora ya Elimu.

UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI BUSAMBARA WAENDELEA KWA KASI KUBWA 

WANANCHI WA KATA YA BUSAMBARA (Vijiji vya Maneke, Kwikuba na Mwiringo) Wakijitolea kusomba mchanga, mawe, kokoto, kufyatua tofali, kusomba maji ili kumsaidia Fundi ujenzi.

Na Hamisa Gamba Msaidizi wa Mbunge
Hivi karibuni WANANCHI wa Kata ya Busambara, Jimboni Musoma Vijijini WAMEAMUA KWA KAULI MOJA KUONGEZA KASI YA Ujenzi wa Vyumba Vipya vya Madarasa ya Shule Mpya ya Sekondari Busambara baada ya kuwa umesimama kwa muda.
Hatua hii ilifikiwa baada ya Mbunge wa Jimbo hilo, Prof Sospeter Muhongo kuwatembelea wananchi wa Kata hiyo ya  Busambara na KUWAHAMASISHA kuendelea na Ujenzi na Kuukamilisha ifikapo Disemba 2018 kama ILIVYOKUSUDIWA.
Tarehe 14/7/2018, Mbunge wa Jimbo, Prof Muhongo aliwakabidhi Wananchi wa Kijiji cha Kwikuba Saruji Mifuko 50 baada ya Kijiji hicho KUONYESHA ARI KUBWA YA KUKAMILISHA kwa wakati Vyumba vya Madarasa ilivyopangiwa. Saruji ilinunuliwa Kijijini Kwikuba.
Wakiendelea kufanya jitihada za Ujenzi wa Madarasa, tarehe 23/7/2018 Msaidizi wa Mbunge aliwatembelea Wananchi hao wa kutoka Vijiji 3 wakiwa katika majukumu yao kadri walivyojipangia na kukuta yafuatayo:
(1) Kijiji cha Kwikuba:
– Wananchi walikuwa katika hatua za ukamilishaji wa Msingi wa Vyumba viwili vya Madarasa.
(2) Kijiji cha Maneke:
– Wananchi walikuwa katika ufyatuaji wa matofali.
(3) Kijiji cha Mwiringo:
– Wananchi walikuwa wakisomba mchanga wa kufyatua matofali. Kazi ilipangwa kuanza Jumatano, tarehe 25/7/2018.
Kutokana na MAKUBALIANO YA MBUNGE na WANANCHI wa Vijiji vya Maneke na Mwiringo kuendelea na ujenzi kuanzia tarehe 25.07.2018, Mbunge wa Jimbo Prof Muhongo ALITIMIZA AHADI YAKE ya KUCHANGIA Saruji Mifuko 50 kwa kila Kijiji, na saruji imenunuliwa Kijijini  Kwikuba.
WANANCHI WA KATA YA BUSAMBARA (Vijiji vya Maneke, Kwikuba na Mwiringo) WAMEKUBALI KUJITOLEA KUSOMBA mchanga, mawe, kokoto, kufyatua tofali, kusomba maji na kumsaidia Fundi ujenzi. WANAOMBA MCHANGO WAKO WAKAMILISHE UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI BUSAMBARA.
Mchango wako uwakilishwe kwa Serikali ya Kijiji cha Maneke, Kwikuba na Mwiringo. Ikishindikana Wasiliana na Msaidizi wa Mbunge wa eneo hilo:
Simu:
   0762 626 881

SHEREHE ZA UZINDUZI WA SHULE YA MSINGI NYEGINA B, KIJIJI CHA NYEGINA

Tarehe 15.07.2018, Mbunge Prof Sospeter Muhongo (Mgeni Rasmi) na Viongozi wa Vyama vya Siasa (CCM, CHADEMA, ACT) na Serikali walishiriki Sherehe za Uzinduzi wa S/M Nyegina B.

Jumapili, 15.07.2018,  Sherehe za Kuzindua S/M Nyegina B zilifana sana.
Kijiji cha Nyegina, Kata ya Nyegina, Musoma Vijijini,  kinayo historia nzuri ya  ELIMU na MAENDELEO.
Shule ya Msingi Nyegina ya Kanisa la Katoliki ilijengwa Mwaka 1928 na Darasa la Kwanza lilianzishwa Mwaka 1930. Kanisa la Katoliki lilijengwa Kijijini hapo Mwaka 1911.
Kijiji cha Nyegina kimekuwa KITOVU CHA ELIMU kwani kuna Shule ya Msingi, Sekondari na High School. Kuna Maktaba ya kisasa na Kituo cha TEHAMA kinaendelea kupanuliwa hapo Kijijini. Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo amegawia MAKTABA hiyo VITABU alivyopewa kutoka Marekani na Uingereza. Baba Paroko Kazeri ni Kiongozi Mahiri wa masuala ya Elimu, Afya, Kilimo, Mazingira, TEHAMA  na Maendeleo ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.
Jumapili, 15.07.2018, Mbunge Prof Sospeter Muhongo (Mgeni Rasmi) na Viongozi wa Vyama vya Siasa (CCM, CHADEMA, ACT) na Serikali walishiriki Sherehe za Uzinduzi wa S/M Nyegina B.
CCM iliwakilishwa na M/Kiti Wilaya (Ndg Nyabukika), Katibu Wilaya (Ndg Koyo) na Kaimu K/Wilaya Wazazi (Ndg Lucia John). M/Kiti wa Halmashauri (Ndg Magoma),  Diwani wa Kata hiyo, Ndugu Majira, na Wafanyakazi wa Halmashauri waliungana na Wananchi wa Kijiji cha Nyegina, na Waalikwa mbalimbali kwenye UZINDUZI huo.
HARAMBEE ilipigwa ya KUCHANGIA UJENZI wa Vyumba vingine vya Madarasa vya Shule hiyo. Saruji Mifuko 215 na Fedha Tshs 495,000 vilichangwa kwenye HARAMBEE hiyo. Mbunge Prof Muhongo alichangia, kwa awamu hiyo ya ujenzi, Saruji Mifuko 50 iliyonunuliwa Kijiji cha jirani cha Etaro.
Shirika la EQUIP la Uingereza na Kanisa la Angalikani la Marekani nao WANACHANGIA ujenzi wa Shule ya Msingi Nyegina B.
Picha hapo chini zinaonyesha KILELE CHA SHEREHE ZA UFUNGUZI wa Shule ya Msingi Nyegina B.
UJENZI UNAENDELEA TUNAOMBA SANA MCHANGO WAKO. WANAVIJIJI WAMEAMUA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUCHANGIA MAENDELEA YAO TUWAUNGE MKONO.

UJENZI NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU JIMBONI

 

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini akishirikiana na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Musoma Vijijini, Ndugu Nyabukika KUHAMASISHA ujenzi wa Vyumba vya Madarasa vya Shule za Msingi na Sekondari Jimboni mwao

Jumamosi, 14.07.2018, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini alishirikiana na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Musoma Vijijini, Ndugu Nyabukika KUHAMASISHA ujenzi wa Vyumba vya Madarasa vya Shule za Msingi na Sekondari Jimboni mwao. Katibu wa CCM Wilaya Ndg Koyo na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Ndg Mwalimu Kerenge walishiriki kwenye ziara hiyo ya UHAMASISHAJI wa uboreshaji wa miundombinu ya Elimu kwenye Jimbo la Musoma Vijijini.

(1) SHULE MPYA YA MSINGI YA MWIKOKO, Kijiji cha Chitare, Kata ya Makojo: Picha Namba 1-4 hapo chini zinaonyesha Mkutano wa Wanakijiji wa Chitare wakishiriki HARAMBEE ya kuchangia ujenzi wa Vyumba Vipya vya Madarasa ya Shule hiyo ya Msingi. Kwa awamu hii ya ujenzi, Mbunge Prof Muhongo amechangia Saruji Mifuko 5O iliyonunuliwa Kijiji jirani cha Bukima.

(2) SEKONDARI YA KATA YA USAMBARA: Kata hii yenye Vijiji 3 (Maneke, Kwikuba na Mwiringo) haina Sekondari.

Wananchi wa Kata ya Busambara WAMEAMUA KWAMBA IFIKAPO JANUARI 2019 Sekondari hiyo iwe IMEKAMILIKA na kuanza kutoa elimu.

Wananchi wamepiga HARAMBEE kwa kutoa fedha taslimu na vifaa vya ujenzi. Mbunge Prof Muhongo, amechangia Saruji Mifuko 50 iliyonunuliwa Kijijini hapo. Michango mingine atatoa baada ya KURIDHIKA na KASI ya ushiriki wa Vijiji vya Maneke na Mwiringo kwenye ujenzi wa Sekondari hii. Ushiriki wa Vijiji hivi viwili kwa sasa ni hafifu.

Picha Namba 5-8 zinaonyesha Mkutano wa Wananchi wa Kata ya Busambara wakishiriki kwenye HARAMBEE ya ujenzi wa Sekondari ya Kata yao.

Wananchi wa Vijiji vya CHITARE (Kata ya Makojo), na KWIKUBA, MWIRINGO na MANEKE (Kata ya Busambara) wanaomba MCHANGO WAKO UWASAIDIE ujenzi wa shule zao ambazo WAMEAMUA KUZIJENGA KWA KUJITOLEA na kwa kushirikiana na Serikali.

KILIMO CHA MVUA ZA VULI

JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI – TUJITAYARISHE KWA KILIMO CHA MVUA ZA VULI

Wataalamu wetu wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma WANATUSHAURI hivi:

KILIMO cha MTAMA, MIHOGO na MAHINDI cha Msimu wa Vuli huanza mwishoni mwa Mwezi SEPTEMBA, na kuendelea hadi OKTOBA na NOVEMBA.

