"Tovuti Rasmi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo, Kwaajili ya Kuwasiliana na Wananchi Jimboni "
A CONCISE PROFESSIONAL CV OF PROF. SOSPETER MWIJARUBI MUHONGO
(1) Fellowships in the topmost Science Societies/Academies of the World
*Honorary Fellow of the Geological Society of London, (est. 1807), HonFGS
*Honorary Fellow of the Geological Society of America (est. 1888), HonFGSA
*Honorary Research Fellow of the Chinese Academy of Geological Sciences (est. 1956), HonRFCAGS
*Fellow of The World Academy of Sciences, FTWAS
*Fellow of the African Academy of Sciences, FAAS
*Fellow and Life Member of the Geological Society of Africa, FGSAf
*Member of the Academy of Science of South Africa, MASSAf
(2) World's Top Science Leadership
*Former Vice President of the Commission of the Geological Map of the World (CGMW)
*Former Chair of the Science Programme Committee of the UN-proclaimed International Year of Planet Earth (UN-IYPE)
*Former Chair of UNESCO-IUGS-IGCP Scientific Board of the International Geoscience Programme
*Former President of the Geological Society of Africa (GSAf)
*Former Regional Director (Africa) for the International Council of Scientific Unions (ICSU-ROA)
(3) Preparation & Publication of Geological Maps
*Co-Author of Geology & Mineral Maps of Africa, East Africa, and Tanzania
*Co-Supervision for the publications of the geological maps of the world
(4) Publication of Science Books
*Senior Author of a Book (2009) on Science, Technology and Innovation for Socio-Economic Development: Success Stories from Africa
(5) Publication of Science Policy Booklets
*Cordinator for the preparation and publication of 4 Science Plans for sub-Saharan Africa (2007, ICSU ROA). They are on:
+Sustainable Energy
+Health and Human Well-being
+Global Environmental Change
+Natural and Human-induced Hazards and
Disasters
(6) Science Journal Publications
*More than 200 publications in international learned journals of high to moderate Impact Factors (IFs)
*Editor-in-Chief Emeritus of the Journal of African Earth Sciences (JAES), published by Elsevier, Amsterdam
*Editorial Board Member of the Precambrian Research Journal, published by Elsevier, Amsterdam
(7) Keynote Speaker
*Invited Keynote Speaker to over 500 national and international conferences
(8) Convener of Conferences for high-level science experts
*Co-Organizer/Convener of over 100 Science Experts' Conferences around the World
(9) Major International & National Awards
Many scholarly, professional, and research awards and scholarships, including:
*Officier, The Ordre des Palmes académiques. An academic decoration introduced by Emperor Napoleon in 1808
*The Prof Robert Shackleton Award for Outstanding Research on the Precambrian Geology of Africa
*The Nigerian Mining and Geosciences Society (NMGS)/AMNI Petroleum Award of Prof.M.O. Oyawaye
*The National Award for Research in Science and Technology (NARST), Tanzania.
*The Best First Year Student in the Faculty of Science of the University of Dar es Salaam (1976/1977)
*The 1971 Best Debating Student at Mara Secondary School, Musoma, Tanzania. He was in Form III.
(10) University Education
*Dr.rer.nat. graduate of the Technical University of Berlin (TU-Berlin), Germany
*MSc Research Student of the University of Góttingen, Germany
*MSc, BSc (Hons) (Geology) graduate of the University of Dar es Salaam, Tanzania
Prof Sospeter Mwijarubi Muhongo is a very distinguished world-class scholar, a Chartered and a European geologist. He is a retired Full Professor of Geology. He writes and speaks fluent Kiswahili, English, and German languages. His French is basic.
Prof Dr.rer.nat. Sospeter M Muhongo
Officer, Ordre Palmes Academìques
(FGSAf, FAAS, MASSAf, FASI, FASSAf, FTAAS, FGIGE, FTWAS, HonRFCAGS, HonFGSA, HonFGS, CGeol, EurGeol)
Homepage:
www.musomavijijini.or.tz
Telephone:
+255 754 400 800
Date:
Tuesday, 14.11.2022
Matukio katika picha - (Toa Maoni Hapa)
Habari Mpya Toka Jimboni
TAARIFA MPYA JUU YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO JIMBONI MWETU --MPYA--
(1) BARABARA
1a. Musoma-Makojo-Busekera
*TANROADS wako kwenye utaratibu wa manunuzi kwa ajili ya uwekaji lami kwenye barabara hili ambalo Serikali imeamua kulijenga kwa awali mbili.
