JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Prof. Sospeter Muhongo

Mh. Mbunge, Prof. Sospeter Muhongo

"Tovuti Rasmi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo, Kwaajili ya Kuwasiliana na Wananchi Jimboni "

MBUNGE WETU MH. PROF. SOSPETER MUHONGO ANATUHAMASISHA KUTEMBELEA WEBSITE HII KILA MARA, KWA MAENDELEO YETU SOTE.

UCHUNGUZI NA MJADALA WA HALI YA ELIMU NA MAPENDEKEZO
YA UBORESHAJI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MUSOMA
TAARIFA YA AWALI

A CONCISE PROFESSIONAL CV OF PROF. SOSPETER MWIJARUBI MUHONGO

CONCISE CV:

Prof Dr. rer. nat. Sospeter Mwijarubi Muhongo 

He is a very distinguished world-class scholar, a Chartered and a European earth scientist. He holds a Dr.rer.nat. degree from the Technical University of Berlin, Germany. He writes and speaks fluent Kiswahili, English, and German languages. His French is basic.

Recognition by the world's topmost learned professional societies:

*Honorary Fellow, Geological Society of London (est. 1807), HonFGS

*Honorary Fellow, Geological Society of America (est.1888), HonFGSA

*Honorary Research Fellow, Chinese Academy of Geological Sciences (est. 1956),

HonRFCAGS

Top International professional services & leadership:

*Former Vice President of the Commission of the Geological Map of the World (CGMW)

*Former Chair of the Science Programme of the UN-proclaimed International Year of Planet Earth (UN-IYPE)

*Former Chair of UNESCO-IUGS-IGCP Scientific Board of International Geoscience Programme

*Former President of the Geological Society of Africa (GSAf)

*Former Regional Director (Africa) for the International Council of Scientific Unions (ICSU-ROA)

*Editor-in-Chief Emeritus, JAES, Elsevier

*Selecting Expert: UNESCO & TWAS international science awards

Top National Leadership:

*Member of Parliament for the Musoma Rural Constituency

*Former Minister for Energy and Minerals

*Former Chair of the State Mining Corporation (STAMICO) Board of Directors

*Former Head of the Department of Geology of the University of Dar es Salaam

Fellowships & Recognitions in abbreviation:

Prof Dr.rer.nat. Sospeter M Muhongo Officer, Ordre Palmes Academìques

FGSAf, FAAS, MASSAf, FASI, FASSAf, FTAAS, FGIGE, FTWAS,

HonRFCAGS, HonFGSA, HonFGS, CGeol, EurGeol

For additional information: www.musomavijijini.or.tz

Date: Monday, 10 November 2025

CLICK TO OPEN THE CV

 

MSIKILIZE PROF. SOSPETER MWIJARUBI MUHONGO

MADIWANI TUINGIE KAZINI: FURSA ZA KI-UCHUMI NA AJIRA MUSOMA VIJIJINI

Waheshimiwa Madiwani:

1. Kila Diwani atayarishe Kikao kinachojumuisha Wananchi wanaohitaji MIKOPO midogo midogo na MIKOPO mikubwa yenye RIBA NAFUU kutoka Benki ya NMB
Mikopo ya:
Biashara, Kilimo, Uvuvi na Ufugaji

2. Diwani akitayarisha Kikao hicho ahakikishe Viongozi wahusika wa Halmashauri yetu wanakuwepo. Wasipokuwepo, Kikao kiendelee kwa manufaa ya wananchi

3. Tarehe za Kikao zipelekwe kwa Manager wa NMB Musoma ili yeye apange Timu yake ya kuelezea FURSA mbalimbali za ki-uchumi zilizopo kupitia Benki hiyo

Mawasiliano:
Manager,
NMB Musoma
Sospeter Pontain
Simu: 0782 442 243

Waheshimiwa Madiwani:
Hili suala la AJIRA ni letu sisi sote. Kila Diwani alitekeleze hili la Benki ya NMB kwa uharaka sana, ifikapo tarehe 1.12.2025 tuwe tunaanza kuona fursa mbalimbali za ki-uchumi zinawafikia Wananchi wa Jimboni mwetu.

Ninawasiliana na Benki nyingine kuhusu mikopo nafuu ya ki-uchumi kwa wananchi wa Musoma Vijijini

Tuingie kazini, tunafanikiwa!

