JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Prof. Sospeter Muhongo

Mh. Mbunge, Prof. Sospeter Muhongo (CV1)AND (CV2)

"Tovuti Rasmi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo, Kwaajili ya Kuwasiliana na Wananchi Jimboni "

MBUNGE WETU MH. PROF. SOSPETER MUHONGO ANATUHAMASISHA KUTEMBELEA WEBSITE HII KILA MARA, KWA MAENDELEO YETU SOTE.

A CONCISE PROFESSIONAL CV OF PROF. SOSPETER MWIJARUBI MUHONGO

(1) Fellowships in the topmost Science Societies/Academies of the World

*Honorary Fellow of the Geological Society of London, (est. 1807), HonFGS

*Honorary Fellow of the Geological Society of America (est. 1888), HonFGSA

*Honorary Research Fellow of the Chinese Academy of Geological Sciences (est. 1956), HonRFCAGS

*Fellow of The World Academy of Sciences, FTWAS

*Fellow of the African Academy of Sciences, FAAS

*Fellow and Life Member of the Geological Society of Africa, FGSAf

*Member of the Academy of Science of South Africa, MASSAf

(2) World's Top Science Leadership

*Former Vice President of the Commission of the Geological Map of the World (CGMW)

*Former Chair of the Science Programme Committee of the UN-proclaimed International Year of Planet Earth (UN-IYPE)

*Former Chair of UNESCO-IUGS-IGCP Scientific Board of the International Geoscience Programme

*Former President of the Geological Society of Africa (GSAf)

*Former Regional Director (Africa) for the International Council of Scientific Unions (ICSU-ROA)

(3) Preparation & Publication of Geological Maps

*Co-Author of Geology & Mineral Maps of Africa, East Africa, and Tanzania

*Co-Supervision for the publications of the geological maps of the world

(4) Publication of Science Books

*Senior Author of a Book (2009) on Science, Technology and Innovation for Socio-Economic Development: Success Stories from Africa

(5) Publication of Science Policy Booklets

*Cordinator for the preparation and publication of 4 Science Plans for sub-Saharan Africa (2007, ICSU ROA). They are on:
+Sustainable Energy
+Health and Human Well-being
+Global Environmental Change
+Natural and Human-induced Hazards and
Disasters

(6) Science Journal Publications

*More than 200 publications in international learned journals of high to moderate Impact Factors (IFs)

*Editor-in-Chief Emeritus of the Journal of African Earth Sciences (JAES), published by Elsevier, Amsterdam

*Editorial Board Member of the Precambrian Research Journal, published by Elsevier, Amsterdam

(7) Keynote Speaker

*Invited Keynote Speaker to over 500 national and international conferences

(8) Convener of Conferences for high-level science experts

*Co-Organizer/Convener of over 100 Science Experts' Conferences around the World

(9) Major International & National Awards
Many scholarly, professional, and research awards and scholarships, including:

*Officier, The Ordre des Palmes académiques. An academic decoration introduced by Emperor Napoleon in 1808

*The Prof Robert Shackleton Award for Outstanding Research on the Precambrian Geology of Africa

*The Nigerian Mining and Geosciences Society (NMGS)/AMNI Petroleum Award of Prof.M.O. Oyawaye

*The National Award for Research in Science and Technology (NARST), Tanzania.

*The Best First Year Student in the Faculty of Science of the University of Dar es Salaam (1976/1977)

*The 1971 Best Debating Student at Mara Secondary School, Musoma, Tanzania. He was in Form III.

(10) University Education

*Dr.rer.nat. graduate of the Technical University of Berlin (TU-Berlin), Germany

*MSc Research Student of the University of Góttingen, Germany

*MSc, BSc (Hons) (Geology) graduate of the University of Dar es Salaam, Tanzania

Prof Sospeter Mwijarubi Muhongo is a very distinguished world-class scholar, a Chartered and a European geologist. He is a retired Full Professor of Geology. He writes and speaks fluent Kiswahili, English, and German languages. His French is basic.