MBEGU ZINAZOHITAJIKA

Kiasi cha MBEGU kinachohitajika
(1) Mahindi: Kilo 82,500 kwa Ekari 20,625
(2) Mtama: Kilo 21,000 kwa Ekari 7,000
(3) Mihogo: Pingili 78,000,000 kwa Ekari 19,500

BEI ZA MBEGU (ASA MOROGORO)

(1) Mtama: Tshs 2,300 kwa kilo moja
(2) Mahindi: Tshs 2, 300 kwa kilo moja
(3) Vijiti Vya Mihogo: Tshs 200,000 vinavyotosha ekari moja

Ndugu zangu MADIWANI, HALMASHAURI, MKUU WA WILAYA, MBUNGE wa JIMBO, na WADAU wa MAENDELEO YA MUSOMA VIJIJINI tunaombwa tujitayarishe KUZIPATA MBEGU HIZI KWA WAKULIMA JIMBONI KWENYE MWEZI AGOSTI 2018 (mbegu kuanza kugawiwa Jimboni katikati mwa Agosti 2018).

Nashauri tufanye Kikao tarehe 10 Julai 2018 Ofisini kwa DC wa Musoma kujadili na kuweka bayana namna ya kuzipata mbegu hizo.

Je Wanavijiji wauziwe mbegu au Wanavijiji wapewe mkopo wa mbegu hizo au Wanavijiji wasaidiwe kwa kugawiwa mbegu hizo bure kutokana na uchumi wao kuwa hafifu.

WANANCHI WAMEKUA NA MWITIKIO MKUBWA WA KUJITUMA NA KUJITOLEA KUHARAKISHA UPATIKANAJI WA MAENDELEO YAO

Mbunge wa Musoma Vijijini, akifuatana wa Viongozi wa Wilaya wa CCM (Katibu wa CCM, Katibu wa WAZAZI na Katibu wa UVCCM) kukagua MIRADI YA UJENZI inayotekelezwa Jimboni humo.

Jumatano, 13.06.2018, Mbunge wa Musoma Vijijini, akifuatana wa Viongozi wa Wilaya wa CCM (Katibu wa CCM, Katibu wa WAZAZI na Katibu wa UVCCM) wamekagua MIRADI YA UJENZI inayotekelezwa Jimboni humo kwa wakati huu.

Kijiji cha Bukima kimeamua KUPANUA ZAHANATI YAKE kwa kuongeza Jengo lenye WADI 3 (Wadi ya Wazazi, Watoto & Akina Mama, na Wadi ya Wanaume). Picha za kwanza 3 zinaonyesha eneo la ujenzi huo. Mbunge wa Musoma Vijijini amechangia Saruji Mifuko 100 na wananchi wanaendelea kuchangia saruji, kusomba mawe, mchanga, n.k.

Kijiji cha Saragana wameamua kujenga KITUO CHA POLISI kitakachohudumia Kata zaidi ya 2. Wananchi wamejitolea kusomba mchanga na maji ya kufyatua tofali zaidi ya 4,000. Polisi Wilaya (OCD) imechangia Saruji Mifuko 60 na leo Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter amechangia Saruji Mifuko 100. Picha namba 4 na 5 hapo chini zinaonyesha tukio hilo Kijijini Saragana.

Kijiji cha Nyambono kimekubali KUSHIRIKIANA na Wazaliwa wa Kijiji hicho (Wafadhili) kujenga KITUO CHA AFYA. Wiki hii wanamaliza ujenzi wa msingi wa Jengo la Matibabu. Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo amechangia Saruji Mifuko 100. Picha 2 za mwisho zinaonyesha msingi unaojengwa.

Wananchi wa Vijiji vyote 68 vya Jimbo la Musoma Vijijini wamekuwa na hamasa ya KUJITOLEA kuharakisha Ujenzi na Uboreshaji wa Miundombinu ya Elimu na Afya vijijini mwao kwa kushirikiana na Serikali.

UJENZI WA ZAHANATI VIJIJINI KWA NJIA YA KUJITOLEA WAPAMBA MOTO

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof Sospeter Muhongo akikagua ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Kigera Etuma

Na Fedson Masawa, Msaidizi wa Mbunge

Ujenzi wa zahanati umezidi kupamba moto katika vijiji mbalimbali vya vya Jimbo la Musoma Vijijini ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (2015-2020).

Hatua hiyo imefikiwa ikiwa ni matokeo ya hamasa kubwa kutoka kwa wananchi wa Musoma Vijijini walioamua kuungana na serikali, viongozi wao na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kusogeza huduma ya afya kwa kila kijiji Jimboni humo.

Awali akiungana na wananchi, viongozi na wadau mbalimbali wa maendeleo Jimboni mwake  Mei 1, 2018, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof Sospeter Muhongo alishirikiana na Madiwani na wakazi wa kijiji cha Kurwaki na kijiji cha Kigera Etuma na kufanikiwa kuchangia zaidi ya mifuko 350 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Kurwaki kata ya Mugango na mifuko 150, nondo na misumali katika zahanati ya Kigera Etuma kata ya Nyakatende.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa zahanati ya Kigera Etuma, mtendaji wa kijiji hicho ndugu Antony Ndege alisema, wachangiaji wa ujenzi wa Kijiji cha Kigera Etuma ni Wafadhili,Halmshauripamoja na wakazi wa kijiji hicho na tayari jengo la matibabu (OPD) limekamilika kwa asilimia 80 na nyumba ya Mganga na Muuguzi (two in one)  inajengwa kwa kasi kubwa.

Mtendaji ameongezea kuwa “malengo ya wananchi na serikali ya kijiji cha Kigera Etuma  ni kukamilisha ujenzi huo mapema ifikapo Desemba 2018  zahanati hiyo iwe imeanza kazi”

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Musoma na Diwani wa kata ya Mugango Mhe Charles Magoma kwa niaba ya wananchi amemshukuru Mbunge na wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini kwa kuungana kufanimisha miundombinu ya Elimj, Afya na Kilimo Jimboni.

MABARAZA YA WAZEE WA USHAURI, USHAWISHI NA MAADILI

Na Fedson Masawa, Msaidizi wa Mbunge

PROF. MUHONGO AZINDUA MABARAZA YA WAZEE WA USHAURI, USHAWISHI NA MAADILI

Wazee wa mabaraza ya kata 21 za jimbo la Musoma vijijini wakiwa kwenye kikao cha uzinduzi wa mabaraza yao uliotekelezwa na Mbunge wa Jimbo holi Prof. Muhongo (hayupo katika picha)

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof Sospeter Muhongo leo April 30 amefanya uzinduzi wa mabaraza ya wazee wa ushauri na maadili ngazi ya kata kwa kata zote 21 za Jimbo hilo.

Akizungumza na wazee wakati wa uzinduzi wa mabaraza hayo kijijini Chumwi, Prof Muhongo amewaeleza wazee hao kuwa majukumu yao makubwa ni kutoa ushauri na kuhamasisha shughuli za maendeeo bila kuingilia miimili ya serikali za vijiji, kata n.k ili kuharakisha mafanikio chanya Jimboni.

Kwa upande wao wazee kutoka kata 21 za Jimbo la Musom vijijini wameungana pamoja kuhakikisha wanasimamia majukumu yao ya ushawishi, ushauri na uhamasishi katika mendeleo na uchumi hasa Elimu, Afya na Kilimo vikiwa ni vipaumbele vya Jimbohilo.

“Tutahakikisha Elimu, Afya na Kilimo ndio itakuwa nguzo ya kuinua uchumi na maendeleo ya Jimbo letu” alisema mzee Chriphod Nyaturo kwa niaba ya wazee wa hao.

Hii ni mara ya pili Prof Muhongo akizindua mabaraza ya wazee ambapo kwa mara ya kwanza alizindua mabaraza ya wazee ngazi ya vijiji  mwishoni mwa mwezi Machi 2018, lengo likiwa ni kuimarisha nguvu ya ushawishi na uhamasishaji wa shughuli za maendeleo na uchumi Jimboni.

Kwa upande mwingine,  Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini amefanya Kikao na Wenyeviti wa CCM wa Kata za Jimbo lake wakijadili juu ya usimamiaji wao wa utekelezaji wa Miradi ya Uchumi na Maendeleo (Ilani ya CCM ya Uchaguzi)  kwenye Kata zao.

WANAWAKE WATAKIWA KUUNDA VIKUNDI VYA MAENDELEO

Na Hamisa Gamba

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi CCM (UWT) Mkoani Mara, Wegesa Hassan amewataka wanawake mkoani humo kuunda vikundi ili kufanya miradi mbalimbali itakayowaletea maendeleo.

Wegesa alitoa wito huo kwenye kikao cha Jumuiya hiyo kilichofanyika Murangi, kwa lengo la kuhamasisha mshikamano na suala la maendeleo, ambapo aliwataka wanawake kuachana na makundi yasiyo na tija ndani ya Jumuiya yao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Musoma vijijini Abia Masaule kwa niaba ya wajumbe wake, ametoa shukrani kwa Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo kwa umoja alioonesha na kuungana na wanawake hao katika kuwezesha kikao hicho kilichofanyika Machi 21, 2018.

MBUNGE MUSOMA VIJIJINI AWATEMBELEA WAHANGA WA KIMBUNGA

Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo (katikati aliyevaa fulana ya bluu) akiwa katika shule ya msingi Bukumi ambapo vyumba vitatu vya madarasa paa zake zimeezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua. Kulia kwake ni Diwani wa viti maalum kata ya Mgango Kadogo Kapi wakiwa na Diwani wa Kata ya Bukumi John Manyama.

