
MAABARA ZA MTIRO SEKONDARI: HARAMBEE YA KUPAUA MABOMA YALIYOKAMILISHWA
Harambee:
Jumanne, 22 April 2025
Gharama za upauaji:
Tsh milioni 25 (Tsh 25m)
Mtiro Sekondari ni Kata ya Bukumi
Vijiji: Buira, Bukumi, Buraga na Busekera
Sekondari hii iliyofunguliwa Mwaka 2006 haina maabara hata moja!
Mtiro Sekondari inakamilisha ujenzi wa maabara 3 za masomo ya sayansi (physics, chemistry & biology laboratories)
Harambee ya kupata vifaa vya ujenzi:
Malengo makuu:
(i) kukamilisha ujenzi wa maabara 3 za masomo ya sayansi (Tsh 25m za kupaua)
(ii) Wanafunzi 672 (Forms I to IV) kusoma masomo ya sayansi kwa vitendo kwenye mazingira sitahiki
(iii) kuanzisha "High School" ya masomo ya sayansi kwani bweni, maji na umeme vipo
Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha:
Maboma ya Maabara 3 (fizikia, kemia & baiolojia) za Mtiro Sekondari ya Kata ya Bukumi, Musoma Vijijini.
Harambee ya Mbunge ya kuezeka maboma hayo itapigwa shuleni hapo siku ya Jumanne, 22.4.2025, saa 8 mchana.
WOTE MNAKARIBISHWA KUCHANGIA UJENZI WA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI ZA MTIRO SEKONDARI
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Alhamisi, 10 April 2025