Sospeter Muhongo
Dodoma

Sat, 8 Nov 2025

 

Matukio katika picha - (Toa Maoni Hapa)

Habari Mpya Toka Jimboni

TAARIFA MPYA JUU YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO JIMBONI MWETU --MPYA--

(1) BARABARA
1a. Musoma-Makojo-Busekera
*TANROADS wako kwenye utaratibu wa manunuzi kwa ajili ya uwekaji lami kwenye barabara hili ambalo Serikali imeamua kulijenga kwa awali mbili.

*Nimewasisitizia (Mbunge wa Jimbo) kwamba ujenzi unaotafutiwa Mkandarasi uwe wa kuendeleza ujenzi wa Lot 2 (Kusenyi-Makojo-Busekera) ambapo kilomita 5 za lami zilijengwa kwa miaka minne (4)!

1b. Utengenezaji wa barabara la Musoma-Mugango-Makojo-Busekera
*TANROADS Mkoa wameanza matengenezo ya uboreshaji wa barabara hili kwa kipande cha Musoma-Mugango

(2) KILIMO CHA UMWAGILIAJI
2a. BONDE LA BUGWEMA
*"Consultant" ameanza kufanya "feasibility study" (tarehe 17.9.2023 - 16.10.2023). Nimempa taarifa kwamba nitawatembelea wakiwa kazini Bugwema.

*Mazao makuu yatakayoliwa kwa umwagiliaji ni: mahindi, mpunga, alizeti, dengu, pamba na mboga mboga

2b. BONDE LA SUGUTI
*"Consultant" atafanya "feasibility study" baada ya kukamilisha kazi kwenye Bonde la Bugwema

3. ELIMU
3a. ELIMU YA SEKONDARI - MAABARA
*Tunaendelea na ujenzi wa maabara 3 (Physics, Chemistry & Biology) kwa kila Sekondari. Tuendelee kuchangia ujenzi huu na tunashukuru kila mara Serikali inapotuunga mkono kwa michango yake mikubwa

*Halmashauri yetu (Musoma DC) iendelee kukumbushwa kuchangia ujenzi wa maabara 3 kwenye kila Sekondari yetu ya Kata (kwa saa tunazo 25 na tunajenga mpya 5. Sekondari za Binafsi ni 2)

3b. SCIENCE HIGH SCHOOLS
*Tunaendelea kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu muhimu inayotakiwa kwenye uanzishwaji wa science high schools.

*Vinavyohitajika kwa uanzishwaji wa "science high school" ni: maji ya bomba, umeme, maabara 3, bweni, na bwalo la chakula.

*Lengo letu ni mwakani, 2024, Jimbo letu liwe na angalau HIGH SCHOOLS 2-3 za masomo ya sayansi. Ile ya Kasoma ni ya masomo ya "arts."

3c. ELIMU YA MSINGI - MRADI WA BOOST
*Shule za Msingi tisa (9) zimepewa jumla Tsh bilioni 1.35 kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya elimu kwenye shule hizo.

*Wananchi, Mbunge wa Jimbo na Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya waendelee kufuatilia mradi huu kwa ukaribu sana.

*Shule za Msingi zilizopewa fedha ni: Bugoji, Buira, Bulinga B, Kanyega, Kataryo B, Kigera B, Mabuimerafuru B, Masinono na Nyambono B

4. MAJI YA BOMBA KUTOKA ZIWA VICTORIA
4a. Maji ya MUWASA kupelekwa kwenye Kata za Etaro, Nyegina, Nyakatende na Ifulifu

*MUWASA inaendelea kukusanya baadhi ya vifaa hitajika kwa kutumia vyanzo vyake vya fedha.