Na Verdiana Mgoma

MBUNGE wa Jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo amezitembelea kaya zilizopatwa na matatizo ya nyumba zao kuezuliwa na upepo na nyingine kubomoka kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali Jimboni humo.

Kwenye ziara yake aliyoianza Machi 15, 2018, Prof. Muhongo ameshuhudia kaya 86 zikiwa zimekumbwa na matatizo hayo na kusababisha baadhi ya familia kukosa makazi.

Mbali na kutembelea kaya hizo na kutoa pole, mbunge huyo alitembelea shule ya msingi Bukumi iliyopo kijiji cha Bukumi ambapo ameshuhudia vyumba vitatu vya madarasa paa zake zikiwa zimeezuliwa na upepo na mashamba ya pamba yenye takribani hekari 200 yaliyoharibiwa vibaya na mvua ya mawe katika kijiji cha Bugwema.

Akizungumza na wananchi waliokumbwa na matatizo hayo, Prof. Muhongo amewataka kuwa watulivu wakati viongozi wakiendelea kufanya tathimini ya uharibifu uliotokea na kuwasihi wasitegemee msaada kutoka serikalini peke yake kwani suala hilo ni la jamii nzima kwa kushirikiana na serikali.

“Kuweni wavumilivu, viongozi na wasaidizi wangu watapita na kuchukua tathimini ya madhara yaliyotokea. Pia tambueni, serikali peke yake haiwezi kutoa msaada kwa kila mtu. Kilichopo ni ninyi wananchi na sisi kujipanga tuone tutalitatuaje hili” alisema Prof Muhongo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi wa maeneo yaliyopata tatizo hilo mbali na kusikitishwa na matukio hayo yanayojirudia kila mara, walimpongeza mbunge wao na uongozi wa Halmashauri ya Musoma kwa kuwatembelea na kuwapa pole.

“Tunamshukuru sana Prof. Muhongo na viongozi wenzake wa halmashauri kwa kuguswa na kutufikia wananchi wao kwa wakati hasa tunapopatwa na matatizo ya aina hiyo” alisema Furaha Sumuni.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Musoma Charles Magoma alisema, ili kupunguza matatizo ya mara kwa mara, wameshaagiza kila kaya kupanda miti 40, shule miti 500 na zahanati miti 100 kwa kila mwaka huku akikazia kuwa zoezi hilo ni la lazima.

PROF. MUHONGO ASAIDIA MATIBABU YA FAMILIA ILIYONG’ATWA NA MBWA

Na Hamisa Gamba

MBUNGE wa Jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo amesaidia matibabu ya chanjo kwa kumi wa familia moja waliopatwa na tatizo la kung’atwa na mbwa katika kijiji cha Bugwema, kata ya Bugwema na kusababisha vifo vya watu wawili.

Wakati alipotembelea familia hiyo, mmoja wa ndugu Samwel Onunda, alimuomba mbunge kuwasaidia matibabu na chanjo ili kuokoa maisha ya wanafamilia hao kutokana na madhara waliyoyapata baada ya kushambuliwa na mbwa na kusababisha majeruhi na vifo vya watu wawili Charles Gilbetus na Martin Gilbetus..

Akijibu maombi hayo, Prof. Muhongo alisema atasaidia matibabu ya wahanga hao, huku akiiomba jamii kuchukua tahadhari na magonjwa mlipuko yanayosababishwa na wanyama hao.

Kwa upande wake diwani wa Kata ya Bugwema Ernest Maghembe na viongozi wengine wa eneo hilo wameahidi kushirikiana na Mbunge kuhakikisha familia hiyo inapata matibabu ya kuzuia maambukizi ya magonjwa yanayosababishwa na mbwa.

Naye Musa Oyugi alitoa shukrani kwa Mbunge wa Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo kwa jinsi alivyojitolea kunusuru uhai wa wananchi wake.

WANANCHI KIGERA ETUMA WAFIKIA HATUA NZURI UJENZI WA ZAHANATI

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Kigera Etuma wakishiriki ujenzi wa nyumba ya mganga wa zahanati ya kijiji chao.

Na Fedson Masawa

WANANCHI wa kijiji cha Kigera Etuma kilichopo kata ya Nyakatende kwa kushirikiana na viongozi wa Kata na serikali ya kijiji hicho wamefikia hatua nzuri ya ujenzi wa zahanati na kuonesha matumaini ya kupata huduma ya afya kijijini hapo.

Diwani wa Kata ya Nyakatende Rufumbo Rufumbo alisema haikuwa kazi rahisi kwa wananchi na serikali ya kijiji cha Kigera Etuma kufanikisha ujenzi wa zahanati hiyo, lakini kutokana na nia, ushirikiano na mipango yao thabiti, wamekamilisha jengo la zahanati na sasa wameelekeza nguvu zao katika ujenzi wa nyumba ya mganga ili zahanati hiyo ianze kutoa huduma mapema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kitongoji cha Mwiryanyo na Mjumbe wa serikali ya Kigera Etuma, Mnada Nyatago ameishukuru serikali na wafadhili mbalimbali wanaoendelea kuwaunga mkono ili kufanikisha ujenzi wa zahanati hiyo ambapo alisema wanatarajia ifikapo Machi, 26 mwaka huu nyumba ya mganga iwe imekamilika.

Kwa upande wake Albinusi Nyatago akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Kigera Etuma, alitoa shukrani zake kwa Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo katika kuunga mkono jitihada za ujenzi wa zahanati Jimboni.

Nyatago aliongeza kwa kutoa ombi kwa Mbunge kuwapa nguvu wananchi wa Kigera Etuma katika kukamilisha ujenzi wa nyumba ya mganga ili zahanati yao ianze kutoa huduma mapema kijijini hapo.

AFYA BORA MUSOMA VIJIJINI – DARUBINI (MICROSCOPES) 2 ZATOLEWA

Uhuru Hospital ya Mwanza imetoa DARUBINI MPYA 2 zitumiwe Jimboni. Dr Derick Davis Nyasebwa, Kiongozi wa Uhuru Hospital na mzaliwa wa Kijiji cha Rusoli, Musoma Vijijini amemtaarifu Mbunge wa Musoma Vijijini kwamba DARUBINI hizo zikachuliwe Mwanza siku ya Jumatatu, tarehe 19.3.2018. Wananchi Jimboni wanaendelea kujenga Zahanati (vijijini, jumla 68) na Vituo vya Afya (Kata, jumla 21). Wasomi, Wataalamu na Wafanya biashara wanaofanya kazi zao ndani na nje ya Jimbo wameamua kushirikiana na ndugu zao vijijini kwenye miradi ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya elimu na afya Jimboni. JITOKEZE, TUTOKOMEZE UMASKINI JIMBONI MWETU.

Ofisi ya Mbunge

MAADHIMISHO YA WIKI YA WAZAZI MKOA WA MARA – MITI 12,500 KUPANDWA

Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya sherehe za wiki ya Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) walipokutana na Afisa misitu na wasaidizi wa Mbunge katika vitalu vya miche kwa ajili ya ukaguzi wa miche hiyo kabla ya kusambazwa vijijini.

Na. Fedson Masawa

MAADHIMISHO ya sherehe za wiki ya Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) yatakayofanyika kimkoa katika wilaya mpya ya Musoma vijijini Mkoani Mara yameanza jana kwa kampeni maalumu ya upandaji miti katika ofisi za Taasisi mbalimbali na kwenye nyumba za watu binafsi.

Katika kufanikisha maadhimisho ya sherehe hizo ambazo zitafikia kilele chake Machi, 29, 2018, Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo ameungana na wazazi wa Mkoa wa Mara kwa kuchangia ununuzi wa miche 5,555 kati ya miche 12,500 iliyopendekezwa na Jumuiya hiyo.

Aidha, Halmashauri ya wilaya ya Musoma nayo imenunua miche 5,555 ikiwa ni hatua ya kuunga mkono jitihada za wazazi katika kupambana na majanga ya asili kama kimbunga na mengineyo huku miche 1,390 iliyobaki, itanunuliwa na Jumuiya hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kukamilisha idadi iliyokusudiwa.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Musoma Dkt. Vincent Naano Anney, amechangia huduma ya kusafirisha miche yote 12,500 kutoka Musoma mjini na kusambazwa kwenye Kata tisa zenye vijiji 28 kama ilivyopangwa.

Awali, akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Katibu wa Wazazi Mkoa wa Mara Robert Manjebe alisema, kata ambazo zimepewa kipaumbele kwenye zoezi hilo, ni zile zinazokumbwa na majanga ya kimbunga mara kwa mara na kusababisha maafa makubwa kwenye jamii.

Manjebe amezitaja kata hizo kuwa ni Nyegina, Ifulifu, Mugango, Kiriba, Bugwema, Musanja, Murangi, Bukima, Bukumi na vijiji viwili vya Bwasi na Chimati.

“Zoezi la upandaji miti pia ni kampeni ya kitaifa, hivyo kwa kata nyingine zitakazobakia, bado zitaletewa miche kwa ajili ya kuendelea kulinda mazingira yetu” aliongeza Manjebe.

Manjebe pia ametoa shukrani zake kwa Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo kwa kujitoa kwa hali na mali pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Halmashauri ya Musoma na wadau wengine katika kufanikisha maadhimisho ya sherehe za wiki ya Wazazi kimkoa.

