Mgeni Rasmi:
Ndugu Gerald Musabila Kusaya
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara

Mahali:
Kijijini Kwibara, Kata ya Mugango

Leo, Alhamisi, 19.12.2024 Benki ya CRDB imefungua Tawi lake Kijijini Kwibara, Kata ya Mugango.

Mgeni Rasmi alikuwa Ndugu Gerald Musabila Kusaya, Afisa Tawala wa Mkoa wa Mara, na mwenyeji wake alikuwa Ndugu Boma Raballa, Afisa Mkuu Biashara wa Benki ya CRDB.

Wananchi kutoka baadhi ya vijiji vya Jimbo la Musoma Vijijini walihudhuria sherehe za ufunguzi wa Tawi hilo

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, na Mkurugenzi Mtendaji (DED) wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC), Ndugu Nitu Msongela Palela, nao walihudhurulia hafla hiyo muhimu sana kwa uchumi na utunzaji wa fedha wa wananchi wa Jimboni mwetu.

Tawi la CRDB Mugango limeanza shughuli zake kwa mafanikio makubwa - wateja zaidi ya elfu moja (1,000) wameishapatikana ndani ya miezi mitano, wengi wao wakiwa wavuvi, wakulima, wafugaji wa wafanya biashara ndogo ndogo.

Benki ya CRDB ina Mawakala 35 kwenye vijiji mbalimbali ndani ya Jimbo letu

Tawi hilo la CRDB tayari limeanza kutoa huduma zote za ki-benki ikiwemo ya ukopeshaji wa mitaji ya kibiashara kwa wavuvi, wakulima na wafugaji wa Jimboni mwetu.

Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha:Sherehe za uzinduzi rasmi wa Tawi la CRDB Mugango ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Alhamisi, 19 Dec 2024