Prof Dr.rer.nat. Sospeter M Muhongo
Officer, Ordre Palmes Academìques
(FGSAf, FAAS, MASSAf, FASI, FASSAf, FTAAS, FGIGE, FTWAS, HonRFCAGS, HonFGSA, HonFGS, CGeol, EurGeol)

Homepage:
www.musomavijijini.or.tz

Telephone:
+255 754 400 800

Date:
Tuesday, 14.11.2022

 

 

Matukio katika picha - (Toa Maoni Hapa)

Habari Mpya Toka Jimboni

TAARIFA MPYA JUU YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO JIMBONI MWETU --MPYA--

(1) BARABARA
1a. Musoma-Makojo-Busekera
*TANROADS wako kwenye utaratibu wa manunuzi kwa ajili ya uwekaji lami kwenye barabara hili ambalo Serikali imeamua kulijenga kwa awali mbili.

*Nimewasisitizia (Mbunge wa Jimbo) kwamba ujenzi unaotafutiwa Mkandarasi uwe wa kuendeleza ujenzi wa Lot 2 (Kusenyi-Makojo-Busekera) ambapo kilomita 5 za lami zilijengwa kwa miaka minne (4)!

1b. Utengenezaji wa barabara la Musoma-Mugango-Makojo-Busekera
*TANROADS Mkoa wameanza matengenezo ya uboreshaji wa barabara hili kwa kipande cha Musoma-Mugango

(2) KILIMO CHA UMWAGILIAJI
2a. BONDE LA BUGWEMA
*"Consultant" ameanza kufanya "feasibility study" (tarehe 17.9.2023 - 16.10.2023). Nimempa taarifa kwamba nitawatembelea wakiwa kazini Bugwema.

*Mazao makuu yatakayoliwa kwa umwagiliaji ni: mahindi, mpunga, alizeti, dengu, pamba na mboga mboga

2b. BONDE LA SUGUTI
*"Consultant" atafanya "feasibility study" baada ya kukamilisha kazi kwenye Bonde la Bugwema

3. ELIMU
3a. ELIMU YA SEKONDARI - MAABARA
*Tunaendelea na ujenzi wa maabara 3 (Physics, Chemistry & Biology) kwa kila Sekondari. Tuendelee kuchangia ujenzi huu na tunashukuru kila mara Serikali inapotuunga mkono kwa michango yake mikubwa

*Halmashauri yetu (Musoma DC) iendelee kukumbushwa kuchangia ujenzi wa maabara 3 kwenye kila Sekondari yetu ya Kata (kwa saa tunazo 25 na tunajenga mpya 5. Sekondari za Binafsi ni 2)

3b. SCIENCE HIGH SCHOOLS
*Tunaendelea kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu muhimu inayotakiwa kwenye uanzishwaji wa science high schools.

*Vinavyohitajika kwa uanzishwaji wa "science high school" ni: maji ya bomba, umeme, maabara 3, bweni, na bwalo la chakula.

*Lengo letu ni mwakani, 2024, Jimbo letu liwe na angalau HIGH SCHOOLS 2-3 za masomo ya sayansi. Ile ya Kasoma ni ya masomo ya "arts."

3c. ELIMU YA MSINGI - MRADI WA BOOST
*Shule za Msingi tisa (9) zimepewa jumla Tsh bilioni 1.35 kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya elimu kwenye shule hizo.

*Wananchi, Mbunge wa Jimbo na Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya waendelee kufuatilia mradi huu kwa ukaribu sana.

*Shule za Msingi zilizopewa fedha ni: Bugoji, Buira, Bulinga B, Kanyega, Kataryo B, Kigera B, Mabuimerafuru B, Masinono na Nyambono B

4. MAJI YA BOMBA KUTOKA ZIWA VICTORIA
4a. Maji ya MUWASA kupelekwa kwenye Kata za Etaro, Nyegina, Nyakatende na Ifulifu

*MUWASA inaendelea kukusanya baadhi ya vifaa hitajika kwa kutumia vyanzo vyake vya fedha.

*Vilevile, MUWASA imewasilisha Serikalini Bajeti ya kutekeleza mradi huu

*MUWASA imeishaanza kusambaza maji ya bomba kwa baadhi ya maeneo ya kata hizi

*Kijiji cha Nyasaungu cha Kata ya Ifulifu kimeanza kupata maji ya bomba kutoka kwenye bomba la zamani la Mugango-Kiabakari-Butiama

4b. Bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama
*Ujenzi umekamilika kwa asilimia 92 (92%) na ifikapo Disemba 2023 kazi zote muhimu zitakuwa zimekamilishwa

4c. MIUNDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI NDANI YA KATA YA TEGERUKA
*Maji ya bomba kwenye Kata hii yatatoka kwenye Bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama

*Mabomba yametandazwa ndani ya vijiji vyote vitatu vya Kata hii, ambavyo ni Kataryo, Mayani na Tegeruka

*Tenki la ujazo wa LITA 135,000 tayari linakamilishwa ujenzi kijijini Mayani

4d. MIUNDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI NDANI YA KATA YA MUGANGO
*Kata hii nayo itapata maji ya bomba kutoka kwenye Bomba la Mugango- Kiabakari-Butiama

*Mabomba yamesambazwa kwenye vijiji vyote vitatu vya Kata hii, ambavyo ni Kwibara, Kurwaki na Nyang'oma.