Naye, Katibu wa wazazi wilaya ya Musoma vijijini Lucy John alisema, pamoja na zoezi la upandaji miti, maadhimisho ya sherehe za wiki ya wazazi pia zinalenga kuwatembelea na kuwapa pole wagonjwa na wazazi waliolazwa mahospitalini, watoto yatima na kuwatembelea watoto waishio katika mazingira magumu hasa katika taasisi za shule, dini na nyinginezo.

Wakipokea miche hiyo, viongozi wa Jumuiya ya wazazi  katika ngazi ya matawi na kata, wameshukuru utaratibu wa ugawaji wa miche kuelekea kilele cha maadhimisho ya hayo na kuahidi kusimamia miti hiyo kwa manufaa ya jamii nzima ya Musoma vijijini.

“Tuwashukuru wote waliofanikisha kazi hii, nasi tunaahidi kuelekea kilele cha maadhimisho ya sherehe za wiki ya wazazi, sisi kama wazazi tutasimamia na kuilinda miti hii kwa manufaa ya jamii yetu” alishukuru na kusema Labani Kuboja wa kata ya Bukumi.

 

MVUA YASABABISHA MAAFA MENGINE KIJIJI CHA BUKUMI NA BURAGA

Walimu na uongozi wa Shule ya Msingi Bukumi na wananchi wa kijiji hicho wakikagua athari zilizotokana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali na kusababisha paa za vyumba vya madarasa vya shule hiyo kuezuliwa huku familia tisa zikikosa makazi kwenye kijiji cha Bukumi na Buraga.

Na. Fedson Masawa

MVUA kubwa iliyoambatana na upepo mkali imeezua paa za vyumba vitatu vya madarasa na nyumba mbili za walimu katika shule ya msingi Bukumi iliyopo Kata ya Bukumi.

Mvua hiyo iliyonyesha Machi 9, majira ya saa tisa usiku pia imesababisha familia tisa kukosa makazi kutokana na paa za nyumba zao kuezuliwa na upepo katika kijiji cha Bukumi na Buraga.

Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Bukumi Jumanne Chacha amesema, mbali na kuezuliwa kwa majengo ya madarasa na nyumba za walimu, mvua hiyo pia imesababisha uharibifu wa chakula, vitabu na madaftari ya wanafunzi mali zilizokuwemo kwenye ofisi na stoo ya shule hiyo.

Mwalimu William Rungongo ambaye ni mmoja wa walimu ambao nyumba zao zimeezuliwa alisema: “haikuwa hali ya kawaida kwa usiku wa leo, nimeangaika na familia yangu namshukuru Mungu nimetoka salama.”

Wakijadili kwenye kikao cha dharura cha kamati ya shule kilichowashirikisha wajumbe wa serikali ya kijiji cha Bukumi na uongozi wa kata ya Bukumi, wamekubaliana kuwatafutia walimu hao nyumba za kuishi kwa muda kijijini hapo wakati serikali ikifanya maandalizi ya kukamilisha nyumba moja ya mwalimu ambayo ipo katika hatua nzuri ya ujenzi na kujenga nyumba nyingine za walimu.

Hata hivyo, Diwani wa kata ya Bukumi John Manyama amebainisha kuwa tukio hilo ni kubwa ndani ya kata yake na atashirikiana na serikali ya kijiji na wananchi na wadau mbalimbali kufanikisha ukarabati wa miundombinu iliyoharibiwa na kuongezea kuwa, limekuwa jambo jema kwa kuwa familia za walimu wa shule yake zimetoka zikiwa salama.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wananchi wa kijiji cha Bukumi wamesikitishwa na matukio ya namna hiyo ambayo yanaendelea kujitokeza mara kwa mara ndani ya kijiji chao na kata ya Bukumi kwa ujumla.

Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo ameahidi kuwatembelea wahanga wa tukio hilo na kutoa msaada ikibidi, huku ofisi yake ikiendelea kufuatilia kwa karibu suala hilo ambalo ni mara ya pili kwa siku za karibuni; wiki iliyopita watu watatu walifariki dunia kwenye kijiji cha Bwai Kumsoma baada ya nyumba waliyokuwa wanaishi kuanguka kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali.

SIKU YA WANAWAKE YAADHIMISHWA KIPEKEE KIJIJI CHA BWAI

Baadhi ya akinamama waliojitokeza kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani zilizofanyika kwenye kijiji cha Bwai Kumsoma, Jimbo la Musoma vjijini.

Na. Verdiana Mgoma

MAADHIMISHO ya siku ya wanawake duniani Jimbo la Musoma vijijini yameadhimishwa kwenye kijiji cha Bwai Kumsoma kwa kufanyika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Akizungumza kwenye sherehe hizo mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt. Vincent Naano Anney aliwataka wanafunzi wa kike wa shule ya msingi Bwai kusoma kwa bidii ili wakabiliane na vitendo vya ukatili kwa watoto wa kike kwa kuzitambua haki zao.

Dkt. Naano alisema, Serikali inaendelea na jukumu lake la  kumlinda na kutetea haki ya mtoto wa kike ili aweze kutimiza malengo aliyojiwekea bila kujali itikadi za kisiasa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Musoma Flora Yongolo alisema, lengo kuu la maadhimisho hayo ni kuongeza mshikamano wa wanawake na kuhimiza mapambano dhidi ya ukatili wa mtoto wa kike ili kutimiza malengo ya kufikia kwenye uchumi wa kati.

Mkurugenzi huyo alisema, kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kudhibiti baadhi ya vitendo vya unyanyasaji na ukatili dhidi ya mwanamke kwenye jamii za vijijini, ingawa jitihada zaidi zinahitajika ili kutokomeza kabisa vitendo hivyo.

Akieleza jukumu la Serikali kwa kushirikiana na vitengo vya haki za binadamu alisema, wameendelea kutoa ushirikiano hasa kwenye usawa wa kijinsia na kumuwezesha mwanamke kisiasa, kiuchumi, kielimu na kiafya ili aweze kufikia malengo.

Mkurugenzi Yongolo aliendelea kusema, katika uundaji wa majukwaa ya kuwawezesha wanawake kiuchumi, wametoa elimu kwa vikundi vya wanawake vinavyojishughulisha na ushonaji, ubunifu, ujasiliamali kwa kutengeneza vitu vya asili na makundi mengine ya wanawake.

Aidha, Yongolo aliwataka akina mama kujikita zaidi kwenye kilimo cha umwagiliaji ili kujiinua kiuchumi ambapo vikundi vya akinamama kutoka vijiji vya Suguti, Lyasembe, Nyambono na Mugango vilikabidhiwa mashine za umwagiliaji.

Mbali na mashine hizo, katika maadhimisho hayo shilingi milioni 23 zilitolewa kwa vikundi 10 vya akina mama na vijana kwa ajili kujiendeleza katika shughuli za kilimo na biashara.

Vikundi vilivyopokea fedha hizo ni Kikundi cha akinamama cha Mshikamano, We grow, Jitahidi ufaidike, Nyakabhungo, Juhudi, Jaribu, Bomafa, Amani na Upendo na kikundi cha Karpentas.

Naye Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo aliungana na akinamama kuadhimisha kilele cha siku ya wanawake duniani kwa kutoa mchango wa miche ya miti ili kuwahamasisha watoto wa kike kulinda mazingira ambapo katika sherehe hizo miti 3,000 ilipandwa kwenye shule ya Msingi Bwai.

Prof. Muhongo pia alitoa mabati 54 kwa kikundi cha wanawake wa kijiji cha Bwai Kumsoma (We grow) kwa ajili ya kuezeka vyumba vya madarasa vilivyojengwa na kikundi hicho.

MVUA KUBWA YASABABISHA MAAFA MUSOMA VIJIJINI

Msaidizi wa Mbunge James Francis akikabidhi mchango ikiwa ni rambi rambi kutoka ofisi ya mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini kwa familia ya ndugu waliopatwa na maafa kufuatia mvua kubwa iliyonyesha jana usiku.

Na. Verdiana Mgoma

MVUA kubwa iliyonyesha jana usiku imesababisha maafa makubwa ikiwemo vifo vya watu watatu wa familia moja waliopoteza maisha baada ya kuangukiwa na nyumba kwenye kijiji cha Bwai Kumsoma, Musoma vijijini.

Msemaji wa familia hiyo ambaye ni baba wa majeruhi Makukumbile Chrismas alisema, mvua hiyo kubwa ilianza kunyesha mnamo saa sita usiku huku mke na watoto wake wakiwa wamelala, ndipo walipoangukiwa ukuta wa nyumba na kupoteza maisha.

Makukumbile alisema, iliwachukua muda mrefu hadi majirani kujua kama mtoto wake na familia yake wamepatwa na tatizo hilo, ambapo mmoja wa marafiki wa mwanaye ndiye aliyegundua tatizo hilo alipokwenda kumfuata rafiki yake ili waende ziwani kuvua samaki ambapo alimkuta akiwa amelala huku akiomba msaada kwa majirani.

Kwa upande wake Mtendaji wa kata ya Bwai, Pendo Mwita alisema, kabla ya kupatwa na dhoruba hiyo, tayari nyumba ya Michael Makukumbile ilikuwa na nyufa ambazo wao hawakutambua mapema kama zingeleta madhara.

Aidha, mtendaji huyo alithibitisha vifo vya watu watatu ambao ni wanafamilia akiwemo mama anayeitwa Stella Magembe na watoto wawili Ester (3) na Chrismas (miezi saba) huku baba wa familia hiyo Michael Makukumbile akiendelea na matibabu katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) kutokana na majeraha aliyoyapata.