*Vilevile, MUWASA imewasilisha Serikalini Bajeti ya kutekeleza mradi huu

*MUWASA imeishaanza kusambaza maji ya bomba kwa baadhi ya maeneo ya kata hizi

*Kijiji cha Nyasaungu cha Kata ya Ifulifu kimeanza kupata maji ya bomba kutoka kwenye bomba la zamani la Mugango-Kiabakari-Butiama

4b. Bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama
*Ujenzi umekamilika kwa asilimia 92 (92%) na ifikapo Disemba 2023 kazi zote muhimu zitakuwa zimekamilishwa

4c. MIUNDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI NDANI YA KATA YA TEGERUKA
*Maji ya bomba kwenye Kata hii yatatoka kwenye Bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama

*Mabomba yametandazwa ndani ya vijiji vyote vitatu vya Kata hii, ambavyo ni Kataryo, Mayani na Tegeruka

*Tenki la ujazo wa LITA 135,000 tayari linakamilishwa ujenzi kijijini Mayani

4d. MIUNDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI NDANI YA KATA YA MUGANGO
*Kata hii nayo itapata maji ya bomba kutoka kwenye Bomba la Mugango- Kiabakari-Butiama

*Mabomba yamesambazwa kwenye vijiji vyote vitatu vya Kata hii, ambavyo ni Kwibara, Kurwaki na Nyang'oma.

*Tenki la ujazo wa LITA 500,000
limejengwa kwenye Mlima Kong'u kijijini Nyang'oma

4e. MINDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI KWENYE KATA ZA BUSAMBARA NA KIRIBA
*Maji ya bomba ya Kata hizi mbili yatatoka kwenye Tenki ya LITA 500,000 liliojengwa Mlimani Kong'u. Maji yake yatatoka kwenye Bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama

*RUWASA imepata vibali vyote hitajika kutoka Serikalini, na ndani ya miezi miwili miundombinu ya usambazaji maji ya bomba ndani ya Kata hizi itaanza kujengwa.

4f. MINDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI KWENYE KATA YA BWASI
*Vijiji vyote vitatu vya Kiti hii, yaani Bwasi, Bugunda na Kome vinatandaziwa mabomba ya maji

*Ujenzi wa Tenki la ujazo wa LITA 150,000 tayari limekamilishwa Kijijini Bwasi

4g. MINDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI YA BOMBA KWENYE VIJIJI VYA CHUMWI & MABUIMERAFURU
*Ujenzi wa Tenki la ujazo wa LITA 300,OOO umekamilika kijijini Mabuimerafuru

*Mabomba yanaelendelea kutandazwa

*Maji kutoka kwenye Tenki hili yatasambazwa kwenye vijiji vya Masinono na Bugwema (Kata jirani ya Bugwema)

4h: MAJI YA KISIMA CHA RUSOLI SEKONDARI
*Tunaendelea kuwashukuru baadhi ya WAZALIWA wa RUSOLI kwa ufadhili wa uchimbaji wa kisima hiki.

*RUWASA imekamilisha ujenzi wa Tenki la LITA 75,000 kwa ajili ya usambazaji wa maji kijijini hapo.

5. AFYA
5a. HOSPITALI ya Halmashauri yetu yenye hadhi ya Hospital ya Wilaya imeanza kutoa HUDUMA za AFYA hapo ilipojengwa kwenye Kitongoji cha Kwikonero, Kijijini Suguti.

*Hospitali hii inavyo vifaa tiba vya kisasa sana, ikiwemo Digital X-ray, Ultrasound, Vifaa vya Upasauji, Mitambo ya kutengeneza Oxygen.

5b. VITUO VYA AFYA
*Kwa sasa tuna jumla ya Vituo vya Afya sita (6) ambavyo ni: (i) Murangi, (ii) Makojo (mpya), (iii) Kiriba (mpya), (iv) Kisiwa cha Rukuba (Zahanati yake imepanuliwa), (v) Mugango (Zahanati yake imepanuliwa), na (vi) Bugwema (ilikuwa Zahanati ya Masinono, imepanuliwa)

5c. ZAHANATI
*Tuna jumla ya Zahanati 42
*Zahanati 24 zinatoa Huduma za Afya vijijini mwetu
*Zahanati 14 zinaendelea kujengwa na baadhi karibu zitakamilishwa ujenzi.
*Zahanati 4 za Binafsi zinatoa Huduma za Afya vijijini mwetu.

5d. MAGARI YA WAGONJWA (AMBULANCES)
*Tunayo magari ya kusafirishia wagonjwa (ambulances) matano (5). Mbunge wa Jimbo ndiye aliyefanikisha upatikaji wa ambulances hizi.