*Tenki la ujazo wa LITA 500,000
limejengwa kwenye Mlima Kong'u kijijini Nyang'oma

4e. MINDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI KWENYE KATA ZA BUSAMBARA NA KIRIBA
*Maji ya bomba ya Kata hizi mbili yatatoka kwenye Tenki ya LITA 500,000 liliojengwa Mlimani Kong'u. Maji yake yatatoka kwenye Bomba la Mugango-Kiabakari-Butiama

*RUWASA imepata vibali vyote hitajika kutoka Serikalini, na ndani ya miezi miwili miundombinu ya usambazaji maji ya bomba ndani ya Kata hizi itaanza kujengwa.

4f. MINDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI KWENYE KATA YA BWASI
*Vijiji vyote vitatu vya Kiti hii, yaani Bwasi, Bugunda na Kome vinatandaziwa mabomba ya maji

*Ujenzi wa Tenki la ujazo wa LITA 150,000 tayari limekamilishwa Kijijini Bwasi

4g. MINDOMBINU YA USAMBAZAJI MAJI YA BOMBA KWENYE VIJIJI VYA CHUMWI & MABUIMERAFURU
*Ujenzi wa Tenki la ujazo wa LITA 300,OOO umekamilika kijijini Mabuimerafuru

*Mabomba yanaelendelea kutandazwa

*Maji kutoka kwenye Tenki hili yatasambazwa kwenye vijiji vya Masinono na Bugwema (Kata jirani ya Bugwema)

4h: MAJI YA KISIMA CHA RUSOLI SEKONDARI
*Tunaendelea kuwashukuru baadhi ya WAZALIWA wa RUSOLI kwa ufadhili wa uchimbaji wa kisima hiki.

*RUWASA imekamilisha ujenzi wa Tenki la LITA 75,000 kwa ajili ya usambazaji wa maji kijijini hapo.

5. AFYA
5a. HOSPITALI ya Halmashauri yetu yenye hadhi ya Hospital ya Wilaya imeanza kutoa HUDUMA za AFYA hapo ilipojengwa kwenye Kitongoji cha Kwikonero, Kijijini Suguti.

*Hospitali hii inavyo vifaa tiba vya kisasa sana, ikiwemo Digital X-ray, Ultrasound, Vifaa vya Upasauji, Mitambo ya kutengeneza Oxygen.

5b. VITUO VYA AFYA
*Kwa sasa tuna jumla ya Vituo vya Afya sita (6) ambavyo ni: (i) Murangi, (ii) Makojo (mpya), (iii) Kiriba (mpya), (iv) Kisiwa cha Rukuba (Zahanati yake imepanuliwa), (v) Mugango (Zahanati yake imepanuliwa), na (vi) Bugwema (ilikuwa Zahanati ya Masinono, imepanuliwa)

5c. ZAHANATI
*Tuna jumla ya Zahanati 42
*Zahanati 24 zinatoa Huduma za Afya vijijini mwetu
*Zahanati 14 zinaendelea kujengwa na baadhi karibu zitakamilishwa ujenzi.
*Zahanati 4 za Binafsi zinatoa Huduma za Afya vijijini mwetu.

5d. MAGARI YA WAGONJWA (AMBULANCES)
*Tunayo magari ya kusafirishia wagonjwa (ambulances) matano (5). Mbunge wa Jimbo ndiye aliyefanikisha upatikaji wa ambulances hizi.

*Ambulance iliyoko Kituo cha Afya cha Murangi ni ya kisasa ambayo upasuaji unaweza kufanyika wakati mgonjwa akiwa anasafirishwa. Serikali ya Japan ilimpatia Mbunge wa Jimbo ambulance hii.

*Ambulance nyingine nne (4) zilinunuliwa na Mbunge wa Jimbo akishirikiana na rafiki zake.