*Nimewasisitizia (Mbunge wa Jimbo) kwamba ujenzi unaotafutiwa Mkandarasi uwe wa kuendeleza ujenzi wa Lot 2 (Kusenyi-Makojo-Busekera) ambapo kilomita 5 za lami zilijengwa kwa miaka minne (4)!
1b. Utengenezaji wa barabara la Musoma-Mugango-Makojo-Busekera
*TANROADS Mkoa wameanza matengenezo ya uboreshaji wa barabara hili kwa kipande cha Musoma-Mugango
(2) KILIMO CHA UMWAGILIAJI
2a. BONDE LA BUGWEMA
*"Consultant" ameanza kufanya "feasibility study" (tarehe 17.9.2023 - 16.10.2023). Nimempa taarifa kwamba nitawatembelea wakiwa kazini Bugwema.
*Mazao makuu yatakayoliwa kwa umwagiliaji ni: mahindi, mpunga, alizeti, dengu, pamba na mboga mboga
2b. BONDE LA SUGUTI
*"Consultant" atafanya "feasibility study" baada ya kukamilisha kazi kwenye Bonde la Bugwema
3. ELIMU
3a. ELIMU YA SEKONDARI - MAABARA
*Tunaendelea na ujenzi wa maabara 3 (Physics, Chemistry & Biology) kwa kila Sekondari. Tuendelee kuchangia ujenzi huu na tunashukuru kila mara Serikali inapotuunga mkono kwa michango yake mikubwa
*Halmashauri yetu (Musoma DC) iendelee kukumbushwa kuchangia ujenzi wa maabara 3 kwenye kila Sekondari yetu ya Kata (kwa saa tunazo 25 na tunajenga mpya 5. Sekondari za Binafsi ni 2)
3b. SCIENCE HIGH SCHOOLS
*Tunaendelea kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu muhimu inayotakiwa kwenye uanzishwaji wa science high schools.
*Vinavyohitajika kwa uanzishwaji wa "science high school" ni: maji ya bomba, umeme, maabara 3, bweni, na bwalo la chakula.
*Lengo letu ni mwakani, 2024, Jimbo letu liwe na angalau HIGH SCHOOLS 2-3 za masomo ya sayansi. Ile ya Kasoma ni ya masomo ya "arts."
3c. ELIMU YA MSINGI - MRADI WA BOOST
*Shule za Msingi tisa (9) zimepewa jumla Tsh bilioni 1.35 kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya elimu kwenye shule hizo.
*Wananchi, Mbunge wa Jimbo na Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya waendelee kufuatilia mradi huu kwa ukaribu sana.
*Shule za Msingi zilizopewa fedha ni: Bugoji, Buira, Bulinga B, Kanyega, Kataryo B, Kigera B, Mabuimerafuru B, Masinono na Nyambono B
4. MAJI YA BOMBA KUTOKA ZIWA VICTORIA
4a. Maji ya MUWASA kupelekwa kwenye Kata za Etaro, Nyegina, Nyakatende na Ifulifu
*MUWASA inaendelea kukusanya baadhi ya vifaa hitajika kwa kutumia vyanzo vyake vya fedha.
*Vilevile, MUWASA imewasilisha Serikalini Bajeti ya kutekeleza mradi huu
*MUWASA imeishaanza kusambaza maji ya bomba kwa baadhi ya maeneo ya kata hizi
*Kijiji cha Nyasaungu cha Kata ya Ifulifu kimeanza kupata maji ya bomba kutoka kwenye bomba la zamani la Mugango-Kiabakari-Butiama
4b. Bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama
*Ujenzi umekamilika kwa asilimia 92 (92%) na ifikapo Disemba 2023 kazi zote muhimu zitakuwa zimekamilishwa
4c. MIUNDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI NDANI YA KATA YA TEGERUKA
*Maji ya bomba kwenye Kata hii yatatoka kwenye Bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama
*Mabomba yametandazwa ndani ya vijiji vyote vitatu vya Kata hii, ambavyo ni Kataryo, Mayani na Tegeruka
*Tenki la ujazo wa LITA 135,000 tayari linakamilishwa ujenzi kijijini Mayani
4d. MIUNDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI NDANI YA KATA YA MUGANGO
*Kata hii nayo itapata maji ya bomba kutoka kwenye Bomba la Mugango- Kiabakari-Butiama
*Mabomba yamesambazwa kwenye vijiji vyote vitatu vya Kata hii, ambavyo ni Kwibara, Kurwaki na Nyang'oma.