“Kuna rafiki wa majeruhi ambaye ni Baba wa familia hii, alikuwa akijishughulisha na uvuvi alimfuata waende ziwani alipofika nyumbani kwake akawa anasikia sauti za kuomba msaada, ndipo naye akatoa taarifa kwa majirani ili kumsaidia kumtoa majeruhi huyo” alisema Pendo.

Kutokana na tukio hilo, mtendaji huyo amewataka wananchi wa eneo hilo kufuata ushauri wanaopewa kuhusiana na ujenzi ulio bora kuliko kujenga bila kufuata utaratibu, huku akiahidi kushirikiana na viongozi wa eneo hilo kutoa elimu kupitia mikutano ya hadhara pamoja na makanisa.

Naye Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Ibrahimu Kaale alimshukuru Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo kwa kuungana nao katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo, ambapo kupitia ofisi ya mbunge ametoa rambi rambi ili kuwafariji wahanga hao huku akiahidi kuwatembelea wote waliopatwa na tatizo hilo.

SHULE YA SEKONDARI KASOMA KUJENGEWA MAABARA YA KISASA

Naibu Waziri wa Elimu William Ole Nasha (wa pili kulia) akiwa kwenye ukaguzi wa shule ya Sekondari Kasoma. Wengine kwenye picha ni Ibrahimondi Malima (wa kwanza kulia) ambaye ni Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma na Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt. Vincent Naano Anney (wa pili kushoto).

Na. Fedson Masawa

NAIBU Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William  Ole Nasha ameahidi ujenzi wa maabara kubwa ya kisasa katika shule ya Sekondari Kasoma ikiwa ni hatua muhimu ya kutoa elimu bora kwa masomo ya sayansi nchini.

Ole Nasha alitoa ahadi hiyo wakati alipozungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Kasoma katika ziara yake aliyoifanya kwenye Halmashauri ya Musoma ambapo alikagua miradi miwili; Lipa kulingana na matokeo (P4R) uliokuwa ukitekelezwa katika shule mbili za Musoma vijijini ambazo ni shule ya msingi Kamguruki iliyopo kata ya Nyakatende pamoja na shule ya sekondari Kasoma iliyopo kata ya Nyamrandirira.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri huyo aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri na wakuu wa idara kutoka Halmashauri ya Musoma, ambapo alikiri kuridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo na kusema ni ishara ya matumizi mazuri ya fedha za serikali.

“Hongereni sana Musoma vijijini kwa kutumia vizuri fedha za serikali na wafadhili. Hii inatupa chachu ya kuendelea kusaidia miradi ya maendeleo alisema Naibu Waziri Ole Nasha.

Katika miradi hiyo miwili, mradi wa shule ya msingi Kamguruki uliotumia Shilingi milioni 112 umekamilika kwa kujengwa vyumba vinne vya madarasa, choo cha wanafunzi matundu 20, ofisi mbili za walimu, maktaba moja na ukarabati wa vyumba vya madarasa.

Katika shule ya sekondari Kasoma iliyopokea jumla ya Shilingi milioni 236, Naibu Waziri amejiridhisha na ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa, kazi ambayo imekamilika na ujenzi wa mabweni mawili yenye vyumba 24 kazi ambayo inaelekea mwishoni.

Hata hivyo, Naibu Waziri Ole Nasha alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo kwa jitihada kubwa anazozifanya Jimboni mwake za kuboresha elimu hasa katika uchangiaji wa madawati katika shule zote za Musoma vijijini, ujenzi wa vyumba vya madarasa na usambazaji wa vitabu kwa shule zote za sekondari na msingi.

Kwa upande wao wanafunzi wa shule ya sekondari Kasoma wametoa shukrani zao kwa serikali kupitia kwa viongozi wao na kuahidi kufanya vizuri katika masomo yao hasa watakapopata maabara kwa ajili ya masomo ya Sayansi.

“Tunashukuru serikali na viongozi wetu kwa kuweka elimu kama kipaumbele cha maendeleo. Ujenzi wa maabara kwetu utatoa fursa kwetu kufanya vizuri zaidi hasa katika masomo ya sayansi” alishukuru Elizabeth Michael, mwanafunzi wa kidato cha nne.

WAKULIMA WAPOKEA MBEGU ZA ALIZETI NA UFUTA MUSOMA VIJIJINI

Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo akizungumza na baadhi ya wakulima waliokabidhiwa mbegu za alizeti na ufuta, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt. Vincent Naano Anney.

Na Fedson Masawa

WAKULIMA wa vijiji na kata mbalimbali ndani ya Jimbo la Musoma vijijini wamepokea mbegu za alizeti na ufuta kutoka kwa Mbunge wa jimbo hilo Prof. Sospeter Muhongo ikiwa ni maandalizi ya msimu wa kilimo ambao tayari umeanza mwezi Februari, mwaka huu.

Zoezi hilo la ugawaji wa mbegu ambalo lilifanyika kwa kanda tano Bukwaya, Mugango, Murangi, Saragana na Busekera, liliongozwa na mbunge Prof. Muhongo, Mkuu wa wilaya ya Musoma Dkt. Vincent Naano Anney pamoja na Kaimu Afisa kilimo wa wilaya ya Musoma Ismail Masogo.

Wakizungumza baada ya kupokea mbegu hizo, wakulima hao walisema wamefurahishwa na tukio hilo muhimu na kuahidi kutoa ushirikiano mkubwa ili kuhakikisha wanapanda na kuvuna vizuri na kutumia mazao hayo kwa ajili ya kuinua uchumi wa familia zao na maeneo wanayotoka.

“Tunamshukuru sana Mbunge na Halmashauri yetu kwa kutupa mbegu bure. Tutapanda kwa wakati, tutayatunza mashamba vizuri hatimaye tutoe mavuno yaliyo bora ili kuinua kipato cha familia zetu” alisema Pili Julius,  mkulima kutoka kijiji cha Mayani kata ya Tegeruka.

Kwa upande wake Kaimu Afisa Kilimo Ismail Masogo alisema, ofisi yake kwa kushirikiana na Maafisa kilimo wa kata, watatoa usimamizi na elimu kwa wakulima kuhusu utayarishaji wa mashamba, upandaji, upaliliaji, uvunaji na utunzaji wa mazao hayo ili kuhakikisha msimu huu unakuwa na mafanikio makubwa Jimboni humo.

Aidha, katika kuimarisha soko na utunzaji wa zao la alizeti, tayari mitambo miwili ya watu binafsi imejengwa Jimboni katika kijiji cha Kusenyi na Saragana ambapo itasaidia kuongeza thamani ya mazao hayo.

Hata hivyo, wakiwa katika ziara ya ugawaji wa mbegu hizo bila malipo, Mkuu wa Wilaya na Mbunge pia walitembelea shamba la pamba lililopo kijiji cha Kinyang’erere kata ya Bugwema.

Kwenye ziara hiyo, Mkuu wa Wilaya Dkt. Naano aliwataka maafisa kilimo wa kata na vijiji wahakikishe wanawatembelea wakulima wa pamba kila mara ili kuona maendeleo yao na changamoto zinazowakabili na kuwatatulia kwa lengo la kuongeza mavuno na ubora wa zao hilo.

PROF. MUHONGO AWATAKA WANANCHI KIJIJI CHA NYASAUNGU KUKAMILISHA UJENZI WA ZAHANATI

Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye kijiji cha Nyasaungu.

Na. Verediana Mgoma

MBUNGE wa Jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo amewataka wananchi wa kijiji cha Nyasaungu kuweka nguvu zao katika kumalizia ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho uliosimama kwa miaka sita.

Prof. Muhongo alisema hayo leo wakati wa ziara yake aliyoifanya kwenye kijiji hicho, ambapo aliwataka wananchi hao kujitolea kwa hali na mali kukamilisha ujenzi wa zahanati hiyo mapema na kuahidi iwapo watakamilisha ujenzi huo kufikia Juni, mwaka huu, atachangia mabati kwa ajili ya kumalizia ujenzi huo ili wananchi wa kijiji hicho wawe karibu na huduma ya afya.

Aidha, katika mkutano huo Prof. Muhongo alichangia mifuko 100 ya saruji pamoja na shilingi 200,000 kwa ajili ya malipo ya fundi na wananchi waliendesha harambee na kufanikiwa kupata fedha ambazo zitatumika kununua mifuko 109 ya saruji.

Mwenyekiti wa kijiji cha Nyasaungu Magesa Chacha alisema, zahanati ya Nyasaungu ilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi mwaka 2012, ambapo walikuwa wakichangia nguvu kazi na fedha, hata hivyo ujenzi huo ulisimama kwa muda baada ya kuwepo kwa changamoto za ukosefu wa fedha, vitendea kazi na wataalamu.

“Baada ya kilio chetu kufika ofisi ya mbunge, tulipata ushirikiano wa kutosha wa namna ya kufanikisha ujenzi wa zahanati ya Nyasaungu, mpaka sasa wananchi wameongeza nguvu zao na kukusanya mchanga, mawe pamoja na kufyatua matofali” alisema Chacha.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Nyasaungu Manyama Meru, alitoa shukrani za pekee kwa mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini kwa kuweka nguvu kwenye sekta ya afya ndani ya kata hiyo na kuwasaidia wananchi wa kijiji cha Nyasaungu kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma ya afya.

Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Musoma Thadeus Makwanda aliahidi kutoa ushirikiano kwa wananchi wa kijiji hicho ikiwa ni pamoja na kumpeleka mkandarasi kutoka Halmashauri ili kuwaelekeza namna ya kujenga zahanati hiyo kitaalamu.