*Tunaendelea kufuatilia miradi ya usambazaji UMEME vijijini mwetu (REA & TANESCO). Miradi ya REA itaanza hivi karibuni

*Tunaendelea kufuatilia miradi ya ujenzi na uboreshaji wa barabara zetu vijijini (TARURA & TANROADS)

*Tunaendelea kufuatilia uboreshaji wa miundombinu ya usambazaji maji ya bomba vijijini mwetu (RUWASA & MUWASA)

Usisahau kutembelea TOVUTI ya Jimbo letu ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz

SHUKRANI
Serikali yetu chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na WADAU wengine wa uchangiaji wa Maendeleo na Ustawi wa Jimbo letu wanapewa shukrani nyingi sana - tafadhali endeleeni kutuunga mkono.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumatano, 20.9.2023

TAARIFA ZA MIRADI MBALIMBALI YA MUSOMA VIJIJINI

1. Barabara ya Musoma-Makojo-Busekera (km 92)

*Ujenzi wa kilomita 5 (Kusenyi hadi Suguti, Kwikonero) umekamilika wiki jana

*Ujenzi wa kilomita 87 zilizosalia:

Ombi liko ndani ya Wizara la kushawishi Mradi huu wa KM 87 uwekwe wote kwenye Bajeti ya Mwaka unaoanza tarehe 1.7.2023, yaani, Mwaka wa Fedha 2023/2024

2. Maombi ya Mikopo ya UVUVI

*Tulituma jumla ya maombi 10 yakiwa ya: (i) boti za uvuvi na (ii) vizimba vya uvuvi.

*Taarifa niliyopewa (Mbunge) ni kwamba sehemu kubwa ya maombi yetu imekubalika.

*Wapo watakaopata mikopo ya boti yenye thamani ya kati ya Tsh Milioni 16 na 72

*Wapo watakaokopeshwa vizimba 8 vyenye thamani ya Tsh Milioni 130

*Orodha na maelekezo ya upokeaji wa mikopo hiyo utatolewa hivi karibuni na Wizara husika.

3. Ujenzi wa VETA Musoma Vijijini

*Serikali imeamua kujenga VETA moja kwa kila Wilaya

*Sisi Wilaya yetu inayo VETA hapo Mwisenge, Musoma Mjini. Hii ilikuwa VETA ya Mkoa wa Mara, sasa inakuwa VETA ya Wilaya ya Musoma.

*Wizara imeshawishiwa na kuona umuhimu wa Musoma Vijijini kupata VETA yake.

Tumeombwa tukabidhi VETA MAKAO MAKUU eneo lililoainishwa kwa ajili ya ujenzi wa VETA tunayoiomba.

Mbali ya ufinyu wa Bajeti, Wizara itajitahidi kutafuta fedha za ujenzi wa VETA ya Musoma Vijijini. Halmashauri itekeleze hili!

4. Minara mipya ya Mawasiliano

Ombi letu linafanyiwa kazi, pamoja na maombi mengine ya nchini kote. Tutajulishwa.

5. Ujenzi wa Sekondari ya Kisiwa cha Rukuba

*Taarifa ya uamuzi wa Wakazi wa Rukuba kuwa na Sekondari yao hapo Kisiwani imefikishwa kwa Wahusika TAMISEMI, na hakuna kuzuizi cho chote kilichopo.

*Wakazi wa Kisiwa cha Rukuba waanze matayarisho ya mradi huu. Mbunge wa Jimbo ataenda huko kupiga Harambee ya ujenzi wa Rukuba Sekondari.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Alhamisi, 9.2.2023

Kalamu ya Mh. Mbunge, Prof. Sospeter Muhongo

KITUO CHA AFYA CHA KISIWA CHA RUKUBA CHAPATA FEDHA ZA KUFUNGIWA UMEMEJUA (SOLAR)

Taarifa kutoka REA:

Tsh 345,600,000 (Tsh 345.6m) zimetolewa na EU (Nchi za Umoja wa Ulaya) kufadhili mradi wa ufungaji wa solar (umemejua) kwenye Kituo cha Afya cha Kisiwa cha Rukuba.

Mkataba wa mradi huo umesainiwa tayari kwa utekelezaji

Shukrani nyingi sana kwa EU, Serikali yetu na REA kwa hatua kubwa iliyofikiwa ya kuhakikisha Kituo cha Afya cha Kisiwa cha Rukuba kinapata umeme wa uhakika kwa shughuli za matibabu Kisiwani humo.