*Tenki la ujazo wa LITA 500,000
limejengwa kwenye Mlima Kong'u kijijini Nyang'oma
4e. MINDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI KWENYE KATA ZA BUSAMBARA NA KIRIBA
*Maji ya bomba ya Kata hizi mbili yatatoka kwenye Tenki ya LITA 500,000 liliojengwa Mlimani Kong'u. Maji yake yatatoka kwenye Bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama
*RUWASA imepata vibali vyote hitajika kutoka Serikalini, na ndani ya miezi miwili miundombinu ya usambazaji maji ya bomba ndani ya Kata hizi itaanza kujengwa.
4f. MINDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI KWENYE KATA YA BWASI
*Vijiji vyote vitatu vya Kiti hii, yaani Bwasi, Bugunda na Kome vinatandaziwa mabomba ya maji
*Ujenzi wa Tenki la ujazo wa LITA 150,000 tayari limekamilishwa Kijijini Bwasi
4g. MINDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI YA BOMBA KWENYE VIJIJI VYA CHUMWI & MABUIMERAFURU
*Ujenzi wa Tenki la ujazo wa LITA 300,OOO umekamilika kijijini Mabuimerafuru
*Mabomba yanaelendelea kutandazwa
*Maji kutoka kwenye Tenki hili yatasambazwa kwenye vijiji vya Masinono na Bugwema (Kata jirani ya Bugwema)
4h: MAJI YA KISIMA CHA RUSOLI SEKONDARI
*Tunaendelea kuwashukuru baadhi ya WAZALIWA wa RUSOLI kwa ufadhili wa uchimbaji wa kisima hiki.
*RUWASA imekamilisha ujenzi wa Tenki la LITA 75,000 kwa ajili ya usambazaji wa maji kijijini hapo.
5. AFYA
5a. HOSPITALI ya Halmashauri yetu yenye hadhi ya Hospital ya Wilaya imeanza kutoa HUDUMA za AFYA hapo ilipojengwa kwenye Kitongoji cha Kwikonero, Kijijini Suguti.
*Hospitali hii inavyo vifaa tiba vya kisasa sana, ikiwemo Digital X-ray, Ultrasound, Vifaa vya Upasauji, Mitambo ya kutengeneza Oxygen.
5b. VITUO VYA AFYA
*Kwa sasa tuna jumla ya Vituo vya Afya sita (6) ambavyo ni: (i) Murangi, (ii) Makojo (mpya), (iii) Kiriba (mpya), (iv) Kisiwa cha Rukuba (Zahanati yake imepanuliwa), (v) Mugango (Zahanati yake imepanuliwa), na (vi) Bugwema (ilikuwa Zahanati ya Masinono, imepanuliwa)
5c. ZAHANATI
*Tuna jumla ya Zahanati 42
*Zahanati 24 zinatoa Huduma za Afya vijijini mwetu
*Zahanati 14 zinaendelea kujengwa na baadhi karibu zitakamilishwa ujenzi.
*Zahanati 4 za Binafsi zinatoa Huduma za Afya vijijini mwetu.
5d. MAGARI YA WAGONJWA (AMBULANCES)
*Tunayo magari ya kusafirishia wagonjwa (ambulances) matano (5). Mbunge wa Jimbo ndiye aliyefanikisha upatikaji wa ambulances hizi.
*Ambulance iliyoko Kituo cha Afya cha Murangi ni ya kisasa ambayo upasuaji unaweza kufanyika wakati mgonjwa akiwa anasafirishwa. Serikali ya Japan ilimpatia Mbunge wa Jimbo ambulance hii.