*Ambulance iliyoko Kituo cha Afya cha Murangi ni ya kisasa ambayo upasuaji unaweza kufanyika wakati mgonjwa akiwa anasafirishwa. Serikali ya Japan ilimpatia Mbunge wa Jimbo ambulance hii.

*Ambulance nyingine nne (4) zilinunuliwa na Mbunge wa Jimbo akishirikiana na rafiki zake.

*Tunaendelea kufuatilia miradi ya usambazaji UMEME vijijini mwetu (REA & TANESCO). Miradi ya REA itaanza hivi karibuni

*Tunaendelea kufuatilia miradi ya ujenzi na uboreshaji wa barabara zetu vijijini (TARURA & TANROADS)

*Tunaendelea kufuatilia uboreshaji wa miundombinu ya usambazaji maji ya bomba vijijini mwetu (RUWASA & MUWASA)

Usisahau kutembelea TOVUTI ya Jimbo letu ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz

SHUKRANI
Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na WADAU wengine wa uchangiaji wa Maendeleo na Ustawi wa Jimbo letu wanapewa shukrani nyingi sana - tafadhali endeleeni kutuunga mkono.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatano, 20.9.2023

TAARIFA ZA MIRADI MBALIMBALI YA MUSOMA VIJIJINI

1. Barabara ya Musoma-Makojo-Busekera (km 92)

*Ujenzi wa kilomita 5 (Kusenyi hadi Suguti, Kwikonero) umekamilika wiki jana

*Ujenzi wa kilomita 87 zilizosalia:

Ombi liko ndani ya Wizara la kushawishi Mradi huu wa KM 87 uwekwe wote kwenye Bajeti ya Mwaka unaoanza tarehe 1.7.2023, yaani, Mwaka wa Fedha 2023/2024

2. Maombi ya Mikopo ya UVUVI

*Tulituma jumla ya maombi 10 yakiwa ya: (i) boti za uvuvi na (ii) vizimba vya uvuvi.

*Taarifa niliyopewa (Mbunge) ni kwamba sehemu kubwa ya maombi yetu imekubalika.

*Wapo watakaopata mikopo ya boti yenye thamani ya kati ya Tsh Milioni 16 na 72

*Wapo watakaokopeshwa vizimba 8 vyenye thamani ya Tsh Milioni 130

*Orodha na maelekezo ya upokeaji wa mikopo hiyo utatolewa hivi karibuni na Wizara husika.

3. Ujenzi wa VETA Musoma Vijijini

*Serikali imeamua kujenga VETA moja kwa kila Wilaya

*Sisi Wilaya yetu inayo VETA hapo Mwisenge, Musoma Mjini. Hii ilikuwa VETA ya Mkoa wa Mara, sasa inakuwa VETA ya Wilaya ya Musoma.

*Wizara imeshawishiwa na kuona umuhimu wa Musoma Vijijini kupata VETA yake.

Tumeombwa tukabidhi VETA MAKAO MAKUU eneo lililoainishwa kwa ajili ya ujenzi wa VETA tunayoiomba.

Mbali ya ufinyu wa Bajeti, Wizara itajitahidi kutafuta fedha za ujenzi wa VETA ya Musoma Vijijini. Halmashauri itekeleze hili!

4. Minara mipya ya Mawasiliano

Ombi letu linafanyiwa kazi, pamoja na maombi mengine ya nchini kote. Tutajulishwa.

5. Ujenzi wa Sekondari ya Kisiwa cha Rukuba

*Taarifa ya uamuzi wa Wakazi wa Rukuba kuwa na Sekondari yao hapo Kisiwani imefikishwa kwa Wahusika TAMISEMI, na hakuna kuzuizi cho chote kilichopo.

*Wakazi wa Kisiwa cha Rukuba waanze matayarisho ya mradi huu. Mbunge wa Jimbo ataenda huko kupiga Harambee ya ujenzi wa Rukuba Sekondari.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Alhamisi, 9.2.2023

Kalamu ya Mh. Mbunge, Prof. Sospeter Muhongo

UJENZI WA SEKONDARI MPYA ZA MUSOMA VIJIJINI UNAENDELEA

Michango ya Mbunge wetu Prof Sospeter Muhongo kwenye ujenzi wa sekondari mpya za Jimboni mwetu inaendelea kutolewa.