Maeneo mengine ya Kisiwa cha Rukuba nayo yatafungiwa solar (umemejua). Mradi wake unatayarishwa.

Sospeter Muhongo (Mb)
Dodoma

Tarehe, 22.8.2024

MAELEZO YA ZIADA KUHUSU MIRADI YA MAJI YA BOMBA NDANI YA KATA YA NYAMRANDIRIRA

Jana nilipokuwa (Mbunge wa Jimbo) kwenye mkutano wa hadhara Kijijini Kasoma maswali kuhusu usambazaji wa maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria yalihitaji ufafanuzi zaidi kutoka RUWASA.

Maelezo ya Meneja wa RUWASA (W) kuhusu maji kwenye Kata hii ni haya hapa:

Kata ya Nyamrandirira ina vijijiji vitano (5), na vijiji vyote vinayo miradi ya maji ya bomba.

1. Kijiji cha Mikuyu
Maji ya bomba yameishafikishwa Kijijini hapo kutoka kwenye Tenki la Mlimani Nyabherango. Chanzo cha maji kiko Kijijini Suguti (ziwani)

RUWASA inaendelea na maboresho na upanuzi wa mradi huu

2. Kijiji cha Chumwi
Maji yameishafika Kijijini Chumwi, na maji yanatoka kwenye Tenki lililojengwa Kijijini Mabuimerafuru. Chanzo chake kiko Kijijini Chumwi (ziwani)

3. Kijiji cha Kasoma na Kitongoji chake cha Rwanga
Maji ya hapa yatatoka kwenye Tenki linalojengwa Mlimani Kwikonero. Chanzo chake kiko Kijijini Suguti (ziwani).

Utekelezaji wa huu mradi wa thamani ya Tsh Milioni 500 unakaribia sana kukamilika

4. Kijiji cha Kaboni & (5) Kijiji cha Seka
Maji ya bomba ya vijiji hivi viwili yatatolewa kwenye Tenki la ujazo wa Lita 150,000 linalojengwa Mlimani Seka

Chanzo cha maji kiko Kijijini Chumwi (ziwani)

Gharama ya mradi ni Tsh Milioni 800.

Maendeleo ya utekelezaji wa mradi ni mazuri.

Kwa hiyo, vijiji vyote vitano (5) vya Kata ya Nyamrandirira vina miradi ya maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria. Baadhi ya miradi hiyo imekamilika na mingine inaendelea kuboreshwa na kukamilishwa.

Taarifa kutoka:
Ofisi ya RUWASA (W)

Taarifa imepokelewa na:
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini

Tarehe:
Jumatano, 21.8.2024

USAMBAZAJI WA UMEMEJUA (SOLAR ENERGY) KISIWANI RUKUBA

Kisiwa cha Rukuba kinayo miradi mwili (2) ya umemejua. Matayarisho yanafanywa na REA:

(i) Umemejua kwenye Kituo cha Afya:
REA imeishampata Mkandarasi. Taratibu za kisheria zinakamilishwa.

(ii) Umemejua kwenye maeneo mengine ya Kisiwani
REA ina mradi kabambe wa kusambaza umemejua kwenye visiwa vyote vya Ziwa Victoria na Bahari ya Indi. Wakandarasi wanatafutwa

(iii) Pampu ya maji ya kutumia umemejua
RUWASA inasubiri upatikanaji wa umemejua ili ianze kutekeleza mradi wa usambazaji wa maji ya bomba hapo kisiwani.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumamosi, 10.8.2024

MIKUTANO YA HADHARA NA HARAMBEE ZA UJENZI WA SEKONDARI MPYA MUSOMA VIJIJINI

Wito:
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, ameombwa na wananchi wa baadhi za kata aungane nao kwenye ujenzi wa sekondari ya pili na ya tatu ya kata zao - Mbunge amekubali.

Takwimu:
Jumla ya Sekondari Jimboni mwetu:
(i) Sekondari 26 za Kata/Serikali
(ii) Sekondari 2 za Madhehebu ya Dini

(iii) Sekondari mpya 3 zinazojengwa kwa nguvu za wanavijiji na viongozi wao: Kisiwani Rukuba (Kata ya Etaro, sekondari ya pili), Kijijini Nyasaungu (Kata ya Ifulifu, sekondari ya pili) na Kijijini Muhoji (Kata ya Bugwema, sekondari ya pili - Serikali imeanza kuchangia).

