Kijiji cha Muhoji kimeamua kujenga sekondari yake ili kutatua tatizo la umbali mrefu wanaotembea watoto wa kijiji hicho kwenda masomoni kwenye Sekondari ya Kata iliyoko Kijijini Masinono - umbali wa zaidi ya kilomita kumi (10)
Ujenzi ulianza kwa kupitia Harambee za Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, ambae anachangia fedha zake binafsi.
Mfuko wa Jimbo unachangia baadhi ya vifaa vya ujenzi.
Wanakijiji wanachangia fedha za ujenzi na nguvukazi zao.
Orodha ya michango inayotolewa na majina ya wachangiaji wote inatunzwa kwenye Ofisi ya Kijiji cha Muhoji
Serikali yetu imeanza kuchangia ujenzi wa sekondari hii kwa kutoa Tsh milioni 75 (Tsh 75m) - tunashukuru sana!
Muhoji Sekondari iko tayari, mwezi huu (Januari 2025) kuanza kupokea wanafunzi wa Kidato cha Kwanza kutoka kijijini humo.
Sekondari hii mpya, kwa miaka ya karibuni, itapokea wanafunzi kutoka vijiji jirani vya Kaburabura (Kata ya Bugoji), Saragana (Kata ya Nyambono) na hata wanafunzi kutoka Wilaya ya Bunda, Kitongoji jirani sana cha Kinyambwiga!
Majengo yaliyokamilishwa:
(i) Vyumba vya madarasa vitatu (3)
(ii) Ofisi moja (1)
(iii) Vyoo: matundu 8 wasichana, na 6 wavulana
(iv) Chumba cha Maktaba
(v) Chumba cha Huduma ya Kwanza (matibabu)
Michango bado inahitajika:
Ujenzi wa miundombinu ya elimu kwenye sekondari hii mpya unaendelea, k.m. maabara tatu za masomo ya sayasi, vyumba vipya vya madarasa, na nyumba za walimu.
Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha:
+Majengo ya sekondari mpya ya Kijijini Muhoji (Muhoji Secondary School)
+Wanakijiji wakisafisha eneo la sekondari yao mpya
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Jumapili, 5 Jan 2025