ZAHANATI NYASAUNGU

Ofisi ya Mbunge inapenda kuwataarifu kuwa, kesho tarehe 15/02/2018 saa 5:00 Asubuhi, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo atatembelea eneo la ujenzi wa zahanati ya Nyasaungu na kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho kuhusu utaratibu wa kuendeleza ujenzi wa zahanati yao

Katika ziara yake hiyo, Prof. Muhongo ataambatana na Mganga Mkuu wa wilaya, Madiwani n.k.

KARIBUNI NYASAUNGU

Ofisi ya Mbunge
www.musomavijijini.or.tz

ZAHANATI YA KIJIJI CHA MWIRINGO KUANZA KUTOA HUDUMA MWEZI UJAO

Mbunge wa Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo mapema leo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwiringo (wengine hawapo pichani) mbele ya jengo la zahanati ya Mwiringo ambayo itaanza kutoa huduma za afya Machi, 1, 2018.

Na. Mwandishi Wetu

WAKAZI wa Kijiji cha Mwiringo, Halmashauri ya Musoma vijijini na Mbunge Prof. Sospeter Muhongo, wamekubaliana huduma za matibabu kwenye zahanati ya kijiji hicho zianze kutolewa Machi, 1, mwaka huu.

Uamuzi huo umefikiwa kwenye mkutano uliofanyika kwenye kijiji cha Mwiringo, Kata ya Busambara ambapo Prof. Muhongo amechangia  meza, viti na vifaa vingine vinavyohitajika ili kuharakisha ufunguzi wa zahanati hiyo.

Wiki chache zilizopita, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt. Makwanda alisema, jambo linalochelewesha zahanati hiyo kuanza kutoa huduma, ni ukosefu wa meza nne na viti nane na vifaa vingine, hivyo kwa mchango huo wa mbunge kero ya muda mrefu ya wananchi wa kijiji cha Mwiringo ya kukosa huduma za afya inaelekea kupata ufumbuzi.

Zahanati hiyo ilianza kujengwa Mwaka 2011 kwa nguvu za wananchi na kwa mchango mkubwa wa vijana wasomi na wataalamu kutoka Kijiji cha Mwiringo, ujenzi wake ulikamilika mwaka 2014 na awali zahanati hiyo ilipangwa ianze kutoa huduma Mei, 1, 2018, lakini kutokana na hamasa iliyopo, itaanza kutoa huduma mwezi ujao.

KIKUNDI CHA AKINAMAMA WA LYASEMBE WAFURAHIA MAFANIKIO KWENYE KILIMO

Baadhi ya akinamama wa Kikundi cha kijiji cha Lyasembe wakiwa kwenye picha ya pamoja na Msaidizi wa Mbunge, Verdiana Mgoma alipowatembelea kwenye eneo wanalofanya mradi wao wa kilimo.

Na. Verdiana Mgoma

KIKUNDI cha akina mama wa kijiji cha Lyasembe wamesema wamepata mafanikio makubwa kiuchumi baada ya kujitosa kwenye kilimo cha umwagiliaji.

Kikundi hicho ambacho ni miongoni mwa vikundi vilivyopata ufadhili wa fedha za mfuko wa jimbo, kinajishughulisha na kilimo cha bustani za mboga mboga na matunda.

Katibu wa kikundi hicho Mawazo Jumbura alisema, baada ya kupokea mashine, mipira na mbegu kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji, walitambua kuwa wana jukumu kubwa katika jamii yao na kuamua kutumia vifaa hivyo kutafuta maendeleo yao, familia zao na jamii inayowazunguka.

Katibu huyo alisema, tangu wameanza kilimo hicho, hali zao kimaisha zimebadilika na wanamudu mahitaji ya familia zao ikiwemo kusomesha watoto na kununua mahitaji yao binafsi na wamejiwekea malengo ya kununua mashine nyingine za umwagiliaji na kuanzisha miradi mingine mbali na kilimo ili kujiongezea kipato zaidi.

Mbali na faida walizopata kupitia kikundi hicho, Katibu huyo pia ameelezea changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na ukosefu wa eneo kubwa la kulima, ukosefu wa soko la kuuzia bidhaa zao baada ya kuvuna, ugumu wa upatikanaji wa elimu kupitia matamasha, wahamasishaji na maonyesho kwa ajili ya kuboresha zaidi kilimo chao.

Hata hivyo, licha ya changamoto hizo wamemshukuru Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo kwa kuwaonyesha fursa hiyo ya kilimo cha umwagiliaji ambacho wanaamini kitawainua kiuchumi.

Naye, Afisa kilimo wa Kata ya Murangi Maricha Mgono akizungumza kijijini Lyasembe alisema, mpango wa kilimo cha umwagiliaji ni harakati zilizowekwa kuhakikisha akina mama na vijana wanajiajiri kupitia kilimo na kuinua hali zao kiuchumi.

Mgono alisema, hivi sasa kumekuwepo na muamko mkubwa wa kilimo cha umwagiliaji katika kata hiyo tofauti na ilivyokuwa awali wakazi wa eneo husika walijikita zaidi kwenye uvuvi.

“Tumefanya jitihada za kuhamasisha uundwaji wa vikundi kwa maendeleo ya akina mama na vijana ili kuwepo kwa upatikanaji wa mikopo itakayowasaidia kuwainua kiuchumi na kufungua miradi mbalimbali” alisema.

Kwa upande wake Mtendaji wa kijiji cha Lyasembe Chikonya Chikonya alisema, kadri siku zinavyokwenda, mwitikio wa wananchi kwenye kilimo unazidi kutokana na hamasa ya Prof. Muhongo ambaye aliwahimiza kujikita kwenye kilimo hicho cha umwagiliaji na kuacha kutegemea mvua ambazo hazina uhakika kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

“Kijijini hapa nimepokea mbegu za mtama, mihogo, alizeti kutoka ofisi ya mbunge na mpaka sasa kuna mikakati ya kilimo cha ufuta, kwa ujumla muitikio wa kilimo kwa wakazi wa eneo hili unakuwa siku hadi siku” alisema Chikoya.

MAADHIMISHO YA MIAKA 41 YA CCM YAPAMBA MOTO BUGWEMA

Baadhi ya akinamama wakiimba wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 41 ya kuzaliwa CCM yaliyofanyika kwenye kijiji cha Bugwema

Na. Mwandishi Wetu

DIWANI wa Kata ya Bugwema Ernest Maghembe amesema, Chama cha Mapinduzi (CCM) kimefanya mageuzi makubwa kwa kipindi ilichokaa madarakani.

Akizungumza kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 41 tangu kuzaliwa CCM yaliyofanyika kwenye kijiji cha Bugwema, diwani Maghembe alisema, CCM imefanya mageuzi makubwa ambayo wanachama wake wanapaswa kujivunia hususani kwenye elimu, afya, na kilimo.

Aidha, diwani Maghembe alitumia fursa hiyo kutoa pole kwa familia na watanzania wote kufuatia msiba wa mmoja wa waasisi wa chama hicho Mzee Kingunge Ngombale Mwiru aliyefariki wiki iliyopita na kuzikwa leo jijini Dar es Salaam.

“Tutakumbuka mchango wa mzee Kingunge kwa nchi yetu na chama, tutamuenzi kwa uzalendo wake” alisema diwani Maghembe.

Kwa upande wake msaidizi wa mbunge Hamisa Gamba aliwaomba wanachama wa CCM kuachana na makundi yanayoweza kuleta mgawanyiko ndani ya chama na badala yake maadhimisho hayo yatumike kuwajenga kifikra na katika uwajibikaji hasa kwenye kilimo, elimu na afya.

Msaidizi huyo pia aliwataka wanachama wa CCM na wananchi wote kujiandaa kwa kilimo cha alizeti na ufuta kwa kuwa mbegu zinatolewa bure na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini huku akisisitiza uwepo wa soko la uhakika kwenye mazao hayo.

Sherehe hizo ziliadhimishwa kwa michezo mbalimbali ya vijana ikiwemo kwaya na mpira wa mguu kutoka kwa timu zilizopo kwenye kata hiyo.

 

VIJANA WAHIMIZWA KUONYESHA VIPAJI VYAO KATIKA SOKA

Msaidizi wa Mbunge Fedson Masawa akimpongeza nahodha wa timu ya Zahanati Mafuru Majogoro (kushoto) na kumkabidhi zawadi yao ya mbuzi watatu baada ya kuibuka mabingwa wa Ligi ya ‘Bashiri Vitongoji Ndondo Cup Bukima.’

Na Mwandishi Wetu

VIJANA wametakiwa kujitokeza kwa wingi na kuonyesha vipaji vyao katika mchezo wa mpira wa miguu na hatimaye kutumia vipaji hivyo kujiajiri kupitia timu kubwa za ndani na nje ya Jimbo la Musoma vijijini.

Hayo yamesemwa na msaidizi wa Mbunge Fedson Masawa aliyekuwa mgeni rasmi katika fainali za Ligi ya vitongoji vya kijiji cha Bukima maarufu kama “Bashiri Vitongoji Ndondo Cup Bukima,” iliyoshirikisha timu kutoka vitongoji nane, ikiwa ni maandalizi ya ligi kubwa inayotarajiwa kuanza hivi karibuni kwenye kata ya Bukima.

Masawa alisema, kufanyika kwa mashindano hayo ni hatua nzuri ya kufungua njia kwa vijana wa Musoma vijijini katika kutumia vizuri  vipaji vyao na kumpongeza muandaaji wa mashindano hayo Bashiri Chirwa kwa jitihada anazofanya katika kuhamasisha mpira wa miguu kwenye kata hiyo.