*Ambulance nyingine nne (4) zilinunuliwa na Mbunge wa Jimbo akishirikiana na rafiki zake.
*Tunaendelea kufuatilia miradi ya usambazaji UMEME vijijini mwetu (REA & TANESCO). Miradi ya REA itaanza hivi karibuni
*Tunaendelea kufuatilia miradi ya ujenzi na uboreshaji wa barabara zetu vijijini (TARURA & TANROADS)
*Tunaendelea kufuatilia uboreshaji wa miundombinu ya usambazaji maji ya bomba vijijini mwetu (RUWASA & MUWASA)
Usisahau kutembelea TOVUTI ya Jimbo letu ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz
SHUKRANI
Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na WADAU wengine wa uchangiaji wa Maendeleo na Ustawi wa Jimbo letu wanapewa shukrani nyingi sana - tafadhali endeleeni kutuunga mkono.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Jumatano, 20.9.2023
TAARIFA ZA MIRADI MBALIMBALI YA MUSOMA VIJIJINI
1. Barabara ya Musoma-Makojo-Busekera (km 92)
*Ujenzi wa kilomita 5 (Kusenyi hadi Suguti, Kwikonero) umekamilika wiki jana
*Ujenzi wa kilomita 87 zilizosalia:
Ombi liko ndani ya Wizara la kushawishi Mradi huu wa KM 87 uwekwe wote kwenye Bajeti ya Mwaka unaoanza tarehe 1.7.2023, yaani, Mwaka wa Fedha 2023/2024
2. Maombi ya Mikopo ya UVUVI
*Tulituma jumla ya maombi 10 yakiwa ya: (i) boti za uvuvi na (ii) vizimba vya uvuvi.
*Taarifa niliyopewa (Mbunge) ni kwamba sehemu kubwa ya maombi yetu imekubalika.
*Wapo watakaopata mikopo ya boti yenye thamani ya kati ya Tsh Milioni 16 na 72
*Wapo watakaokopeshwa vizimba 8 vyenye thamani ya Tsh Milioni 130
*Orodha na maelekezo ya upokeaji wa mikopo hiyo utatolewa hivi karibuni na Wizara husika.
3. Ujenzi wa VETA Musoma Vijijini
*Serikali imeamua kujenga VETA moja kwa kila Wilaya
*Sisi Wilaya yetu inayo VETA hapo Mwisenge, Musoma Mjini. Hii ilikuwa VETA ya Mkoa wa Mara, sasa inakuwa VETA ya Wilaya ya Musoma.
*Wizara imeshawishiwa na kuona umuhimu wa Musoma Vijijini kupata VETA yake.
Tumeombwa tukabidhi VETA MAKAO MAKUU eneo lililoainishwa kwa ajili ya ujenzi wa VETA tunayoiomba.
Mbali ya ufinyu wa Bajeti, Wizara itajitahidi kutafuta fedha za ujenzi wa VETA ya Musoma Vijijini. Halmashauri itekeleze hili!
4. Minara mipya ya Mawasiliano
Ombi letu linafanyiwa kazi, pamoja na maombi mengine ya nchini kote. Tutajulishwa.
5. Ujenzi wa Sekondari ya Kisiwa cha Rukuba
*Taarifa ya uamuzi wa Wakazi wa Rukuba kuwa na Sekondari yao hapo Kisiwani imefikishwa kwa Wahusika TAMISEMI, na hakuna kuzuizi cho chote kilichopo.
*Wakazi wa Kisiwa cha Rukuba waanze matayarisho ya mradi huu. Mbunge wa Jimbo ataenda huko kupiga Harambee ya ujenzi wa Rukuba Sekondari.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Alhamisi, 9.2.2023
Kalamu ya Mh. Mbunge, Prof. Sospeter Muhongo
KAMPENI ZA CCM KWENYE VISIWA VIKUU VYA MUSOMA VIJIJINI
Jana, Mbunge Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Mwijarubi Muhongo, alizunguka na boti kwenye Visiwa vya Rukuba, Iriga na Kagongo kuwaombea kura wagombea wa CCM.
