Kipaumbele namba moja cha Jimbo la Musoma Vijijini kinatekelezwa kwa kasi ya kuridhisha.
Kipaumbele hicho ni: ELIMU
Jimbo lina Kata 21 zenye vijiji 68 na vitongoji 374. Tunazo Sekondari za Kata 26 na za Binafsi ni 2
Sekondari mpya zilizopagwa kufunguliwa mwakani (2025) ni:
(i) Sekondari zinazojengwa kwa michango ya fedha na nguvukazi kutoka kwa wanavijiji na viongozi wao:
(ia) Rukuba Island Secondary School
(ib) Nyasaungu Secondary School
(ic) Muhoji Secondary School - hii imepokea mchango wa Tsh milioni 75 kutoka Serikalini
(ii) Sekondari zinazojengwa kwa michango mikubwa ya fedha kutoka Serikalini, na kwa michango ya nguvukazi kutoka kwa wanavijiji:
(iia) Butata Secondary School
(iib) Nyamrandirira Technical Sec School
(iic) David Massamba Memorial Sec School
Kila sekondari imepokea Tsh milioni 584, kutoka Serikalini, za kuanza ujenzi wake.
Sekondari mpya zilizopata vibali vya kuanza kujengwa:
Vijiji sita (6) vimekubaliwa kuanza kujenga sekondari mpya. Vijiji hivyo ni: Chitare, Kataryo, Kiriba, Mmahare, Musanja na Nyambono
Miradi ya ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi kwa kila sekondari ya Kata:
Miradi hii inaendelea kutekelezwa kwa kutumia michango ya fedha kutoka vyanzo mbalimbali. Taarifa itatolewa kwa kila sekondari.
Uanzishwaji wa "high schools" za masomo ya sayansi Jimboni mwetu:
Mwakani (2025), "high schools" mbili za masomo ya sayansi zitaanzishwa - Suguti & Mugango
WITO:
Wana-Musoma Vijijini, rafiki zetu, na Wadau wa Maendeleo, tuendelee kuchangia miradi iliyoainishwa hapo juu.
Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha:
Prof Sospeter Muhongo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini akikagua majengo ya sekondari mpya itakayofunguliwa Januari 2025. Hiyo ni Muhoji Sekondari ya Kijijini Muhoji, Kata ya Bugwema. Ukaguzi huo ulifanyika siku ya Jumatatu, tarehe 23 Dec 2024
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Alhamisi, 26 Dec 2024