
MUSOMA VIJIJINI YAENDELEA NA UJENZI WA "HIGH SCHOOLS" ZA MASOMO YA SAYANSI
Mahitaji makubwa ya sasa ya Dunia ni kuongeza wataalamu kwenye nyanja za sayansi, teknolojia na ubunifu (science, technology and innovation, STI).
Msingi mkuu wa wataalamu wa aina hiyo ni masomo ya sayansi kuanzia shule za awali hadi kidato cha sita.
Jimbo la Musoma Vijijini linatekeleza miradi ifuatayo, ikiwa ni sehemu ya kupata wana-sayansi wengi:
(i) kila sekondari iliyoko Jimboni mwetu kuwa na maabara tatu za masomo ya fizikia, kemia na baiolojia (sekondari zote za Kata & Binafsi)
(ii) kuongeza idadi ya "high schools" za masomo ya sayansi Jimboni mwetu
Idadi ya "high schools" Jimboni mwetu:
1. Kasoma High School
Kata ya Nyamrandirira
Combinations: HKL, HGL & HGK
2. Suguti High School
Kata ya Suguti
Itafunguliwa Julai 2025
Combinations: PCM, PCB & CBG
3. Mugango High School
Kata ya Mugango
Itafunguliwa Julai 2025
Combinations: CBG & EGM
Tunashauri: PCM & PCB ziongezwe
Matayarisho ya "high schools" nyingine:
4. Mtiro High School
Kata ya Bukumi
*Vilivyopo: bweni, umeme & maji ya bomba
*Tunakamilisha: maabara 3 za masomo ya sayansi
5. Makojo High School
Kata ya Makojo
*Vilivyopo: maabara mbili, maji ya bomba & umeme
*Tunakamilisha: maabara moja iliyosalia
*Tunajenga: bweni, Tsh 130m (EP4R)
6. Bugwema High School
Kata ya Bugwema
*Vilivyopo: maabara tatu, umeme
*Tunasubiri: maji ya bomba, mradi upo
*Tutajenga: Bweni
7. Kiriba High School
Kata ya Kiriba
*Vilivyopo: maabara tatu, umeme
*Tunakamilisha: bweni
*Tunasubiri: maji ya bomba, mradi upo
8. Nyakatende High School
Kata ya Nyakatende
*Vilivyopo: maabara tatu, umeme & vyumba ziada vya madarasa
*Tutajenga: bweni
*Tunasubiri: maji ya bomba, mradi upo
9. Etaro High School
Kata ya Etaro
*Vilivyopo: maabara mbili, chumba chenye kompyuta 25 & umeme
*Tunakamilisha: maabara moja iliyosalia
*Tutajenga: bweni
*Tunasubiri: maji ya bomba, mradi upo
Wachangiaji wa ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi kwenye sekondari za Jimboni mwetu:
(i) Serikali Kuu
(ii) Halmashauri yetu
(iii) Wanavijiji & Viongozi wao
(iv) Mbunge wa Jimbo
(v) Mfuko wa Jimbo
(vi) Wamiliki wa sekondari za binafsi
Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha:
Mfano wa Maabara za masomo ya sayansi zinazojengwa kwenye sekondari za Jimboni mwetu. Hiyo ni Maabara ya Kemia ya Kigera Sekondari, Kata ya Nyakatende
KARIBUNI TUCHANGIE UJENZI WA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI KWENYE SEKONDARI ZA JIMBONI MWETU
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Jumanne, 8 April 2025