Sekondari hizi 3 zitafunguliwa Januari 2025

(iv) Sekondari mpya 3 zinajengwa kwa kutumia fedha nyingi za Serikali: Kijijini Butata (Kata ya Bukima, sekondari ya pili), Kijijini Kasoma (Kata ya Nyamrandirira, sekondari ya tatu) na Kijijini Kurwaki (Kata ya Mugango, sekondari ya pili)

Sekondari hizi 3 zitafunguliwa Januari 2025

Jimbo letu lina Kata 21 zenye Vijiji 68 (jumla ya Vitongoji ni 374)

Ratiba ya Mikutano ya Hadhara na Harambee za ujenzi wa sekondari mpya:

Jumanne, 13.8.2024
Saa 4 Asubuhi: Kijijini Kataryo, Kata ya Tegeruka (sekondari ya pili)

Saa 9 Alasiri: Kijijini Mmahare, Kata ya Etaro (sekondari ya tatu)

Jumatano, 14.8.2024
Saa 4 Asubuhi: Kijijini Chitare, Kata ya Makojo (sekondari ya pili)

Saa 9 Alasiri: Kijijini Kiriba, Kata ya Kiriba (sekondari ya tatu)

Alhamisi, 15.8.2024
Saa 4 Asubuhi: kazi maalumu

Saa 9 Alasiri: Kijijini Nyambono, Kata ya Nyambono (sekondari ya pili)

Ratiba ya Vijiji vya Butata (Kata ya Bukima), Kasoma (Kata ya Nyamrandirira) na Kurwaki (Kata ya Mugango) itatolewa baadae.

KARIBUNI TUCHANGIE UJENZI NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU JIMBONI MWETU

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Ijumaa, 9.8.2024

MWENGE WA UHURU MUSOMA VIJIJINI: MIRADI YA THAMANI YA TSH 3.5 BILIONI YAKAGULIWA NA KUKUBALIKA

Mwenge wa Uhuru ulipokelewa kwa shangwe nyingi mno kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC) yenye Jimbo la Musoma Vijijini. Hiyo ilikuwa juzi, Jumatano, 31.7.2024

Miradi yote 7 ilikaguliwa na kukubalika. Miradi hiyo ni ya ujenzi wa shule (miradi 2), zahanati, na barabara. Mingine ni ya usambazaji wa maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria (miradi 2) na kikundi cha vijana (uchumi).

Wananchi wa Musoma Vijijini walitoa shukrani nyingi za dhati kwa Serikali yetu inayoongozwa vizuri na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Tafadhali sikiliza VIDEO/CLIP iliyoambatanishwa hapa.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Ijumaa, 2.8.2024

ELIMU YA SEKONDARI NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Ukubwa wa Jimbo letu:
Kata 21 zenye vijiji 68 na vitongoji 374

Idadi ya sekondari Jimboni mwetu:

+26 za Kata zinatoa elimu
+2 za Binafsi zinatoa elimu
+3 mpya zinajengwa kwa fedha za Serikali Kuu. Wanavijiji kuchangia nguvukazi
+3 mpya zinajengwa kwa michango ya wanavijiji na viongozi wao
+6 ujenzi kuanza Julai/Agosti 2024 kwa kutumia michango ya wanavijiji na viongozi wao

(a) Uanzishwaji wa miradi ya ujenzi wa sekondari mpya Jimboni mwetu

Malengo:
+kutatua matatizo ya umbali mrefu wa kwenda masomoni
+kutatua matatizo ya mirundikano madarasani
+kujitayarisha vizuri kwenye mfumo mpya wa elimu - wanafunzi wote watakaomaliza elimu ya msingi kwenda wote sekondari

Wanavijiji wanamuomba Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini washirikiane nae kuanza miradi yao ya ujenzi wa sekondari mpya.