Masharti ya michango ya Mbunge:
1. Ujenzi uwe unafanyika kwa kuwashirikisha wanakijiji
2. Ujenzi ufanyike bila ubaguzi wa aina yo yote ile
3. Kamati ya Ujenzi iliyoteuliwa na wanakijiji isimamie ujenzi wa shule yao
4. Taratibu nyingine zote zikiwemo za matumizi ya fedha ni zile zitolewazo na Halmashauri yetu

Mchango wa Mbunge wa Jimbo wa SARUJI ya ujenzi

Siku: Jumanne, 11 Nov 2025

1. Kanderema Sekondari
Kijiji cha Kanderema, Kata ya Bugoji

Diwani: CUF
Mwenyekiti S/Kijiji: CCM
Saruji: Mifuko 50

2. Sekondari ya Kisiwani Rukuba (Rukuba Island Sec School)
Kisiwa/Kijiji cha Rukuba, Kata ya Etaro

Diwani: CCM
Mwenyekiti S/Kijiji: CCM
Saruji: Mifuko 50

3. Nyambono Sekondari
Kijiji cha Nyambono, Kata ya Nyambono

Diwani: CCM
Mwenyekiti S/Kijiji: CCM
Saruji: Mifuko 50

4. Mmahare Sekondari
Kijiji cha Mmahare, Kata ya Etaro

Diwani: CCM
Mwenyekiti S/Kijiji: CCM
Saruji: Mifuko 50

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatatu, 10 Nov 2025

KAMPENI ZA MUSOMA VIJIJINI: KIJIJI KWA KIJIJI

Prof Muhongo tayari amepiga kampeni ndani ya Vijiji 40 kati ya 68 vya Jimbo la Musoma Vijijini.

Kijiji kwa kijiji maana yake:
Utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya kila kijiji kwa miaka mitano iliyopita na ile mitano ijayo (Ilani za Uchaguzi za CCM za 2020-2025 & 2025-2030), na Dira ya Maendeleo ya Taifa (2025-2030)

Leo, Prof Muhongo alikuwa ndani ya Kata ya Nyegina akipiga kampeni kwenye vijiji viwili (Nyegina & Mkirira)....Angalia na sikiliza viambatanisho vya hapa!

Timu ya Kampeni
Jimbo la Musoma Vijijini
Wed, 24 Sept 2025

KAMPENI ZA CCM ZA KIJIJI KWA KIJIJI: KILA KIJIJI KINATOA HAMASA YA AINA YAKE

Jana, Prof Sospeter Muhongo alipiga Kampeni kwenye vijiji viwili (Chimati & Chitare) vya Kata ya Makojo.

Vijiji hivi tayari vimefikishiwa umeme na maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria. Usambazaji unaendelea kwenye ngazi ya vitongoji.

Kwa maendeleo yaliyokwishapatikana, vijiji hivi vimeamua kutoa kura nyingi sana kwa wagombea wote wa CCM, wakiongozwa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Hamasa: tafadhali sikiliza muziki (Video/Clip iliyoambatanishwa hapa) utokao kwenye gita za zamani za Wanamuziki wa Kijijini Chimati.

Kamati ya Uchaguzi
Jimbo la Musoma Vijijini

Wed, 17 Sept 2025

KIJIJI KWA KIJIJINI - KAMPENI ZA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Idadi ya Vijiji vya Jimbo: 68

Hamasa za kampeni:
Ngoma za Asili, Kwaya, Mashahiri, n.k.

Tafadhali Msikilize HAPA Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kome, Kata ya Bwasi, Ndugu Abel Bogohe akitoa hamasa za uchaguzi (shahiri) kwenye kampeni za jana kijijini mwake.

Timu ya Kampeni
Jimbo la Musoma Vijijini

Mon, 15 Sept 2025

Vipaumbele vya Mh. Mbunge

  • Elimu

    Kila mtoto aliyefikia umri wa kwenda shule, awe shuleni na kuinua kiwango cha ufaulu

  • Afya
    Kusogeza huduma bora za afya zinazokidhi uhitaji kwa wananchi
  • Kilimo
    Kilimo cha kisasa, endelevu na chenye uzalishaji mkubwa kwa eneo
  • Maji
    Gharama nafuu katika upatikanaji wa maji safi na salama kwa kila kaya