Mbunge huyo na Timu yake ya kampeni walikumbwa na mvua na upepo mkali wakati walipokuwa Ziwani (Ziwa Victoria)
Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO kutoka Visiwani Musoma Vijijini - imeambatanishwa hapa.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Jumatatu, 25 Nov 2024
UVCCM YATEMBEA KWA MIGUU IKIFUATA NYAYO ZA BABA WA TAIFA KUTOKA BUTIAMA HADI MWANZA
Vijana 2,100 wakiwemo 32 wa kutoka Musoma Vijijini, walianza matembezi ya miguu kutokea Butiama hadi Mwanza siku ya Jumatano, 9.10.2024.
Matembezi haya yanafuata nyayo za matembezi ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyoyafanya Mwaka 1967 akiunga mkono Azimio la Arusha lililozaliwa mwaka huo (1967)
Vilevile, matembezi haya ni sehemu ya sherehe za kilele cha ukimbizaji Mwenge wa Uhuru zitakazohitimishwa Jijini Mwanza tarehe 14.10.2024
CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa inaelezea baadhi ya matukio ya tarehe 9.10.2024 ya Kijijini Butiama - tafadhali isikilize.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Jumamosi, 12.10.2024
RAIS SAMIA AONDOA GIZA JIMBO LA PROF. MUHONGO
Na Shomari Binda-Musoma
MKUU wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuling'arisha jimbo la Musoma vijijini kwa mwanga wa taa za barabarani.
Shukrani hizo amezitoa jana septemba 25 mara baada ya kukitembelea usiku Kijiji cha Suguti kilichopo kwenye jimbo hilo.
MAOMBI YALIYOKO TEMESA: VIVUKO VYA MUSOMA VIJIJINI
Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini kupitia kwa Mbunge wao wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo, wameiomba TEMESA yafuatayo:
1. Kivuko cha Kurugee-Iramba
Kivuko hiki kinaunganisha Wilaya mbili, yaani Wilaya ya Musoma (Kurugee, Kijiji cha Buraga) na Wilaya ya Bunda (Iramba)
Maombi:
1a. Ijengwe Gati mpya isiyoathirika na ujazo mkubwa wa maji ndani ya Ziwa Victoria.
1b. Jumba la Wasafiri (Abiria) lenye viti na vyoo
2. Kivuko kipya cha Kisiwa cha Rukuba-Musoma Manispaa
TEMESA inaangalia njia ya kutumiwa na Kivuko hiki.
TEMESA iangalie uwezekana wa Kivuko hiki kuunganisha Wilaya ya Musoma (Kisiwa cha Rukuba) na Wilaya ya Rorya (Kibui)
3. Kivuko kipya cha Bukima-Kisiwa cha Irugwa
Kivuko hiki kikipatikana kitaunganisha Wilaya ya Musoma (Bukima) na Wilaya ya Ukerewe (Kisiwa cha Irugwa).
Wakazi wa Kisiwa cha Irugwa wanapata mahitaji yao mengi Kijijini Bukima.
Tunaendelea kufuatilia maombi yetu ofisini TEMESA.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O .Box 6
Musoma
Tarehe:
Alhamisi, 26.9.2024
MATAIFA MAKUBWA YANAPUNGUKIWA WAFANYAKAZI KWENYE MAENEO MUHIMU YA DUNIA YA LEO
Tuendelee kuwekeza kwenye ELIMU itakayotuwezesha kushindania AJIRA za nje ya nchi.
Taarifa ya hapa ni ya kutoka Uingereza. Hali ni hiyo hiyo kwa Ujerumani, Japan, Ufaransa, n.k....tafadhali soma hapo chini.
Sospeter Muhongo
25.9.2024
Top 9 in-demand skills in the UK as govt opens doors to foreign workers https://www.vanguardngr.com/2024/09/top-9-in-demand-skills-in-the-uk-as-govt-opens-doors-to-foreign-workers/
SHUKRANI NYINGI MNO KWA SERIKALI YETU - Barabara ya Musoma-Makojo-Busekera kuendelea kujengwa
Barabara kuu na pekee inayounganisha Vijiji vyetu vyote 68 (ndani ya Kata 21) ni hii ya Musoma-Makojo-Busekera yenye urefu wa kilomita 92.
Barabara hili ni muhimu sana kwa ukuaji na uimarijaki wa uchumi wetu na wa Taifa letu. Vilevile, barabara hili ni muhimu sana kwa usambazaji, utoaji na uimarishaji wa huduma za jamii.