Mbunge wa Jimbo amekubali. Miradi hiyo ni hii ifuatayo:

1. Kijiji cha Chitare:
Ujenzi wa sekondari mpya. Hii itakuwa sekondari ya pili ya Kata ya Makojo yenye vijiji vitatu

2. Kijiji cha Buanga:
Ujenzi wa sekondari mpya. Hii itakuwa sekondari ya pili ya Kata ya Rusoli yenye vijiji vitatu

3. Kijiji cha Nyambono:
Ujenzi wa sekondari mpya. Hii itakuwa sekondari ya pili ya Kata ya Nyambono yenye vijiji viwili

4. Kijiji cha Kataryo:
Ujenzi wa sekondari mpya. Hii itakuwa sekondari ya pili ya Kata ya Tegeruka yenye vijiji vitatu

5. Kijiji cha Kiriba:
Ujenzi wa sekondari mpya. Hii itakuwa sekondari ya tatu ya Kata ya Kiriba yenye vijiji vitatu

6. Kijiji cha Mmahare:
Ujenzi wa sekondari mpya. Hii itakuwa sekondari ya tatu ya Kata ya Etaro yenye vijiji vinne

SEKONDARI MPYA 6

(b) Sekondari zitakazojengwa kwa kutumia fedha kutoka Serikali Kuu.

Wanavijiji wanashawishiwa wachangie nguvukazi ili tupate miundombinu mingi ya elimu kutoka kwenye fedha hizo za Serikali Kuu

7. Kata ya Bukima:
Kijijini Butata. Hii itakuwa sekondari ya pili ya Kata ya Bukima yenye vijiji vitatu.

8. Kijiji cha Kasoma:
Kijijini Kasoma. Hii ni sekondari ya kwanza ya amali (technical?) ndani ya Jimbo letu. Itakuwa sekondari ya nne ya Kata ya Nyamrandirira yenye vijiji vitano.

Kasoma Sekondari yenye High School iko ndani ya Kijiji cha Kaboni.

9. Kijiji cha Kurwaki:
Kijijini Kurwaki. Ujenzi wa David Massamba Memorial Secondary School. Sekondari ya kumuenzi Hayati Prof Massamba.

Hii itakuwa sekondari ya pili ya Kata ya Mugango yenye vijiji vitatu.

SEKONDARI MPYA 3: zitafunguliwa Januari 2025

(c) Ukamilishaji wa sekondari zilizoanzwa kujengwa kwa michango ya wanavijiji na viongozi wao

10. Kijiji cha Muhoji
Hii itakuwa sekondari ya pili ya Kata ya Bugwema yenye vijiji vinne. Michango ya ujenzi inatoka kwa wanakijiji na viongozi wao.

+Serikali imechangia Tsh 75m
+Mzaliwa wa Muhoji, Mhe Maboto amejenga na kukamilisha darasa moja

11. Kijiji cha Nyasaungu
Sekondari mpya ambayo michango ya ujenzi inatolewa na wanakijiji na viongozi wao. Hii ni sekondari ya pili ya Kata ya Ifulifu yenye vijiji vitatu.

12. Kisiwa cha Rukuba
Ujenzi wa sekondari hii unachangiwa na wana-Rukuba, na viongozi wao. Hii itakuwa sekondari ya tatu ya Kata ya Etaro yenye vijiji vinne.

Kisiwa cha Rukuba ni kijiji kinachojitegemea.

SEKONDARI MPYA 3: zitafunguliwa Januari 2025

(d) Ujenzi na ukamilishaji wa maabara 3 za masomo ya sayansi (chemistry, physics & biology)

+Huu ni mradi endelevu hadi sekondari zote za Kata na Binafsi zitakapokamilisha maabara hizo.

+Wana-Musoma Vijijini tuendelee kushirikiana na Serikali yetu kuchangia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya elimu ya Jimboni mwetu.

+Wazaliwa wa Musoma Vijijini waanze na waendelee kujitokeza kuchangia maendeleo ya vijijini kwao.

Taarifa za shule za msingi, hususani ujenzi wa shule shikizi mpya, na vyumba vipya vya madarasa zitatolewa baadae.

ILANI YA CCM YA UCHAGUZI YA MWAKA 2020-2025 INATEKELEZWA KWA MIPANGILIO MIZURI NA KWA MAFANIKIO MAKUBWA JIMBONI MWETU

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumatano, 10.7.2024

Vipaumbele vya Mh. Mbunge

Elimu
Kila mtoto aliyefikia umri wa kwenda shule, awe shuleni na kuinua kiwango cha ufaulu
Afya
Kusogeza huduma bora za afya zinazokidhi uhitaji kwa wananchi
Kilimo
Kilimo cha kisasa, endelevu na chenye uzalishaji mkubwa kwa eneo
Maji
Gharama nafuu katika upatikanaji wa maji safi na salama kwa kila kaya