MATOKEO YA HARAMBEE YA MBUNGE WA JIMBO YA UJENZI WA NYABAKANGARA SEKONDARI YA KIJIJI CHA NYAMBONO

Tarehe ya Harambee:
Jumanne, 25.3.2025

Mahali:
Kitongoji cha Kamatondo, Kijijini Nyambono, Kata ya Nyambono

Washiriki wa Harambee:
*Wanakijiji
*Wazaliwa wa Kijiji cha Nyambono
*Viongozi mbalimbali wa CCM na Jumuiya zake
*Wadau wa Maendeleo wa Kijiji cha Nyambono
*Mbunge wa Jimbo, kiongozi wa Harambee

Matokeo ya Harambee:

(i) Saruji Mifuko 204
Tripu 5 za mawe
Fedha: Tsh 448,000
*Michango kutoka kwa Wanakijiji, Wazaliwa wa Kijiji cha Nyambono na Wadau wa Maendeleo

(ii) Saruji Mifuko 250
*Mchango kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini

Mchango wa awali:
Mfuko wa Jimbo: Saruji Mifuko 150
*Matofali 3,700 yameishafyatuliwa

Kamati ya Ujenzi:
Iliundwa jana kwa kila Kitongoji kutoa mjumbe mmoja. Kamati ina wajumbe saba (7)

Uamuzi wa Wanakijiji:
Ujenzi uanze mara moja. Halmashauri yetu iharakishe upatikanaji wa ramani za ujenzi

Leo, Mbunge wa Jimbo anapiga Harambee ya ujenzi wa Kataryo Sekondari ya Kijiji cha Kataryo, Kata ya Tegeruka

Kata ya Nyambono yenye vijiji viwili inaanza kujenga sekondari ya pili ya Kata hii.

Kata ya Tegeruka yenye vijiji vitatu inaanza kujenga sekondari ya pili ya Kata hii.

KARIBUNI TUCHANGIE UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO YA MUSOMA VIJIJINI - UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM

Picha ni kutoka kwenye Harambee ya jana ya Kijijini Nyambono, Kata ya Nyambono

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumatano, 26 Machi 2025