Katika mashindano hayo, timu ya Zahanati ilichukua nafasi ya kwanza kwa kushinda magoli 2 dhidi ya Senta iliyopata goli 1 na kushika nafasi ya pili ambapo mshindi wa kwanza alipata zawadi ya mbuzi watatu na mshindi wa pili alipata mbuzi wawili.

WANANCHI NYASAUNGU WAFICHUA SIRI YA MAFANIKIO YAO

Wananchi wa kijiji cha Nyasaungu waliojitolea kushiriki ujenzi wa zahanati ya kijiji chao wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Na. Fedson Masawa

WANANCHI wa kijiji cha Nyasaungu wamesema siri ya maendeleo kijijini hapo ni umoja, mshikamano na kuheshimiana baina ya wananchi na viongozi ambao kwa kiasi kikubwa ndio wanahusika kusimamia shughuli hizo.

Wananchi hao walisema, maendeleo ni kuwa na mipango ya pamoja, kusikilizana na kuwajibika katika kuchangia shughuli yoyote ya maendeleo bila kusukumwa, hali ambayo inawapa moyo wafadhili mbalimbali na kuungana nao ili kuwapatia huduma bora kijijini hapo.

Katika hatua nyingine, wananchi hao wameishukuru Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini kwa namna ambavyo imewarudisha katika utaratibu wa maendeleo kupitia hamasa na kuwapa moyo wa matumaini ili kufanikisha ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Nyasaungu.

Naye Kaimu Mtendaji wa kijiji hicho  Janas Itembe alisema, baada ya kukamilika kwa maandalizi ya kukusanya kokoto na mchanga, shughuli rasmi ya kurekebisha msingi wa zahanati itaanza Februari 5, 2018 baada ya mhandisi wa wilaya kufika kwa ajili ya maelekezo.

ZAHANATI YA MWIRINGO KUANZA KUTOA HUDUMA MEI MOSI

Msaidizi wa mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini (Fedson Masawa) akipewa maelezo ya ujenzi wa zahanati ya Mwiringo na Mwenyekiti wa kijiji cha Mwiringo Claudian Ihunyo.

Na Mwandishi Wetu

MSAIDIZI wa Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Fedson Masawa ametembelea zahanati ya kijiji cha Mwiringo kilichopo kata ya Busambara kwa lengo la kujua sababu za kuchelewa kuanza kwa zahanati hiyo kutoa huduma za matibabu.

Zahanati hiyo iliyokamilika ujenzi wake tangu mwaka 2014, imejengwa kwa msaada wa mzaliwa wa kijiji hicho kwa kushirikiana na wananchi hadi kufikia kukamilika kwa ujenzi huo, lakini imeshindwa kutoa huduma za afya.

Akizungumza na msaidizi wa Mbunge, Mganga mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt. Makwanda amethibitisha kuwa zahanati ya kijiji cha Mwiringo tayari imekamilika na wao kama idara ya afya ngazi ya wilaya wameshaandaa mahitaji yote na watumishi wa zahanati hiyo wapo tayari kuanza kazi muda wowote.

Dkt. Makwanda alisema, jambo linalochelewesha zahanati hiyo kuanza kutoa huduma ni ukosefu wa meza nne na viti nane ambavyo gharama yake ni shilingi 2,400,000 na zinatakiwa kuchangwa na wananchi wa kijiji hicho ili kufanikisha mahitaji ya zahanti hiyo na kufunguliwa.

Mwenyekiti wa kijiji cha Mwiringo Claudian Ihunyo Maganya amekiri kukosekana kwa meza na viti, jambo ambalo linasababisha wananchi hao kuendelea kukosa huduma ya afya na kulazimika kutembea umbali mrefu zaidi kwa ajili ya kuitafuta huduma ya afya kwenye vijiji vya jirani.

Mwenyekiti huyo alitoa ombi kwa Prof. Muhongo kuwaunga mkono wananchi hao, kwani kwa kipindi kirefu wamekuwa wakielekeza michango yao katika kufanikisha ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Naye Mtendaji wa kata ya Busambara Victor Kasyupa alisema: “ipo haja ya zahanati ya Mwiringo kufunguliwa haraka ili kuwanusuru akina mama na watoto wanaolazimika kusafiri umbali usiopungua kilomita nne kuitafuta huduma ya afya.”

Hata hivyo, Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo amekubali kushirikiana na Halmashauri na wananchi wa Mwiringo katika kukamilisha mahitaji ya zahanati hiyo na kuhakikisha inaanza kufanya kazi Mei, 1, 2018.

MKUU WA WILAYA AENDELEA NA ZIARA YA KIKAZI MUSOMA VIJIJINI

 

Mkuu wa wilaya ya Musoma Dkt. Vicent Naano Anney (kulia) akikaribishwa kuzungumza kwenye mkutano uliofanyika kwenye kijiji cha Bukima.

Na. Verdiana Mgoma

MKUU wa wilaya ya Musoma Dkt. Vicent Naano Anney ameendelea na ziara yake ya kuzunguka kwenye maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo na kusikiliza kero za wananchi wake.

Akiwa katika Jimbo la Musoma Vijijini, Dkt. Naano alifanya ziara katika kata ya Bwasi na Bukima na kufanya mikutano ya hadhara kusikiliza kero zinazowakabili wananchi wa kata hizo ikiwemo changamoto za elimu, maji, mradi wa kilimo cha umwagiliaji (Nyakanda) ambao umesimama na haufanyi kazi

Akijibu kero hizo Dkt. Naano kwanza aliwashukuru wananchi hao kwa kuungana na serikali kuhakikisha wanapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ya vyumba vya madarasa hasa kwa msaada mkubwa kutoka kwa Mbunge wa jimbo hilo Prof. Sospeter Muhongo ambao umefanikisha ujenzi wa vyumba saba na kuviezeka.

Mkuu huyo wa wilaya aliahidi kushirikiana na wananchi hao na Mbunge wao katika kuhakikisha ujenzi wa vyumba vya madarasa vilivyosalia na maabara kwenye kata hiyo vinakamilika mapema.

“Kwa juhudi mnazoendelea kuonyesha kwa kuipa elimu kipaumbele katika kata yenu, nitaungana nanyi na mheshimiwa Mbunge kuhakikisha tatizo la vyumba vya madarasa linakwisha kabisa” alisema Dkt. Naano.

Kwa upande wa sekta ya afya, mkuu huyo wa wilaya aliwataka wakazi wa eneo husika kutoa ushirikiano zaidi katika kutimiza malengo yao hasa kwa upande wa ujenzi wa kituo cha afya cha Bukima ili kuboresha zaidi huduma za afya kwenye kata hiyo.

Mbali na hayo, Dkt. Naano amewataka wakazi wa eneo hilo kujikita zaidi katika kilimo hasa cha umwagiliaji kutokana na kuwepo kwa miradi ya kilimo na fursa ya upatikanaji wa maji kwa urahisi, hivyo amewataka kulima zaidi mazao ya nafaka.

WANAFUNZI WANYERE ‘A’ WAELEZEA CHANGAMOTO YA UPUNGUFU WA MADARASA

Na Hamisa Gamba

WANAFUNZI wa shule ya msingi Wanyere A, iliyopo kata ya Suguti, Jimbo la Musoma vijijini wanakabiliwa na uhaba wa mkubwa wa vyumba vya madarasa hali inayowalazimu kusoma wakiwa chini ya miti.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi shuleni hapo, wanafunzi wa darasa la tano wa shule hiyo walisema, hivi sasa hawana tatizo la madawati kama ilivyokuwa mwanzo, lakini wanakabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa.

Mmoja wa wanafunzi hao Jackson Malima alisema, mbali na changamoto ya ukosefu wa vyumba vya madarasa inayowafanya wasome kwenye mazingira magumu ikiwemo kuchomwa na jua kwa muda wote wa masomo, lakini bado darasa lao hilo la nje halina ubao wa kufundishia.

“Madarasa tuliyonayo ni machache sana, hivyo inatulazimu wakati mwingine kubadilishana chumba cha darasa na wanafunzi wa darasa lingine pale tunapohitaji kujifunza kwa maandishi hususani somo la hisabati ambalo ni lazima ubao utumike” alisema Malima.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Wanyere ‘A,’ Buriro  Manyama, alisema ukosefu wa madarasa ni changamoto kubwa inayowakabili shuleni hapo na kuchangia kwa kiasi kikubwa kushusha kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wao.

Mwalimu Manyama alisema, sambamba na hilo bado shule yao haina vyoo, hivyo huwalazimu kuchangia choo cha shule ya msingi Wanyere ‘B,’ ambacho hakikidhi mahitaji ya wanafunzi 900 wa shule zote mbili.

Kutokana na hali hiyo, wanafunzi na mwalimu mkuu huyo waliomba msaada wa serikali, viongozi na wazazi ili kukabiliana na changamoto hizo za upungufu wa vyumba vya madarasa na vyoo.

KILIMO CHA ALIZETI NA UFUTA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Wakulima wa Jimbo Musoma Vijijini wameendelea kupata uzoefu wa kulima ALIZETI na kwa sasa wanaingia msimu wa 3. Mbunge wa Musoma Vijijini, DC, DED na Afisa Kilimo wa Halmashauri wamefanya Kikao leo tarehe 25 Jan 2018 kukamilisha utaratibu wa upatikanaji wa mbegu za ALIZETI na UFUTA kwa ajili ya kilimo cha mazao hayo kwa msimu huu mpya.