Tenda ya tarehe 18.9.2024:
Tunaishukuru sana Serikali yetu kutangaza TENDA ya ujenzi wa KILOMITA 40 za barabara hili (soma kiambatanisho)
Ujenzi wa awali: 5 km
Ujenzi wa awali wa kilomita tano (5) za barabara hili ulifanyika kuanzia Kijijini Kusenyi hadi Kijijini Suguti (Lot II)
SHUKRANI:
Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wanamshukuru sana Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kupokea na kushughulikia ombi la ujenzi wa barabara hili.
Ombi hilo liliwasilishwa kwa Mhe Rais wetu na Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo. Hiyo ilikuwa tarehe 6.2.2022, Kijijini Kwibara, Kata ya Mugango.
KIAMBATANISHO
Tenda ya tarehe 18.9.2024 ya TANROADS
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Jumamosi, 21.9.2024
UJENZI WA SEKONDARI MPYA 12: FAMILIA MOJA YAJITOLEA KUCHANGIA TSH MILIONI 30
Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kushirikiana vizuri sana na Serikali yetu kwenye miradi ya ujenzi wa sekondari mpya Jimboni mwetu.
Familia ya Mashenene (na rafiki zao) ya Kijiji cha Kiriba tayari imejitayarisha kuchangia takribani Tsh Milioni 30 kwenye ujenzi wa sekondari mpya itakayojengwa kijijini kwao - hongereni sana!
(a) Idadi ya Sekondari Jimboni mwetu:
(i) Sekondari za Kata/Serikali: 26
(ii) Sekondari za Madhehebu ya Dini: 2
(b) Sekondari mpya 3
Hizi zinazojengwa kwa mchango mkubwa wa Serikali, na Wanavijiji wanachangia nguvukazi
Sekondari hizi zinajengwa Vijijini Butata (Kata ya Bukima), Kasoma (Nyamrandirira) na Kurwaki (Mugango)
(c) Sekondari mpya 3
Hizi zinazojengwa kwa michango ya Wanavijiji, Viongozi wao, na baadhi ya Wazaliwa wa vijiji vyenye miradi ya ujenzi
Vijijini Nyasaungu (Kata ya Ifulifu), Muhoji (Bugwema) na Kisiwani Rukuba (Etaro)
+Serikali imeanza kuchangia ujenzi wa Muhoji Sekondari
+Sekondari hizi zitafunguliwa Januari 2025
(d) Sekondari mpya 6
Hizi zinaanza kujengwa mwaka huu na Wanavijiji wenyewe wakishirikisha Viongozi wao, na baadhi ya Wazaliwa wa vijijini mwao:
Vijijini Buraga (Kata ya Bukumi), Chitare (Makojo), Kataryo (Tegeruka), Kiriba (Kiriba), Mmahare (Etaro) na Nyambono (Kata ya Nyambono)
+Familia Mashenene na rafiki zao wamejitayarisha kuchangia takribani Tsh Milioni 30 kwenye ujenzi wa sekondari mpya ya kijijini mwao.
+Matayarisho wa ujenzi wa sekondari hizi mpya yanaendelea. Mbunge wa Jimbo ameishapiga Harambee za awali kwa baadhi ya sekondari hizi.
WITO:
Wadau wa Maendeleo wa Jimbo la Musoma Vijijini, wakiwemo Wazaliwa wa Jimbo hili, wanaombwa kuchangia ujenzi wa sekondari mpya kwenye Kata zetu.
Malengo makuu ya ujenzi wa sekondari mpya ndani ya Kata zetu 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374 ni:
(i) kutatua tatizo la umbali mrefu unaotembewa na wanafunzi kwenda masomoni
(ii) kutatua tatizo la mirundikano ya wanafunzi kwenye vyumba vya madarasa.
Ongezeko la wanafunzi mashuleni, kwa kila mwaka, ni kubwa!
(iii) miaka michache ijayo elimu ya chini kabisa kwa vijana wetu nchini itakuwa Kidato cha Nne (Form IV). Kwa hiyo, sekondari mpya zinahitajika.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
Tarehe:
Jumapili, 15.9.2024