Viongozi hao wamekubaliana kununua mbegu za ALIZETI kilo 4,974 zitakazonunuliwa na Mbunge wa Jimbo (Prof Sospeter Muhongo), na kilo 2,651 za UFUTA zitakazonunuliwa na Halmashauri. Imeazimiwa kwamba mbegu zote hizo zipatikane na kuwafikia Wakulima Jimboni kuanzia tarehe 10 Feb 2018. Jimbo la Musoma Vijijini limeazimia kuwa na ukulima mkubwa wa mazao ya PAMBA, ALIZETI, UFUTA, MUHOGO na mazao mengine ya chakula.

Ofisi ya Mbunge
www.musomavijijini.or.tz

WAZEE WA MUSOMA VIJIJINI WAUNDA BARAZA LAO

Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wazee kutoka kwenye vijiji mbalimbali ndani ya jimbo lake ambao walikutana kwenye kijiji cha Murangi na kuunda baraza ambalo litafanya shughuli za kijamii ndani ya jimbo hilo.

Na. Mwandishi Wetu

WAWAKILISHI wa wazee wa vijiji 68 vya Jimbo la Musoma vijijini wamekutana na kuunda baraza lao ili kurahisisha na kuboresha mawasiliano baina ya wazee na jamii inayowazunguka.

Malengo mengine ya kuanzishwa kwa baraza hilo ni  kuweka pamoja mawazo ya wazee katika kusimamia maadili ndani ya jamii na kuishauri serikali katika suala zima la utekelezaji na ufuatiliaji wa shughuli za maendeleo.

Kikao hicho cha wazee hao kilichofanyika Januari, 23, katika kijiji cha Murangi, kilihudhuriwa na mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo, madiwani na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Musoma pamoja na wazee wawili kutoka katika kila kijiji walio wawakilisha wazee wenzao kutoka vijijini.

Wakizungumzia muundo wa baraza hilo, wazee wa Jimbo la Musoma vijijini wamekubaliana kuwa, muundo wa baraza hilo uanzie ngazi ya kijiji, kata hadi jimbo ambapo kila muundo utakuwa na wajumbe wake watakaochaguliwa na wazee wenyewe kutoka kila ngazi husika.

Aidha, wazee hao wamemshukuru Mbunge wao Prof. Sospeter Muhongo kwa ubunifu wake na kwa kuwajali wazee na wananchi wote wa Jimbo la Musoma vijijini.

Wakati huo huo, Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini Prof. Muhongo alitumia fursa hiyo kugawa kwa uwazi milioni 26 fedha za mfuko wa jimbo ambapo jumla ya shule 15 zimenufaika na mgao huo.

Shule hizo zimetengewa fedha hizo za kununulia mabati 54 kwa kila shule kwa ajili ya kuezeka chumba kimoja cha darasa katika harakati za kupunguza uhaba wa vyumba vya madarasa kwenye shule za msingi na sekondari ndani ya jimbo la Musoma vijijini.

Shule zilizonufaika na mgao huo kwa upande wa shule za msingi ni Nyegina, Kambarage, Mugango, Chanyauru B, Tegeruka, Rusoli, Busekera, Butata, Bugoji, Kamatondo, Kusenyi B na Kanyega, huku shule za sekondari ni Busamba, Bulinga na Mabui.

 

HALMASHAURI KUU YA CCM MUSOMA YAKUTANA KUJADILI MAENDELEO

Katibu wa CCM Wilaya ya Musoma Joseph Gatty (aliyesimama) akisisitiza jambo kwa wajumbe wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (hawapo pichani) huku akisikilizwa kwa makini na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Musoma Vijijini Nyabukika Bwire (kulia), Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt. Vincent Naano (wapili kushoto) na Msaidizi wa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini James Francis (mwenye fulana nyeusi) pamoja na viongozi wengine.

Na Fedson Masawa

HALMASHAURI Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Musoma Vijijini, Mkoani Mara imefanya kikao maalum kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya wilaya hiyo na kukubaliana kuwaunganisha wananchi bila kujali itikadi zao za vyama.

Kikao hicho kilichohudhuriwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM ngazi ya wilaya, pia kilihudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Musoma ambaye pia ni mjumbe, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini aliyewakilishwa na Msaidizi wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Musoma na Madiwani wote wanaotokana na chama hicho.

Akizungumza wakati wa ufunguzi Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Musoma na mwenyekiti wa kikao hicho Nyabukika Bwire, aliwataka viongozi wa kata kusimamia na kufuatilia utendaji kazi wa viongozi kuanzia ngazi ya mashina, matawi, kata hadi wilaya hasa katika uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Mwenyekiti huyo alisema, ili kufanikisha hayo suala la mawasiliano baina ya viongozi katika chama na serikali ni muhimu katika kuondoa tofauti za utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt. Vincent Naano Anney aliwashukuru wananchi wanaoendelea kuungana na serikali katika kufanikisha suala la kuchangia elimu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa maabara pamoja na vyumba vya madarasa na kusema hatua hiyo imefikia pazuri.

“Shule nyingi za sekondari na msingi bado zina changamoto ya upungufu mkubwa wa madawati hali inayopelekea baadhi ya wanafunzi wanaojiunga na masomo kukaa chini na serikali inaendelea kufanya jitihada kwa kushirikiana na wazazi kuhakikisha tatizo hilo linakoma” alisema Dkt. Naano.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Musoma Charles Magoma alisema, kwenye shule za msingi na sekondari kumejitokeza changamoto ya upungufu wa madawati haswa kwa wanafunzi wapya wanaojiunga darasa la kwanza na kidato cha kwanza.

“Suala la madawati ni changamoto katika shule zetu za sekondari na msingi hasa pale wanafunzi wanapojiunga kidato cha kwanza na darasa la kwanza. Sisi halmashauri tumeshakubaliana tutashirikiana na wazazi katika kufanikisha suala la madawati katika shule zetu” alisema Magoma.

Akitoa taarifa kwa wajumbe wa kikao hicho, Katibu wa CCM wilaya ya Musoma Joseph Gatty alisema, katika kufanikisha kikao hicho, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo alichangia usafiri kwa wajumbe 108 ili kuhakikisha wanawahi kufika kwenye kikao na kurudi majumbani mwao kwa wakati uliopangwa.

Kutokana na mchango huo, Gatty alimpongeza Prof. Muhongo kwa jitihada anazoendelea kuzifanya katika kufanikisha shughuli mbalimbali za chama na serikali ndani ya Mkoa wa Mara.

UVCCM MUSOMA WATAKIWA KUTUMIA VIZURI FURSA ZA MAENDELEO

Wasaidizi wa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini James Francis (kulia) Verdiana Mgoma na Hamisa Gamba wakifuatilia Kikao cha Baraza la Umoja wa Vijana wa CCM ( UVCCM) kilichofanyika kwenye kijiji cha Suguti.  

Na. Verdiana Mgoma

UMOJA wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Musoma umefanya kikao chake kwenye Kijiji cha Suguti na kujadili masuala mbalimbali ya kiuchumi na maendeleo.

Akizungumza kwenye kikao hicho Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mara Jacob Mangalaya alisema, Jumuiya hiyo inapaswa kuachana na utegemezi na ili kufikia malengo hayo wanatakiwa kuunda vikundi vitakavyo wanufaisha kiuchumi, kijamii na kisiasa kulingana na fursa zilizopo.

Mwenyekiti huyo alisema, vikundi vitakavyoundwa vinatakiwa kupewa elimu ya kutosha, huku akisisitizia wajumbe kujitokeza kwenye suala la michezo na kugusia zoezi la uhakiki wa mali za UVCCM.

Kwa upande wake Katibu wa UVCCM Wilaya ya Musoma Joseph Mbogo alielezea jinsi ambavyo mfuko wa vijana ulivyowasaidia kuwapa mikopo na kuwawezesha katika miradi ya kilimo, uvuvi na urandaji mbao.

Katibu huyo alisema, mbali na mafanikio hayo waliyoyapata kutokana na mikopo, wanakabiliwa na changamoto mbalimbali katika utendaji wa kazi zao za kila siku ikiwemo kukosa usafiri, sare na kadi kwa wanachama wapya pamoja na upungufu wa vitendea kazi kwa watendaji ngazi ya kata na wilaya.

Hata hivyo, alimshukuru Mbunge wa Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo kwa juhudi na mchango wake kwenye chama na maendeleo ya jimbo kwa ujumla.

KILIMO CHA ALIZETI & UFUTA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI – VIKUNDI VYA VIJANA – JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI – Msimu wa kilimo cha ALIZETI na UFUTA Jimboni umewadia. Vikundi vya Vijana vikiwemo vya UVCCM vinaombwa viwakilishe maombi ya mbegu za ALIZETI na UFUTA kwa Wasaidizi wa Mbunge au Madiwani wa maeneo yao kabla ya tarehe 25 Januari 2018.

Ofisi ya Mbunge.

www.musomavijijini.or.tz

KIKAO CHA UMOJA WA WAZEE WA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Tarehe: 23 Januari 2018
Mahali: Kijiji cha SUGUTI
Ajenda: Uzinduzi Rasmi wa Umoja huo
Wajumbe wa Awali wa Umoja huo: Wazee wawili (2) kutoka kila Kijiji. Tunavyo Vijiji 68.
Wasaidizi wa Mbunge na Madiwani watayarishe orodha ya Wajumbe wa Awali wa Umoja huo. Wazee wajichague wenyewe kutoka Vijijini mwao.

Ofisi ya Mbunge